Laana

Je, Nini maana ya LAANA?

Advertisements

9 thoughts on “Laana

 1. Laana ni mfumo wa mapatilizo yanayompata mtu kutokana na matendo yaliyotendwa na waliotangulia (DHAMBI) yaana MA-BABU na MA-BIBI wa pande zote mbili kwa BABA na MAMA. Dhambi zao katika kizazi chao inakuwa LAANA, hivyo Dhambi zako wewe zinakuwa LAANA kuanzia kwa watoto wako mpaka wajukuu zako. Biblia inatuambia MUNGU atakipatiliza kizazi1/ cha pili2/ cha tatu3/ mpaka cha nne kwa matendo yako4/. yawe mazuri au mabaya ni mpaka kizazi cha nne.

  Hivyo kiongozi wa kusimamia LAANA ni MUNGU mwenyewe sio shetani na ndio maana laana haikemewi bali inavunjwa, maana uwezi kumkemea MUNGU ndio maana ugonjwa wowote usiosikia maombi ni LAANA.

  Tukirudi ktk mapatilizo tunaona DAUD alipozini na mke wa URIA akapata mimba mtoto akafa, akabeba mimba ya pili mtoto akazaliwa. Akaitwa SULEMAN Mtoto alipokua akawa mfalme akafatiliwa na mapatilizo ya jinsi alivyopatikana akawa mfalme anayependa uzinzi,maana kapatikana kwa mfalme/ akawa mfalmme. mfalme katembea na mke wa mtu na kumwaga damu ya URIA/ Suleman akafanya kuoa oa kila anayemuona.

  Soma Biblia 2 SAMWELI 11:2-27

  Hivyo LAANA ilianzia kwenye kizazi cha kwanza cha DAUD ambaye ni mtoto wake mhusika kabla ya kufuatililia watakaozaliwa na mtoto mwenye LAANA.

  KAZI YA LAANA.
  Laana uzuia mafanikio ya mtu.
  Laana ikmbana mtu kama hana ujasili uamua kutenda Dhambi.
  Laana ni mtambo aliouweka Mungu ili tujifunze nono la MUNGU.
  Laana ni nino la kiroho, kimwili ni Raha hana.
  Laana umfanya mtu kuwa na RAHA YA MUDA mfupi.

  KWA NINI NI KUSUDIO LA MUNGU.
  Bila laana watu wasingemfahamu MUNGU hivyo siku yoyote ukiona mtu ana magumu ya maisha juwa ya kuwa MUNGU anamtafuta.

  Pia ukiona mtu anaenda kwa mganga wa kienyeji mwambie MUNGU anakutafuta hacha kujipendekeza kwa shetani maana ungekuwa wa shetani ungekuwa umepewa tayali maana shiriti la shetani ni kumsujudia tu.

  Kwa MUNGU ni kujifunza neno.

  MUNGU awabariki.

  Ni MCHUNGAJI MLAKI JB.
  Wa KANISA: DELIVERANCE CHURCH FOR ALL NATIONS.
  La TANGA.

 2. Wapendwa Orbi na Paul? Utukufu apewe Kristob YESU?

  Nashukuru kwa kusoma mawazo yangu na kisha kupata maswali kutokana na maoni yangu.

  Kwa mujibu wa maswali yenu inaonekana kwenye kipengere cha KAZI YENYE KIPATO CHA KUTOSHA MAHITAJI YA KILA SIKU.

  Naomba nieleweke kwanza hapa. Maana yangu hapa ilikuwa kwamba KAZI NI BARAKA. Kwa upande mwingine kuishi bila KAZI NI LAANA.

  Hapa nataka tuwasaidie watanzania wengi wenye mitazamo HASI juu ya kazi. Kuna watu wanadhani kuwa KAZI NI MATESO au LAANA. Kwamba akikutana na mtu mepndwa anafanya kazi ya Mkokoteni haoni kama huyo mtu AMEBARIKIWA.

  Maana yangu hapa ni kwamba; KULE TU KUWA NA KAZI NI BARAKA. Swala la kama kipato kinatosha au hakitoshi mahitaji yake ya kila siku linabaki ni mjadala wa kudumu.

  Bwana Orbi ametoa mfano wa wakulima wa Vijijini kwamba wanafanya kazi sana lakini hawapati kipato cha kutosha mahitaji yao; je wamelaaniwa?

  Tunapaswa kuelewa LAANA HUJA KWA NJIA ZIPI?

  Kuna LAANA zinazotokana na Makosa ya viongozi wa Jamii nzima au Familia. Kwa mfano kosa la mama au baba mzazi linaweza kuleta LAANA kwa watoto, wajukuu, na vitukuu hadi kizazi cha NNE.

