TANZANIA IMEKATAA MASHARTI YA UINGEREZA YANAYOTAKA NCHI ZINAZOTAKA MISAADA YAKE ZIRUHUSU VITENDO VYA USHOGA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alitoa msimamo huo leo Jijini Dar es Salaam akisema huko ni kwenda kinyume na sheria na utamaduni wa nchi yetu inayotambua ndoa ya mme na mke kama kiini cha familia.

Membe alisema hayo alipokuwa akizungumzia mkutano wa Jumuia ya Madola uliofanyika wiki iliyopita Perth, Australia.

Alitoa msimamo huo kufuatia kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kuwa wana mpango wa kusitisha misaada kwa nchi ambazo katiba na sheria zake hazitambui mashoga na ndoa zao. “Nchi yetu inaheshimu sheria na utamaduni wake hivyo hatupo tayari nchi nyingine kutuwekea masharti kama hayo ya kuwa na uhusiano wa jinsi moja, hili ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano na nje”, Waziri Membe aliwaambia waandishi wa habari.

Alisema tamko hilo ni msimamo wa chama cha Conservative na kibaya zaidi linatoka Uingereza ambako ndio wenye Jumuia ya Madola hivyo linaweza kusababisha kuvunjika kwake na Cameroun na nchi hiyo ndio watawajibika jumuia hiyo ikivunjika.

Alisema miongoni mwa nchi 54 za Jumuia ya Madola kati yake nchi 13 ushoga ni sehemu ya katiba yao wakati 41 hazina utamaduni huo hivyo msimamo wa Tanzania ni kuwa na ndoa za jinsi mbili tofauti, kinyume na hapo unafungwa kifungo miaka 30.

Alisema kuendelea kukumbatia ushoga si jambo zuri na si la kulishabikia hata kidogo vinginevyo wanaweza kujuta nchi ikijihusisha na ushoga na kuukubali kupata misaada ya maendeleo.

 ”Tanzania hatuwezi kuyumbishwa kwa masharti ya kipuuzi bora tuitunze nchi yetu.

Tanzania ni nchi maskini lakini kamwe haturuhusu kuingiliwa na nchi nyingine.

Kama ndio hivyo basi wakae na hela zao,” alisema Waziri Membe wizarani kwake.

Alisema katika mkutano wa Madola, walijadili mabadiliko ya hali ya hewa ambapo walibainisha nchi zinazotegemea mvua zichukue hatua gani kuishi bila kuathiri hali hali ya hewa.

Pia alisema walijadili kuhusu hatua za kuchukua ili kuvisaidia visiwa vidogo kama Maldives vinavyoliwa na maji ya bahari yanayojaa kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa.

Alisema watakuwa na mkutano London Aprili mwakani kujadili mikakati hiyo.

Advertisements

25 thoughts on “TANZANIA IMEKATAA MASHARTI YA UINGEREZA YANAYOTAKA NCHI ZINAZOTAKA MISAADA YAKE ZIRUHUSU VITENDO VYA USHOGA

 1. Now we are going to our destiny when this mud things are allowed for sure we will be nothig but i believe the one who arranged this before will not allow to be reversed let us keep on preying.

 2. Pamoja na kwamba sina uhakika kama CHADEMA wanao uhusiano na chama cha Bwana Cameroon wa UK maana hata mimi nasikia hivyo, ila kusema ukweli hakuna chama ambacho hakina chama rafiki Ulaya au Urusi au China.

  Mtu aliyechomeka hoja hii katika mjadala huu wa ushoga alitaka tu kusababisha chuki dhidi ya CHADEMA ili watu waachane na mtazamo mzuri juu ya Chama hicho cha siasa. Mbona Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina urafiki na chama cha Kikomonisti cha Urusi na kile cha wachina ambavyo vinaamini kuwa HAKUNA MUNGU. Mbona watanzania hawakusema lolote. Je, tukisema kwamba taifa hili linapinga kuwepo Mungu kwa sababu ya kutawaliwa na CCM inayoshirikiana na vyama rafiki visivyoamini uwepo wa Mungu itakuwa sawa?

  Kwa nini mambo mengi watu huwa wanakimbilia kuitazama CHADEMA? Kukitokea mashoga kuandaa maandamano watasema kuna mkono wa CHADEMA. Kukitokea maandamano ya wamachinga Mbeya,na Mwanza wanasema kuna mkono wa CHADEMA.

  Bwana Cameroon na UK yake wanakuja na sera ya Ushoga watu wamesharukia kuisema CHADEMA. Kwa nini CHADEMA inapewa umaarufu usio na sababu?

  Hivi hamjui kwamba pamoja na kwamba tunapinga Uingereza isituwekee masharti ya ama kukubali HAKI za mashoga na ziwekwe katika sheria zetu au siyo tutakosa misaada, bado waingereza wataendelea kutuletea misaada iliyotolewa na MASHOGA?

  Kama Mashoga wa Uingereza wanatuletea misaada kupitia bajeti ya Serikali kama ambavyo tumesikia kuwa Uingereza imetoa msaada wa gharama za kufanya sensa mwaka 2012, na misaada hiyo tunaipokea, kuna haja gani sasa kukataa kuwatambua rasmi mashoga. Ukitaka usiwatambue mashoga, kataa na misaada yao.

  Mbona Tanzania tunaendelea kupokea misaada ya Uingereza ambao ni mashoga watupu (maana sheria yao imewatambua) huku tukiwakatalia masharti yao? HII NI ZERO POINT. HAKUNA MAANA YOYOTE.

  Mimi nasema hivi, BORA TUWATAMBUE MASHOGA KISHERIA KULIKO KUTOWATAMBUA KISHERIA HUKU TUKIENDELEA KUPOKEA MISAADA YAO KWA MAENDELEO YA TAIFA.

  Mzee Bernad Member naomba umshauri Waziri wa Sheria na Katiba Mama Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bwana Werema wapeleke Mswaada Bungeni wa kuwatambua mashoga haraka iwezekanavyo. LA SIVYO……. MISAADA YA UINGEREZA SERIKALI ISIIPOKEE TENA. AU TUJULIKANE KUWA TAIFA LOTE LA TANZANIA NI LA WANAFIKI WAKUBWA. (Nisamehe kama nimekuudhi).

