Mstari unaoniliza Kuliko Yote katika Biblia – XIV

Kila ninaposoma mstari ule wa Luka 13:22 huwa ninamuona, mtu huyu aliyemuuliza Bwana Yesu kiasi cha watu wanaookolewa, kuwa alikuwa na busara. Aliuliza kutaka kujua idadi kama ikiwezeka asipoteze muda wake. Jibu alilopewa na Bwana ni: Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba kwa maana nawambia kuwa wengi watataka kuingia wasiweze. Ndio maana mstari huu hunifanya nilie kuliko mistari yote: Watu kutaka kuingia mbinguni lakini wasiweze! Hata Bwana Yesu aliwaambia wamama kuwa WASIMLILIE, bali wajililie wenyewe na watoto wao, kwa ajili ya yale yanayokuja mbele yao.

Luka 23:27-31 “Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata, na wanawake waliokuwa wakimuombolezea, Yesu akawageukia akawaambia, enyi binti za Yerusalem, msinililie mimi, bali jililieni ninyi wenyewe, na watoto wenu, kwa maana tazama siku zinakuja, watakaposema, heri walio tasa, heri matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha. Ndipo watapoanza kuiambia milima  tuangukieni, na vilima tufunikeni, kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwa katika mti mkavu?”

Mpendwa, maelezo hayo juu ni mazito kweli kweli, na marefu. Unatakiwa uyasome kwa utulivu na kutafakari, uelewe yana maana gani.

Msitari unaoniliza kuliko mistari yote katika Biblia, unanifanya nilie kwa ajili ya nafsi yangu na kwa ajili ya watoto wangu wote wa KIMWILI na KIROHO pia. Paulo alisema mahali fulani hivi: “Vitoto vyangu,, nawaonea utungu mpaka Kristo auimbike ndani yenu”

Hadi sasa tumeshaona sababu mbali mbali ambazo zitafanya wengi washindwe kuingia mbinguni wakati wanataka. Leo, katika sehemu ya Kumi na Nne (14) ya somo hili, tutaendelea kuona tena sababu nyingine:

19. WATAMALIZA  VIBAYA.

Mhubiri 7:8, ”Heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo wake” Hapo Biblia inatufundisha kabisa kuwa makini na namna tutakavyomaliza. Watu wengi wanafurahia mwanzo wa jambo lolote, bila kujali mwisho utakuwaje. Ndiyo maana Sulemani aliomba hivi: “Uniwezeshe nijue kuingia na kutoka”. Watu wengi hujali tu namna ya kuingia/kuanza, ila hawaangalii namna ya kutoka/kumaliza. Swali linakuja: Tutamalizaje safari tuliyoianza.?

Katika Zaburi 30:6-7 Daudi anasema hivi: “Nami nilipofanikiwa nalisema sitaondoshwa milele, nawe Bwana uliuficha uso wako nami nikaaibika”

Ndugu zangu watu wengi huwa tunaanza vizuri sana, tunakuwa na bidii kweli kweli. Mara tunapoanza kufanikiwa, hapo ndipo mambo yanaanza kuwa vingine; tunafikiri tumefika, hata wakati mwingine tunaridhika kabisa. Tunaweza kuangalia mwenendo wa Yusufu kama mfano wa kuigwa: Ysufu  alipokuwa nyumbani kwa Potifa, angeweza kudhani amefika, kuwa sasa mambo yamekuwa mazuri, akae ale anywe. Nakuambia kama angewaza hivyo ingekuwa rahisi kwake hata kuanguka dhambini na yule mama Potifa. Angefikiri kuwa sasa maisha yamemnyookea. Kumbe bado nyumbani kwa Potifa hakukuwa na chakula cha kuwatosha na ndugu zake; na hatujui kama alikuwa analipwa mshahara kwa kuwa alikuwa mtumishi tu wa ndani. Bado alikuwa na safari ndefu. Ndiyo maana akasema: Nifanyeje Dhambi Nimkose Mungu?

Hebu endelea na safari! Usijifikirie wewe tu, kama tulivyo wengi wetu leo: mtu ukiishajenga nyumba, ukanunua gari, unasema ‘sasa nini tena?’ Hebu nikukumbushe kuwa ndugu zako bado wako Misri, wanatakiwa kuja hapo ulipo ukawahudumie.

