NDOA NI NINI?

Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).

i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.

ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.

iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.

“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana naye”. Mwanzo 2:18.

Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.

“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.

Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.

i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe

ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana

iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.

TENDO LA NDOA

Ukizingatia kanuni za MUNGU kibiblia kuhusu tendo la ndoa kwa wanandoa;-

i) Ni tukio dogo lenye umuhimu mkubwa.

ii) Kusudi kubwa la tendo la ndoa ni uzazi.

iii) Ni kinga dhidi ya majaribu.

iv) Ni burudani/starehe.

v) Ni suala la kuwa na uvumilivvu na kujitoa.

NDOA -TAASISI TAKATIFU

Ndoa yenye furaha na kuheshimika ni ile ambayo kila mmoja anafahamu na kutimiza wajibu wake katika ndoa kwa mujibu wa nafasi yake. Na hii ndio sharti la msingi kutupelekea kwenye ndoa yenye mafanikio.

i) Kumheshimu mwenzi wako kutokana na hadhi aliyonayo kama MUNGU alivyoagiza.

ii) Heshima inasaidia kutuepusha na ubinafsi na kuongozwa na hisia.

iii) Heshima katika ndoa inachochea mapenzi.

NDOA NI KUTOA

1. Ndio sio mkataba wa kijamii bali agano la kiroho. Waefeso 5:31-33 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa, ila mimi nanena habari ya KRISTO  na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.

Hapa tunajifunza

i) Ndoa ni fumbo la ajabu la kiroho linalowaunganisha watu wawili, mwanamume na mwanamke (mst.31)

ii) Ndoa ya kikristo inaliganishwa na uhusiano uliopo kati ya KRISTO na Kanisa (mst.32)

iii) Mpango wa MUNGU katika ndoa unahitaji upendo wa kujitoa sadaka kama KRISTO anavyofanya kwa Kanisa (mst.33)

2. Ndoa ya Kikristo ni kujitoa sio kupokea. Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake mwenyewe. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Hapa tunajifunza

i) Kutokuwa wabinafsi

ii) Unyenyekevu

iii) Roho ya kutoa na kujitoa.

Wewe mume/mke, mahusiano yako na mwenzi wako yakoje? Unampenda mwenzi wako kama KRISTO anavyolipenda Kanisa lake?  Kama wewe ni mmojawapo wa wasiofuata kielelezo cha KRISTO katika ndoa usijisikie vibaya kwani hakuna aliye mkamilifu. Hata hivyo wajibu huu haukwepeki kwani ni agizo la MUNGU na lazima kutii maagizo yake, kumpenda MUNGU kwa moyo waklo wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Na kumpenda jirani yako kama nafsi yao. Marko 12:30-31. Hivyo, hii ni nafasi yako ya kumwonyesha mwenzi wako upendo ambao wa muda mrefu ameukosa, upendo ambao KRISTO ameuonyesa kwa kanisa lake.

Barikiwa sana.

Jane Lawi Sijaona

Kwa ushauri kuhusu Mahusiano na Ndoa, wasiliana na Askofu John Bigirimana kwa Email: rnominfo57@yahoo.com

Advertisements

32 thoughts on “NDOA NI NINI?

 1. Nimependa kila kilichoandikwa hapa kwani nimeweza kujifunza mambo mengi sana ambayo kwangu ilikuwa ni changamoto kubwa sana. As ante na mbarikiwe.

 2. nashukuru sana kwa mafundisho haya nmepata mwanga mkubwa juu ya ndoa.
  ila ningependa ushaur wenu watumishi wa bwana, mimi nmemuoa bint wa kiislam na tumefanikiwa kupata mtoto mpaka sasa pia nmejaribu kumshaur kuingia kansan akakubal mpaka sasa lakini uhusiano wetu umekua washida sana, m namuona kama hana hekima wala unyenyekevu kwa kuwa anapenda kulazimisha maamuz pia hajal mawazo yangu. mbal na hayo pia anajeul sana kias cha kutishia kuvunja mahusiano

 3. napenda kuwashauri ndugu zangu nyote! mtambue ndoa ni makubaliano ya wawili kuishi kama Mke au Mume na wala sio pete wala sio harusi! shaidi wakwanza ni Mungu na yeye ndio anayefanya unganisho hilo la ndoa na kuzaa matokeo ambayo ni watoto! kwaiyo kama ulikuwa na mwanaume au mwanamke na ulimtambua kama mke wako na mkaishi pamoja kwa Muda fulani na ukajulikana kwao na watu pia, kuwa wewe ndio mke wa fulani au mume wa fulani. hiyo ni ndoa na kinyume na hapo unaitafuta jehanamu na unazini.

