Uvaaji kwa kina dada!

Wapendwa nawaombeni mnisaidie nielewe vizuri swala la mavazi. siku hizi naona wachungaji hawazungumzii tena suala la mavazi kwa mkristo hasa huku mjini. Ninaona wakristo wakivaa nguo zisio na heshima wala maadili sio mitaani tu bali sasa wanaingia nazo kwenye ibada. Nijuavyo mimi wapendwa vazi kwa mwanamke ni muhimu sana. Maumbile ya mwanamke siku zote yanagusa hisia za mwanaume aliye kamili. Tukisema kwamba tumeendelea sana au tuko kiroho sana kiasi kwamba wadada hata wakivaa nguo zinazoonesha maungo yao haitusumbui sidhani kama ni kweli.Naamini kila mwanamme aliye kamili akiwa katika ibada akaona mazingira ya uvaaji nilioutaja hapo juu itamsumbua nafsini mwake. Nauliza wanawake kuvaa kwa kuzingatia viwango vya biblia ni ushamba au kuptwa na wakati?. Nawaombeni kama ni mimi nina shida mnielimishe wapendwa.

Dan Kileo

Advertisements

22 thoughts on “Uvaaji kwa kina dada!

 1. tatizo hasa la mavazi hayo kuwa mabovu ni kutokujitambua kwa mvaaji mwenyewe na pia ni ujinga wa mtu na mtu vinachangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili ya uvaaji wa nguo za kike. vilevile mavazi hayo yanashusha heshima kwa wanawake wote posipokujali ni mvaaji au si mvaaji. wapendwa tuelewe kuwa si kila umbile la mwanamke linatakiwa kuonekana kwa kila mtu. kuna muda na wakati na mtu wa kuona. tuelewe kuwa kila nguo ina maana pale inapovaliwa na si kila nguo inayofaa kuvaliwa. vaeni nguo kulingana na muda husika. kuna baathi ya wasichana sasa wameamua kutembelea night dresss. tumuheshimu mungu na kanuni na sheria zilizowekwa. tutambue kuwepo kwa maisha mengine baada ya maisha ya hapa duniani.

 2. Wapendwa Shalo Aleichem!
  Kwanza nawaombeni muache dialogue zisizo na msingi bali kupelekeshana kwenye makwazo.

  Ndugu Mubelwa uliniuliza swali kuw NINA UHAKIKA GANI NA YALE NILIYOAINISHA HAPO JUU ON “WANAOVAA MAVAZI YASIYOSTAHILI WANAFANYA MAKUSUDI”.
  Kwa kuanza naomba tuelezane kuwa kwa wenye miaka kuanzia 30 na kuendelea wanawajua dada zetu na mama zetu jinsi walivyovaa wakati fulani mfupi uliopita. Kwa kadiri siku zimeendelea mavazi hayo yameendelea kubuniwa na mengine “yakichakachuliwa”. Mfano rahisi ni haya mavaziya kuacha maziwa nje, kwa kweli hata wasiookoka miaka hiyo ya nyuma hawakuwahi kuacha maziwa nje. Mimi sikuwahi kumuona mama/dada yangu, mama/dada wa jirani/rafiki zangu wakiwa waameyaacha nje. Sasa tujifunze kitu hapo; Je watu hawa walikuwa wanaambiwa na nani kuwa kuacha maziwa nje ni tatizo? Hawakuwa wameokoka wala hatukuwa tunajua kuna kuokoka. Nijuavyo mimi ni kuwa “Roho wa Mungu yupo kote/kila mahali” akimshuhudia kila mtu juu ya hukumu, haki… Sasa basi kama kwa ulimwengu wote ndio hivyo, JE KWA WANA WA MUNGU AMBAO ROHO WAKE ANAKAA NDANI YAO SI ZAIDI?

 3. Hakika swala la mavazi yasiyo na maadili lina wakera wengi sana, mimi nipo chuo kikuu mkoani morogoro.Huku ndio mbaya kuliko maeleezo kuhusu swala la uvaaji kwa kina dada/mama.Ila ashukuliwe Mungu wapo vijana wengi ambao wanakereka sana na uvaaji huu na wanawaasa marafiki zao wakike kuhusu uvaaji mbaya.Nawashauri kina dada/mama ya kuwa wasitafute kibali kwa uvaaji mbaya kawni hayo sio mapenzi ya Mungu.

