Kuachana


Luka 16:1 8  “Kila amwachaye mkewe na kumuoa mke mwingine azini naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.”

Wapendwa katika Bwana, nawasalimu wote katika Jina la Yesu Kristo Mwokozi wetu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa. Nimesukumwa leo kulizungumzia suala hili zito: Suala la kuachana watu wawili waliokwisha kuoana, waliokwisha kukubaliana kuwa MKE na MUME. Maandiko yamesema hapo juu kuwa kila amwachaye na kuoa mwingine AZINI, na yule amwoaye yule aliyeachwa AZINI. Nimekuwa nikisuluhisha ndoa za watu wengi zenye machafuko, zenye shida, na baada ya hayo yote, nikasukumwa kuwa niandike ujumbe huu, ili uwasaidie wale ambao tayari wamekwisha kuoana, na wale ambao wataoana.

Efeso 5:33 “Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, na mke asikose kumstahi mumewe”

Mpendwa, hebu tuendelee kujifunza kutoka kwenye Neno la Mungu. Wajibu wa MUME ni kumpenda mke wake kama nafsi yake. Suala hili ni gumu; ni agizo gumu, lakini aliyetuagiza anajua kuwa wanaume wataweza kumpenda mke KAMA mtu apendavyo nafsi yake. Mtu anapojikwaa mguu, kwa kuwa anaupenda mguu wake, haupigi, wala haukati, anaupuliza, anaushughulikia kama umeumia, hawezi kuuliza kuwa ‘ulikuwa unatembeaje mpaka ukajikwaa?’. Na MKE ameambiwa asikose KUMSTAHI mumewe. KUMSTAHI ni KUMHESHIMU MUMEWE. Kumheshimu kwa njia gani?

Efeso 5:22 “Enyi wake watiini waume zenu, kama kumtii Bwana wetu, kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo, viyo hivyuo nao wawatii waume zao katika kila jambo”

Naomba twende pole pole tukijifunza, ili ndoa zipone maana nyingi zimeoza, hazifai. Wamama wameambiwa wawatii waume kama kumtii Kristo. Hapo napo huwa kuna matatizo, maadam wote wameokoka, basi wanajihesabu kuwa wako sawa. Hapana! Soma vizuri: MUME NI KICHWA. Sasa kama mume ni kichwa, ndiye anatakiwa kuongoza nyumba, kwa kuwa kichwani kuna- MACHO, MASIKIO, UBONGO, MDOMO, n.k

Nazungumzia mambo ya rohoni: wamama wengi wamebomoa nyumba zao kwa mikono yao, pale walipojaribu kuongoza, wakidhani wanaweza. Kumbuka neno hili kuwa Adamu aliishi bila Hawa lakini Hawa hakuwahi kuishi bila Adamu.  Hawa alipoishi bila Adamu kwa dakika chache tu aliondoka akakutana na nyoka, wakati Adam hayupo pamoja naye, akajitahidi kuzungumza na nyoka akijibu maswali aliyokuwa anaulizwa, lakini hakufua dafu!

1Tim 2:13-14 “Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudangaywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa, akaingia katika hali ya kukosa

Biblia inaeleza wazi wazi kuwa Adam hakudanganywa. Aliyedanganywa ni Hawa. Sasa tuendelee kujiuliza: kama Adam hakudanganywa, ilikuwaje Ale tunda? Je, Alilazimishwa?; Kwa nini alikula?

Nilipokuwa natafakari mambo haya niliyaona kwa ndani zaidi. Utakumbuka wakati Bwana alipokuja ili akutane nao Bustanini, hakuwakuta, akamwita Adam na  kumuuliza alikokuwa! Adamu akasema “nimejificha, kwa kuwa niko uchi”; akamuuliza “nani amekwambia kuwa uko uchi?” [au umekula tunda nililokukataza?] Adamu akasema “Mwanamke uliyenipa ndiye amenipa tunda nikala”.

