Nasumbuliwa na magonjwa; Nahitaji Maombi

Bwana Yesu asifiwe!

Mimi ninaishi Ubungo Dar es salaam. Nimekuwa nikisumbuliwa sana na magonjwa kwa miaka mingi. Magonjwa ambayo yananisumbua ni: Vidonda vya tumbo; Vidonda vya koo; Vidonda vya ulimi; Vidonda kichwani; Kuhema kwa shida; Maumivu ya kifua; Allergy za mayai,manukato na kudhoofu kwa mwili. Nimeshaonana na madaktari wengi bila mafanikio.

Nahitaji maombi ili Mungu aweze kuniponya! Pia naomba Neno la kusimamia na kutunza uponyaji wangu na namna ya kuliatamia ili hadi uponyaji udhihirike.  Natanguliza shukurani zangu.

Mungu awabariki na kuwafanikisha.

Lucas L. Maro

Advertisements

5 thoughts on “Nasumbuliwa na magonjwa; Nahitaji Maombi

 1. ASANTENI SANA KWA MICHANGO YENU NA MAOMBI.
  NAMBA ZANGU ZA SIMU NI
  0719 501 505
  0753 009 082
  MUNGU AWABARIKI.

 2. pole sana ndugu Lucas naomba uandike namba yako ya simu tuweze kuwasiliana.

 3. Mimi nakushauri kama huna Biblia nunua, halafu soma Mithali 3 yote, Zingatia sana Mithali 3: 1-2, 7-8. ikiwezekana pigia mistari kisha tafakari sana. Msingi wa afya yako unajengwa katika neno la Mungu. Biblia imeweka wazi kabisa kile Mungu anachoona katika Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa….”
  Maarifa kwa kiingereza ni Knowledge brother, Ukijua Mungu amesema nini juu ya afya yako, na ukajua mungu ni mfalme na neno lake ndiyo sheria katika ufalme wake, magonjwa yanakosa nguvu ya kukushikilia. Ukisha elewa kilichoandikwa kwenye Mithali 3 sasa soma Zaburi 103:3-5. tafakari sana na pigia mistari, hakikisha kweli hii inaingia ndani ya Moyo wako. Endelea kutafuta neno la Mungu kuhusu Uponyaji na afya yako then mwambie roho mtakatifu akutakase, kwa kuwa biblia inaweka wazi kwamba tunatakaswa na roho kwa kuiamini kweli. tena imeandikwa, Utaijua kweli na hiyo kweli itakuweka huru. neno la Mungu juu ya afya yako ndiyo KWELI YOTE. forget what the doctors say, wanajua kidogo tu kile Mungu alichowajalia. wewe sema na aliyewapa hayo maarifa.
  Msingi wa afya yako unajengwa katika ufahamu ulionao kuhusu neno la Mungu. Jenga msingi wa afya yako kwenye neno. maombi ni kama Panadol, yatapooza ugonjwa wako leo, lakini usipojua kile mungu alichosema juu ya afya yako kesho unaweza ukaumwa tena. Jenga msingi wa afya yako katika neno, magonjwa yatakukimbia kabisa.
  Shetani anatumia kile usichojua kukutesa, ukisha jua anakosa nguvu ya kukutesa tena katika eneo hilo. jaza Moyo wako neno la Mungu kuhusu afya yako shetani hata kutesa tena na magonjwa.

  Ubarikiwe.

 4. Mungu ni mponyaji.sasa kanunue Kitabu kinaitwa hivi ( SIRI YA KUTUNZA MUUJIZA WAKO ) Kimeandikwa na Pastor NTEPA. kumbuka hili Luka 1:37 yeremia 32:27 Ndugu yangu Uzima ni haki yako.

 5. Kaka Lucas,pole sana kwa magonjwa hayo yanayokusumbua.Lakin nikupe hongera pia kwakuwa umetambua Mungu ni zaidi ya madaktari,hivyo anafanya na hashindwi.Kama inawezekana jitahid ufike pale Biafra kesho Jumapil jion,kuna mkutano wa injili unaoisha Jpili,fika pale viwanja vya Biafra na hakika utakutana na muujiza wako.Usikate tamaa MUNGU ni muweza na anaweza yote.Amen

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s