“Masanja Mkandamizaji” anaitangaza Injili!

Mchekeshaji maarufu kama Masanja Mkandamizaji, majina halisi Emmanuel Mgaya wa kundi la Ze Komedi Orijino ya TBC 1 inayorusha vichekesho vyao kila alhamis kuanzia saa moja usiku, amempa Yesu maisha yake na tayari muda mrefu ameonekana sehemu mbalimbali akiendeleza kipaji chake huku akihubiri na kuimba nyimbo za Injili na wengi wakimpa Yesu maisha yao.

Hivi karibuni alisikika kwenye kipindi cha redio moja maarufu kinachokuwa hewani kila jumapili kuanzia saa 12.30 alfajiri hadi saa 3.00 kikiongozwa na Mtangazaji, Mchungaji Harris Kapiga, Masanja alisema “Mimi ni mchungaji mtarajiwa lakini huduma yangu ya uchungaji nimeanzia kwenye kundi langu hili la Ze Komedy, kupitia hilo nina washirika wangu ambao natamani wawe kama mimi mchungaji wao wafuate nyayo zangu, naomba maombi ya watumishi wengine wamuombee Joti” alisikika kwa msisitizo!

Kwa sasa, Masanja anaabudu kanisa la EAGT, Mito ya Baraka pia amefanikiwa kutoa nyimbo 10 za Injili na tayari album yake ya HAKUNA JIPYA iko mitaani!

Pichani Juu: Masanja kushoto akiwa na Apostle Ndegi wa Living Water na Emmanuel Myamba, Anayevuma na Filamu ya Temptation inayopatikana sokoni!

Masanja akiwa kwenye moja ya mikutano ya Injili, Hapa ni Nzega Tabora, Mtumishi wa Mungu, Daniel Kulola alipofanya mkutano wa Injili

Akiwa kwenye kwaya yao ya New Jerusalem kutoka Mito ya baraka

Chini ni moja kati ya video iliyosambazwa, ikimuonesha Masanja akihubiri Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo!

—Picha: Masanja Mkandamizaji na Filamu Central

Advertisements

49 thoughts on ““Masanja Mkandamizaji” anaitangaza Injili!

 1. Nahisi wachangiaji wote wako sahihi tu ila hawakujua kuwa BABA MUNGU NA MKOMBOZI WETU KWA MWANAYE YESU KRISTO alimaliza kilakitu kwamba ukishakubali kumfuata utaacha mizigo yako yote. Hiini sidhani kama kuna mtu asiye juwa maana yake. Ndugu wapendwa katika KRISTO Dunia ya sasa hivi neno la MUNGU limebaki kama bihashara ndugu zangu. Ndugu yangu MARTI KILEO. BWANA NA MWOKOZI wetu akujalie , makanisani watu wanao jiita wachungaji na watumishi wanatafuta watu maarufu ili kuwavutia washiriki wengi makanisani ili sadaka iwenyingi . Sasa tunacho paswa kufanya imefika wakati wa kanisa la LAUDEKIA shikilia ulichonacho.

 2. SALAAM,
  Wokovu matendo yako jamaniiiii na lazima uongozwe na roho ,kuacha haraka mambo ya kazi na utani vitaondoka tu taratibu akikazana kumtafuta mungu, jamani kila mmoja wetu hapa nadhani alivyompokea bwana yesu kuna vitu vilikuwa vimeng’ang’ania lakini kwa kuzidi kusimama hata bila ya mchungaji kusema wewe mwenyewe unaamua kuviacha!,
  tuzidi kumwombea mungu ajifunue kwake maana hicho ni chombo ndani ya nyumba ya bwana,

  barikiwa

 3. Nafikiri tunatakiwa kuwa makini tunapojaribu kutumia maandiko, ni vyema mawazo yetu yafiti kwenye maandiko kuliko kutaka maandiko yafiti mawazo yetu. Maneno ya Paulo hayana mahusiano na maisha ya Masanja kwa kuwa Paulo alikuwa akizungumzia watu kama wewe, waliomhubiri Yesu huku wakimfitini Paulo. Maisha ya mtu na Yesu hayapimwi kwa mapokeo ya kidini au dhehebu, nina uhakika kwamba hata wewe kama leo Yesu angekuja na kukuuliza ufafanue mahusiano yako naye, ungeishia kumnukulia Rumi 10:9-10 lakini ukashindwa kuelezea mahusiano. Wokovu siyo ushabiki wa taratibu za kidini, ikiwa ni hivyo Yesu asingetumia muda mwingi kukemea Mafarisayo ambao naona kuwa chanzo cha mawazo yako. MASANJA KAOKOKA,

 4. Ubariwe sana masanja kwa uamuzi wa kumpokea yesu kuwa bwana na mokozi wa maisha yako kwani yeye ni waebrania 4:12

 5. Ohh i forgot to write this
  hakuna aliyenikwaza hata mmmoja sijui kwanini ulifikiri hivyo kaka Kinyau ? kama kuna wengine mlifikiri hivyo Iam sorry mimi sijakasirika wala sijakwanzwa -maana hakuna la kunikwaza !

  nitakwazwaje na maoni ya watu wanajengana kwenda mbiguni ? hiyo itakuwa ni upofu wa kiroho kwangu ikiwa nitafanya hivyo . Ninachojua mimi ni kwamba hii ni blog ambayo ni stricly gpspel which means utakatifu na sio kukwazana . What i believe ni kwamba kila kinachoandikwa na mtu kina maana nzuri tu . In one way or another tunafundishana tunasaidiana na hakuna anayejua kila kiltu bado tunajifunza.
  kwa mtizamo wangu kufikiria wengine wamenikwanza ni kutokutambua maana ya healthy discussion -hapa tunakula mifupa ya kiroho -sio watoto wachanga wa kiroho bali akili zetu zimezoezwa kuchambua mambo magumu kikristo
  .Hatushindani maaana mashindano ni katika tamaa za mwili – hakuna competition kwa watu wa Mungu , kwamba nani ana pointi au nani hana ila woote tunacho kitu cha mgawia mwingine .Tena basi tuko kwenye team moja ya Yesu ili tuweze kufikia utimilifu wa kimo cha Kristo na baadaye tutaridhi uzima . Tunachofanya ni kusismama katika zamu yako na kueleza kile roho anachokuongoza na mafundisho aliyokujalia kujua -kinaweza kisisaidie watu wote lakini kikamsaidia mwingine -nadhani ndio maana ya hii blog -so Kinyau kaka yangu uwe na amani tu hatujazuia kuhukumu lakini tunachosema ni kwamba mshukuru Mungu kwa ndugu yetu kuokoka ,kisha mwombee na halafu mkanye kwa yale unayoyaona hayana faida za kiroho kwake -lakini tusimwite mbwa mwitu . As much as Yesu alisema watakuja Mabwa mwitu wakali kweeli hatuna uhakikaikiwa huyu naye ni mbwa mwitu .ikiwa unao huo uhakika basi kamuonye !

  kama nilivyosema ikiwa kuna kitu uanakiona hakiko sawa kwake -ukiweza nenda kamwonye -na kumwombea Mungu amjalie kujua yale asiyoyajua
  Hebu tumtie moyo Massanja na kumwombea ili kesho na kesho kutwa tuwe naye mbinguni .kanisa liwe la kwanza kumtia moyo – lawama kwamba ni mbwa mwitu tungojee hadi tutakapooona amerarua kondoo . kama amejificha kwenye kichaka cha wakovu mbona hiyo ni simple tu itajulikana? -hebu tujaribu kuwaamini wainjilisti wanaoinuka kwa staili zao kisha tutawaonya tukiona wanaenda kombo -That is Love !!

  Ubarikiwe sana

 6. Asante sana Kaka yangu Kinyau

  nakuomba tu ufanye jambo moja la hekima -ikiwa anayo dhambi yoyote katika commedy zake nenda personally ukamuonye -kama unahakika na dhambi hiyo ukamuonye na kama ni Roho anakuongoza nilazima utampata ndugu yako . pia usisahau kumuombea ili Mungu amfundishe yake asiyoyajua

  pia naomba ujue sikuandika kwa hasira kama unavyodhani -nimeokoka ninayo safari

  ubarikiwe sana

 7. Ndugu Hilly,
  Kwanza nikupe pole kwa kukwazwa na post za watu wengi kwenye mada hii kiasi cha kukupelekea kuandika kwa hasira namna hiyo kwenye post yako ya tar.14 March. Hata kama waliomsema au kumwelekeza Masanja kuachana na comedy baada ya kuukiri wokovu wangekuwa wamekosea sana kufanya hivyo, ni imani yangu kwamba haikukupasa wewe kuandika kwa ukali na hasira ya kiasi hicho. Hapo ndipo nilipothibitisha usemi anaoutumia mara nyingi nabii T.B.Joshua na ndugu yetu Mubelwa kwamba wakati mwingine tunafanya makosa zaidi katika kushughulika au kutatua au kusahihisha makosa ya wengine.

  Angalia jinsi unavyotaka kuhalalisha kiurahisi sana kwamba kwa vile Yesu alisema tu kwamba kila ambaye hayuko kinyume chetu basi huyo ni mwenzetu; lakini ukashindwa kutafakari maswali haya: Je, waweza kutuambia nini pale Yesu aliposema kwamba miongoni mwenu watatokea mbwa mwitu wakali watakaolivuruga kundi? Au unasemaje kuhusu kauli ya Yesu huyo huyo aliposema kwamba watatokea makristo wa uongo nao yamkini watawadanganya/watawapoteza/watawaangusha hata wateule wake? Au unasemaje juu ya kauli ya Yesu aliyowaasa wanafunzi wake wa wakati huo na sisi wa leo kwamba si wote watakaomwita Bwana , Bwana watakaoingia kwenye Ufalme wake? Mifano ipo mingi sana aliyoyasema Yesu kututahadharisha kwamba si kila aliye nasi (upande wetu), tupo pamoja katika safari ya kwenda mbinguni, wengine wamevaa ngozi za kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu wakali.

  Tutawatambua tu kwa matunda yao, na matunda ni nini? Naomba ujibu mwenyewe swali hilo. Kama wewe huwezi kuona matunda ya Masanja kwenye comedy zake, basi una kazi ngumu kupambanua usanii wa sasa ulipo au unaovuma katika maisha yetu ya kila siku ya wale wanaodai wameokoka na kumfuata Yesu wakati kiuhalisia sio kweli. Wapo wengi ambao wanasema hivyo lakini ni mbwa mwitu wakali, wapo wengi wanaosema hivyo kumbe wanafanya hivyo ili iwe kichaka chao cha kuficha mambo yao machafu. Kwa taarifa yako ndugu Hilly, wapo watumishi wakubwa sana na wanaoheshimika mno mbele ya jamii lakini ni miongoni mwa wanaorarua kondoo wa Bwana, kama hujaliona hilo basi ipo kazi kubwa mbele yako. Sasa sembuse………

  Inasikitisha sana watu wa Mungu wa kizazi hiki kwamba kila kitu cha kumsaidia mpendwa fulani katika kumfuata Yesu kwa unyoofu wa moyo, kinaonekana ni kumhukumu, nadhani shetani amefanikiwa sana kwenye eneo hili na mkakati wake wa kuwafanya watu wa Mungu wasionyane na kuelekezana kwenye njia sahihi kwa kutumia neno “usimhukumu mwenzio”. Kwa sababu hiyo watu tumeshupaza shingo zetu kwa kisingizio kwamba tusihukumiane. Ni kweli kwamba biblia inatukataza kuhukumiana, lakini je, inatukataza kuonyana na kuelekezana njia sahihi ya kufuata?