 4. Ahsante mtumishi wa Mungu kwa mafundisho ya ndoa,ila mimi nipo na matatizo nilisha achana na mke wangu mwaka mmoja sasa,nimeishi naye kwa mwaka na nusu kwa ajili ya kufuata maagizo ya marafiki wake wanaofanya nao kazi,nimemuomba msamaha ili turudiane ila amekataa, nilimuoa akiwa na mtoto aliezaa na aliekua rafiki tuu ni vyema kumrudia mke wangu naomba ushauri

 5. nashukuru kwa maelezo mazuri juu ya ndoa lakini naomba mzidi kunifafanuria hili!! ndoa ni tendo la ndoa hiyo ndio ndoa, na mengine huja kama mfungamano wa hiyo ndoa lakini ndoa ni lile tendo,,,,,,! tunaweza kumzungumzaje hopo?

 6. Mbarikiwe wote mnaojishughulisha na masuala ya ndoa katika jamii, maana ndoa nyingi kwa sasa wanandoa wanakaa pamoja lakini waliisha achana zamani sana.

 7. Nikweli eti kama upendi saana kufanya tendo la ndoa na mkeo anaweza akatoka nje?

 8. Mbarikiwe wapendwa wa Mungu. Hakika tukifata haya mafundisho. MIGOGORO KTK NDOA ZETU ITABAKI KUWA HISTORIA

 9. Asante sana kwa mafundisho mazuri yenye maadili,Na Mungu awabariki ili mzidi kuzitumia karama zenu katika uinjilishaji kwa maana kuishi bila neno la Mungu ni sawa na
  kuisukuma gari iende mbele bila dereva.Hivyo tunapaswa kuitumia biblia ituongoze katika maisha yetu.Ahsante.

 10. Kwa sheria za Kikatoliki au Kiktristo kwa ujumla,inaruhusiwa kuoa mtoto wa mama wa ubatizo kua mke halali?

 11. Asante sana mtumishi wa Mungu kaka Mtangoo. Kwa kweli umenifafanulia mpaka nimeamua kuprint mafunzo yako. Nimeguswa sana na ushauri kwamba pale ambapo tumeshindwa kukubaliana ktk maamuzi, tulipe suala hilo muda.

  Katika suala hili hili la utii na unyenyekevu, naomba uniongoze tena kufahamu balance katika kumtii mume na kumtii mungu. Nafahamu andiko ya kwamba tutii katika yale yampendazayo Bwana. Hapa ndipo naomba ufafanuzi.

  Kwanza, nikiwa namtii mume nikajua hapa ananielekeza kumkosea Mungu, ntajinasuaje? Na je, hata kama anamjua Mungu si atadhani namdharau na kujidai namjua Mungu sana?

  Pili, sasa amani ya Moyo wangu itakuwaje, nimeacha kumtii Mume na kumpendeza Mungu mwenye mamlaka yote, Mume amekasirika hata hanisemeshi, how do I balance?

