Mke kumzidi Umri mumewe

Jamani naomba mnijuze; Kuna ubaya kwa  mwanamke kuolewa na mwanaume mdogo kuliko yeye;  yaani nina maana mwanamke awe mkubwa kwa umri kumzidi mume?

Ni kawaida kwa mume kumzidi mke lakini kwa mke kumzidi mume ndio nauliza kama Biblia inasema kuhusu hili na ni nikifungu gani kinakataza? Naomba mnijuze wapendwa.  Mbarikiwe sana!

Arthur Moore

Advertisements

13 thoughts on “Mke kumzidi Umri mumewe

 1. Bwana yesu asifiwe wapendwa naomba maombi yenu kwani kwa kipindi hiki nahitaji kuoa lakini bado cijaona wa mke anaee nifaa cjui nifanyeje.

 2. mapenzi haya chagui umri wala nini tusidanganyane ukimuacha basi uja penda ulikua una tamani but kamaumependa lazima ukubala umri si kigezo cha kukataa kuolewa

 3. Nawasalimu katika jina la Yesu Kristo.
  Kwanza ni kama bahati kutembelea website/ blog hii.
  nimepata maarifa mengi

 4. Kwa ufupi sana” MUNGU kumuumbia Adam mwanamke baada yake ni ishara tosha kwamba inatubidi kuenenda na taratibu za MUNGU wetu

  Mwanamme anapoitwa Nguzo ya familia inachukuwa maana nyingi sana sambamba na umri
  Huwezi kujengea Nguzo ndogo kama muhimili then ukaweka nguzo kubwa juu yake””

  Xo kwa uelewa wangu kuoa mwanamke aliyemdogo kwako ni matakwa ya MUNGU wetu aliyejuu

  Thnx

 5. Wapendwa mimi nina umri wa miaka 22 ila kuna bint ambaya napenda nimuoe tatizo amenizi miaka5 naombeni ushauli wenu

 6. Ubarikiwe dada kwa kuwa jasiri kiasi cha kuhitaji msaada wa maombbi kwa Bwana.
  Wewe si wakwanza kuchelewa kuolewa wapo na wengine wakubwa zaidi yako wametulia kwa Mungu, mwamini Mungu nawe atakupa haja ya moyo wako nami ntakuombea Mungu akukumbuke katika haja yako.
  Hakuna kitu kibaya kama kukata tamaa naomba usikate tamaa kwani wapendwa wanakuombea halafu wewe unakata tamaa? usijali Mungu ni mwema atakujilia kama alivyomjilia sara na Ibrahimu.

 7. ninaomba munikumbuke katika maombi mwenzenu nimeokoka na ninajitegema pia nina watoto watatu wa kaka yangu wanaonitegemea mimi bado sijaolewa natamani sana kuwa na mwenzi wangu atakaye nijali maishani kwani inafika wakati nakata tamaa kabisa ya kuishi kwani umri wangu naona umeenda sana nina miaka 32

 8. umri sio kigezo kwani nawafahamu watu wa aina hiyo tena wanaishi kwa upendo mkubwa. swala muhimu ni upendo na kuheshimiana, mbarikiwe.

 9. Ndugu yangu Moore na wachangiaji wengine Bwana Yesu asifiwe!
  Naomba nianze kwa kunukuu kitabu cha mith. 19:14 “….mke mwenye BUSARA, mtu hupewa na BWANA”, Mithali 18:22 inasema “apataye mke apata kitu chema; naye ajipatia KIBALI kwa BWANA”
  Hapa bible inazungumza KIBALI kutoka kwa Mungu kupata mke mwenye BUSARA, hajazungumza wazi habari ya umri ila Mungu akikupa KIBALI kuoa mke mwenye umri mkubwa hakuna shida yeye Mungu ni zaidi ya elimu ya kisayansi na kadhalika.
  Sikiliza nini Mungu anasema juu mke ambaye anataka uwe naye ambaye atakuwa chachu ya maisha safi ya kiroho ktk KRISTO YESU.
  Barikiwa na Bwana.

 10. Arthur Napenda kukujuza kwamba mila na tamaduni zetu ndizo zinazotazama mambo kwa mazoea. Kama utafungwa na mitazamo ya tamaduni zetu huna budi kuoana na mtu munayezidiana kwa umri.

  Zipo sababu za kitamaduni kama utazijali sana. Mke kama ni mkubwa kwa mume ataanza kuzeeka kabla ya mume. Hii imewafanya wengi waamini kwamba siyo vyema kuoa mke ambaye ana umri mkubwa kukuzidi.

  Hata hivyo, uzoefu wa kisayansi unaonesha kwamba wanaume hufariki mapema zaidi kuliko wanawake. Kwa mfano kuna mifano mingi ya wanaume waliokufa wakiwa na umri wa miaka 60 wakawacha wajane wakiwa na umri wa miaka 56. Wajane hao ambao ninawafahamu kwa sura wameendelea kuishi hadi sasa takribani miaka 20 tangu kufiwa na waume zao. Huu ni ushuhuda tu wa kukuonesha kwamba wanawake wanaishi miaka mingi zaidi ya wanaume ingawa huenda ikatokana na tamaduni zetu za kumfanya mwanaume awe mtafutaji mkuu wa mahitaji ya familia zaidi ya mwanamke.