 4. ” Denice says:
  Friday, May 20, 2011 at 12:45 pm
  Mr Mubelwa T Bandio,KUMBUKA Mungu habadiliku ni yeye yule jana,leo na hata milele.Na aliposema mwanamke avae mavazi ya kujisitiri alimaanisha hivyo hata kama
  tutaendelea namna gani.Hakuna sababu ya kusema eti zamani watu walijifunika kidogo na hapakuwa na shida.Hiyo ni mawazo yako lakini Neno la Mungu linabaki palepale.”MWANAMKE AVAE MAVAZI YA KUJISTIRI”.Usijaribu kuleta maoni ya kisiasa kwenye Neno la Mungu.Hata kama wanawake wangekuwa wanaishi peke yao bado NENO linawawajibisha kuvaa mavazi ya kujistiri.
  Tatizo ni kwamba mwanadamu anaendelea lakini Mungu haendelei kwani yeye ni mtakatifu.Siku hizi tumeendelea sana kiasi kwamba tunaona vitu ambavyo ni dhambi kama vya kawaida na tunatafuta maneno ya kuvihalalisha.Hata Wachungaji wanaogopa kukemea haya mambo kwani watakosa watu na kukataliwa,kwani makanisa yamekuwa biashara.Hao watu unaosema walijifunika walikuwa Wakristo?Mfano kama mtu ni mzinzi sio lazima apate ukimwi ndo ujue kuwa kuzini ni dhambi,su sio lazima ulewe na upige watu ndo ujue kuwa pombe ni dhambi.Aliyekunywa pombe kujiko kimoja,na aliyekunywa pombe mpaka akalewa na kufanya fujo na aliyelewa bila kufanya fujo wote wamefanya dhambi mbele za Mungu.
  Kwa hiyo tusitetee dhambi,kama zamani walijifunika na hapakuwa na vitendo vya ubakaji au ulawiti hiyo haimaanishi kuwa sio dhambi.Dhambi ni dhambi,nami naamini mwanamke anayevaa mavazi ambayo hayamstiri ANATENDA DHAMBI,hata awe mwimbaji mashuhuri,mke wa mchungaji au chochote.Kwani neno la Mungu halibagui ni Upanga ukatako kuwili tena ni kali.
  Nami siku zote nahubiri kinyume na hiyo tabia.
  ACHENI KULETA UKISASA NA FASHION MAKANISANI.”

  Ndg DENICE
  Labda unionyeshe nilipoandika kuwa tumeendelea na ndio maana tusijisitiri. Umekuja na hukumu ya “maoni ya kisiasa kwenye neno la Mungu” jambo ambalo pia ningefurahi kama ungelifafanua. Ukanieleza NI WAPI NILIPOWEKA SIASA KWENYE NENO LA MUNGU.
  Mimi nimeuliza kulingana na kilichoandikwa na kama unahisi kuna siasa katika hilo, tambua kuwa hivyo ndivyo uonavyo tatizo, na unalitatua kwa mujibu wa uonavyo na hilo ndilo tatizo.
  Kwa hiyo usiniweke nisipo ili unihukumu utakavyo. Na by the way HUNA MAMLKAKA YA KUNIHUKUMU. NI MUNGU PEKEE MWENYE HILO.
  Lakini kwanini hukubali ukweli kuwa KUNA MABADILIKO NA MAENDELEO? Na bado NAKUBALI UKWELI KUWA SI MABADILIKO NA MAENDELEO YOTE YANAYOIFAA JAMII AMA KANISA. Lakini ujue hayo maendeleo unayoonekana kuyasimanga ndiyo yanayokuwezesha hata kunihukumu hapa. Unapotumia mtandao wa intanet ni lazima utambue kuwa asilimia kubwa ya matumizi yake hayampendezi Mungu. Huwezi kuulaani mtandao mzima sababu hiyo kwani mpo mliochagua kuingia humu kujifunza kitu (japo wakati mwingine mnakuwa carried away na kuhukumu watu kama ulivyofanya)

  Bado nasubiri majibu ya Ndugu yangu Iqualiptus na nashukuru kwa majibu ya Ndugu Dan Kilewo.

  Nawe na ndugu Ray (kama ni watu tofauti) mnaweza kuendelea kujibu na / ama kujadili mada
  BARAKA KWENU

 5. ” ray says:
  Monday, May 23, 2011 at 8:58 am
  wewe mubelwa usitafute kila comment ya mtu kuitafutia swali hapa si mahala pa kujifunzia siasa umeshaambiwa biblia inasema mavazi ya kujistili unaanza kuuliza ni yepi unataka biblia iorodheshe gauni suruali hizo ni fashen zinapita kwa kipindi fulani cha muhimu ni kujisitiri kama una kuwa na mada leta mada sio viswali vyako vya kitoto kwenye comments za watu”

  Ndugu yangu Ray.
  Ninalofanya ni KUSOMA maoni na ninapoona ninahitaji kufafanuliwa ninafanya hivyo. Kama unaamini kuwa ni mimi peke yangu ninayefanya hivyo basi some vema. Na kama unaamini hapa hapastahili kuulizwa maswali, basi siamini kama kuna haja ya kuelimishana. Na kama unaweza kudhani kuwa una upeo wa kuita maswali ya mwingine ni ya kitoto, pengine huyo mwenye “maswali ya kitoto” ama wewe upo mahala pasipostahili.
  Lakini niliambiwa kuwa ninaruhusiwa kusoma, kutoa maoni, maswali na majibu.
  Kwa hiyo naamini NIPO NINAPOSTAHILI.
  Kwa hiyo huna sababu ya kusoma kila ninachoandika, na huna sababu ya kukereka kwa kisichokuhusu.
  Kama unahisi wewe u-mtu mzima kuliko maswali yangu, just SKIP ‘EM uendelee na mengine.