  Hapa Tanzania kuna LAANA zinatuandama kutokana na makosa ya Viongozi wa Nchi hii au wazazi wetu. Viongozi wa nchi wakitia saini mkataba wa kuchimba madini au kuvua samaki au kuchukua mashamba makubwa au kujenga barabara; mikataba hii kwa njia moja au nyingine itatuletea BARAKA AU LAANA kutegemeana na ubora wa mikataba hiyo.

  Tangu nchi nyingi za Afrika zipate Uhuru wa Bendera bado wananchi wengi wameendelea kukaa katika LAANA ya umaskini wa kipato, elimu, uchumi, fikra, nk kutokana na viongozi wanaotawala nchi huska. Kwa mfano wakati nchi hii inatawaliwa na Bwana Benjamini Wiliam Mkapa mfumuko wa bei uliteremshwa hadi 4%. Hii ilisaidia kuimarika kwa fedha ya Tanzania kiasi kwamba ukiwa na Tshs 10,000 mfukoni ungeweza kuitumia kwa siku 5 au wiki nzima. Kwa sasa tunavyoongea, Mfumuko wa bei umepanda hadi 17%. Hii huenda ikapanda zaidi na kuwa kama Enzi za Rais Alli Hassan Mwinyi ambapo mfumuko wa bei ulipanda hadi 36%. Pesa wakati ule ilikosa thamani kabisa. Nchi nyingi zenye uchumi imara mfumko wa bei huwa unacheza kati ya 3% hadi 9%. Hii ndiyo ishara ya uchumi imara.

  Kwa hiyo kama ni mikosi na laana zinazotokana na maamuzi ya viongozi wa kitaifa huwakumba wananchi wote bila kujali wamemwamini Mungu ama la. Hii huwa laana kwa taifa lote.

  Sodoma na Gomora walipokazana na dhambi ya ufilaji na usagaji (ushoga) Laana ilishukia miji yote. Wote waliokuwemo vijana, watoto wanawake, wazee wote walichomwa moto akaokoka Luthu na watoto wake tu. LAANA ile ya ushoga iliwapata hadi watoto wote waliokuwepo ingawa hawakuwa wamefanya dhambi za ushoga. Hata wakati wa Nuhu pia watoto wote waligharikishwa kwa maji kwa sababu ya wazazi wao kutokutii. Inaaminika na baadhi ya wahubiri wa Injili kwamba hata siku ya Mwisho watoto wa watu wasiomwamini Mungu nao watapata ghadhabu ya Moto wa milele kwa sababu ya wazazi wao.

  Kwa hiyo Bwa. Orbi na Paul ni kwamba kwa upande mmoja unaweza ukawa na BARAKA na kwa upande mwingine ukapata LAANA isiyozuilika kwa sababu ya makosa ya watu wanaokuongoza kama vile wazazi, na viongozi wa jamii yako au taifa lako.

  Kumbuka kuwa Biblia inasema kuwa AMELAANIWA AANGIKWAYE JUU YA MTI…. Yesu aliposulubiwa kwa nyakati zile ilikuwa ishara ya LAANA. Na ni kweli alibeba LAANA ambayo ingetupata wanadam wote ili sisi tuokolewe. Kwa kumwamini Yesu tunafutiwa LAANA zote ambazo zingetupata kwa kuwa mbali na Mungu. Yesu alikubali kubeba LAANA ya msalaba ili kila aaminiye apate BARAKA ya ukombozi. Hapa pia tunapata tafsiri ya BARAKA kwamba KUOKOKA ni KUBARIKIWA. Ukiokoka dhambini UMEBARIKIWA hata kama wewe ni maskini kama Razaro. Hata kama ungekuwa nchi masikini kabisa duniani kama Tanzania (The second from the poorest country) bado wewe UMEBARIKIWA KWA KUMWAMINI YESU KAMA MWOKOZI WA ROHO YAKO MILELE YOTE. Razaro alikuwa hana MIBARAKA ya kimwili (fedha, dhahabu, vyakula, nguo, magari, nk.) lakini alikuwa na BARAKA za Rohoni. Tunapaswa kuelewa kuwa kuna BARAKA za MWILINI na BARAKA za ROHONI.

  Ukimwamini Yesu Kristo UNAHESABIWA HAKI NA BARAKA YA KURITHI UZIMA WA MILELE. Ukimkana Yesu Kristo Unahesabiwa HAKI YA KURITHI LAANA YA HUKUMU YA KUTOMWONA MUNGU MILELE MAISHA YAKO YOTE YAKIWA JEHANAM.