  Ipo kazi kubwa mbele yetu, na Mungu wetu mwenye wingi wa rehema na neema, aturehemu na kutufunika kwa neema yake ili tuweze kufikia ukamilifu wa kuujenga mwili wa Kristo yaani kanisa!

  Ubarikiwe na Bwana.

 8. Msiwe waalimu wengi kwa sababu matapata hukumu iliyokubwa zaidi .Mtu ameokoka jambo ambalo wengi wameshindwa .hata kama hajajua vingine yeye tayari ni mwenzetu ana safari ya kwenda mbiguni na ameanza uinjilisti kutumia umaarufu aliokuwa nao .Sisi tunaanza maneno .Hizo dhambi za Masanja mlizijuaje kama sio nyie ndio huwa mnaangalia pia hizo commedy ? Sasa basi mbona mwamuhukumu yeye kufanya commedy na wakati nyie mnaziangalia ? yesu alisema kwa wanafunzi wake Asiye kinyume chetu yuko upande wetu .watu wa Mungu GROW UP!! kuna mengi ya kujadili tuifane vipi kazi ya Bwana kuliko kumshambulia masanja wakati dunia sasa imebanwa na roho ya ,mpinga Kristo .Laiti ungeliejua ungemshukuru Mungu hata kwa mtu kama huyo kuokoka kisha umuombee na uombe actors wengine waokolewe .Kiroho cha kujiinua bila kupima na kuwa na hekima ni kiroho shalow sana
  Jaribu kumuombea mtu na ukiona kuna dosari kama unweza kumfikia mweleze .
  Hizi commedy na mikanda yoote ya movie manazoangalia je huwa mnatenda dhambi ? So it that is the case mbona mnakuwa mbele kuhukumu ?

 9. Ndugu Beda,

  Nina imani hujaisoma biblia yako vizuri ndio sababu umeweza kuona kwamba uigizaji au vichekesho sio dhambi!! Nakuomba kaisome tena kwa upya biblia yako tena ukiwa umetulia vizuri; lakini kubwa ninalotaka kukuambia ni kwamba utakuwa unafanya makosa makubwa kama utakuwa unaisoma biblia yako kwa kutafuta list ya dhambi zilizoorodheshwa ndani yake; kwa maana hiyo usipoona mahali pameandikwa uigizaji au vichekesho ni dhambi basi wewe unaona kila kinachoigizwa na kuchekesha sio dhambi.

  Labda nikupe mfano mmoja tu wa maigizo kwamba wapo wengi sana huwa wanaigiza filamu za mapenzi, pamoja na kwamba kweli hawafanyi mapenzi halisi, je kwako wewe uliyeokoka na kumpa nafasi Yesu ndani yako kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, hiyo ni dhambi au sio dhambi? Kama nafsi yako inakushuhudia kuwa hiyo ni dhambi, wapi pameandikwa katika biblia? Najua biblia imeliandika jambo hilo kwa namna nyingine kwenye Wimbo Ulio Bora 3:5. Hapa biblia imeliandika jambo hili kwa upana wake kwamba msiyachochee mapenzi, kwa sababu kupitia kuangalia uigizaji wa filamu za mapenzi, vijana au watu wengi huyachohea au huamusha hisia za mapenzi kiasi kwamba wengi huishia kuzini au kufanya uasherati. Hebu soma vizuri kile alichaandika ndg Noel Msanjila hapa tarehe 30/1/2012 kuhusu jambo hili.

  Ndugu Inno,
  Naomba nikuulize swali moja tu, kwa uelewa wako Yesu kufundisha kwa mifano maana yake ni kwamba alikuwa anaigiza? Hivi neno ‘mfano’ na neno ‘uigizaji’ yana maana sawa?

  Mbarikiwe.

 10. Jamani hivi ni wapi imeandikwa ya kuwa uigizaji au vichekesho ni dhambi? Hiyo ni kazi yake ya kuingiza kipato, kama mnataka aache basi mtafutieni kazi mnayo ona inamfaa, kama kuchekesha ni dhambi basi hata mimi siungi mkono, bali kama kuchekesha si dhambi mwacheni masanja wa watu aelimishe jamii kwani hayo ni ya kaisari mpeni na Mungu mpeni pia vyake.

 11. tukumbuke kuwa hata Yesu mwenyewe alifundisha kwa mifano na mataifa wakageuka na kuziacha njia zao mbaya iweje masanja amtangaze kristu aliye hai then yaibuke maswali.Tukumbuke maneno ya wimbo hakuna jipya anaposema WEWE UNAYEFIKIRI TUNAFANYA MZAA NDUGU YANGU HAKUNA MZAA KWENYE KAZI YA MUNGU.cha msingi kama maneno ambayo huwa anatamka yanakuchoma kwa sehemu ni moja ya kukwambia ukweli nakushauri usimdic sana masanja ukiona unazidi kuumia ni vyema ukajirekebisha sababu ukweli siku zote unauma.INNOCENT,DOM

 12. Noel Msanjila, amani iwe kwako!

  Hicho ulichokisema ndicho wengine tunakipigia kelele juu ya wokovu wa Masanja na maigizo yake! Kwa mtu makini huwezi kabisa kufurahia kitendo kama hicho ulichokieleza ndg Msanjila. Kama kweli Masanja ameokoka, ni kitu gani hasa anakifundisha katika kufanya hivyo? Na huyo anayecheka au kufurahishwa na kitendo hicho alichokuwa anakiigiza Masanja, kinamsaidiaje mwongofu kwenye safari ya kwenda mbinguni?

  Ninasema na ninarudia tena kusema wokovu usiombadilisha mtu tabia na mwenendo wake kwenye jamii, huo ni wokovu fake! Haiwezekani biblia iseme mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, yakale yamepita, tazama yote yamekuwa mapya, halafu mtu huyo huyo aendelee na mambo yake ya kale yaliyokuwa yanamtambulisha kutokuokoka kwake, halafu tukisema, watu wengine wapige kelele kwamba tunamhukumu mtu.

  Sikiliza ndugu yangu Beatrice Musa, mtu hahukumiwi na mtu mwingine bali uhukumiwa na maneno na matendo yake mwenyewe. Hebu soma vizuri kitabu cha Ufunuo wa Yohana 14:13, neno linasema hivi;

  “Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema; ‘Andika: Wamebarikiwa wale wafao katika Bwana tangu sasa. Naam’ asema Roho, WATAPUMZIKA KUTOKA KATIKA TAABU ZAO, KWA KUWA MATENDO YAO YATAWAFUATA”

  Sasa ona kuna vitu muhimu sana kwenye mstari huo;
  1. Wanaokufa katika Bwana wana heri yaani wamebarikiwa.
  2. Wanaokufa nje ya Bwana wana ole yaani wamelaaniwa
  3. Matendo ya kila mtu anayekufa anafuatana nayo ili yatumike kama kigezo katika kupata hukumu ya haki.

  Kama wewe ulisema umeokoka halafu unafanya mambo ya mzaha mzaha wa kupapasa mapaja ya mwanaume mwenzio (hata kama ni kwa kuigiza), basi matendo hayo utafuatana nayo utakapofika pale kwenye kiti cha hukumu.
  Pamoja na biblia kusema matendo lakini usisahau kwamba kila neno tulisemalo tutalitolea hesabu yake siku hiyo.

  Kwa hiyo dada Beatrice na wengine mnaosema tunamhukumu Masanja, ukweli ni kwamba hatuna mamlaka ya kumhukumu, isipokuwa tuna mamlaka ya kumwelekeza kwenye njia sahihi ya wongofu na kama ameamua kweli kumpa Yesu maisha yake, basi lazima aishi maisha yanayolingana na toba hiyo. Wokovu si kitu cha kusemwa mdomoni tu, bali wokovu ni jumla ya badiliko la maneno, matendo na tabia kwa ujumla ya huyo anayesema au anayekiri kuokoka. Ndio maana mtume Paulo kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume alisema maneno haya kwa kila anayeamua kutubu na kuokoa kwamba;

  (Matendo 26:19-20) “Hivyo basi, Mfalme Agripa, sikuacha kuyatii yale maono yaliyotoka mbinguni, bali niliyatangaza kwanza kwa wale wa Dameski, kisha Yerusalemu na katika vijiji vyote vya Uyahudi na pia kwa watu mataifa, KWAMBA INAWAPASA KUTUBU NA KUMGEUKIA MUNGU NA KUTHIBITISHA TOBA YAO KWA MATENDO YAO”

  Hebu dada Beatrice, fikiri pamoja na mimi kwamba Mtume Paulo kabla hajawa Paulo tunayemsoma sasa kwenye nyaraka zake, angesimama mbele za watu na kusema amekutana na Bwana Yesu na Bwana Yesu amemuokoa na kumwita kuwa Mtume kwa mataifa, lakini bado akaendelea kulitesa kanisa kama alivyokuwa akifanya wakati akiitwa Sauli, nani angeamini wokovu wake? Nadhani dada Beatrice jibu unalo mwenyewe! Kwa nini sasa isiwe hivyo kwa Masanja? Hivi unataka kuniambia Mungu huyu aliyemuokoa Masanja hana uweza wa kumbadilishia kazi ya kufanya, ni lazima tu afanye kazi ya maigizo tena maigizo ambayo hayampi Mungu utukufu kama alivyoeleza ndugu Noel Msanjila hapo juu?

  Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya Masanja kwamba amemuonyesha kweli yake na kumfungulia mlango wa toba, sasa lililobaki ni kwake (Masanja) kuonyesha matendo yanayolingana na toba hiyo; hapo ndipo penye utamu na ugumu wa wokovu!

  Baraka kwenu nyote!

 13. Kwa kweli kama Masanja anataka kusimama imara ktk wana na asiwe kwazo kwa wengine,inabidi awe makini sana kutokana na fani yake ya uchekeshaji,mfano juzi nilimuona Masanja ktk the org comedy akimpapasa yule mfupi sana alikuwa anampapasa mapajani,kwa kweli haina ushuhuda kwani ni lazima kumpapasa mtu mapaja ndo uchekeshe watu,Masanja uwe makini wokovu siyo dini !watu wanatazamia kujifunza kutoka kwako.