  Nasubiri Mswaada Bungeni wa Kueleza adhabu kali watakazopewa Mashoga (Wafilaji na Wasagaji) watakaopbainika wakijihusisha na mambo yoyote yafananayo na ushoga .

  Au upeleke mswaada bungeni wa kuwabariki mashoga wote Tanzania na kuwakubali kuwa nao ni watu tena wenye pesa na yeyote atakayeonekana kuwapinga afungwe ili Tanzania iendelee kujipatia misaada ya Maendeleo kutoka kwa mashoga walioko Uingereza wanaolipa kodi kwa serikali hiyo.

  Nasubiri Mswaada kuhusu USHOGA, USODOMA, UGOMORA, UFIRAJI, USAGAJI na matusi kama hayo. (Samahani kwa wale ambao hayo ni maneno machafu). Lakini lazima sheria itungwe haraka ama IBARIKI au ILAANI VITENDO KAMA HIVYO, La sivyo, Taifa hili KWISHA MBALI.

  Tuendelee Kusubiri Mswaada. Time will tell the truth.

 3. Ndugu Kinyau Haggai,

  Nashukuru kwa jibu lako. Nimekuelewa!

  @Mpendwa John Haule,

  Ninavyofahamu mimi ni kuwa sheria zipo. Ndiyo maana hata waziri alibainisha hata adhabu ya kosa hilo kwa Tanzania kutokana na sheria iliyopo. Hivyo mi naona tatizo si uwepo wa sheria bali HATUNA TEKELEZAJI WA MAMBO TUNAYOYAPANGA!

  Ni jambo la kusikitisha kuwa pamoja na sheria hiyo kuwepo lakini sidhani kama kuna mhusika ye yote anaweza kutaja wangapi walishafungwa kifungo hicho kwa kubainika na kosa hilo. Watanzania ni wasikilizaji tu wa neno na wala si watendaji. Maazimio ni mengi mno lakini utekelezaji hakuna!

  Mi huwa sipati jibu: Kwa nini hatuna utekelezaji wa kuridhisha katika mamb tunayokubaliana? Kama sheria ipo na wavunjaji wa sheria hiyo wapo, SASA KWA NINI HAWASHITAKIWI, Kwa nini mkondo huo unakuwa mgumu kwa sheria hiyo kuufuata? Au ndiyo yale yale ya Yesu alipowaambia wale Jamaa kuwa “asiye na dhambi awe wa kwanza kumrushia mawe” yule mama waliyesema wamemkamata anazini?

  Je, hatuna kiongozi safi Tanzania wa kutekeleza sheria zilizoko against uhalifu wa maadili na uovu?

  Sijuwi ni kwa nini: Yaani baada ya Cameron kutoa sharti hilo utafikiri imekuwa kama vile YEYE NDIYE ANATAKA KUWALETA MASHOGA NCHINI KWA MARA YA KWANZA. Mbona wapo tu! Kwa nini TGNP walipofanya kampeni za kutambua haki za ushoga waTz wote, almost wote yaani, tulikuwa kimya?

  Ndg Kinyau ameeleza kuwa KKKT, Dodoma walitoa tamko kukataa mambo hayo. Lakini 2009 hadi sasa ni kipindi kirefu. Mi nashauri badala ya kutoa tamko na kukaa kimya, Viongoi wa kiroho wanatakiwa kuendelea kuelimisha jamii. Ibabidi hata ikiwezekana wakaununua kurasa kwenye magazeti na vipindi kwenye TV na Redio ambavyo vitakuwa vinatoa msimamamo na kuelimisha umma wa waTz kuhusiana na mambo kama hayo. Panatakiwa kuwa na jitihada endelevu, zinazovuka milango na kuta za majengo ya makanisa na kuingia mitaani na angani ili watu wasikie, waelimike.

  Siyo jambo zuri kabisa kwa viongozi wa kiroho kushupalia jambo baada ya kuona serikali nayo inalipinga. Wanatakiwa watangulie mbele na serikali ifuate. Siyo serikali ianze ndio nao wafuate. Wakati mwingine wanatakiwa kuwa KINYUME NA SERIKALI juu ya mambo fulani na msimamo huo udumu.

  Najua nchi haiogozwi kidini lakini angalau inaweza kuongozwa kwa utamaduni na maadili ya kitanzania, kama bado yapo! Na mambo hayo yanavuka mipaka ya dini na kuwakutanisha watanzania na utanzania wao!

  Najiuliza sana: Ni nani aliyeturoga watanzania hata TUNASHINDWA kusimamia mambo yetu wenyewe?

  Sasa, kinachouma zaidi ni pale unapofika katika kanisa fulani, watu wananung’unika kuhusu utovu wa nidhamu wa kiongozi wao lakini HAKUNA WA KUCHUKUA HATUA. Watu wanabaki na manung’uniko moyoni na kiongozi wao anaendelea na kutokuwa na nidhamu!

  Sasa kama hadi makasani hatuwezi kuwekana wazi kuhusu HAKI na KWELI, inawezekanaje huko serikalini ambako kwa viongozi wengi hata hofu ya Mungu hakuna?

  Nimalizie kwa kunukuu maneno toka mpendwa John Haule, ambayo mimi yamenigusa sana:

  “Tunahitaji kusimama pale palipo bomoka tukianza kutoa kibanzi kwenye nyumba ya BWANA. Ambayo imenajisika .Tuombe Toba ya utakaso wa Damu ya Yesu natumlilie Bwana kwa machozi ili tupate Rehema, Mungu Atupe Neema na kuwa na kibali(HAKI) mbele zake ili kukemea hii roho bila sisi (Kanisa)kunyoshewa kidole
  CAMERON AMETUONYESHA KUWA HII ROHO INATENDA KAZI KATIKATI YETU NA SASA INADAI HAKI..

