Ujana ndio muda wa kumtumikia Mungu na pia KUMJUA MUNGU – ELANDRE

Jina halisi anaitwa Emmanuel Andrew Mkumbwa,  Anajulikana na marafiki zake kwa jina la ELANDRE. Kwa wanaofahamu muziki wa Gospel Hip Hop, sio jina geni kwao kutokana na radha ya  sauti yake na ujumbe wa maneno anavyopangilia. Kwa sasa anasikika na wimbo wa ‘I am what I am’ aliyoifanya, Dreamers Park recording studios chini ya usimamizi wa Sam Mwangati wa CCC. Ambapo wimbo huu uliingizwa kwenye albam ya APRaW,  mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za waimbaji wa Injili.

ELANDRE, amekua akishirikishwa na waimbaji wengine wa miondoko hiyo kama Pona Hurst kwenye nyimbo ‘Justice Reign’ na ‘Watch Out’ pia Gee&Seth wimbo wa “This is my Year”, Nicky Urio au NABII nyimbo kama ‘Gospel Party’ na ‘Chapa Snare’ zilizo katika albam yake iitwayo Ladha ya Kinabii, Baltazari kwenye wimbo wa ‘Popote Yupo’ na Mac Elvis wa Uganda amemshirikisha kwenye wimbo wa ‘Church Boy’ wimbo uliomuinua katika chati za muziki wa Injili, nchini Uganda.

“Nilianza christian rap mwaka 2004 kutokana na kikundi cha maombi nlichokua nashiriki kilikua kinaitwa Youth Life Prayers (YLP); pia kutokana na profecy za watu juu yangu na jinsi Mungu atakavonitumia. Single yangu ya kwanza iliitwa ‘Praise the Lord’ inspired by the book of Psalms 150. Ilibamba sana kipindi kile. 2007 nikatoa single ya pili ambayo niliirekodi AM Records ndugu yanu mmoja anaitwa Casy ndo aliiproduce hii track iitwayo ‘KEEP MOVING’. Nayo ilifanya vizuri maana ilifungua milango mpaka ya airplay katika radio ya Praise Power. Hii track ndo ilisababisha mpaka international doors kufunguka. Mchungaji wangu Fred Okello alikuja na kikundi cha waGanda wanaitwa Soul 5..wakarudinayo Kampala. Baada ya hapo nikajulikana huko Uganda” anasema Elandre

Elandre yuko Lusaka, Zambia akirekodi albam ya yake ya kwanza ‘Goemmi Records’ chini ya producer TAZ, ambapo amepata mkataba wa kurekodi kutoka R.I.O.T  “Namshukuru sana Pastor Isaac wa Tehillah, Mungu amfungulie milango zaidi”

Anaendelea kusema “Ujana ndo muda wa kumtumikia Mungu na pia KUMJUA MUNGU. Unaweza ukawa unamtumikia lakini humjui na wala hakujui wewe, ndo maana mwisho wa dunia atawaambia wengi sikujui na wala sikuwahi kukujua na wataishia motoni. Mungu anakupenda sana, kaa nae, keti nae mchonge mambo ya maana na sio kupoteza mda na unnecessary business. Nimeokoka, na passion yangu iko kwa vijana, maana wanakua na ni nani ataelekeza the right direction kama sio sisi tulioijua kweli. Blessings, peace and love to you all”

…..Tunakutakia kila la heri na Mungu akuinue katika utumishi aliokuitia…..

4 thoughts on “Ujana ndio muda wa kumtumikia Mungu na pia KUMJUA MUNGU – ELANDRE

  1. Mawazo hayownimuhimu kwani vijana wengi wana sahau kwamba ndani ya kipindi cha ujana ndicho cha kumtumikia MUNGU.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s