Mume anapoachwa na mke…!

Kuna wanaume wengi ambao huachwa na mke na kisha mke akaolewa kwingine, nao kubakia katika njia panda wakiwa hawajui kama ni sahihi au si sahihi kuoa mwanamke mwingine.

Je! Katika Ukristo ni halali au si halali kwa mwanaume aliyeachwa na mke wake akioa mke mwingine?

Advertisements

13 thoughts on “Mume anapoachwa na mke…!

 1. “Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana,mke asiachane na mumewe; lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.”
  1 Wakorintho 7:10,11

 2. mke aliemwacha bwana wake aliyeza na watoto watatu na waliishi miaka ishirini na sita akaamua kuolewa pengine na kuzaa watoto wawili tena na akawa mkristo je atakuwa katika kundi gani la maisha

 3. Mpendwa, Obedi V. Milinga.

  Sifa ni kwake Kristo Yesu.

  Wamebarikiwa wote wanaomtafuta Bwana kwa bidii, kwa ajili ya kuurithi ufalme wa mbinguni. Mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa bali tutakuwa kama malaika, Marko 12:25!.

  Jina la Bwana libarikiwe!

 4. Bwana Bernard Mwenda, Ubarikiwe sana. Umeeleza vizuri sana kwani kuna watu wanaelewa tofauti maandiko hayo.

  Watu wengi wamekuwa wakidhani neno “UASHERATI” ni sawa na neno “UZINZI” na wamekuwa wakijaribu kuhalalisha TALAKA kwa kusimamia maandiko hayo. Huu ni upotoshaji mkubwa. Natamani maelezo yako wahubiri na waumini wote wa Kikristo na Kiislam wangeyachukua kuyatumia kuhubiri kanisani au misikitini mwao ili upotoshaji ukome.

  Kila mpendwa akumbuke kuwa Yesu aliposema mtu akikosea umusamehe 7 X 70 = 490 KWA SIKU MOJA alimaanisha pia kwamba hata ukimfumania mkeo au mume mara 490 kwa siku akiwa anazini UMSAMEHE. Yesu hakusema kwamba umpe talaka.

  Katika Agano Jipya TALAKA ni msamiati ambao ulifutwa kabisa. Kumbuka zamani za Musa, TALAKA ilikuwa inaruhusiwa kwa sababu yoyote hata kama mkeo ameweka chumvi nyingi kwenye mboga, sababu kama hizo zilitosha KUTOA TALAKA.

  Yesu alipokuja akasema “STOOOOOP” Achana na TALAKA.

  Wapendwa tunapaswa kuelewa kwamba TALAKA ina madhara makubwa sana kiroho na kimwili, kiuchumi na kijamii. Hii ndiyo sababu Mungu anachukia kuachana kwa wanandoa.