  Katika maisha haya tuna pande mbili za maisha ROHO + MWILI, au BARAKA + LAANA. Kama vile Roho bila mwili haiwezi kuendelea kukaa hapa duniani, vivyo hivyo BARAKA bila kuwepo LAANA haitaonekana. Hakuna taifa lolote ambalo limeweza kuondoa LAANA ZOTE katika mataifa yao wakabaki na BARAKA tu ndani ya mataifa yao. HAKUNA TAIFA KAMA HILO. TAIFA LITAKALOKUWA NA BARAKA kuanzia mwanzo hadi mwisho ni MBINGUNI TU.

  Kama tukingali hapa duniani, tutaendelea kukumbana na matukio kadhaa ya Kupata au kuishiwa, kufarahi au kuhuzunika, kuoana au kuachana kwa sababu za kifo, kuwa na wanawake tasa, kuwa na wanawake wanaotokwa mimba, tutaendelea kuwa na watu maskini, tutaendelea kuwa na viongozi wanaotusababishia Laana bila sisi kutaka, tutaendelea kuwa na ukame, mafuriko na vimbunga, tutaendelea kuwa na mafisadi, nk. Hayo yote ni LAANA ambazo zitaendelea kutuzunguka pande zote hata kama Tumeokoka. LAANA ZINGINE HATA UNGEFUNA NA KUSALI HAZITOKI KATU.

  Naomba nimalizie kwa kuzungumzia LAANA zitokananzo na wazazi wetu. Chukulia mfano wa Mzazi ambaye alikataa kumpeleka mtoto wake kusoma shule kwa sababu tu aliona mtoto wa kike hana faida yoyote kumpeleka shule. Mtoto huyu atakuwa hajui kusoma wala kuandika. Mtoto huyu atakuwa hawezi kusoma Biblia wala maandiko yoyote ya Mungu. Mtoto huyu atakuwa hawezi kufanya Biashara na mahesabu ya pesa yatamshinda kwa sababu hakusoma. Matokeo yake kwa kutokusoma ATAAMBULIA KUWATUMIKIA WATU WENGINE TU MPAKA KUFA KWAKE. ATASHINDWA KUINUKA KIUCHUMI AU KIMAISHA KWA SABABU TU HANA ELIMU. Hii bila shaka itakuwa ni LAANA ambayo imesababishwa na maamuzi mabovu ya Mzazi. Mtoto huyu atashindwa kulima kilimo cha kitaalam, Mtoto huyu atashindwa kuendesha familia yake na kuiwekea misingi ya kudumu kiuchumi. Watoto wa mtoto huyu na wajukuu wake huenda wote wakawa Hohe Hahe kiuchumi na Kijamii kwa sababu tu Babu wa Mzazi wao alifanya maamuzi ya kutompeleka shule mtoto wake. LAANA ya mfano huu mwenye uwezo wa kuiondoa ni mamlaka ya nchi husika (Serikali) inayoweka sera mathubuti ya kuhakikisha kila mtoto anasoma mpaka ngazi ya mwisho ya shule mzazi wake apende au asipende.

  Kumbuka Watanzania wote tupo ndani ya LAANA ya umaskini wa nchi. Nchi hii inaposemwa kuwa ni Maskini ni pamoja na wote WALIOOKOKA kwa kumwamini YESU. Tukisema nchi hii IMEBARIKIWA pia tunajumuisha wote WANAOMWAMINI na WASIOMWAMINI YESU kama Mwokozi wao. Tunaposema Marekani ni taifa lililobarikiwa, Israeli au Canada ni taifa lililobarikiwa haina maana kwamba wananchi wote wamebarikiwa. Aidha, haina maana kwamba wote wanamwamini Yesu kama mwokozi wa roho zao. Hii ni lugha tu ya kulibariki Taifa au Kulilaani kwa matendo yake au mwonekano wake.

  Pamoja na maelezo yangu yote hayo huenda kukawa na watu wenye maswali na au kuchanganyikiwa zaidi. Hata hivyo, nadhani yote yanatokana na uelewa kila mmoja anavyolielewa neno hili BARAKA na mwingine anavyolielewa neno hili LAANA. Wewe unavyoyaelewa maneno haya BARAKA na LAANA ndivyo itakavyokuelekeza kutoa maelezo au ufafanuzi.

  Mimi nijuavyo sasa: BARAKA ni jumla ya mambo yote yaliyo mema ayapatayo mtu yeyote kimwili na kiroho. Mambo yote ya furaha, raha, burudani ya moyo, utulivu wa maisha na moyo, kuridhika na maisha, kutulia na kuwa na matuini ya baadaye; Hii ndiyo tafsiri yangu binafsi ya neno BARAKA.