 14. Nyie walokole msiwe kama wapumbavu na wajinga kwakukimbilia kuukumu kitu msichokijua,hamjui kwanini Mungu kamuokoa masanja ktk kazi na eneo alilopo badala ya kumshukuru Mungu na kumuombea kijana wa watu mnamkatisha tamaa kwaivyo ni bora hasiokoke au ni bora aokoke na kuitangaza injili.Inamaana nyie hapo mlipo ni watakatifu sana angalieni Kama nyie mmeshindwa kuubili injili wacheni Mungu ainue watu wakuubili nyie endeleeni kukosoa watu muda unakwenda na hakuna ulichokifanya kama kweli mnaupendo wa kiungu na sio unafki ungepiga magoti uombe kwa ajili yake na wengine maana Mungu hapendezwi na watu wanafki.je mnatofauti gani na watu wa duniani?

 15. Mimi naona hili swala linasumbua katika UELEWA!Masanja hufanya maigizo yenye lengo la kuelimisha na kuijulisha jamii mambo yanayoen
  delea kwa njia ya vichekes
  ho,upande wangu sioni tatizo kwenye maigizo yao,cha msingi tuliookoka tuishi kwa kuyaweka balance mambo ya Kiroho,sababu jamii inayotuzunguka inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo tunatakiwa tuzijue ili tuweze kutoa majibu sahihi yanayotokana na Neno la Kristo lililojaa kwa wingi ndani yetu.Kuoka siyo kuwa siliaz kila wakati hata unakosa mda wa kumtania hata mkeo! TUANGALIE SANA KIROHO KIKIZIDI KAWAIDA YAKE HUWA KINAUNGUZA!!

 16. Ndugu Milinga,
  Awali ya yote nikushukuru sasa kuweka wazi msimamo wako juu ya mizaha kwamba unachukia sana hasa mizaha hiyo inapofanywa na wahubiri au wapendwa wakiwa madhabahuni. Lakini mimi ninataka tu kukushauri uchukie mizaha ya wapendwa hawa hata kama hawako madhabahuni kwa sababu popote anapokuwa amesimama mtu aliyeokoka ni madhabahu ya Bwana, kwa kuwa madhabahu ya kwanza na ya kweli ni kwenye moyo wa mpendwa (kwa lugha rahisi mlokole). Ndio sababu mara mtu asemapo ameokoka, jamii inayomzunguka huanza kumwangalia kwa jicho tofauti sana na yule ambaye hajaokoka na kwa maana hiyo ndio sababu biblia ikamwita mtu wa namna hiyo kuwa ni barua inayosomwa na kila mtu, si barua ya siri bali ni barua ya wazi.

  Kama Masanja ameokoka kweli, basi popote anapokuwa, iwe ni kwenye runinga au kwenye jukwaa lolote, anakuwa kwenye madhabahu ya Bwana au anakuwa kwenye mabaraza ya Bwana, hivyo anatakiwa kuacha mizaha. Unajua wokovu huchora mpaka au mstari unaokutenganisha na mambo ya kidunia, sasa kama hataona hilo au hatapata mafundisho ya kumfanya ajue kuwa wokovu wake umemtenga na mambo mengi sana aliyokuwa anayafanya hapo kabla ya kuokoka, kuukulia wokovu kwake itakuwa ngumu sana. Wokovu ni utakatifu na utakatifu maana yake ni kuwekwa wakfu na kuwekwa wakfu maana yake ni kutengwa kwa kazi maalum ya Mungu. Hilo lazima Masanja alijue kama kweli anataka sasa kumtumikia Mungu katika Roho na kweli.

  Kitu kingine muhimu cha kuzingatia kwenye mjadala huu ni hiki ambacho naona tunakichanganya sana. Aliyeokoka kwenye kundi la orijino Komedi ni Masanja, si kundi zima, kwa maana hiyo anayetakiwa kuacha mambo ya mzaha ni Masanja sio kundi zima kwa sababu yeye sasa amepata neema ya kuzijua siri za ufalme wa Mungu na sasa anajua kuwa kila tendo au neno analolifanya atatakiwa kulitolea hesabu mbela za Mungu.
  Lakini nikaenda mbali zaidi ili kujua nini biblia inataka tujue kuhusu ule mstari wa kwanza wa Zaburi ya Kwanza ilipozungumza habari za mabaraza ya mizaha. Hivyo nikaona ni afadhali tujue nini Kamusi ya Kiswahili Sanifu inaeleza maana ya neno mzaha au mizaha. Nikapata maana zifuatazo;
  Mzaha: Maneno au vitendo vya kumfanyia mtu masihara, goya, utani, dhihaka.
  Masihara: Matendo ayafanyayo mtu kwa ajili ya kumtania mwingine.
  Goya: Maneno au vitu vya kumfanyia mtu utani, mzaha au maringo pasi na faida.
  Sasa kama maana ya mzaha ni matendo au maneno afanyayo mtu kwa ajili ya kumtania mtu mwingine, hebu tujiulize swali moja muhimu kwamba biblia inatuambiaje juu ya kila tufanyalo iwe kwa neno au kwa tendo (hapa naongelea kwa wale tu waliompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao yaani waliookoka). Wakolosai 3:17 inatupa jibu kwamba;
  “Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika Yeye”

  Pia 1 Petro 4:11 (hasa nalenga kipengere cha pili cha mstari huu) kwamba;

  “…….. ili Mungu apate kutukuzwa katika MAMBO YOTE kwa njia ya Yesu Kristo…….”

  Ayubu 31:14 inaonyesha jinsi Ayubu alivyokuwa anaogopa sana kufanya tendo au kusema neno lolote tu bila kufikiria atajibu nini atakapokuwa amesimama mbele za Mungu pale aliposema hivi;

  “Nitafanya nini Mungu atakaponikabili? Nitajibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?”

  Msisitizo wa kutofurahia mizaha na kutoendelea kushikamana na wenye mizaha tunaupata tena kutoka kitabu cha Mithali 1:22 kwamba;

  “Enyi wajinga, matang’ang’ania ujinga wenu hadi lini? Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha na wapumbavu kuchukia maarifa?”

  Nimezipitia kwa umakini mkubwa sababu zako za kutomkataza Masanja kuendelea na mizaha wanayoifanya na kundi lake, sababu ya nne ndio imenifanya nijiulize maswali yafuatayo ambayo kama utanifafanulia, nitaielewa vizuri zaidi.

  i). Nini hasara ya taifa lisilocheka? Jibu li-base kwenye kiroho zaidi.
  ii). Nini asili ya kucheka? Iwe ni kucheka kutokana na maigizo ya kijamii au ya kidini.
  iii). Je ni kweli kwamba kila achekaye hufarahishwa na hicho kinachomchekesha?
  iv). Je msongo wa uchovu wa kutwa nzima huondolewa na maigizo ya vichekesho tu au niseme vichekesho au maigizo ndio njia kuu ya kuondoa msongo wa uchovu?
  V). Mwisho, je, pumziko la kweli kwa mtu aliyeokoka hulipata baada ya kuangalia maigizo na vichekesho kama vya akina Masanja Mkandamizaji?

  Maswali hayo yamenifanya nisipate mantiki ya sababu yako hiyo ya nne, na natarajia utanifafanulia zaidi kwenye majibu ya maswali hayo.

  Nakutakia baraka za Bwana.

 17. Habari zenu ndugu zangu,

  Ni vizuri imani ya mtu iendane na matendo, ndivyo Biblia inavyotufundisha. Lakini mtu anapookoka inawezekana isiwe rahisi kwa yeye kujua na kushika yote ambayo Biblia inafundisha wakati huo huo kwani anakuwa bado ni mkristo mchanga, hivyo anatakiwa aendelee kujifunza zaidi na zaidi. Mtu akishampokea Kristo na kuikubali kweli yote, roho wa Mungu hukaa ndani yake na ataendelea kumfundisha taratibu na hatimaye huyo mtu moyo wake utaanza kumshuhudia kuwa matendo fulani kwanza hayampi yeye amani ya kiroho na hayampendezi Mungu. Vitu vingine ni “debatable” lakini kipimo kizuri ambacho mtu aliyeokoka anaweza kukitumia kuona kama matendo yake yanampendeza Mungu, kwanza ni Neno la Mungu, halafu pili, ni amani ya Moyo wake – yaani anachofanya moyo wake unajisikia amani na furaha vinavyompa Mungu utukufu? Sharti hapa ni kwamba, mtu akitaka kubadilishwa na roho wa Mungu awe tayari kuipokea, kuishika na kuitii kweli yote.

  Kwa mujibu wa mchangiaji mmoja, maombi ni muhimu sana, kama ilivyo Neno (Biblia) – kumbuka Neno la Mungu linatuambia kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa! Kusoma neno la Mungu inahitaji jitihada kama vile mwanafunzi mwenye hekima afanyavyo juhudi katika kusoma somo lolote lile kwa ajili ya mtihani, kwa nia ya kuelewa ili aweze kuwa na majibu sahihi. Mkristo hasomi Biblia ili apate uwezo wa kujenga hoja, kwa ajili ya midahalo, ubishi au aonekane amebobea au kufuzu katika mafundisho ya Biblia, bali ili kuijua kweli itakayomuweka huru na hiyo kweli aweze kuwaambia na wengine pia.

  Kuhusu mizaha ambayo ndio mjadala wake unaendelea hapa, ningependa mjaribu kufikiri kama inawezekana vitu viwili tofauti vinajadiliwa halafu vyote vinalinganishwa kama vile vinafanana, ambavyo ni “mizaha” na “maigizo”. Ili maelewano yawepo ni vizuri pia ikaelezwa kwa kirefu mizaha ni nini kwa mujibu wa Biblia. Kuna mtu ametaja filamu inayoigiza mateso ya Yesu. Katika hiyo filamu naweza kusema kwa uelewa wangu, filamu yenyewe sio mzaha ila ni “igizo” linaloonyesha jinsi Yesu alivyoteswa na kufanyiwa mzaha. Mifano mingine ya filamu zinazoigiza mambo yanayohusiana na ukristo ni jinsi watakatifu watakavyonyakuliwa, jinsi yule mnyama mwenye chapa 666 atakavyofanya kazi yake nk. Ieleweke kwamba maigizo haya sio matukio halisi bali yanatoa dhana inayokaribia na uhalisia kwa mujibu wa watunzi. Maigizo ambayo yapo katika hali ya kuonya, kufundisha, kukemea au kutia moyo halafu yanayotumia lugha na picha zenye staha sidhani kama yana matatizo yoyote.

  Kuhusu mizaha ya akina Masanja kama wengi walivyoita, mfano mimi binafsi huwa sipendezwi pale mwanaume anapovaa/onekana na kuongea kama mwanamke au zinapotumika lugha zisizo na staha au zinazofuatisha na kuchochea maisha ya namna ya dunia hii.

  Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

 18. Shalom!

  in my first comment mwanzoni mwa mada hii, i commented in respect of the attitude of passing judgment about others nikinukuu maneno kutoka Mathayo 7:1-2. in my view kinachoendelea kwenye mjadala huu ni kile ambacho nilikuwa nikikitarajia kutokea wakati nilipokuwa nikiandika comment yangu. kinachojadiliwa sasahivi ni wokovu wa masanja ambao unahukumiwa kwa sababu ya kazi ya maigizo anayoifanya. Mimi nadhani kuna haja ya Kutafsiri vizuri neno “MIZAHA”
  Ikiwa imefika mahali pa Kudhania mpaka filamu kama Passion of Christ kuwa ni mizaha, eti kwa kuwa tu wale waliotengeneza ni watu wa mizaha na walikuwa kibiashara zaidi. then we have a very serious problem. hii ni kazi ambayo kwa kiasi fuklani imechangia kwa kiwango kikubwa kuwaelewesha watu habari za gharama aliyobeba yesu kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu. kama hata hii inahukumiwa kwa madai ya kuwa ni mizaha then nachelea kusema kwamba tunakoenda tunachukua tabia za mafarisayo. Ni kwa sababu ya Mambo kama haya mimi huwa naguswa sana maneno yaliyoandikwa katika maombolezo 3:22 – 33. Nanukuu biblia ya kiingereza (Amplified version)

  “22It is because of the Lord’s mercy and loving-kindness that we are not consumed, because His [tender] compassion fail not. 23They are new every morning; great and abundant is Your stability and faithfulness 24The Lord is my portion or share, says my living being (my inner self); therefore will I hope in Him and wait expectantly for Him. 25The Lord is good to those who wait hopefully and expectantly for Him, to those who seek Him [inquire of and for Him and require Him by right of necessity and on the authority of God’s word]. 26It is good that one should hope in and wait quietly for the salvation (the safety and ease) of the Lord.
  27It is good for a man that he should bear the yoke [of divine disciplinary dealings] in his youth. 28Let him sit alone uncomplaining and keeping silent [in hope], because [God] has laid [the yoke] upon him [for his benefit]. 29Let him put his mouth in the dust [in abject recognition of his unworthiness]–there may yet be hope. 30Let him give his cheek to the One Who smites him [even through His human agents]; let him be filled [full] with [men’s] reproach [in meekness]. 31For the Lord will not cast off forever! 32But though He causes grief, yet will He be moved to compassion according to the multitude of His loving-kindness and tender mercy. 33For He does not willingly and from His heart afflict or grieve the children of men.”

  Mtumishi wa Mungu Jentezen Franklin katika sermon moja inayoitwa “Make room for the mercy seat” amewahi kusema “The closest you can be to God on earth is when you show Mercy to another person”
  Mimi nafikiri huu ni wakati wa kuonesha rehema kwa kiwango cha juu zaidi. Hii habari ya kuhukumu wokovu wa watu kwa sababu ya kazi halali zinazowapatia kipato cha kuendesha maisha yao sidhani kama itatufikisha popote. Tuhubiri injili ya kweli, ndiyo yenye uwezo wa kubadili maisha ya watu na kuleta personal conviction itakayowafanya waishi maisha matakatifu. Yanayoendelea katika mjadala huu yananifanya nizidi kuelewa Mungu ni wa rehema kwa kiasi gani.

  Mbarikiwe.

 19. Ndugu Kinyau,

  Nashukuru kwa majibu yako mazuri. Kusema ukweli katika watu wanaochukia mizaha madhabahuni au popote pale mimi nimo pia. NACHUKIA SANA MIZAHA. Katika mambo ninayoyachukia hata ninapopata nafasi ya kuhubiri au kuongea na watu MIZAHA ni namba moja.

  Ninachopenda kueleweka sawasawa hapa ni kwamba mizaha ifanywayo na watu wa komedi mimi hainikwazi kutokana na sababu zifuatazo:

  1. Masanja Mkandamizaji na wenzake wamejiajiri kufanya kazi za mizaha au vichekesho. Wao kila wafanyalo wanalenga kuelimisha, kuburudisha, kurekebisha jamii, kuonya na kuchekesha kwa pamoja.

  2. Unapowasha TV yako kuwatazama, lengo kuu ni kucheka na kuburudishwa na vichekesho vyao tu. Na unafungulia TV ukijua unachoenda kutazama ni vichekesho. Hii ni tofauti na Mhubiri wa Injili au Mchungaji au mpendwa akitoa mzaha mbele za waumini kama kwamba ni ukweli anaohubiri kumbe uongo. Mfano siku ya wajinga duniani tarehe 01 Aprili kila mwaka. Hii ni siku ya mizaha. Kama kuna mpendwa anajiingiza kudanganya watu kama mizaha ajue anatenda dhambi. Niliwahi kudanganywa siku hiyo na mpendwa mmoja aliponiambia kuwa niwahi kwenye msiba wa mfanyakazi mwenzetu tena ilikuwa siku ya Jumapili, nikaahirisha kwenda kusali ili tukazike mfanyakazi mwenzetu. Nilipouliza wenzangu wengine wakanishangaa. wakanikumbusha kuwa ni siku ya wajinga. Hii niyo mizaha.

  3. Sababu nyingine inayonifanya nisiwe kinyume na kazi za komedi ya akina Masanja ni kwamba ile ni sanaa ya maigizo waifanyayo. Sanaa ya maigizo mimi naichukulia kama taaluma ya kusomea shuleni kama vile udaktari, ualimu, uhandisi, ufundi, ushonaji, udereva, nk. Kazi ya kuigiza ili watu walionuna wacheke wakati huo huo wapate somo na mausia ni taaluma ya kuheshimika kama zilivyo zingine.

  4. Sababu nyingine inayonifanya nisiwahi kumkataza Masanja na wenzake wasiache kazi ile ni kwamba, kama taifa halina wachekeshaji wa kwenye runinga au jukwaani, huenda taifa likawa na watu wasiocheka kabisa. Inafika mahali familia hukaa pamoja na kujaribu kutazama maigizo yachekeshayo ili tu kuondoa msongo wa uchovu na mawazo ya kutwa nzima.

  5. Mizaha wafanyayo akina Masanja ni kweli siyo ya kiroho kama alivyogusia ndugu Kinyau bali ni ya kijamii zaidi. Ni vichekesho vinavyowalenga watu wa kada zote. Kuna kipindi huigiza mahubiri au nyimbo za dini na kwa kweli ujumbe wa Injili umewahi kuwafikia watu wengi wa dini tofauti kupitia maigizo yao ya nyimbo au mahubiri. Kuigiza nyimbo za Injili wakati watazamaji wengi siyo wa dini hiyo nao ni ujasiri.

  Kutokana na sababu hizo zangu binafsi, nasita kuwakataza akina masanja kuachana na maigizo ya ucheshi kwa taifa mapema kwa sababu tu wameokoka. Bado naendelea kujifunza.

  Ubarikiwe zaidi.

 20. Ndugu Milinga,

  Naomba nijibu maswali yako matatu kama ifuatavyo;
  Swali la kwanza linasema hivi;
  “Kuna tofauti gani kati ya maigizo ya filamu ya Yesu na maigizo ya komedy za Masanja na wenzake. Je, Masanja akiigiza kutoka katika maandiko akaigiza kama Yesu utakubaliana naye kwa sababu tu anaigiza kutoka katika maandiko kuhusu kuzaliwa, kuteseka, kufa na kufufuka kwa Yesu?”

  JIBU: Tofauti iliyopo ni kwamba komedi za akina Masanja ni secular comedies, hazihusiani kabisa na mambo ya dini ingawa kuna wakati wanawaiga waimbaji na kuimba nyimbo za dini hasa ya Kikristo, lakini lengo na makusudi ya kundi hili si maigizo ya kidini. Hiyo ndiyo tofauti.

  Sehemu ya pili ya swali lako, siwezi kulijibu kwa sababu Masanja na wenzake hawajawahi kuigiza filamu ya Yesu, hivyo siwezi kuwahukumu kwa kitu cha kufikirika, kitu ambacho hakijafanyika. Mpaka hapo watakapoigiza ndipo nitakuwa kwenye nafasi ya kutolea maelezo. Nasema hivyo kwa sababu wanaweza kuigiza kinyume na maandiko au sawasawa na maandiko yasemavyo, hivyo hili siwezi kulijibu kwa kudhania tu.

  Swali la Pili linasema hivi;
  “Je filamu ya maisha ya Yesu walioigiza unajua kwamba wako kibiashara zaidi kuliko wengi wanavyofikiri? Unajua kwamba hata wokovu hawana wala hawana habari kuhusu Yesu waliyemwigiza? Kama hujui hilo kaulize aliyeigiza filamu ya ‘Passion of Christ”

  JIBU:Ndugu Milinga, wewe ni nani hadi ukaingia kwenye nyoyo za wote walioigiza filamu ya Yesu na kujua kwamba walifanya hivyo kibiashara zaidi kuliko uwakilishaji wa ujumbe waliotaka uwafikie watu wanao na watakao angalia filamu hiyo? Kitu gani kimekupelekea u-conclude kwamba walikuwa au wako kibiashara zaidi kuliko wengi tunavyofikiri? Ndio sababu nilisema itafika mahali tutakuwa tunadhania kuwa kila kitu kipo kibiashara zaidi, kwa mfano, wasambazaji wa maandiko ya Mungu kama Bible Societies of Tanzania na Kenya, tutasema nao wako kibiashara zaidi kwa sababu wanauza biblia na maandiko mengine. Mimi sijaielewa hii dhana yako ya kusema kibiashara zaidi, je ni kwa vile filamu hiyo inauzwa? Je maana ya kutokuwa kibiashara zaidi ni kutolewa bure au ujumbe uliomo ndani yake ni wa kibiashara zaidi?

  Ndugu Milinga umejuaje kwamba walioigiza filamu hiyo hawana hata habari kuhusu Yesu waliyemuigiza! Utafiti huu umeufanya lini na wapi hadi ukafikia kujidhirisha kwamba walioigiza hawajui kabisa habari za Yesu, tena ukafikia conclusion kwamba hawana wokovu? Wokovu una matunda yake, je umewahi kuwaona hawa walioigiza na kuona hawana matunda ya wokovu ili ufikie mahali pa kusema hawana wokovu?

  Swali la Tatu umeuliza hivi;
  “Kinyau unajua kwamba walioigiza filamu ya Yesu nao ni watu wa mizaha na kejeli dhidi ya kazi ya Mungu? Unajua kwamba vile walivyoigiza kifo cha Yesu sio ukweli wenyewe? Unajua kwamba Yesu alisulubiwa akiwa uchi kabisa wa nyama, tofauti na senema ya Yesu tunayoitazamishwa?”

