Maana ya Wokovu – CASFETA

Utangulizi
Wokovu unahusisha hali ya usalama, uhifadhi, uponyaji au kutoa kitu kutoka katika hali isiyo na usalama, nzuri na kupeleka katika hali iliyo nzuri au bora zaidi. Katika maisha ya Mkristo wokovu ni muhimili wa maisha yake kwa sababu ya historia ya mwanadamu.

Inafahamika kuwa mwanadamu aliumbwa katika hali ya ukamilifu, na isiyokuwa na dhambi, Mwanzo1:26. Mungu alimkusudia mwanadamu aishi maisha yaliyojaa hali ya utawala ndani yake. Alimtaka mwanadamu awe shirika naye katika tabia ya Mungu. Mwanadamu huyo alikusudiwa aishi sawasawa na neno la Mungu. Kwasababu neno la Mungu ni kile alichokisema/anachokisema Mungu juu yako. Wanadamu wa kwanza Adam na Eva wakalisikiliza neno la Shetani na kulihalifu neno la Bwana. Kosa walilolifanya Adam na Eva ndilo linaloendelea kutendwa siku za leo kwa wanadamu kushindwa kuisikiliza sauti ya Mungu wao.

Anguko la mwanadamu lilileta kifo cha kiroho na kimwili. (maana ya kifo ni kutengana) Mwili na roho vikitengana ni kifo cha kimwili, Roho na Mungu vikitengana ni kifo cha kirohoMwanzo 3:15 Mungu anatoa unabii wa wokovu kwa mwanadamu aliyepotea. Ifahamike kuwa baada ya mwanadamu kuanguka alianza kutafuta njia mbalimbali za kumrudia Mungu ambazo hazikuzaa matunda. Jambo ambalo lilizaa dini mbalimbali.

Dini – Ni mpango wa wanadamu kumtafuta Mungu
Wokovu- Ni mpango wa Mungu kuwatafuta wanadamu Yoh 3:16

Wokovu ni tukio linalohusisha mwanadamu kutambua kuwa amemwacha Mungu na kutubia uasi huo kwa toba ya kweli, ambayo itazaa badiliko ndani yake, litakalosababisha asirudi tena katika maisha ya kale na kumwezesha kufikia kilele cha nia ya Mungu, yaani kuishi na Mungu milele. Yoh. 3:8a Kutokumtii Mungu huzaa kitu kinachoitwa dhambi, na dhambi ni uasi dhidi ya Mungu. Ni kushambulia sehemu ya utakatifu na heshima ya Mungu, dhambi inapozoeleka huitwa uovu. Uovu unapomfikia Mungu huzaa ghadhabu ya Mungu, na ghadhabu ya Mungu huondolewa kwa malipizi.

Wanadamu wengi hujiuliza kwanini Mungu asingetangaza msamaha bure kwa watu wote, bila hata kazi ya msalaba? au kwanini Yesu amekuja na watu watubu? Mungu ana sifa nyingi lakini katika hili ana sifa za kipekee tatu zinazomfanya asishawishike kumwesabia mtu mwenye hatia kuwa hana hatia Kutoka 34:6-7 Rumi 2:4-16

(1) Mungu ni Mtakatifu
Kwa asili anapingana na kila kitu kinachoitwa dhambi, Dhambi ni kushambulia utakatifu wa Mungu na heshima yake, Kwahiyo mtu yeyote anapofanya dhambi anajihusisha na kutengeneza silaha ya kupambana na uungu wa Mungu.Pia wanadamu wanapofanya dhambi wanakuwa ni waamuzi wa nafsi zao wenyewe. Kwasababu hiyo ni miungu/ bwana wa nafsi zao. Kwa maana nyingine dhambi ni kukomesha utawala wa Mungu katika maisha ya mtu. Kwa hiyo kuwaachilia wanadamu wote kuendelea kufanya dhambi ni Mungu kujitangaza kuwa yeye si Mungu kati ya wanadamu. Na Mungu ana wivu na kila kitu kinachojiinua kutaka kuchukua nafasi yake. Kwahiyo lazima uovu ukichipua kwa wakati wake uadhibiwe. Ili Mungu abaki kuwa yote katika yote (Absolute controller)