  LABDA NIKUHAKIKISHIE KWAMBA NILIKUWEPO, NIPO NA NITAENDELEA KUWEPO HAPA STRICTLY GOSPEL. Nitakaposhindwa kuelewa (iwe ni kwa uelewa wangu mdogo ama kwa mwandishi kutoweka bayana) nitauliza na wewe una haki ya kuita niandikacho vile uandikavyo. At the end of the day, naamini nitakuwa nimepata jibu ninalohitaji.
  BARAKA KWAKO

 6. Article copied from http://www.gotquestions.org

  Question: “Should Christian women wear pants?”

  Answer: The question about whether Christian women should wear pants or slacks is an issue that is raised about externals when the life of the child of God should rather be about a spiritual relationship based upon our position in Christ as believers. The obedience of a child of God is not measured by what clothing we wear but by our walk in the Spirit (Galatians 5:16).

  When looking at “doubtful things,” we need to use Scripture in context for the principles that will help us walk as believers, which means considering the dispensation and the whole counsel of God and not taking passages out of context. There is a passage in the Old Testament that speaks about a woman wearing men’s clothing: “A woman must not wear men’s clothing, nor a man wear women’s clothing, for the LORD your God detests anyone who does this” (Deuteronomy 22:5). The context of this passage is the second giving of the law to the nation of Israel as they were poised to enter the Promised Land. Deuteronomy 22:5 is an admonition not to live as a transvestite. This has to do with more than just clothing; it also speaks of a life that emulates in every way those of the opposite sex. Transvestitism was a practice of the Canaanites, and Israel was to consider it an abomination. We take a principle from this and apply it to our lives as believers, but we must use it in the context in which it is given and do so in relation to the dispensation of grace.

  The Apostle Paul wrote extensively on the difference between the law and grace in Romans. We are not justified by our adherence to the law, but we are justified by faith in Christ (Romans 3:21-28). The believer in Christ Jesus is “dead” to the constraints of the law. “But now, by dying to what once bound us, we have been released from the law so that we serve in the new way of the Spirit, and not in the old way of the written code” (Romans 7:6). Therefore, a believer does not live by legalism, nor by license, but rather by grace.

  What has that to do with a believing woman wearing pants? There is no biblical law that says what a woman should wear or not wear. Rather, the issue is one of modesty. Paul addresses the modesty of women in his first letter to Timothy. “I also want women to dress modestly, with decency and propriety, not with braided hair or gold or pearls or expensive clothes, but with good deeds, appropriate for women who profess to worship God” (1 Timothy 2:9-10). The Greek word translated “modest” is the Greek word kosmios, which is translated twice in the New Testament, once as “modest” in this passage and once as “of good behavior” in 1 Timothy 3:1. It came to mean “well-arranged, seemly, and modest.”

  The word clothes is the Greek word katastole. The meaning of the word was “to send or to let down or lower.” It was primarily a garment that was let down and in that day referred to a stole or a loose outer garment worn by kings and persons of rank. Since we know that Paul was not speaking to people of rank, the context here is simply modest attire, and it does not specify what that entails. Paul addressed this issue here because the women in the church were trying to outdo each other in how they dressed, and the flashier the better. They were losing sight of the things that should adorn a godly woman—humility, sobriety, godliness, and good works. The words “dress modestly” are not used here in the context of specific garments, but rather to being clad in a modest covering. It should not be used to prove a prohibition against wearing pants (also see 1 Peter 3:3-4).

  So, the issue is that a woman should wear modest clothing. Whether or not that includes a pair of slacks should be a matter for the woman’s own conscience before the LORD. If a woman allows her outward appearance to be the measure of her inward relationship with Christ, she is living under the constraints of legalism. Born-again women are free in Christ to wear whatever modest apparel they choose, and the only judgment they should be under is that of their own conscience. “Everything that does not come from faith is sin” (Romans 14:23). We are not to allow our consciences to be dictated to by legalism and the consciences of others, but by our own relationship with Christ. “I have been crucified with Christ and I no longer live, but Christ lives in me. The life I live in the body, I live by faith in the Son of God, who loved me and gave himself for me” (Galatians 2:20). God will take care of the outward woman if we walk in obedience in the inward woman.

  Question: “What does it mean to dress modestly?”