  JIBU:Nimepitia kwa makini sana katika Injili zote yaani Mathayo 27:35, Marko 15:24, Luka 23:34 na Yohana 19:23-24. Sehemu hizi zote ndiko ulikopata msingi wa wewe kusema kwamba Yesu alisulubishwa akiwa uchi wa nyama! Hili nalo naliona kama kusema kile ambacho biblia haijakisema. Kule biblia kusema ‘Walipokwisha kumsulubisha wakagawana mavazi Yake kwa kuyapigia kura….’ haina maana ya mavazi yote au haina maana ya kuachwa uchi wa nyama! Ili kupata mantiki ninayotaka uione hebu tusome Injili ya Yohana 19:23-24, neno linasema hivi;
  “Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo Zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. ILA WALIKUBALIANA WASILICHANE LILE VAZI LAKE kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini. Wakaambiana, ‘Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani alichukue…….” Hapa kuna ‘nguo zake’ na ‘lile vazi lake’ inayotupa maana kwamba Yesu alikuwa na nguo nyingi lakini pia alikuwa na vazi lake lilomtambulisha au lililotambulika kuwa ni vazi la Yesu.

  Ninachotaka ndugu Milinga akielewe ni kwamba biblia haijasema kwamba Yesu aliachwa uchi wa nyama, kama biblia haisemi hivyo kwa nini yeye afikie kusema hivyo? Kuchukua mavazi yake haina maana ya moja kwa moja kwamba alibaki uchi wa nyama, labda kama kuna andiko linalosema hivyo naomba anionyeshe nami nitakubaliana na dhana yake bila ubishi wowote.

  Kwa maana hiyo basi siamini mpaka sasa kama walioigiza filamu ya maisha ya Yesu wameikejeli kazi ya Mungu. Lakini akina Masanja ndio wanakejeli kazi ya Mungu kwa kujigeuza wanawake wanapotaka kuigiza kitu kinachohusu jinsia ya kike wakati Mungu amewaumba wanaume, huo ndio mzaha na kejeli dhidi ya kazi ya Mungu, nami naukataa mzaha huo. Kwa nini ndani ya kundi lao wasiwepo wanawake ili waigize kwenye nafasi hizo? Labda ndg Milinga anifafanulie ana maana gani kusema watu hao ni watu wa mizaha na kejeli dhidi ya kazi ya Mungu lakini akina Masanja sio watu wa kejeli wala mizaha!

  Mwisho ndugu Milinga umeandika hivi;
  “Kiongozi wa Mkutano alikuwa Mchungaji Gecha (watu wa Mwanza wengi watamjua). Mzaha ambao mimi sikuupenda ulihusu mbwembwe alizozitumia wakati akimkaribisha mwimbaji wa nyimbo aliyekuwa amevalia vazi la kimasaai. Aliweka vimaneno vya mizaha au tuiite kejeli aliposema; Huyu mwimbaji ametoka Arusha na ndege leo leo. Watu tuliokuwepo tulidhani ni ukweli kumbe uongo mtupu. Nilipouliza wapendwa waliokuwepo wakaniambia huyu ni mtu wa mwanza tu wala hakutoka Arusha. Nilikwazwa sana na huo mzaha. Kinyau atasema kwamba huyu mchungaji hajaokoka?”

  Ndugu Milinga, huo sio mzaha wala kejeli tu, bali ni UONGO. Biblia iko wazi kabisa juu ya waongo kama hawatatubu nini kitatokea kwao mara waiachapo dunia hii. Mathayo 15:19 inasema; “Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio” Kwa hiyo mchungaji huyo alikuwa anashuhudia uongo juu ya mwimbaji huyo. Ushahidi wa uongo si tu usimame mahakamani na kusema uongo, hata hilo alilolisema mch. huyo ilikuwa ni ushahidi wa uongo.

  Ndugu Milinga nakushukuru kwa kunisaidia kujibu swali uliloniuliza hapo juu kwamba ‘Kinyau atasema kwamba huyu mchungaji hajaokoka?’

  Kwa nini nasema kwamba umenisaidia kulijibu swali hili? Ni kwa sababu kwenye maelezo yako umesema kwamba mchungaji huyo alikukwaza sana kwa mzaha wake huo ambao mimi nimeuita uongo. Kama wewe mwanadamu ulikwazwa na mzaha wa mchungaji huyo, je kwa Mungu ilikuwaje? Sasa unaweza kuona mwenyewe ubaya wa mizaha na kejeli, lakini pia unaweza kuona mwenyewe jinsi gani watu hata wale ambao kwa macho yetu tunawaona kama ni watakatifu kumbe wanafanya dhambi ambazo hata hawajui kuwa wanafanya dhambi maana sidhani kama mchungaji huyo alijua kuwa ametenda dhambi kwa mzaha wake huo na akatubu! Lakini mbaya zaidi alikwaza watu kama akina Milinga na biblia imesema ole wake asababishaye makwazo.

  Lakini kubwa zaidi hata wewe Milinga kama hukuchukua hatua ya kumweleza mchungaji huyo kwamba alichokiongea ni uongo na amekukwaza na asifanye hivyo tena, basi dhambi hiyo ipo juu yako pia, ndivyo maandiko ya Mungu yanavyosema kwamba tukiona mwenzetu anapotea tumrejeshe kwa upole huku tukijihadhari sisi pia tusitende dhambi katika kufanya hivyo. Je ulifanya hivyo?

  Mwisho kabisa naomba nimuulize ndugu Milinga, kama ulikwazika kwa ‘uongo’ kejeli na mzaha wa huyo Mchungaji, kwa nini basi hukwaziki na mizaha ya Masanja hasa baada ya kukiri hadharani kwamba ameokoka? Nini kilikufanya ukwazike na mzaha wa mch. halafu mzaha wa Masanja haukukwazi?
  Je mizaha ya wahubiri wanaosema wameokoka inapokuwa mingi au michache kwenye mikutano ya walokole inaondoa ubaya wa mizaha? Na kwa vile wewe mwenyewe umekiri kuwa mizaha ni gonjwa kubwa kanisani, je tuendelee kuliacha tu gonjwa hilo likiendelea kuwatafuna watu wa Mungu?

  Ubarikiwe sana.

 21. Wapendwa Baraka za Bwana ziwe kwenu?

  Nasikitika kwamba ninatofautiana na Ndg Kinyau Haggai kuhusu maoni yake aliyotoa kuhusu mada hii ya kejeli na mizaha. Kinyau anaonekana kukubaliana na filamu ya Yesu ila hakubaliani na magizo ya Masanja Mkandamizaji.

  Kinyau anasema hivi, “Kuhusu swala la picha au maigizo ya maisha ya Yesu hadi kufa na kufufuka kwake kuyaweka kwenye ngazi sawa na maigizo yanayofanywa na akina ‘Masanja’, nafikiri hilo sio sawa. Kinachoigizwa kwenye picha ya Yesu ni maandiko yaliyoko kwenye biblia ambayo hutoa ujumbe ule ule ambao mtu anausoma kwenye biblia”

  Kinyau ningependa ajibu maswali haya ili kuweka sawa mada hii;

  1. Kuna tofauti gani kati ya maagizo ya filamu ya Yesu na maagizo ya Komedi za Masanja na wenzake. Je, Masanja akiigiza kutoka katika maandiko akaigiza kama Yesu utakubaliana naye kwa sababu tu anaigiza kutoka katika maandiko kuhusu kuzaliwa, kuteseka, kufa na kufufuja kwa Yesu?

  2. Je, Filamu ya maisha ya Yesu walioigiza unajua kwamba wako kibiashara zaidi kuliko wengi wanavyofikiri? Unajua kwamba hata wokovu hawana wala hawana habari kuhusu Yesu waliyemwigiza? Kama hujui hilo kaulize aliyeigiza filamu ya “Passion of Christ”.

  3. Kinyau unajua kwamba walioigiza filamu ya Yesu nao ni watu wa mizaha na kejeli dhidi ya kazi ya Mungu? Unajua kwamba vile walivyoigiza kifo cha Yesu siyo ukweli wenyewe? Unajua kwamba Yesu alisulubiwa akiwa uchi kabisa wa nyama, tofauti na senema ya Yesu tunayoitazamishwa?

  Watu wote wanaodhani kwamba filamu ya Yesu ni sawa kuishabikia na kwamba haina matatizo kwa sababu inatoa ujumbe wa maandiko naomba wajiulize maswali hayo na wato majibu kwanza kabla ya kugeukia vichekesho vya Orijino Komedi na kumtaka “Masanja Mkandamizaji’ aachane navyo.

  Kuhusu hoja Kinyau aliyoitoa akiuliza nanukuu, “Una uhakika gani kwamba wakristo wa leo wanaoangalia komedy au picha za Ki-Nigeria n.k wote wameokoka?”

  Hapa Bwana Kinyau inaonekana kwamba anayo darubini ya kuweza kuwajua waliookoka. Sijui yeye anatumia kipimo gani kuwajua waliookoka zaidi ya mtu kukiri kwa kinywa chake na matunda ya nje ya ukiri huo. Mimi hili nahitaji msaada zaidi toka kwa Kinyau. Unawajuaje waliookoka?

  Mwisho napenda kuwapa kisa kimoja cha Mizaha ambayo nimewahi kuishuhudia madhabahuni wakati wa Mkutano Mkubwa wa EAGT Mwanza wakati Askofu Kulola akihubiri pale uwanja wa Furahisha mwaka 2008.

  Kiongozi wa Mkutano alikuwa Mchungaji Gecha (watu wa Mwanza wengi watamjua). Mzaha ambao mimi sikuupenda ulihusu mbwembwe alizozitumia wakati akimkaribisha mwimbaji wa nyimbo aliyekuwa amevalia vazi la kimasaai. Aliweka vimaneno vya mizaha au tuiite kejeli aliposema; Huyu mwimbaji ametoka Arusha na ndege leo leo. Watu tuliokuwepo tulidhani ni ukweli kumbe uongo mtupu. Nilipouliza wapendwa waliokuwepo wakaniambia huyu ni mtu wa mwanza tu wala hakutoka Arusha. Nilikwazwa sana na huo mzaha. Kinyau atasema kwamba huyu mchungaji hajaokoka?

  Kama unataka kuelewa kwamba mizaha ni gonjwa kubwa kanisani, nenda uhudhulie mikutano ya Injili ya walokole. Kama umewahi kuhudhuria mikutano ya Mtume Dustan Maboya ukakosa mzaha hata mmoja basi ujue mhubiri huyu kabadili uelekeo. Mifano ya wahubiri wanaosema wanahubiri wokovu na huku wana mizaha sawa na ile ya Masanja Mkandamizaji ni mingi. Kwa leo naishia hapa.

  Nategemea kupata majibu yangu toka kwa Kinyau na wasomaji wengine pia.