II. Mungu ni mwenye haki
Haki ya Mungu inamadai mbele za Mungu kumtaka atimize Neno lake sawasawa na alivyosema. Inakumbusha Mungu kutoa Malipo kwa kadri ya matendo. Zab 34:15-16. Kutokutimiza neno lake ni kumfanya kuwa muongo na kigeugeu. Na kamwe hatakuwa hivyo. Ikiwa amesema mshahara wa dhambi mauti. akiwatangazia Adamu na Eva kuwa siku mtakayo kula matunda ya mti wa katikati kufa mtakufa hakika. Haki ya Mungu inasimama kudai kutimizwa. “Ogopa sana Mungu anaposimama kwenye haki yake” Hakikisha muda huo upo upande wake maana ni hatari.

III. Mungu ni mwenye rehema
Laiti Mungu asingelikuwa na rehema maisha ya mwanadamu yangaliishia bustani ya Edeni. Kwa mujibu wa aya mbili zilizotangulia mwanaamu hakustahili kuishi, lakini ajabu ni kuwa rehema za Mungu zinafanya kazi ya kumshikilia Mungu asiachilie ghadhabu yake kwa upesi, Hapa ndipo tunapoongezewa muda wa sisi kutubu Zab 100:5.

N:B. Rehema za Mungu zinakikomo. ili kuruhusu Mungu kujilipizia kisasi (Usichezee kipindi cha rehema).

Sababu hizi zinatufanya tuone kuwa kumbe asili na umbile la dhambi ya mwanadamu ilikuwa inatangaza mauti yake. Ndipo tunapopata Yoh 3:16 upendo wa Mungu wa agape. Aliupenda ulimwengu hali ukiwa umejaa dhambi na uovu. Akaandaa mipango mwenyewe udhubuti wa wokovu.

Kosa la Adamu na Eva lilizaa kizazi kilichoanza kuwa na asili ya dhambi (mtaji wa dhambi) yaani mtu akiwekwa katika mazingira ya dhambi anaweza akafanya dhambi. Yesu anakuja ndani ya mtu kuleta dawa ya kuondoa asili ya kuasi/ kipingana na Mungu ndani ya Mwanadamu.

NB Kuna imani zinasema tunazaliwa na dhambi ya asili lakini imani yetu ya kipentekoste inasema tunazaliwa na asili ya dhambi. Yaani dhambi haijafanywa na sisi. Ila tumepokea asili ya dhambi ambayo kwahiyo inatoa mtaji wa kufanya dhambi popote panaporuhusu.

Sasa: Yesu ni mdhamini wa agano jipya

Sifa za mwokozi
(I) Alitakiwa kuwa mtu wa karibu na mwanadamu, mwenye kuwajua na kuwaelewa wanadamu (Yesu akazaliwa kama mtu, akachukua mwili)
(II) Alitakiwa awe na uwezo wa kulipa gharama. (Alitoa damu isiyo na hatia)
(III) Alitakiwa kujitoa kwa hiari (nitume mimi Bwana)
Wokovu ulianzishwa na Mungu Baba ukaletwa kwetu na Mungu mwana na unapokelewa kwa Roho.

Ni neema ambayo inapatikana pasipo mtu kuitaabikia, Kwa hali ambayo mwanadamu alikuwa nayo haiwezekani kujiokoa mwenyewe kwa jinsi yoyote. Fikiri hivi
(i) Mwanadamu mwenye Mungu
– Moyo umejaa Mungu
– Anatembea nuruni
– Sauti ya Mungu ikisemwa, ndani yake yumo Mungu (kunatengeneza mazingira ya makubaliano)

(ii) Mwanadamu Mwenye dhambi
– Moyo umekaliwa na shetani
– Anatembea gizani
– Sauti ya Mungu ikisema, ndani yake yumo shetani. Hakuna mzingira ya makubaliano kati ya Sauti ya Mungu na moyo wake. Ndiyo Maana inahitajika aliyejuu ya yote mwenyewe aingilie nyumba hii amkamate mwenye umiliki amtoe nje, aweke makazi yake (Mungu) ndipo mwanadamu huyu aanze kusikiliza Mungu anasema nini kwa ajili ya maisha yake.