  Kuhusu LAANA: Hii ni jumla ya mambo yote mabaya yampatayo mtu kwa sababu ya matendo yake mwenyewe au wengine au viongozi walio juu yake. Mambo yote mabaya hapa nina maana ya mambo yote kama vile adha isiyokoma, huzuni isiyo na mwisho, umaskini usiokoma, karaha za maisha zisizo na mwisho, magonjwa yasiyopona wala kutibika, kukosa kipato kinachokutoa katika umasikini, kukosa chakula kinachotosha familia kwa mwaka mzima, ukame wa mara kwa mara kutokana na kuyaharibu mazingira, mafuriko, njaa kali, kukosa mavazi, nk. yote haya ni jumla ya mambo yanayowekwa katika upande wa LAANA. Hapa ieleweke kwamba inakuwa LAANA pale tu unapokuwemo katika hali hii bila matumaini ya kuweza kujitoa kabisa. (Hii ni tafsiri yangu).

  Asanteni wapendwa kwa maswali yenu.

  Bado na mimi ninajifunza zaidi toka kwa wengine.

 3. Ndugu Millinga,

  Kama ambavyo imekuwa kwa ndugu Orbi, nami niliposoma maelezo yako ya kina nimepata mambo ambayo naona yanapingana kwa hivyo nami ningefurahi sana kupata ufafanuzi.

  Katika kipengere chako cha 1 umeelezea mtu ambaye AMEBARIKIWA na Kinyume chake ni kuwa AMELAANI. Kipengere hicho kinasomeka:

  “Kufanya kazi halali na ikakupa kipato cha kutosha mahitaji ya kila siku hapo Umebarikiwa. Kutokuwa na kazi ya kukupa kipato ni LAANA”.

  Sasa, kama kuna mtu anafanya kazi HARAMU, labda ni mwajiriwa lakini najiongezea mshahara kwa kuiba pesa toka katika maeneo tofauti au kuandika OT (over-time) za uongo lakini mtu huyo akawa ANASAIDIA SANA WENYE MAHITAJI ya msingi, sasa huyo TUTAMWITAJE?

  Lakini pia wako wanaofanya kazi halali, labda ni mkulima na hivyo anajitosheleza kwa kipato cha kutosha mahitai yake ya kila siku, ambaye kwa tafsiri yako umesema AMEBARIKIWA. Lakini utakuta watu hao hawana zile sifa ulizozieleza katika vipengere 4 na 6; yaani utakuta hajali watu wengine wasiokuwa na ukamilifu wa mahitaji yao ya msingi wa maisha au utakuta anajua ufumbuzi wa matatizo fulani lakini hafanyi bidii kuyatatua, pengine kwa sababu ananufaika na kuwepo kwa matatizo hayo. Sasa mtu wa hivyo kwa maelezo yako ni mtu ALIYELAANIA.

  Sasa mimi hapo nimeona kuna MGONGANO. Mtu huyo huyo kuwa ndani ya LAANA na BARAKA kwa wakati mmoja naona sijaelewa.

  Kama kunaweza patikana ufafanuzi kuwa Je, Yawezekana mtu mmoja akawa AMELAANIWA KWA BAADHI YA MAMBO halafu kwa wakati huo huo AKAWA AMEBARIKIWA KWA MAMBO MENGINE? [Can laana and baraka exist within/on the same person?]

  Maelezo ya nyongeza kutokana na maelezo katika kipengere cha 4 ni hili,

  Wako watu “wanaojua kuwa Mungu ndiye muumba” na zaidi ya kujua wamekubali kumpa Yesu maisha yao. Kwa hiyo ni watu wanaomuabudu Mungu, achilia mbali kumjua tu. Kwa hiyo kwa mtazamo wa tafsiri yako ni kuwa kwa upande huo mtu wa namna hiyo AMEBARIKIWA. Lakini kutokana na hali ya maisha ki-nchi nchi, na pengine kibinafsi mtu huyo utakuta hawezi kujitosheleza kwa mahitaji ya kila siku [kama alivyoeleza kwa kirefu ngd Orbi] kwa hiyo kwa upande huo mtu huyo atakuwa AMELAANIWA

  Hicho ndicho kinachonichanganya nishindwe kuelewa kuwa yawezekanaje mtu huyo akawa na matokeo ya kubarikiwa ndani yake halafu kwa wakati huo huo kuna matokeo ya kulaaniwa?

  Nasubiri toka kwako ili tuendelee kujadiliana kuhusu suala hili.

  Asante sana!