 22. Ashukuruwe Mungu wetu mwenye kuchukuliana nasisi katika upumbavu huu!!!,

  Si komedy tu yapo mengi, japokuwa komedy inaonekana kwa wengi, pia tukumbuke hii ni ajira kama ajira nyingine, ni kazi za mikono yake mwenyewe, na yale wayafanyayo au wanayoigiza ni mambo ya mitaani kwetu tunakoishi mimi na wewe ni KWELI, mara nyingine wametumika kama elimisha jamii kurekebisha mitindo ya kuishi kwa wanadamu.

  lakini tumeshazoea kujaji tu ilimradi unadhani kwamba unayeMUNGU zaidi ya mwingine, maana nimeona mtu anakuja kunihubiri niokoke tena wakati namwambia hata mimi nimeokoka, ati kwamba pale niliposio sahihi, sasa sahihi ya kwenye Biblia ni ipi? baadaye huyu huyu unamwona mitaani, au unakuta maisha yake kwa majirani hayana ushuhuda kabisa.

  Nimeshangaa mzee wa kanisa liitwalo la kiroho pasipo kujua mimi nimeokoka ananiomba 10% ili anipe mradi. na baada ya kumwambia nimeokoka ananikwepa na kuninyima tenda.

  NDUGU SIMAMA KWA NAFASI YAKO, katika enzi yetu tungekuwa tunaingia mbinguni kwa sheria kama za Lawi, na Kumbukumbu la Torati, 99% wangebaki,

  Lakini nitende dhambi kwa sababu neema ipo? lahasha, NAPIGA MBIO KUFIKIA USTAHIMILIVU WA UTAKATIFU.

  MBARIKIWE!

 23. YESU ALISEMA HAKUNA ANAYEWEZA KUJA KWANGU KAMA ASIPOVUTWA NA BABA. HIVYO YEYE MUNGU ALIYEMWITA KUTOKA KTK GIZA NA KUJA KWENYE NURU KWA KUPITIA NENO LAKE. HIVYO KWA KUPITIA NENO LAKE ATAZIDI KUMTAKASA KWANI NENO LA MUNGU NI JEPESI KUYATAMBUA MAKUSUDI YA MOYO NA AKUZAYE NI MUNGU KWA ILE MBEGU ILIYOPANDWA. ILA MAHALI ALIPO ANAPATA NENO SAHIHI?.

 24. Ndugu Nathan,

  Una uhakika gani kwamba wakristo wa leo wanaoangalia komedy au picha za Ki-Nigeria n.k wote wameokoka? Si wakristo wote wameokoka, hivyo wasiookoka wana uhuru wao wa kuangalia vipindi hivyo kwa sababu roho zao haziwashitaki kwa hayo wanayoyaangalia kwa kuwa roho zao zimekufa. Kitu kinachozungumzwa juu ya ‘Masanja’ ni kule kuokoka na kuendelea kufanya mambo ya mizaha wakati biblia imeweka wazi kabisa juu ya swala hilo (kama ameokoka kweli Mungu ndiye anayejua). Nadhani mjadala huu ungejikita zaidi kwenye nini biblia inasema juu ya mtu aliyeokoka na bado ni comedian kuliko kusema kuwa mbona wakristo wanaangalia movie za ki-Nigeria na watu hawalalamiki.

  Kuhusu swala la picha au maigizo ya maisha ya Yesu hadi kufa na kufufuka kwake kuyaweka kwenye ngazi sawa na maigizo yanayofanywa na akina ‘Masanja’, nafikiri hilo sio sawa. Kinachoigizwa kwenye picha ya Yesu ni maandiko yaliyoko kwenye biblia ambayo hutoa ujumbe ule ule ambao mtu anausoma kwenye biblia. Ninachokiona hapa ni kwamba itafika mahali watu wataanza sasa hata kuuliza uhalali wa kusoma maandiko kwenye biblia na kuyafananisha na kuigiza.

  Masanja kama ameamua kweli kumfuata Yesu katika maisha yake, basi mambo ya mzaha ambayo yanamfanya akae kwenye mabaraza ya mizaha aachane nayo. Hebu fikiri Masanja ameokoka halafu anaigiza ni mwanamke kahaba, ametinda nyusi na kuvaa gauni au mini-skirt, halafu siku nyingine anasimama na anazisema siri za ufalme wa Mungu, watu watamuelewaje? Kwa kifupi mimi toka kikundi hiki cha akina Masanja kianze kufanya maonyesho yao sibarikiwi nacho na nimekuwa nikiwaeleza watu waziwazi wakiwapo watoto wangu, ndivyo roho na dhamiri vinavyonishuhudia ndani mwangu.

  Baraka kwenu nyote.

 25. Biblia ndiyo ramani yetu ya kutupeleka mbinguni. Yesu alisema tuwafanye mataifa kuwa wanafunzi wake na kuwafundisha kushika yote Yesu aliyoyafundisha..Biblia yote ni kwa ajili yetu tujifunze na kuifanyia kazi. Hatufuati maoni ya watumishi. Tunapaswa kufuata maelezo yote ya Bwana Yesu. Hatuwezi tukasema shika maneno fulani kwenye Bible na mengine uyaache. Hivyo ni kuwadanganya watu. Neno lote la Mungu ndio maelekezo yakutukamisha na kutufikisha mbinguni kwa Baba. Tuwalete mataifa kwa Yesu na kuwafundisha kweli yote.

 26. Mimi nashangaa wakristo wa leo, inawezekanaje kuangalia vichekesho(commedy), Bongo star seach, video za kinigeria, video za wasanii mbalimbali wanaoigiza, na mambo mengine mengi kwenye TV isiwe kesi, lakini Masanja akiwa ameokoka akaendelea kufanya maigizo ni kesi kubwa sana?

 27. Joseph, Thanks for the nice article. Ambacho ningependa kusema ni kwamba. si kila kitu kinapaswa kukemewa na kutoa “OLE” hya ni maneno magumu sana. Mungu nimjuaye mimi ni wa rehema sana. inawezekana kabisa bwana masanja anafanya yale ambayo baadhi wanadhani si halali kwake kama mtu aliyeokoka kuyafanya. lakini ni nani ajuaye kama bwana huyu anajua hivyo? imani chanzo chake ni kusikia, kama hakusikia mafundisho ya kweli yanayokataza maswala yanayohusu kazi yake, sidhani kama anaweza kuacha kwa urahisi. Napenda kuweka angalizo, Nerno linasema Tunatakaswa na roho kwa kuiamini kweli. Mwalimu mwakasege amewahi kusema “Biblia ni kwa ajili ya watu wote, maneno yaliyoko ndano ya biblia sio yote ni ya kwako, ila kila neno lenye pumzi ya Mungu linafaa.” ieleweke kwamba liko neno ambalo masanja amelisikia, likajenga imani yake, akaamua kuokoka. anayeweza kujua ukweli na uhakika wa wokovu wake ni Mungu anayemshuhudia ndani yake kwa roho mtakatifu. Ni roho Mtakatifu ambaye ndiye anayeendelea kumtakasa kwa kadiri anavyosikia neno na kuiamini kweli ya kristo. Yanayoendelea katika maisha yake sasa si yatakayoendelea kesho provided ana nafasi ya kusikia neno la mungu na kuiamini kweli. Suala la kuacha matendo ya awali ni conviction ambayo Mungu humuumbia mtu ndani yake, si suala la kulazimishana tu. kwa maana ikumbukwe kwamba mtu huyu amekuwa akiishi kwa njia hiyo na kujipatia kipato chake halali. si jambo rahisi kuacha. but with aconviction from God, hakika anaweza kuacha. Badala ya kupeana hizi Ole.hebu kila mtu atumie muda wake kunena kweli ya kristo kwa ujasiri, kwa kuwa ndiyo itakayotengeneza mazingira ya kanisa kutakaswa na roho.

  mbarikiwe.

 28. Jamani Zaburi 1 inatukataza kufanya mizaha na kejeli.Tufuate Neno la Mungu. Tusicompromise ati kwa kuwa makanisa yanaruhusu kufanya mizaha! Hakuna kanisa linalompeka mtu mbinguni. Yesu ndiye anayetoa cheti cha kuingia mbinguni kisicho cha kanisa kwa wale waliompenda kwa kulishika Neno lake. Tusipende kuangalia watu wengine wanafanya nini. Tumuangalie na kumfuata Yesu mwenye kuanzisha na kukamilisha imani yetu. MANABII NA MITUME WENGI WA UONGO WAPO DUNIANI LEO WAKIDANGANYA WENGI YAMKINI HATA WATEULE! Wote tunajua kusoma Kiswahili na tunazo Biblia zetu sasa UKIKUBALI KUDANGANYWA ITAKUWA HASARA YAKO MWENYEWE! Tupo wakati wa hatari. Siku hizi ni za lala salama! Mteule UWE MACHO! Soma Neno ,mwombe Msaidizi Roho Mtakatifu akufunulie kweli yote!

 29. Neno linatukataza kufanya mizaha na kejeli. Zaburi ya 1. Haijalishi makanisa leo hii yamecompromise sisi tutaendelea kualimini Neno. Mimi namshukuru sana Mungu maana sisi sote tunajua kusoma Kiswahili na Biblia iko very clear yaani ipo wazi. Kama ukitegemea kuambiwa na watu nini cha kufanya kisha wakakudanganya HUTAMWAMBIA MUNGU ULIDANGANYWA! Wewe soma Neno mwenyewe na lifuate kama lisemavyo MAANA MANABII WENGI NA MITUME WENGI WA UONGO WAPO DUNIANI LEO HII WAKIDANGANYA WENGI HATA YAMKINI WATEULE! Mimi leo hii siamini kila kinachosemwa na waitwao watumishi wa Mungu. Mtumishi akihubiri au kufundisha LAZIMA TUYAPIME MAFUNDISHO YOTE, JE YANAENDANA NA UKWELI WA BIBLE? Kama mafundisho hayo ni kinyume na Bible TWAPASWA KUYAKATAA NA KUTOYAFUATA. Hatuko hapa kufuata makanisa yanasemaje! Tupo hapa kumfuata MCHUNGAJI MKUU WA ROHO ZETU YAANI KRISTO YESU KWA KULISHIKA NENO LAKE -BIBLE! Kwani kuna kanisa lenye uwezo wa kukupa nafasi ya kuishi mbinguni? Mbingu ni ya Yesu na kama twataka kuingia sharti tuyashike maneno yake yote!

 30. Labda kwa kuongezea aliyosema ndugu Milinga niseme kwamba wapo watu waliookoka ambao kazi yao ni kuburudisha wengine kwa njia ya vichekesho yaani Christian comedians ambao nimewaona TBN nao ni maarufu kwa kazi hiyo. Japo vichekesho vyao havina lugha mbaya lakini nami huwa najiuliza je ni sawa kwa mujibu wa neno la Mungu?

