Huduma za Malaika!

Bwana Yesu asifiwe! napenda kujifunza kuhusu huduma za malaika na majina yao, na wanafanyaje kazi? Mungu awabariki!

–David

Advertisements

7 thoughts on “Huduma za Malaika!

 1. Hongera sana kaka David kwa sababu unataka kujifunza jambo jema sana katika maisha yako hasa ukijua malaika ni watenda kazi wetu. Hatujui kuwatumia ndio maana hata wakati mwingine tunakwama katika maisha yetu. Kuna kitabu cha angles ameandika mchungaji wangu ( Pastor Ntepa ) wa Oasis of Healing Ministry (OHM). Kanisa lipo nyuma ya ubungo plaza .

 2. Ndugu David,

  Mimi ninajibu suala lako kutokana na ninavyofahamu Biblia isemavyo juu ya habari ya malaika na utumishi wao. Yawezekana jibu langu likazua swali jingine. Ikitokoea hivyo usisite kuuliza. Lakini pia yawezekana kabisa jibu langu likawa ni mwanzo ili mtu mwingine aendeleze pale nitakapokuwa nimeishia.

  Katika Ebrania 1:14 tunaona kuwa malaika ni roho watumikao, ambao Mungu huwatuma “kuwahudumia” wale watakatifu watakaourithi wokovu. Andiko hili linaweza kuwa msingi wa suala hili la Huduma za Malaika.

  Biblia inaonyesha huduma tofauti tofauti zinazofanywa na malaika. Zifuatazo ni baadhi ya huduma hizo (maana yawezekana kuna zaidi) zifanywazo na malaika:

  1. Kupeleka/Kupasha habari.
  Kuna malaika ambaye ametajwa katika Biblia ambaye ndiye anahusika na kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu:
  -Luka 1:26; “Mwezi wa sita, malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti”
  -Daniel 9:21-22; “..naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabriel, niliyemuona katika njozi hapo kwanza….., alinigusa panapo wakati wa dhabihu, …akaniagiza, akaongea nami akasema…”.
  -Luka 1:19; “Malaika akamjibu akawambia, mimi ni Gabriel, nisimamaye mbele za Mungu, nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.”

  2. Ulinzi/Vita
  Tukisoma Biblia pia tunaona kuwa kuna malaika ambaye ametajwa katika mambo yanayohusiana na vita au ulinzi.
  -Yuda 1:9 “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema Bwana na akukemee”
  -Ufunuo 12:7,” Kulikuwa na vita mbinguni, Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka….”
  -Daniel 10:13; “Lakini mkuu wa ufalme wa uajemi alinipinga siku ishirini na moja, bali tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia….”.
  Neno “wakuu wa mbele” linaamaisha wakuu wa mbele katika vita.

  3.Wokovu kutoka katika hatari, ajali nk.
  Tukisoma katika kitabu cha Mwanzo sura ile ya 19 tunapata habari za Lutu (Lot) na miji ya Sodoma na Gomora. Lutu alipewa habari juu ya kuondoka humo lakini yeye alikuwa mzito sana hadi ikalazimika atolewe kwa nguvu na malaika hao.[Mwanzo 19:16].

  Zipo shuhuda wa watu mbali mbali ambao kutokana na jinsi walivyookoka walijua dhahiri kuwa ilikuwa ni mkono wa Mungu kupitia Malaika. Namfahamu Engineer John Njau, ambaye kati ya shuhuda zake za kusisimua ni ule ambao alikuwa akisafiri usiku na akafika sehemu ambayo alikuta magogo yamewekwa barabarani [kwa ajili ya kuteka magari]. Lakini katika hali yakushangaza gari lake liliinuliwa kuvuka yale magogo na yeye akaendelea na safari! Mambo ya ajabu kabisa.

  Ndugu David, naomba niiishie hapa kwa sasa na nitaendelea kuangalia aina nyingine ya utumishi ambao hufanywa na malaika kwa watu wa Mungu kisha nitaandika hapa. Lakini kama nlivyosema mwanzo kama kuna mtu yeyote mwenye mchango juu ya mada hii anaweza kuchangia tu ili tuendelee kujifunza.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s