 4. BWANA ASIFIWE WANDUGU WOTE USOMA BLOG IYI .

  ZAIDI KWA NDUGU MILINGA NIMESOMA NA INANIFUNDISHA MUCHANGO YAKO JUU YA LAANA.UBARIKIWE SANA .NA PIA NIMESOMA JUU YA DADA ROSE MOHANDO JUU YA KUFAA NGUO MBELE YA WATU AMA YA KUACHA MIGUU ICHE AMA MAKWAPA AMA MATITI. KWELI NIMUBAYA SANA ILE NDIO SHETANI ANA TAFUTA KUINGIYA POLE POLE NDANI YA WATOTO YA MUNGU .JUU YANGO ZAIDI TUWASAIDIE NDANI YA MAOMBI YETU JUU YA KAZI WANAPOFANYA YA KUHUBIRI INJILI AO KUTANGA NENO LA MUNGU KWA IMANI YA BWANA WETU YESU KRISTU

  1– JUU YA LAANA VILE BIBLIA INASEMA TUTAFUTE KWANZA UFALME YA MUNGU AMA
  KUSHIKA SHERIA ZAKE NA KUITUMIKIA KILA SAA NA DAKIKA KATIKA HAKI
  NA KWELI NA UPENDO MNO APA CHINI YA JUA NA VINGINE VITAONGEZEWA KWETU

  NA KAMA TUKISHIKA SHERIA ZAKE KWA KWELI KAMA VILE ANAPOSEMA HATUWEZI
  KUWA MUKIA TUTAKUWA KICHO KWA VITU YOTE APA DUNIANI SIO MBINGUNI VILE
  BIBLIA INAPOSEMA MAANDIKO MATAKATIFU

  2– JUU YA DADA ROSE MUHANDO JINSI ULIPOONA MAVAZI ALIPOVAA LAKINI MIMI
  BADO SIJAONA ILE DVD YA UTAMU YA YESU NA SIKIYA TU NYIMBO KWA MAONI
  YANGU KAMA VILE TUNA JUWAKA ASKARI AMA MWANAJESHI AMA POLISI KWA
  UNIFORM YAO YA KAZI WANAPOFANYA NA SISI PIA WAKRISTU YA FAA TUKUWE
  NA MUFANO YA YESU KRISTU…..KUSEMA YETU,,,KUTEMBEA YETU,,, KWA KAZI
  PALE TUNAPOFANYA ,,,ATA MATAZAMO YETU,,,NA KUHUMBIRI YETU,,,NA KUIMBA
  YETU NA ZAIDI KUFAA YETU MANGUO,,,

  TUJUWE ULE ADUI YETU IKO NA SIASA SANA JUU YA KUTEGA WANA WA MUNGU
  KU NJIA MINGI ANATAFUTA . LEO IYI ANATUMIYA SANA WAKINA WAMAMA KWA
  MAVAZI JUU YA TAMAA YA MACHO KWELI IKO VITA TUKO NAYO APA DUNIANI KAMA
  KAMA VILE NDUGU ALIPOSEMA KWA KUTENDA DHAMBI INAANZA KWANZA MAWAZO
  KISHA NJIA KUBWA YA KUINGIYA DHAMBINI NI MACHO NA KUSIKIYA

  KWA JINA LA YESU TUKO NA USHINDI KUPITIA DAMU YA YESU

  NDUGU KAMA NIMEKOSEA UNISAMEHE

  MUBARIKIWE WOTE

 5. Ndugu yangu Milinga,

  Naomba ufafanuzi kwa hili………

  1. Kufanya kazi halali na ikakupa kipato cha kutosha mahitaji ya kila siku hapo Umebarikiwa. Kutokuwa na kazi ya kukupa kipato ni LAANA.

  Nimezunguka sana Tanzania hasa vijijini ambako Watanzania wengi wanafanya kazi mashambani na katika kazi za uvuvi…..na ufugaji…..lakini kupata mahitaji yao ya kila siku ni kazi…..Je wana LAANA HAWA? …….Je kima cha chini Tanzania ni kipato cha kutosha kukidhi mahitaji ya kila siku ya Mtanzania? Je watanzania wenye kipato hicho WAMELANIWA?Vipi vijana waliomaliza vyuo na kuwa katika kipindi cha mpito pasipo ajira kwa muda mrefu? Je wako chini ya Laana? .Mungu amenipa kibali cha kuwepo katika nchi tajiri ulimwenguni……ambayo kwa sasa uchumi wake unapitia katika matatizo na wengi kupunguzwa kazi na hata wengine kazi zinashindwa kukidhi mahitaji ya kila siku…..Je Wana Laana?

  Utasemaje maneno ya Yesu “Maskini tutakuwanao siku zote” au mfano wa Tajiri na Lazaro? Hatujambiwa Lazaro alikuwa AMELAANIWA! Au utasemaje juu ya Paulo ambaye kuna kipindi anasema alikuwa anajua KUPUNGUKIWA! Yaani hakuwa na kipato cha kumtosha? Utasemaje juu ya Kanisa la Yerusalemu ambalo ilibidi lifanyiwe changizo? Je lilikuwa chini ya Laana?

