Agano la ndoa!!

Bwana Yesu Asifiwe, Napenda kuuliza! Agano la kweli la ndoa ni lipi? Suala la mkataba wa ndoa (kanisani, serikalini nk) na kuvishana pete ni kibiblia? na je? huwezi kumtolea mahari binti na nikamuoaa pasipo kufunga harusi?

“Kwa hiyo mwanamume atamuacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakua mwili mmoja” – Mwanzo 2:24

“Akasema, kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakua mwili mmoja? hata wamekua si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” – Mathayo 19:5-6

“Kwa sababu hiyo mtu atamuacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao watakua mwili mmoja” – Waefeso 5:31

Advertisements

5 thoughts on “Agano la ndoa!!

 1. Naomba kuuliza kama swali la nyongeza katika mada hii: je dhana ya “ndoa takatifu” maana yake ni nini hasa? Naomba hoja za Kimaandiko. Mniwie radhi kama hii dhana ilipata kuzungumzwa huko nyuma na mimi ninaileta upya.

 2. Asheri nilikuwa na maana kuwa ndoa ni Imani katika mantiki ya kuwa kuaminiana ndio kunaleta ndoa na pia kumuamini mwenzio kuwa ni mtu sahihi, kwahiyo mtu akija na kukuambia huyu ni mwenzi wangu suala hapo ni kumwamini tu la usipomwamini itakuwa shida kimawasiliano hata kiimani (kidini) na kitamaduni.
  Tunamwamini mtu kwa lile alilokiri kwetu

 3. Shalomu,

  Nawapongeza wote waliochangia, wasemema vizuri na kama vijana wakiwa na mtazamo sahihi kuhusu ndoa, itawasaidia kupunguza baadhi ya changamoto wanazokabliana nazo kuhusu kuao na kuolewa.

  Naomba nimuulize ndugu Gbukuku Gwmaka unaposema kuwa ndoa ni imani unamaanisha nini? Nashukuru umesema kama umekosea ukosolewe, lakini ungetupatia angalau maelezo kidogo tungepata faida na kujifunza zaidi.

  Ni kweli kumekuwepo gharama nyingi katika masuala ya sherehe za ndoa, na kama walivyochangia wengine hapo juu, suala hili limekuwa kikwazo kwa baadhi ya wapendwa kutokana na uwezo mdogo kifedha. Aidha, kumekuwepo mashindano ya umaarufu wa sherehe za ndoa (arusi) makanisani kitu ambacho kimesababisha baadhi kuchelewa kufunga ndoa zao na wengine kujikuta wamemtenda Mungu dhambi kwasababu tu ya kutaka umaarufu wa sherehe za ndoa (arusi).

  Kwa mtizamo wangu, nadhani kuna haja kwa viongozi wa makanisa kuwaelimisha wakristo kuhusu gharama za sherehe za ndoa (arusi) ili kuwasaidia wasio na uwezo mkubwa kifedha kufurahia kufunga ndoa kwa gharama ndogo.

  Nadhani umefika wakati makanisa kuwahamasisha waumini kuandaa sherehe za gharama nafuu, lakini kwa wale wenye uwezo wa gharama kubwa, waruhusiwe kuendelea na matumizi kama wanavyoona inafaa, lakini watu wahamasishwe kuwa umaarufu wa sherehe za ndoa (arusi) hauna mchango wowote katika kuboresha ndoa ya wahusika, na kuwa suala la sherehe ya ndoa ni la masaa machache tu, kinachofuata baada ya hapo ni maisha.

  Kwa upande mwingine, nimewaona vijana wengi wakiacha kusimamia hata imani zao ili tu kufanya sherehe za ndoa zionekane kuwa nzuri. Utaona kwenye sherehe ya ndoa (Arusi) ya mtu aliyeookoka kuna pombe, miziki ya kidunia, mavazi yasiyo na maadili ya wokovu n.k. Ukichunguza sana utagundua kuwa mengine ni mashinikizo kutoka kwa ndugu/marafiki waliochangia fedha kwa ajili ya ndoa hiyo na wakati mwingine ni maharusi wenyewe kutafuta Fashion bila kujali masuala ya kiimani na ushuhuda wa Kristo.

  Ushauri wangu ni kuwa mtu anapoandaa sherehe ya ndoa akumbuke kuwa sherehe ya ndoa ni siku moja tu, lakini kinachofuata hapo ni maisha ya ndoa ambayo unamhitaji sana Mungu akuwezeshe.

