Kufunguliwa kutoka katika ndoa ya mapepo au majini mahaba!

Biblia inatuambia:

“Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti yaani,Mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na tanzi na mikono yake ni kama vifungo; Yeye ampendezaye mungu atamponyoka,bali mwenye dhambi atanaswa na yeye“(Mhubiri 7:26)

Mpendwa mapepo dume na mapepo jike yapo na ni halisi.pepo mahaba dume kwa kiingereza linaitwa incubus. Pepo jike linaitwa sacubus. pepo dume linauwezo wa kulala na mwanamke kadhalika na pepo jike lina uwezo wa kulala na mwanaume katika ndoto. Mapepo mahaba yanatoka baharini au kwenye mito au kwenye maziwa.(wote niwatendakazi wa shetani asili yao kuzimu)kuna wanaume ambao wameoa katika hali halisi na pia wameoa katika ulimwengu wa roho.hivyo kunauwezekano wamtu kuwa na mwanamke katika halihalisi na kuwa na kuwa mwanamke katika ulimwengu wa roho. Solomoni anasema “Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti,yaani mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na tanzi,na mikono yake nikama vifungo; yeye ampendezaye mungu atamponyoka,bali mwenye dhambi atanasw na yeye” (Mhubiri 7:26).

Andiko hili linatuonyesha picha ya utendaji kazi wa mapepo mahaba.Na haya mapepo yapo katika jinsia zote.kwahiyo ukipenda dhambi utanaswa na ukichagua kumpendeza mungu utaponyoka.uamuzi ni wako kunaswa au kuponyoka (nimeshakupa maarifa). Mungu akusaidie uponyoke ndiyo sababu nimeleta kwako samo hili iliujue dalili za mapepo mahaba na ufunguliwe kutoka katika kifungo cha ndoa za mapepo mahaba. Pepo mahaba ni pepo awezaye kumtawala mwanaume au mwanamke katika ulimwengu wa roho, pepo huyu mchafu ana madhara mengi sana mfano kuzuia kushika mimba au kuharibu mimba,au kuzuia kuoa au kuolewa (kuvunjika uchumba/ndoa) pepo mahaba hujidhihirisha katika ndoto,kwani mtu aliyenaswa na pepo mahaba huota ndoto akifanya ngono.

UTAJUAJE KAMA UNA VIFUNGO VYA KIPEPO MAHABA/JINI MAHABA?

Unaweza ukawa umeoa au hujaoa / umeolewa au hujaolewa katika hali halisi.

UNAJUAJE KWAMBA UNAHITAJI HUDUMA YA KUFUNGULIWA KUTOKA VIFUNGO VYA MAPEPO MAHABA?

Ilikujibu swali hili ngoja tuone dalili za mapepo mahaba katika maisha ya watu mbalimbali.Kwa ufahamu huu utajua kwamba unahitaji huduma ya kufunguliwa.

DALILI ZA MAPEPO MAHABA

1.Kuchoka katika ndoa – Kabla ya kuoa au kuolewa kila mtu alikuwa na shauku ya kufurahia ndoa.lakini baada ya muda mfupi wanandoa wamechokana na ndoa imekosa ladha.Wakati mwingine mwnandoa mmoja anamchoka mwenzi wake.Kama ungepewa nafasi ya kuamua kwaupya huenda usingekubali kuolewa na mwanaume huyo au kuoa mwanamke huyo. Mpendwa msomaji kama unajisikia kuchoka ndoa hiyoni dalili ya kuwepo kwa mapepo ya mahaba tafuta msaada wa huduma ya kufunguliwa

2.Kufanya tendo la ndoa au mapenzi kwenye ndoto na mtu unayemfahamu au usiyemfahamu.

3.Kuchukia kuoa au kuolewa (unajuta kama usingeolewa au usinge oa)

4.Kufanya maamuzi yasiyo sahihi wakati wa kuoa au kuolewa. Kuolewa au kuoa  mtu asiye sahihi.

5.Kuachwa na mume au mke.Kila mwanamume akikuoa baada ya muda mfupi anakuacha.Ujue unamapepo mahaba yanayofukuza wanaume katika maisha yako.Unakuta mwanamke mzuri amesoma na ana (uwezo) kazinzuri lakini anaachwa na wanaume au anatelekezwa na wachumba hapo unahitaji huduma ya fufunguliwa.

6.Kuchukia mahusiano ya kindoa na mumeo au mkeo.Wakati usiku unatembelewa na mapepomahaba.

7.Kunyonyesha watoto kwenye ndoto wakati huna mume wala mchumba /au umeolewa na huna mtoto kabisa! Ni dalili ya kifungo cha pepo mahaba.

8.Kuogesha watoto kwenye ndoto wakati hujaolewa ni dalili mapepo mahaba.

9.Kuota una familia kwenye ndoto wakati hujaolewa / au kuoa na wala huna mchumba.

10.Kuota unafanya shopping na mwanaume au mwanamke wakati hunahata mchumba.

11.Kumchukia mwenzi wako kiasi cha kutamani afe ili uoe au uolewe na mtu mwingine.

12.Kuota wanawake au wanaume wako uchi,au wewe mwenyewe kujiota ukouchi.

13.Wanandoa kuota mwanaume au mwanamke yuko katikati yenu au pembenimwa kitanda chenu wakati mmelala.

14.Mwanaume kukosa nguvu na kushindwa katika tendo la ndoa.

15.Mwanamke kupata maumivu makali sana wakati wa hedhi (maumivu makali ya tumbo)

16.Matatizo ya mfululizo ya magojwa ya kike mfano ya tumbo la uzazi,kuziba mirija ya uzazi.

17Kuotaunabakwa ndotoni.Kuharibu mimba baada ya kuota unafanya tendo la ndoa.

18.Kujutia kuoa / kuolewa bila sababu ya msingi

19.Kukosa hamu / moyo wa kuambatana na mwezi wako.Hujisikii tena kuongea na mwenzi wako wa ndoa unapenda kucheka na wanawake / wanaume wengine kuliko mwenzi wako hizi nidalili za kifungo cha pepo mahaba tafuta msaada wa kufunguliwa haraka upone!.

20.KIla wakati kuwaza kwamba ndoa itavunjika unapotazama miaka miaka mitano ,kumi huoni kudumu kwa ndoa yako hata hapo ulipo unaonakama muujiza.

21.Kukosa utoshelevu w moyo kat ika ndoa uliyonayo.

22.kama ni msichana huoni kijana yeyote aliye wahi kukusemesha kwamba atakuoa ujue maranyingine hata wachawi wanaweza wakawa wamekufunga.

24.Kupewa ahadi za kuolewa bila kutimiwza / kama hakuna anayemaanisha unahitaji huduma ya kufunguliwa.

25.Kuachwa baada ya wanaume kuujua mwili wako au kuchukiwa baada ya mwanaume kulala na wewe.

26.Kucheza na nyoka ndotoni wala hung’ati hili sijambojema ni hatari.

27.kubakwa mara kwa mara katika halihalisi.

28Kumpamimba msichana mwingine halafu unaoa mwanamke mwingine.

29.Mchumba kufariki kabla ya ndoa (kufaghafla mipango ya harusi imeandaliwa)

30.Kuachiswa kazi au biashara kufa mara baada ya kuoa au kuolewa.

31.Kupata ajalimba ya baada tu ya kuoa au kuolewa.

32.Mwenzi wako hakubaliani nawewe katika jambololote mnalopanga (anakuwa mpinzani tu!)

33.Kila mwenzi anaye kuoa au unaye muoa anakufa

34.Kuwa na uamuzi wa kutoolewa au kuoa kwa kuogopa matatizo ya ndoa (hofu ya ndoa).

35.Mwenzi kutokukujali wakatiunaumwa unajihudumia mwenyewe hadi unapona nayeye yupo hata ulalamike maumivu anaendelea na shughulizake bila kujali.

36.kupigwa mara kwa mara bila huruma na mume wako.

37.kutishiwa kufukuzwa mara kwa mara na mumewako.

38.Kupotelewa na pete ya ndoa au cheti cha ndoa ktk mazingira ya kutatanisha.

39.Kupewa pete za mapenzi na waganga wa kienyeji au wanajimu.Vua hiyo pete katika jina la yesu ni antena / agano la kuvutia mapepo katika maisha yako.

40Kujuta kuolewa au kuoa mwenzi huyo.

41.Kupanga kwamba niki rudi nyumbani tu nitapokeana na mwenzi wangu kwa furaha ghafla unawasili unaingiwa na chuki moyoni juu yake.

42.Kuchelewa kurudi nyumbani bila sababu ya msingi (Baada ya ndoa mwenzi wako anabadili tabia ghafla).

Sura yako kuonekana mzee kuliko umri wako.

43.Kutokwa damu sana au kwa muda mrefu wakati wa hedhi kukiambatana na maumivu makali (maranyingine siku zinzkuwa za mvurugiko mvurugiko).

44.Unakuwa na roho ya liwalo na liwe hujali ndoa yako hata ukishauriwa hushauriki.

45.Kutokupata mimba katika ndoa yako hata vipimo vya kidaktari vikionyesha huna tatizo au kuharibika mimba mara kwa mara.

46.kutengana kwa wana ndoa hata ingawa mnakaa nyumba mmoja (mzungu wa nne) kila mtu ana chumba chake.

47.Tumbo lako kuonekana unamimba hata watu wana kuona hivyo wakati hauna.

48.Matiti kutoa maziwa wakati huna mimba wala mtoto.

49.Kujisikia mjeuri,hasira,ukaidi kutokuelewana ktk ndoa.

50.Kuonywa na mtu ktk ndoto kwamba hutaolewa.

51.udhihirisho wa wazi wa mapepo mahaba wakati wa usiku.

52.kukumbuka mahusiano ya mapenzi na rafiki zako wa zamani wakati una mkeo / mumeo kitandani.

53.Kujichua au kujiridhisha mwenyewe bila mwenzi usiku au bafuni.

Mpendwa msomaji hizi ni dalili kadhaa ktk nyingi kama unaona hapo ikosehemu inakugusa tafuta mahala penye huduma ya kufunguliwa upone, haya mapepo machafu yana leta hata kukufanya uwe unaishiwa kila mara hata ungekuwa na pesa ya kutosha wewe mda mchache huna kitu, amani katika ndoa ni ndogo sana ni hekaheka tu!na kama kuoa au kuolewa kuna zuiwa na haya niliyo kupa mbinu jinasue ktk jina la Yesu !

Njia kubwa ni umpe Yesu maisha yako. Na usiogope hata wewe ambaye ulisha mpa Yesu maisha yako kama una dalili hizi nenda kafunguliwe sio dhambi kufunguliwa uweze kuoa / kuolewa. Na uliyeko katika ndoa ikiwa na mambo ya jinsi hii hauko salama hata kidogo kafunguliwe uweze kufurahia ndoa yako katika Jina la Yesu.

Frederick D Marandu

Advertisements

68 thoughts on “Kufunguliwa kutoka katika ndoa ya mapepo au majini mahaba!

 1. Jamani hebu tuweni na moyo wa kumwogopa ama kumwamini MUNGU, maana kwa IMANI ” twaweza kumushinda shetani.
  Tuweni na Imani ilituweze kumushinda shetani.

  Tunashukuru kwa mafundisho yako mpendwa ,
  nauzidi sana ktk kazi ya Bwana.
  UBARIKIWE.

 2. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,mimi naona shida ni kutokulielewa neno na imani za watu wengi zimepoa wapo makini kuamini hadithi za kidunia kuliko mtu awambie mambo ya rohoni kwavile tu hawayaoni watapinga na pia unaweza ukajiona uko sahihi kwa Mungu kumbe ndo unapotea kwa ukaidi wako,pinga san lkn ukweli wa Mungu utabaki palepale.Mubariwe.

 3. kwa kweli wanaobisha hii mada ya kufunguliwa katika vifungo vya mapepo na majini ni vile tu hawajakutwa na hayo mambo na waombe Mungu awaepushe nayo coz wakiyapata ndio watajua kua yapo au hayapo mara nying ucijifanye mjuaji sana kwenye mambo haya its not good kwakweli Mungu awasaidie’

 4. ukisoma yohana 1 utaona kuwa yesu alileta uzima na nuru kwa wanadamu,nayo hiyo nuru iling’aa giza halikuweza kuishinda..kama yesu alileta nuru kwako kwa njia ya wokovu na bado giza linakuandama,ujue bado kunasehemu umeachia mwanya wa giza kuingia.neno pia linasema pepo mchafu amtokapo mtu haenda mbali anazunguka kisha anarudi kama umerudi gizani anakuvaa na kualika wenziye wabaya kama yeye.kama tumepokea nuru ya yesu na kuenenda ktk nuru hiyo na kujishughulisha kutenda mema nini basi kitatuzuru?jibu ni hakuna.

 5. Nimesikitika sana kuona baadhi ya watu wanatoa comments ambazo hazioneshi ni wakristo.Namshukuru sana mtumishi wa Mungu Bwana Marandu kwa kueleza vizuri kuhusu dalili za mtu mwenye Jini mahaba na nimefurahi sana kwani matatizo mengi ambayo ndoa inakumbana nayo ni kutokana na mapepo na majini kuingilia wanadamu. Wengi wenu hapa inaonekana hamjaelewa kabisa anachozungumzia.Naona kabla sijaendelea niwaulize maswali mawili ya msingi
  1. Daktari aweza kumtibu mgonjwa bila kuona dalili za ugonjwa?
  2.Daktari anaweza kuja kukutibu kama hujamfuata na kumweleza shida zako?
  3.Dakatari anaweza kumpa mtu dawa bila kujua ana ugonjwa gani?
  Napenda kuendelea kwa kujibu maswali hayo hapo juu.Ni vigumu sana daktari kuitwa daktari kama hajui aina za dawa.Yesu Kristo Peke yake ni Dawa ya matatizo ya wanadamu.Je waweza kumtumia Yesu Kristo kuponya ndoa yako kama humjui au haujaokoka? Mtumishi wa Mungu Marandu hapa anawafungua macho wale ambao hawaelewi nini sababu ya matatizo ya ndoa zao na ameeleza vizuri kuhusu sababu au chanzo cha shida hii.Ndiyo ninaweza kuja nikakuombea ndoa yako ikatulia siku mbili lakni Je kama huwezi Kumshikilia Yesu Mwenyewe tatizo litarudi palepale.Mapepo/majini mahaba haya ni wafuasi wa shetani kwa hiyo ni vizuri kama mkristo akayafahamu jinsi yanavyofanya kazi na jinsi ya kuyakabili.
  2. Maelezo ya Ndugu marandu ni mazuri kwani ni sawa na daktari kutoa dalili za ugonjwa fulani.Ukishajua dalili za ugonjwa fulani basi inakuwa ni rahisi kuukabili.Kila tatizo la mwanadamu lina maombi yake.Huwezi kuniambia kuwa maombi ya mtu aliyefunga ni sawa na mtu ambaye hajafunga.Ndiyo maana ukubwa wa tatizo humalizwa na ukubwa wa imani ya mtu.Ndoa zina matatizo mengi lakni chanzo kikubwa ni shetani na wafuasi wake na kama adui namba moja wa kanisa ni shetani nitawezaje kupambana naye bila kufahamu mbinu zake?
  NB: Hatuko hapa kwa ajili ya kushindana lakini tusifanye haraka sana kukomments tukatenda dhambi. Watumishi wengi wana shida na vifungo kwa sababu hawataki kujifunza.Shetani yupo na anatenda kazi na kama wewe ni mfuasi wake basi hutapenda kumzungumzia wala kumwadhibu.Haya ni maoni yangu kama yamekukwaza basi tusamaheane.