  Naomba sana tuwe waangalifu na tutumie maneno ya Mungu…….haya mafundisho ya LAANA LEO yamezagaa kwa kuwe wengi hatuangalii kwa mapana na marefu Neno la Mungu linafundisha nini hasa……

 6. BWANA YESU asifiwe!Kwaufupi sana laana ni maapizo / matamko mabaya anayotamkiwa mtu na wazazi inaweza ikawa yalitamkwa baada ya magombano. Mfano “Wewe na uzao wako kwa jambo hili ulilonitendea hamtakaa mkafanikiwa”. Sasa pale roho za uovu zinafuatilia neno lile sawasawa na neno lile kwamba uzima na mauti vimo ktk kinywa cha mtu.Au baba / mama akamlaani mtoto wake kwa tabia mbaya, makosa aliyotenda kinachofuata ni mateso ambayo ndiyo udhihirisho wa laana yenyewe (matokeo ya maneno yaliyotamkwa)pia mara ingine watu wana weza hata wakawa walimuua mtu kwa mateso makali akatamka maneno ya laana juu ya wahusika na laana hiyo inaweza ikasumbua ukoo huo hapo inageuka laana ya ukoo inasumbua wanaofuata bila wao kujua mpaka wapate delivarance (wafunguliwe ktk kifungo hicho)mbarikiwe!

 7. Kusema ukweli John Paul ameeleza vyema mada hii hadi amenigusa sana.

  Wapendwa, watu hatupaswi kuchanganyikiwa na kuhangaika huku na kule eti kutafuta baraka. Baraka inaweza kutafsiriwa na kila mtu kutokana na aonavyo yeye au atakavyo maisha yake yawe. Wewe una maono gani na maisha yako. Unataka kumiliki nini maishani mwako? Unajilinganisha na nani anayekuzunguka au aliye karibu na wewe hadi useme yeye AMEBARIKIWA na wewe unayo LAAANA?

  Watu wengi wamedhani kwaMmba kupata BARAKA ni kule kuwa katika hali ya kutougua mara kwa mara, kwamba baraka ni kule kupata watoto wengi, fedha nyingi, nyumba nzuri na nyingi, magari mazuri na ya kifahari, nguo nzuri na za kutosha, makabati ya vyombo vya nyumbani, TV, Makochi mazuri,Umeme nyumbani, maji ya bomba nyumbani, kuwa na digrii za elimu ya juu, kuwa na fedha nyingi katika akaunti benki, kulala mahala pazuri; vitanda vizuri au vikubwa vya sita kwa sita (6 x 6 Feets bed), kunywa maji ya chupa kila unapoyataka, kunywa vinywaji vya kila aina, nk.

  Lakini je, ukweli ni upi kuhusu Baraka Au Laana? Nionavyo mimi; baraka kwa upande mmoja ni:

  1. Kufanya kazi halali na ikakupa kipato cha kutosha mahitaji ya kila siku hapo Umebarikiwa. Kutokuwa na kazi ya kukupa kipato ni LAANA.

  2. Kuweza kutawala mazingira yako na ukayafanya yapendeze machoni pako na wengine wanaoyatazama huku ni kubarikiwa.

  3. Kutawala viumbe vyote vilivyoko nchi kavu na majini na angani huko ni kubarikiwa. Mungu alituweka duniani tutawale viumbe wote. Kutawala viumbe wengine ni ishara ya KUBARIKIWA. Mbwa, kuku, Ng’ombe, nguruwe, sungura, Bata, Punda, Ngamia, Samaki, Njiwa, n.k tunapaswa kuvitawala siyo vitutawale. Kutawaliwa na kitu chochote ni ishara ya kuwa chini ya LAANA. Kwa mfano kama mtu anatawaliwa na fedha badala ya kuzitwala fedha hizo huyo AMELAANIWA. Kuna wapendwa wengi hushindwa kutawala fedha hasa wanapopata fedha nyingi hasa mamilioni. Hii ni dalili ya kuwa chini ya LAANA. Kuna watu wanashindwa kufuga kuku au ng’ombe kwa kufuata kanuni za ufugaji na kujikuta wakiacha mifugo kuzurura hovyo, hii ni dalili ya kushindwa KUTAWALA VIUMBE VYOTE NA NI LAANA.

  4. Baraka ni kule kujua kwamba Mungu yupo na ndiye muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na Visivyoonekana. Kutokujua hili ni LAANA.