Sasa ona hapa, Je, Hawa alimlazimisha?  Kwa nini alikula?  Watu wengi wanasema kuwa Adam aliposema kuwa ni huyo mwanamke uliyenipa, alikuwa anamlaumu Mungu kwa kumpatia mwanamke. Hapana!  Hebu leo nikuonyeshe kitu hapo: Biblia inasema “Apataye mke apata kitu chema, tena hujipatia kibali kwa Bwana

Sasa Adam alipojibu kuwa “ni huyo mwanamke uliyenipa” alikuwa akisema hivi: “Huyu mwanamke uliyenipa, najua hukunipa kitu kibaya, ulinipa kitu chema kabisa, na mimi kama mimi hajanikosema, amekukosea wewe. Na kawa kuwa wewe Mungu wangu ulinipa kitu chema basi sitakiacha, nitaongozana nacho kokote kitakakokwenda, sitakiacha. Wewe Mungu una uwezo, kwanza unajua kuwa ni chombo dhaifu, wewe ungeweza kukizuia kabisa kisile tunda lakini ukakiacha kikala, basi nakufa nacho!”.

Alipomaliza kusema hayo akalipokea tunda kwa hiari yake, akala  na akajua sasa hawawezi kumuona Mungu wakiwa na hali hiyo; wakakubaliana waondoke  shambani.

Sababu nyingine iliyofanya ale ni kuwa alijua kuwa yeye Adam aliishi bila Hawa  na wala hakuomba Mungu ampe mke, ni Mungu tu alisema “si vema sasa uwe peke yako nitakufanyia msaidizi”, na akamfanyia  wa kufanana naye, yaani alimfanyia mwili wake, sasa mwili wako utaukataje uutupe? Akajua kuwa UBAVU wenyewe hauwezi kuishi  bila kichwa, ndio maana alisema basi nitaendelea kuwa na ubavu huu.

Ruth 1:16-17 “Naye Ruth akasema, usinisihi nikuache, nirejee nawe, maana wewe uendako nitakwenda, nawe ukaapo nitakaam watu wako watakuwa watu wangu, pale utakapokufa nitakufa nami, na papo hapo nitazikwa. Bwana anitende hivyo na kuzidi, ila kufa kutatutenga wewe na mimi”

Huyo ni Ruth alipokuwa anamwambia mama mkwe wake, wakati amemsihi aondoke kama Olpa alivyofanya. Ndugu zangu nazungumza habari za KUACHANA, siku tulizonazo, limekuwa ni tatizo kubwa katika maisha ya wana ndoa wengi, wengine maombi yao yamekwama hayajibiwi kwa sababu ya ndoa zao.

1Pt  3:7 “Kadhalika nanyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima, kama chombo ksicho na nguvu, na kama warithi pamoja na neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe”

Neno linasema wazi wazi kuwa mume ukae na mke wako kwa akili. Unaona hiyo? Kukaa na mke inatakiwa akili itumike. Je, Ni akili ya namna gani? : Kuwa ni chombo kisicho na nguvu, japo wakati mwingine wanajitutumua kana kwamba wana nguvu, lakini Biblia inabaki pale pale kuwa ni chombo kisicho na nguvu, ya kwamba mume umpe mke Heshima. Kumpa heshima ni kufanyaje?

Hayo yote tuyaangalie vizuri maana ndiyo yanayoleta matatizo iwapo mmoja atashindwa kutimiza wajibu wake. Unajua kama madereva wote wangefuata sheria za barabarani, nakwambia hakungekuwa kunatokea ajali barabarani, pale pa “keep left”, mwendo gani unatakiwa hapo, wakati gani umpite mwezako aliye mbele, wakati gani usimame n.k!

1 Pt 3:1-6 “Kadhalika nanyi wake watiini waume zenu, kusudi, ikiwa wako wasioliamini Nneo, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile neno. Wakiutazama mwenendo wenu safi na wa hofu. Kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje, yaani kusuka nywele, na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi, bali uwe utu wamoyoni, usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika, yaani roho ya upole, na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumikia Mungu, na kuwatii waume zao,kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana. Nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yoyote”

Soma kwa makini hayo yote hapo juu, utaelewa. Je,  wewe mama unamwitaje mumeo?