 6. Bwana asifiwe

  Wandugu tusibishane kweli mapepo ziko duniani iyi . na ndio unacheza na watu wa Mungu na wana wa Mungu .

  tuombeane sana juu ya safari yetu ya kwenda Mbinguni

  Monga

 7. Mi naomba kuchangia hivi kinachosababisha haya yote watu wanakaa na wokovu mguu moja ndani na mguu moja nje ndio maaana mapepo na majini yanakuwa kazini. atu wangapi wanachakachuliwa na dhambi izingayo upesi kama vile hasira; uongo ulafi na mengineyo. kama hivi tu ni dhambi kwa nini shetani asikunyakue ukawa wa kwake? ndio maana kila iituvyo leo wanchungaji na walimu na watumishi wote wanatafuta kumfanya mtu kutoka kwenye maangamizo kama hayo. hata ukichapa injili mpaka asubuhi andiko litabaki ni kweli na amina ila watu wenyewe hawataki kukaa kwa Yesu kimojaaaaaaaa. ndio maana unaona mafunio kama haya. chukua wanandoa waulize maswali utakauja kuta kila mmoja ana kitu ambacho anajutia kwa mwingine na hamna msamaha wa kweli kati ya wakristo. watu wamejaa uchungu manunguniko, kwa nini mapepo yasimvae na huku nje wadau tunajua ameokoka. Wokovu ni wa mtu peke ndio maana huwezi jua mtu anamaanisha ameokoka au la. Huyu mtumishi anasaidia watu kama hawa nilioelezea hapa.

 8. Mi binafisi nashukuru sana kwa fundisho, natumaini hata ndoa nyingi zitaimarika kwa kuzingatia ujumbe huu!.

 9. Yote ni ktka kujenga na kuijua kweli mana ni hyo tu ndio itatuweka huru,Tumuombe Roho mtakatifu atupe milango ya fahamu ya kiroho tuzidi kuijua na kuifuata hyo kweli

 10. Halleluja, Bwana Yesu alie hai asifiwe, namshukuru mungu kwa haya mafundisho, na nikwaajili ya revelations ambazo mungu anawapa watumishi na kanisa lake katika siku za mwisho,Bibilia inasema kwamba tutajua ukweli na huo ukweli utatuweka huru, tena linasema wana wa Mungu huangamia kwakukosa maarifa, kwa wakristo wachanga ambao bado wana nyonya maziwa, haya mafundisho hawawezi kuielewa, japokua wakati ambao watakomaa kiasi yakutafuna mifupa wata elewa, mimi mwenyewe nimeteseka miaka nyingi kwakutojua ni nini ama shida gani ninayo, na hataviho nimeokoka Kristo ni Bwana na mwokozi wa maicha yangu, lakini kwa vile Mungu alipenda kuyafungua macho yangu kiwango ingine, nakatika kufunguliwa kiwago hiyo ndipoza niliweza kuelewa jinsi shetani, mapepo na majini wametesa watu hata kanisani, hadi kanisa la Bwana Yesu, imepoteza watu wengi sana kwakutojua nijambo lipi linalowakandamiza, Ephessians 6 toka mstari wa 10 inaeleze kanisa kwanjia taratibu yakwamba mkristo ambaye akokatika safari ya ufalme wa Mungu lazma apigane vita vikali sana, na si vya damu na nyama bali ni vya kiroho Vs 12 to 18 inaeleza kwakina kwamba tunapambana na majini, pepo sugu nakama huta uliza Mungu akupe maarifa na ujasiri naguvu yakushina hutayaweza, maana wakristo wengi, wengi wameshindwa katika vita hizi nawakafa wakazikwa, hali Bibilia inasema tumepewa Nguvu na Mamlaka juu ya mapepo, lakini jiulize nikwanini umeshindwa ?????

 11. Faith,

  Huwa tunafuata Biblia inasemaje….kama nikufunguliwa tu hata Bagamoyo wanafunguliwa ama sivyo watu wasingelikuwa wanakwenda huko! Biblia nikiwa na maana KUYAISHIA MANENO YA MUNGU…..NDIO UFUMBUZI WA MATATIZO YOTE…..NA WOKOVU NDIO DELIVERANCE KAMILI!

 12. Binafsi naona hamna ufahamu na mambo haya laiti mgefahamu mngejua huyu mtumishi anafundisha mambo ya maana sana na kanisa la sasa limejaa uovu na shida ambazo nafikiri nyie hamjazipitia mgepitia nafikiri mgethamini huduma hii ya deliverance ndoa nyingi zimefungwa kuliko mnavyofikiri hayo yote mnayosema wanandoa wangefanya hivi wameishayapitia lakini ndoa bado mbovu sasa mnafikiri tatizo nini? msipotoshe watu haya ni mafundisho ambayo wenye Mungu wa kweli pekee ndio wanayajua sasa huduma ya delivarance imefungua watu wengi labda ungesikia shuhuda zao ungeamini nawasihi nyie msiyofahamu huduma hii hebu fuatilieni badala ya kuzungumza vitu msivyovijua. AMEN

 13. Shalom Kinyau, Urbi, Joel.

  Naona sasa tumefikia mahali ambapo binafsi, nasikia kuelewa zaidi moyoni mwangu hasa points zilizoelezwa na ndg. Joel na kama ilivyo rudiwa na Kinyau. binafsi nimekuwa sikubaliani nayo kwa 90% huduma hizo au dhehebu hilo la deriverence. na ndo maana nilikuwa nasisitiza kwamba wengi wao kwa 90% ni feki. Nashukuru sana kwa michango yenu ambayo naamini kila mmoja aliyeipitia imempa changamoto na kumsadia kwa namna moja au nyingine.

  Barikiwa.

 14. Joel, shalom.
  Nikushukuru sana kwa jinsi ulivyotutafakarisha swala hili la deliverance kwa maswali mazuri mno. Lakini nikushukuru pia kwa mchango wako hasa maneno uliyoandika hivi;

  “Kwa kumalizia niseme kuwa; binafsi ninaunga mkono mafundisho ya kufunguliwa ambayo hayakinzani na injili ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mafundisho ambayo yanatambua nguvu iliyopo kwenye wokovu mkuu uliogharimu damu ya Yesu pale msalabani. Kwa bahati mbaya sana mafundisho yaliyo mengi ya deliverance tunayoyasikia hivi leo yako nje ya mstari; na ukiyaangalia kwa makini hayatofautiani sana na yale yanayofanyilka kwa waganga wa kienyeji.”

  Huo ndio ukweli wa Injili ya wokovu, mwenye sikio na asikie.
  Ubarikiwe sana.

 15. Mada ya “deliverance” (almaarufu kama “kufunguliwa” katika lugha yetu ya taifa) ni moja ya mada ambazo siku zote mjadala wake huwa moto sana. Ila ni mada muhimu kwa sababu suala hilo limekuwa likileta mkanganyiko mkubwa miongoni mwa jamii ya Wakristo.

  Yangu ni machache kwani hoja za msingi ambazo ningezisema zimeshaelezwa vizuri na wachangiaji wengine kama vile Orbi na Kinyau.

  Kama Wakristo yatupasa kuwa na nia ya dhati toka moyoni ya kutaka kuufahamu ukweli wa Neno la Mungu. Kuna mafundisho mengi hivi leo ambayo ukiyapima kwa kutumia kigezo cha Maandiko Matakatifu utakutana na upotofu. Na tunapoyaangalia Maandiko Matakatifu lazima tumwombe Mungu kwa unyenyekevu atuelekeze jinsi ya kuyaelewa.

  Moja ya hatari KUBWA zinazolikabili Kanisa la leo ni kuchukua maaandiko na kuyatafsiri nje ya muktadha (context) yake ili kujenga fundisho ambalo halipatikani mahali popote katika Agano Jipya.

  Matatizo ambayo mafundisho mengi ya deliverance yanaelezwa kuyashughulikia si mapya. Suala la muhimu ni Je, ndivyo Bwana Yesu Kristo pamoja na mitume wake walivyoyashughulikia matatizo hayo? Kwa maneno mengine, je ndivyo Injili, kitabu cha Matendo ya Mitume pamoja na nyaraka zinavyofundisha namna ya kushughulikia matatizo husika?

  Taabu zinazotokana na nguvu za uchawi pamoja na pepo wachafu zimekuwepo tangu zamani. Je Yesu na mitume wake walipambana nazo vipi?

  Dhambi mbali mbali ambazo nyingine tunaambiwa hivi leo kuwa wanaozifanya wanatakiwa wafanyiwe deliverance; je Maandiko yanasemaje kuhusu dhambi hizo?

  Kwa kumalizia niseme kuwa; binafsi ninaunga mkono mafundisho ya kufunguliwa ambayo hayakinzani na injili ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mafundisho ambayo yanatambua nguvu iliyopo kwenye wokovu mkuu uliogharimu damu ya Yesu pale msalabani. Kwa bahati mbaya sana mafundisho yaliyo mengi ya deliverance tunayoyasikia hivi leo yako nje ya mstari; na ukiyaangalia kwa makini hayatofautiani sana na yale yanayofanyilka kwa waganga wa kienyeji.

  Naendelea kujifunza.

 16. Anthony,

  Biblical counselling ni kitu tofauti kabisa na baadhi ya hizi sarakasi za baadhi “deliverance” zinazofanyika leo.Counselling ya Kikristo imejengwa katika MSINGI wa Neno la Mungu ikihusisha ufahamu wa Psychology ya Mwanadamu…! Biblical Counselling inatendeka katika ufahamu wa wigo wa maneno ya Mungu tu!……..Kwa kifupi tu baadhi ya watu wengi naowafahamu mimi ambao wanafanya Huduma ya Counselling hata ufahamu wa Psychology ya mwanadamu hawana…… ambao ni msingi katika kufanya huduma ya counselling!

  Hivyo ndugu yangu Anthony….naamini katika Christian Couselling…….nikiwa na maana Counselling yenye MSINGI KATIKA MANENO YA MUNGU NA UFAHAMU WA SAIKOLOJIA YA MWANADAMU!

 17. Mimi najua kuna mtumishi alikuwa ameokoka na ni mhubiri WA MIUTANO alikuwa akipata matatizo hayo kwa mke wake na sasa Mungu amemfungua,mke pia alikuwa ameokoka na ni mtumishi, sijui lakini nasisitiza labda uelewa wa hiyo kufunguliwa kama ni kitugani?? maana kuna madhehebu mengi yenye imani ya kufunguliwa kwa UONGO!!. Mimi nijuavyo watu wanaofanya huduma hiyo ya kufunguliwa wanafanya pia counselling. Sijui labda nitazua swali lingine kuwa counselling imeandikwa wapi?

 18. Stina.

  Naomba kukusahihisha kidogo kwamba hapa watu hawalumbani bali wanaelimishana. Na katika kuelimishana huko ndiko kunakoweza kuleta ufumbuzi wa kweli wa matatizo yako/yetu yanayokukabili/yanayotukabili kwenye ndoa yako/zetu.

  La muhimu hapa ninalotaka kulijua kwako ni hili kwamba umempa Yesu maisha yako? Ndoa yako imesimama katika msingi upi, wa Mungu au wa Mkuu wa anga hili? Je mwenzi wako naye amempa Yesu maisha yake?

  Nasema hili kwa maana kwamba hata ukienda mahali ambapo ndugu Marandu anasali UNAWEZA, (nasisitiza tena ‘unaweza’ maana yake si lazima) ukaendelea kuwa na matatizo yaliyo kwenye ndoa yako sawa na wakati ambapo ulikuwa hujaenda mahali anaposali ndg Marandu. Kwa maana pana ni kwamba bila kujua chanzo cha tatizo lako ni vigumu sana kupata suluhisho la tatizo hilo. Mimi nakushauri wewe na mwenzi wako kaeni chini na mtafakari kwa makini (kama mmeokoka au hata kama hamjaokoka mkimsihi Mungu awafunulie neema ya wokovu) ili kuweza kupata chanzo cha matatizo mliyonayo kwenye ndoa yenu; baada ya hapo mtakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kuyatafutia dawa au suluhisho matatizo hayo; vinginevyo unaweza kwenda sehemu zote ambazo ‘deliverance’ inafanyika na bado matatizo yako yakawa pale pale.

  Neema ya Mungu ikufunulie chanzo cha matatizo yako kwenye ndoa na hatimaye Mungu akuongoze kufikia suluhisho la kudumu la matatizo haya ili uweze kuifurahia ndoa yako. Mungu ametuingiza kwenye ndoa ili tu-enjoy na kula matunda ya nchi sio ndoa hizo zitutese. Kuteseka kwenye ndoa si mpango wa Mungu, ni mpango kamili wa shetani ndio sababu taasisi ya kwanza kabisa iliyoathirika baada ya shetani kuingiza dhambi duniani pale kwenye bustani ya Edeni ilikuwa ni ndoa.

  Adamu akamtupia lawama mke wake kuwa ndiye aliyemdanganya (mafarakano na umoja wao ulivurugwa), lakini akaenda mbali zaidi kumlaumu hata Mungu aliyempa huyo mke kana kwamba Mungu alimpa Adamu kitu kibaya. Kwa hiyo ndoa nyingi zina matatizo ili shetani aendelee kulivuruga kanisa. Kanisa la kweli linalomtukuza Mungu katika Roho na kweli linaanzia kwenye ndoa yaani baba na mama na kisha watoto. Na kwa kuwa shetani anajua kabisa kanisa imara linaanzia kwenye familia, baba, mama na watoto, basi ana hakikisha kila wakati anazishambulia na kuzivuruga ndoa za watu wa Mungu.

  Pole sana Stina na Mungu akuwezeshe kupata suluhisho la kweli ili uweze kuifurahia ndoa yako.

  Be Blessed.

 19. To Frederick D Marandu

  Nimeolewa na nina matatizo mengi uloainisha hapo juu. Naomba maelekezo ya wapi naweza pata huduma hiyo ya maombezi ili nifunguliwe.
  Hayo malumbano nyie endeleeni nayo. Nahitaji msaada.
  Asante.

 20. Ndugu Nathani,

  Uliuuliza maswali yako sita…….ambayo uliomba majibu yake, hebu na mimi naomba unijibu mswali haya……labda itatusaidia katika mjadala wetu…

  1.JE ROHO MTAKATIFU YUPO?
  2. JE ROHO MTAKATIFU ANAWEZA KUINGIA NDANI YA MTU?
  3. JE ROHO MTAKATIFU ANAFANYAJE KAZI NDANI YA MTU?
  4. ULIMWENGU WA KUISHI KATIKA ROHO WA MUNGU UPO? NI HALISI?
  5. JE INAWEZEKANA KUONGOZWA NA ROHO WA MUNGU NA AKAUTIISHIA MWENENDO WAKO NA MAPITO YAKO?
  6. UNAWEZAJE KUJUA MTU KAMA ANA ROHO WA MUNGU?…

  Kwa kutumia maneno ambayo nayanukuu nami “ninaomba kupewa msingi wa kimaandiko na si kushambulia tu kama baadhi ya wachangiaji mahiri walivyofanya katika mada hii.
  Ninaomba uvumilivu utumike tafadhali ili tupate kuelimishana.”

  UBARIKIWE

 21. Nathan,

  Hata mimi naweza kusema kama ulivyosema watu wangu wanapotea kwa Kukosa maarifa pia…! Kama muumini amekosa maarifa ni nini kimetendeka ndani ya maisha yake na hasa kutambua Yeye ni nani katika Kristo ni rahisi kabisa kuchukuliwa na mafundisho ambayo hayajajengwa kabisa katika msingi wa maneno ya Mungu!

  Paulo aliwaambia wazi Wagalatia ni nani aliyewaloga…..na ni Paulo huyo huyo aliyesema pia “tusiwe watoto wachanga tukitupwa huku na huku na kuchukuliwa na upepo wa elimu”

  Kama ukisoma nyaraka za Paulo ni nini kinatokea au kinatendeka ndani ya Muumini anapompokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wake na kama alivyoowaambia Waefeso ” Nanyi mnajengwa na kuwa Maskani ya Mungu katika Roho” Ni vigumu mno kuja na mafundisho hayo ya “Deliverance’ kwa muumini! Kama yanavyofundishwa leo!

