Marekani Washerehekia Miaka 50 Kwa Maombi!

Ilikua ni baraka kwa Watanzania waliohudhuria ukumbi wa kanisa la Bethel World Outreach Church, Silver Spring, MD. Tarehe 12, Novemba na kumshukuru Mungu kwa Tanzania kufikisha miaka 50 tangu imepata uhuru, Sherehe hizo za shukrani zilifunguliwa kwa nyimbo na mapambio huku waimbaji wa sifa na kuabudu wakiongoza WIMBO WA  TAIFA, na kuimbwa kwa heshima na wahudhuriaji wote waliohudhuria. Palikua na watu kutoka mataifa mbalimbali ya Africa ambapo pia alihudhuria Askofu Mkuu wa kanisa hilo Bishop Darlingston G. Johnson ambaye ni wa Liberia, alisema ” Tanzania imekuwa ni wivu kwa mataifa mengine, tunamshukuru Mungu kwa ajili ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere na viongozi wote waliofanya Tanzania ikawa Nuru, usiku wa leo tutaiombea Tanzania iwe yenye amani na mafanikio” Alisema Askofu.

Pichani ni Mbeba maono wa IGO Ministries na mwenyeji wa sherehe hizo Dk. Nicku Kyungu Mordi, alisimama kutoa Neno la kuongoza shughuli yenyewe. “Mungu ameipenda sana Tanzania, napenda kuiita ni Garden of Eden, kumepambwa vizuri na madini ya pekee ya Tanzanite, mbuga nzuri za wanyama, Mlima wa Kilimanjaro, tunapendana, watu wengi wanajua uthamani wa nchi yetu.

Tusiongee mabaya kuhusu Tanzania, ebu tamka baraka zilizo kwenye nchi yetu, badilisha mtazamo wako, nani atatatua matatizo ya Tanzania? Sio USA, UN au Wanasiasa ni wewe ukibadilisha mtazamo wako.

Katika umaskini patakuwa utajiri, palipo na ugonjwa patakua na uzima, palipo na rushwa itakuwepo haki. Katika Biblia kuna mahali imeandikwa ilifikia hatua ya akina mama wakula watoto wao, sisi hatutafika huko, tunamtumikia Mungu wa yanayowezekana! Hakuna kinachoshindikana kwake, Kanisa lijitambue wao ni akina nani katika nchi. Watu wachache wanaweza kuleta histori katika nchi yetu!

Katika 2Wafalme 7:3-13 Tunasoma habari ya wakoma, waliofanya makubwa, walikaa wakajiuliza kwa nini wakae tu mpaka wafe? wakaamua kuchukua hatua waliendee jeshi la Washami. Watanzania, tusiongee bila kuchukua hatua, Wakoma walichukua hatua ya imani, hawakujua waende wapi wakaamua wawafuate adui zao. Na ajabu ni kwamba maadui waliposikia kishindo cha wale wakoma wanne, wakaacha kila kitu wakakimbia.

Inabidi ujitambue wewe ni nani na uchukue hatua gani. Tusingoje matajiri watusaidie, Mungu anawatumia walio tayari kufanya kitu kwa ajili ya Tanzania!! Miaka 50 ya Uhuru inabidi kubadilisha mtazamo, waza tofauti. Tunawafuata adui zetu na kuchukua kilicho chetu” Alimalizia kusema Dk. Nicku!

Pastor Catherine Abihudi Akiongoza maombi.

Dr. Frank Mwakasisi akiongoza maombi ya kwenye simu, walishirikishwa watu kutoka nchi mbalimbali, ambao hawakuweza kuhudhuria.

 

Apostle Robert Kaguma akiwakilisha kutoka Uganda

Katikati ni Makamu wa Balozi wa Tanzania, Marekani alihudhuria maombi ya Thanksgiving na miaka 50 ya Uhuru

Pia, IGO Ministries wanaiombea Tanzania na Africa kila mwezi, Jumamosi ya tatu.

Advertisements

6 thoughts on “Marekani Washerehekia Miaka 50 Kwa Maombi!

 1. Kipekee nashukru sana kuiombea Tanzania. Mmetimiza ambacho Mungu anataka, ila ufisadi ni zaidi ya ujambazi katika nchi yetu kwani rasilimali za Taifa zinawafaidisha wachache. Tuendelee kuiombea Tanzania ili viongozi wawaheshimu watanzania kwa kulinda rasilimali kwa ajili ya watanzania wote.

  Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa, lakini pia kumcha Mungu ni kuchukia uovu. Jitahidi kupata vitabu vyangu, ANGUKO KUU TANZANIA, OLE KWA MATAIFA,YAJA NA KIKOMBE CHA BABU na Freemasons pamoja na KIONGOZI MWAMINIFU. Utaijua Tanzania imekwama wapi.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.

 2. Bwana asifiwe wandugu wote

  NIMESHUKURU SANA WATANZANIA KWA YOTE MNAPOFANYA JUU YA INCHI YENU. KWELI MUNGU ANAPENDA INCHI YENU NA PIA IMEKUWA NA MAENDELEO SANA BILA TATIZO LOLOTE NI JAMBO YA KUMUSHUKURU MUNGU .

  WANDUNGU NAOMBA SANA PIA MUTUKUMBUKE SISI WANDUGU YENU KWA MAOMBI YA INCHI YETU YA CONGO ( KINSHASA ) KWELI TUMEPITIA SANA KWA SHIDA NA VITA HATUNA AMANI KILA MWAKA ATA ATUKULE MALI KWA RAHA YA INCHI YETU JUU YA VIONGOZI WETU HAWANA UPENDO YA INCHI, NA WAO WENYEWE KWA KAZI YAO. IMESIKIKA KAMA TUKO NA MALI NDANI YA CONGO LAKINI SISI WENYEWE ATUONE RAHA YA MALI ENYEWE AMA MAENDELEO YA INCHI . KAMA VILE MASHARIKI YA CONGO KILA SIKU NI VITA NA KUBAKA WAKINA WAMAMA NA KUPORA MALI YA WARAIYA NA ZAIDI MAINCHI JERANI KAMA VILE MUNAPOJUWA . WANDUGU WATANZANIA NALIPITA PALE DAR ES SALAM NI PALE SOPHIA KAWAWA STREET KWELI NIKAONA MAENDELEO IKO NA TENA IKO NAONGEZEKA MNO KIUCHUMI NA NENO LA MUNGU NA ZAIDI WAIMBANJI YA NENO LA MUNGU AMA KUHUBIRI KATIKA NYIMBO MUNGU ANAWAPENDA SANA LAZIMA TUMUSHUKURU.

  ,,,,, OMBI LANGU NI IYI CONGO INAJITAYARISHA UCHAGUNZI YA RAISI WETU MUTUZAIDIYE PIA IPITE VIZURI BILA MAMBO MENGI NA SISI TUSHUKURU MUNGU.NA KIMIA IKAKUWA NA NENO LA MUNGU ITAKWENDA POPOTE ATA WAIMBANJI WENU WATAFIKA KWETU KUTANGAZA UKUBWA YAKE.

 3. Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa,
  Mungu awabariki kwa kutumia muda wenu wa kusherehekea miaka 50 ya uhuru kwa maombi.
  Ila tu jinsi Apostle Robert Kaguma alivyoweka alama za vidole hapo juu inakuwa kama nembo ya Free manson, natambua kabisa kuwa yeye sio free mason ila tu ni vema wapendwa tukaepukana kabisa na uwekaji wa vidole hivyo.
  Mungu awabariki

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s