Kubariki Ndoa

Je!

1. Kuna umuhimu wowote wa kubariki ndoa kwa watu, mke na mume, walioanza kuishi pamoja kabla ya kufunga ndoa?

2. Je! Tendo hili la kubariki ndoa ni halali/sawa Kibiblia?

Advertisements

16 thoughts on “Kubariki Ndoa

 1. Bwana asifiwe ndugu EVA

  Kweli ndugu ile unapo sema ni kweli kama unaposema ama kwa ndika na kizungu endelea na iyo kama kiswahili endelea nao pia juu ya kwelewa mchango wako juu ya kusaidiya wengine.

  Juu ya ndoa inakubalika kubarikiwa mno.Mfano bwana na bibi walikutana na wote ni wapagani ama wakristu vmda kitambo wamepata NENO kwa Kanisa fulani wakaguswa na Roho ya Mungu juu ya kutengeneza maisha yao ya kiroho mbele ya Mungu dhamiri yao ni Police ya maisha yao ya Kiroho…..Na hapo wakakamata hatua ya kwenda kwa Mtumishi fulani na kusema hali ya maisha yao ama ndoa yao vile walipotukutana . na wakaomba usaidizi ama kubariki ndoa yao. pale sio mubaya kwa mafikiri yangu iyo

  Tafazari kama nimekosea munisaidiye wandugu

  Mubarikiwe wote

 2. Bwana Yesu asifiwe,
  Napenda kutoa maoini yangu kama ifuatavyo

  Napenda kuwashukuru wote mnaochangia hoja mubarikiwe sana .ila nawaomba wote mnaochangia hoja zenu kuwa mjitahidi kutumia lugha moja husika,kama ni kiswahili basi tumia kiswahili bila kuchanganya na lugha nyingine,na kama ni English basi ni vizuri kutumia lugha uliyoipenda. Tatizo sio wote wanaoelewa English na wakasoma nakufunguliwa na pia sio wote wanaoelewa kiswahili wakasoma na wakafunguliwa hivyo tujitahidi kuwa na utaratibu mzuri kwan hata biblia niya utaratibu na kiasi.

  Mungu awabariki samahani ikiwa nitakuwa kinyume na mada husika.

 3. Mtu wa Mungu Mubelwa T Bandio shalom!
  Kama nimkuelewa naomba kujibu swali lako hasa kwamba ndoa ifungwe wapi? Ndoa inaweza kufungwa serikalini zamani walisema kwa AREA COMMISSIONER, Kienyeji yaani kwa mila za kiafrika, kanisani, msikitini au popote pale penye mamlaka ya kufunga ndoa. Nasema hivi kwasababu cheti cha ndoa hutolewa na serikali bila kujali ndoa imefungwa nanani. Ila hapa penye swala letu la kubariki ndoa ndio tunataka kujua kubariki ndoa kunatakiwa au ni lazima? Hapa kuna vitu naviona kwamba siyo vya lazima kama 1) Mtu ameokoka akiwa amefunga ndoa na anaona abariki ndoa hili ni chaguo la mtu kwani mtu akiokoka tu automatically anabarikiwa yeye na familia yake. 2) Kufanya harusi au sheree kwa ndoa tena hapa mimi naona ni tatizo hasa siku hizi vijana wengi wameshindwa kuoa kutokana na gharama kubwa za harusi za siku hizi. Ndugu yangu ndoa siyo gharama ila sheree inayoambatana na ndoa hiyo yaani harusi. Siku hizi bila kuanzia milioni 10 hadi 40 harusi haijafanikiwa sasa vijana wetu inabidi watumie mbinu mbadala kama kuomba misaada, kukopa au ikibidi kutumia njia mbadala kama udanganyifu (wizi) ili kupata fedha za harusi vinginevyo wanaoshindwa wanaishia kuoana kinyemela kwani harusi hawaziwezi. nina mengi ila samahani kama nitakuwa sijajibu swali lako.
  Barikiwa in Jesus Name!

 4. Bwana asifiwe wapendwa, nashukuru kwa majibu mazuri ambayo yametolewa. Mimi nadhani nijibu kisheria zaidi, ndoa ni makubaliano ya kisheria kati ya watu wawili waliokubaliana kuishi pamoja kama mume na mke(marriage is a legal agreement) and hence enforceable by law once the contract is breached by either party (husband and wife) huu ni mkataba ambao wa kiserikali na wa kimungu pia.ndio maana hati/cheti cha ndoa inaofungwa popote hutolewa na serikali si kanisa. Ndio maana tunakuwa na ukiri wa baadhi ya maneno ambayo karibu yanafanana popote..kwa upande wa ndoa kisheria niachie hapo .harusi ni sherehe inayofanywa kusherekea ndoa husika.

