Chakula kizuri Kwenye Chombo kichafu

Chakula kikishapikwa ni sharti kiwekwe katika chombo safi, kilichoandaliwa ili mtu anayekula chakula hicho aweze kula pasipo kusitasita. Chakula kikipikwa na kuwekwa kwenye chombo kichafu, hata kama chakula hicho ni cha gharama na kizuri/kitamu namna gani, hakiwezi kuliwa vizuri. Kitakachotokea ni kuwa chakula hicho kitamwagwa kisha kitafutwe chombo safi kwa ajili ya kuweka chakula kingine! Kwa hiyo hali ya chombo huathiri thamani ya chakula!

Mtu anayemtumikia Yesu anaweza kufananishwa na chombo na Ujumbe wa Neno la Mungu anaoubeba ukafananishwa na chakula. Binadamu kama chombo anaweza kujiweka katika hali chafu, kwa mtazamo wa kiroho, ambayo itaathiri ujumbe wa Neno anaotaka uwafikie watu. Ujumbe huo waweza kuwa wa kuzungumza ikiwa ni pamoja na  kuhubiri au kufundisha, au waweza kuwa ni kwa njia ya nyimbo na pengine hata kwa kuandika.

Je, Ni mambo gani yanayoweza kusababisha mtumishi wa Mungu aonekane kama chombo kichafu kilichobeba chakula kizuri, na hivyo kufanya ujumbe wake ushindwe kuwafikia watu?

Advertisements

5 thoughts on “Chakula kizuri Kwenye Chombo kichafu

 1. BWANA YESU ASIFIWE!Nikweli ikiwa mtumishi wa MUNGU anaishi maisha ambayo yakotofauti na ujumbe anaofundisha yanaharibu uleushuhuda wa neno lenyewe na hii maranyingi husababisha watu wasiamini kile kinachofundishwa na mtumishi wa namna hiyo na pia siihivyotu hata nihatari kuombewa na mtumishi ambaye anajichanganya unaweza kupandikizwa roho za uovu ukawa muovu (ukaharibika) hapo nisawa kabisa na chombo kichafu chenye chakula kizuri.mbarikiwe
  F.Marandu

 2. ni kweli kabisa chombo kikiwa kichafu chakula kilichopo kwenye chombo hicho huwa hakitamanishi kula hata kidogo, sana sana kinaweza kusababisha kichefu chefu na hatimaye chakula kutapikwa hata kama kilikuwa kizuri hivyo kutoweza kumsaidia mlaji, kwenye mambo ya kiroho kama mtumishi atakuwa mchafu alafu anahubiri neno zuri madhara yake ni kutengeneza ngome mioyoni mwa watu wanaomsikia endapo wanajua mambo yake ayafanyayo gizani, hivyo watu kushindwa kuliamini neno asemalo hata kama ni zuri.

 3. Wakati mwingine unaweza kukutana na mtumishi wa Mungu au hata wapendwa wakifanya mambo ambayo ni kinyume kabisa na mafundisho ya Biblia ukiwauliza wanajibu eti wao ni binadamu na wanaishi duniani. Hivyo hufanya mambo yaliyo machukizo mbele za Mungu wakiwa nje ya kanisa .Watu wa aina hii ni sawa na chakula kizuri kwenye sahani chafu . Na wanasahau kuwa Mungu anapendezwa na watakatifu walioko duniani

 4. Bwana asifiwe ndugu

  NIMESHUKURU SANA KUPATA WAKATI NA KUPIMA KUSOMA NA KUJIBU SWALI ENYE UNAPOULIZA ZAIDI KWA MTUMISHI WA MUNGU
  1- kWANZA AWE NA HAKI NA KWELI MITHALI 23:16 23:23

  2-MUTUMISHI YA MUNGU KWANZA KWAKE NYUMBANI MAFUNDISHO YAKE ISIKIKE NA JAMAA YAKE NA MATENDO PIA NA WAJIRANI WAEFESO 4:5

  NDIO KWA MAONI YANGU KIDOGO NA PIA MUNISAIDIYE NIJUWE VILE NINYI NUNAPOFIKIRIYA KUPITIA BIBLIA

  MUNGU WA MAPENDO AWABARIKI

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s