 12. Mtumishi wa Mungu,
  Kwa uelewa wangu unyenyekevu hauondoi hekima na busara ya kuamua ama kuona mambo. Unyenyekevu haimaanishi kuonewa. badala yake unyenyekevu ni hekima inayoongoza mambo na kuyaamua kwa musara bila kuwa kwazo. Kwa unyenyekevu ndani ya nyumba unaweza kuangalia mambo mengi lakini kwa uchache yafuatay
  1. HAKI YA NDOA
  – kwa mujibu wa Biblia haki ya ndoa kwa mwanaume ni kupenda na kwa mwanamke ni kutii. Lakini tofauti ni wengi wanavyodhani haki ya mwanamke kutii haiondoi haki yake ya kuchangia mawazo. Ndipo hapo hekima ya kujenga au kubomoa nyumba mwanamke kwa mikono yake inapo kuja. Mwanaume kumpenda mwanamke kama kristo alivyolipenda kanisa ni kujaribu kufikiria udhaifu wa mwanamke na kuuchukulia kama chombo chema cha Mungu kwa ajili ya utukufu wake. Unyenyekevu wa mwanamke unaanzia hapa
  (a) WAKATI WA MATATIZO (stresses)
  Ikiwa mumeo ana msongo wa mawazo halafu na wewe ukajikuta unaongeza msongo kwa mumeo hapo inakuwa umefeli sana. wanawake wengi hawajui kwamba eneo hili ndilo huleta ugomvi sana. mathalan uchumi ukiwa chini ndipo na mwanamke na yeye anaongeza uhitaji wa fedha. Hekima na unyenyekevu hapa ni kukata matumizi yasiyo na lazima na kutumia kulingana na kinachopatikana.
  (b)SHINIKIZO LA NDUGU au MARAFIKI
  wanawake wengi wanasifa ya kutenda sio kwa muono wao bali kutokana na kumuona mwingine anafanya au kushinikizwa. Mfano wanawake wengi sana wanatumia uhuru wanaopewa na wanaume wao vibaya. Ni kawaida kwa mwanamke aliyeolewa na mwanaume mpole na anayemjali kusikia akijitapa kwamba amemkamata mumewe.lakini akiolewa na mkorofi ni kilio. UNYENYEKEVU NI KUZICHUKUA BARAKA ULIZOPEWA NA MUNGU KWA SHUKRANI.
  2.HAKI YA KUISHI
  Mungu alituumba kwa ajili yake na makusudi yake. YEREMIA 1:5 na EFESO 1:5. Yesu Kristo mwenyewe ndiye alikuja ili afe kwa ajili ya dhambi zetu. hakuna mwanadamu alizaliwa ili afe bali tutakufa baada ya kukamilisha kilichotuleta duniani.Unyenyekevu hauondoi haki yako ya kuishi. Kunapokuwa na manyanyaso na mateso hii sasa sio unyenyekevu bali ni maumivu.UNYENYEKEVU SIO KUISHI NA MAUMIVU
  3.HAKI YA KUTOA MAAMUZI
  Kinyume cha unyenyekevu ni KIBURI. mabishano mengi ndani ya nyumba huwa ni ya kugombea haki ama kutafuta ukuu.Wanawake wengi wakitoa maamuzi mawili matatu yakaonekana yanafanya kazi basi kiburi na majivuno huanza kujionesha. Kila mwanamke ni lazima ajue kwamba ni haki na wajibu wake kutoa maamuzi sahihi yeye akiwa kama ni msaidizi.Kama katika kutoa uamuzi kunaleta ubishani sio lazima jambo lile lifanywe wakati ule. wakati mwingine kulipa jambo muda huwa ni njia nzuri ya kufikia muafaka. UNYENYEKEVU NI KUWA NA SUBIRA.
  4.TENDO LA NDOA
  Hili eneo wakristo hatupendi kulijadili sana. kwa ukweli mwanamke anayetosheka huwa ana tabia ya kuheshimu. Dalili ya kwanza ya mwanamke anayetoka nje ya ndoa NI KUWA NA KIBURI NA MASIMANGO. Kutokana na hali ya maisha kubadilika wanaume wamekuwa na msongo wa mawazo hivyo kutokufanya vizuri katika eneo hili. Mwanamke mwenye hekima atamsaidia mumewe, watajadiliana, atajitahidi kushusha msongo wa mawazo ili kumuweeka sawa mumewe.
  5.KUNUNA
  hii ni silaha kubwa kwa mwanamke yeyote. Huwezi kulazimisha maamuzi yako kwa mwanaume kwa kununa. changia mada, elewa changamoto zilizopo, jipe muda wa kutafakari halafu fikia maamuzi. kama kuna kwazo liweke bayana ili lisijitokeze tena. Jitahidi hasira zisikutawale bila sababu. kama unaamka asubuhi umenuna maana yake unatawaliwa na nguvu za giza.
  6.MASHUTUMU
  bahati mbaya sana wanawake wamekuwa ni wahanga wa mashutumu. Mfano ugumba(wengi hawaamini kuhusu wagumba wa kiume). Mahusiano na ndugu wa kiume pia huwa ni magumu kutokana na vita ya asili ya kugombea umiliki wa mume(kwa mke) na mtoto au kaka(kwa ndugu wa kiume). Unyenyekevu ni kuangalia mashutumu yanaanzia eneo gani. Lakini ni vizuri kwa mwanamke mnyenyekevu kuulinda ulimi wake. ongea unapoona umeshapima na kujiridhisha uko sahihi.
  7.MGAWANYO WA MAJUKUMU
  Ni haki ya msingi ya mwanamke kupata stahili zote za maisha. Lakini kuna eneo la usawa wa kijinsia. wanawake wengi sana wamekurupuka sana hapa. wanataka usawa bila kujali mgawanyo wa majukumu. kabla hujadai unachoita usawa hebu angalia mpaka wa maumbile yako, jiulize kama unachotaka ni stahili yako, halafu jiulize kama unaweza chukua jukumu la mumeo. UNYENYEKEVU NI KUJUA MIPAKA YA MAJUKUMU YAKO
  MUNGU AKUBARIKI