  Naomba uniruhusu nikueleze machache tu

  Kwanza, huleta uharibifu wa kisaikolojia kwa wanandoa walioachana.
  Pili, husababisha uwezekanao wa kuambukizana magonjwa ya zinaa endapo mmoja atajikuta ameolewa au kuoa aliye na maambukizi ya magonjwa yoyote ikiwemo HIV.
  Tatu, wanandoa hao wote bila kujali nani alikuwa na kipato, wote wanaathirika kiuchumi. Kipato lazima kitashuka au kila alifanyalo halitafanikiwa.
  Nne, Watoto waliokuwa wamezaliwa katika ndoa hiyo hawatapata malezi ya upande mmoja wa wazazi. Hii itasababisha watoto hao kukosa ulari wa maisha yao baadaye wakiwa watu wazima (Children will live unbalanced parental care and unbalanced pyschological life due to lack of either of the parents). Mtoto aliyelelewa na mama tu atakapoolewa atashindwa kuishi na mume vyema kwani alipokuwa kwa mama hakuwahi kuona au kujifunza kwa vitendo mume na mke wanavyopaswa kuishi, kupendana, kuheshimiana, kutatua matatizo, kuchapa kazi kwa bidii,n.k. chembechembe za maisha toka kwa Baba au kwa mama atakuwa anazikosa.
  Tano, TALAKA ni chanzo cha watoto wanaozurura au kurandaranda barabarani au mitaani katika miji yetu. Sababu kubwa zinazochangia watoto kuzagaa na kuishi mitaani bila uangalizi siku hizi, ni talaka na magomvi yasiyokwisha katika ndoa nyingi za wakristo, waislam na wapagani. Hebu fikiria, uwaonapo watoto wa mitaani unajisikiaje? Huwa inapata mawazo gani? Unaposikia kuwa wanandoa fulani wametelekeza watoto wao na kutokomea kusikojulikana unajiskiaje? WEWE UNAONA NI SAWA? Je, hili ndilo agizo la Mungu kuwa tukaijaze dunia kwa watoto wa mitaani wasiokuwa na mwelekeo wowote, vibaka, wezi, majambazi, nk. kazi wanazozifanya kwa sababu wazazi wao waliachana?
  Sita, taifa linakuwa na watu wasiokuwa na nguvu kiafya na kichumi. Kumbuka Taifa ni muunganiko wa familia moja moja. Kama familia zina nguvu kiuchumi hata kanisa na taifa huwa imara. NGOs na Serikali wataendelea kuanzisha vituo vya kulelea watoto wa mitaani hadi lini?

  Mwanamke au mwanaume anayemwacha mwenzake kwa kisingizio chochote anakuwa amedhihirisha UBINAFSI ALIONAO wa kutotaka watoto wake nao kupata haki ya kutunzwa na wazazi wote wawili wakiwa pamoja. Watu wengi huachana kama ishara KUU ya UCHOYO uliotopea dhidi ya kizazi kijacho.

  Ninamalizia kwa kusema kwamba, hata kama ni wanandoa ambao hawajapata watoto, kwa sababu tu walishafunga ndoa na kwa sababu mojawapo nilizozitaja hapo juu, HAWANA RUHUSA YA KUACHANA.

  Yesu alipoweka STOOOOP kuhusu kutoa talaka hakuwa anaangalia upande wa masuala ya mapenzi ambacho ndicho kisababishi kikubwa kiletacho TALAKA. Yesu alitazama mbele zaidi madhara yatakayotokea KIZAZI cha kwanza hadi cha nne cha wanandoa hao na taifa kwa ujumla.

  Kila mtu anayeunga mkono suala la Talaka awe mwislam au Mkristo au Mpagani atoe majibu kwanza kwa upande wa pili wa madhara yanayotokea kwa wanandoa wenyewe, watoto wao, kanisa lao, taifa lao, uchumi wa nchi, na tatizo kubwa la sasa juu ya watoto wa mitaani kuongezeka kila uchao.

  Vinginevyo, watu wanatetea haja ya tamaa za miili yao badala ya kizazi hiki na kijacho. TUPONYWE NA ROHO YA TALAKA.

 5. Mbarikiwe wapendwa,

  Suala la ndoa kwa sisi waKristo, mimi nakumbuka kuna wakati fulani kati ya mwaka jana niliwahi kufafanua ninavyofahamu juu ya ndoa za ki-Kristo.

  Wengi tunapotoshwa na hatujaelewa vizuri maana halisi ya maneno haya mawili yalivyotumika katika biblia “UASHERATI” na “UZINZI”.

  Ninapenda nieleze kuwa; uasherati na uzinzi ni maneno mawili tofauti japo yanahusiana. Tukisoma katika Mathayo 5:32 tunaona maneno haya “…lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya UASHERATI, amfanya kuwa MZINZI; na mtu akimwoa yule aliyeachwa AZINI” Maana yake ni nini..! Katika maandiko haya, tunajifunza wazi kabisa kuwa uzinzi ni dhambi, na wafanyao huo uzinzi maandiko yanatuambia kuwa hawataurithi ufalme wa Mungu. Tunasoma hilo katika Ufunuo 21:8 Bali waoga……..na WAZINZI…..sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti…..

