‘Yesu’ Atua Dar!

Mwigizaji wa sinema za Yesu Randy Brooks ametua nchini kwa ajili ya kuonesha maigizo mawili katika kanisa la City Christian Centre lililopo Upanga jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Brooks alisema atakuwa na maonesho mawili yatakayooneshwa kwa siku mbili katika kanisa hilo.

“Onyesho moja tutaonesha leo na jingine litakua kesho katika kanisa hilo na maonesho hayo pia kutakua na huduma nyingine za uponyaji na maombezi” alisema Brooks.

Akizungumzia sababu ya kuamua kuigiza maisha ya Yesu Kristo alisema haikua rahisi ulimwengu kukubaliana na maandiko juu ya maisha ya Yesu, tangu kuzaliwa kwake hadi kufa kwake:

“baada ya kutafakari kwa kina juu ya suala hilo ndipo nilipoamua kuigiza maisha ya Yesu, ili kuuweka ulimwengu pamoja na kutafakari upya juu ya binadamu kuishi maisha yanayompendeza Mungu, wanayopaswa kuishi hapa duniani”

Msanii huyu wa Kimarekani, maarufu kama Yesu, ameambatana na kikundi chake chote huku kivutio kwa watu wengi katika kikundi hicho akiwa ni kijana aliyeigiza kama shetani.

Akiwa na msafara wa watu 120 ambao wote wanashiriki katika kuigiza maisha ya Bwana Yesu kama ambavyo waumini wa dini ya Kikristo wanavyomtambua, Brooks alisema kuwa ameamua kuzunguka dunia nzima akiwa na kundi lake hilo ili kujitambulisha moja kwa moja kwa watu wasio mfahamu.

SOURCE: Mwananchi, Jumanne Julai 12, 2011.

—————————————————————————

More than 100 actors from US performing live in Tanzania

Dates

July 14th – 7:00 pm
July 15th – 3:00 pm and 7:00 pm
July 16th – 3:00 pm and 7:00 pm
July 17th – 7:00 pm

Venue: City Christian Center
Olympio Street, Dar es Salaam
(Opp Mzumbe University Dar es Salaam Campus)

Entrance Fee: FREE

Get your Free ticket today at City Christian Center or Ubungo TAG.
Or call 0655 100 200

http://thepromisenewyork.c​om/

Advertisements

9 thoughts on “‘Yesu’ Atua Dar!

 1. Bwana asifiwe nashukuru leo kuona apa kwetu Danmark nimeona mutu moja pia anapoingiya kwenye iyi Blog ya kutafuta USO ya Bwana pale ku capital Købenavn ndugu kama umenisoma mimi unijibu mimi niko apa Århus Town ya pili apa Danmark

  Mungu apewe sifa

 2. Labda niulize je ni wangapi wetu wamewahi kuangalia sinema ya Musa au David and Goliath…? Nimeona kama si kwa watu wazima basi watoto wadogo wengi iliacha kumbukumbu isitofutika kuliko hata mafundisho wanayoyapata katika madarasa ya Sunday school makanisani….!

  Kuna kipindi nimewahi kufanya huduma na shirika fulani la wamissionary…..na mojawapo ya umisheni wa huduma hii ilikuwa ni kuonyesha picha ya maisha ya Yesu vijijini au ningesema maporini…ambako hakuna shule…….wala makazi ya kudumu…hasa kwa makabila ambayo yana hama hama…..Kwa kifupi Picha ya maisha ya Yesu ilikuwa ni kivutio kikubwa sana…..na baada ya kuionyesha ilitolewa nafasi ya watu kumpokea Yesu……wengi walimpokea Yesu na tuliweza kuanzisha makanisa katika mapori hayo…….!

