Nitajuaje kama Mungu amepokea kazi yangu?

Bwana Yesu asifiwe!
Mimi ni kijana mlutherani; kweli huwa napata shida moyoni wakati ninapokuwa naimba au kusali: Je? Nitajuaje kama Mungu amepokea kazi yangu? Kwa kweli huwa nakosa amani nikianza kufikiria kuhusu jambo hilo. Vile vile natamani sana niweze  kuhisi moyoni mwangu kwamba Bwana amenigusa. Nahitaji kusaidiwa.

Boniface.

Advertisements

6 thoughts on “Nitajuaje kama Mungu amepokea kazi yangu?

 1. kitu cha kwanza ni imani, biblia ina sema pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, na kila amwendeaye aamini kuwa yupo, Ebrania 11:6, na imani na aina hiyo huweza kuwa nayo pasipo kuwa umemwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Rumi 10:9-10, yapo mengi lakini zaidi hayo ni ya muhimu, By P. Mosile. Ubarikiwe.

 2. Ndugu yetu Boniface;
  Ni kweli kabisa hali na maswali uliyonayo iko kwa mamilioni ya “WAKRISTO” si kwako tu.

  Yesu alipokuwa na wanafunzi wake kuna baadhi ya maeneo aliwapa “ROHO MTAKATIFU”. Pia wakati akiaga aliwaambia “…mtapokea nguvu akiisha kuwajiliya Roho Mtakatifu…”.
  Kabla ya hapo, Bwana Yesu alimuelezea Roho mtakatifu kuwa; atatufundisha yote etc.
  Paulo anasema “…NDIYE ARABUNI” n.k.

  Tukichukua mstari huo mmoja wa 2Wakorintho 5:5 kwa kiingereza inasema “Now He who has prepared us for this very thing is God, who also has GIVEN US THE SPIRIT AS A GUARANTEE.
  Neno lingine nisingependa kuliacha ni 1Wakorintho 2:10-16.
  Mstari wa 11 unatoa msisitizo kuwa BILA KUWA NA ROHO WA MUNGU (ambaye ndiye Roho Mtakatifu) haiwezekani kuyajua ya Mungu na Warumi 8:14 inasema “…WANAOONGOZWA NA ROHO WA MUNGU HAO NDIO WANA WA MUNGU.”

  Sasa basi nini kifanyike?
  Kila anayemtaka au kumtafuta Mungu ni lazima awe na Roho wake. Roho wa Mungu anakuja ndani ya mtu kwa “kumsihi Mungu sawa na neno lake kuwa akupatie Roho wake ili kuunganishwa nae.

  Baada ya kumpata Roho mtakatifu, ukiomba unajua kama limekwenda au la, ukiwa popote au ukifanya chochote unakuwa nae na unakuwa na uhakika kwakuwa atakuelekeza kila kitu. Tunamuhitaji Roho wa Mungu kwa uhakika wa yote.

  Mbarikiwe!

 3. Shalom Boniface,
  maoni yangu ni haya, haijalishi wewe ni mlutheri ila ufuate neno na kulitenda. Unapoimba au kuabudu au kusifu ni kwamba unaongea na Mungu. Sasa ndipo tunapokuja kwenye suala la lugha. Nipo busy kidogo nitaweka mistari Mungu akijalia. Ktk Yohana Mt Yesu anasema Mungu ni roho, inatupasa kumwabudu ktk roho, anasema kuanzia muda wake Mungu anaabudiwa ktk roho na kweli sio majengo, madhehebu au sauti na nyimbo ni roho hivyo ujilulize je wewe unawasiliana vipi na Mungu au wewe unawaimbia watu wakusikie aua unamwimbia Mungu uongee naye?
  Pili ktk Yohana Mt Yesu anasema atatupa msaidizi ambaye atakaa nasi siku zote tofauti na Yeye anarudi kwa Baba….. lakini huyo msaidizi akiishakuja atawafundisha yote… huyu Roho Mt ni kiungo kati yetu na Mungu baba hivyo anatuwezesha kuwasiliana na Mungu moja kwa moja, ndipo utajua nini Mungu anasema na wewe, anapendezwa na nifanyacho au la, anakusudi gani na mimi ktk maisha yangu, anapendezwa na huduma au kazi yangu?
  Tatu ktk waraka wa Paulo kwa wakorintho anasema kuna namna mbalimbali za lugha, anaendelea kuwa anayehutubu yaani kuwaimbia au kuwahubiria watu anawajenga au analijenga kanisa, lakini anayeomba au kunena kwa lugha anajijenga binafsi kiroho, hivyo anasema tuombe kwa Mungu tuweze kunena kwa lugha na pili tuweze kuhutubu pia ili kuwajenga wengine.
  Nne ktk waraka kwa warumi Paulo anasema …sisi hatujui itupasavyo kuomba, lakini huyo Roho aliye ndani yetu anatuombea kwa baba namna impendezevyo… Hivyo naona ndg jitahidi sana kumwomba Mungu upokee Roho mtakatifu kama bado kisha jibidiishe kuomba ktk Roho ili uweze kusikia Mungu anasema nini na sio kusubiri nabii sijui kitabu kikutafsirie, pazia limeishapasuka ktk patakatifu kila mmoja anaweza kuingia na kuwa kuhani (kuongea na Mungu) mradi tu usimame ktk haki. Ni maoni yangu