Unajipambaje? Wengi wamesoma wakaelewa vibaya kuwa Biblia imetukataza kujipamba, hapana. Inakueleza jinsi unatakiwa kujipamba, usidhani ukiisha vaa nguo nzuri, ukasuka nywele zako, ufikiri kuwa hapo umemaliza; hapana. Kumbuka Bwana anaangalia MOYO, na jambo hili Yesu aliliweka hivi:

Math 23:27-28 “Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki, kwa kuwa mmefanana na makaburi, yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivi ninyi kwa nje mwaonekana na watukuwa wenbye haki bali ndani mmejaa unafiki na maasi.”

Unaona alichosema Bwana Yesu hapa? Wala hakusema makaburi yasipakwe chokaa, hapana! Kama ambavyo hakusema watu wasivae mavazi mazuri, ila pamoja na kuvaa, tuelewe kuwa kuna cha zaidi ya kuvaa: mioyo ni muhimu kuliko kuvaa! Hapo inabidi tuelewe vizuri, maana wapo watu wanasema kuwa Biblia inasema haturuhusiwi kuvaa mavazi ya thamani. Hapana hiyo siyo maana yake!Mtu akikwambia kuwa uanajeshi wako usiwe wa kuvaa buti, hapo hajasema usivae buti, ila anasema ukiisha vaa buti, usije ukadhani umemaliza, kuna zaidi ya hapo!

Biblia inasema kuwa katika siku za mwisho watu watakuwa na tabia fulani, ambapo mimi nimechagua mambo matatu ambayo hayo ni mabaya mno! Hebu jipime:

1.Wenye kuvunja maagano.

2.Wasiotaka kufanya suluhu.

3.Wasio na shukurani.

Tafakari hayo mambo hapo juu. Mtume Paulo aliona siku za mwisho kuwa watu watakuwa wanavunja maagano. Katika kuoana huwa kuna maagano, wengine wanavalishana pete, wanasema maneno mbele za Mungu na mbele za watu, vigelegele vinapigwa, Neno linasomwa na watumishi wa Mungu.! Lakini baada ya siku si nyingi, hayo maagano yanavunjika; unasikia ndoa hiyo imekwisha wala haipo tena! Ni wengi wamevunja, na tayari wameshaoa tena. Lakini wanasema bado wanasonga kuelekea Mbinguni! Hivi ni kweli kuna kuelekea mbinguni hapo? Endelea kutafakari!

Wengine hawataki kabisa kufanya suluhu. Biblia imesema kuwa “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.” Wapo wana wa Mungu, wazuri kabisa katika kuwapatanisha wapendwa wanapokoseana. Lakini kwa sababu siku za mwisho watu hawatakubali kufanya suluhu, basi hakuna kinachofanyika isipokuwa kuachana tu. Endelea kutafakari!

Watakuwepo watu watakaovaliwa na roho ya kukosa shukurani. Hivi kweli, mkeo/mumeo ambaye mmekaa naye miaka kadhaa unayoijua wewe; Hakuna hata jambo moja tu ambalo aliwahi kukufanyia zuri? Ukilikumbuka hilo, naamini kuwa litageuza hasira yako na utaumba roho ya kushukuru, na mwisho msamaha utaumbika na utamsamehe, na utajikuta mnasameheana.

Kol 3:12 “Bsi kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana na kusahemeana; mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake, kama Bwana alivyowasamehe ninyi; vivyo nanyi”

Napenda nimalizie kwa kusema kuwa Mungu atusaidie: ndoa ziponywe; talaka zisitajwe kwetu kamwe; vinginevyo tunaelekea kwa wenzetu wan chi zilizoendelea hasa za Ulaya na Marekani ambao wanaoana kwa mkataba, ukiisha wanaongeza. Hiyo siyo Biblia.

Nawatakia kila la kheri katika ndoa zenu. Amina!

Mchungaji Samnuel Imori.

Advertisements

13 thoughts on “Kuachana

 1. Mama Isaack, pole sana na yanayokusumbua, kwa Yesu yote yanawezekana. 0765446611. Tuwasiliane kwa maelekezo zaidi. Mungu akubariki.