  Answer: In describing the mode of dress appropriate for women in church, the apostle Paul exhorts them to dress “modestly” with “decency and propriety” then goes on to contrast immodest dress with the good deeds which are appropriate for those who profess to be true worshipers of God (1 Timothy 2:9-10). Modesty in the way we dress is not just for church; it is to be the standard for all Christians at all times. The key to understanding what constitutes modesty in dress is to examine the attitudes and intents of the heart. Those whose hearts are inclined toward God will make every effort to dress modestly, decently, and appropriately. Those whose hearts are included toward self will dress in a manner designed to draw attention to themselves with little or no regard for the consequences to themselves or others.

  A godly woman endeavors to do everything with a “God-ward” perspective. She knows that God wants His people to be concerned for His glory and the spiritual state of their brothers and sisters in Christ. If a woman professes to be a Christian and yet she dresses in a way that will unduly draw attention to her body, she is a poor witness of the One who bought her soul by dying for her on the cross. She is forgetting that her body has been redeemed by Christ and is now the temple of the Holy Spirit (1 Corinthians 6:19-20). She is telling the world that she sees her own worth as purely physical and that her attractiveness to others depends on how much of her body she reveals to them. Further, by dressing in an immodest fashion, displaying her body for men to lust after, she causes her brothers in Christ to sin, something condemned by God (Matthew 5:27-29). Proverbs 7:10 mentions a woman “dressed like a prostitute and with crafty intent.” Here we see the description of one whose heart condition is displayed by her manner of dress.

  The Scripture says that a woman is to dress modestly, but what exactly does that mean in modern society? Does a woman have to be covered from head to toe? There are cults and religions in the world that demand this of women. But is that the biblical meaning of modesty? Again, we have to go back to the matter of the attitudes of the heart. If a woman’s heart is inclined toward godliness, she will wear clothing that is neither provocative nor revealing in public, clothing that does not reflect negatively upon her personal testimony as a child of God. Even when everyone else in her circle is dressing immodestly, she resists the temptation to go along with the crowd. She knows these types of clothes are designed to draw attention to her body and cause men to lust, but she is wise enough to know that type of attention only cheapens her. The idea of causing men to sin against God because of her dress is abhorrent to her because she seeks to love and honor God and wants others to do the same. Modesty in dress reveals a modesty and godliness of the heart, attitudes that should be the desire of all women who live to please and honor God.

  Question: “How can I know if the desires of my heart are from God?”

  Answer: Jesus answers this question for us: “For out of the heart come evil thoughts, murder, adultery, sexual immorality, theft, false testimony, slander” (Matthew 15:19). And then: “What comes out of a man is what makes him ‘unclean.’ For from within, out of men’s hearts, come evil thoughts, sexual immorality, theft, murder, adultery, greed, malice, deceit, lewdness, envy, slander, arrogance and folly. All these evils come from inside and make a man ‘unclean’” (Mark 7:20-23).

  In these passages, Jesus reveals the very springboard of our wants: our fleshly desires come from our innermost being. Sin does not just come about as a result of outside forces. It is borne from those hidden little niches residing in our thoughts and intentions, from the secret desires which only the mind and heart can envision. The bottom line is that, in our fallen state, the desires of our hearts do not come from God. Jeremiah further confirms the nature of man’s heart: “The heart is deceitful above all things and beyond cure. Who can understand it?” (Jeremiah 17:9)

  It has long been the view of many that all humans are basically good and decent and that it is the circumstances of life such as poverty or poor nurturing that turn us into murderers and thieves. But the Bible teaches that all men suffer from a common frailty—sin. The apostle Paul calls it our sin nature. “I know that nothing good lives in me, that is, in my sinful nature. For I have the desire to do what is good, but I cannot carry it out. For what I do is not the good I want to do; no, the evil I do not want to do–this I keep on doing. Now if I do what I do not want to do, it is no longer I who do it, but it is sin living in me that does it” (Romans 7:18-20). Our evil hearts lead us to sin.

  Furthermore, the heart is so corrupt and deceitful that our motives are unclear even to ourselves. As sinful creatures we devise and create evil things in the arrogance and self-sufficiency of our hearts (Proverbs 16:30; Psalm 35:20; Micah 2:1; Romans 1:30). The truth is that only God can examine our deepest motives and inward desires and only by His power can we ever hope to untangle the uncertainty and depravity that is bound up within our hearts. He alone searches all and knows us intimately (Hebrews 4:11-13).

  Fortunately, God does not abandon us in our struggles with hurtful desires and sinful tendencies. Instead, He provides us the grace and strength we need to resist and overcome sin when it crouches at the door of our hearts. The psalmist tells us to: “Delight yourself in the LORD and He will give you the desires of your heart. Commit your way to the LORD; trust in Him and He will do this: He will make your righteousness shine like the dawn, the justice of your cause like the noonday sun” (Psalm 37:4-6).