  YATUPASA TUKIOSHE KIKOMBE NJE NA NDANI”

 4. Ndugu Wapendwa ktk Bwana wetu Kristo Yesu.
  Nafahamu kwa Sehemu kuwa vyama vya Upinzani kati ya Nchi na Nchi vinakuwa na Uhusiano/ushirikiano/muungano wa vyama vyao vya upinzani na hata kupeana misaada mbalimbali.Chama cha Cameroon kilikuwa cha upinzani Nchini Uingereza kwa muda mrefu,kwa hiyo si jambo la kushangaza Chadema kuwa na uhusiano naye Cameroon na chama chake,Mpendwa Haggai umeona ni hatari Chadema kuwa na uhusiano na Cameroon na wala hauoni hatari Tanzania kuwa na uhusiano na Cameroon na Serikali yake mpaka anafikia kutuambia tutambue haki ya ndoa ya jinsia moja la sivyo hatutapewa msaada na bado hatujavunja uhusiana naye.Nchini Uingereza ushoga unatambulikana na chama cha Cameroon tu?!!!!!!na vyama vingine Uingereza havitambui ndoa ya jinsia moja?!!!!.Hii mimi inanipa shida kidogo kwamba Je?Tanzania hatujitambui kuwa tuna mashoga mpaka serikari ya Uingereza inatupa masharti ya msaada au tunatambua ila uwepo wao Kisheria ndio shida kwetu!!!!!!

  (Tunaona Yesu akikemea UNAFIKI wa Kifarisayo mara13 kwenye Injili ya Mathayo).
  Tuache UNAFIKI,Sote tunafahamu kuwa ushoga kwetu hapa Tanzania umeshamiri kupita kiasi,Tumesikia hata kuona baadhi ya wachunga kondoo wa Bwana wakifanya/kufanyiwa ushoga na hata wenngine kushitakiwa mahakamani,Mengine bora usiyasikie kwani utanajisika bure na kukwazwa hasa utakapotambua kuwa kiongozi wako ktk Serikari au Imani uliye mwamini ni mteja anafanya au kufanyiwa matendo hayo ya Ushoga,Tumepata sikia ndoa ngapi za mashoga zikifungwa hapa Tanzania na wala hakuna anayekemea,Wapendwa Tunahitaji kusimama pale palipo bomoka tukianza kutoa kibanzi kwenye nyumba ya BWANA. Ambayo imenajisika .Tuombe Toba ya utakaso wa Damu ya Yesu natumlilie Bwana kwa machozi ili tupate Rehema, Mungu Atupe Neema na kuwa na kibali(HAKI) mbele zake ili kukemea hii roho bila sisi (Kanisa)kunyoshewa kidole
  CAMEROON AMETUONYESHA KUWA HII ROHO INATENDA KAZI KATIKATI YETU NA SASA INADAI HAKI..

  YATUPASA TUKIOSHE KIKOMBE NJE NA NDANI.

  Amani ya Mungu Baba iwe nanyi,
  Amen

 5. Ndugu John,
  Ahsante kwa uliyoyasema kuhusu yale niliyodhani kuwa jamii yetu sasa ichukue hatua ya kuonyesha kwa vitendo kwamba tunachkizwa na tabia hii ya ushoga.

  Kuhusu chanzo cha habari ya urafiki wa Chadema na chama cha Bw. Cameroon, kama ambavyo niliandika kuwa sina uhakika na hilo, ndio sababu nikapenda mwenye uhakika nalo, basi atueleze na ikiwezekana tuwaulize viongozi wetu wa Chadema wana msimamo gani kuhusiana na kauli ya Bw. Cameroon. Kwa hiyo sina chanzo hasa cha uhakika ambacho naweza kukiamini, ni maneno yanayosemwa mitaani, ambayo kwangu mimi sio chanzo cha kuaminika ndio sababu nikaomba mwenye uhakika na hilo alisema kwamba ni kweli au sio kweli.

  Kingine kilichonisukuma kusema hivyo ni ukimya wa viongozi wetu wa Chadema juu ya kauli ya huyu Waziri Mkuu wa Uingereza (niombe msamaha mapema kama wamesema nami nimepitiwa sikusikia au kusoma kwenye media yoyote).

  Vyama vinapokuwa rafiki, mara nyingi (sio mara zote) hushauriana na kupeana sera na kusaidiana kifedha, hivyo nilipenda kujua kwa hakika msimamo wa viongozi wa Chadema kuhusiana na masharti haya ya Bwana Cameroun maana yanaweza yasiwe kwa nchi tu zinazosaidiwa na Uingereza, badala yake swala hili likaenda mpaka kwenye vyama rafiki na asasi zingine za kiraia na madhara yake yatakuwa kwetu sote.

  Kwa kuuliza hivyo ndg yangu John sikuwa na chanzo cha uhakika juu ya hili, la sivyo nisingeomba mwenye ukweli atueleze.

  Baraka kwako.

 6. Ndugu Kinyau Haggai,

  Nakumbuka kwenye miaka ya 80, kule maeneo ya usukumani vivijijini kulikuwa na tiba ya wenye matatizo kwenye jamii ya KUWATENGA. Mtu anatengwa, yaani inabidi hadi kisima cha kuchotea maji atafute kingine maana hafai kabisa katika jamii. Hiyo ilikuwa inasaidia maana watu walikuwa wanaogopa kufanya maovu kwa kuogopwa atatengwa. Kilichoharibu ni huku kuvunjwa kwa tamaduni nzuri zilizokuwa zinasaidia kutunza maadili katika jamii.

  Kwa hiyo idea yako ya kuzomea, mi naona inaweza kufanya kazi!

  Pamoja na kuandika hayo ninaomba kufahamu CHANZO cha habari zinazohusu urafiki wa CHADEMA na chama cha Cameron. Sasa hivi nchi inapita pabaya kisiasa. Tunahitaji KWELI na HAKI illi tuvuke salama mahali hapa!

  NItashukuru nikipata chanzo hicho cha habari!

 7. Wapendwa,
  Hakika hii ni hatari!!
  Nimepata habari ambazo sina uhakika nazo, naomba mwenye uhakika atueleze hapa, kwamba chama cha huyu bw. Cameroon ni chama rafiki na chama kimojawapo cha siasa hapa nchini, yaani Chadema!