  Hivyo mimi naamini waumini wengi wanayumbishwa na mafundisho haya kwa vile hawana maarifa ya maneno ya Mungu! Na kama ukisoma post zangu sipingi “Deliverance” pasipo kusimama katika maneno ya Mungu! Wala sitokee hewani na kukosa sehemu ya kusimama katika maneno ya Mungu……La hasha….Isipokuwa ni hao wanaotupinga tunaokataa mafundisho haya naona hawana mahali pa kusimama isipokuwa wanakuja na “experience” zao! tu na wanashindwa kukanushwa kwa hoja za Kimaandiko! Sikuzote experience zetu hazijengi mafundisho…..hata ziwe zina msisimuko wa namna gani…..kila kitu lazima kiangaliwa katika mwanga wa Maandiko…..sio tafsiri za mtu…..!

  Kwa kifupi Nathani wapi Paulo katika Nyaraka zake zote kafundisha “Deliverance kwa muumini? Wapi Kanisa la Kwanza lilifanya “Deliverance kwa waumini?Tunachoona Paulo anafundisha kuwa Wokovu ndio kufunguliwa kwenyewe!Tunaona Paulo anafundisha waumini wapate kukua Kiroho.Kanisa la Korintho na madhaifu yake yote huduma hii haikufanyika….wala yale makanisa saba ya Asia…..ambayo yalikuwa na madhaifu kadhaa wa kadhaa…. Hata vile vita vya Kiroho katika Waefeso mlango wa sita havizungumzii “Deliverance” kwa muumini………Bali muumini kuzipinga Nguvu za Giza katika maisha….kwa kutumia Neno….Maombi……Roho Mtakatifu……!

  Kwa kifupi natambua wazi utendaji wa Mungu na Nguvu za Mungu za Kuponya na kuokoa…….Natambua wazi nini kinafanyika mtu anapompokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wake…..Natambua wazi ni nini kinatokea Muumini anapojazwa Na Roho Mtakatifu na kuamua kuishi kwa kuongozwa na Roho huyo…..Maandiko yako wazi kabisa…….na maandiko yako wazi pia kuwa Kazi za Ibilisi zinavunjwa ndani ya Mtu asiyemjua Yesu…ili aiingizwe katika Ufamle wa Mungu……!

  Hivyo ndugu Nathani…..na mimi nasema tena Watu wa Mungu wanapotea kwa kukosa maarifa ya Neno la Mungu……! Wanachukuliwa na kila upepo wa mafundisho…..mradi tu yanakuja kwa kutumia Biblia……Paulo akasema….”KWA KUWA MNAMWACHA ALIYEWAITA NA KUIGEUKIA INJILI YA NAMNA NYINGINE……WALA SIO NYINGINE…..WAPO WATU WAWATABISHAO NA KUTAKA KUIGEUZA INJILI YA KRISTO! Kwa upande wangu mimi unapomwambia Muumini aliyeokoka aliyejazwa Roho Mtakatifu…..akafanyiwe “Deliverance” ni kuigeuza Injili ya Kristo na kufanya ile kazi ya Msalabani ya kumkomboa haikukamilika! Muumini yoyote akitambua ni nini Kilifanyika Msalabani kwa ajili yake….na yeye amekuwa nani katika Kristo Yesu…….na ni nini Bwana anafanya kwazi ndani yake sasa hiv KWA KUPTIA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU……naamini kwa Ufahamu huo itavunja kabisa haya mafundisho dhaifu ya “deliverance ambayo yamekuja kuwayumbushwa baadhi ya waumini! kuwatia hofu za kuogopa ndoto……! Kupotelewa pete…..na mambo ambayo yanaweza kuitwa mafundisho ya wanadamu….ambayo hayana kabisa msingi katika Neno la Mungu…bali unaona wazi yanatukuza nguvu za kuzimu…na kuzifanya zina nafasi katika maisha ya Muumini!……Kwangu mimi sioni Yesu na Roho wake mwenye uwezo anapewa utukufu kutoka na mafundisho haya…….bali “nguvu za majini mahaba” na utendaji wake ndio unachukua nafasi….!

  UBARIKIWE!

 22. Ndugu Nathan,

  Hebu nijibu maswali yako kwa Kifupi

  1. MAPEPO NA MAJINI YAPO?…….YAPO
  2. MAPEPO NA MAJINI YANAWEZA MUINGIA MTU?…… NDIO
  3. MAPEPO NA MAJINI YANAFANYAJE KAZI?…. Kwa njia nyingi mno
  4. ULIMWENGU WA ROHO UPO? NI HALISI?…..UPO
  5. JE INAWEZEKANA KUMKEMEA PEPO NA AKATII NA KUMTOKA MTU?……..NDIO
  6. UNAWEZAJE KUJUA MTU KAMA ANA MAPEPO?…. Kwa njia mbali mbali…..huwezi kuwa na jibu moja kwa swali hili

  Na kwa kifupi tu Mtu aliyempokea Yesu na akamruhusu Roho wake aingie ndani yake anatolewa kutoka nguvu za giza na kuingizwa katika ufamle wa Mungu……..Injili ya Yohana inaonyesha wazi Yesu na Roho wake anafanya makao katika muumini huyo!……..Paulo anasema tunafanyika HEKALU LA MUNGU…..!
  ………..tukiokoka au tukimpokea Yesu tunaingizwa katika Ulimwengu mpya wa Kiroho…..Biblia inasema UHAI UMEFICHWA KATIKA YEYE……TUNAFANYIKA WATOTO WA MUNGU……..!

  Naamini umepata ufafanuzi wa majibu yako

  UBARIKIWE

  https://strictlygospel.wordpress.com/2011/09/08/kufunguliwa-kutoka-katika-ndoa-ya-mapepo-au-majini-mahaba/#comment-form-load-service:Twitter

 23. Mpendwa John Paul.

  Kimsingi ni baada ya kukosa majibu kwa muda mrefu ndipo nami nilipoamua kusema kile ninachoona kitasaidia wapendwa. kimsingi nilikuwa nikitafutan kujifunza zaidi juu ya mswali niliyotoa kabla sijapata kusema kile nilichokusudia. lakini hata hivyo sikupata mtu mwenye kunijibu kwa wakati. nitafurahi kama wachangiaji watajibu maswali niliyouliza yoye ikiwa ni kuelimishana tupate kujifunza zaidi. ninachoamini mimi, ni kwa kujua tabia na njia za Mungu pekee ndipo tunaweza kutambua hila za shetani, otherwise kama hatujafikia uelewa wa kutosha wa tabia ya mungu na njia za Mungu ni vigumu sana kuweza kutofautisha kazi ya shetani na kazi ya Mungu.

  Ubarikiwe.

 24. Dad Eliza,

  Samahani kwa kuwa mimi siyo Marandu lakini nimeguswa tu na maelezo yako na uhitaji wako wa kufahamu namna ambavyo mkristo anatakiwa asimame mwenyewe. Nimeguswa sana na maneno haya:

  “Ni vizuri mkristo ujue jinsi ya kusimama mwenyewe, na ndio maana mbali na kufudisha dalili zake ungesaidia pia kufundisha watu wasali vipi mistari katika biblia na jinsi ya kufunga na kuomba, kwani imani ya mtu ndio inayomponya”.

  Katika paragraph ya mwisho ya maneno aliyoandika ndugu Marandu ameandika kuwa JAMBO KUBWA ktika kuepukana na hayo ni MTU KUMA YESU MAISHA YAKE. Aliandika hivi:

  “Njia kubwa ni umpe Yesu maisha yako”!

  Kwa hiyo mimi niliona kama ameshaelekeza jinsi mtu anayesumbuliwa na matatizo hayo anavyotakiwa kuwafanya. Kwanza ni kumpokea Yesu ili AINGIE MAISHANI na Yesu akishaingia pamoja na Nuru yake, Shetani pamoja na Giza lake vitaondoka. Na huo ndio umekuwa msisitizo wa ndg Orbi, Kinyau na wengine wanaosisitiza katika Nguvu ya Mungu ipatikanayo katika UTAKATIFU.

  Suala ambalo uliandika ukimtaka ndugu Marandu “kufundisha watu wasali vipi mistari katika biblia na jinsi ya kufunga na kuomba” mimi naliona kama vile linaweza kutupeleka nje kabisa ya IMANI YA KIKRISTO. Kwa nini nasema hivyo?

  Imani ya Kristo ni uhusiano hai kati ya mtu na Mungu kupitia Yesu Kristo. Siyo suala la kukariri mistari, kwa mfano, kwamba “mstari fulani unatakiwa usomwe mara 4 kisha ufuatiwe na mstari mwingine mara 7”, halafu mtu akishafanya hivyo aamini kuwa tayari “ameshasali”. Ukristo unampa mtu ufahamu wa kutambua uhusiano wake na Mungu kama Baba na kuwa kuna uhuru wa kuomba kwa Mungu kadri mtu anavyosukumwa ndani ya moyo wake. Lakin hayo hayawezi kufanyika pasipo mtu kumpokea Yesu kama Mwokozi wake. Jambo la mtu kumpokea Yesu hufungua ufahamu uliofungwa kwa sababu ya dhambi na kumfanya mtu atambuwe kuwa anaye Baba wa kiroho na ambaye yuko tayari kusilikiza maombi ya mahitaji kutokana na mahitaji yaliyoko wakati huo na wala si KUSALI KWA KUSOMA MISTARI KATIKA BIBLIA.

  Daniel alipokuwa akiomba wakati wa mfalme Dario katika kitabu cha Daniel kwenye Biblia hakuwa anaomba kwa kusoma mistari iliyoandikwa katika Biblia. Elia, naye wa kwenye Biblia, alipoomba mvua isinyeshe na kisha inyeshe hakuwa anaomba kwa kutumia mistari ya Biblia. Daudi, Yeremia, Paulo, Petro na Watakatifu wa kwenye Biblia kwa ujumla wao hawakuwa wanaomba/wanasali kwa kutumia kusoma mistari fulani bali WALIBUBUJIKA yaliyojaza mioyo yao. Ni maombi yanayoambatana na tatizo husika lililopo wakati huo. Maandiko ya kwenye Biblia yanaweza kutusaidia tu kuonyesha kuwa jambo fulani linastahili kuwekwa katika maombi kwa kuwa mahali fulani katika Biblia imeandikwa habari ya watu/mtu kuomba juu ya jambo kama hilo. Yanasaidia kukuza Imani. Hata katika Waraka wa mtume Paulo kwa Wafilipi aliandika kuwa:

  “Msisumbuke kwa jambo lolote bali kwa kuomba na kusali pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu”
  Wafilipi 4:6.

  Maandiko hayo yanaonyesha kuwa suala la kuomba ni la haja zilizopo wakati maombi yanafanyika. Si kusoma mistari kwenye Biblia bali ni kupeleka mbele za Mungu kile kilichoko moyoni. Inaweza kutokea kabisa kuwa tatizo fulani alilo nalo mtu linafanana kabisa na tatizo alilokuwa nalo mtu fulani aliyeandikwa kwenye Biblia. Lakini hiyo nayo siyo sababu ya kumfanya mtu aanze kuomba kwa kusoma mistari ya Biblia kwa kuirudia rudia. JAMBO KUBWA HAPA NI ULE MGUSO WA MUNGU ULIOKO NDANI YA MTU. Mtu anaweza kusoma mistari ya maombi lakini SIYO RAHISI kupata zile hisia/feelings alizokuwa nazo mtu huyo wa kwenye Biblia wakati anaomba maombi hayo kwa Mungu. Ndiyo maana ni vizuri mtu akawa na uhusiano HAI ambao kupitia huo nafsi ya mtu huhuishwa na mtu huyo, wa sasa, anaweza kumuomba kwa maneno yenye uhusiano na uzito wa tatizo kwenye moyo wa mtu pamoja na wakati huu uliopo.

  Umeandika kuwa “siku hizi kuna makanisa mengi ya kitapeli kiasi kwamba (mtu unakuwa) hujui wapi pa kuelekea. Mimi nasema kuwa KUBWA INAYOFANYWA NA MAKANISA YA KITAPELI KUWAONDOA WATU KWENYE MSINGI IMARA WA NENO LA MUNGU na KUWAINGIZA KATIKA MAFUNDISHO YASIYOWAPELEKA WATU MIKONONI MWA MUNGU na kisha kuwatumainisha kuwa mtu atajibiwa tu mahitaji yake hata pasipo kukaa ndani ya familia ya watoto wa Mungu.

  Moja ya kazi kubwa ya makanisa ya “kitapeli” ni KUWAFANYIA WATU DELIVERANCE na kisha kuwaruhusu waendelee na maisha yao ya dhambini na kuwadanganya kuwa “WAMESHAKUWA DELIVERED”. Watu wengi leo wako mitaani wakiwa wanaishi maisha ya “duniani/dhambini” kabisa lakini ni MAFUNDI WA KUTAMKA MANENO MAKALI YA KUMKEMEA SHETANI wakati wao wenyewe WANAFANYA YALIYO YA SHETANI. Huu ni utapeli mkubwa!

  Makanisa ya kitapeli yanawatumainisha watu kwenye KUSALI MISTARI KATIKA BIBLIA pamoja na KUFUNGA NA KUOMBA KWA IDADI FULANI YA SIKU (kujenga imani juu ya “idadi” ya siku) lakini watu hao wakiwa hawana kabisa FURAHA YA WOKOVU katika maisha yao. Yesu alisema alileta “amani” ambayo “dunia” haiwezi kumpatia mtu. Watu hawa wenye kusali kwa kusoma maandiko yanayopendwa zaidi katika Biblia, huku wakiwa hawana Yesu mioyoni mwao, hawafahamu kabisa juu ya “amani ya Kristo” na namna inavyoweza kujaa ndani ya maisha ya mtu. Ni mafundi sana wa kusali sala mbali mbali lakini kiukweli, narudia tena kiukweli kabisa maneno hayo yanaishia mdomoni tu lakini mioyoni Yesu hayumo kabisa. Mungu atusaidie sana!

  Maombi ya DELIVERANCE yanaweka msisitizo mkubwa sana katika kufunguliwa kutoka katika matatizo ya Kimwili kuliko KUOKOA ROHO KWANZA mbao ndio ufunguo mkuu wa kupokea toka kwa Mungu. Kwa hilo ninaungana kabisa na ndugu Marandu. Bila kumpokea Yesu hizo deleverance ni bure kabisa, haziwezi kumaliza matatizo ya kushambuliwa na guvu za giza. Ndiyo maana kuna watu kila wiki wanafanyiwa deliverance. Leo deliverance ya ndoa, kesho ya biashara, keshokutwa ya safari, siku inayofuata ya kuishi vizuri na majirani, halafu kuondoa mikosi, kupata kibali mbele za watu nk nk. Yaani ni deliverance juu ya deliverance. Hapana. Huo SIYO MPANGO WA MUNGU!

  DELIVERANCE KUBWA KULIKO ZOTE NI KUMKARIBISHA YESU AKAE NDANI. YESU AKISHAINGIA NA KUFANYA MAKAO MAISHANI MWA MTU KILA KAZI ZA NGUVU ZA GIZA HAZIWEZI KUFANIKIWA TENA. Nuru na giza havikai pamoja! Huko ndiyo kuokoka. Kumfanya Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha, yakiroho pamoja na ya kimwil!

  Kwa hiyo mtu anayeona anahangaishwa sana na mambo ya namna hiyo anatakiwa atafute mahali panapohubiriwa Wokovu, aende aongee na mchungaji kuwa anahitaji kumpokea Yesu. Sehemu hizo zinazohubiri wokovu zimeenea nchi nzima na sehemu kubwa sana dunia. Labda kama kuna anayesoma hapa na anakaa nchi ambazo UKRISTO UNAPIGWA MARUFUKU anaweza kuandika ili ashauriwe namna ya kuishi ndani ya Yesu hata hapo hapo alipo. Lakini kwa sehemu kubwa Jina la Yesu na habari za Wokovu kwa ujumla zinapatikana kwa urahisi kwa kuwa Neema ya wokovu ilishafunuliwa!

  Na kisha dada Eliza ulimalizia kwa kuandika kuwa:

  “kwani imani ya mtu ndio inayomponya”

  Mimi pia nakubaliana nawe katika hilo. Lakini kuna zaidi ya “imani ya mtu”. Suala si imani tu ya mtu bali ANAAMINI KATIKA NINI. Maneno hayo aliyasema Yesu akimwambia yule dada aliyekuwa anatatizo la kutokwa na damu kwa muda mrefu sana. Baada ya kugusa pindo la vazi la Yesu akapona. Alipona kwa sababu IMANI yake aliilekeza kwa Yesu. [pindo la vazi la Yesu]. Kwa hiyo nimeona tupaweke sawa hapo ili pasomeke hivi:

  “Kwani imani ya mtu kwa Yesu ndiyo inayomponya”.