  Kama wa-Kristo tunaoutazamia ufalme wa Mungu, katika sehemu hii lazima tujiulize. Kwa nini Mungu aruhusu kuachana na kuoa/kuolewa na mwingine tena Mungu huyo huyo aseme kuwa wazinzi hawataurithi ufalme wa Mungu? Anayefanya uzinzi ni yupi; aliyeachwa au aliyeacha? Tukisoma andiko; Mathayo hiyo hiyo 5:32, linasema; “…..na mtu akimwoa yule ALIYEACHWA azini!. Unaona! Je aliyeacha akioa/olewa?!.. Tusome tena Mathayo 19:9…..Kila mtu ATAKAYEMWACHA mkewe……akaoa mwingine, AZINI, naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Katika ufafanuzi huo, tunaoneshwa kuwa kuacha mke/mme na kuoa/kuolewa tena ni dhambi kabisa mbele za Mungu.

  Uzinzi ni nini?!. Uzinzi ni tendo la mtu mume aliyeoa au mtu mke aliyeolewa anapotoka nje ya ndoa na kufanya ngono na mtu asiye mumewe/mkewe, huo ndiyo uzinzi. Mungu anakataza kabisa kwa mtu anayetazamia kumwona Mungu kufanya huo uzinzi.

  Uasherati ni nini?! Tukisoma katika Mathayo hiyo hiyo 19:9, inatuambia, “Kila mtu atakayemwacha mkewe, ISIPOKUWA NI KWA SABABU YA UASHERATI akaoa mwingine, azini”. Tunapoangalia kwa makini, katika eneo hili, tunaona kuwa Yesu anaruhusu kuoa/kuolewa tena, iwapo mmoja ataonekana amefanya uasherati. Uasherati ni nini tena?! Kwa kifupi, uasherati haufanywi na watu waliooana tayari, bali hufanywa na wachumba au watu ambao hawajaoa au kuolewa bado.

  Uchumba katika biblia haukutajwa sana, isipokuwa kila waliokuwa wachumba, walitambulishwa kama mke na mme. Ndiyo maana sasa tunaona katika Mathayo 1:18 inasomeka; “……Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, KABLA HAWAJAKARIBIANA, alionekana ana mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”. Kabla hawajakaribiana maana yake walikuwa wachumba si ndiyo?!…. Mst. wa 19 tunasoma… “Naye Yusufu MUMEWE kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, ………aliazimu KUMWACHA…….”.
  Hapa tunaona anatajwa Yusufu kuwa ni mumewe Mariamu japo walikuwa wachumba. Lakini pamoja na kutajwa hivyo, bado tunaona Yusufu alitaka kumwacha. Kumbe hatua alizotaka kufanya Yusufu za kumwacha Mariamu mkewe, mbele za Mungu ilikuwa ni halali kwa sababu yule mke alikuwa ni chumba tu; walikuwa bado hawajaanza kushiriki unyumba, hivyo ilikuwa ni halali kumwacha kwa sababu Mariamu alidhaniwa kuwa si mwaminifu.

  Yesu Kristo alipokuwa anawaeleza wale mafarisayo juu ya ndoa, alikuwa anawaeleza waliooana na waliokuwa wachumba bado. Nyakati zake, alipokuwa akitaja, isipokuwa kwa habari ya “UASHERATI” walikuwa wanamwelewa kuwa anazungumzia nini na pia alipokuwa anataja juu ya habari ya “UZINZI” pia walimwelewa alimaanisha nini.

  Kwa ujumla wake ni kwamba, uasherati huhusika na watu ambao hawajaoa/olewa au wachumba. Kama ni wachumba mmoja anapoona mwenzi wake amekengeuka, kimaandiko mwingine anaruhusiwa kumwacha na kuoa/kuolewa na mwingine.

