Barua ya Wazi kwa TGNP kuhusu ushoga!

YAH: MAONI BINAFSI JUU YA HALI YA USHOGA NA TAMASHA LA JINSIA

Mimi ni miongoni mwa wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu, maliasili na mazingira. Nimekuwa nikipigania haki za kimsingi za kibinadamu kwa nadharia na vitendo. Ushiriki wangu umesaidia kupambana na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa namna moja au nyingine katika nchi yetu na nchi jirani.

Nitumie fursa hii kuipongeza kwa dhati kabisa Tanzania Gender Networking  Program (TGNP) kwa mchango wake wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii ya kitanzania. Mchango wa TGNP ni mkubwa na wanaharakati wa haki za binadamu, rasilimali na Mazingira kwa ujumla wanautambua na kuuthamini.

Baada ya pongezi hizi, napenda kutoa maoni yangu juu ya Tamasha la Jinsia liloandaliwa na TGNP kuanzia tarehe 13-16 katika viwanja vya TGNP.

Ni kweli kuwa kuna mambo mazuri mengi yalifanyika wakati wa Tamasha hili, ikiwemo jamii za pembezoni kutoa na kupaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali nyeti yanayozifanya jamii hizi kukosa au kunyimwa haki zao za  kimsingi za kibinadamu.

Pamoja na hayo mazuri, kwa maoni na mtizamo wangu, mazuri hayo yalifutwa kabisa na msimamo na upigiaji chapuo  wa TGNP kuhusu masuala ya USHOGA katika jamii ya kitanzania. Binafsi sikatai uwepo wa USHOGA/USENGE katika jamii ya kitanzania. Sina mtizamo wa kihafidhina wala wa kuwatenga watu hawa, lahasha. Tatizo langu ni kupigia chapuo kwa TGNP suala hili la USHOGA/USENGE.

Hoja yangu ya kupingana na TGNP kuhusu mtizamo wenu ni jinsi mlivyolichukulia na kulienzi suala hili. Nashindwa kupata dhamira nyingine zaidi ya kuwa TGNP mna malengo kadhaa na suala hili.  Nashawishika kuamini kuwa mnapigania kuleta mabadiliko hasi kwa jamii yetu, yaani jamii ya kitanzania ilione suala hili kuwa la kawaida, hivyo watoto wetu wajihusishe na USHOGA/USENGE.

Pengine, utetezi wenu kuwa mnataka jamii ijue kuwa tatizo hili lipo na ichukue hatua. Lakini hoja hii haina mashiko wala miguu.

Utetezi wenu pia kuwa watu hawa, MASHOGA/WASENGE wameingia katika matendo haya machafu kwa sababu za kiuchumi na kibiojia nayo hayana maantiki hata kidogo.

Je, mbona masikini wa Tanzania wapo wengi tu! Na wao mnataka waingia katika USHOGA/USENGE? Je ukishakuwa SHOGA/MSENGE ndiyo matatizo ya kibiolojia na kiuchumi yanaisha? Nini mnataka watoto wetu wafanye zaidi ya kuona USHOGA ndiyo suluhisho la umasikini?

Je kama watoto wenu wangekuwa mashoga/wasenge mngewaleta kwenye tamasha hili?

Jibu rahisi ni kuwa TGNP mnapata fedha za kuwa na miradi hii toka kwa mashoga/wasenge wa kimataifa wanaotaka kufanya jamii nzima iwe kama wao. Ni tamaa ya fedha tu ndiyo inayowafanya mpigie debe suala la ushoga/ushoga nchini mwetu na si vinginevyo. Kuna tofauti gani kati ya RUSHWA/UFISADI mnaoukataa katika serikali yetu na kutumia fedha chafu za watetea USHOGA/USENGE. Fedha yao ni chafu, hata ikitumika kuutokommeza USHOGA bado itakuwa chafu tu.

Je, unaweza kutumia fedha ya mtetea USHOGA/USENGE kuwafanya mashoga waache tabia hii? Mbona haiwezekani! Lengo ni kuwatetea tu waendelee na tabia hii chafu na si vinginevyo.