Tukio hili linatupa kuamini tumeokolewa bure kwa neema hakuna kazi tuliyoifanya. Ila deni yetu yote Yesu aliilipa Msalabani Isaya 53. La muhimu kwetu ni maamuzi ya kuamua ama kuokoka au kutookoka ila huruma na rehema za Mungu ni tele.

NB: huu ni ufupisho, inahitaji maelezo mapana kujua nini kmefanyika unapookoka ili usirudi tena ulikotoka. Wokovu unapokelewa kwa toba inayohusisha

– Kumwamini Yesu ya kuwa ndiye njia pekee ya Mungu kuwakomboa wanadamu Rumi 10:9
– Toba- ni huzuni ya kweli juu ya dhambi na juhudi za makusudi ya kutokutenda dhambi hiyo tena.
– Ni kuichukia dhambi kiasi cha kuiacha
– Ukiona mtu ametubu kisha anarudi rudia yale ya zamani, anakuwa hajazaa matunda yapatanayo na toba.
– Wokovu pia unahusisha kutambua nini kimefanyika katika maisha ya mtu (kuzijua haki zake ili asiishi tena kama mtumwa kwenye nchi yake mwenyewe.
– Wokovu unahusisha kuhamishwa kutoka kwenye ulimwengu wa giza kuingia kwenye ulimwengu wa nuru
– Kanuni za ulimwengu huu ni kila mtu kuishi chini ya utawala wa Bwana wake (Utawala wa Nuru ni neno la Mungu, utawala wa giza ni neno la Ibilisi (uovu)
– Asije mtu akafanya dhambi na kuhisi kuwa ufalme wa Mungu utamhifadhi (It will never happen) Efeso 2:1
Tunapookoka roho zetu zinarudishiwa uhusiano zilioupoteza mbele za Mungu
Lakini nafsi zetu kwakuwa ziliharibiwa na utu wa kale tunazigeuza kwa neno la Mungu. kweli inatufungua kila iitwapo leo.

Lakini miili yetu tuaitoa dhabihu na kuisulibisha ikubaliane na kweli. Maana mara zote mwili hautatupa ushirikiano sana lakini tunaisulubisha imfuate Kristo. Nafsi ni kiungo kati ya roho na mwili ila inategemea sana nguvu iliyopo katika roho au mwili ili nafsi ifanye kazi.nafsi inaendeswa na Maamuzi yanayofanyika ama ktk mwili au roho Baada ya kukiri wokovu anahusisha yale yote tunayoyafanya mpaka tunaingia mbinguni

– Hivyo basi tunaweza tukagawanya wokovu katika makundi ya wakati (yaani nyakati tatu) za misingi katika maisha yako.uliopita, uliopo, ujao.

Yaani – ulifanya nini (ulikiri)
– Unafanya nini (unaishi maisha matakatifu)
– Utapata nini (Nitakwenda kukaa na Bwana milele)
Inashauriwa: Ni vyema sana ukasoma vizuri kitabu cha Yohana na kisha warumi, Vitabu hivi vinamjengo mzuri wa kimafundisho ya kukua katika wokovu

Daudi katika roho anayoona hayo katika Zab 32 na kukiri “Heri aliyesamehewa makosa yake ……..” Luka 1:73, 2kor 5:17 yakale yote yemepita.
Baada ya kuokoka tunaambiwa kuwa ya kale yote yemepita
– Hakuna nguvu ya dhambi juu yetu tena
– Magonjwa hayana nafasi
– Laana haziwezi kutufuatilia kabisa

NB: Kunabaadhi ya imani zinazosema umeokoka lakini hauja kombolewa. Hivyo kujihusisha na kuvunja laana.
Elewa Hivi – Kazi ya msalaba ilitosha kutufanyia matukio yote mawili
Laana ililetwa na dhambi
Magonjwa yaliletwa na dhambi.