  Lakini hilo sio muhimu sana, la muhimu ni je msimamo wa viongozi wa Chadema ni nini kuhusu hili kama kweli ni vyama rafiki?

  Pamoja na mwandishi kuonyesha wasiwasi wake kuhusu matamshi ya Waziri Membe, lakini kwangu mimi naona ni hatua moja mbele katika kupinga swala hili. Nakumbuka kanisa la Kilutheri (KKKT) lilishawahi kutoa tamko kali sana juu ya swala hili mwaka 2009 huko Dodoma, lakini sijasikia makanisa mengine yakitoa tamko lolote, labda kwa sababu yamehusishwa na ushoga huko Ulaya na Amerika.

  Shida inakuja kwa jamii kwa ujumla wake. Hawa mashoga hawadondoki toka hewani, ni watu tunaoishi nao humu humu mitaani mwetu, na inawezekana kabisa ni ndugu na marafiki zetu lakini tunawafumbia macho na wakati mwingine watu na akilini zao wanaushabikia ushoga. Mimi nataka jamii tuchukue hatua kubwa zaidi ya kuwakataa mashoga kuishi kwenye jamii yetu, tuwanyanyapae kwa kila hali mpaka hapo watakapoacha tabia hiyo mbaya. Najua wengine watasema kuwa haisaidii kufanya hivyo, lakini angalau kila anayejulikana kuwa ni shoga akizomewa kila anapopita mitaani, inaweza kumfanya akaacha vitendo hivyo vichafu!!

  Ukifanya utafiti utaona kwamba wanaoendekeza mambo hayo ni watu wenye heshima zao na wana nguvu ya pesa. Haitasaidia sana kama tukikataa kutunga sheria ya kutambua haki zao, wakati vitendo vyao vinaendelea kushamiri siku kwa siku kwenye jamii zetu. Tuwakatae wao na vitendo vyao viovu.

  Mungu na atuepushe na balaa hilo la Sodoma na Gomora.

 8. Nimependa maneno yafuatayo toka Gazeti la Tanzania Daima, yaliwa yameandikwa na Happiness Katabazi na nikaona niyaweke hapa ili kuendeleza mjadala huu:

  “WATANZANIA TUACHE UNAFIKI

  WIKI iliyopita Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alihutubia mkutano wa marais wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Australia.
  Imeripotiwa kuwa katika mkutano huo Cameron aliwahutubia viongozi hao mambo mengi likiwamo agizo la kuzitaka nchi za Afrika kwenda kutunga sheria itakayoruhusu ndoa za jinsia moja, la sivyo nchi yake itazinyima misaada.
  Baada ya kuripotiwa na vyombo vya habari kuhusu agizo hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alijitokeza na kutoa tamko kwa niaba ya serikali kuhusu agizo hilo.
  Membe alisema serikali haitatekeleza agizo hilo kwa sababu si utamaduni wetu na kwamba heri Watanzania wafe maskini kuliko kutunga sheria hiyo.
  Ieleweke wazi kuwa hadi sasa sheria na Katiba ya Tanzania haitambui ndoa za jinsia moja.
  Licha ya vitendo vya ushoga na usagaji kuzidi kushika kasi kila kukicha, huku baadhi viongozi wa serikali, dini na wananchi wakifahamu kuhusu hilo wamekuwa wakilifumbia macho.
  Lakini leo hii Cameron ametoa agizo hilo mbele ya marais wetu, ndipo serikali, wananchi na viongozi wa dini wanaibuka na kutoa tamko la kupinga utekelezwaji wake.
  Nakubaliana na matakwa ya Ibara 18(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inampa uhuru kila mwananchi kutoa maoni na kutoa fikra zake, lakini huu ni unafiki wa kujitokeza kupinga agizo hilo wakati tayari kuna baadhi ya Watanzania wamekwishakubuhu kwa vitendo hivyo.
  Inaelezwa hata baadhi ya wanaume waliofunga ndoa huamua kuwasaliti wake zao na kuwatafuta mashoga kwa siri ili wawapatie huduma ya ngono.
  Hapa nchini, hususan jijini Dar es Salaam, zile sherehe maalumu za kumfunda bibi harusi mtarajiwa (Kitchen Party), ni kawaida kabisa kuwakuta mashoga wakicheza muziki wakiwa wametamalaki na ‘kujishebedua’ bila wasiwasi.
  Kitchen Party nyingi siku hizi mashoga hukodishwa kwa ajili ya kuja kusasambua sanduku analotuzwa bibi harusi mtarajiwa na kucheza muziki wa mwambao ili kuchangamsha sherehe.
  Lakini wakati mashoga hao wakiwa wanafanya vitendo hivyo, wazazi wa bibi harusi mtarajiwa na ndugu wa mwanamume ambao mtoto wao wa kiume siku chache zijazo hutarajia kumuoa bibi harusi huyo, nao huwa wanakuwepo ukumbini na kushuhudia hali hiyo na wala hawakemei au kususia sherehe hizo, ndiyo huwa wa kwanza kuwatuza fedha mashoga hao.
  Kwa muktadha huo hapo juu, sioni sababu ya kupinga utekelezwaji wa agizo la Uingereza licha ya tayari serikali yangu imetoa tamko la kulipinga.
  Hakuna ubishi kwamba Tanzania licha ya kuwa na utajiri mkubwa, taifa letu limeamua kuwa tegemezi kwa nchi zilizoendelea.
  Na si tu serikali yetu imeamua kuwa tegemezi pia hata vyama vya siasa navyo vimegeuka kuwa ombaomba ‘Matonya’ kwa wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi au vyama vya siasa vya nchi zilizoendelea kikiwamo cha Conservative cha huyo Cameroon na vimekuwa vikipatiwa misaada ya kifedha, mafunzo na vifaa mbalimbali.
  Ukizigeukia hizo taasisi binafsi zinazojiita taasisi za wanaharakati uchwara ambazo kila kukicha zimekuwa zikiishutumu bajeti ya serikali kutegemea wafadhili, wakati kumbe taasisi hizo nazo zinaendeshwa kwa kutegemea fedha hizo hizo za wafadhili.
  Tumuulize Membe, ni kwanini asingepinga agizo hilo pale pale wakati swahiba wetu Cameron anaongea kule Australia?
  Membe kasubiri amefika hapa nchini ndipo anatoa tamko la kupinga agizo hilo?
  Binafsi nazifahamu fika hulka za wanasiasa wa Tanzania, wengi wao ni wanafiki, kwani wanachokisema hadharani si wanachokifiria wala kukitenda.
  Ieleweke wazi ule mshikamano na umoja wa kweli wa nchi za Jumuiya ya Afrika haupo tena, kila nchi inaangalia masilahi yake kwanza, tofauti na awali.
  Hivyo katika utekelezwaji wa agizo hilo mwisho wa siku msije mkashangaa nchi nyingine za Afrika ikiwamo Tanzania zikaridhia kwa madai kwamba wanaogopa kunyimwa misaada.
  Wanasiasa kama mnakataa sheria hiyo isitungwe hapa nchini basi hata wakati wa uchaguzi mkatae kupigiwa kura za ndiyo na hao mashoga na wasagaji.
  Katika mawazo yangu, nitabaki nikiamini kuwa David Cameroon hakutoa agizo lile kwa bahati mbaya ndani ya mkutano ule maana hatukuona hata rais yeyote ndani ya mkutano ule aliyejitutumua kunyosha kidole kupinga agizo hilo la bwana mkubwa ‘Cameroon’, ambaye nchi yake imekuwa ikitupatia misaada kila wakati kulipinga.
  Nimalizie kwa kuwataka Watanzania watambue misemo hii: “Maskini hana kiapo, hakuna bingwa wa shida na ukijua kupokea, ujue na kutoa.”
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika”