 2. Mchungaji mimi ni Mkristo na nimeolewa na Mkristo mwenzangu.Ninaamini katika ndoa kuna kukwazana lakini tunasisitiziwa kusamehe na kusahu. Swali langu mimi huwa namkwaza Mume wangu nagundua hilo na kumwomba msamaha au hata kabla ya kumwomba msamaha yeye hukasirika na kuamua kukaa kimya hata kwa siku zaidi ya mbili(silent treatment) halafu hatajaribu hata siku kuanza kunisemesha akiwa ok.Kila nitakapo jaribu kuongea nae atanijibu sitaki kuongea na wewe ama naomba uniache lakini hili huwa linaenda mpaka siku nne wakati mwingine haongei na mimi. je mimi kama mke ninayetakiwa kumtii mume wangu natakiwa kufanya nini wakati huu? Swala la pili nimeshajaribu kuongea nae na kumueleza ubaya wa yeye kukaa kimya naona haelewi nashindwa kuelewa tatizo.Kitu kimoja najua namkosea sifanyi makusudi lakini mara nyingi ni mtu wa kufyumu. Na je tatizo inaweza kuwa kwasababu mimi ndio ninaeprovide kwa asilimia kubwa nyumbani?na je natakiwa nifanyaje ili niache yeye aongoze familia?maana akikasirika kidogo tu hata kusali hataki wala kwenda kanisani.sasa je ninafanya kosa kwenda kanisani na watoto na kusali nao niwapo nyumbani? najitahidi kuliombea hili na kujiombea mwenyewe kuwa na reaction iliyo njema lakini naona kama nakosea kwa sababu ni kama tutakuwa na siku za amani tano halafu zinakuja hizo.Ni kama cycle hivi.Kingine ni kuwa anafanya kazi serikalini mshahara wake kidogo, hili nalielewa lakini nilimshauri kutafuta kazi sehemu nyingine maana ana masters kabisa na ni mwanaume mchapakazi na mwenye akili katika kazi.Analalamika sana kuhusu kazi yake kwamba haimtoshelzi lakini simuoni akifanya juhudi katika kutafuta kazi sehemu nyingine.je amefungwa na ninatakiwa kufanya maombi gani afunguke? Sisi ni wakatoliki lakini mimi niko tayari kuokoka na kuishi katika maombi maana najua katika hilo nitaweza kufanikiwa.
  Ninahitaji msaada wako.

 3. Mungu akubariki sana Mtumishi wa Mungu. Mafundisho haya yameniinua kutoka katika kiwango kikubwa. Namshukuru Mungu aliyeniongoza kusoma maana niko kwenye wakati huo. Mwenzangu anataka kuoa mwanamke mwingine ila mimi nimesimama kuangalia kusudi la Mungu. Nashukuru katika maelezo yako nimepata jibu.

  Lipo kusudi la Mungu ndani yako Mungu akutie nguvu uendelee kufunuliwa mafundisho yenye kutujenga.

 4. Ndugu Sungura Steve,
  Nakusalimu kwa Jina la Yesu, bila shaka hujambo, napenda nikujibu swali lako ulilouliza,
  Umeuliza Mtu akioa mke, na huyo mke akaamua kuondoka na kwenada duniani, kuolewa na mtu mwingine, wewe utafanyaje?

  Ok Biblia inasema kuwa 1 Kor 7;10–
  Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala hapo si mimi, ila Bwana, mke asiachane na mumewe.
  Lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe, tena mume asimwache mkewe.
  Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye, asimwache,
  Na mwanamke ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache.
  Kwa maana yule asiyeamini hutakaswa katika yule anayeamini.
  Mstari wa 15—-
  Lakini yule asiyeamini akiondioka na aondoke, hapo huyo ndugu mke au ndugu mme hafubgiki, lakini Mungu ametuita katika Amani.

  Nimekujibu kirefu kidogo, maana wako wengine wana hali hiyo, na kama mmke huyo ameamua kuondoka, na kwenda kuolewa kwingine basi mme huyu hafungiki.
  LAKINI BWANA AMETUITA KWA AMANI, MAPENZI YAKE NI KUTOKUACHANA KABISA KAMA NILIVYOFUNDISHA.
  Asante.