  Shalomu

 4. Hatua ya kufunga ndoa kwa sasa imeathiriwa na tamaduni mbali mbali za nje na ndani kwa ujumla tunaweza kusema ni mkorogo lakini maana ni ileile kwamba umeachana na wazazi wako na umeambatana na mmoja ambaye unaamini ndiye mwenzi, mkaamua kuishi pamoja. Hii aina ya kuiga imewakwaza wengi sana kufikia katika ndoa takatifu kwani wengi wamekosa mahari ili kutimiza mila. Na wengine wamekwazika kabisa kisa kukosa maelfu kwa ajili ya pete ambayo mila za kigeni. Au kukosa suti shela ambayo kimsingi si alama ya ndoa ila yafuatanayo kutokana na akili yako ilivyoamini.

  Niliwahi kusikia huko nyuma kuwa wakristo hawana ndoa kisheria mpaka zithibitishwe na serikali tofauti na waislamu ambao ndoa zao ni halali, wanaweza kuoa na kutaliki bila uthibitisho wa serikali, kwa hiyo kama wanataka iwe katika sheria ya nchi labda waamue kuisajili RITA.

  Hivyo ndoa yeyote ya mkristo bila kusajiliwa iliamuriwa kuwa ni ya kienyeji hata ukipewa cheti cha sakaramenti ya ndoa kama wafanyavyo wakatoliki inahesabiwa ya kienyeji mpaka isajiliwe serikalini. Hivyo mkristo hata ndoa ikimshinda kama aliisajili ni lazima ikaamuliwe mahakamani si kwingineko wakati ya kiislamu kama ndoa imeshindikana wanapeana talaka na inakubalika labda ukitaka iwe kisheria zaidi ukaisajili talaka yako RITA. Huo ndio udadisi wangu kama kuna mtu mwenye ufahamu katika hili anaweza kuchangia zaidi.

  Kwa hiyo nakubaliana na Joel, katika vipengele vitatu hapo juu yupo sahihi kabisa Kibiblia. Kwa hiyo mbwembe za kisasa hizi za leo zisikusumbue kama mmepatana na mwenzako hata ikawa vizingiti katika kuifikia ndoa takatifu, ili uwe na amani na watu wote IBARIKI hapo kanisani mwako japo hilo nahisi limekaa zaidi kibinaadamu si kimaandiko.

  Ndiyo maana mtu akija na mwanaume au mwanamke hatumdai cheti cha ndoa kama jinsi mtu akija akadai ameokoka huwa hatumuulizi kuwa aliokoka wapi na lini kwani ni imani kama ndoa ilivyo imani pia(Nikosoe kama nimekosea)
  Ukristo ni uhuru katika Yesu kristo na wala si utumwa katika sheria maana mwili huleta sheria bali roho huleta imani katika ushindi na kama ukristo ulivyo imani wala si dini, na maisha yetu katika Kristo ni Imani. Kwani kwa ajili ya mwili Sheria kumi za Mungu zilizaa zaidi ya mia sita ili kukidhi matakwa ya mwili.

  Kwa hiyo dada yangu haya ya ziada yamesababishwa na mwili ndio maana mizigo. Mizigo hii imekua tanzu na imeongezeka mara Kitchen Party mara send off, mara Reception Party na enzi zetu Inner party kwa waliojiona wazungu zaidi, kwa ujumla kipindi cha nyuma upande wa Bwana Arusi na Bibi Arusi tulikuwa tunashiriki katika kuaandaa arusi pamoja na wala haikuwa mzigo kama ilivyo sasa,……! Yote ni kutimiza matakwa ya mwili na kuongeza nira kwa waumini dhaifu wapenda kuwaridhisha binadamu kuliko Mungu aliyewaita.

 5. Kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu, ndoa ili iwe ndoa, inahitaji kuwepo au kutokea kwa mambo matatu yafuatayo:
  1. Mwanamme na mwanamke kuachana na wazazi wao;
  2. Na kuamua kuambatana; na
  3. Kuwa mwili mmoja (kupitia tendo la kujamiiana).

  Jambo la kwanza na la pili yanapatikana katika Mwanzo 2:24, wakati hilo la tatu linaonekana dhahiri katika 1 Wakorintho 6:15-16.

  Hakuna mahali katika Maandiko Matakatifu ambapo pametolewa maelekezo ya jinsi (hatua kwa hatua) ya kuingia katika ndoa. Ila katika Maandiko tunasoma baadhi ya watu jinsi walivyoingia katika ndoa (mfano Isaka alivyomuoa Rebeka, na Boazi alivyoana na Ruthu, pamoja na harusi ya Kana).

  Ila Maandiko yanaonyesha kuwa Mungu anatambua ndoa ambazo watu wamefunga kulingana na utamaduni na taratibu za jamii wanakoishi. Kuvishana pete na kufunga ndoa kanisani ni miongoni mwa taratibu zilizopo katika jamii ya Wakristo katika kizazi chetu. Kama hakuna sababu za msingi, ninafikiri si vibaya kuzifuata almradi hazikupelekei kutenda dhambi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s