Yesu anakuja kukufufua!


SIKILIZA: Lazaro alikuwa anapendwa na Bwana Yesu…lakini ujumbe ulipotumwa kwa Bwana Yesu kuhusu ugonjwa wake, Yesu hakuacha shughuli zake alizokuwa anafanya kwenda kwa Lazaro. Nataka kuongea na mtu mmoja ambaye amekuwa akimuita Bwana Yesu na akidhani Yesu hamsikii, umejaribu maombi mengi, mara nyingi, umeshirikisha watumishi wengi wakati mwingine kwa kufunga, hayo yote ili Yesu akusikie na atende jambo kwako… Bwana Yesu anakuja kukutoa mahali ulipo, subiri!

Kwa nguvu zote ulizojaribu kupata msaada kwa Bwana Yesu umeona umbali umekuwa mkubwa na unazidi kuwa mkubwa siku hadi siku unaona kama hausogei na Bwana Yesu yuko mbali….Lakini ilikuwa ni baada ya Lazaro kufariki ndiyo Yesu akaenda kwake. Ni wakati utakapofika mwisho wa kifo cha tatizo lako ndiyo Yesu atakutokezea. Kifo kinapotokea hapo hakuna tena huruma, hakuna sababu ni kifo na ni mwisho baada hayo unapelekwa kuzikwa…Tatizo unalopitia sio kifo, halitakuua, ni sababu ya ushuhuda utakaowaleta wengi kwa Kristo. Ni kwa sababu Bwana Yesu ili akainuliwe kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yako. Yesu akawaambia wanafunzi wake “Rafiki yetu Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha”  Yohana 11:11-15.

Unapita kwenye tatizo? liambie “Hautakaa sana, Yesu anakuja kufufua, utaishi tena”

Yuko njiani…hiyo ndoa itaishi tena, ile furaha itarudi tena, pesa zitajibu tena kwako…ile karama iliyokufa itafufuka tena. Familia yako itarudi tena pamoja…Ile kiu ya kumtumikia Mungu itarudi tena…miguu yako itatembea tena…afya yako itarejea tena kwa Jina la Yesu Kristo. Anakuja!!

Advertisements

7 thoughts on “Yesu anakuja kukufufua!

 1. Ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu Madundo
  Binafsi nimebarikiwa na mafundisho yako. Ni kweli,tumwogope Mungu si kwa sababu ya Jehanam bali ni kwa sababu ya kazi ya msalaba. Amen.

 2. Msingi wa ukristo sasa hivi ni uoga wa moto wa jehanamu, si msingi wa kweli uliofundishwa na Yesu kuwa watu wawe na kiasi, wawe watakatifu, wajikane wenyewe na waache dhambi kabisa.
  Kwa kuwa msingi wa ukristo umebaki woga wa moto wa jehanamu, ndio maana mtu anapoanguka dhambini roho yake haiumii na dhambi aliyoitenda.
  Maswali muhimu ya kujiuliza, ni haya:
  • Je, unamgojeaje Yesu?
  • Kwa nini watu wengi hawatoi kwa Mungu na badala yake ni wepesi wa kutoa kwa shetani (kutoa kwa vya dunia)?
  • Je, unaishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu na kama mpango wa Mungu ulivyo?
  • Je, utaacha sasa kusikiliza na kuchukuliwa na kila roho zenye mvuto zidanganyazo?
  • Je, mahali pako unaposali ni salama kwa msingi wa ukristo?
  • Je, katika kuishi kwako, ni mara ngapi Mungu amefurahishwa na njia zako?
  • Je, katika kuishi kwako, ni mara ngapi Mungu amesikitishwa na njia zako mbaya?
  • Je, umeamuaje sasa?
  • Je, utaendelea kutoa kwa shetani na kuacha baraka ulizoahidiwa na Mungu kama ukimtolea?
  • Je, unatambua kuwa kutomtolea Mungu ni kujipatia laana?
  • Je, kwa nini utoe kwa shetani?
  • Je, kwa nini uendelee kuziamini tiba za jadi zisizo na kipimo, zinazoweza kuhatarisha afya na maisha yako?
  • Je, unajuaje kama kiongozi wako wa kiroho si muumini wa Freemasons? FUATILIA.
  • Je, naweza kubadilisha maisha yangu leo yakampendeza Mungu? NDIYO WAWEZA. MPOKEE YESU SASA.
  UWE MACHO.

 3. Hi, i salute you in the name of our Lord Jesus Christ . It is ma hope that you are so good in health.My intention to drop this line to you is to thank you for your good news u’ve sent me.It was so courages to me. Be blessed.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s