  5. Baraka ni kuwa na ubinadamu wa kujali wanadamu wenzako ambao wana mahitaji ya lazima kama vile mavazi, chakula, malazi na afya. Kukosa moyo wa upendo na ubinadam kwa watu wengine hata ungekuwa na mali zote za dunia hii bado uko chini ya LAANA. Wewe UMELAANIWA. Hata kama unasali kanisa la kilokole, la RC, KKKT, Freemasonry, Islam, Judaism, Hinduism, Budha, nk. kama hujali watu wengine wasikokuwa na ukamilifu wa mahitaji ya msingi wa maisha na ukawa unajipendelea tu kwa kujilundikia mavazi mengi sandukuni, vyakula tele katika stores, pesa nyingi Benki, na huwapi maskini hao chochote toka katika mali ulizonazo, wewe UMELAANIWA.

  6. Baraka ni kule kuwashirikisha watu wengine kile unachojua. Kama wewe unajua NENO la Mungu lakini huwapi wengine kile unachojua kuhusu Mungu na Neno lake, Kama wewe unayo elimu lakini huitumii kuwasaidia wengine wasiokuwa nayo, kama wewe unaelewa njia za kutatua matatizo yaliyopo katika jamii lakini hufanyi bidii ya kutatua matatizo hayo yawe ya kiroho au kisaikolojia au kifedha au kimaendeleo au kisiasa, basi wewe UMELAANIWA. amebarikiwa yule atumiaye maarifa yake kutatua matatizo ya jamii au kanisa lake.

  Mimi ninamtazama mtu kwamba amebarikiwa pale tu anapokuwa katika hali hizo nilizoeleza. Na nimwambiapo mtu UMEBARIKIWA namaanisha kuwa anazo sifa hizo za KUBARIKIWA. Kinyume chake ni LAAAAANA.

  UBRIKIWE SANA SANA.

 8. Bwana awe nasi

  Kweli ndugu JOHN PAUL mambo unaposema ni kweli kabisa juu ya LAANA . ata mimi na pata mafundisho mengi kusomo lako ..Ni kweli dunia ni mwisho kabisa mambo ni mengi mno duniani iyi kwa sasa .

  Ndugu naomba usaidizi juu ya safari yangu niko na taka nifike pale kwenu kumwezi ya 12 ao ya kwanza .kama unapoomba juu ya wasafiri uniweke pia na mimi kati ya ombi lako siku moja nikuone kimwili na wandugu wote. turudishe sifa kwake MUNGU wetu

  UBARIKIWE

 9. Katika Yeremia 17:5-6 kuna maneno haya:

  “Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu,
  Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake,
  Na moyoni mwake amemuacha BWANA.
  Maana atakuwa kama fukara nyikani,
  Hataona yatakapotokea mema,
  Bali atakaa jangwani palipo na ukame,
  Kaika nchi ya nchumvi isiyokaliwa na watu”

  Na katika mstari ule wa 7 hadi wa 8 kuna maneno yafuatayo:

  “Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA,
  Ambaye BWANA ni tumaini lake.
  Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji,
  Uenezao mizizi yake karibu na mto,
  Hautaona hofu wakati wa hari ujapo,
  Bali jani lake litakuwa bichi,
  Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua,
  Wala hautaacha kuzaa matunda”

  Kutoka katika maneno hayo ya kwenye Biblia, mimi nimeona kuwa LAANA ni kinyume cha BARAKA. Na kwa kuwa Baraka ustawi au kufanikiwa kwa yale ayatendayo mtu, [kwa uchache] basi LAANA ni ile hali ya kukosa/kushindwa kufanikiwa katika yale ayatendayo mtu. Ni hali ya kupungukiwa ufaulu wa yale ayatendayo mtu.

  Katika mstari wa 7-8 maandiko yanasema kuwa kinachosababisha mtu abarikiwe ni kule kumtumaini BWANA Mungu; kuweka tumaini lote kwa Mungu. Hapo ndipo mtu anaweza kuona baraka. Kna mahali pengine Biblia inasema “…..hapo ndipo Bwana alipoamuru Baraka [Zab 133:3]. Kwa hiyo kama vile Baraka inaweza kuamuriwa hali kadhalika na LAANA pia inaweza kuamuriwa.

  Lakini wakati natafakari suala hili, nilifikia mahali pa kuwaza kuwa NI KWA KIASI GANI LAANA INAKUWA DHAHILI kwa mtu? Je, yawezekana kumwangalia mtu na kufahamu kuwa huyu yuko vile kwa sababu amelaaniwa? Je, inawezekana kutenganisha kukwama/kushindwa kwa mtu kusikotokana na laana na kule kunakotokana na laana?

  Nilipofika hapo nikakumbuka suala la LAANA ZA MABABU. Nikakumbuka jinsi kuna ibada nyingi zana siku hizi, hasa Afrika Mashariki, na maombezi mengi ya watu wakienda kuombewa ili KUONDOA LAANA ZA MABABU zillizowafanya washindwe katika Biashara, washindwe kuishi na majirani vizuri, na matatizo mengine ambayo husemekana chanzo chake ni laana za mababu!