  Tukimwamini Yesu kulishika neno lake UPONYAJI ni mwingi mno, hata siyo wa kutafuta kwa namna hiyo.

  Baada ya maneno hayo mimi napenda kukushauri dada yangu kuwa hebu mpokee Yesu [kama bado hujafanya hivyo] na hiyo ndiyo njia itakayokuelekeza katika kila kitu chema ambacho Yesu anacho katika stoo yake kwa ajili ya watu wanaomumini na kumfuata Yeye. Lakini kama ulishampokea Yesu basi zingatia katika kuutafuta utakatifu na hatimaye utaona kuwa unayo maneno ya kutumia katika maombi hata zaidi ya yale yaliyoandikwa katika Biblia!

  Ninamalizia hapa na kama kuna swali ambalo linaweza kuwa limejitokeza kutokana na maelezo yangu USISITE kuuliza kwa kuwa tuko hapa kujifunza, na kujifunza Neno la Mungu!

 25. Ndugu Nathan,
  September 12, 2011 uliandika maswali 6 na kuomba ujibiwe na kisha ukamalizia kwa maneno yafuatayo:

  “ninaomba kupewa msingi wa kimaandiko na si kushambulia tu kama baadhi ya wachangiaji mahiri walivyofanya katika mada hii.
  Ninaomba uvumilivu utumike tafadhali ili tupate kuelimishana”

  Lakini baadaye umeandika maelezo mengi ambayo yanaambatana na maandiko, na katika kuandika kwako mimi noana kuwa majibu ya maswali hayo mengine tayari umeshayajibu kwenye maelezo yako ya tarehe 19, September 2011.

  Sasa, kwa upendo kabisa, ninauliza kama ni kweli kuwa hufahamu majibu ya mswali hayo au ulihitaji tu majibu mengine ili ulinganishe na yale ambayo unayo wewe?

  Nimeona niulize hivyo maana naona maswali yamekaa karibu wiki mbili sasa pasipo kujibiwa na pengine wewe unahitaji sana majibu hayo. Naomba kufahamu kama bado unahitaji majibu ya maswali hayo ili nami nishiriki kuyajibu.

  Asante!

 26. Nimesoma na kuelewa sana mafundisho yako. Tatizo ni kwamba hujatoa msaada wa nini cha kufanya mtu binafsi, siku hizi kuna makanisa mengi ya kitapeli kiasi kwamba hujui wapi pa kuelekea. Ni vizuri mkristo ujue jinsi ya kusimama mwenyewe, na ndio maana mbali na kufudisha dalili zake ungesaidia pia kufundisha watu wasali vipi mistari katika biblia na jinsi ya kufunga na kuomba, kwani imani ya mtu ndio inayomponya

 27. Hongereni kwa kuendelea kuchangia mada hii yenye ujumbe “mgumu kwa wachanga na wa kati kwa wanaoendelea kukua”.
  Wakati tukiendelea kujifunza ninaomba nitoe swali langu lingine; JE HILA ZA SHETANI NI NINI? NA NI ZIPI AMBAZO MUNGU NATAKA TUZIJUE AS PER HIS WORD?

 28. One last thing, Tunafahamu kwamba, Tangu mwanzo shetani ana tabia ya kutumia kitu halisi kwakukigeuza kuwa si halisi ilimkuleta upotovu kwa mwanadamu. Shetani huyohuyo, kama alivyotumia maneno/ maagizo ya Mungu na kuyabadili kisha kumletea upotovu mwanaamu, lijaribu kufanya hivyo kwea kutumia maandiko kumjaribu Bwana Yesu pia. JE SHETANI AMEBADILIKA? HAWEZI AKATUMIA KITU CHA MUNGU KWA KUKIGEUZA KISIWE HALISI NA KUHARIBU MAISHA YA WALE WATAKAOMAINI?
  IKIWA ALITUMIA NENO KUMJARIBU YESU, HAWEZI TUMIA DELIVERANCE (AMBAYO INAWEZEKANA KABISA NI YA MUNGU) KWA KUIBADILI KIDOGO TU NA KUWAHARIBU WANADAMU?
  Mbona tunajua kwamba shetani ni bingwa wa kuiga, ameiga matumizi ya damu, tunaona jinsi waganga wa kienyeji wanavyodai kuku, na mbuzi, njiwa yote hii ikiwa ni kutumia damu za wanyama kufanya maagano. Haya yote si shetani ameyaiga kwa Mungu? infact Kila kitu anachofanya shetani ameiga kwa Mungu na anakibadilisha na kukitia uovu ili kuwapotosha wanadamu. Kwa nini tunafikiri hawezi kutumia deliverance kama ni ya Mungu?
  Tuendelee Kutafakari Pamoja na Mungu awabariki.

 29. Shalom wapendwa.
  Mungu ananena katika Hosea 4:6 6 “My people are destroyed for lack of knowledge;…” How do we get knowledge? Its through Learning. Katika safari yangu nimegundua kwamba silaha kubwa anayotumia shetani kuwamaliza watu ni UJINGA. Mtu amekuwa mshirikina kwa miaka 30, akazama humo na kujenga tabia ya ushirikina, anafikiri tabia hiyo inaweza toweka in a second? sidhani kwamba ni kweli. Ifahamike kwamba maisha ya kiroho huanza kama maisha ya kimwili yanavyoanza. kuna utoto pia,/ Uchanga, wakati ule ambapo mtu kaokoka, lakini kwa kuwa hana msingi wa kujua jinsi ya kuishi maisha ya wokovu, anakuwa bado anashindana na Maisha yake ya awali. Mwili kupitia nafsi yake unaendelea kumvuta kuelekea mauti, wakati huo huo Roho ikimvuta kuelekea uzia. Ieleweke kwamba. Ukipambanisha mbwa wawili ambao mmoja wao amelishwa chakula na mwingine ana njaa, li lazima yule mwenye njaa atashindwapambano hilo. ndivyo ilivyo katika maisha ya wokovu, Baada ya kuufuata mwili, na kuulisha mwili wako na kuwaka tamaa kwa kila namna kwa miaka 30, kisha unataka kuanza kuishi maisha ya kiroho, ni lazima utegemee kuwa Mwili wako unaweza ukakishinda, kwa kuwa tu Roho yako haijajengewa msuli wa kutosha katika mafundisho ili kuushinda mwili. Hapa ndipo shetani anapotumia advantage hii, na mapepo yake yanapofanya kazi kwa nguvu zaidi. Nijuavyo mimi, mtu anatakaswa na Roho kwa kuiamini KWELI. Tunakubaliana kwamba imani ya mtu huweza kuongezeka kwa kadiri mtu anavyozidi kusikia na kuelewa neno la Mungu (Warumi 10:17 inaweka wazi jambo hilo) kwa maana hiyo, kwa kadiri mtu anavyozidi kusikia neno la Mungu, na kupokea imani ndivyo anavyozidi kutakaswa na ROHO kwa kadiri ya imani yake inavyoongezeka na ndivyo anavyozidi kufunguliwa kutoka katika vifungo na kila laana na uovu uliokuwa ukizingira maisha yake. Hivi kama ukishaokoka tu mara moja Tayari unakuwa umeshakamilika kiroho, no mapepo tena na vifungo vinakuachia mara moja, Ni kwa nini basi Roho mtaka tifu anaendelea kufanya kazi ya kututakasa mpaka pale tutakapofikia cheo cha kimo cha utimilifu wa kristo? kwa nini kazi hiyo iwe endelevu kama inakuwa imekamilika mara tu mtu anapookoka?
  Wachangiaji wengi sana wameyakataa mafundisho ya deliverance Moja kwa moja kuwa si ya Mungu, Nisingependa kuungana nao kuyakataa Moja kwa moja au kuyakubali, ila ninachotaka kusema na kuchangia ni kwamba. katika Mada hii, Je kweli hakuna kitu tunachoweza kujifunza either kwa kumjua Mungu au Ibilisi anavyofanya kazi? Kukataa moja kwa moja pasipo kutoa mwanya wa kuyachunguza mambo vizuri ndiko kunakokumbatia UJINGA ambao husababisha maangamizo kwa wana wa Mungu. Lakini pia Kukataa pasipo kutafakari ni matokeo ya “Ngome”, “Elimu” na Fikra Zilizojengeka ndani ya kichwa cha mtu zinazopingana na kila elimu ya Mungu. Kama Umeyapinga maelekezo ya mtoa mada pasipo kutafakari vizuri Soma upya habari za vita vya kiroho (Waefeso 6:11-18) imeandikwa pia katika 2corinthians 10:3-6 “For though we walk (live) in the flesh, we are not carrying on our warfare according to the flesh and using mere human weapons. For the weapons of our warfare are not physical [weapons of flesh and blood], but they are mighty before God for the overthrow and destruction of strongholds,
  [Inasmuch as we] refute arguments and theories and reasonings and every proud and lofty thing that sets itself up against the [true] knowledge of God; and we lead every thought and purpose away captive into the obedience of Christ (the Messiah, the Anointed One),
  Being in readiness to punish every [insubordinate for his] disobedience, when your own submission and obedience [as a church] are fully secured and complete.”
  Kama unapinga pasipo kutafakari vizuri maandiko na kujifunza, Pasipo kuchunguza vizuri kile unachokipinga, unahitaji kujifunza upya habari za vita vya kiroho. USHAURI WANGU MIMI NI KWAMBA TUTOE NAFASI YA KUJIFUNZA, KUNA MAMBO MENGI SANA MTOA MADA AMEYATAMKA KATIKA MADA YAKE, TUNGEWEZA KUMUULIZA MASWALI ZAIDI JUU YA HAYO PENGINE TUNGEPATA KUJUA EITHER MUNGU ANAVYOFANYA KAZI AU IBILISI ALL TO OUR ADVANTAGE.
  MUNGU WANGU AWABARIKI.

 30. Antony,

  Nakushukuru kwa post na hasa mifano yako, labda na mimi nikiri kwa sehemu kuwa nimekuwa biased against na misisitizo ya “Deliverance” kwa yale ambayo nimeyaona.
  Naifahamu familia moja ya mzee mmoja wa Kanisa ambaye ameokoka msomi na anaheshimika katika kanisa, yeye na watoto wake wote walikuwa wameokoka na kuenenda vizuri katika Bwana, taratibu baadhi ya wanafamilia hao wakaanza kuhudhuria mikutano na mafundisho ya Delivarance kwa kifupi tu baada ya kuanza hizo delivarance teachings familia ikaanza kushikana uchawi….kuitana washirikina……na kwa kifupi familia hiyo hivi sasa mtu anasali kanisa lake na hawasalimiani na kutembeleana…..kisa hawa wameikataa “Deliverance”hawataki kufunguliwa na wana uchawi…..na wengine wanaona hawa wamepotea…..!

  Kisa kingine….kuna mchungaji toka mikoa ya kusini…..Mchungaji msomi….na amefanya kazi kubwa ya Bwana, ghafla mkewe akaanza kutembelea hiyo mikutano ya delivarance…….na mara akaja na tuhuma za kuwa Mumewe mchungaji ana jini mahaba! Lazima akafanyiwe delivarance…..mchungaji alipokataa mke akaomba talaka….na ajabu mahakama ikatoa talaka….sio kwa sababu ya jini mahaba….ila waliona wazi waamini hao wakristo wanatofauti za kiimani zisizoweza kupatanishwa! Ndoa ya miaka mingi yenye watoto watano imeisha kuvunjika! Kisa tu mke kafanyiwa “Delivarance” na akaona mumewe akafanyiwe pia “delivarance!Na mume anaikataa…

  Na dada mmoja ambaye aliianza kuvutiwa huduma za Mitume na manabii…..na alipokwenda huko akambiwa afanyiwe “delivarance” kwa kuwa ana pepo wa Uzinzi, ilimshtua binti huyo….kwani kaolewa bila kuwa na Mahusiano nje ya ndoa,na hajawahi kusaliti ndoa yake……..

  Hivyo Antony kama ulivyosema mwenyewe kuwa haya mafundisho ya “delivarance” asilimia 90% ni ya upotofu naungana na wewe kabisa……Na kama kuna mafundisho ambayo ndani yake yamebabe sumu ni lazima wakristo tuwe na tahadhari…….shetani alitumia maandiko katika bustani ya Aden…..na alijaribu pia kutumia maandiko alipomjaribu Yesu……..na leo anatumia maandiko hivyo hivyo ili kuwapoteza wateule!

 31. Shalom!

  Nashukuru kwa ufafanuzi wako Mzuri sana ndugu Orbi. mimi nilidhani hayo yaliyoandikwa na ndugu Marandu ni kwa ajili ya wote hata wale wasiookoka na wale ambao kwa sehemu wameokoka lakini bado wanazipata dalili hizi kwa sababu ya udhaifu wao. Hivyo kwa sababu chombo hiki ni kwa ajili ya watu wengi waliookoka na wasiookoka ndio maana niliitetea hoja kwa misingi kwamba wapo waliookoka lakini wameadhirika na hizo dalili na hali kadhalika wasiookoka.

  (kuna AYA ya mwisho ya ndugu marandu ina sema —Njia kubwa ni umpe Yesu maisha yako. Na usiogope hata wewe ambaye ulisha mpa Yesu maisha yako kama una dalili hizi nenda kafunguliwe sio dhambi kufunguliwa uweze kuoa / kuolewa. Na uliyeko katika ndoa ikiwa na mambo ya jinsi hii hauko salama hata kidogo kafunguliwe uweze kufurahia ndoa yako katika Jina la Yesu) HIVYO ALILENGA WASIOOKOKA MAANA MTU ALIYEOKOKA KAMA BADO NA DALILI HIZO ANAHITAJI MSAADA. Ktk kukuwa kwangu kwa wokovu mchg wangu alikuwa anasisitiza kwamba ukiona unaota ndoto umelala na mwanamke na kufanya mapenzi hiyo SIYO, HIVYO AKATUSAIDIA TUKAWA AWARE NA VITU KAMA HIVYO HAVITOKEI KABISA.

  Labda ngoja niandike kisa kimoja hapa. Kuna dada na mumewe niliwahi kuwafanyia counselling kwenye ndoa yao lakini wameokoka na wanasali ktk makanisa ya wokovu makubwa, kisa mke alikuwa hajisikii kimapenzi na mumewe, na walikuwa wanakaa hadi miezi sita bila(dada alikuwa anapata maumivu). sasa baada ya kujifunza sana maelezo yao, wakanishuhudia kwamba hata mdogo wake wa yule dada nae anafanya hivyo hivyo, na nikagundua tena na mamayake mzazi nae alikuwa hivyohivyo na akaachana na mume wake(yaani baba wa yule dada). Nikamuuliza kama ameokoka akasema nimeoka na kila mkutano napita niombewe lakini shida naendelea kuiona. Je hili lilihitaji nini hapa??. kwa kifupi mapepo yalikuwa yanavuruga ndoa zao kwa kuwaoa bila kujitambua, hivyo kulikuwa na manuizi tangia kwa mama yao —–, maana kaka yao hao dada, siku ya kuokoka alipoongozwa sara ya toba alianguka kwa masaa mawili bila kupata fahamu.

  Pia kuna wengine wengi wa kiume na kike ambaye kwa ushahidi wako na mimi tumeona wakipewa special deleverence kwenye mikutano kwa sababu ya matatizo yao magumu kama kuolewa au kuowa au n.k.

  Cha msingi na kusisitiza kwangu si kila deliverence yafaa kwa kila mtu. Na pia wanaofanya hivyo isiwe kama kanuni na msisitizo kwa wote,

  Pia matatizo mengi yanayowakumba waliookoka ni kwa sababu ya kukosa Ujirani na Mchungaji wao tangia siku ya kwanza ya kuongozwa sara ya toba, na mtu anakuwa na siri bila kumwambia mchgj mambo yale anayoyaona si ya kawaidi ktk wokovu ili amsaidie. Tungekuwa kama wale waganga wa kienyeji wakiookoka wanapeleka tunguli zote na kila kitu wanamwambia mchgj. na wanasaidiwa vizuri na hata sasa wengine ni watumishi wa Mungu wazuri.