 5. Ndugu yangu Melckzedek Mbise. SHUKRANI.
  Nimefurahia ufafanuzi wako. Nami nilikuwa na mawazo yanayorandana na hayo japo nilipenda kupata uhakika kabla sijaendelea.
  Katika maelezo yako umesema “kufunga ndoa siyo hiari ukitaka kuishi na mwanamke kama mke wako au mwanamme kama mume wako sharti ufunge ndoa.”
  Hapa unazungumzia ndoa inayofungwa wapi na vipi. Ni kwa kwenda mahala kusema “I DO” ama kukubaliana kwa wapendwa? Kwa kuwa nilikuwa (na bado) naamini kuwa kwenda mahala mnakoambiwa kusema NITAFANYA ni harusi na si ndoa. Ninalojaribu kutafuta hapa ni kama “ili ndoa ijulikane kuwa ndoa ni lazima iwe na makubaliano mbele ya watu (ambayo tayari yatakuwa harusi), ama hata bila kusema lolote kwa yoyote zaidi ya wawili mpendanao mnakuwa MMEFUNGA NDOA?
  Na kwa mantiki hiyo, haimaanishi kuwa ni wengi waliooana ambao wanaonekana hawajafunga ndoa?
  Baraka kwako

 6. Shalom!
  Mubelwa T Bandio.
  Tofauti ya ndoa na arusi ni kwamba Ndoa ni kuoana kati ya mwanaume na mwanamke lakini harusi ni sheree inayofanyika siku ya kufunga ndoa. mfano katika Biblia harusi ya Kana ya Galilaya ambapo ilitajwa kwamba wametindikiwa na mvinyo inaonyesha ilikuwa ni sheree ya kula na kunywa baada ya kufunga ndoa ingawa maharusi hawajatajwa. Ila tunafahamu harusi ni sheree ya wakati wa kufunga ndoa tu. unaweza kufunga ndoa na kusiwepo na harusi na bado ndoa ikawa halai lakini huwezi kufanya harusi bila kufunga ndoa. Maana huo ni uamuzi wa mtu tu kfanya sheree lakini kufunga ndoa siyo hiari ukitaka kuishi na mwanamke kama mke wako au mwanamme kama mume wako sharti ufunge ndoa.

  Barikiwa na Bwana Yesu!

 7. Mtumishi JWM

  Ninashukuru kwa swali zuri ulilouliza, maana ya “ndoa takatifu” mimi napenda kukujibu kama ifuatavyo.

  Kama ni mtu unayesoma biblia kwa kutafuta kujua tabia ya Mungu, utakuwa umejua kwamba pamoja na mambo mengine mfano Uaminifu, Mungu ni Mkamilifu na ni Mungu wa Ukamilifu. Pia ni mtakatifu na imeandikwa “Mtakuwa watakatifu kama vile yeye alivyo mtakatifu.”
  Kila kitu alichokiumba na kukianzisha Mungu, ndani yake kimebeba tabia ya Mungu, there is a character of God inscribed in every creation. Ikiwa tunakubaliana kwamba asili ya ndoa ni Mungu mwenyewe, na kwamba Msingi wa ndoa ya kikristo haujengwi katika mapenzi ya kimwili bali katika Imani thabiti ya Mke na Mume kwa Mungu, ambayo ndiyo iliyowafanya wafike mahali pa kutambua kwamba Huyu ndiye mwanamke/mwanamme niliyepewa na Mungu. then Tunatambua kwamba ndoa hii imejengwa katika msingi ambao ni Mungu mwenyewe, na Kama jinsi Yeye alivyo Mtakatifu, ndivyo Ndoa hii inavyobeba character ya Mungu na kuwa takatifu.
  Kama ndoa imefungwa katika misingi ya jinsi hii, basi hakuna sababu ya kubariki tena, kwa kuwa tayari imejengwa katika msingi wa Baraka, yaani Mungu mwenyewe.
  Thats why biblia inaweka wazi kwamba, Mtu apataye mke, amejipatia kitu chema, naye atapata kibali machoni pa Bwana. tena imeandikwa Fedha na mali ni urithi apatao mtu toka kwa baba yake, bali mke mwema hutoka kwa Bwana.
  Mahala pengine wanaume tumeonywa kuishi na wanawake kwa akili ili maombi yetu yapate kukubaliwa na Bwana.
  Kimsingi, katika ndoa iliyofungwa katika msingi wa kweli wa kikristo kama nilivyoainisha hapo mwanzo, machoni pa Mungu ubinafsi wa wahusika unakuwa haupo tena, God either sees the two of you or he sees none of you,(Kwa habari ya Mafanikio ya maisha ya kawaida) Hii ndio dhana ya Mwili Mmoja. na kwa jinsi hiyo Msingi wa Mafanikio huwa ni mapatano baina ya Mume na mke ambayo hupata kibali mbele za Mungu.

  Mungu awabariki wote.