 13. Mtumishi wa Mungu mimi ni mwandandoa, changamoto nyingi zipo ktk ndoa, naomba maelezo ktk swala zima la unyenyekevu (submission), kama impasavyo mwanamke. Najaribu sana kulifanyia kazi kwa vitendo ila marakadhaa nashidwa/nagundua kuwa nimeshindwa.

  Nataka kujua jinsi gani ntafanikiwa kuwa mnyenyekevu kwa mume wangu hata ktk changamoto kubwa mfano kushutumiwa uongo, mjadala mkubwa wenye kutofautiana/a hot argument.

  Au, wakati tunazungumza kwa ugomvi/ukali, suala la unyenyekevu linawezekana?

 14. Bonjour frère MILINGA

  Merci beaucoups á ta reponse que Dieu vous benissé.
  Zaidi sana nimeshukuru kwa yote unaponipa moyo ya kusonga karibu na Mungu kupitia IMANI yetu aksati sana kwa yote Mungu akubariki na zaidi tusaidiane tu kwa maombi na kufunga . na zaidi Mungu anipe uvimilivu sana kufatana kwa inchi tunapoishi na zaidi sijuwe nitakushukuru ipi. Mungu ndio alipenda tukutane ku iyi Blog juu ya kusaidina kwa NENO ya Mungu .na kweli iyi Blog ndio inanisaidia sana kila siku na pata barua ama mafundisho ya kuniche ki IMANI.kweli iko vita tuko nayo apa duniani ata sikujuwa kama tendo kama iyi inaweza kufika katika jamaa yangu kwa yote nimeshukuru Mungu kwa yote

  Merci de nouveau de trop pour ta reponse .
  Namba yangu umepata sasa yako sijuwe unaweza kunitumiya

  salamu na jamaa na marafiki wote na wote wanapopitia kusoma Blog iyi

  Mungu awabariki

 15. Mpendwa Monga?

  Bon Jour? Comment alez vous messieur? Dieu vous benisse beaucoup.

  Pole sana sikujua kwamba hata kiingereza hujui. Hata hivyo naona unajitahidi sana kwa kiswahili. Mimi najua kifaransa kidogo tu kwani nimejifunza kifansa miaka 15 iliyopita na kwa kuwa sikiongei na mtu yeyote nakisahau.

  Ukweli ni kwamba Mungu atakusaidia matatizo yote uliyo nayo kuhusu ndoa yako. Kuna watu walirudiana hata baada ya kutengana kwa miaka 5 hadi 10 au zaidi. Alichounganisha Mungu hakuna wa kukitenganisha. Mke wako hata kama hataki kukusamehe pamoja na kwamba uliwashirikisha watumishi wa Mungu pamoja na wazazi akakataa kusikiliza neno lolote, wewe mwache kwanza atulie. Ukipata zawadi yoyote ya kuugusa moyo wewe mtumie. Endelea kufanya lolote linaloonesha kwamba wewe ulishasahau makosa ya zamani na kwamba huna kinyongo kabisa naye. Muombee kwa Mungu. Omba roho ngumu ya kutosamehe imtoke.