  Uzinzi huhusika na watu waliooana tayati; mmoja anapotoka nje ya ndoa na kufanya ngono, huyo anakuwa anafanya uzinzi, na iwapo mmoja akagundua kuwa mwenzi wake anafanya uzinzi, bado haruhusiwi kumwacha.

  “1Wakorinto 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana NAWAAGIZA; wala hapa si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mkewe; lakini , ikiwa ameachana naye , na akae ASIOLEWE, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”.

  Maneno haya, Paulo anayanukuu katika Mathayo hiyo hiyo 5:32 kwamba kwa waliooana ni mwiko kuachana kwa sababu yoyote ile. Ndivyo Mtume Paulo alivyomwelewa Yesu, na pia ndivyo alivyomaanisha Yesu Kristo.

  Bwana azidi kuwa pamoja nasi, hasa nyakati hizi za mwisho, Shalom.

 6. Ndugu Chuwa na wengine Andiko haliko moja linalozungumza kuhusu hiyo issue. Je kutoka nje ya ndoa hamkusoma? Someni kwa makini na si kwasababu tu kiapo cha “mpaka kifo kitutenganishe” kinatumika ndoa inapofungwa. Yako meeengi zaidi ya andiko hilo kwenye Neno.

 7. Kifo ndicho kiwatenganisha. Zaidi ya hapo ni janja ya shetani kubadilisha maana ya andiko. Katika Mathayo 5:32 na 19:9, Yesu anaruhusu kumwacha mke kwa hoja ya uzinzi. Lakini hakuna anaposema ukimwacha huyo mzinzi uoe. Maana yake ni kwamba umwache lakini wewe ubaki kama ulivyo. Na iwapo utamwacha maana yake ni kwamba wewe umeshindwa kusamehe la hasha ungemsamehe kama neno linavyosema tusamehe hata saba mara sabini usingemwacha. Kuishi upweke ndilo litakalokuwa pigo lako (Ebra. 12: 5-7) vumilia ukimtii na kumpenda Bwana kwa kukurudi mpaka utakapofika kwa Baba au utakapofunguliwa kwa huyo mzinzi kuondoka kwenye uso wa dunia.

 8. Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971,
  Ndoa ya Kikristo haina talaka. Talaka haijaruhusiwa Kibiblia wala kwa sheria za nchi kwa Wakristo. Ukitaka kutoa talaka lazima uwe umeacha Ukristo na kwa ushahidi wa maandishi kwamba wewe siyo Mkristo tena. Soma baadhi ya vifungu vya sheria ya NDOA ili uone sheria inasema nini kuanzia Kifungu cha 9 cha sheria hiyo hasa Kifungu kidogo cha 5. Mkristo akitoa talaka kwa sababu yoyote anavunja sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anaweza kufungwa au kushitakiwa.

  9. Meaning of marriage
  (1) Marriage means the voluntary union of a man and a woman, intended to last for their joint lives.
  (2) A monogamous marriage is a union between one man and one woman to the exclusion of all others.
  (3) A polygamous marriage is a union in which the husband may, during the subsistence of the marriage, be married to or marry another woman or women.
  10. Kinds of marriage
  (1) Marriages shall be of two kinds, that is to say–
  (a) those that are monogamous or are intended to be monogamous; and
  (b) those that are polygamous or are potentially polygamous.
  (2) A marriage contracted in Tanzania whether contracted before or after the commencement of this Act, shall–
  (a) if contracted in Islamic form or according to rites recognised by customary law in Tanzania, be presumed, unless the contrary is proved, to be polygamous or potentially polygamous; and
  (b) in any other case, be presumed to be monogamous, unless the contrary is proved.
  11. Conversion of marriages
  (1) A marriage contracted in Tanzania may be converted–
  (a) from monogamous to potentially polygamous; or
  (b) if the husband has one wife only, from potentially polygamous to monogamous,
  by a declaration made by the husband and the wife, that they each, of their own free will, agree to the conversion.
  (2) A declaration under subsection (1) shall be made in the presence of a judge, a resident magistrate or a district magistrate and shall be recorded in writing, signed by the husband and the wife and the person before whom it is made, at the time of its making.
  (3) The judge or magistrate before whom a declaration is made under this section shall forthwith transmit a copy thereof to the Registrar-General.
  (4) No marriage shall be converted from monogamous to potentially polygamous or from potentially polygamous to monogamous otherwise than by a declaration made under this section.
  (5) No marriage between two Christians which was celebrated in a church in Christian form may, for so long as both the parties continue to profess the Christian faith, be converted from monogamous to polygamous and the provisions of this section shall not apply to any such marriage, notwithstanding that the marriage was preceded or succeeded by a ceremony of marriage between the same parties in civil form or any other form.
  12. Duration of marriage
  A marriage, whether contracted in Mainland Tanzania or elsewhere, shall for all purposes of the law of Mainland Tanzania subsist until determined–
  (a) by the death of either party thereto;
  (b) by a decree declaring that the death of either party thereto is presumed;
  (c) by a decree of annulment;
  (d) by a decree of divorce; or
  (e) by an extra-judicial divorce outside Tanzania which is recognised in Tanzania under the provisions of section 92.