 8. Wapendwa,

  Wakati fulani nilipata kuuliza mahali fulani kuwa ni nini kinachofanya ndoa iitwe “takatifu”. Kwa maneno mengine, nilitaka kujua maana (definition) ya “ndoa takatifu”. Hata sasa natamani kupata hiyo maana, halafu tuipime kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu.

  Nije kwenye swali husika.

  Katika kujifunza kwangu Maandiko Matakatifu, nimeelewa yafuatayo ambayo naona yanahusiana na mada hii tunayoijadili sasa:

  1. Maandiko yametaja ndoa sehemu nyingi, na kuielezea kama uhusiano wa mwanamke na mwanamme ambao wameamua WAO WENYEWE kuachana na wazazi wao ili waambatane pamoja kuwa MWILI MMOJA (jambo ambalo linakamilika kupitia tendo la ndoa).
  2. Ndoa zilikuwa zifanywa zaidi kulingana na utamaduni wa mahali husika.
  3. HAKUNA mahali popote katika Maandiko Matakatifu panaposema kuwa Wakristo hawana budi kufungia ndoa kanisani, na kwamba wasipofanya hivyo ndoa yao itakuwa batili.
  4. Ndoa zilizofungwa kabla ya watu kuokolewa zinaendelea kutambuliwa hata baada ya wanandoa kuukubali wokovu.

  Nimeandika kwa haraka lakini ningeweza kunukuu vifungu vya Biblia kwa kila hoja niliyoitoa hapo juu.

  Sasa niseme yafuatayo:

  1. Pamoja na pointi zote nilizoziandika hapo juu, hatuna budi kuzingatia pointi namba 2: utamaduni wa mahali husika. Kwa Wakristo, kufunga ndoa kanisani ni “utamaduni wetu”! Mie sijaona lililo baya katika hilo, hivyo ninashauri kuwa kama hakuna sababu ya msingi, Wakristo wanapotaka kuoana wafunge ndoa kanisani.
  2. Dhana ya kubariki ndoa inahitaji ufafanuzi: Ni kwamba ndoa iko katika laana na hivyo inahitaji kubarikiwa? Na hiyo laana imetokana na nini? Ufafanuzi wa Kimaandiko utasaidia zaidi kuliko wa kimapokeo.
  3. Kupata ridhaa ya wazazi wa pande zote mbili kabla ya kuoana ni jambo jema sana. Lakini pale ambapo upande mmoja umegoma kumruhusu mtoto wao kuoa au kuolewa, wakati mwingine ni kwa sababu wanataka kumlazimisha aoane na chaguo lao wazazi, mimi ninaamini kuwa vijana husika wanaweza kuoana bila ya ridhaa hiyo. Hata hivyo nitoe ANGALIZO: Wakati mwingine wazazi huwa na sababu za msingi za kukataa kijana wao (mvulana au msichana) kuoana, hivyo wahusika wawe tayari kuwasikiliza na kuzitafakari sababu hizo kabla ya kufanya uamuzi wa ama kuendelea na mpango wa kuoana au la. (Sina muda wa kufafanua hili kwa sasa).

 9. Amani, Heshima na Upendo kwenu.
  Ni nini tofauti ama mfanano wa NDOA na HARUSI? (ikiwezekana kwa mujibu wa Biblia).
  Naamini hii itasaidia kujua kama kinachofanyika mbele ya kadamnasi “kwa watu, mke na mume, walioanza kuishi pamoja kabla ya kufunga ndoa” ni “kubariki ndoa” ama “kubariki harusi”.

  BARAKA KWENU

 10. Mimi sijaona katika Biblia ambapo watu wamebariki ndoa ila sehemu walipooa ni wengi. Pengine tunatajiwa harusi kama ya kana ya Galilaya lakini kwa wale wote katika Biblia ambao hawakufanya harusi hatukuona mahali ambapo Yesu aliwakumbusha habari ya kubariki ndoa zao. Mimi naona kama watu waliooana kabla hawajaokoka na wakafunga ndoa kwa namna yoyote isiyokuwa ya mizimu yaani isiyohusisha ushirikina basi wakiokoka tu inatosha na ndoa yao inabarikiwa automatically. Just imagine watoto wamezaliwa katika ndoa ya watu wasiookoka na hawakubarikiwa na wamekuwa wakubwa je watabarikiwa upya? Ninachoona kama watu waliookoka wakioana bila kufunga ndoa watakuwa wametenda dhambi na itabidi waokoke halafu wafunge ndoa basi.
  Blessed