  Baada ya kusoma maneno hayo mimi nilijuiliza maswali machache yafuatayo:

  Je, Kanisa la Tanzania linafahamu uwepo wa jambo hili katika jamii yetu?
  Na kama jambo hili linafahamika, kanisa limeshachukua hatua gani kabla ya tangazo la wazi wazi la waziri mkuu wa Uingereza?

 9. Wapendwa Ndg Lwitiko na Millinga, Nashukuruni kwa pongezi zenu. Lakini katika yote sifa na utukufu vitabaki kuwa ni vya Mungu.

  Kwa ndugu Milinga, nilipotoa mfano wa harakati za Beijing sikuwa na maana yoyote ya kuingiza suala hilo katika mjadala huu bali nilitoa mfano tu wa kuonyesha jinsi hicho kinavyoitwa UTAMADUNI kinaweza kubadilika wakati wowote, bila kujali mabadiliko hayo ni hasi au ni chanya! Lakini kwa kutambua uwepo wa hayo uliyoyaandika kuhusu mila potofu Ndiyo maana nikaweka na upande wa pili wa maoni yangu nilipoandika kuwa “nakubaliana kuna mambo yanayokandamiza haki fulani kwa wanawake…..”.

  Sasa kwa kuwa hapa si mahali pa mjadala wa harakati za kumkomboa mwanamke toka mila potofu, sitakuwa na mengi ya kuandika.

  Naona hapa tuachie tu mada hii ya ushoga iendelee……

  Nakushukuru kwa changamoto hiyo!

 10. Mpedndwa John Paul

  Umenena vyema mambo mengi katika maoni yako. Yote nimeyakubali kwa mtazamo wangu yako sawa kama alivyokupongeza ndugu yetu Lwitiko Kitule hapo juu.

  Hata hivyo kuhusu swala la Beijing na Usawa wa mwanamume na Mwanamke napenda kutokukubaliana na wewe ulivyosema, nanukuu, “Kuna mambo ya Beijing, ndoa hazikaliki tena maana mke anataka kuwa sawa na mwanaume, jambo ambalo si utamaduni mwa Mtanzania kwa asili……”

  Maelezo haya huenda yakapotosha maana ya harakati za Beijing zilizoanza miaka zaidi ya 15 iliyopita. Neno ambalo nadhani ndg Paul hakuonekana kuliweka sawa ni, “mke anataka kuwa sawa na mwanaume”… Ukweli ni kwamba harakati za usawa wa Jinsia hazilengi kumfanya mwanamke kuwa sawa na Mwanamume kama ambavyo wapendwa wengi makanisani huonekana kutaka lieleweke hivyo.

  Usawa wa Kijinsia unaopiganiwa na wanaharakati wengi haupaswi kuingizwa katika mjadala huu wa ushoga. Usawa wa Kijinsia unaopiganiwa mimi nauunga mkono kwani unakubaliana na maandiko matakatifu yasemapo, “…..Mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi….” na sehemu nyingine maandiko yanasema, “….Mungu akawabariki na kuwaweka bustani ya Edeni ili wailime na kuitiisha nchi na kutawala viumbe vyote wa angani, majini na nchi kavu…..” Harakati za Usawa wa kijinsia unajikita hapo kwamba wanaume na wanawake wote waweze kupewa fursa sawa ya kufurahia mema ya nchi waliyopewa na Mungu bila ubaguzi wa JINSI. Kwamba Mungu alimuumba mwanamke na mwanamume na akawapa amri ya kutawala viumbe wote. Adam alipewa haki hiyo sawia na Hawa pia.

  USAWA unaotetewa na wanaharakati siyo wa kumbadirisha mwanamume awe na maumbile sawa na ya mwanamke. Ukweli ni kwamba Mwanamke HATABADILIKA MAUMBILE YAKE MILELE HALI KADHALIKA MWANAMUME.

  Maumbile tu ndiyo yanayotutofautisha kuwa mwanamke au mwanamume na wala siyo majukumu ya kijamii tuyafanyayo kila siku.