  15. Subsisting marriage
  (1) No man, while married by a monogamous marriage, shall contract another marriage.
  (2) No man, while married by a polygamous or potentially polygamous marriage, shall contract a marriage in any monogamous form with any other person.
  (3) No woman who is married shall, while that marriage subsists, contract another marriage.
  (4) Nothing in this section shall be construed as preventing the parties to a marriage to go through another ceremony of marriage:
  Provided that where parties who are already married go through another ceremony of marriage, such subsequent ceremony shall not, subject to the provisions of subsection (5) of section 11, affect the status or the legal consequences of their first marriage.

  Mwanamke akimwacha mumewe na akaolewa na mwingine, lazima ushahidi uwepo kuwa huyo mwanamume kamwoa kisheria au kamuiba tu. Je wakati anamwoa huyo aliyekuwa mke wako ulipata taarifa za tangazo la ndoa na ulitoa pingamizi mahakamani likakataliwa? Unaweza kufungua mashitaka dhidi ya huyo mwanamke au mwanamume aliyeingia makubaliano ya ndoa wakati wewe hujatoa talaka na kwa kuwa wewe ni Mkristo talaka ni MWIKO KISHERIA na KIBIBLIA PIA. Soma vizuri vifungu hivyo vya sheria ya ndoa, kama utakuwa na maswali nipigie tuongee zaidi: 0767 285417
  Mr. V. Milinga, KIGOMA.

 9. Ndugu John swala hapa sio mamlaka ya kuoa ila ni jambo linalohitaji unyenyekevu wa hali ya juu sana mbele za Mungu kwa huyo mwanaume aliyeachwa. Kwa nini unyenyekevu? kwa sababu yeye anaweza kuwa sababu ya mke kukimbia. Anahitaji ushauri wa watumishi wenye roho ya Mungu soma Mwanzo 41:38: ndivyo Mungu alivyojiwekea roho yake ndani yao apate kuwasaidia wenye matatizo kama huyo aliyeachwa.

 10. Aggrey kifo hapana kwani mke ameondoka na kwenda kuolewa na mume mwingine. Je? Mke yule atahesabiwa na waume 2 ? Nafikiri mke akiolewa na mume mwingine basi mume aliyeyaachwa ana mamlaka ya kuoa mke mwingie!!!!!!!!!!!!!

 11. 1.0 Mtu amwachaye mke au mme akaoa au kuolewa na mwingine huyo anazini.