 11. Mtumishi Wakumoto!

  Kila mahali pana taratibu zake na same as ukristo/imani ya kikristo. the foundation of marriage in a christian life is God Himself, that is your faith in God that makes you know that this is a Woman/Man that God has Given to Me. and since Your faith in God is the foundation of Marriage, ndoa inafungwa kanisani ikiwa ni sehemu kamili ya kukiri (acknowledging)na kupokea kwa shukrani kile ambacho God has ordained for a man and a woman who by faith came together and they are about to become one.
  Any marriage that is found outside this conception of marriage (outside your faith in God) ni ubatili mtupu.
  Otherwise ingekuwa hivyo tusingekuwa na sababu za kwenda kufunga ndoa kanisani, na mawazo kama haya ndiyo yanayohalalisha ndoa zisizo rasmi. haiwezekanikibali mbele ya watu kikawa na thamani kubwa mbele za macho ya mtu kuliko Kumkiri Mungu aliye waunganisha na kuipokea baraka ya ndoa kwa shukrani.
  Ikiwa kweli unaamini this is a woman that God has Given to you, whats wrong with Going to the church and receiving the blessing of marriage kwa shukrani na kuomba baraka ya Mungu?

  kwa msisitizo nasema ndoa ya kikristo ni lazima ipate baraka kanisani, no short cuts. watu walichukuana tu huko, upon becoming christians wakishajua maana halisi ya ndoa ya kikristo wanawiwa kuja mbele za Mungu, mbele za watakatifu wake kukiri kupokea baraka hii na kumrudishia Mungu utukufu

  ndivyo nijuavyo mimi

  Be blessed

 12. Shalom,
  kwa ufahamu wangu “baraka” ni kitu mtu anapokea kutoka kwa Mungu kupitia kwake moja kwa moja au kwa mkono wa wengine hasa watumishi wa Mungu kwa kuombewa, kuwekewa mikono nk.
  Kama wawili waliamua tu kuishi bila kuapa au kumhusisha Mungu ktk ndoa yao, wanakosa baraka kwani Mungu hatambui huu umoja wao, na tujuavyo kazi ya Mtumishi wa Mungu ni kumwakilisha Mungu kwetu akituonya, akitutia nguvu nk hivyo sio ajabu kiapo hiki unachojifunga mbele za Mungu uhusishe watumishi wake kama ambavyo ukitaka kujifung akisheria ungehusisha watumishi wa serikali husika.
  Ndio maana pamoja na kuwa Herode wakati wa Yohana mbatizaji aliamini mafundisho ya Yohana lakini ile ndoa yake na Herodia mke wa mdogo wake ilikuwa inakemewa na Yohana, kwa maneno mengine haikuwa na “baraka” za Mungu. Kama kila mtu angekuwa anajiamulia bila kumshirikisha mzazi wake wa kiroho na kuanza kuishi na mwenza je matatizo ya kiroho yakiwapata watamwendea nani?
  Mbarikiwe

 13. Kwa mtizamo wangu: Suala la kubariki ndoa linahusu kupata uhalali mbele ya kadamnasi/jamii inayowazunguka hao walioanza maisha bila kufunga ndoa. Ndoa ni halali bila kujali kama imefungwa kanisani, msikitini, bomani (kwa DC), au imefungwa kimila. Uhalali wa ndoa unaanza pale familia za pande mbili zinaporidhia vijana wao waoane kwa taratibu zinazotawala jamii hiyo. Kwenda kaisani au msikitini ni desturi inayotumika katika kuhalalisha uwepo wa ndoa hiyo.
  1. Ndoa haiwezi kuwa halali hata kama imefungwa kanisani/msikitini endapo mmoja wa wanandoa amelazimishwa kuolewa.
  2. Ndoa haiwezi kuwa halali kama wafunga ndoa wenyewe (wawili tu) wanaaamua kufunga bila ridhaa ya wazazi wa pande zote mbili kuridhia.
  3. Lakini tujue kwamba ndoa inaanzishwa na watu wawili kwa ridhaa yao ambao baadaye huja kutambulika kama mume na mke. Hawa wawili wakikubaliana tayari ndoa ipo, na wanaweza kuamua kuanza maisha. Ila ndoa hiyo sio halali.

  4. unapobariki ndoa, ina maanisha kwamba ndoa tayari ipo ila mazingira yaliyotumika katika kuianzisha hayakuwa wazi mbele ya jamii, kwa hiyo unaoomba ridhaa ya jamii kutambua uwepo wa ndoa yako. Hapa ina maana wawili hao labda walikutana na kuamua kuanza kuishi kama mume na mke bila hata ridhaa ya wazazi. Baadaye wanaaamua kuwasiliana na familia zao ili wapate uhalai wa ndoa yao.

 14. kwa uelewa wangu ni kuwa ni bora kubariki ndoa kwa sababu watu wale au wanandoa kwa sabau baada ya kuokoka inatakiwa wabariki ndoa kwa kuwa ndo ni jambo la baraka na pia kwa makusudi ya mungu ni kuwa wanandoa hao wanatakiwa kuishi maisha yaliyo barikiwa

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s