 32. Ndugu Antony,

  Nadhani hujanielewa kabisa……na yale yote mimi niliyozungumza nimejaribu kusimama katika maandiko tu…..na nimesema wazi sipingi Delivarance….nakubali Yesu anaokoa…..nakubali Yesu anaponya…..Maandiko yanasema hivyo…..na wote tunathibitisha hivyo….!

  Hebu turudi kwenye mifano yako mwenyewe uliyoiitoa…..Yesu kumpaka tope yule kipofu, Sasa unataka kusema nini hapo? Mfano uko wazi Yesu kampaka kipofu matope akapona Period! Au watu walileta vitambaa kwa Paulo vikaombewa na wakapona iko wazi kabisa! Lakini hatujengi mafundisho yoyote kwenye kitambaa…..au Matope!

  Mafundisho ya deliverance mengi yanavuka kabisa ule wigo wa msingi wa Imani! Hebu rudia tena zile sababu 53 za kufunguliwa alizozitoa ndugu Marandu…..baadhi ya mambo aliyoyasema kwanza hazitakiwi kuwa sehemu ya mtu aliyempokea Yesu! Au anayeishi kwa kufuata maneno ya Mungu! Je kama mume anampenda mkewe kama Kristo alivyolipenda kanisa anaweza kufanya haya?

  28 Kumpamimba msichana mwingine halafu unaoa mwanamke mwingine.

  46.kutengana kwa wana ndoa hata ingawa mnakaa nyumba mmoja (mzungu wa nne) kila mtu ana chumba chake.

  41.Kupanga kwamba niki rudi nyumbani tu nitapokeana na mwenzi wangu kwa furaha ghafla unawasili unaingiwa na chuki moyoni juu yake.

  Nataka kukuuliza ndugu Antony Mkristo aliyejaa Roho Mtakatifu…..anayelisoma Neno la Mungu…..aliyeamua kumuishia Mungu anaweza kumpa mimba msichana mwingine halafu akaoa msichana mwingine? Je ni jini mahaba HAPA au huyu mtu yuko dhambini tu? Je huyu mtu anatakiwa afunguliwe na na nini hasa! Huoni ya kwamba kinachotakia ni toba ya kumpokea Yesu! Mkristo wa namna hii hahitaji “Delivarance” anahitaji kumjua Yesu na maneno yake! Au kutengwa asieneze dhambi hiyo katika kundi la waumini.

  Sitaki kuendelea na mengi…..Lakini naona umesema jambo la Msingi……hebu niirudie nukuu yako:

  “Labda tahadhari, unaweza ukawa umeona kufunguliwa kunakofanywa na imani za siku hizi ambazo 90% curt(imani potofu)
  Kiukweli mimi sipo huko!!”

  Kumbe unatambua kwamba kufunguliwa kwingi kunakofanywa na siku hizi kumejengwa KATIKA imani potofu? Sasa ndugu yangu Antony kama kweli kwa tathimini yako ni asilimia 90% ya mafundisho haya ya “Deliverance” ni potofu Kwa nini basi tusitoe tahadhari?

  Hivyo ndugu yangu kuandika kwangu kote nakokufanya ni kutoa tahadhari tu katika mwili wa Kristo! Sina lengo wala nia yoyote ile ya kudunisha au kupinga huduma ya yoyote katika mwili wa Kristo.

  UBARIKIWE!

 33. Shalom wana wa Mungu;

  Amani ipo?Kwa sababu hapa wanasoma wengi sipendelei sana kujibizana kama hakuna sababu ya msingi watanisamehe wale wanaotaka promptly answer.

  NIJUAVYO MIMI Si kila mahali (dhehebu) au kila ufunuo(ie. kufunguliwa) utakufaa wewe ndugu wachangiaji elewa kwamba kusudi la MUNGU ni kukutoa wewe toka vifungo vya shetani sitiri. Kwenye Biblia Wengine waliambiwa ”paka tope kwenye macho”, wakafunguliwa, wengine waliambiwa walete vitambaa, wengine waliambiwa simama na uende zako imani imekuponya, wengine waliambiwa wakanywe kidogo ili tumbo lipone. Sijui Ndugu yangu Orbi, Kinyau na wengine uliambiwa ufanye nini? Mimi nilitembelewa na YESU BILA KUWEKEWA MIKONO MIDA YA SAA 8-9 USIKU(11YEARS AGO) akakinyofoa kifua changu kilichokuwa kimekwisha na kukivisha kipya nikapona UGONJwA WA MOYO Wakati madokta walisema nitaendeleaa na matibu maisha yangu yote na nilikuwa nimeshatibiwa miaka 14 lakini baada ya miaka8 (2008) nilipiga x-ray ambayo nilihitajika kufanya kwa sababu ya kazi(ajira) na ikiwa safi GLORY TO GOD.

  JAMANI WATU WANASHIDA HIZO, WAONEENI HURUMA MSIWAKATISHE TAMAA bila kuweka bayana wafanye nini KAMA WANAPONA KTK MWILI NA ROHO ZAO ZIKASTAWI KATIKA KRISTO waende tu. AU MNATAKA WAENDE LOLIONDO???. au mnadhani hao wenye shida hizo hawajaokoka vizuri????

  Binafsi sijawahi kwenda huku kwenye deliverence kwa sababu sijapata ufunuo huo, ila siipingi deliverence kwa sababu wengi wamepona kwa jina la Yesu matatizo yao likiwemo kama la mchangiaji hapo juu (Kokusima) nina ushahidi kuna machimbuko ya matatizo mengine yanahitaji kufunguliwa, labda kama sielewi kufunguliwa kunakopingwa na Orbi, Kinyau n.k ni nini?

  Labda tahadhari, unaweza ukawa umeona kufunguliwa kunakofanywa na imani za siku hizi ambazo 90% curt(imani potofu)
  Kiukweli mimi sipo huko!!

 34. Kokusima,

  Naomba urudie maelezo yangu…….nimeeleza maana ya kufunguliwa Kibliblia……ni nini? Kwa kifupi mimi nayeeandika nilipoteza pete ya ndoa miaka mingi! Na kila naponunua napoteza……..na Hata sikumbuki pete ya mwisho wapi nilipotezea wapi……na napoandika sasa hivi sina pete ya ndoa kidoleni! LAKINI ……! Ndoa yangu ni Imara kabisa…..!Tuna watoto wazuri wawili…….tuna maisha ya furaha na kama kuna up and down ni za kawaida tu……maana Ndoa yangu haikujengwa kwenye pete….wala sikuunganishwa na mke wangu kwa Pete……..!Ila na Yesu……!Kiapo changu cha uaminifu katika ndoa hakiko kwenye Pete……..bali moyoni…….!Kwa kifupi najua nimemwacha baba yangu na mama yangu na kuambatana na mke wangu……..! Na biblia inanifundisha nimpende mke wangu kama Yeye alivyolipenda KANISA!

  Sasa huo uoga na hofu ya kupoteza pete unatoka wapi?Hapo ndipo tunaposema hayo mafundisho ya “Deliverance”yanajenga hofu…..woga…..wasiwasi na kufanya watu wasiamini NENO LA MUNGU LINASEMA NINI KATIKA MAISHA YAO

 35. Binafsi naona kama mijadala inayoendelea haisaidii sana kujenga. Napenda tu mjue kuwa hapa wanatembelea watu wengi tuu, waliookoka na wasiookoka nawengine wengi tu, kwa mtazamo wangu ni vizuri kama tunapingana katika hilo tukawa na maelezo mazuri kwa wale wanaokumbana na hali au walio na dalili alizozisema mtoa mada. Nasema hivyo kwasababu binafsi nimeguswa na dalili alizozieleza na kwakweli nina tatizo sana tu kwenye ndoa yangu. siwezi kueleza mengi lakini kama ni kuomba nimeomba sana na kuombewa pia. dalili zake zimenigusa sana kwani pamoja na nyingine alizozitaja lakini pia amenigusa aliposema kupoteza peta ya ndoa katika hali ya kutatanisha, kwani hata mimi ilishanitokea na mpaka ninapoandika sasa sina pete ya ndoa kidoleni na ni kweli ilipotea katika mazingira ya kutatanisha kwani hata leo ukiniuliza ilipoteaje siwezi kueleza kwani nilikuwa nimeivaa na nilikuja tu ghafla kushtuka haipo kidoleni, wala ilikuwa hailegei, wala sikuwa na kawaida ya kuivua hata siku moja niwe bafuni au wakati wa kulala, wala sikunyang’anywa na mtu, yaani nasema ni katika hali ya kutatanisha kweli na imeniletea matatizo makubwa kwa mwenzangu wa ndoa kwani pamoja na kuwa siku niliposhuta haipo kidoleni tulikuwa wote, lakini haamini. Labda kufupisha story kama hizo nivizuri mjue kuwa watu wenye matatizo kama aliyoyataja hapo juu wapo wengi tu na nivizuri wakaelezwa cha kufanya ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwani kwa uelewa wangu huko ndiko watakutana na wokovu kama bado hawajaokoka. tukisema tu hakuna mambo kama hayo au tukajiangalia tu sisi tuliookoka na kusema kama watu wanahayo matatizo kwanini wasiokoke bila kuwa polite katika maelezo yetu tutakuwa hatuwasaidii wengi na hasa wale walio wachanga au ambao hawalijui neno na wanakiu ya kupata suluhisho la matatizo yao kupitia kwa Yesu tunayemwamini.

  Mbarikiwe

 36. Ndugu Anthony,

  Naomba nifafanue kidogo swali langu la 5. Natumaini uliposema spiritual war ulikuwa na maana ya vita vya kiroho kwa kiswahili. Je vita hii imekuwa juu zaidi upande upi; wa shetani au upande wa Mungu au pande zote mbili? Swali hili limezingatia pande mbili za ulimwengu wa roho.

 37. Ndugu Anthony na wachangiaji wengine,

  Mimi huwa nina kawaida ya kupitia tena comment za watu wengine ili kuona kama kuna kitu kilichoandikwa ambacho sikukielewa au nilikisoma kwa haraka haraka na kufanya nisipate kile kilichokusudiwa na mchangiaji. Na katika kupitia tena comment ya Anthony ya tarehe 13/09/2011, macho yangu yakaganda sana kwenye kifungu hiki;

  “Kwa kifupi, hali ya maisha ya wokovu yamebadilika sana, hata spiritual war imekuwa juu zaidi; mambo aliyoeleza ndugu fredric, ndio yamepelekea kanisa hadi aibu nyakati zetu(hapa nadhani ndg Anthony aliruka neno ili kuleta maana aliyokusudia)…….. Ndugu wachangiaji hapo juu, mnahabari kwamba hizi roho za kikahaba ndivyo zilivyopenya zikaingia kama mchwa na kufanya watu wawe mashoga? roho hizi ndio hizo zinazofanya mtu asipende mke wake ila ampende mwanaume mwenzie……”

  Nakubaliana na ndg Anthony kuwa nyuma ya shoga na ushoga kuna roho chafu, lakini nina maswali haya kwake;

  1. Je roho hizi zimewaingia watu waliokoka kweli?

  2. Unaposema maisha ya wokovu yamebadilika sana, una maana wokovu kwa sasa upo kama fashion za nguo zinavyoweza kubadilika kufuatana na muda, mahali n.k?

  3. Je wokovu kwa mtu aliyeokoka unakuwa governed(unaendeshwa) na hali ya maisha yake au hali ya maisha ya mtu yanakuwa governed na wokovu wake kwa njia ya Yesu Kristo?

  4. Je hizi roho za kikahaba hazikuwepo wakati wa kanisa la mwanzo? Na kama zilikuwepo, wenzetu wa kanisa la mwanzo waliwezaje kuzishinda roho hizi kiasi kwamba hazikuweza kuingia kama mchwa kwao na kuwafanya wawe mashoga? [(yaani wale waongofu wa kanisa la kwanza (sio jamii ya wakati huo)]. Je kwa nini sisi(kama kanisa la sasa)kama waongofu wa sasa tumevamiwa na roho hizi? Wakati unajibu swali hili zingatia au fanya marejeo(reference) kwenye kitabu cha Mwanzo 19:4-11, nanukuu mstari wa 5 tu; “Wakamwita Loti wakisema, ‘Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? WATOE NJE KWETU ILI TUWEZE KUWALAWITI” Pia kama marejeo soma Warumi 1:18-32, nanukuu mstari wa 27 tu; “Vivyo hivyo wanaume pia wakiacha matumizi ya asili ya wanawake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wakafanyiana matendo ya aibu na wanaume wengine nao wakapata katika maisha yao adhabu iliyowastahili kwa ajili ya upotovu wao”

  5. Una maana gani kusema spiritual war imekuwa ya juu zaidi?

  Ndugu Anthony, katika comment yako ya tarehe tajwa hapo juu, umetuomba tutafakari toka 1 Thesalonike 5:23 na Nehemia 1:4-7. Ni kweli kwamba kila aliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake anatakiwa atakaswe roho, mwili na nafsi yake; LAKINI, je anatakiwa atakaswe kwa huduma ya ‘deliverance’? Nini kinachotakasa roho, mwili na nafsi ya mtu?

  Hebu soma maneno haya toka Injili ya Yohana 17:17
  “UWATAKASE KWA ILE KWELI, NENO LAKO NDILO KWELI”

  Kwa hiyo Neno la Mungu ndilo limtakasalo mtu na biblia inasema wazi kuwa Neno ni Yesu. Neno la Mungu ni chakula cha roho zetu, Neno la Mungu ni uzima wetu, Neno la Mungu ni taa na mwanga wa njia zetu zote, Neno la Mungu ni kila kitu kwetu sisi tulionunuliwa kwa damu ya thamani ya Bwana wetu Yesu Kristo.

  Kwa kifupi niseme tu kwamba wokovu is a full package and deliverance is within it. Mtu akiokolewa anakuwa amepata a complete package; deliverance, redemption, salvation, etc, zimo ndani na anakuwa amepata yote. Pakitokea mtu amefungulia mlango(amebomoa boma au ukuta) na shetani kurudisha nguvu zake za giza ndani yake baada ya kuokoka, dawa sio kufanyiwa ‘deliverance’, bali ni KUTUBU ILI KUZIBA TUNDU MAHALI PALIPOBOMOKA na kuruhusu uovu kuingia tena ndani yako (Methali 28:13,1 Yohana 1:8-10, Ezekieli 13:5,22:30, Isaya 1:18, Ufunuo 7:14 n.k).

  Mungu atuwezeshe kulijua zaidi Neno lake kuliko kitu kingine chochote.

 38. Ndugu Kinyau,

  Asante kwa Mchango wako, na umenigusa sana kwa yale maneno ya Yesu…..kwamba tukimpokea Yeye na Baba watafanya makao ndani mwetu! Na kwa wale ndugu zangu ambao wanadhani napinga “DELIVERANCE” Msimamo wangu ndio huu;

  Ugonjwa mkubwa ambao nauona katika mafundisho haya ya “Delivarance” ni kuwa Wakristo wengi leo hawafundishwi wao ni nani katika Kristo Yesu! Na kama wanafundishwa wao ni nani katika Kristo Yesu basi ni wakati wanatafuta “baraka” na “mafanikio” LAKINI SIO KATIKA KUENENDA KATIKA NJIA!

  Napenda nieleweke wazi kuwa sipingi mafundisho ya “Deliverance” bali napinga mafundisho haya ya “Deliverance” ambayo iko kinyume na maneno ya Mungu! Ningependa kusema pia mimi NIMEOKOKA nimekubali WOKOVU…..Lakini napinga mafundisho ya WOKOVU yanayosema tunaupata Wokovu tulipobatizwa watoto wachanga…..au…nilipopata Kipa Imara…..au…..niliposhika mafundisho ya Kanisa! Kumbuka mafundisho haya yote yanafundisha WOKOVU……Lakini si ule Wokovu ulio ndani ya NENO LA MUNGU! Kwa Mantiki hiyo pia nakubali mafundisho ya “Deliverance” au “Kufunguliwa” Lakini ambayo yamesimama katika Msingi Imara wa mafundisho yaliyo katika wigo wa Biblia tu….au mafundisho ya Yesu na mitume wake!