 31. Wapendwa nimefurahia kuona baadhi ya watu wakichangia na kukemea mambo yafanywayo na ndugu yetu Emanuel Mgaya wa Orijino Komedi au OK kama anavyoiita yeye mwenyewe.

  Baadhi ya watu wameonekana kumtaka au kumpa ushauri aache kazi yake ya Mizaha na Kejeli azifanyazo katika kipindi chake cha TBC1 kila siku ya Alhamisi saa moja jioni.

  Wakati nikichangia katika mjadala wa kumpongeza Ndg yetu Joseph Msami na Adela, nilitoa mifano ya dhambi ambazo wapendwa wengi pamoja na kutangaza kuokoka huonekana wakizifanya ama hadharani au sirini.

  Wapendwa wengi waliochangia hawakukubaliana na mimi wala maoni yangu kwa hoja nyingi walizotoa kwa kutumia ushahidi wa maandiko.

  Katika hili la masanja mkandamizaji (Emanuel Mgaya) wanasemaje?

  Mimi nimesema kwamba mtu aweza kuokoka akashindwa kuachana na baadhi ya vitu alivyokuwa akitenda kabla na kwa kadri anavyoendelea kupata mafundisho yaliyo hai na yanayochambuliwa kwa kina na kwa mantiki (logical analysed biblical teachings) mtu huyo hubadilika siku kwa siku. Ni kweli kwamba anatakiwa kuacha dhambi zote anapookoka, lakini huenda baadhi ya mambo anaweza asiyaache kwa ghafla mara tu anapokiri kumpokea Yesu mbele za watu.

  Kwa mfano fani ya maigizo ya kuchekesha, filamu za runinga au jukwaani, watu wengi waliookoka wanazifanya sana. Tena wengi huzifanya makanisani siku za mikesha ya Krismas, Mwaka Mpya, Pasaka, n.k. Vichekesho hivyo vinavyofanyika nyakati hizo tena makanisani havina tofauti na yale ayafanyayo Masanja Mkandamizaji.

  Kama wapendwa wanataka Masanja aachane na fani ya maigizo ya kuchekesha watazamaji wake, wasimtazame yeye tu na kumkataza yeye peke yake bali pia makanisa yaachane na au yakemee waumini wao kujiepusha na kutazama filamu ya Yesu na Filamu yoyote ile iwe ya vichekesho au ya maigizo ya kawaida. Kwa sababu waliocheza filamu ya Yesu ambayo imejizolea umaarufu duniani, hawana tofauti na kile afanyacho masanja mkandamizaji. Wanaomtaka aachane na fani hiyo wanapaswa kutoa maoni yao pia kuhusu filamu ya Yesu.

  Aidha, tunapaswa kuelewana vyema, je kushiriki maigizo ya jukwaani au kanisani, au kwenye runinga iwe vichekesho au tamthiliya, maigizo, nk ni dhambi? Huenda kila mmoja ana mtazamo wake.

  Mchungaji Kakobe wa kanisa la FGBF nimewahi kumsikia akikemea waumini wake kwa nguvu zake zote wajiepushe na kutazama maigizo yoyote yale ikiwemo filamu ya Yesu, Wachungaji wengine sijawahi kuwasikia misimamo yao, ingawa nimeshashuhudia maigizo mengi sana makanisani yachekeshayo na yaburudishayo waumini wasipate kuchoka haraka hasa kwenye mikesha.

  Wanaopinga vichekesho na filamu wanafanya hivyo kwa kusoma maandiko hasa ya Zaburi 1:1 yasemayo; heri wasiokwenda katika shauri la wasio haki…… wasiokwenda katika baraza la wenye mizaha…..

  Siku hizi kuna kituo cha televisheni ya Kikristo inayorusha filamu mbalimbali za humu ndani na za nje. Je, wao wanatumia maandiko gani kuhalalisha urushaji wa maigizo na filamu?

  Kwa hiyo tunapomshauri ndugu yetu Masanja Mkandamizaji, tunapaswa kuyatazama maeneo yote yahusuyo maigizo na vichekesho makanisani kwanza kabla ya runinga na kabla ya kumwambia Masanja aachane na kazi hiyo ya vichekesho atafute kazi nyingine ingawa wengi hawataji mifano ya kazi awezazo kuzifanya. Tunapaswa pia kumshauri dada yetu Jeniffer Mgendi aachane na kazi yake ya kutoa mikanda ya maagizo na filamu za Yesu zipigwe marufuku kabisaa kama kuigiza ni dhambi????

  Naendelea kufuatilia mjadala huu hadi mwisho. Ubarikiwe.

 32. Question: “What does the Bible mean that we are not to judge others?”

  Answer: This is an issue that has confused many people. On one hand, we are commanded by the Lord Jesus, “Do not judge, or you too will be judged” (Matthew 7:1). On the other hand, the Bible also exhorts us to beware of evildoers and false prophets and to avoid those who practice all kinds of evil. How are we to discern who these people are if we do not make some kind of judgment about them?

  Christians are often accused of “judging” whenever they speak out against a sinful activity. However, that is not the meaning of the Scripture verses that state, “Do not judge.” There is a righteous kind of judgment we are supposed to exercise—with careful discernment (John 7:24). When Jesus told us not to judge (Matthew 7:1), He was telling us not to judge hypocritically. Matthew 7:2-5 declares, “For in the same way you judge others, you will be judged, and with the measure you use, it will be measured to you. Why do you look at the speck of sawdust in your brother’s eye and pay no attention to the plank in your own eye? How can you say to your brother, ‘Let me take the speck out of your eye’ when all the time there is a plank in your own eye? You hypocrite, first take the plank out of your own eye, and then you will see clearly to remove the speck from your brother’s eye.” What Jesus was condemning here was hypocritical, self-righteous judgments of others.

  In Matthew 7:2-5, Jesus warns against judging someone else for his sin when you yourself are sinning even worse. That is the kind of judging Jesus commanded us not to do. If a believer sees another believer sinning, it is his Christian duty to lovingly and respectfully confront the person with his sin (Matthew 18:15-17). This is not judging, but rather pointing out the truth in hope—and with the ultimate goal—of bringing repentance in the other person (James 5:20) and restoration to the fellowship. We are to speak the truth in love (Ephesians 4:15). We are to proclaim what God’s Word says about sin. 2 Timothy 4:2 instructs us, “Preach the Word; be prepared in season and out of season; correct, rebuke and encourage — with great patience and careful instruction.” We are to “judge” sin, but always with the goal of presenting the solution for sin and its consequences—the Lord Jesus Christ (John 14:6).

 33. Na mimi nilikuwa nataka kukumbusha kwasababu ninaona kama ulikuwa umekisahau hiko kipengele cha kuwaombea, ndio maana ulikuwa umebased sana upande mmoja, lakini ukaacha upande mwingine, sasa kwa kuwa umekubaliana nami kwa kile nilichokiandika ambacho ni kwa habari ya kuomba, mimi sikatai na kubaliana na wewe kabisa kwa habari ya kuwaonya kwa neno hai la Mungu, sasa nafikiri unaweza kwenda na vyote kwa wakati mmoja, ukaonya kwa mafundisho vilevile ukaomba. Yote hayo ni mema kabisa

 34. m naungana na ndugu Kilewo katika mchango wake kwa kiasi fulani amegusia mambo muhimu yanayopaswa kuonekana kwa mtu anayejiita mtakatifu. Ni vyema kama mtu anasema amempokea Kristo basi na ajitenge na mizaha isiyo na ulazima, kwa ajili ya sifa kwa Kristo.

 35. Ndugu Lwitiko, kila jambo lina nafasi yake. Maombi yana nafasi yake na Kuwaambia watu Neno la Mungu linawataka waishije na wafanye kazi zipi ni muhimu sana. Tunapaswa kufanya Maombi na kuwaonyesha watu dhambi yao. Ezekiel 3:17-21. Tusijidanganye kwamba ati tunapowaambia watu dhambi zao kwamba tunawahukumu! Huo ni wajibu wetu, tuwaonyeshe Mungu anasema nini juu ya uovu wao ili yamkini wapate kutubu. Hivi muuza pombe akiokoka wewe utaacha kumwambia asiendelee kuuza pombe? Utamuacha aendelee kuuza pombe kisha uendelee kumwombea tu? Hasha, upendo wa kweli utakusukuma kumwombea na kumwonyesha Neno linavyotukataza kuuza au kunywa pombe! Sasa hii kazi ya ndugu Masanja ya kuchekesha watu kwa kejeli na mizaha wewe unaona tukae kimya tusimwambie aachane nayo? Tunapaswa, walezi wake wa kiroho wanapaswa wamwambie aachane na hiyo kazi maana imejaa kejeli na mizaha mingi! Paulo aliwaonea Wagalatia utungu na kuwaombea sambamba na KUWAANDIKIA MAFUNDISHO YA KUWAONGOZA WAISHIJE! Kama utaniambia tuwaombee watu tu bila ya kuwaeleza Neno linataka waishije, sasa kazi ya huduma tano ktk mwili wa Kristo nini? Na kuna haja gani basi ya huduma kama ya mwinjilisti au wamisionary? Tujifungie majumbani mwetu tuombe tu bila ya kutoka na kufumbua vivywa vyetu tuwaonye wenye dhambi kuhusu uovu wao na hukumu za Mungu zitakazokuja juu yao waovu? Je, Yesu hakusema tuwafanye mataifa kuwa wanafunzi na KUWAFUNDISHA KUSHIKA YOTE ALIYOTUAGIZA? Mbona manabii wote na mitume waliwaonya watu na kuwaonyesha ukweli wa Neno? Sisi leo tunajidanganya kuwa tukiwaambia watu uovu wao ati tunawahukumu? Sisi tumeokolewa na kuachwa humu duniani ili tuhukumu uovu wao! Yaani kama wewe umeokoka na unaishi na wenye dhambi, wenye dhambi wanapaswa kusikia hukumu mioyoni mwao wanapokuangalia maisha yako, wajione kuna tofauti kati yao na wewe maana WEWE NI NURU na wao ni giza. Lazima watajisikia hukumu! Sasa mtu akiokoka anapaswa kuombewa na kuonyeshwa Neno lisemavyo. Kama alikuwa akifanya kazi za kejeli na mizaha tumwambie aziache maana Mungu anazo kazi nyingine nyingi za kumpa utukufu!