  2.0 Yesu alisema si halali kumwacha mke isipokuwa kwa uzinzi waweza kumwacha. Huyo mwanamke anayeolewa na mme mwingine akaacha mme wake anazini na wala huyo mume hana uwezo wa kwenda kumrudisha maana hapo atakuwa anaingia katika vita ambayo kwa mkristo hatakiwi kupigana. Kwa hapo ni halali kabisa mme kuoa mke mwingine. Lakini angalizo ni hili:

  Kumbuka makanisa yetu yamewatesa sana washirika wao kwa kusema ” alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe” Mathayo 19:6 (kumbuka Neno laweza kuua na kuhuisha ole wako likikuua) Maana yake ni hii: Mwanaume huyo hatakiwi kuoa hadi yule mwanamke atakapokufa.

  Kwa taarifa, huyu mwanaume usiku na mchana atakuwa anawaza lini huyu mwanamke atakufa maana atamchukia kwa kumkimbia? Kwa maneno mengine huyu mwanaume ataanza kufanya dhambi ya kuua na hivyo hatakwenda mbinguni hata akifa leo hata kama ameokoka ananena kwa lugha zote maelfuelfu za mbinguni. (1Yohana 3:15).

  Lakini jambo moja la kujifunza ni hili, hivi kuna mwanadamu aliyewatenganisha huyu mwanaume na mkewe? Mimi ninaona si kweli!! Hayuko mwanadamu anayeweza kusema” ninyi wanandoa achaneni” Halafu wakakubali kuachana, kusudi iweje? Ninachoona dhambi ndiyo iliyowatenganisha na si mtu. Kama ni hivyo tutaihukumu namna gani hiyo dhambi ili huyu mwanaume awe huru? Mwanaume huyu afakiri sana juu ya kuihukumu hiyo dhambi

  3.0 Wakristo wengi wameng’ang’ana na maneno ya Mt. Paulo ya
  1 Wakorintho 7, kumbuka mtume Paulo alikuwa akijibu maswali aliyoulizwa na waumini wa mji wa Korintho. Na mengi ya majibu yake alisema hayo ni maoni yake. Shika sana maneno aliyosema Yesu Mathayo 5:32 na 19:9

  Lakini je aende na kuoa mke mwingine sasa! sasa!? La hapana anayo mengi ya kufanya kabla ya kufikia uamuzi huo

  i) Lazima kushauriana na wakuu wa kanisa lako, wakikufunga kwa mistari ya moyo kubali ufe katika hayo na mbingu ama uikose au uipate.

  ii) Aombe ushauri kwa wajuzi wa neno maana ninakwambia huyo aliyeachwa na mke hatakuwa na ibada na Mungu hata siku ya kuingia kaburini maana aweza kufa kabla ya mke kufa.

  Ibada ni muhimu sana kwa mwanaume ndiyo maana Mungu alipoona Adamu anasumbuliwa na upweke ” maana kulikuwa na wanyama lakini hakuwepo wa kufanana naye” akasema “si vema mtu huyu akae peke yake tutamfanyizia msaidizi wa kufanana naye” Na bila ibada si rahisi kuiona mbingu maana ibada inaanzia katIka ndoa.

  iii) Kutokuoa kutamfanya asifike mbinguni, maana maisha yake yote anakuwa amejaa majeraha ya ndoa ambayo lazima yatampelekea kutenda dhambi zaidi. Furaha ya moyo itakuwa hakuna, sikuzote atakuwa anamlaumu huyo mke aliyemwacha.

  Kumbuka Mungu hakumuumba mwanadamu aje duniani apate shida, la hasha ila ashiriki baraka alizoziweka duniani azae kwa furaha, amwabudu na kumfurahia Mungu.

  Katika yote linahitajika neno la ufunuo na la hekima ili kumtoa huyo jamaa katika mzigo alio nao. Na neno hilo liko na wale watumishi wenye uwezo wa kusimamia maneno magumu aliyosema Yesu mfano:
  “Sikuja kuleta amani bali nalikuja kuleta upanga, yaani wao wanasema Yesu sio wa amani.” Mathayo 10:34

  Hao ambao wana neno la ufunuo juu ya tatizo hilo na awatafute hao watampa ufumbuzi nao si wengine ila ni MITUME NA MANABII na Tanzania tuna bahati kubwa maana tunao. A contradiction?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s