  Mpelekee zawadi mbalimbali kila unapozipata iwe pesa, mavazi, gari, vifaa vya nyumbani, mwandikie barua ya mapenzi, nk. fanya hivyo mwaka hadi mwaka. Fanya hivyo kwa sara na maombi ya kufunga, Baada ya muda kama miaka 2 au 3 utakuja kuniambia kama hakuna mabadiliko. Vumilia mpaka mwisho kabisa. Usikate tamaa na kuamua kuoa mke mwingine. Hapo utakuwa umekosea milele.

  Pole sana na Mungu akupe Moyo mkuu wa kustahimili mitihani na majaribu. Kila lenye mwanzo lina mwisho wake.

  Dieu est puisant il peut te done qui tu aime. Merci beaucoup Dieu vous benisse aussi.

  Aurevoir mon ami. Salu tous la en Danmark. Prie en Dieu tout les jours.

 16. Mpendwa Milinga
  Nashukuru sana kwa kunipa mashauri juu ya shida niko nayo basi mimi ni mucongomani ya kutoka Kinshasa kweli swahili yangu ni zaifu kidogo na pia kizungu mimi sijuwe naongea kifarasa na lingala na kiswahili kidogo vile unaponisoma na kidenishi juu naishi apa Danmark.
  Shida yangu kweli mbele ya Mungu nalimukoseya Bibi yangu na nika rudi sana kumuomba masamaha ata kwa machozi Mungu anihurumiye na yeye pia anihurumiye lakini akupenda kusikiya ata neno moja ata watumishi walipima kumushauri akupenda kuwasikiya ata wazazi wake.tatizo yango sana sheria yote ya NDOA nimefanyaka yote leo iyi juu ya kuingiya mbinguni ndio inakuwa kwangu na yeye shida sana juu ya mambo tuko naye sijuwe nifanye nini ?

  na mimi mbinguni sitaki kukosa kabisa nimefanya kazi mingi ya Mungu kwa nini nikose faida enyewe Ndugu MILINGA Email yangu iyi rova_isa@yahoo.com na namba ya simu iyi +4571194665

  Mungu awabariki

 17. Mpendwa Monga

  Mungu akubariki sana. Pole kwa mitihani mikubwa inayoikabili ndoa yako. Mungu atakuwezesha kushinda majaribu au mitihani uliyonayo.

  Hata hivyo nakushauri kama unajua kiingereza maelezo yako uyaandike kwa kiingereza ili wale wanaojua kiingereza waweze kukupa ushauri kwani naona katika maelezo yako Kiswahi kinakupa shida sana kiasi kwamba baadhi ya maneno uliyoandika mimi sikuyaelewa kabisa.

  Kwa kuwa blogi hii inasomwa kote ulimwenguni naamini ukiwa na mahitaji unayotaka wapendwa wakupe ushauri na ukawa huwezi kuyawasilisha kwa kiswahili vizuri, labda jitahidi tu kuyaleta kwa kizungu. Utapata msaada tu. Haya ni maoni yangu tu.

  UBARIKIWE NA TARAJIA NGUVU YA MUNGU KATIKA NDOA YAKO NA TARAJIA KUONA UKIPIGA HATUA KUBWA ZAIDI KATIKA NDOA NA KAZI YAKO.

 18. Bwana asifiwe ndugu JULIUS DARCY na MILINGA na yote munapotuzaidiya juu ya NDOA na shukuru sana ndugu JULIUS kwa kunipa moyo juu ya NDOA yangu kweli niko kushida tena vile MILINGA anaposema ATA PIA UNAWEZA KUKOSA ATA MBINGUNI na mimi nataka sana kuingiya MBINGUNI munisaidiye sana na maombi siku moja nishuhudiye niko apa EUROPA na tuko na watoto wawili .

 19. Mpendwa Baraka,

  Nadhani unajaribu kujifariji kwa maneno yasiyo na baraka za maandiko kabisa. Agano la Jipya halijaruhusu kumpa mke talaka kabisa. Biblia inasema Mungu anachukia kabisa kuachana na mke wa ujana wako.

  Katika maisha yako usifanye kosa kumwacha mke wa ujana wako ni kosa kubwa ambalo utalijutia maisha yako yote yaliyobakia duniani huenda hata mbingu ukaikosa kwa kosa kama hilo.