 36. Maombi yana sehemu yake na kuambiwa ukweli wa Neno la Mungu una sehemu yake.Maombi na Neno vinaenda pamoja.Paulo aliona utungu akawaombea Wagalatia lakini hakuomba tu, ALIWAANDIKIA NA MAFUNDISHO WANAYOPASWA KUFUATA! Tatizo la watumishi wengi leo wanaogopa kuwaeleza watu ukweli ati wakisema tuwe na hekima,hekima ya kutousema ukweli wa Injili? Hivi muuza pombe akiokoka leo, utamuacha aendelee kuuza pombe ? Hutamwambia aiache kazi hiyo ya kumtukuza adui Shetani? Sasa kazi hiyo ya mizaha aifanyayo Masanja nyie mnaogopa kumwambia aachane nayo afanye kazi ambazo hazimpi Shetani utukufu? Tunapaswa tumuambie kama kweli ameamua kuokoka aachane na kazi za mizaha na kejeli. Tusijidanganye kwamba tutaomba tu! Maombi peke yake hayatoshi. Inabidi Tuombe na kusema Neno! Tuwaombee watu na tufungue midomo yetu tuwaambie dhambi yao! Tusipofumbua vivywa vyetu kuwaonya watu tutadaiwa damu zao. Ezekiel 3:17-21

 37. Martin njia nyembamba sio kwa masanja hata kwako pia, tusipokaa katika wokovu na kumshika Yesu sawasawa, Mimi naona ningekuona upo wazi sana kama ungekuwa wa kwanza kumuombea. Tatizo la wakristo waliookoka tulionao leo ni wavivu wa kuomba kwa ajili ya wakristo wengine waliookoka. Yesu aliyempokea Masanja ndio huyu huyu uliyempokea na wewe. hata wewe kusimama katika neema hii, si kwa bidii na nguvu zako, bali umevutwa, ni haki ambayo kila aliyeokoka na kusimama katika neema ya wokovu ameipata pale msalabani, wala sio kwa haki yetu, akili wala ujanja wowote ule.

  Wakristo waliookoka, wanaomba sana kwenye semina na mikutano ya Injili watu waokoke, watu wakishaokoka, maombi huwa hayaendelei tena, kesho au keshokutwa ukimuona yule aliyeokoka amerudi kule alikotoka wataanza kusema, angalia yule hakumaanisha wakati anaokoka, ila ni kweli alimaanisha sana, kwa sababu watu walimwombea sana, na kwa maombi yale MUNGuU akafunua ile neema ya wokuvu iokoayo ambayo kila ayeokoka neema hiyo imefunuliwa juu yake hata akapata wokuvu kwa njia toba na kumpokea yesu ndani ya Moyo wake, ila tatizo baada ya hapo, watu wakaacha kumwombea, kesho yake akirudi nyuma wanaanza kumnyoshea kidole,

  sasa na wewe inabidi uutese mwili wako na nafsi yako, kama Paulo alivyosema katika 1 Kor 9:27 pia na wewe fanya kama paulo alivyofanya katika wagalatia 4: 19 anaposema ” vitoto vyangu ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka kristo aumbike ndani yao,
  Anaona shauku na utungu ndani yake, na hicho kitu kikamsukuma kuwaombea wale wagalatia waliompokea kristo, mpaka kristo aweze kuumbika ndani yao. Je kama una utungu kama wa Paulo kwa vitoto vyake, unaweza ukawa na utungu kwa ajili ya Masanja na kumwombea mpaka kristo aumbike ndani yake badala ya kuanza kumdiscourage mtu ambaye amempokea yesu kama wewe ulivyompokea.

  Watu waliokoka, huo utungu wa kuwaombea watu ambao wameingia katika familia ya kristo kama sisi tulivyokwishaingia, huo utungu upo wapi? nina uhakika kabisa wakristo waliookoka wengi hawafanyi maombi ya namna hii.

 38. Yesu Kristo alishasema njia ya kuingia uzimani ni nyembamba. Hivi tuache kukosoana/kurekebishana tunapokuwa tunafanya dhambi kwa kisingizio kwamba tunahukumu? Sasa tusiposema sasa hivi tutaacha mpaka mtu aende motoni? Kama unampenda mtu utamwonyesha ukweli hata kama ataumia! Paulo alisema, mimi nautesa mwili wangu na kuutumikisha ili nisije wahubiri wengine mimi niwe wakukataliwa! 1 kor 9:27.

 39. Watu wasichukulie kuigiza kwake kama ndio sababu kwamba hana MUNGU.HILO NDIO SHAMBA LAKE, HUO UJASIRI WA KUKEMEA UOVU NA KUTAMKA BAYANA KAUTOA WAPI? Jamani masanja hata akiongea tu anachekesha wewe unataka awe amekunja ndita ndio ionekane ameokoka? au awe ananyenyekea kinafiki huku akiwe sirini ni mchafu, wacha afanye kazi ya BWANA, Mungu anainua hata miti ilete injili kama binadam wanashindwa. na biblia inaposema, wacha yakue magugu na ngano pamoja HUJASOMA HAPO?

 40. Hivi nyie hamjui kuwa sisi tutawahukumu malaika walioasi?
  Hivi mtu akiokoka anaweza kufanya kila kazi? Mtu akiokoka anaweza kuuza pombe bar/kilabuni?
  Mtu akiokoka anaweza kuendelea kufanya kazi zenye mizaha ili mradi tu apate pesa na kuwapa wachungaji sadaka? Zaburi 1 inakataza mteule kuwa mtu wa mizaha na kukaa na wenye mizaha.. Hawa watumishi wanaomlea Masanja wanapaswa wamwambie aachane na kazi yenye mizaha kama kweli wanataka utumishi wake usilaumiwe 2 Kor 6: 3-10.

 41. Nimebahatika kumsikia Masanja LIVE siku ya mkutano wa Moses Kulola Jangwani. Niliona kuna kitu cha kimungu ndani yake, Hata hivyo, Hatuwezi kusema au kuhukumu fulani anafaa kumtumikia Mungu au hafai, Mwenye kuwapa vipawa na Karama ni Mungu mwenyewe, na ndio watasimama kutoa hesabu ya kazi wamefanya hapa duniani, napenda kuwaona vijana kama Masanja wanatumia vipaji vyao kwa kuwaleta watu kwa Yesu. Glory TO God!

 42. Sempoli hajahukumu bali ameonyesha jinsi sisi tunaojita walokole tunahubiri kitu fulani lakini tunaishi kitu kingine. Kama mtu anahubiri Injili basi pia maisha yake yaonyeshe kuwa kama hiyo Injili anayoihubiri!

 43. Mtume Paulo amewahi kuandika katika Wafilipi 1:14-18 nanukuu “Na wengi wa hao ndugu walio katika Bwana, hali wakapata kuthibitika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kunena neno la Mungu pasipo hofu. Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema. Hawa wanamhubiri kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa ili niitetee Injili; bali wengine wanamhubiri Kristo kwa fitina, wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza dhiki za kufungwa kwangu. Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.” Mwisho wa kunukuu
  Mtumishi Sempoli, Ikiwa mtume paulo alifurahia hata watu waliohubiri injili kwa fitina kwa sababu tu “YESU ANAHUBIRIWA,” kuna tatizo gani kwa mtu kuhubiri injili “YA KWELI” kwa kile ulichoita “FASHION”
  Mimi ningekuwa na mashaka kama hujakubaliana na kile alichokuwa akisema, LAKINI KAMA NDANI YAKO UNAONA AMEHUBIRI INJILI YA KWELI, KAZINENA HABARI ZA KWELI ZA YESU. Then mimi ntasema kama mtume paulo alivyosema, iwe ni kwa fashion au kwa namna nyingine yeyote “KRISTO ANAHUBIRIWA”
  Imani chanzo chake ni kusikia, wapo watakaosikia habari za kweli za yesu toka kwa huyo mhubiri anayechukulia ulokole kama fashion wakaamini na zikabadili maisha yao.
  Kwenye comment yako umeonesha 100% tabia ya kuhukumu ambayo hata maandiko yanatukataza. tumeambiwa “Msihukumu msije mkahukumiwa” na “Kipimo upimacho ndicho utakachopimiwa”
  Ninapenda sana maneno haya kutoka Mathayo 7:1-2 yalivyoandikwa karika amplified bible (mathew 7:1-2) “DO NOT judge and criticize and condemn others, so that you may not be judged and criticized and condemned yourselves. For just as you judge and criticize and condemn others, you will be judged and criticized and condemned, and in accordance with the measure you [use to] deal out to others, it will be dealt out again to you.”
  Walokole wengi wamekuwa wepesi sana wa kutoa maneno dhidi ya wahubiri wengine na watu wanaotoa muda wao kuhubiri habari za yesu wakati wao wenyewe hawawezi hata kumshuhudia mtu aliye kaa naye kiti kimoja kwenye daladala. ikumbukwe wajibu wa kuhubiri injili ni wa kila mtu anayemkiri Yesu kuwa bwana na Mwokozi wa Maisha yake. kama hukusimama katika nafasi yako kuhubiri injili si busara kunyosha kidole kuwahukumu na ku kriticise wengine. kila mtu atekeleze wajibu wake kwa Mungu na utume tuliopewa yesu wa kuihibiri injili ulimwenguni mote. Hii itatusaidia kama mwili wa kristo na si kushambuliana.
  Mungu awabariki

 44. Enyi walokole ni nani aliewaloga ninyi hata mkadhani ulokole ni fashion kama fashion za mavazi n.k.Siku hizi utasikia msanii fulani kaokoka,lakini club yumo,msondo ngoma yumo,twanga pepeta yumo,hivi kwa nn mnaleta utani na injili?
  Mtu akishampokea Yesu tunahitaji kuona badiliko halisi,mtu hawezi akasema amempokea Yesu halafu bado yupo pale pale,ni lazima mabadiliko yatokee maana mtu huyo amefanywa kuwa kiumbe kipya,
  Mtu akishafanywa kuwa kiumbe kipya lazima chuki juu ya dhambi ionekane dhahiri,chuki juu ya ulevi,uasherati n.k.Huwezi kusema umeokoka halafu bado unapenda kwenda baa au kwenye kumbi za starehe! huko ni kujidanganya,kwa nini mnawafariji watu hawa halafu siku ifikapo waingie hasara,naam hawataingia peke yao hata ninyi mliowapoteza mtakwenda nao.
  Ndio maana inawalazimu watu kubadilisha hata kazi ili waweze kuenenda sawasawa na mpango wa Injili.Roho Mtakatifu akiwa ndani yako atakuongoza katika kweli yote.Hakuna usanii katika wokovu acheni mchezo,mtu atavuna alichopanda!
  Kwenu wachungaji na wote mnaoitwa watumishi wa Mungu kwa vyeo vyenu,hebu wahubirini watu Injili ya kweli,msitafute kujaza makanisa yenu kupitia wasanii,acheni usanii katika kazi ya Bwana,waambieni watu kweli ili ulokole urudishe heshima yake,ili nguvu ya Mungu irudi katika makanisa,hamuoni shida iliyopo sasa makanisani?kukemea pepo tu kunawachukua watu masaa,ile ni amri,inapotolewa itekelezwe hapo hapo,sasa pepo analeta ukaidi,inabidi ujiulize kuna nn hapo?uliona wapi kuruta akambishia afande?
  MUNGU ATUSAIDIE

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s