  Kwa kifupi kabisa WOKOVU WA YESU UNAMKOMBOA MTU! Ndio “Deliverance” yenyewe! Na wala sio “package” tofauti au ianyotolewa mbali na WOKOVU! Na Yesu alipoanza kuhuburi maneno yake ya Kwanza kwa kusoma kitabu cha Luka alisema hivi “ROHO WA BWANA YU JUU YANGU, KWA MAANA AMENITIA MAFUTA KUWAHUBIRI MASKINI NJEMA, AMENITUMA KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO…….KUWAACHA HURU WALIOTESWA…….KUTANGAZA WAKATI WA BWANA ULIO KUBALIKA!

  Sipendi kuchukua muda kufundisha nini kinatokea katika maisha ya Mkristo anapofungua moyo wake kwa njia ya toba……na kuamua kuacha maisha ya dhambi na kuamua kumfuata Kristo…….lakini linatokea ni jambo kubwa mno! ni kuwa Muumini huyo anakuwa AMEFUNGULIWA! AMEFUNGULIWA NA KAMBA ZOZOTE ZILE ZA IBILISI…….HATA KAMA MUUMINI HUYO HAONI KWA MACHO YAKE LAKINI NENO LA MUNGU LINASEMA HIVYO!

  Paulo anasema Yesu “AMETUHAMISHA KUTOKA NGUVU ZA GIZA NA KUTUINGIZA KATIKA UFALME WA MWANA WA PENDO LAKE……TUNATIWA MUHURI WA ROHO YULE WA AHADI…….UHAI WETU UMEFICHWA KATIKA KRISTO YESU…..na Paulo anasema…SASA TUSIENDELEE KUVITOA VIUNGO KUWA SILAHA ZA DHAMBI…….KWA MAANA TUMEUNGANIKA NAYE…..hivyo TUNATAKIWA TUENENDE KATIKA UPYA WA UZIMA!

  Hivyo wapendwa hakuna “package” ya tofauti au package ya “deliverance baada ya kumkabali Yesu kama Bwana na Mwokozi!

  Kama hatuenendi kwa ushindi…..au tunaishi katika Dhambi……basi ni kuyaangalia maisha yetu what went wrong! Neno la Mungu halikosei! Yesu hawezi kukaa na “Jini mahaba” pamoja ndani ya mioyo yetu! Jini mahaba HAWEZI kuingia katika maisha yetu kama HATUJAMRUHUSU! Kwa kifupi tu kukiruhusu maisha yetu yaenende KINYUME na maneno ya Mungu……tunaruhusu kila kitu kutoka kwa mwovu! Na dawa yake si DELIVERANCE……bali ti toba……na KUMRUDIA MUNGU! Hivyo ndivyo Neno la Mungu linafundisha!

 39. Wapendwa,

  Huu ni mjadala unaoendelea….hii ni nukuu yangu ya August 4th 2010……”Kwa nini bado mtu anasumbuliwa na vifungo”

  Watu wa Mungu msimamo wetu kwenye jambo lolote lazima uwe katika maneno ya Mungu, wala sio mafundisho ya mtu yoyote, experience zetu zisitulazimishe tutengeneze doctrines ambazo haziko kwenye Neno la Mungu……..

  Sijaona mahali popote ndani ya Biblia ( Agano Jipya) Huduma ya “Delivarence” …………..Kwa kifupi kuanzia kitabu cha matendo ya mitume hadi ufunuo humuoni Petro, Yohana, Paulo, Luka akiwafanyiwa wakristo waliookoka “Delivarence” hata kuwafundisha tu……….!

  Nini tunachoona katika makanisa yote ndani ya Agano jipya, Ni wakristo ( Watu wenye Dhambi) wakipokea msamaha wa Mungu katika Kristo Yesu, wakizaliwa upya katika roho, na kujazwa na Roho Mtakatifu……wakihamishwa kutoka nguvu za giza na kuingia katika ufalme wa Mungu, Wakilindwa na nguvu za Mungu, wakiambiwa tazama yote yamekuwa mapya, wakiambia walikufa pamoja na Kristo na na wamefufuliwa pamoja naye na sasa wanatakiwa waenende katika upya wa uzima, na uhai wao umefichwa katika kristo Yesu, na pia wemekirimiwa tabia ya kiungu na mzao mtakatifu wa Kikuhani, na wanakumbushwa kuwa hapo awali walikuwa wazinzi, waaasharati, wachawi, watukanaji, wafiraji…..lakini SASA wamesafanishwa na kufanywa wapya!!! na wanaambia wakienenda Kwa ROHO KAMWE HAWATAZITIMIZA TAMAA ZA MWILI!……Hatuoni kabisa huduma ya “Delivarence” !

  Isipokuwa Wakristo waliokoka wanaambia wakue wasiwe tena watoto wachanga, ili wamfikie Yeye ( Kristo) katika yote……na wanambia kushindana kwetu sisi ni dhidi ya pepo wabaya na nguvu za giza katika ulimwengu wa roho……na tuzivae silaha zote za Mungu ili tupate kushinda! Sio kufanyiwa ” Delivarence” na hata tukishindwa tunakumbushwa Kutubu na kumrejea Mungu….kama vile makanisa saba ya Asia yalivyofanyiwa……!!!

  Hivyo ndugu yangu ni Imani ile ile iliyotuokoa, na ile ile iliyotufanya tumpokee Roho wake ndio itakayo tusimamisha! Tulianza kwa Roho je tunataka tumalize kwa”Delivarance” ? Tumelogwa kiasi hicho…..! Mungu na atubariki na kutufungualia neema yake tujue uweza waka kwetu sisi tuaminio, kwani Injili ni Uweza wa Mungu uletao Delivarence kwa kila aaminiye

 40. Pepo dume, pepo jike, bla blaa vyote hivyo ni elimu ahera na elimu dunia. Sijaona hii kwenye Biblia

 41. Ndugu katika Kristo, Bwana wetu. Naomba Roho Mtakatifu awe pamoja nasi sote ili tupate kutenda na kupokea yampendezayo Yeye aliye Mtakatifu sana.
  Nina uhakika sawa na mchangiaji Rosemary hapo juu ya kwamba labda ni jinsi mpendwa Marandu alivyoweza kuwakilisha mbele yetu kile alichofundishwa, ya kwamba labda hakijaeleweka vizuri au kimeeleweka vizuri; na natumai amekaa kimya kuona ni kwa jinsi gani atawezeshwa kuwakilisha mada hii kwa utimilifu.

  Yohana 5:39

 42. Shalomu,

  TAZAMA IMEKUWA MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA, YA KALE YAMEPITA, YOTE YAMEKUWA MAPYA.

  Kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako ndiyo suluhisho la kila kitu. Yesu anasema kuwa Yeye (Yesu) na Baba (MUNGU) watakuwa ndani ya huyo mtu aliyeamini na huyo mtu atakuwa ndani ya Yesu na Baba. Sasa kama Mungu na Kristo wapo ndani ya mwamini, na mwamini yupo ndani ya Yesu, hayo majini yatakaa wapi?

  Wapendwa, kama walivyosema wengine hapo juu, deliverance ya kweli ni kuokoka, mtu anapookoka anapata deliverance kwa kuwa anahamishwa kutoka katika ufalme wa giza na kuingizwa katika ufalme wa Mwana wa Pendo lake. Baada ya kuingizwa katika ufalme huo, huyo mtu anapewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule mwovu. Hivi kweli mapepo na majini yanaweza kuingia na kukaa mahali alipo Kristo Mfalme wa Wafalme? Yaani Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai akae Hekalu moja ya Majini? Hivi majini na mapepo yanawezaje kuendelea kukaa ndani ya Mtu aliyepewa mamlaka kuyakanyaga?.

  Tatizo la mafundisho ya Deliverance ni kuufanya wokovu uonekane kuwa duni na kuwa kuokoka hakutoshi bali deliverance, huu si msingi wa neno la Mungu.

  Katika maisha yangu nimeona watu wanaokoka na kwa kitendo cha kule kuokoka wanafunguliwa na kuwa huru kabisa kutoka kwenye kila aina ya vifungo, ni kile kitendo cha kuokoka, ndicho humuweka huyo mtu huru mbali na kila aina ya vifungo. Baada ya hapo huyu mwamini anatakiwa aendelee kuukulia wokovu ili aweze kumjua zaidi Kristo.

  Naomba niseme kuwa mtu anaweza kupagawa na mapepo au majini, lakini hayo yatatokea kama amefungua mlango kwa maisha ya dhambi yaliyo kinyume na Mungu na ndipo shetani kuweza kuingia na kumletea mateso ambayo dawa yake ni toba ya kweli itakayorudisha uhusiano wa huyo mtu na Mungu wake. Mtu hawezi kuendelea kusema uongo, kufanya uzinzi, kuvuruga ndoa yake kwa kisingizio kuwa hajafanyiwa deliverance, hapana, anaendelea kwa kuwa hajaamua kutubu na kuachana na maisha ya dhambi. Dawa ya dhambi ni toba na siyo deliverance.

  Shalomu,

  Mungu awabariki na kuwazidishia neema na wema wake siku zote.

 43. Ndugu Anthony.

  Sidhani kama kuna mtu anatoa comment zake kwenye blog hii ili aonekane msomi kumzidi Mtume Paulo au mwana theolojia yeyote wa Kitanzania aliyepo kwa wakati huu.

  Kwenye masuala haya ya Mungu hakuna usomi wa kumzidi mwenzako, bali ni jinsi unavyojikabidhi na kujinyenyekeza kwa Roho Mtakatifu ili akufundishe na kukufunulia siri zilizoko nyuma ya maandiko yake. Kumbuka Yeye(Roho Mtaktifu) ndiye aliyewaongoza waandishi wote wa Biblia(neno la Mungu) katika kuandika haya tunayoyasoma leo akiwepo Mtume Paulo, hivyo anajua kila kitu; kazi ni kwako wewe kujinyenyekeza kwake na kusema kuwa una udhaifu wa kuelewa kile kilichoandikwa ili akufungulie macho yako ya ndani na akili zako na ufahamu wako ili uweze kuelewa na maandiko.

  Hebu soma kifungu hiki toka Yohana 7:14-15;
  “Ilipokaribia katikati ya Sikukuu, Yesu alipanda kwenda hekaluni na kuanza kufundisha. Wayahudi wakastaajabia mafundisho Yake wakasema, ‘Mtu huyu amepataje kujua mambo haya bila kufundishwa?”

  Hawa watu walimshangaa sana Yesu kwa mafundisho yake kwa sababu kwenye jamii hiyo hakuonekana kuwa msomi hasa wa masuala ya dini na sheria za Musa yaani Torati. Siyo tu kwamba alikuwa anakijua kile alichokuwa anakifundisha, bali aliwawezesha hata waliokuwa wanamsikiliza kuona au kufahamu kitu kilichokuwa tofauti na kile walichokuwa wanafundisha wasomi wa masuala ya dini na sheria za Musa. Huo ndio uzuri wa kukaa na kumsikiliza na kunyenyekea na kumpa heshima anayostahili Roho Mtakatifu.

  Roho Mtakatifu anaweza kumfundisha mambo ya Mungu mtu ambaye wewe unamuona sio msomi na asimfundishe yule ambaye wewe unamuona msomi sana. Mungu huviinua vilivyo vinyonge na vidhaifu ili aviangushe vile vinavyoonekana vina nguvu.

  Orbi amezungumza mambo ya msingi sana kwenye mchango wake wa leo na kwa kweli hili swala la ‘deliverance’ limeliletea kanisa ugonjwa mbaya sana wa watu kutotaka kulitafakari neno la Mungu mchana na usiku (Yoshua 1:8) badala yake watu wanataka kufanyiwa deliverance tu. Rosemary amesema sasa watu wanaanza kwa nje kwenda ndani badala ya ndani kuja nje, maana yake tumekuwa kinyume kabisa na kusudi la Mungu. Neno la Mungu ndilo linalookoa na kuondoa nguvu zote za giza ndani ya mtu. Hakuna hata mahali pamoja kwenye biblia ninayoisoma mimi panaposisitiza watu watafakari deliverance au miujiza yoyote ile kwa ajili ya wokovu wao. Kolosai 3:16 inatusisitiza kuwa neno la Mungu likae kwa wingi ndani mwetu.

  Swali ninalojiuliza ni kwamba inakuwaje mtu aliyeokoka kikweli awe bado ndani yake na majini na mapepo yanayomsumbua? Kama Orbi alivyosema ukiona kitu kama hicho, shida haiko kwenye uweza wa neno la Mungu katika kuokoa, bali shida ipo kwa huyo mtu mwenyewe, bado anakuwa kwenye mashaka juu ya uwezo na nguvu za Mungu za kushinda nguvu za giza zilikuwa ndani yake kabla hajaokoka. Mashaka ni adui mkubwa wa wokovu! Na shetani hutumia mwanya huo kurudisha majeshi yake kwa mtu mwenye mashaka juu ya wokovu wake.

  Kwa hiyo ndugu yangu Anthony hakuna mtu anataka kuwa msomi kumzidi Paulo wa bible, bali kila mtu binafsi anajitahidi kunyenyekea kwa Roho Mtakatifu ili Roho mwenyewe aweze kumfundisha, kitu ambacho hata Mtume Paulo alisema hivyo kwenye Wagalatia 1:11-12;
  “Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu. KWA MAANA MIMI SIKUIPOKEA HIYO INJILI KUTOKA KWA MWANADAMU, WALA SIKUFUNDISHWA NA MTU, BALI NILIIPATA KWA UFUNUO KUTOKA KWA YESU KRISTO”

  Yesu bado ni Yeye yule jana, leo na hata milele na kupitia Roho wake bado anatufulia na kutufundisha hata sisi wa kanisa la leo.

  Ubarikiwe na Bwana.

 44. shalom wapendwa,
  ni kweli hii mada inaleta mkanganyiko, ndugu Marandu anaweza kuwa na nia nzuri ila mafundisho alipewa au kutoa ndio sio sahihi.
  Ni kweli hata mie mwanzo sikuwa najua kwanini sio sahihi ni kwasababu unaanzia mwilini(majini) badala ya Rohoni ndio kama wagalatia waliambiwa na Mt Paulo: Galatia 4:9 Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena?
  Ndugu zangu tunachopinga wenzenu ni hiyo glorification au kuukuza uwezo wa ibilisi badala ya kuukuza na kuuelezea uwezo mkuu wa Mungu wetu.
  Mtume Paulo anasema Filipi 4:8-9 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
  Kwa kifupi wewe hubiri neno lal Mungu, watu watubu, waokolewe, kama wapo vifungoni watafunguliwa kwa Jina la Yesu, Roho Mt atawaongoza ktk kufunguliwa kutoka hizo nguvu za giza. lakini ukianzia vifungo na aina zake, je haya mafundisho unayatoa wapi? ndipo unapokuta mtu anajifunza na kutafakari aina za majini na kazi zake na uwezo wake kwa binadamu, sasa unakoipata hiyo elimu ndo kurudi ktk mafundisho yasiyofaa na rahisi wewe kutekwa ili upate ufumbuzi wake au muumini mchanga kupotea. Unachopaswa ni kuhubiri ukuu wa Mungu na unapokiri uwezo wake na walio wachanga wanapokiri pia wanakuwa kiimani na wanafunguliwa. Tunapaswa kuutafakari ukuu wa Mungu, tunapaswa kutafakari yaliyo ya haki tu, Yeye Mungu atatupa amani ndani yetu ipitayo yote. Ndivyo ninavyoelewa kwa ufahamu wangu tuzidi kujuzana.