 5. Dada Rose Vikori,
  Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo Bwana wetu.
  Nakupa pole sana kwa yote yaliyokupata katika maisha yako, Nakuombea kuwa yasikupate tena.
  Napenda nikushauri, hivi,
  1. Samehe yote, sahau.
  2. Kama umeokoka, nakushauri utafute kanisa la Kiroho litakalokulea
  Katika misingi ya Biblia, linalofundisha kweli yote ya Biblia.
  3. Kama haujaokoka, nakushauri kuwa hakuna njia nyingine ya kupona, isipokuwa KUOKOKA tu.
  4. Pata muda wa kutosha kujifunza Neno la Mungu, ufanye bidii, kuhudhuria ibada kwa uaminifu, na kuwa mtendaji wa Neno la Mungu lile unalofundishwa.
  5. Marafiki zako wawe wale wanaompenda Mungu, watakaoendelea kukufundisha njia za Bwana.
  Nadhani ukifanya hayo kwa uaminifu, utakua kiroho, utajua kupigana vita vya kiroho, na utapata ushindi.
  Mungu akubariki pamoja na nyumba yako.
  Mch. Imori.

 6. Mchungaji,naomba kuuliza; mtu akioa mke halafu huyo mke akaamua kumwacha Yesu na kwenda kuolewa na mtu mwingine ninatakiwa kufanyaje?

 7. Mchungaji nimefurahishwa sana na mada yako natamani ningeipata kabla hayajaharibika kwangu. Niliolewa miaka kumi na kitu iliyopita nilipata taabu za kila aina kipigo kwangu ilikuwa kawaida. Nilisulihishwa mpaka nikachoka nilipata kipigo kikubwa mpaka siku moja nikateguka mbavu na kuchubuka goti zima nakuguzwa na ndugu zangu, nilipopona sikurudi tena kwangu, kila ninapo kumbuka napata uchungu sana baada ya mwaka mwenzangu alioa nami nakaamua kuolewa ana watoto nami nina watoto. Nampenda Mungu na nataka kwenda mbinguni. Je nifanyeje ili niishi maisha yanayo mpendeza Mungu,

 8. Halleluya ubarikiwe sana baba mchungaji na kizazi hiki kitapona kwa jina la Yesu

 9. ubarikiweeeeeeeeeeeeeeeee sn nimepona hapa ubarikiwe mnooooooo yaani mpaka ushangae

 10. Nashukuru mchungaji kwa kuandika kile kinachisumbua jamii yetu kwa sasa pia ni somo tosha kwa vijana kama mimi ambaye muda si mrefu naingia kwenye ndoa kwa mapenzi ya mungu baada ya kumaliza masomo yangu ya elimu ya juu. Kwa vijana wenzangu mlioko vyuoni tafakiri sana kuhusu somo hili mana wengi tunaingia kwenye mapenzi/uhusiano bila kuwa na ulewa nini maana ya mahusiano.

  Hii ni changamoto kubwa sana kwa sisi tunaotaraji kuingia kwenye ndoa kama vijana tunaye mjua kristo na nini tuwafanyie wenzi wetu tuwapo katika ndoa. Mana wengi hasa wana zuoni tunaishia kupeana promise za kuoana ambazo hazitimiliki. Hii inatokana wengi hasa sisi wavulana kuwarubuni wasichana kwa udhaifu walioumbiwa angali moyoni hatuna nia ya dhati ya kuwaoa baadaye, “part time kind of love” ..mana maandiko kwenye biblia dhahiri yanasema uonavyo nafsini mwako ndivyo ulivyo ..lakini tukumbuke kwamba unaochotaka kufanyiwa anza kufanya kwanza kwa wenzio ..MCHUNGAJI SAMUEL IMORI ubarikiweeee na usichoke na huduma ya bwana aliyo kukirimia ..mimi ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kitivo cha uhandisi “civil engineering” nilikuwa naomba mawasiliano yako mostly e-mail

 11. Bwana asifiwe Mchungaji IMORI

  Kweli iyi ndio neno la kwanza ndani ya ulimwengu ya Kiroho. juu ya NDOA .Mungu akubariki ndugu zaidi tubaki kwenye maombi .juu Ndoa yote ilipoachana irudiane katika Jina la YESU.
  tusome sana Kol 3:12

  Ubarikiwe kundi lote

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s