  Here we see that God can literally plant His own desires into the heart of man, the heart that, without Him, is desperately wicked and deceitful. He replaces the evil with good and sets our hearts on the path toward Him, removing our own desires and replacing them with His. This only happens when we come to Him in repentance and accept the gift of salvation through the Lord Jesus Christ. At that point, He removes our hearts of stone and replaces them with hearts of flesh (Ezekiel 11:19). He accomplishes this by the supernatural implanting of His Spirit into our hearts. Then our desires become His desires, our wills seek to do His will, and our rebellion turns to joyous obedience.

 7. MAVAZI YENYE KUSITIRI” maana yake si mavazi yenye kufunika viuongo vya mwili ila ni mavazi yenye kukubalika katika jamii yanapovaliwa.

  Unaposema kuwa mwanaume aliyekamili hata kama ameokoka akiona maungo ya mwanamke akiwa kanisani yako wazi itamsumbua nafsini mwake ujue tatizo si la aliyevaa hayo mavazi ila ni huyo anayesumbuka nafsini.

  Nasema hivyo kwa sababu kanisa ni sehemu ndogo ya jamii nzima,kama mwanaume akiwa na hilo tatizo basi atakuwa salama tu wakati anapokuwa kanisani ila akitoka atatamani sana kwa sababu huko nje atayaona sana hayo maungo ya wanawake.

  Kwanza wanaume tuliookoka wenye tatizo hilo tupone kabla hatujaanza kuwaambia wanawake wafunike maungo yao,je wakikataa tuendelee kuwatamani?Hii ni kwa sababu muda mwingi hatuishi kanisani (ambako hayatakiwi kuvaliwa hayo mavazi), ila tunaishi kwenye jamii ambako yanavaliwa sana.Tunapaswa kuwa watakatifu aidha tuko nje ya kanisa au kanisani.

  Halaf kinachotakiwa kufundishwa kwa wanawake si kuvaa mavazi marefu au yasiyobana n.k, bali ni kuvaa mavazi yanayokubaliwa na jamii inayotuzunguka. Suala la mavazi na kanisa ki msingi ni kuonesha tofauti ya kanisa na dunia, lakini si la kuwalinda wapendwa wasitamani. Tukiwalinda wasitamani kanisani watatamani nje ya kanisa ambako hatuwezi walinda.Kumbuka uvaaji ni mtindo ambao hubadilika kulingana na jamii husika pamoja na hali ya hewa,lakini hivyo vyote neno la Mungu limevitangulia.

  Kama kanisani inapendeza kuvaa nguo ndefu ili kuwavuta wengi kwa kristo basi tufanye hivyo, hata ufukweni pia kama wapendwa tunapaswa kuvaa nguo ndefu basi tufanye hivyo kwa ajili ya jamii kuja kwa kristo. La kama haisaidii kuwavuta wengine kwa kristo, iwe ndefu au fupi,yenye kubana au yenye kuachia, yenye kuonesha maungo au yenye kufunika vyote ni ubatili wala havimsumbui Mungu.

  Mavazi ni ya kimazingira na hali ya hewa zaidi, hivyo inabidi tu wenye kutamani wapone.
  Hata hivyo si lazima ukiona ungo la mwanamke utamani, unaweza kuamua kutokutamani.
  Halaf tutofautishe kusisimuka na kutamani. Kila mwanaume kamili akihisi mahaba kwa kuona au kuwaza anaweza kusisimuka, lakini huko si kutamani, na wala kusisimuka si dhambi maana si tendo la hiari hata hivyo.
  Mbarikiwe!

 8. my pastor recently preached about “Death of one’s Spiritual Conscious”
  wengi wetu dhamiri zetu za kiroho zimesha kufa wala hatujihukumu sisi wenyewe specially upande wa mavazi
  kama vile ndugu amesema It’s very distracting to the opposite gender in church. sio tu kina dada hata kina kaka. The bible says that RESIST THE DEVIL WILL FLEE FROM YOU
  but this sort of temptation is VERY IRRESISTABLE
  no matter how spiritual you are that’s why WE ARE TO RUN, RUN FROM IT.
  sasa hata makanisani tunapo kimbilia yame tukuta

  GOD HELP US ALL:)

 9. wewe mubelwa usitafute kila comment ya mtu kuitafutia swali hapa si mahala pa kujifunzia siasa umeshaambiwa biblia inasema mavazi ya kujistili unaanza kuuliza ni yepi unataka biblia iorodheshe gauni suruali hizo ni fashen zinapita kwa kipindi fulani cha muhimu ni kujisitiri kama una kuwa na mada leta mada sio viswali vyako vya kitoto kwenye comments za watu