Tukisoma mistari katika 2Nyakati 26:1-15 tunaona jinsi mfalme Uzia alivyo fanikiwa, lakini  mwisho akafanya vitu vya ajabu na utaona yale yaliyomkuta, ni marefu kidogo sitayakopi ila soma ujionee. Lakini kwa ajili ya somo letu tutaangalia mstari wa 16 ili tuende pamoja:

“Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi BWANA, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa BWANA, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia”

Mfalme Uzia alipofanikiwa moyo wake uliinuka, akafanya mabaya: akaamua atoe kafara, kinyume cha utaratibu, wakati ilikuwa ni kazi ya makuhani. Lakini kwa kuwa yeye  alishafanikiwa hata hakuwaheshimu tena waliokuwa na jukumu la kufukizia.  Hivyo alimaliza vibaya:  alimaliza na ukoma, alimaliza na kutengwa!

Ndivyo ilivyo kwa wengi wetu: wanakuja makanisani, wengine hawana kitu, na kwa kuwa Mungu ni mwema, watumishi wa Mungu huomba, humlingana Mungu, na Mungu huitika na humbariki mtu huyo. Baada ya hapo huwaoni tena wakiendelea na Mungu. Wengine hurudi nyuma kabisa, hurudi hadi kufikia hatua kuvunja ndoa zao, wengine hurudi tena vilabuni. Ndugu yangu, inatisha!

Na kwa sababu hiyo, kupitia somo hili mimi naomba upokee angalizo ninalokupatia kutoka katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 8:11-18:

Mistari 11-14 inasema: Jihadhari usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake na sheria zake, ninazokuamuru leo. Angalia utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga  nyumba nzuri na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoogezeka, na kila kitu ulichonacho kitakapoongezeka, basi hapo moyo wako usiinuke ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa”

Mistari ya 15-18 inaendelea kusisitizia matemdo makuu ambayo BWANA, Mungu wetu, aliwatendea Wana wa Israel na kwa mfano wa hayo anatutendea nasi leo. Na anamalizia katika ule mstari wa 18 kwa kusema kuwa BWANA, Mungu wetu, ndiye atupaye nguvu ya kupata utajiri. Hivyo hatutakiwi kabisa kumsahau!

Mungu atusaidie! Maana najua atatubariki, kwa kuwa imeandikwa “Anatuwazia mawazo mema, kutupatia mema katika siku zetu za mwisho.”

Ee Mungu, tusaidie tumalize safari yetu vizuri! 

Mbarikiwe nyote mnapoendelea kuvipiga vita vizuri vya Imani.

Ndugu yenu Mch. Samuel Imori

Advertisements

6 thoughts on “Mstari unaoniliza Kuliko Yote katika Biblia – XIV

 1. mtumishi nafarijika sana na ninatiwa nguvu na uwepo wa Mungu katika huduma yako ila nashindwa kuelewa namna ya kupata mafundisho yako ya awali kwa mfano hili ni fundisho la 14 nitapata vp la 1mpaka la 13 MUngu akubariki sana

 2. Mungu atukuzwe milele.

  Ee Mungu tunakusihi utusaidie tuwe wadumifu katika kukupenda na kukutumikia mpaka mwisho wa safari yetu tukakuone na kufurahi nawe milele mbinguni. Amina.

  Asante sana rafiki kwa kutukumbusha hayo. Tusichoke ndugu zangu na tusonge mbele. Mungu kwetu ni msaada wakati wa shida na majaribu.

  Mungu ni kinga ya waadilifu.

 3. Mafundisho haya ni mazuri nimejifunza kuwa nakiwa kuulinda wokovu wangu na pia kuishi katika wokovu ili siku za mwisho niwe miongoni mwa watakaoingia

 4. Bwana asifiwe na apewe utukufu zake

  Mch Samuel Imori

  Kweli hapa umetufikisha mahali inatakika sisi Wakristu kwa somo la leo ata mimi nalia kwenye moyo Mungu anisaidiye nifike mwisho vizuri kwa safari yangu ya kwenda Mbinguni.zaidi mistari ya Kumbukumbu la Torati 8 : 18 mbele ya watu ndipo inanipa nguvu.Zaidi Mungu anipe nguvu ya kufata sheria zake na kutumia HAKI mbele zake na kusema KWELI kwa mambo yote kwa kila mutu pamoja na IMANI yangu kwa YESU KRISTU zaidi kama vile tunaposoma WAFILIPE 4 : 4-7

  FREE NETWORK yetu ni MAOMBI

  Ubarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s