Vile vile naona TGNP kupoteza staha na heshima iliyojijengea katika jamii yetu ya Tanzania kwa muda mrefu. TGNP kwa kujiingiza kwenye suala hili ni kupoteza dira na mwelekeo sahihi. Siwahukumu ila ndiyo ukweli mwenyewe. Mnataka tuwe na taifa la aina gani? La mashoga/wasenge? Ukuaji wa taifa utakuwaje ikiwa watu wote watakuwa kama dhamira ya wasenge ilivyo?

Uungwana huanzia nyumbani. Ikiwa matendo na sera zenu zitakosa staha kwa watanzania kazi yenu itakuwa ni mfu na isiyo na tija. Uungwaji mkono wenu wa kwaida utapotea sana.

Nawasihi mtafakari upya mwelekeo wenu ili heshima na staha yenu irudi kwa watanzania. Kuteleza siyo kuanguka, chukueni hatua hamjachelewa. Chukueni maamuzi magumu ya kukataa fedha za watetea USHOGA/USENGE. Zipo nyingi tu na ndizo zilizowaingiza katika mtego huu mchafu.

 Stanslaus Nyembea

Advertisements

8 thoughts on “Barua ya Wazi kwa TGNP kuhusu ushoga!

 1. ANAETEMBEA NA SHOGA NAE NI SHOGA TUSISHANGAE HATA HAO VIONGOZI WA TGNP NI MASHOGA

 2. Kweli nimeamini binaadamu wengine wa sasa wanazidiwa akili na wanyama huwezi kukuta wanyama wa jinsia moja wanafanya upuuzi.

 3. Nimeona habari hii inahusu hapa nikaona niiweke. Katika kifungu cha mwisho Dr. Mvungi ametoa siri kwa nini TGNP walilipigia debe suala la ndoa za jinsi moja ambalo kwa sasa liko moto moto likipingwa na waTz wengi! Soma maneno ya Dr. Mvungi kuhusiana na suala la sharti la ndoa za jinsi moja ndipo Tz ipewe misaada ya Uingereza.

  DK. MVUNGI: TULIKATAA FEDHA ZA UINGEREZA

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, amesema anatamani kufa na kutangulia ahera ili asione Tanzania wakati itakaporuhusu ndoa ya jinsia moja kama inavyoshinikizwa na Uingereza.

  Dk. Mvungia aliyasema hayo jana jijini Dare s Salaam jana wakati akitoa mada kwenye warsha ya kujenga uwezo wa ushiriki katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ambayo iliwashirikisha wanaharakati na waandishi wa habari.

  Alisema ni aibu kubwa kwa Tanzania ikiwa siku moja itaruhusu ndoa ya jinsia moja, na kwamba ikiwa itafanya hivyo, itakuwa inakwenda kinyume na sheria za nchi kwa kuwa tendo la kulawiti ni kosa la jinai.

  Alitaka Watanzania kupinga sula hilo kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha halipati nafasi na kwamba umasikini usiifanye Tanzania ipoteze heshima yake.

  “Naomba Mungu siku ikitokea ushoga ukaruhusiwa mimi niwe nimekufa ili nisione kitakachokuwa kinaendelea,” alisema Dk. Mvungi ambaye pia mwanaharakati

  Alifafanua kuwa Uingereza inataka kuwaona Watanzania na Waafrika kwa ujumla ni wajinga na kuwashinikiza wakubali ndoa za aina hiyo wakati wao suala hilo hawajaliingiza kwenye Katiba yao.

  “Jambo hili likiingizwa kwenye Katiba litapotosha taifa kwa kuwa lilianza kujipenyeza kwenye Kanisa la Anglikana, lakini halikupata nafasi hivyo ni lazima lipingwe,” alisema.

  Dk. Mvungi ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC), alisema kuna wakati Uingereza ilikipatia kituo hicho fedha kwa ajili ya kuhamasisha kutambuliwa kwa ndoa za jinsia moja, lakini walizikataa zikapelekwa kwa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

  ….makubwa!

 4. Hawa ni mafisadi zaidi kuliko hao wala rushwa kwa sababu wanataka kuua asili ya mwanadamu na kizazi chake. Allah aliiangamiza qaumu Liti kwa kosa hilo tu. Na wala si kweli kwamba jamii ya mashoga inahitaji huruma ya jamii na kukubalika kwa namna walivyo kwa sababu si jambo la asili. Hakuna mwanaume anayezaliwa na hamu ya kulawitiwa au kulawiti,isipokuwa ni kujifunza kwenye mazingira ya mtu mmojammoja au yaliyowekwa na jamii ambayo mashoga wanataka kuyaweka.Tukatae ushenzi na laana hii mbona wabakaji na wezi hatuwakubali. Tanzania bila ushoga inawezekana. Abiria chunga mzigo wako.