 10. Mr Mubelwa T Bandio,KUMBUKA Mungu habadiliku ni yeye yule jana,leo na hata milele.Na aliposema mwanamke avae mavazi ya kujisitiri alimaanisha hivyo hata kama
  tutaendelea namna gani.Hakuna sababu ya kusema eti zamani watu walijifunika kidogo na hapakuwa na shida.Hiyo ni mawazo yako lakini Neno la Mungu linabaki palepale.”MWANAMKE AVAE MAVAZI YA KUJISTIRI”.Usijaribu kuleta maoni ya kisiasa kwenye Neno la Mungu.Hata kama wanawake wangekuwa wanaishi peke yao bado NENO linawawajibisha kuvaa mavazi ya kujistiri.
  Tatizo ni kwamba mwanadamu anaendelea lakini Mungu haendelei kwani yeye ni mtakatifu.Siku hizi tumeendelea sana kiasi kwamba tunaona vitu ambavyo ni dhambi kama vya kawaida na tunatafuta maneno ya kuvihalalisha.Hata Wachungaji wanaogopa kukemea haya mambo kwani watakosa watu na kukataliwa,kwani makanisa yamekuwa biashara.Hao watu unaosema walijifunika walikuwa Wakristo?Mfano kama mtu ni mzinzi sio lazima apate ukimwi ndo ujue kuwa kuzini ni dhambi,su sio lazima ulewe na upige watu ndo ujue kuwa pombe ni dhambi.Aliyekunywa pombe kujiko kimoja,na aliyekunywa pombe mpaka akalewa na kufanya fujo na aliyelewa bila kufanya fujo wote wamefanya dhambi mbele za Mungu.
  Kwa hiyo tusitetee dhambi,kama zamani walijifunika na hapakuwa na vitendo vya ubakaji au ulawiti hiyo haimaanishi kuwa sio dhambi.Dhambi ni dhambi,nami naamini mwanamke anayevaa mavazi ambayo hayamstiri ANATENDA DHAMBI,hata awe mwimbaji mashuhuri,mke wa mchungaji au chochote.Kwani neno la Mungu halibagui ni Upanga ukatako kuwili tena ni kali.
  Nami siku zote nahubiri kinyume na hiyo tabia.
  ACHENI KULETA UKISASA NA FASHION MAKANISANI.

 11. mimi naamini tukitumia tu maandiko kwenye mavazi, tutafaulu tu pale tunapoongozwa na Roho. nadhani kujisitiri ni neno zuri, kwa sababu mavazi mengi tunayoyavaa leo hayakuwepo wakati wa Biblia. jambo lingine ni kwamba, somo kuhusu wadada na mavazi limerudiwa sana mara nyingi hata kufikia wao kuona kama wanaonewa kwa sababu swala la mavazi ni la jinsia zote, ingawa kweli, lina mtazamo unaogusa zaidi jinsia ya kike. siku hizi hata wanaume wanaingia makanisani wakiwa wamevaa nguo za ajabu,mashati mafupi,suruali za milegezo, na marashi, usiseme sasa,akiingia kanisa lote linajua. hatari ni kwamba tu wapendwa wameacha kumsikiliza Roho, na ninavyojua, Yeye ni mngwana sana,hatashindana nasi daima. mtu akikosa kusikiliza sauti yake ni shauri. kuna nguo kweli tunaziona, mtu anashangaa,je mtu huyo alijua kabisa anaenda kanisani? nadhani pia tuanzie kuiweka misingi tangu kwa watoto wetu. baadhi yao wanavyovalishwa inatisha!

 12. Hapo ni tisa, kumi ni vazi la harusi la kike (gauni) linaloishia kifuani huku mabega yakiwa nje, hapo wapendwa mnasemaje?

 13. Thanks much Dan Kileo,
  Natumaini mada hii imekuja kwa wakati ili watu wapate kupona na sio kwa mazoea tu. Mara nyingi tumekuwa ni watu wa kuchagua ipi ni DHAMBI NA IPI SIO DHAMBI. madhalani hili la mavazi Baadhi ya Mitume na Manabiii wa sasa pamoja na wachungaji wameliingiza kwa dhana zao wanazozijua.
  Biblia inasema “WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKUSA MAARIFA” Naomba nikumbushe maarifa yasemwayo hapa ni yale yalio chimbuko la maarifa yoote ya Ulimwengu Huu yaani “NENO LA MUNGU”.Kwa mafundisho haya kama ni sahihi mavazi yasiyositiri Miili kwa akina dada ni DHAMBI……….. wewe sema ni mapokeo ila Mungu wangu anajua BIBLIA imekataza mavazi hayo. kama wewe hupendi kwa kuwa Mchungaji wako anakubembeleza basi Jua yeye anakupenda uishie hapa bila kuona raha ya Yerusalemu milele.
  kigezo kingine kidogo ni kuwa je tutawafundisha nini watu wa dunia kama wapendwa tunakuwa na mavazi ya cassino? acheni KUJIFARIJI MRUDIENI MUNGU. Katazo la BIILIA halina nyakati ni lile lile jana leo na Milele.
  NAWAOMBENI SANA TUEPUKANE NA DHAMBI YA KUCHAGUA DHAMBI NA KUHALALISHA DHAMBI KWA KIGEZO CHA KUSEMA UMEOKOKA……… NO! DHAMBI NI DHAMBI HAKUNA YA KALE NA YA SASA.