  Kufunga ndoa na mke anayekuzidi umri hakuna tatizo lolote litakalokupata katika maswala yote ya ndoa na kibayolojia. Isipokuwa tu hutajisikia vizuri kisaikolojia kutokana na mitazamo ya jamii inayokuzunguka kutokuwa na mtazamo kama wako kwamba umri siyo tatizo katika maswala ya mapenzi na ndoa.

  Tatizo letu tulio wengi huchukua mitazamo ya mila na tamaduni na kuifanya kuwa ya Biblia wakati siyo. Hakuna andiko linaloelekeza uwiano wa umri baina ya wanaotaka kufunga ndoa.

  Kwa kuwa hakuna andiko linalotoa uwiano wa umri mimi nakushauri uchukue MSIMAMO WAKO BINAFSI kisha usimame kuutetea milele wala usikatishwe tamaa na jamii au wapendwa watakaokuona wa tofauti. Jambo kuu katika NDOA NI UPENDO SIYO UMRI.

  UPENDO HUSTIRI MABAYA YOTE. Kama mwenzi wako unampenda hutamunyanyapaa kwa sababu ya umri wake mdogo au mkubwa kwako. UPENDO NDICHO KIPIMO KISICHOKOMA NA KINACHOWAUNGANISHA WANANDOA KUKAA PAMOJA MIAKA DAHARI.

  Wasikupotoshe watu. Kama umempenda mwanamke hata kama angekuzidi miaka 10 mfano wewe una miaka 30 yeye anayo 40 bado UPENDO UTAWASHIKAMANISHA MILELE HAPA DUNIANI.

  Hata hivyo kibayolojia Mwanamke akitimiza miaka 40 huenda akaacha kuona siku zake za hedhi ikiwa ni dalili kwamba hawezi kushika mimba tena maishani mwake. Wanawake wanashauriwa kuacha kuzaa kabisa wakiwa katika umri huo wa miaka 40. Nakushauri usioe mwanamke mwenye zaidi ya miaka 40 kama una maono ya kuzaa watoto hapa duniani. Lakini kama huna maono ya kuzaa watoto duniani, mwanamke mwenye umri kama huo ni bomba sana. ANAFAA SANA SANA SANA. Nasema hivyo kwa sababu hamtakuwa na purukushani za watoto tena bali mtakuwa mnakula wakati mzuri tu (vijana husema kula good time) bila kuzuiliwa na majukumu ya malezi kwa watoto.

  Unao uamuzi wewe mwenyewe. AMUA WEWE. USISUBIRI WATU WAKUAMRIE HATMA YA MAISHA YAKO.

  UBARIKIWE.

 11. Ndugu Arthur,

  Katika kusoma kwangu Biblia sijawahi kukutana na andiko linaloonyesha namna uwiano wa umri unavyotakiwa kuwa kati ya mume na mke. Ila kama yuko anayefahamu andiko hili anaweza kutusaidia.

  Hata hiyo unayoita ni “kawaida” kwa mume kuwa mkubwa kuliko mke wake natumaini inatokana tu na mazoea, jambo ambalo limekuwa likifanyika tangu zamani za kale.

  Lakini naona kama vile watu wanaweza kutumia andiko linalohusu Adam kuumbwa kabla ya Hawa (Eva). Maana Hawa alitengenezwa baada ya Adamu kuwepo. Mwanzo 2:22. Kwa hiyo “mume” kama “Adam” anatakiwa kuwa mkubwa kuliko “mke” kama Hawa.

  Yawezekana kukawa na sababu nzuri tu za kimwili (zisizopotosha mambo ya imani) ambazo zinatoa angalizo na tahadhari kwa mke kuwa mkubwa (sana) ki-umri kuliko mumewe, ambazo pengine ulishazisikia. Kwa hiyo kama zina manufaa mimi naona ni vizuri tu kuzifuata kuliko kutokuzifuata kwa kisingizo cha kutokuwepo kwenye Biblia.

  Huo ndiyo mchango wangu, natumaini tutapata michango zaidi!

 12. jamani wapendwa naomba mniombee niko katika kipindi kigumu sana kuna mtu naishi naye ananipa majaribu sana yaani huyu mtu akishiba tu anakuwa mgovi mimi namhudumia kwakila kitu maana ni mgonjwa sasa wandugu yaani ananipa majaribu sana ni vigumu sana kumuhudumia mtu ambae hana shukurani shukurani yake akisha shiba tu anakutukana na ugomvi juu lakini kama hakushiba utamuonea huruma maana anakuwa mnyonge sana naomba mniombee sana kwani hakuna linalomshinda mungu hi unaweza kuona kama kichekesho lakini ni kitu cha kweli ambayo inanitatiza sana mbarikiwe wote wapendwa

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s