Alichokifanya Yesu ni hiki
(i) Kulipa Deni – Ndiko kukombolewa
(ii) Kutuhamisha – Ndiko kuokoka
Kwa hiyo haya ni matukio mawili yanayofanyika mara moja
Kumwambia mtu umeokoka bali huja kombolewa ni kusema tumekutoa jela lakini bado unadaiwa madeni laazima uyalipe.
Sisi tunaamini deni ya dhambi ilimalizikia msalabani Yesu akitangaza imekwisha kazi ya kumuokoa mwanadamu
– Kinachobaki baada ya kuokoka ni mtu kuifahamu kweli, na Yesu akatuhakikishia ya kuwa mtaijua kweli na hiyo kweli itawaweka huru.
Kwahiyo basi.

Maeneo matano muhimu ya nguvu za mwamini, Ni muhimu mkristo akayajua haya kwasababu ndipo hasa chemchem za nguvu na uhai wa kiroho na hapa ndipo watu wanapopaharibu na ghafla kuonekana hawapo kiroho.

I: MAOMBI
Ni mazungumzo baina ya mwanadamu na Mungu. Ni sehemu ya ibada ambapo mwanadamu anatulia chini ya uwepo wa Mungu na kuzungumza naye.
NB kunatatizo kubwa hapa katika nyakati zetu ambapo maombi yamekuwa ni one way traffic. Ni tukio la watu kumweleza Mungu bila kujua Mungu ananena nini. Zingatia yafuatayo (What are the demands for effective prayer)
– Maombi yanahitaji utakatifu
– Maombi yanahitaji muda
– Maombi yanahitaji kujitoa (Devotion)
– Maombi yanahitaji muendelezo (hayana cut is a continuation)
– Maombi yanahitaji utulivu (Uhusika wako)
– Maombi yanahitaji umakini
– Maombi yanahitaji ulijue neno la Mungu vizuri
– Maombi yanahitaji imani
– Maombi yanahitaji uhakika juu ya uwepo wa Mungu (kuna watu wanaomba kama watu wapiga kelele tu maana uwepo wa Mungu haupo hapo). Yaani hawajatengeneza mazingira ya kukutana na Mungu. Maana Mungu hashuki popote, hashawishiwi ila anaguswa.
Jumla ya hayo na mengine mengi yamezaa maneno mengi lakini matokeo hafifu.

(NB somo hili la maombi ni somo pana linahitaji nafasi yake). Lakini tunaweza kuyagawa katika maeneo mengi
Prayer at first level – Maombi ya kusikizisha dua, matatizo maombezi na kila aina ya kitu kilichopo katika fahamu.
Prayer at the second level –Maombi ya mtu aliyekomaa kiroho ya kutafuta kukaa na Bwana. Kujenga fellowship, kuutafakari ukuu wa Mungu uwepo na nguvu zake (Kumbuka Mungu ………… kwenye maombi primarily objective sio, kusikiliza shida zetu maana anazijua zaidi kuliko sisi.

II. NENO
Neno ndilo kiongozi wa maisha ya mkristo
– Utaomba sawasawa na neno
– Utafunguliwa kadri unavyolijua neno
– Utaishi neno
– Utasema neno ili ufanikiwe
Popote Mungu anapotaka kufanya kazi atalituma Neno.Alipotaka kuwakomboa wanadamu alilituma neno kutoka mbinguni likafanyika mwili, na Neno ni Yesu mwenyewe na ndiyo maana maandiko yanasema yeye aliyemwamini mwana anao uzima.Refer maelezo ya mwanzo.

