Ujumbe wa Matumaini!!

Ndugu, dunia imeoza na imepoteza matumaini yote. Watu wanahangaika na hawana amani ya kweli. Wengi wanajitahidi tu kuishi maisha bandia. Ndio maana Biblia inasema “wote wamepotea, wameoza wote pia, hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawaijui.” (Warumi 3:9-18).
 
Watu wamechanganyikiwa na hawana amani maishani. Si watoto, si wakubwa. Si wanaume, si wanawake. Si wanafunzi, si walimu. Si matajiri, si masikini. Si viongozi wa serikali, si raia n.k. Biblia inasema wala njia ya amani hawaijui. Huu ukosefu wa amani husababishwa na dhambi! Watu wamepoteza mwelekeo wa maisha na amani ya kweli. Wapo matajiri wanaokumbwa na matatizo ambayo kila wayafikiripo husema, “bora kuwa masikini”.
 
Watu hukimbiza upepo usiku na mchana na hukusanya hela nyingi, lakini mwisho wa siku pesa hizo huyeyuka na kupeperuka pasipo wao kuzifanyia kazi yeyote. Wengine hukosa usingizi kabisa. Usiku kucha husumbuliwa na mapepo na ndoto za kutisha. Watu wengi huishi na magonjwa ya kutisha kama sehemu ya miili yao. Leo hii watu wengi wana wasiwasi na afya zao kwasababu ya maisha yao ya zinaa. Tena imeandikwa, mshahara wa dhambi wa ni mauti’ (warumi 6:23). Usisubiri mtu atoke mahali na kisu au bunduki kwaajili ya kukuua, ila dhambi hiyohiyo uliyonayo ndiyo itakayo kuua (roho, nafsi na mwili). Tendo moja la uasherati au uzinzi latosha kukuzawadia na virusi vya ukimwi papohapo pasipo kupoteza muda. Maisha ya ulevi, maisha ya uongo, maisha ya wizi, maisha ya rushwa, maisha ya uasherati, maisha ya ya uchawi, maisha ya utukunaji, maisha ya ulawati, maisha ya ufiraji, maisha ya usagaji, maisha ya usengenyaji, maisha ya ufisadi, maisha ya kuabudu sanamu n.k. ni maisha ya mtu aliye chini ya laana na umauti.
 
Yawezekana umejitahidi kwa jitihada zako zote kuacha dhambi lakini umeshindwa, na kila unapotizama maisha yako ya nyuma huoni tumaini lolote mbele yako. Labda umefanya sana zinaa na kuvuna kwaajili yako magonjwa yanayokutesa usiku na mchana na kukuondolea furaha kila dakika. Na labda hujui kwamba unaweza kusamehewa, kuponywa na kurejeshewa hali ya afya, amani, na matumaini. Tumaini la pekee kwaajili yako lipo kwa mtu mmoja ‘YESU KRISTO.’ Mkaribishe Yesu maishani mwako akuokoe na kukubadilisha bila kuwaza watu watakufanyaje. Baba, mama, mume, mchumba, mjomba, shangazi, rafiki n.k. hawana uwezo wa kukuokoa endapo roho yako itahitajika leo kwenda kukabiliana na hukumu ya Mungu (yaani kufa). Kwa maana na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kifo hukumu (waebrania 9:27).
 
Sikufahamu rafiki, ila nataka kukwambia kwamba Mungu anaweza kubadilisha picha nzima ya maisha yako kwa asilimia mia moja endapo utatubu na kuamua kumtii katika kila jambo. Imeandikwa, Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.”(Matendo 3:19). Haijalishi wewe ni nani na unatokea wapi. Uwe mtoto, kijana, binti, mwalimu, mwanafunzi, mwanasiasa, daktari, n.k. waweza fanyika mtu mpya leo. Na kwa ujasiri na uhakika uweze kujiunga na mzaburi na kusema, “Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai!.”(Zaburi103:2-5)
 
Unaweza kupata wokovu na uponyaji sasa kwa kusali sala ifuatayo na kutubu toka moyoni mwako, Bwana Yesu, nakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi kwa asili na kwa kutenda, na ninastahili kuangamia kwasababu ya dhambi zangu. Hata hivyo ulisulubiwa msalabani kwaajili yangu ili nisiteseke sasa na hata milele. Kwa hivyo, Bwana naomba unisamehe na unisafishe toka kwenye dhambi zote. Ingia moyoni mwangu na ubadilishe maisha yangu tangu sasa. Ahsante kwa kuwa umenisikia. Ahsante kwa wokovu wako Bwana katika Jina la Yesu Kristo, Amen.’
 
Kama umesali sala hii kwa uaminifu basi Yesu amekusamehe na kukufanya mtoto wake sawia. Wasiliana nami mara moja ukinieleza juu ya Wokovu wako kwa kutumia anuani ifuatayo.          
 
Takwa David Paul.
Advertisements

5 thoughts on “Ujumbe wa Matumaini!!

  1. @Lwitiko Katule: Amina kaka, Mungu akubariki kwa kusoma ujumbe wote na kuwa na mzigo kwaajili ya wengine. Usijali nitumie anwani yako, nikutumie huu ujumbe. Mungu akubariki.

  2. @ OLOMBI MONGA: Ubarikiwe rafiki kwa kusoma ujumbe mzima na kufuatisha sala ya kumkaribisha Bwana Yesu maishani. Usijali kwani vile umeamua kumkaribisha moyoni, atakulinda mpaka mwisho wa safari. Ishi kwa nguvu zake tangu sasa. kwa maombi na ushauri zaidi, nitapatikana endapo utahitaji.

  3. Amina mtumishi wa Mungu Daudi, ujumbe mzuri sana, kwa kweli huwa napenda sana kuisikia hii injili ya toba na msamaha wa dhambi kwa kweli ambayo wakristo wengi waliokoka wameiacha, ubarikiwe sana, pia naomba ruhusu SG waniruhusu nipate kuichukua na kuiweka kwenye computer yangu ili niweze pia kuihubiri, ni maneno mazuri sana ya injili ile ya uzima wa milele.

  4. Bwana asifiwe. Kwa kweli mambo yote nimesoma ni juu.yangu mwenyewe aksati Kwa sala hiyo na Bwana Yesu aongoze maisha yangu hadi siku ya kurudi yake. Nashukuru na katika imani Kwa yote

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s