  Nilikumbuka pia MAOMBI YAKUVUNJA LAANA! Kwamba watu wanakubaliana katika maombi ili waombe kuvunja laana, na pengine pasipo kuweka bayana laana hiyo inayovunjwa ni ipi, specifically. Kwa mshangao kidogo, ninakumbuka kuoana moja ya maombezi ya kuvunja laana ambapo wahudhuriaji kwenye maombi hayo WALIKWENDA NA MAGARI, yaani watu wako ndani ya ukumbi wanavunja laana lakini nje wamepaki magari, yenye hadhi tofauti tofauti hadi yale ya kifahari kabisa ambayo wenye kuyamiliki ni watu wanaoonekana kwenye jamii kama watu waliofanikiwa. Lakini kumbe wao wenye hayo magari bado wanaona kuna LAANA za kuvunja! Sasa kama ni hivyo, basi LAANA NI NINI?

  Niliendelea kutafakari pia kuwa kama kila mtu asiyemtumainia Bwana ndiye ATAKAYELAANIWA au AMELAANIWA tayari, yaani ndiye atakuwa katika hali ya uduni wa maisha, Je, ni kweli kuwa matajiri wote wa duniani wanatumaini BWANA? Je, kweli ni wote wamefanya BWANA Kuwa tumaini lao? hadi awabariki hivyo na mali walizo nazo?

  Mchana wa leo niliongea na mtu mmoja kuhusu suala hili la LAANA na mali kwa ujumla., Yeye alisema kuwa mali ina njia nyingi sana za kuimiliki. Na yeye katika maisha yake alishakutana na “njia panda hizo” ambapo alitakiwa kuamua kuipata mali kwa njia zisizo halali au kuikosa kwa maana kuna rafiki zake waliamua kuipata kwa njia hizo na sasa ni matajiri wakubwa mijini. Alisema kuwa kama asingefanya “maamuzi magumu” na yeye sasa angekuwa anatambulika kwa mali. Aliendelea kusema kilichomfanya asitake utajiri huo wa njia zilizo sirini ni kuwa “aliogopa masharti” ambayo alisema mfano wake ni rafiki yake mmoja ambaye ana majumba makubwa ya kuishi, ambayo anayapangisha HUKU YEYE AKIWA ANALALA CHOONI katika jumba analokaa! Rafiki yangu huyo, ambaye bado hajaokoka, alisema kuwa kuna watu wengi wanaonekana kama vile wana maisha mazuri kwa wingi wa mali walizo nazo lakini nafsi zao zinateseka. Hicho ndicho kilimfanya aamue kubaki na pesa yake, hata kama ni kidogo, lakini ana amani na hakuna masharti ya kutii! Wakati tunamalizia mazungumzo hayo aliniuliza kama ninafahamu kitu kinachoitwa Freemasonry. Alinieleza kuwa hicho ni kikundi kinachowapa watu utajiri lakini utajiri wenye mashatri ya kafara za damu kutoka katika familia au ukoo wa mtu mhusika. Alimalizia kwa kusema hata utajiri huo wa freemasons hautaki kwa kuwa masharti yake yaleta mateso kwa familia na hata ukoo.

  Hili nalo likaniongezea tafakuri: Kama kuna watu wanautajiri au MAFANIKIO ya njia za kishirikina na machoni pa watu wanaonekana kama wamefanikiwa, Je, hao nao WANA LAANA kwa kuwa hawamtumaini Mungu? Kama ni hviyo LAANA hiyo waliyo nayo ni ipi kwa kuwa kwa macho wanaonekana kama vile “WAMEBARIKIWA’?

  Nikiwa naendelea kutafakari jambo hili nilifikiri kwa kuwa kuna BARAKA ZA MWILINI na ZA ROHONI (Efes0 1:3) basi inawezekana pia kuwa kuna LAANA YA MWILINI na LAANA YA ROHONI! Kama ni hivyo basi, kwa macho twaweza kuona mtu kama vile AMEBARIKIWA lakini kumbe AMELAANIWA. Yaani japo kwa huku nje, kwenye macho haya ya nyama, anaonekana kufanikiwa lakini kumbe kuna mahali fulani, macho yasipoona NI MSHINDWAJI KABISA asiye na amani hata na hiyo mali aliyo nayo!

  Kwa hiyo basi, Je, yawezekana kufahamu mtua aliye laaniwa? Au mtu mwenyewe aliyelaaniwa anaweza kujifahamu kuwa yuko hiyo kwa kuwa AMELAANIWA na hivyo atafute ufumbuzi, kwa uitafuta baraka?

  Hayo ni mawazo ninayoendelea kuwaza huku nikiangalia Neno la Mungu linasemaje kwa upana kuhusu suala hili: LAANA!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s