III.ROHO MTAKATIFU
Mdo 1;8
Kama tulivyoona wokovu ukiandaliwa na Baba ukiletwa kwetu na Mwana ukipokelewa kwetu kwa Roho. Na ni vyema mkristo akaielewa personality(Unafsi Wa Roho Mt) ya Roho mt ili asipate shida wakati wa kuomba ujazo wa Roho Mt na namna ya kuishi naye.Wengi wamemchukulia Roho mt kama kitu cha namna Fulani ambacho baada ya kuomba kitakuja na kuingia kwa kushtukiza au nguvu Fulani. Lakini msingi ni kuwa Roho mt ni Mungu, ni zaidi ya nguvu, si kitu bali ni Mungu mwenyewe na uwepo wake akitembea na mtu.Kujua personality yaRoho mt kutakusaidia kuelewa kuwa Roho Mtakatifu anahisia, akihitajiwa, akipendwa anajua. Na pia akitendewa jeuri ana mwitikio. Hivyo Mungu hawezi kukuacha utaabike anaitaji tuu uelewa wako ili utembee vizuri na Roho mt.
Nani anampokea
-Aliyeokoka,
-Mwenye imani
-kiu
-Shauku
-Uvumilivu na utulivu
Ukimjua vizuri tamaa yako itakuwa sio aingie kwa kiwango gani bali ujitoe kwake kwa kiwango gani ili akumiliki.

IV.USHUHUDIAJI
Ushuhudiaji ni hali ya kuwaeleza wengine kile Mungu alichokifanya ktk maisha. Angalia mfano wa mwanamke msamaria alizunguka kijiji kizima akisema yale aliyeyaona.Hakuna mtu aliyetendewa jambo na Mungu ambaye aliweza kunyamaza kimya.Lakini zaidi ushuhudiaji ni agizo kuu math 28;19 Marko 16;15
Kutoshuhudia ni dhambi kama zilivyonyingine.
Umuhimu wa kushuhudia
-Ni changamoto ya kuishi maisha matakatifu
-Ni kuendelea kushiriki kazi ya upatanishi kati ya Mungu na wanadamu, huduma ambayo tumepewa 2kor 5;19
-ni kuendelea kuujenga ufalme wa Mungu duniani

V.SADAKA NA MAFUNGU YA KUMI
Katika kukamilisha ibada, sadaka ni jambo la Muhimu na ni agizo la Mungu mwenyewe kuwa tusiingie nyumbani mwake mikono mitupu, tunaheshimu kuwa Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata mali na tupo tayari kumtumikia Mungu kwa nguvu zetu zote, akili zetu zote lakini pia kwa mioyo yetu.Hatumpi Mungu kwasababu anahitaji, au kama tusipotoa tutakwamisha kazi yake.Huo ni mtizamo mbaya ambao ndani yake hauna Baraka.
Nitoe namna gani
-Kwa moyo wa uhiari na kupenda
-Kutoa kitu kisicho kidhaifu kulingana na uwezo wako
-Kutoa kwa nia njema na safi
-Kutoa kitu ambacho kitaugusa moyo wa Mungu
-Kutotoa kwasababu ni kawaida kutoa katika muda na sehemu hiyo lakini kwasababu ni ibada.
Fungu la kumi
Ni sehemu ya kumi ya kila tunachokipata, Ni agizo la Mungu kuwa sehemu hiyo ni takatifu kwaajili yake.Hii ni laazima kuwa makini nayo kwasababu tangu zamani hakuna mtu aliyekula kitu kitakatifu akabaki salama.Na sehemu hii inatolewa ktk kanisa lako linalokulea (local church)

Nb
Kifupi wokovu unasura ya nje na ndani
Nje – Ni namna unavyoenenda
Watu wanavyokusoma/ au unavyosomeka (kumbuka sisi ni Barua ya kusomwa na watu wote)
Ndani – Ni namna ya wokovu kiuhusiano na Mungu
Namna Mungu anavyokusoma/ unavyosomeka. (Maana yeye huichunguza mioyo na kuvipima ..)
Sasa kuna kanuni moja ya kufanikiwa kiroho kama tunataka kuendelea kiroho. Nje yetu ya kiroho lazima ifanane sana na ndani yetu ya kiroho. Namna tunavyojihudhurisha mbele za Mungu sawasawa na tunavyoonekana nje. Mfano. Mafarisayo waliikosea kanuni hii wakasubstitute external outlook na viwango vya kiroho vya ndani
Wakaingiza maisha mema nje lakini ndani yao hawana Mungu.
Wokovu ni kuishi maisha halisi sio kuigiza uhalisi
Wokovu ni kufanya kwelikweli sio usanii
Mungu anatuchunguza pande zote mbili yaani undani wetu na unje wetu
Ndani yetu anatakiwa kuumbika kristo ambaye atachonua na kuonekana nje