  Watu wote tunapaswa ku..enjoy… mema ya nchi bila kubagua mwanamke au mwanamume. Kwa mfano mila nyingine zinataka mwanamke asiruhisiwe kufanya kazi za kuajiriwa, mwanamke asiende shule, mwanamke asile nyama kama vile maini, au steki, mwanamke asitoke ndani ya nyumba ashinde chumbani kila siku, mwanamke asipewe nafasi ya kuongoza kanisani au popote au kupewa cheo kama cha Urais, Uaskofu, Uchungaji, nk, mwanamke asiongee mbele ya watu akae kimya tu, mwanamke asifanye lolote la kumuinua kiuchumi, hizi ndizo mila potofu zinazopingana na maandiko yanayotaka tule mema ya nchi wote bila kubaguana. Harakati za kumkomboa mwanamke zinalenga katika hayo.

  Wanaume wengi hasa Wakristo wenzangu wanadhani kuwa hizi harakati ni za kumfanya mwanamke awe sawa na mwanamume SIYO KWELI KABISA. Harakati zote zinalenga kumkumbusha mwanamume kwamba wote tuko sawa mbele za Mungu na tunapaswa kupata fursa sawa za kuinjoyi mema ya nchi bila kujali ni mwanamke au mwanaume.

  Wengi hufikiri kwamba Mungu aliposema Eva atakuwa msaidizi wa Adam ilimaanisha kwamba Eva alipaswa kufanya kazi ndogondogo za nyumbani kama vile kulea watoto, kuwaogesha, kupika, kufua nguo, kuosha masahani, kupiga deki nyumba, kufagia, kutafuta kuni na kazi kama hizo. Lakini ukweli ni kwamba Mwanamume na mwanamke wote wanapaswa kufanya kazi hizi bila kujali JINSI. Hata kama mwanamke ni msaidizi kwa tafsiri hiyo, basi kazi hizi zilipaswa kuwa za mwanaume na mwanamke akizifanya azifanye kama kutoa msaada tu kwa mume wake hasa pale mume anapozidiwa na kazi ndipo mke amsaidie. Vinginevyo mke hapaswi kufanya kazi yoyote zaidi ya KUBEBA MIMBA NA KUZAA NA KISHA MUME ALEEE WATOTO AKISHINDWA NDIPO MKE AMSAIDIE.

  Katika mjadala huu swala la harakati za usawa wa kijinsia zisichanganywe kabisa katika kuukataa au kuukubali ushoga.

  MWANAMKE NA MWANAUME WOTE NI SAWA KATIKA KRISTO ILA HAWANA MAUMBILE SAWA YA UZAZI TU. MAUNGO YA UZAZI NDIYO PEKEE HUTOFAUTISHA MKE AU MUME NA WALA SIYO MAJUKUMU.

 11. ubarkiwe Ndugu John umenena na kuongea katika hekima yote ya Mungu, sifa na heshima kwa Mungu wako anayekuongoza kunena kwa hekima kiasi hiki,

 12. Mambo ya kujadili hapa ni mengi sana!

  Kwanza kabisa, sababu iliyotolewa ya kukataa sharti hilo kuwa ni kuheshimu utamaduni wa Tz ni DHAIFU mno kwa kuwa UTAMADUNI UNABADILIKA. Sina uhakika kama waziri au mtz mwingine ye yote anaweza kutaja utamaduni wa Mtz ambao haujabadilika tangu Tanzania iwe taifa! Kuna mambo ya Beijing, ndoa hazikaliki tena maana mke anataka kuwa sawa na mwanaume, jambo ambalo si utamaduni mwa Mtanzania kwa asili, lakini kwa sababu ya mbinyo wa kiuchumi,kama alivyosema ndugu Millinga, suala hili limeingizwa na moto wake unawaka sana. [nakubaliana kuna mambo ambayo hanakandamiza haki fulani kwa wanawake, lakini ufumbuzi si kwamba mwanamke awe na haki sawa kama mwanaume bali kila mmoja apate haki zetu zinazomstahili. Kuna haki tofauti katia ya mwanamke na mwanaume na zikizingatiwa kwa utofauti huo ndipo tunapata haja ya kuunganishwa mwanamke na mwanamume ili kufanya ndoa].

  Nikiendelea na mada iliyopo, Mimi ningemuona Waziri membe kuwa hoja yake ina nguvu kama angesema kwa sababu TANZANIA INAMCHA MUNGU. [Labda kama haikunukuliwa hapa].

  Katika kupinga suala hili pia watu mbali mbali wamesikika/wamesomeka wakikemea na kupinga suala hili kwa nguvu zao (zote) walizonazo. [Lakini hata swala akutanapo na simba/chui hujitahidi kupambana kwa nguvu zake zote, lakini kwa huwa hakuna msaada maana mwisho wa nguvu zake ndiyo mwanzo tu wa nguvu za simba!]. Katika hao waliosomeka yuko Mwanaharakati kutoka Kikundi cha Kijamii cha Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu, Washabu, Chrispine Nabigambo, aliyesema hivi:

  “Jamii ya watu wa Wilaya ya Ukerewe ni wacha Mungu hawawezi kukubaliana na uhalalishaji wa ushoga nchini. Hata suala la utakasaji (mwanamke aliyefiwa na mumewe kufanya ngono na mwanamme atakayechaguliwa na wanandugu) linapigwa marufuku na jamii ya watu wa Ukerewe, jambo ambalo linaashiria kuwa ushoga hawatakubaliana nao,”

  Mwanaharakati huyo ametumia nguvu zake zote alizonazo katika kupinga jambo hili. Lakini kwa msuli mdogo sana maana nguvu yake iko katika uimara wa jamii ya wakerewe! Lakini jamii ya ukerewe ni nini linapokuja suala la “kutimia nabii za Biblia na mabadiliko ya tamaduni duniani?

  Tamaduni zinabadilika kutokana na maendeleo na ustaarabu na elimu vinavyobadilika siku hadi siku, mwaka hadi mwaka. Ni jambo moja tu ambalo halibadiliki: MUNGU. Mungu habadiliki na wala kanuni za kumcha Yeye nazo hazibadiliki! Hii ndiyo sababu inayoweza kutupatia matumaini ya msimamo huu kuendelea kuwepo lakini si UTAMADUNI!