 4. Maranatha!
  Wapendwa, tutoe kwanza kwa wahusika msaada ule wa kwanzakwanza, yaani wahakikishe wenyewe wamesimama katika mapenzi ya Mungu. Biblia ni moja, ila watu wamepotea ndani. Lazima kila mtu anayemfuata Kristo aitwe “MKRISTO” wala si “MLUTHERI”, asomaye na ajuwe maana yake (mwanafunzi/mfuasi wa Kristo ao wa Lutheri). Kuna mengine majina ya jinsi hiyo, inayoonyesha mtu ni mfuasi/mwanafunzi wa nani. Haya makundi ya kidini ndiyo inasababisha kusiwe na umoja kamili katika Kristo, sote tukifuata Neno hilo la Kristo (Yoh. 12:48).
  baadaye, tuwaonye njia kamili ya kumpendeza Mungu katika kuwa na moyo safi, imani safi, nia safi, … pamoja na wote wanaomuinua BWANA YESU KRISTO kama Mwokozi. Tusiwabembeleze watu kuwaambia eti hakuna ubaya kuweko na makundi ya madini na migawanyiko. Tukimwabudu Mungu katika roho na Kweli (Neno lake ndio Kweli), atayasikia maombi na haja zetu bila kutarajia atupe ripoti yoyote. Tuamini tu, hatuwa zingine atafanya.
  natoa comment hii kwa ufupi.

 5. BWAANA YESU asifiwe!
  Usiogope!nenda ktk maduka ya vitabu vya watumishi wa MUNGU uliza kitabu kinaitwa unaweza kumsikia MUNGU kimetungwa na mchungaji DEBORAH NTEPA ndani yake utapata jinsi ya wewe kujua jibu lako na utaweza kujua unamsikia MUNGU kwa jinsigani wewe mwenyewe na hutahuzunika tena!
  F.Marandu

 6. Bwana asifiwe ndugu Boniface

  Na shukuru sana kusoma swali lako.Mungu anakupenda sana kwa kweli DHAMIRI yako ndio inapokuongoza kwa IMANI yetu kwa YESU kama vile inapoandikwa katika warumi 1: 17 na HABAKUKI 2:4 na YOANI 3:36 na 2 WAKORITHO 5:7 na WAGALATIA 3:11 ndugu jaribu kosoma hii na Mungu atatafsiri ndani yako kupitia Roho Mtakatifu ndio anapotungoza kujuwa kama tuko na wasiliana na Mungu

  MFANO moja ndio hii kama uko na simu yako ya mkononi unaweza kuita ndugu fulani kama network iko sawa mnaelewana lakini kama network iko mbovu hakuna mawasiliano.unaweza kusema leo network iko mbaya

  Ndio pia kwa Mungu wetu tuwe na HAKI na kutumia KWELI na ndipo anapotusikiliza na kujibu maombi yetu wakati inapofaa na wakati isipofaa

  Ubarikiwe

  MONGA

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s