 5. ok jamani katika hili mimi ningependa kusema tu kuwa dunia hii ni kubwa sana na ina mapana yake na katika hilo haya nayo ni sehemu ya mapana yake. Sishangai kabisa kabisa kuona TGNP wanafanya kazi ya kutetea MASHOGA kwa kuwa naamini kabisa ni kwa maslahi yao wenyewe. kifupi watanzania tuwe macho na tumwombe Mungu atupe upeo wa kuona hata vile vilivyofichwa machoni mwa waovu.

 6. Kaka, i just loved your leter to TNGP, but could be very helpful if you could send it to our local news letter to be published.

  Mashishanga

 7. Muda umeenda sana.
  Naam, tukijua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. WE ARE AT WAR! Fighting for the souls of men. THE HOUR IS LATE! The cry of the Spirit for the Body of Christ is that God will break the hardness of our hearts:
  That we will come before Him in times of prayer and fasting for the sins of our cities and nations.
  That we would cry out…weep and intercede for the lost
  That we will have a broken and contrite spirit, where we will weep and mourn for the sin we have allowed to come in our midst.

  What has happened to the Church when we are satisfied to sit in our churches Sunday after Sunday, while over half of the world’s population (3.5 billion) has never heard the Name of Jesus one time?
  What has happened to the Church when we see the streets of our cities filled with homeless, destitute people who are in spiritual darkness; yet we fail to reach out in love and share the Word of God that will set them free?
  What has happened to the Church when we see people all around us dying without God; yet we let days, weeks and even months go by without crying out to God for their souls?
  What has happened to the Church when we see the darkness of sin spreading all around us and infiltrating the Church;yet we are not grieved enough to weep and mourn before God?

  We shout, “Jesus is coming!”…but, do we really believe He is coming? IF WE WERE TRULY AWARE OF THE LATENESS OF THE HOUR, WE WOULD NOT LOSE EVEN ONE ONE OPPORTUNITY TO WARN THOSE WE SEE.

  IE WE TRULY BELIEVED JESUS IS COMING SOON, MANY OF OUR PRIORITIES WOULD CHANGE. Our major concern would no LONGER BE THE CARES OF THIS LIFE,OUR HOMES, OUR CAREERS,OUR OWN DESIRES AND GOALS; IT WOULD BE PREPARING OURSELVES FOR HIS COMING AND WINNING SOULS INTO THE KINGDOM OF GOD.

  Church, we are asleep, and the Spirit of God is WARNING US TO WAKE UP!
  Jesus said,”If therefore you will not wake up, I will come like a thief,and you will not know at what hour I will come upon you” Rev 3:3
  Unless we shake ourselves out of our sleep, we will be unprepared like the disciples were in the Garden of Gethsemane when Jesus was arrested.
  Let us keep alone with God and keep interceding for the lost.
  Let us see and be concerned with those around us who are lost and dying without God.
  Let us not allow even one day to go by without telling someone about Jesus…without warning them of the judgement that is coming upon the earth.
  We need a vision of hell and all its fiery torment. We need to have a revelation of what it means for a soul to be forever lost in burning hell for eternity without God.

  To meet our objective of evangelizing the world before Jesus comes, the Church must WAKE UP FROM ITS SLEEP AND COME TOGETHER as a unified force with every member possessing a BURNING PASSION EOR THE LOST, AND EVERY MEMBER GIVING THEMSELVES IN 100% Commitment an Dedication.

 8. nafikiri sasa kila mwenye macho na masikio anaamini ule Mwisho wa Dunia ndio huuo umekaribia
  Si jambo la busara wala hekima kwa viumbe vya Mungu Kufikiri Ushoga ni halali, lakini kwa Kuwa wamemuasi Mungu basii hata maarifa yameondoshwa kwao. Nawaonea huruna sana ila Mungu wa mbinguni awape kujua………….
  kwa kanisa la Mungu hii ndilo funzo kwetu kuwa ule mwisho umekaribia, mwenye masikio na asikie

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s