  Waziri membe akiongea kuhusu jambi hilo alisema kuwa “sheria ya mwaka 1971 iko wazi kuwa Tanzania inakataza ndoa za jinsia moja hivyo Uingereza isitake kuilazimisha kuivunja kwa kuwa hatua hiyo inaweza kuleta mifarakano.”

  Hayo ni maneno ambayo hayaonyeshi tumaini lolote la kutokubadilishwa kwa sheria hiyo. Si ajabu sasa ikaja sheria ya 2014 ambayo itaruhusu ndoa za jinsi moja. Ni nani ajuaye mambo ya haki za binadamu yanaweza kuingia katika suala hili?

  Naye waziri wa Katiba na Sheria akiongea kuhusu suala hili alisema:

  “Kwa utamaduni wetu hilo halipo na haiwezekani tukawa na sheria ya namna hiyo, sheria zote za nchi yetu zinatungwa na Watanzania wenyewe na mimi kama Waziri wa Katiba na Sheria nimesema hatuna mpango wa kuwa na sheria ya kutambua mashoga wala hatufikirii kuwa nayo kwa sababu sio utamaduni wetu,” alisema Kombani.

  Alisisitiza: “Nasema haiwezekani tukawa na sheria ya namna hiyo.”

  Yale yaleeee!

  Msingi wa KATIBA YA NCHI linakoegemezwa jambo hili si IMARA, maana unaweza badilika wakati wowote!

  Lakini pia ni MAOVU mangapi ambayo YAMERUHUSIWA Tanzania? Hivi watu wanaiba kwa sababu wizi umeruhusiwa, au uzinzi unaoendelea nchini, ni kwa sabb umeruhusiwa? Ufisadi na uporaji wa mali za umma [unaofanywa na viongozi] umeruhusiwa? Ni maovu mengi sana yanayofanyika japo hayajaruhusiwa.

  Kutokana na sheria za Tz, kosa la kuwa katika ndoa ya jinsi moja ni kifungo cha miaka 30. Lakini je, ni wangapi ambao wameshafungwa kwa kosa hili? Au ina maana Tz hakuna mashoga? Na kama wapo, Je! wanafanya hivyo kwa kuwa serikali imeruhusu?

  Ingawa jambo hili si kosa katika nchi hizo 13, siamini kuwa WATU WOTE humo wanaishi katika ndoa ya jinsi moja. Hapana! KURUHUSU siyo KULAZIMISHA. Hivyo pamoja na kuruhusiwa jambo hilo lakini mtu HALAZIMIKI kufanya hivyo. Katika nchi ambazo suala hilo si kosa kisheria wako watakatifu wengi tu, wakiendelea usiku na mchana kumtafuta Mungu, maadam anapatikana!

  Uhuru wa mtu kuchangua afuate nini unabakia pale pale. Na mimi naamini ili mtu apimwe kuwa SI MWIZI ni pale atakapowekwa mahali ambapo KUNA VITU VINGI VINAVYOWEZA KUIBWA. Huwezi kumjua kama mtu ni mwizi kwa kumuweka mahali ambapo HAKUNA HATA KITU KIMOJA KINACHOWEZA KUIBWA. Hata shujaa wa vita hujulikana baada ya kutoka vitani na wala siyo yule ambaye hajapigana kabisa vita yoyote..

  Hivyo maisha ya kumcha Mungu yanatakiwa yaendelee tu pasipo kujali Serikali za kibinadamu zimehalalisha au hazijahalalisha dhambi zipi. Binadamu kuhalalisha dhambi fulani hakutakiwi kumvuruge imani mcha Mungu. Hapo ndipo panapotakiwa kuwa kipimo cha NINI MTU ANAKITII kati ya Mungu na Wanadamu. Kwa hali ya kawaida, mcha Mungu anapaswa kumtii Mungu kuliko wanadamu!

  Enzi za watakatifu wa zamani, Daniel na wenzake, wao WALILAZIMISHWA kuabudu sanamu. Ilikuwa imevuka kutoka RUHUSA na ikawa LAZIMA. Kilikuwa kipimo kikubwa na kikali sana. Lakini hapo ndipo msimamo wao ulipoonekana. Walisimama na Mungu hadi kikaeleweka! na jina la BWANA Mungu likatukuzwa!

  Sisi Je, tutasimamaje katika kizazi hiki ili Mungu atukuzwe kupitia msimamo wetu?

  Biblia katika itabu cha Yuda,mstari ule wa 7 kuna maneno haya:

  “Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele”

  Hivi ndivyo dunia ambavyo imekuwa tangu enzi hizo za Sodoma na Gomora. Iwe ni kwa kuruhusiwa au kutokuruhusiwa na serikali za wanadamu, watu wamekuwa wakitenda maasi kutokana na msukumo wa uovu unaotokea ndani yao.

  Nionavyo mimi, Tanzania kukataa sharti hilo haitakiwi kuwa ndiyo faraja kwa wacha Mungu bali faraja ya mcha Mungu iko katika kushika haki ya Mungu, kama inavyoelekezwa katika Biblia na kwa kumfuata kikamilifu Yesu Kristo aliye mwokozi wa roho zetu!

  [Nyongeza: Tanzania ni nchi ambayo inaweza kabisa kuishi kwa kujitegemea kama tutakuwa wazalendo, na watu wanaopewa dhamana ya uongozi wakiacha kutumia raslimali za umma kwa anasa. Inawezekana kabisa! Tatizo ni kuwa kuna uovu unafanywa na vongozi wetu ambao hata katiba hiyo wanayoiegemea haijaruhusu, lakini wanafanya; hapo napo pana tatizo]

 13. Nasikitika kwamba viongozi wengi wa Africa huwa wanasema vitu ambavyo hawawezi kutekeleza.

  Wakati Libya inavamiwa Tanzania walitoa msimamo kwamba hawaungi mkono waasi wa Gaddaf na hawaitambui serikali ya Mpito ya Libya. Baadaye wakawa hawana msimamo wakaanza kuikubali. Hadi sasa sijui kama bado wanaikataa au la.