  Nadhani hii ni sehemu ya Injili kuhubiriwa kila mahali…..tukumbuke katika Tanzania yetu kuna sehemu zisizofikiwa bado na Injili…..na vigumu kabisa kumfanya mtenda kazi wa Bwana akaweka makao ya kudumu hapo kwa sababu makabila hayo ni wahamaji! Je wataisikiaje Injili watu hawa? Hebu angalia mfano wa baadhi ya wasukuma (sina nia kabisa ya kudhalilisha) AMBAO baadhi yao wanaanza kuhama na mifugo toka Shinyanga…..kuingia Tabora misitu ya Ugalla hadi kufika Mpanda……na hadi kutelemkia Chunya na kufika hata Rukwa…….! Wafugaji hawa wanahama na familia zao….na mara nyingi hawafuati barabara….wao hukatisha maporini tu! Hivyo huduma ya Wamisheni hao ilikuwa ni kuwafuata kwa Pikipiki…au hata kufyeka njia ili gari kama Toyota Landruise Liweze kupita …..na kila wanapoweka makazi wanaonyesha Picha Yesu na kuwahubiria Injili….!Kuna wakati wamiisionary hawa walifuata wahamaji hawa hadi mpakani na Zambia……namfahamu Mtanzania na Mmarekani ambao walifanya kazi hiyo……!

  Hivyo wapendwa Injili inahubiriwa kwa njia nyingi mno! Niko Marekani kwa sasa, na majuzi nimekutana na Mmarekani anayejifunza Kimakonde……anasema kati ya maeneo ya kusini mwa Tanzania na Msumbiji kuna watu hawajasikia Injili….lengo lake ni kuitafsiri Biblia katika lahaja mojawapo ya Kimakonde !

  Hivyo kama picha ya Yesu imefikisha wa watu kumjua Yesu tumshukuru Mungu maana ndivyo Bwana alivyotuagiza…….tusifungwe na wigo mmoja wa kuitangaza Injili……..!

  Huku Marekani watu kutoka Korea wanakuja kwa wingi…..na wengi wao ni kuwafikia Wamarekan kwa Injili…….ambayo Wakorea hao wanaamini kwamba Mungu asipotenda jambo Marekani licha ya heritage yake ya Ukristo inaenda kubaya, Hasa UAMSHO usipopita katika nchi hii!…….na vile vile Korea kina dada wengi waliiokoka wanaomba kazi za nyumbani (Uhausi geli) Japan kwa lengo moja Kuhubiri Injili…..kwani wameona njia rahisi kabisa ya kuwaingia Wajapan ni kuishi nao katika familia zao kama yule Mtumishi Wa Naaman……na kuwaeleza Habari ya Kristo!

  Jumapili moja nimekutana na Mganda mmoja alisikia wito wa kuhubiri Injili Saudi Arabia…..kwa hiyo alijifunza Kiarabu na akasoma Uinjinia na Kuomba kazi Saudia…..alipata…na akaanza kuihubiri Injili kwa wafanyakazi wenzake kwanza KWA kuiishi…..kusoma Biblia….na waarabu wakaanza kumgeukia Yesu…….alipogunduliwa……ilifungwa na baada ya kuombewa sana Msamaha na balozi wa Marekani huko Saudia aliondolewa na sasa ameletwa Marekani kuwahubiria wakimbizi wa Sudan wanaokuja kuishi Marekani.

  Hivyo wapendwa kuna njia mbali mbali za kufikisha ujumbe huu wa thamani…….

  Bwana na ATUBARIKI.