 45. Ndugu Antony na ndugu Taru

  Kukubali kwako mafundisho ya “Delivarance” hakufanyi mafundisho hayo yawe ni ya kweli na mimi kuyakataa mafundisho hayo hakuyafanyi yawe ya uongo!La Msingi ni Je Maandiko yanasemaje!Yesu anasemaje? Mitume walifundisha hilo? Kanisa la Kwanza na Paulo aliyetujengee msingi wa Imani hii alifundisha hilo? Experience zetu haziwezi kupindisha ukweli wa Neno la Mungu! Kila siku lazima tujifunze kusema Je Maandiko yanasemaje! Sio experience zetu zinasemaje!

  Nashangaa sana unaposema kuja kwa “Mafundisho ya Delivarance” ni kwa sababu nguvu za Kanisa zinapungua! Kwa kifupi kabisa kama kuna nguvu au uwepo wa Mungu unapungua katika kanisa ni kwamba Mwenye nguvu hayupo katika kanisa! Yaani Roho wa Mungu…..au Neno la Mungu LILILO HAI HALIFAPEWA NAFASI! Au mafundisho ya msingi ya kuwakuza wauumini yametupiliwa mbali…..na kila mtu amekuja na mafundisho kama aonavyo yeye!

  Kumbuka kuwa uovu au matendo ya giza yako pale pale…….Shetani aliyekuwepo kanisa la kwanza ndiye anayefanya kazi leo! Na kama kweli “mafundisho ya delivarance” kama yanavyofundishwa na wengi leo yangekuwa yamesimama katika msingi wa Maneno ya Mungu basi Paulo angeyafundisha katika nyaraka zake kwa kanisa la Wakorintho! Hebu soma uchafu na maasi katika kanisa hilo……hakuna tofauti na hali za waumini katika baadhi ya makanisa hata yale yanayokiri wakovu leo!

  Paulo anasema kuwa kanisa hilo lilikuwa na mambo machafu ambayo hayakuwapo hata kwa mataifa! ” YAKINI HABARI IMEENEA YA KUWA KWENU KUNA ZINAA ……NA ZINAA YA NAMNA ISIYOKUWAKO HATA KATIKA MATAIFA” (1cor 5:1)

  Je ni wapi Paulo alikuja na haya mafundisho haya ya “Delivarance”? Kama kweli haya mafundisho ndiyo yanaweza “kuwakwamua wauumini wanapokwama na kutatizika na uzinzi…..ulawiti…….ufiraji…..ulevi….utukanaji……tamaa…. basi mahali pake pakuyakuta mafundisho haya katika Agano Jipya palikuwa ni katika Kanisa la Wakorintho! Paulo hakufanya hivyo! Paulo ALIWAFUNDISHA! PAULO ALIWAKUMBUSHA WAO NI NANI KATIKA KRISTO YESU!

  Hebu angalia Paulo alisema nini ” JE HAMJUI YA KUWA MWILI WENU NU HEKALU LA ROHO MTAKATIFU (sio la INCUBUS) ALIYE NDANI YENU MLIYEPEWA NA MUNGU” Na uliendelea kusoma kitabu Kizima cha Wakorintho wanaambia warudi na Kukaa “KATIKA KRISTO” Hakuna mahali hata kidogo alikuja na hii Injili ya “Delivarance kwa muumini!

  Kwa kifupi ndugu yangu Antony…..hata yale Makanisa saba ya Asia….ambayo baadhi yake yalikuwa katika lindi nla UOVU yaliambia “BASI TUBU”

  Na je tukirudi katika mafundisho ya Yesu Sura ya 15 ! Hebu isome tena! “NINYI MMEKWISHA KUWA SAFI KWA NENO NILILO WAAAMBIA……KAAENI NDANI YANGU NAMI NDANI YENU” ……hebu soma sura nzima uone muumini ni nani Katika Kristo!

  Mafundisho haya ya Delivarance kwa mtazamo wangu mimi ni short cut ya Shetani ili waumini tusikae ndani ya Yesu……na tusifanye TOBA halisi kwa uovu ambao wengi tumeuruhusu katika maisha yetu! Na kufungulia nguvu za giza…….au kujenga hofu katika maisha yetu….na kusahau kuwa aliye NDANI YETU NI MKUU KULIKO ALYE KATIKA DUNIA! Na badala ya kumwendea na Kumrudia Yesu Mwanzilishi wa Imani yetu…..tunawafuata “walimu” wenye “mafundisho yenye mfano wa nuru……”ANGALIENI MTU ASIWAFANYE MATEKA KWA ELIMU YAKE YA BURE NA MADANGANYO MATUPU KWA NJINSI YA MAPOKEO YA WANADAMU!

  Kwa kifupi kabisa kama haya mafundisho ya “Delivarance” kama yanavyofundishwa na baadhi ya waalimu au katika baadhi ya mimbari za makanisa mengi ni kweli, basi Waraka wa kitabu cha Waefeso na Wakolosai inabidi tuuondoe katika Biblia!

  Kwangu mimi siogopi kabisa kusema kama Paulo ” NAJUA MIMI BAADA YA KUONDOKA KWANGU MBWA MWITU WAKALI WATAINGIA KWENU WASILIHURUMIE KUNDI (KANISA) NA KATIKA NINYI (yaani kutoka ndani ya Kanisa) WATAINUKA WATU WAKISEMA MAPOTOFU WAWAVUTE WANAFUNZI WAANDAMIE WAO” (Act 20:18)

  Haya mafundisho yameingia katika Kundi na kuleta mkanganyiko! Nimeona ndoa zikivunjika! Nimeona wakristo badala ya Kutubu na kuacha dhambi wanadai watolewe pepo la Uzinzi…..uongo….ukahaba…..nk! Dhambi hutolewa kwa toba…kujuta…..na kuikubali kazi ya Yesu Msalabani……! Kuishinda dhambi hakuji kwa kwa kufanyiwa Delivarance! Paulo wala Mitume hawakufanya hivyo! Yesu akikaa ndani Yetu…..Roho wa Mungu akifanya makano katika Maisha Yetu……Neno lilohai la Kristo likiumbika ndani mwetu…….tutasema kama Paulo…..”KATIKA YOTE TUNASHINDA”

  UBARIKIWE!

 46. Ndugu Taru,

  Sikatazi kabisa mtu kukubali mafundisho ya Ndugu Marandu…..Kama mtu anajiona kaokolewa na Yesu na bado ana hilo jini la “INCUBUS” basi ndugu Marando katoa dawa! Dawa haiko kwenye wigo wa Maandiko bali ni kama mganga yoyote wa kienyeji……!

  Halafu unaponiuliza dalili za mtu mwenye Kiburi ni zipi…naomba nipe ufafanuzi…..maana swali lako ni pana mno!

  Hebu turudi kwenye NENO wapendwa!

 47. Shalom Wana wa Aliye Juu!!

  Ninaomba niwashauri kitu, KAMA HUJAELEWA VIZURI USICOMMENT AS IF WEWE NDIO MSOMI WA ELIMU YA JUU KULIKO PAULO WA KWENYE BIBLE. NA UPOLE WENU UJULIKANE WAZI.

  PILI. kwa ufahamu wangu mdogo siku hizi katika wokovu, kuna watu wanaokubaliana na habari za ”deliverence” . na kuna watu wanapinga ”deliverance” wanaamini kwamba kuokoka ni all about kufunguliwa. Mafundisho ya ndugu Fredric ni yahusuyo deliverence na yako sawa kwa mtu anayeelewa kuhusu kufunguliwa. kama huelewi yanasumbua sana hata mimi niliwahi kupinga sana; lakini kwa kadri ya kukua kwangu nikaja kuelewa kwa neema ya MUNGU.

  TAFAKARI MAANDIKO HAYA:1thesol. 5 :23Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa, roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, nanyi mhifadhiwe kikamilifu bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. 24Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo.

  Nehem1: 4 Niliposikia mambo haya, niliketi na kulia. Kwa siku kadhaa niliomboleza na kufunga na kuomba mbele za Mungu wa Mbinguni. 5Kisha nikasema:
  “Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, mkuu na mwenye kuogofya, ambaye hulishika agano lake la upendo na wale wampendao na kutii amri zake, 6masikio yako na yawe masikivu na macho yako yafunguke kusikia maombi ya mtumishi wako anayoomba mbele yako mchana na usiku kwa ajili ya watumishi wako, watu wa Israeli. Ninaungama dhambi za Waisraeli, pamoja nami na nyumba ya baba yangu, tulizotenda dhidi yako. 7Tumetenda kwa uovu sana mbele zako. Hatukutii amri, maagizo na sheria ulizompa Mose mtumishi wako.

  Kwa kifupi, hali ya maisha ya wokovu yamebadilika sana; hata spiritual war imekuwa juu zaidi; mambo aliyoeleza ndugu fredric, ndio yamepelekea kanisa hadi aibu nyakati zetu, NIKISEMA KANISA NAMAANISHA KANISA LA KRISTO. ndugu wachangiaji hapo juu, mnahabari kwamba hizi roho za kikahaba ndivyo zilivyopenya zikaingia kama mchwa na kufanya watu wawe mashoga? roho hizo ndio hizo zinazofanya mtu asipende mke wake ila ampende mwanaume mwenzie? Jamani kama sisi tunakuwa hatuwezi kutafakari kwa kina hata kujua kwa nini NGUVU YA MUNGU INAPUNGUA KATI YA KANISA LA LEO? HADI wengine wanaongeza nguvu za KiMungu kwa waganga? Hali alizoeleza hapo fredric ndio zimewapata hata watumishi wakubwa hadi aibu leo hii wanaenda gesti na nyumba ndogo huku wakiwa na wake zao wazuri kabisa?

  Kwa kifupi kama watu wangeishi kama siku yao ile ya wokovu mkuu roho hizo zisingewapata na kufunguliwa kungekuwa hakuna maana. kwani YESU mwenyewe angeendelea kuwa fungua day after day. lakini kulingana na maisha ya wakristo wengi leo. imebidi kitu kama deliverance kiwepo; na kwa mtazamo wangu ni uamsho na nguvu mpya.

  niishie hapo na andiko hili.1thesol. 5 :23Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa, roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, nanyi mhifadhiwe kikamilifu bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. 24Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo.
  Anthony

 48. Ndugu Taru,

  Naomba ninukuu ulivyoandika;

  “Bwana Yesu Asifiwe wachangiaji ndugu Orbi, Vaileth, Kinyau naombeni mnielezee kwa kina dalili za mtu mwenye kiburi”

  Sasa ndugu yangu Taru, hapakuwa na mada yoyote inayohusu mtu mwenye kiburi dalili zake ni zipi, mimi nitaanzaje kukueleza dalili za mtu huyo nje ya mada tuliyokuwa nayo? Ndio sababu nikashangaa kwamba sijaandika popote kuwa kwa uchangiaji wa watu wengine au kutoka kwa mtoa mada au somo kuwa ana kiburi, mimi nikueleze wewe dalili za mtu mwenye kiburi kwa msingi gani?

  Kwa mchango wako wa pili ndio umejieleza vizuri kwamba wewe umetuona/umeniona sisi/mimi tuna/nina kiburi kwa comment zetu/yangu kuhusu mada hii, na ndipo nilipokuomba au ninakuomba unionyeshe kwenye mchango wangu mahali ambapo nimechangia kwa kiburi tena kwa kuzuia au kushawishi wengine wafuate tu kile ambacho mimi nilikiandika na kusababisha kuwanyima wengine uhuru wa kuchangia au kuamini kile amabacho ndg Marandu amekifundisha hapa.

  Kwa taarifa yako ndoa yangu ina miaka 19 na miezi mitatu mpaka itakapofika tarehe 20/09/2011, na kwa kipindi chote hicho haijapata kuumwa kiasi cha kutaka uponyaji unaohusiana na somo alilofundisha ndg Marandu. Hata kama ningekuwa katika kuhitaji uponyaji wa ndoa yangu, bado ningeng’ang’ana na neno la Mungu kujua linasema nini kuhusu ndoa na wala sio kwenye kuolewa na majina mahaba na vitu vinavyofanana na hivyo. The Word of God is Supreme to me than anything else. Uhai wangu na wa mke wangu na wa watoto wangu na wa ndoa yangu, wote umefichwa au unapatikana ndani ya Neno la Mungu.

  Nimekusamehe kwa kuniona nina kiburi.

 49. ndugu kinyau haggai
  naomba kusema kuwa hujaelewa swali langu.nimemeuliza vizuri tu kwamba mniambiea mtu mwenye kiburi ana dalili zipi wala sijamaanisha kuwa umesema mtoa mada ana kiburi.na pili nikasema kuwa ninyi ndio wenye dalili ya kiburi kwasababu mtu hawezi toa mada yake halafu mkaiponda saana yaani kama vile mnashawishi watu wasikubaliane nayo na huku ninyi wenyewe ndio msiokubaliana nayo.hebu muwape watu wengine nafasi ya kujifunza.
  samahani kwa kukukwaza ndugu,lakini jitahidi kupitia hilo somo pia ili uweze kuiponya ndoa yako kama umeoa au kama bado uwe na ndoa ya kumpendeza mungu.
  ubarikiwe

 50. Mpendwa ndugu Taru,

  Kabla ya kujibu swali au maswali yako, naomba pitia tena comment zangu juu ya mada hii, halafu unionyeshe mahali popote nilipoandika kwamba kuna mtu ametoa mchango wake kwa kiburi au aliyeleta mada hii ana kiburi!

  Kumwambia mtu kuwa unachokifundisha hapa hakiko katika msingi wa neno la Mungu siyo kumwona mtu huyo kuwa ana kiburi. Nina uhakika umenielewa vibaya na kunidhania kwa jambo ambalo sijalisema kamwe.

  Amani ya Bwana iwe nawe.

 51. Asante sana Orbi. Hivi ni kwa nini watu hawapendi kuwafundisha watu wengine mambo yale yaliyopo kwenye Bible tu? Tusijifanye sisi ni wajuaji kuliko Bwana wetu Yesu. Mbona Yesu na mitume hawakufundisha hayo mambo? Hizi ndizo zile ziitwazo heresy -mafundisho potofu ya kuwapotezea watu muda na kuwaingizia hofu. Speak the Word only! The Word of God is impregnable and infailable! The Word of God will endure forever- Psalm 119:89. When the Word of God is spoken the gates of hell shakes and crambles! Let us speak only the Word. Tuache kuongea mafundisho/mapokeo ya kibinadamu maana hayana lolote,hayataweza kumshinda na kumfukuza adui Shetani.

 52. Bwana Yesu Asifiwe wachangiaji ndugu Orbi,Vaileth, Kinyau naombeni mnielezee kwa kina dalili za mtu mwenye kiburi. Je kutofurahia ndoa kwa mtu mwenye ndoa ni jambo la kawaida tu. Je, biblia inaposema tutaota ndoto,tutaona maono,je tukiota ndoto za kucheza na nyoka hiyo ni ndoto, hasa Mungu alitaka tuote au ni ndoto iliyotoka kwa ibilisi. Hiyo ni dalili mojawapo ya kibur? msipende kuandika comments za kufanya watu wengine wasijifunze, achieni watu uhuru wa kusoma,kutambua na kuchukua uamuzi wenyewe kwenye mioyo yao. Mbarikiwe kwa kubadilika

 53. Iqualiptus,

  Kwa upande wangu sishambulii bali natoa mawazo yangu tu …….si lazima mtu aseme huu ni ufunuo mpya ndio ukawa ufunuo mpya! Paulo alisema ‘LAKINI WAKO WATU WAWATABISHAO NA KUTAKA KUIGEUZA INJILI YA KRISTO”

  Injili ya Yesu inayomtoa Mtu dhambini…..katika nguvu za giza…..halafu mtu huyo tena anaambiwa ana “Jini mahaba” kwa sababu zisizopungua 53! Tena zenyewe zinapingana pingana na hazijasimama katika hata ANDIKO Hii ni Injili nyingine! Hatujaona Paulo na Mitume na hata Bwana wetu Yesu Kristo akifundisha hivyo.

  Kwa kifupi siyakubali KABISA HAYO MAFUNUO/MAFUNDISHO YA NDUGU MARANDU! Sina hata muda wa kwenda kipengele hadi kipengele……nitakuwa napoteza muda wangu!