  Vingozi wengi wanasema wasichokiamini. Wanaongea ili kujifurahisha tu baada ya mbinyo mkubwa wa IMF na World Bank wanalegeza mameno na kukubali. Swala la Ushoga nalo baada ya miaka 2 au 3 viongozi wa Africa utakuta wameshalikubali na usishangae likapitishwa hadi kwenye katiba za nchi zetu.

  Africa ikibanwa sana inalegeza masharti na kuamua kukubaliana na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italy, nk.

  Viongozi wetu hawawezi kuhimili mibinyo ya kiuchumi kwa nchi zetu kwani bajeti ya maendeleo ya nchi hizi hutegemea misaada na mikopo toka kwao kwa zaidi ya asilimia 40. Yaani katika kila shs 100 tunayotumia Tanzania Shs 40 hutoka Ulaya, Amerika, Asia au Uarabuni.

  Kama tungekuwa na uwezo wa kujitegemea kwa asilimia 100 maneno ya Bwana Bernard Membe yangeweza kutekelezeka. Ufisadi mwingi umejaa kwa watendaji wa serikali hadi nchi hii inashindwa kununua vyandarua vya kukinga mbu wajawazito hadi tunasaidiwa na Marekani. Nchi hii inashindwa kutengeneza Madawati ya Shule hadi watoto wa shule wanaketi sakafuni, Barabara nyingi nchini hazina lami, na bado serikali hii inakubali mabilioni yalipwe kwa Dowans na wanasisitiza Dowans ilipwe Tshs 111 bilioni.

  Kwa hali kama hii Membe huenda anailaghai dunia tu. Mbinyo ukiongezwa tu atajikuta anakubali bila masharti.

  Mungu ibariki Tanganyika na Zanzibar.

  Obed Venerando Milinga.

 14. Big up Mh.Membe kwa kuwa na msimamo huo!Wakisitisha misaada yao,na wasitishe tu!In God we trust!!

 15. Mimi naona adhabu ya kufungwa miaka 30 jela haitoshi maana huko kwenye magereza ushoga unafanyika sana kwa hyo watu hawa watakuwa wanakaa kula na kunywa chakula cha watanzania wasiopenda ushoga hali wameowana humo magerezani, wanyongwe kabisa Mungu atusamehe

 16. kwa kweli naomba viongozi wajue kwamba watakapokubaliana na huu uchafu wajue wanaingiza Taifa pabaya kwani Mungu haadhibu mtu bali ataadhibu Taifa zima.

  nampongeza sana ndugu yetu Membe kwa msimamo Mungu akutie nguvu na awafumbue macho viongozi wengine huko Serikalini waseme hapana.

 17. Kweli waingereza hawana akili kabisa, Mbona wanawake ni wengi kuliko wanaume? Kwa nini tuukubali ushoga? Naona hawa wazungu wanatutamani kutuoa wanaume wa Tanzania, TUSIKUBALI ! Neno la Bwana linasema, ‘’Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabuduo sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika roho wa Mungu wetu’’ ( 1Wakorintho 6:9-11), Hosea 4:6, akanena kuwa, ’’Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako’. Kweli waingereza pamoja nchi nyingine 12 walioukubali ushoga wataangamia kwa kukosa maarifa.
  Neno langu la mwisho kwa waingereza , ‘’Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe’’ ( 1Timotheo 4:1-2)., TANZANIA KAZA UZI HATA WAKITAKA KUTOTOA MISAADA YAO WAACHE, HATUNA FAIDA NAYO.

 18. kwa tamko hilo kutoka uingereza nazidi kushawishika juu ya mpango wa shetani kupitia Agent wake mkubwa “freemanson society” kuitawala dunia kwa kuwa na serikali moja na katiba moja.
  Tuwe makini na tusikubali hata kama viongozi wetu wataona kuna ulazima wa jambo hilo maana suala la uhuru wa mtu kufanya anachotaka linaweza kuzungumzika kisiasa,hivyo tuwe makini sana hasa viongozi wa kidini muwe mbele kutupa miongozo wakati huu wa changamoto zenye nguvu kubwa kiasi hiki

 19. Bwana Yesu asifiwe wapendwa! Kauli ya waziri Membe inaonesha kuwa Tanzania haiko tayari kupelekeshwa kwa sababu ya kupata msaada. Ushoga ni dhambi Biblia inatufundisha. Hivyo anaehalarisha ushoga anapinga neno la Mungu. Na anaepinga neno la Mungu huyo atakuwa ni agent wa shetani moja kwa moja. Wakristu inatubidi kuomba sana katika hili maana shetani yuko kazini.

 20. jamani wateule tuwe macho hizi ni siku za mwisho. kinachonitia wasiwasi mimi ni kuwa serikali yetu imezoea sana kusaidiwa hivyo naogopa sana huenda hayo maneno ni ya kuwafurahisha tu watanzania ila watakaposainiana kwani sisi tutakuwepo? cha msingi sisi kama kanisa tuzidi kuomba ili nchi yetu isijiingize katika mtego huu wa mpinga kristo.tuombe pia kwaajili ya kanisa la tanzania ili tusimame na Mungu sawasawa la sivyo tutajikuta tumeipata hiyo chapa ya mpinga kristo.asikiaye na afahamu kwamba hizi ni siku za mwisho na kwa mtini tujifunze watumishi wa mungu.OOH!MUNGU OKOA TAIFA LETU LA TANZANIA.NAWAPENDA WACHANGIAJI.

 21. “Unto the pure all things are pure: but unto them that are defiled and unbelieving is nothing pure; but even their mind and conscience is defiled.
  They profess that they know God; but in works they deny him, being abominable, and disobedient, and unto every good work reprobate.” -Titus 1:15-16

  NI VICHAA HAWA NDUGU ZETU NA WANADHANI WANAWEZA KUWAFANYA WOTE WAWE VICHAA KAMA WAO.

 22. Tumwombe sana Mungu huu ndio mwisho unakaribia, itakuwa kila anayekataa upuuzi kama huu ananyimwa hiki au kile ila Bwana atatutia nguvu tusimame imara hadi mwisho. Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s