 3. Ndugu zangu wapendwa,wakati wote wa huduma ya YESU na mitume walilihubiri neno na kusema ,siyo kuigiza Math 4:17,mdo 2:14,38.2timo 4:2.kiumbe kujifanya YESU ni kufanya uongo kuna kusema uongo na kufanya uongo UFUNUO 22:15 ni dhambi kabisa ni sawa vinyago vya bikra mariam nk.YESU amesema tusifanye kitu chochote kwa mfano wake KUMB 4:12-19 ndugu zangu hali hii imepelekea imani kuwa na utata na Mungu kudharauliwa,ebu tuhubiri neno ambalo ni panga hata kipofu atatubu bila kuona igizo. Tusijikute tunaingia kwenye mtego wa ibilisi, kwani roho hii imewavaa wakristo wengi na kuwa waigizaji lakini mioyo iko mbali na Mungu.hizi ni nyakati za mwisho tuwe makini.mbarikiwe

 4. Mpendwa John Paul naomba nisaidia kutoa mawazo yangu kwa maswali yako uliyouliza ambayo mimi nayaona ya muhimu sana japo nitajibu swali la (ii) tu.

  Igizo ni sawa na masimulizi ambayo yamewekwa kwenye matendo badala ya maneno. Wapo watu wengi sana duniani ambao hawana fulsa kabisa ya kusoma biblia kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwa na hisia zozote akilini za kuisoma hiyo biblia. Ni rahisi sana kwa mtu ambaye hajaamini kukaa chini na kuangalia igizo la Yesu na kuona ni upuuzi kukaa chini na kuisoma biblia

  Kwa hiyo kupitia igizo hilo wapo watu wengi sana ambao wamepata ujumbe kwamba yupo anayeitwa Yesu, alitenda miujiza, alisulubiwa, alikufa, alifufuka na akapaa kwenda kwa Baba.Mbegu imepandwa mioyoni mwao, yaani habari za Yesu (Injili) wamezisikia.

 5. Nukuu:

  [[[Akizungumzia sababu ya kuamua kuigiza maisha ya Yesu Kristo alisema haikua rahisi ulimwengu kukubaliana na maandiko juu ya maisha ya Yesu, tangu kuzaliwa kwake hadi kufa kwake:

  “baada ya kutafakari kwa kina juu ya suala hilo ndipo nilipoamua kuigiza maisha ya Yesu, ili kuuweka ulimwengu pamoja na kutafakari upya juu ya binadamu kuishi maisha yanayompendeza Mungu, wanayopaswa kuishi hapa duniani”]]]. Mwisho wa kunukuu.

  Pamoja na michango iliyoandikwa na wachangiaji waliotangulia, mimi wazo langu ni juu ya maneno hayo niliyonukuu hapo juu. Baaa ya kusoma maneno hayo nilipata maswali kadhaa, kama vile:

  i). Ni kwa kiasi gani ulimwengu umekubaliana na maandiko juu ya maisha ya Yesu KWA SABABU YA IGIZO HILO?

  ii), Je! Kuwepo kwa igizo hilo kumerahisha au kumeongeza kwa kiasi gani kuenea kwa injili ya Yesu Kristo?

  iii). Je! Ni kweli kuwa Igizo hilo limeuweka ulimwengu pamoja, kama ambavyo Brooks anadai?

  Hayo ni baadhi ya maswali ambayo nimekuwa nikitafakari baada ya kusoma maneno hayo!

 6. Jamani hivyo ni vichwa vya wanahabari kuuza magazeti, hawana maana ya kusema Yesu mwana wa Daudi.
  Hata hivyo Yesu siku zote tuko nae Dar!

 7. kweli naungana na hao jamaa waliopinga matumizi ya maneno yaliyotumiwa na waandishi kuhusu ujio wa brooks,sio sahihi”yesu atua dar,ni upotovu wa matumizi ya maneno hasa yanayohusisha”UUNGU.

 8. Brooks sio Yesu na hana hata chembe ya uhalali wa kuitwa Yesu. Tutumie lugha ambayo itamwacha Brooks kuwa mwigizaji na Yesu kuwa Yesu.

 9. Nafikiri si vyema tukisema Yesu ametua Dar, nafikiri tusema Yule mtu aliyeigiza filamu ya Maisha ya yesu atua Dar. Yesu hajatua Dar, Yesu akishuka Dar, unafikiri huu mji utakuwaje, patakuwa hapatoshi,

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s