  Kachukua mstari katika Biblia (out of context) na kuanza kububujika mtiririko wa mafundisho ambayo hayako kabisa katika msingi wa maneno ya Mungu! “JE HIZO DALILI ZA JINI MAHABA ZIKO WAPI KATIKA BIBLIA?

  Kwa kifupi kabisa haya ni mafundisho ya kuwachanganya waumini wasiikulie NEEMA ya wokovu…..Kujenga Hofu na kuwafanya wawe vipofu kwa kutojua ni nini Kilifanyanyika Msalabani!

  Mafundisho haya ndiyo yale Paulo anasema “NASTAJABU KUWA MNAMWACHA UPESI HIVI YEYE ALIYEWAITA KATIKA NEEMA YA KRISTO NA KUIGEUKIA INJILI YA YA NAMNA NYINGINE”

 54. NAOMBA KUJIBIWA MASWALI HAYA.

  1. MAPEPO NA MAJINI YAPO?
  2. MAPEPO NA MAJINI YANAWEZA MUINGIA MTU?
  3. MAPEPO NA MAJINI YANAFANYAJE KAZI?
  4. ULIMWENGU WA ROHO UPO? NI HALISI?
  5. JE INAWEZEKANA KUMKEMEA PEPO NA AKATII NA KUMTOKA MTU?
  6. UNAWEZAJE KUJUA MTU KAMA ANA MAPEPO?

  ninaomba kupewa msingi wa kimaandiko na si kushambulia tu kama baadhi ya wachangiaji mahiri walivyofanya katika mada hii.
  Ninaomba uvumilivu utumike tafadhali ili tupate kuelimishana.

 55. Asante ndugu Kinyau kwa majibu yako mazuri, hata na mimi nina wadogo zangu wengi waliozaliwa baada yangu kwa kweli wanaonekana wamezeeka sana kuliko mimi japokuwa nimewapita miaka mingi sana.

  Nilichotaka kusema juu ya mambo ya udongo ni kuwa maandiko yananena waziwazi kuwa “…ujana wako utarejezwa…” Mtoto mchanga atakufa mwenye umri wa miaka 100 na umri wa watu wa Mungu utakuwa “kama vile miti iishivyo”-…&Isaya 65. So sioni logic ya mtu kuzeeka kabla ya wakati wake wa kuzeeka; I mean something must be wrong. Yesu alijua haya kuwa mazingira yatakuwa magumu, vyakula vitakuwa vimechakachuliwa etc; akasema “…HATA WAKILA KITU CHA KUFISHA…”.

  Nguvu yoyote ya uharibifu ni nguvu ya giza hivyo kama inaharibu umri/afya, ndoa, mahusiano etc; IKILETWA KWENYE NURU YA KRISTO lazima giza likimbie. Kwa kukubaliana na mambo mengi kuwa ni kawaida ya sayansi, binadamu, mazingira, tamaduni, mila etc, imefanya uharibifu mwingi wa adui kutawala.

 56. Ndugu Iqualiptus,

  Ni kweli kwamba hakuna maandiko au andiko linalosema wazi wazi kwamba kuna watu wengine wameumbwa kwa udongo wa mbunga na wengine wa mfinyanzi. Lakini kwenye comment yangu kitu ambacho nilitaka tukielewe ni miili yetu kuumbwa kwa udongo kama ambavyo biblia inaeleza kwenye Mwanzo 2:7, 3:19, Zaburi 103:14; Muhubiri 3:20 n.k. Hapa key word ni udongo au mavumbi, kwa hiyo ‘mfinyanzi’ au ‘mbuga’ ni visifa tu, si key words.

  Na nilichotaka watu wakijue ni kwamba haiwezekani watu wenye umri mmoja wakazeeka wote kwa kiwango sawa, na inapoonekana mmoja amezeeka zaidi ya mwingine au wengine isichukuliwe kwamba yeye ana majini au mapepo. Hicho ndicho nilichotaka watu wakione. Kwa mfano, mimi nina mdogo wangu ambaye alizaliwa tayari mimi nasoma shule ya msingi darasa la tatu au la nne, lakini mara nyingi watu huniambia huyo ni kaka yangu kwa maana kwamba anaonekana kuzeeka kuliko mimi.

  Na nina uhakika hana mapepo wala majini. Kwa hiyo to generalise kwamba mtu anayezeeka kuliko umri wake halisi mtu huyo ana majini, hayo sio mafundisho sahihi kibiblia, ndio sababu nikasema inategemea chakula anachokula, kiwango cha mazoezi anayofanya, nature ya kazi zake za kila siku, n.k.

  Ubarikiwe sana.

 57. Shalom!

  Ndugu Orbi, Kinyau,Sally na wengine, nafurahi sana kuona michango yenu mizuri yenye kutufanya tuendelee kujifunza na kujengana.

  Naomba nianze kwa kuwauliza maswali kama ifuatavyo;-
  *Je ni mahali gani ndugu aliyetuma mafundisho hayo (Marandu) amesema huo ni ufunuo mpya?

  * Je hoja ya ndugu Kinyau kama ninavyomnukuu hapa “….Miili hii ni mavumbi(udongo), kila mtu ana udongo wake, wengine wana udongo wa mfinyanzi na wengine wana udongo wa mbuga n.k. Sasa huwezi kusema kuwa wote mliozaliwa wakati mmoja mtazeeka wote kwa wakati mmoja, kwa kweli hili linategemea lishe na kazi mzifanyazo, it is purely scientific and not spiritual.” INATOKA KWENYE MAANDIKO GANI? Mimi sijawahi kusoma maandiko yanayosema wengine tumeumbwa kwa udongo mfinyanzi, na wengine wameumbwa kwa udongo wa Mbuga, labda mnisaidie hayo maandiko.

  * Hoja nyingine ya ndugu Sally “….ni magonjwa ambayo yana tiba hospitalini, hebu washauri watu wawaone wataalam wa afya na sio kuwadanganya katika jina la Yesu. Kuchoka ndoa ni jambo la kawaida kibinadamu, na sio pepo. kinachohitajika ni wanandoa kulitambua hilo, na kutafuta namna ya kuboresha mahusiano yao kama vile kwenda safari kwa mapumziko, kuonana na watu wanaoweza kuwashauri kuvumiliana mfano wazee, au wataalamu wa sekta hiyo.” JE NI MAGONJWA GANI YASIYO YA KAWAIDA? YATAJE. PIA JE NI MAGONJWA GANI YESU ANANATAKIWA KUPONYA NA NI YAPI HATAKIWI? UNA UHAKIKA KUCHOKA NDOA NI JAMBO LA KAWAIDA? YESU KIKOMO CHAKE CHA KUPONYA AINA ZA MAGONJWA NA MATATIZO KIKO WAPI?. Ni nini msingi wa kimaandiko wa ushauri wako huu “..kuwadanganya watu katika jina la Yesu…(ILI KUWAOMBEA)”?

  Baada ya maswali hayo ambayo nataraji kupata majibu yake hapa kwenye thread hii toka kwenu na wachangiaji wengine, ninaomba niseme kuwa “hakuna jambo lisilo la kawaida linalomtokea mtu kwa utaratibu wa kawaida”. Kama sivyo Yesu asingekemea tufani “ambayo ni kawaida kwayo kutokea baharini” halafu imtii, labda angehitaji tu kujua wataalamu wa hali ya hewa wanasemaje kuhusu hali ya bahari kwa siku hiyo na kuahirisha safari.

  Ni usiku wa kuamkia jana tu Tanzania imekumbwa na janga kubwa la pili la ajali ya meli huko Zanzibar, wengi wanaweza kusema ni “la kawaida ya binadamu na vyombo watumiavyo” lakini nataka kusema kitu hapa; Kama kila jambo au mambo mengi ni ya kawaida “HATUNA HAJA YA KUOMBA LOLOTE KWA MUNGU” kwakuwa yeye anayajua mahitaji yetu yoote hata yale tusiyoyajua na neno linasema “anafanya mambo makubwa/makuu kuliko yale tuombayo na tuwazayo…” LAKINI Yesu alisema “OMBENI MSIINGIE MAJARIBUNI”, HIVYO KWA MAOMBI MTU HUOKOLEWA KUINGIA MAJARIBU NA HUWEZA KUMTOA MTU HUKO.

  Mbarikiwe!

 58. Bwana Asifiwe wapendwa,
  Roho mtakatifu azidi kutuongoza katika kusoma na kulielewa neno linaimanisha nini au linatuonya ili utache nini na tutende nini.
  Nionavyo mimi ni watu tujifunze jinsi ya kuutunza utakatifu tulionao na neema tulioipata bure ya kusamehewa dhambi zetu. Maana kuna tofauti kati ya Shetani na mapepo au majini.
  Shetani anazunguka ili apate mtu wa kummeza ambaye atamuangusha katika dhambi au jaribu na katikati ya jaribu ilo Mungu anadhihirisha baada ya kumtegemea yeye na anakupa nguvu ya kulisha na hapo ndipo mtu anaonyesha kukua kwa imani yake.
  Lakini tukirudi kwenye mpendwa ambaye umeokoka sawa sawa hauwezi ukakumbwa na majini pamoja na mapepo. Kutokana na mtazamo wangu. Maana majaribu ni kipimo halisi cha imani tuliyonayo kwa Mungu wetu.Mungu azidi kutushindia katika safari yetu ya kiroho.

 59. Wapendwa,

  Nimechoka kabisa baada ya kusoma haya aliyofundisha ndugu Marandu. Hivi ni kweli kwamba mapepo na majini yana nguvu kuliko Yesu wetu? Lakini nikirejea maandiko naona mapepo yalikuwa yanajisalimisha yenyewe kwa Yesu hata kabla hajasema kitu. Hebu wapendwa tusome kwa makini maandiko kama vile Marko 5:1-20 na sehemu zingine. Inakuwaje leo mtu aseme Yesu yupo ndani yake au ni Mungu pamoja nasi (Emanueli), halafu asumbuliwe na mapepo namna hiyo? Kama hilo linatokea lazima ipo shida mahali.

  Yesu alijua kwamba utakuwepo wakati watu watamkiri kwa midomo yao tu na mioyo yao itakuwa mbali naye, na ndio sababu alilionya hili mapema sana. Ndugu yangu Orbi, tuendelee kusimamia maandiko yanasema nini kuliko mafunuo ya watu binafsi. Kwa hilo nakupongeza sana.

  Lakini kubwa ninalotaka kumuuliza ndugu Marandu ni kwamba haya mafundisho au hizo dalili zinaonekana kwa mtu aliyeokoka kweli? Je mapepo yanaweza kumuoa hata mtu aliyeokoka kweli? Yanaweza kukaa ndani ya mtu aliyeokoka?

  Jamani, lazima tuwe macho na mafundisho kama haya! Hivi kweli mtu kuonekana amezeeka kuliko umri wake ni kuwa na mapepo? Kuna jamaa zangu wengi sana niliomaliza nao darasa la saba mwanzoni mwa miaka ya sabini, nikikutana nao leo mimi naonekana ni mtoto wao, sasa hapo kuna mapepo kweli? Miili hii ni mavumbi(udongo), kila mtu ana udongo wake, wengine wana udongo wa mfinyanzi na wengine wana udongo wa mbuga n.k. Sasa huwezi kusema kuwa wote mliozaliwa wakati mmoja mtazeeka wote kwa wakati mmoja, kwa kweli hili linategemea lishe na kazi mzifanyazo, it is purely scientific and not spiritual.

  Mungu aturehemu.

 60. ndugu, mengi uliyoyaeleza ni magonjwa ambayo yana tiba hospitalini, hebu washauri watu wawaone wataalam wa afya na sio kuwadanganya katika jina la Yesu. Kuchoka ndoa ni jambo la kawaida kibinadamu, na sio pepo. kinachohitajika ni wanandoa kulitambua hilo, na kutafuta namna ya kuboresha mahusiano yao kama vile kwenda safari kwa mapumziko, kuonana na watu wanaoweza kuwashauri kuvumiliana mfano wazee, au wataalamu wa sekta hiyo.
  jipange upya!

 61. Naogopa sana kuhusu mafundisho ambayo yanatapakaa katika mimbari mbali mbali leo…..huwezi kusema ni mafunuo mapya….maana hakuna ufunuo mwingine nje ya maneno ya Mungu au kile ambacho kilifundishwa na Yesu na Mitume wake……hata kama Yesu alisema tutafanya mengi kuliko aliyoyafanya…..lakini hakuwa na maana na kile ambacho hakiko katika wigo wa Maandiko…….

  Biblia katika kitabu cha wakolosai…..inasema “NAYE ALITUOKOA KATIKA NGUVU ZA GIZA NA AKATUHAMISHA NA KUTUINGIZA KATIKA UFALME WA MWANA WA PENDO LAKE.

  Na Paulo katika nyaraka zake nyingi ametueleza sisi ni nani katika Kristo…….na Kusema “SISI NI HEKALU LA MUNGU ALIYE HAI”

  Mafundisho kama haya ya majini mahaba ndani ya muumini ambayo yametapakaa leo yana maana moja tu! Kwamba Wokovu uloopokelewa na waumini si wokovu! Kuingia kwa Yesu maishani mwetu hakujaleta mabadiliko yoyote yale! Inabidi tena Yesu afanye kazi nyingine upya “kazi ya deliverance” kwani “Deliverance” aliyoifanya alipotuokoa Haikukamilika!

  Na haya mafundisho ya tafsri ya ndoto yamejengeka mahali gani katika maandiko?

  Waaumini hebu tuwa macho na Injili nyingine inayokuja kwa mfano wa Nuru lakini imetoka katika mashimo ya kuzimu…….nimeona ndoa za wakristo zikivunjika kwa madai tu mmoja wa wanandoa anatuhumiwa ana jini mahaba…….Nimeona familia za Kikristo wakishutumiana Uchawi…….na kuishia kuvunja mahusiano na kuwa ushuhuda mbaya kwa jamii inayowazunguka…….Nimeona wakristo wakiogopa kulogwa……….na wengine wakidai wameibiwa nyota zao za “bahati”…..na mambo kadha wa kadhaa…..!

  Jamani wapendwa wa Bwana hebu turudi kwenye maandiko ili tutambue sisi ni nani katika Kristo……kwani tukijitambua sisi ni nani katika Bwana Mafundisho haya hayana nafasi kabisa………! Ama sivyo tusije chelea kuambiwa na Paulo…….Ni nani aliyewaloga!

  Mbarikiwe!

 62. Bwana asifiwe ndugu katika Yesu na shukuru sana na tena sana kusoma maneno ya mapepo enye inasubuwa mandoa mingi . moja yao ni mimi tayari atuko pamoja na bibi yangu juu ya mapepo yote enye unataja ata mimi nalienda inche ya ndoa na niko na PETE ya ndoa kukidole yangu ilikuwa mufukoni ikatoka na kupoteya hadi leo na zile mapepo ya kono ya usiku inapita karibu wiki mbili katika ndoto niko na fanya ngono bibi ya rafiki yangu amekufa kitabo.Kwa kweli mimi nimerudiliya Bwana na nimekiri mbele ya bibi na kulomba masamaha

  NB. ndugu MARANDU ule bibi nilikuwa naye inche ya ndoa alininunuliya MAVAZI ya kuvaa sasa nifanye nini juu ya manguo ile ?

  na apa niko ULAYA EUROPE tufanye nini juu ya mambo yote umesema ni juu yangu unaweza kunipa email yako tuwasiliane zaidi kwa maombi juu mambo iyi itoke kwa maisha yangu?

  TAFUTA NJIA YA KUNIFUNGULA NDUGU EMAIL YANGU rova_isa@yahoo.com wandugu munisaidiye

  Monga

 63. Ndugu Marandu,

  Hiki unachokifundisha ni hakiko katika misingi ya Neno la Mungu……huwezi kuja na andiko nje ya context yake halafu ukabubujika mafunuo yako…..! Mafundisho ya namna hii hayatofautishi Ukristo na Uganga wa kienyeji au waganga wa kienyeji ambao tunawakuta Kariakoo ……..! Hebu fundisha Maneno ya Mungu……!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s