  Huyo dada unayesema unampenda kwa sasa, huo sio upendo wa AGAPE ni upendo unaosukumwa na mazingira yenu ya maisha kurandana na wala siyo Mungu.

  Nakushauri umsamehe mke wako wa kwanza wa ujanani na umtafute mweze kurudiana haraka sana mwendelee kulea watoto wenu kwa gharama yoyote.

  Huyo dada pia anapaswa kuhakikisha anarudiana na mume wake wa ujanani hata kama wametengana zaidi ya miaka 6 au hata ingekuwa zaidi.

  Yesu Kristo anasema amwachaye mkewe na kuoa mwingine anazini. Amwoaye yule aliyeachwa naye pia azini. Kumbuka wazinzi hawana nafasi Mbinguni kabisa. (Math. 19.1-8).

  Usijifariji kwa lolote lile wala usitazame makosa yaliyofanywa na nyie wote kabla ya kuanza ndoa zenu za awali. Kisheria na Kiblia ukishaingia kwenye ndoa kwa namna yoyote ile ndoa hiyo huwa halali mbele za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo tu ulikubali kukaa katika ndoa hiyo kwa zaidi ya miezi 3 mfululizo sembuse ninyi wote mlikaa katika ndoa hadi mkazaa na watoto. Ndoa yoyote hufungwa mbele ya mashahidi, watoto wenu ni mashahidi tosha wa ndoa zenu. Wewe unao watoto na huyo unayetaka kumdandia eti mmependana naye anao mashahidi kuwa mume wake wa kwanza bado yuko hai na alizaa naye.

  Ndoa na iheshimiwe na watu wote, ndivyo maandiko yasemavyo. Unapaswa kuiheshimu ndoa yako ya kwanza bila kisingizio cha kwamba ulilazimishwa na wazazi wako au ndugu zako. Huyo dada pia anapaswa kurudi kwa mumewe bila kujali kwamba alilazimishwa kuolewa ili kulinda heshima ya Mchungaji baba yake.

  Hata kama mtaamua kuoana na huyo dada uliyeanza kumkodolea macho kwa sasa, bado hamtapata baraka mioyoni mwenu kabisa wala machozi hayatafutika usoni mwenu ukizingatia kwamba mtakuwa mnaigiza tu kupendana kumbe hakuna upendo wa AGAPE kati yenu bali matatizo yaliyowapata awali ndiyo kamba itakayowafunga tu.

  Pole sana kwa yaliyokupateni wote na huyo dada, LAKINI NDOA MNAYOTAKA KUANZISHA NI FEKI AU BANDIA MBELE ZA MUNGU, KANISA, MAANDIKO NA SHERIA ZA SERIKALI YA NCHI HII.

  Rudi kwa mkeo wa ujanini tafadhali sana.

 20. Asante mtumishi wa Mungu kwa mada, mimi niko na swali moja,
  Ndoa yangu iko na mgogoro mkubwa sana na tumetengana na mke wangu kwa miaka 5 sasa, watoto wangu wawili nawalea menyewe bila mama yao. huenda kumsalimia wakati wa likizo…. hivi majuzi nimekutana na dada ambaye amenivutia sana na nahisi kumpenda kwa dhahati yeye pia ndoa yake ilivunjika miaka 6 iliyopita na yuko na watoto wawili anaowalea yeye mwenyewe…. kwa kufuata historia zetu tumegundua ya kuwa matatizo yetu yamelandana kwa kiasi kikubwa, mimi nililazimika kumuoa msichana niliyechaguliwa na wazazi bila kumpenda, na kwa upande wa huyu mwenzangu yeye alilazimika kuolewa na mwanaume aliyembaka baada ya kupata mimba kulinda heshima ya babake mchungaji na kanisa…. kwa ujumla ndoa zetu zilikuwa ngumu kwani hazikuwa na mapenzi ya dhati hali iliyosababisha migogiro mikubwa na hata kuachana…. Je inaruhusiwa sisi wawili tuliopendana sasa kuoana? kweli nampenda nae pia ananipenda na watoto wetu pia wanapendana na lengo letu tuishi pamoja tufutane machozi na kuyasahau machungu tuliyopitia mwanzo.
  Ninaomba ufafanuzi na ushauri juu ya hili.