 14. Ndugu Mubelwa nashukuru sana kwa kuniuliza swali, pia nakupongeza kwa uchangiaji wako katika mada mbalimbali.Pia nawashukuru wachangiaji wengine hapo juu na wale watakaoendelea kuchangia.Viwango vya kibiblia ninavyozungumzia ni pale biblia iliposema kuhusu uvaaji kwa mwanamke kwa mfano sifa kuu ya mavazi ya mwanamke yanatakiwa YAMSITIRI MWILI wake. ITimotheo 2:9. Tatizo la uvaaji wa siku hizi ni mavazi yasiyoSITIRI mwili. Kwa lugha ya wenzetu ametumia maneno Modest apparel (KJV) akiwa anamaanisha mavazi yanayoashiria unyenyekevu (meek, humbleness). Ndugu mavazi huwa yanasema. Najiuliza hivi ni kwa nini tufanane na dunia, hatuwezi hata kuifundisha dunia maadili mema ya uvaaji, kwa sababu hata wasiokoka wanapiga kelele kuhusu mavazi ya siku hizi, je tuendelee tu kusema ni kwa kuwa hawana Yesu, ni tamaa zimewajaa? Ndugu zangu tunaweza kuwahubiria mataifa kupitia hata vaa yetu. Wazazi wasiookoka watakuwa tayari kuwaruhusu watoto wao waje kanisani wakijua angalau huko kuna maadili mema kwa sababu wanaona kwa macho kupitia maisha yetu ya kila siku nawaombeni tulione hili.

 15. Tatizo kubwa lililopo ni hawa wachungaji wetu,Mchungaji anapaswa kukemea uovu na asiubadilishe jina uovu akaupaka rangi ufanane na wema! tuache kujidanganya! utamsikia Mchungaji huyu anafundisha,”eeh Mungu anaangalia moyo na siyo ya mwilini” anasahau kwamba nia ya nje hutafsiri yale yaliyo ndani ya moyo wa mtu! Mavazi ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mkristo kwani mavazi pia humtambulisha mtu kwa kazi yake,mfano,polisi,nesi,daktari mara nyingi hutambulika kwa mavazi yao ingawaje wengine hawavai sare hizo1 Wewe dada wa kikristo unaacha sehemu za mwili wako ziwe wazi unamwonyesha nani?Kama kila mtumishi wa Mungu akiwa mkali katika hili naamini hii tabia itakoma! mnashindwa hata na mataifa ambao wao hufunika hata sura zao!

  Napenda kukutia moyo mpendwa huo sio ushamba bali ndio ukristo.KEEP IT UP!

 16. Ndugu yangu Iqualiptus, katika maoni yako umesema “Ni kweli kabisa wanafanya makusudi na “ROHO MTAKATIFU ANAWASHUHUDIA KUWA HAYAFAI ILA WANAJIKAZA KISABUNI”
  Ninasema hivi kwakuwa, kipindi kabla ya mavazi haya nilikuwepo, hata yalipoanza mtaani na baadae kuingia church.”
  Nina maswali mawili katika maoni yako.
  Kwanza…unaposema “WANAFANYA MAKUSUDI” unamaanisha makusudi yapi? Kwamba kusudi ni kutega ama imani yao kuwa wanapendeza? Na ni HAKIKA GANI ULIYONAYO kuwa wafanyapo haya wanadhamiriua ufikiriavyo wewe? Hudhani kuwa UMEHUKUMU?
  Na pili…..Kabla ya mavazi watu walikuwa wakijisitiri sehemu ndogo zaidi ya wanavyojisitiri sasa. Na matendo ya ubakaji, ulawiti na mengine hayaonekani kuwepo kwa wingi kama ilivyo sasa.
  Unadhani ni uvaaji unaoleta shida ama ni fikra za watu kupandikizwa tamaa na anasa ndio chanzo?