Wokovu unaharibiwaje
Kwa mtu kuanza kuonyesha tabia zisizokuwa na uzima /za kimungu
(i) Kutokuitii kweli kwa bidii
(ii) Kuanza kuvutiwa na mambo ya dunia
(iii) Kuona mambo ya kimungu ni mzigo mzito
(iv) Kuanza kufuatisha aina ya maisha ya watu wa dunia hii
(v) Kushindwa kulinda fahamu zake na kuruhusu uchafu ambapo unamnyima Mungu kutembea naye
(vi) Kutokuwa na bidii katika yale anayofahamu kuhusu Mungu
(vii) Kuanza kupata uwezo wa kutetea mambo ya kipagani na kutaka kuyahalalisha kuwa ni ya Kimungu kwa sababu yeye anayafanya.
(viii) Kuigiza wokovu – nguvu za Mungu, utakatifu etc.

Uhusiano wa wokovu/ karama za rohoni na kukua kiroho
Baada ya mtu kuokoka anaweza kupokea karama za rohoni na kuanza kutumika kwa nguvu pengine kuliko hata waliomtangulia kwa kadri ya kiu, shauku kuu na kujitoa. Lakini haimaanishi kuwa amekua kiroho. Kukua kiroho kunahusisha tabia za kristo kuanza kuonekana katika maisha ya mwamini.

Tunda la Roho Galatia 5 kujifunua katikati ya watu. Unaweza ukatumiwa kwa karama nyingi lakini nyenyekea chini ufundishwe yaani ukubali kufundishika ili uukulie wokovu vyema na kuwa chombo kinachofaa kwa kila kazi njema.
Wengi wamezolewa katika eneo hili kwa kuinuka kinyume na watu walio walea kiroho.
Kanisa la Wakoritho lilikuwa na tatizo hilo. Walisisitiza sana karama za rohoni kuliko tunda la roho. Walikuwa ni watu waliokiroho kwa utendaji wa kazi za Mungu lakini waajabu katika maisha yao ya kawaida.
Paulo hakuwakataza kuwa na karama za rohoni lakini anawaonya kuwa mambo haya yanafanyika kwa utaratibu.

KILELE CHA WOKOVU
Baada ya kukiri na kuishi maisha safi tunatarajia siku moja Bwana wetu atakuja kutuchukua ile Yeye alipo sisi nasi tuwe hapo.Biblia inasema kila aliye na matumaini haya ktk yeye hujitakasa.uf 22;20

Heri Yule aliyealikwa katika karamu ya harusi ya Mwana kondoo.

source: CASFETA-TAYOMI MLIMANI BRANCH –DOCTRINE COMMITTEE

Advertisements

6 thoughts on “Maana ya Wokovu – CASFETA

  1. baba mchungaji ubarikiwe sana maana kupitia mafunzo hayo tunapata kuelewa vema na kutoka katika giza!
    naomba kwa matakwa yako ikiwezekana utupe utafsiri wa kutuonyesha umungu wa yesu kristo!

  2. Nampenda Bwana Yesu aliye nipa wokovu nanimshukuru Roho mtakatifu kwa ualimu ulipo katika njia hii,mafunuo yawe mengi haya ndio maombi yangu kwenu,mmebarikiwa.

  3. Taabu yako siyo bure utalipwa usipo zimia moyo tia bidii katika wito ulioitiwa utavishwa taji,Mungu akupe neema kuzitengeneza taji zako kwa dhahabu ili zijapo pitishwa katika moto zing’ae zaidi barikiwa.

  4. Haya ni masomo ya msingi sana kwa waongofu wapya na hata kwa wakristo wakomavu tu. Mungu awabariki sana kwa kuandaa masomo haya muhimu. Amen!

  5. may God bless you richly, by availing powerful doctrine in the web!!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s