 21. nashukuru kwa maelezo mazuri ila ningependa kupata ushahidi wa kibiblia kuhusu kipengele cha kwanza kinachohusu
  i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu

  asante

 22. Ndugu uliyetumia jina la “Mtumishi”,

  SG inapenda kukuambia kuwa blog hii ni blog ya Kikristo ambapo amani ya Kristo inatawala! Kwa hiyo tunakushauri usihofu kutumia jina lako halisi. Kutumia jina halisi kuna faida nyingi sana. Ni vizuri kuwa ‘wewe’ maana hakuna sababu ya kujificha. Hapa hatuna “anonymity”.

  Tunashauri pia kila mchangiaji kutumia jina lake halisi maana itarahisisha kukupatia msaada zaidi iwapo utahitajika!

 23. Mpendwa Mtumishi,

  Napenda kukueleza kwamba umri sahihi wa kuoa/kuolewa ni miaka 18 kwa mujibu wa sheria za nchi hii ya Tanzania. Endapo mtu yuko shuleni ni miaka 21. Ukioa/Kuolewa chini ya miaka 18 ndoa hiyo ni batili kabisa na umevunja sheria za nchi ingawa wasichana wanaruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 pale wazazi tu watakaporuhusu ndoa hiyo.

  Watu wengi wanachelewa kuoa/kuolewa kwa visingizio vya ugumu wa maisha jambo ambalo limeendelea kuongoza idadi kubwa ya watoto wasiokuwa na wazazi na wanaotupwa majalalani, mitaroni, vyooni, kutelekezwa, nk. Tatizo hili limeingia hadi makanisani mwetu kiasi kwamba vijana waliokuwa wakitumainiwa makanisani wameacha wokovu na kujiingiza katika vitendo vya uhuuni na kubeba mimba wakiwa nje ya ndoa.

  Mimi napendekeza kuwa umri mzuri kuoa au kuolewa ni miaka 25 ukikosea katika umri huo, unakuwa umeharibu mlolongo mzuri wa maisha yako hapa duniani hasa katika swala la kuzaa watoto, kuwalea, kuwasomesha, kuwapa mitaji na kuwawezesha kujitegemea maishani mwao.

  Umri wa mwisho kuzaa watoto ni miaka 35-40 kwa wanawake. Mwanaume pia anashauriwa kuacha kuzaa mara tu atimizapo miaka 40 ili kujiepusha na kuzaa watoto ukiwa mzee na kushindwa kuwaandalia mstakabali mzuri wa maisha yao ukiwa bado na nguvu za kutosha.

  NDOA ni taasisi muhimu sana ambayo Mungu aliikusudia iweze kuendeleza na kutunza dunia hii katika mwonekano mzuri na mahala pa kufaa kuishi. NDOA ikivurugwa maana yake dunia imevurugwa.

  UBARIKIWE.

 24. Ndugu yangu Monga Bwana Yesu asifiwe!
  Pole sana kwa kuwa mbali na mwenzi wako ila Mungu anaweza kuifinyanga tena ndoa yako kurudia upya kama ulivyokuwa mwanzo, nimaombi yangu kwa Bwana siku moja ushuhudie uweza wa Bwana juu ya ndoa yako.
  Mungu afanye njia kwako ktk Jina la Yesu.

 25. Mtumishi Mungu akubariki kwa somo lenye kujenga!
  Minimeoa mwaka jana na tumebarikiwa kupata mtoto moja.
  Nashukuru kwa maana nahitaji kuwa karibu na mke wangu na kumpenda kama Kristo alivyonipenda.

 26. Bwana asifiwe nashukuru sana kusoma hii mjadala wa leo.Na niko na swali ngumu juu ya NDOA yangu iko na shida hata leo hatuko pamoja sijuwi kama kuko na njia zingine naweza kukuandikiya juu ya haya!

  Tafazafi unisaidie Mungu awabariki

 27. Ubarikiwe sana mtumishi,
  ila mi nilikuwa nauliza ni umri gani hasa ni sahihi kwa kuoa/kuolewa? Ukizingatia hasa changamoto za maisha,ukuaji na kasi ya mabadiliko ilivyo katika jamii,kanisa na dunia kwa ujumla!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s