  Amani na Baraka kwako

 17. Ni kweli kabisa wanafanya makusudi na “ROHO MTAKATIFU ANAWASHUHUDIA KUWA HAYAFAI ILA WANAJIKAZA KISABUNI”
  Ninasema hivi kwakuwa, kipindi kabla ya mavazi haya nilikuwepo, hata yalipoanza mtaani na baadae kuingia church.
  Sasa inakuwaje mtu/mdada au mmama akae mahali, ajishtukie nguo yake ni fupi aanze kujifunikakw pochi, kitenge au kitambaa? Pia eti anajishtukia maziwa yao nje ana jifunika kwa kitambaa au mikono nk? Mara nyingine wapandishe suruali mara washushe blauzi au shati nk.
  SIAMINI WALA SITAAMINI KAMA HAWAKUFIKIRI NA KUELEWA KAMA WAKITEMBEA AU KUKAA HAWATAKUWA WAMEJISITIRI KWA MAVAZI WANAYOVAA. Ninachojua pale wanapovaa mavazi hayo ni;-
  Roho huwashuhudia juu ya muonekano usio safi kwa Mungu na kwa watu
  Huelewa itawahitaji kushusha au kuirekebisharekebisha marakwa mara nguo husika ili walau imsitiri
  Hujishuhudia kwamba ni watu wa aina gani anatakiwa akutane nao na wa-note hayo mavazi na ambao hawatakiwi
  nk, n.k….
  Ndugu zangu, mavazi mengi ni mazuri lakini si yote “yanafaa”. Sio sketi au gauni tu ndio la heshima bali vazi linalomsitiri mwanamke kwa ujumla wake.

  Kuhusu wanaume, sikuwahi kumuona mwanaume mwenye (1).akili timamu na (1). aliyeokoka akivaa nguo zisizo na heshima (mfano mlegezo n.k).
  Haya mavazi, vijivazi na fashion zisizositiri miili zinatoka kwa adui Shetani wala hakuna cha kujitetea. Kwa kweli ambao wanavaa mavazi ya namna ya “uchokozi” (kama mchungaji mmoja alivyoyaita wakati yakiingia) wako kwenye giza kipande hiyo na wametekwa wanahitaji neema ya Mungu, ndio maana YESU AKASEMA “ANGALIA NURU ILIYO NDANI YAKO ISIJE IKAWA NI GIZA”-Lu:11:35: Take heed therefore that the light which is in thee be not darkness.

  Mbarikiwe!

 18. Ndugu Dan Kileo.
  Swali lako kuu limeuliza kuhusu “wanawake kuvaa kwa kuzingatia viwango vya biblia ni ushamba au kuptwa na wakati?.”
  Binafsi ningependa kuelewa unavyofahamu kuhusu MAVAZI KWA VIWANGO VYA BILBIA NI YAPI?
  Baraka kwako

 19. Tatizo sio mavazi bali wakristo wengi wa kizazi hiki cha dot com hawataki kabisa kukubaliana na neno la MUNGU. Wamesahau lile neno katika mathayo- kua waitwao ni wengi lakini wateule ni wachache.Sasa kama mtu anapingana na neno la MUNGU hiyo ni hatari kubwa sana na ni upotevu mkuu.Maelekezo ya mavazi Paulo ameyaelekeza vizuri sana katika kiatbu cha Thimotheo

 20. mimi ni mwanamke, kwa kweli kama kuna vut vinanisumbua siku hizi ni kuhusu mavazi na hasa kwa mabinti wa kilokole mefikia wakati mtu unakutana nae anaona hata aibu kukuangalia usoni kwa sababu ya uvaaji aliovaa. wenzangu wengi wananiita mshamba, nimekubali hili. jamani hatuwezi kukimbizana na wakati,mbona zipo nguo nyingi za heshima. mi nalipenda sana kanisa moja kule moshi wazee wakanisa au huwatoa nje au huwavisha vitenge wamama/wadada wanaoingia uchi kanisani.
  Jamani matendo huongea kwa nguvu sana kuliko maneno. Mungu atusaidie na niwakumbushe mabinti wenzangu kuwa mambo yooooooooooooooooooooooote yatapita lakini neno litasimama”wanawake na wavae nguo za kujisetiri”

 21. habari kaka
  unachosema ni sahihi kabisa,siku hizi wasichana hawataki kubadilika,ati wanaenda na wakati,lakini biblia imenena wazi katika timotheo kuhusu siku za mwisho na hata katika waraka wa petro imenenwa pia,tatizo watu Mungu wanampenda na dunia pia,lakini wasijue maandiko yanasema watu wa jinsi hiyo Mungu atawatapika,cha muhimu kwa mtu anayependa kwenda mbingubi abadilike na kukubali maonyo.kuvaa mavazi ya heshima si ushamba kwani hata watakatifu waliopita walivaa kwa kujisitiri.jamani tunapitwa hata na watu waiomkiri Yesu!!!!!!!!!!

 22. Kwa mtazamo wangu naona siyo ushamba wala siyo kupitwa na wakati bali ni mavazi yenye heshima yanayokubalika popote pale uwendano hata katika jamii inayokuzunguka yanakubalika tofauti na mavazi yanayoonyesha maumbile ya mwanamke.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s