Tukimtafuta Mungu, Tutamuona!

Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji” Zaburi 63:1

Katika safari ya kupanda mlima, tunapanda mlima unaoonekana ni mrefu sana, lakini tunaufuata. Mpaka wakati tunaumaliza na kushinda, tunajipoza kwa maji na kujipongeza kwamba ulikua mlima mkali na katikati ya mlima hapakua na sehemu kuna kijito cha maji au mahali unapoweza kupoza kiu yako, wakati mwingi ulikua ukipanda mlima masaa mengi ukiwaza jinsi gani utafurahi ukipata maji ya kunywa japo kidogo.

Huu ni mlima wa kawaida, ni sawa kabisa na wakati tunapopata jaribu. Linakua gumu na refu sana wakati mwingine unadhani huwezi kutoka, wakati mwingine unapata jaribu moja kabla halijaisha hutokeza jaribu jingine, na katika majaribu hayo hauna jinsi ambavyo unaweza kupata nafuu, hakuna jinsi unaweza kuburudika na kusahau. Mpaka jaribu likishaisha na ukiangalia ulipotoka unaweza kuona palivyokua pagumu.

Daudi alipoandika “Nafsi yangu inakuonea kiu..katika nchi kame na uchovu, isiyokua na maji” ni wakati adui zake walikua wakimuandama na Mfalme Daudi, akadhani Mungu amemuacha, akajiona yuko peke yake na hana msaada. Je umewahi kuwa mahali hapo? Una uchungu na unadhani Mungu yuko mbali nawe? kama ilivyo kwa kiu ya   kawaida, mwili wako kuna jinsi unakuambia unahitaji maji hivyo hivyo katika roho uko na kiu ambayo hakuna mwingine atakayeiondoa isipokuwa ni Mungu peke yake.

Ndiyo, ni yeye tu awezaye kuiondoa kiu yako, kama (UTAKAPOMTAFUTA) Kwa moyo wako wote (UTAMUONA) Yeremia 29:13

Jinsi gani tumjue Mungu, ni kutengeneza mahusiano na yeye, kukaa karibu yake. Kuna jinsi ambavyo tunaenenda tukidhani tunamjua Mungu, lakini tunaishi tofauti na jinsi tunavyomjua!! tunatamani wengine watuombee bila kujiombea wenyewe, kupewa mistari na kusomewa biblia pasipo kutafuta na kujisomea mwenyewe, Kila mtu anahitaji kujaribu..kutafuta Mungu..kumuona kama ndiye YEYE anayejisema NDIYE. Kama atajibu maombi yako,  kama atakuwa nawe unapomuhitaji, kama atakupa hekima, nguvu na uhakika wa maisha yako. Basi YEYE NDIYE! Na kila wakati atafanya hivyo kwa ajili yako.

5 thoughts on “Tukimtafuta Mungu, Tutamuona!

 1. Imeandikwa uniite wakati wa mateso nitakuokoa nawe utanitukuza, Zaburi 50:15, imeandikwa pia Uniite nami nitakuitikia nitakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua Yeremia 33:3, tumeona mfano wa Daudi alipokuwa ktk hari mbaya , hata wale waliokuwa wakiishi naye wanajifanya marafiki zake wa karibu walimugeuka wakataka kumpiga mawe, lakini neno linasema kuwa Daudi alijitia nguvu ktk Bwana Mungu wake.1Samweli 30:6. na Mungu alimpigania akarudisha kila kitu , alivipokonya vyote. Mungu tu pekee aliyehaidi kuwa kila amuhaminiye hatatahayarika warumi 2:11. Yeye peke yake tukimwendea atatupa msaada na kutupa haja za mioyo yetu, nimemuona ktk maisha yangu, pale ambapo hakuna mwanadamu ambaye angenisaidia , lakini Mungu alinisaidia akatimiza neno lake akaniinua mimi niliyekuwa mnyonge kutoka mavumbini na tena akanipandisha mimi niliyekuwa muhitaji kutoka jahani. 1 samweli 2:8, kwa maana nyingine alibadiri matanga yangu kuwa machezo na tena alinivua gunia akanivika furaha Zaburi 30:11. Yupo na anajibu kweli, anaokoa na anainua , analinda na anabariki, Ninaungana na wewe uliyeandika habari hii kwa asilimia mia moja. Mungu azidi kukubariki hili uzidi kuwa baraka kwetu wenye kiu ya neno lake.

 2. namchukulu Mungu kwa mafundisho yenu hapa strictly on gospel, maana nimebalikiwa sana kupitia blog hii. mungu awabaliki. amen.

 3. Shalom,

  Hakika ni ujumbe unaobariki, nami niongeze machache,

  -Tunapomtafuta kwa bidii huku tukiwa na imani ambayo tunatakiwa kuidhihirisha kwa ukiri wetu,

  Waebrania 10;23

  Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumba–yumba, kwa maana Yeye aliyeahidi ni mwaminifu. Mtihani mkubwa ni wa ukiri, wengi tunasema tunaamini, tunamngoja lakini wakati huo huo tunaogopa kukiri sawa sawa na imani yetu tena unapokuwa mbele za watu wanaoifahamu situation yako. Sababu dalili hazijaanza kuonekana na unaona aibu watu watakucheka. IMANI!!!

  -Hajawahi muaibisha yeye anayemtafuta kwa bidii akitambua kuwa Mungu pekee ndiye msaada wake, maana kuna wakati tunasema tunamtafuta wakati tulishaandaa alternatives nyingine iwapo itaonekana kuwa Mungu hajibu sawa sawa na mapenzi yetu au ndani ya muda wetu,

  Kaahidi atatujulisha siri zilizo ndani yake, njia sahihi

  Zaburi 25; 14- 15

  Siri ya BWANA iko kwa wale wamchao, naye atawajulisha agano lake. Macho yangu humwelekea BWANA siku zote, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka katika mtego.

  Mbarikiwe
  Dada Imani

 4. NASHUKURU MUNGU SANA KUPITIA BLOG HII INAPONISONGEZA KARIBU NA MUNGU KWA MAFUNDISHO YOTE

  MUNGU AWABARIKI SANA

 5. Nabarikiwa sana ninapopata mafundisho na masomo mbalimbali kutoka strictly gosple,Mungu awabariki sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s