Mapato na Matumizi ya Kanisa

Je, kuna Umuhimu wowote kwa washirika kusomewa/kutangaziwa Mapato na Matumizi ya Kanisa?

Advertisements

25 thoughts on “Mapato na Matumizi ya Kanisa

 1. Lakini pia kanisa limejichanganya sana kuwa nao utaratibu wa kutokea kwenye dhehebu au kwa jina lingine ni dini,dini leo imesimama kama Mungu wa makanisa,hivyo kubadilisha mambo mengi kufanyika kama kweli ni biashara hii kazi ya Mungu hivyo kuwepo sababu hata za kuordit.
  Kanisa moja tena la mahala pamoja linatakiwa na kuwa na mipango yake na taratibu zake za uendesha,kanisa la Mungu linakosa utendaji mpana kwa sababu ya watu wachche wanaotoka juu kwa kigezo cha wakuu wa dini lakini hawana nia ya dhati ya kumtumikia Mungu ila kutafuta au kutaka faida zao binafsi kwenye kazi za Mungu.
  Leo kuna baadhi ya watumishi wanaishi maisha ya kifajhari na anasa sana kutokana na sadaka za watu wa Mungu,hiyo ni hatari,inazuia kupanuka kwa huduma kwa sababu ya wachache walio juu kutumia sadaka zinazotoka chini makanisani kwa ajili ya maendeleo ya maisha yao.
  Hivyo utumishi uliopo ni wa watu kutumika kwa ajili ya mtu,kumbuka Yesu alisema hakuja kutumikiwa bali kutumika kwa ajili ya Mungu,naye yeye mwenyewe kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine,je ni kweli utumishi wetu wa sasa unaelekeza watumishi kujitoa kwa hali na mali kwa watu,au watu kujitoa kwa hali na mali kwa watumishi?????
  Kuna fumbo kubwa sana la watu wengi kutumika kwenye utumishi wa kutafuta faida zao lakini sio moja kwa ajili ya Bwana,mbili sio kwa ajili ya kanisa la mahala pamoja na mwisho kwa ajili ya watu wake wenye shida na mateso kama yatima,wajane na wasiojiweza.
  Ule mfano wa yule msamaria MWEMA,mlawi na kuhani ndio hasa UPO LEO,hakuna anayeweza kuangalia uku baada ya kupata sadaka,bali ni kutafuta kwa njia zote kununua gari,kujenga nyumba,kufanya biashara,kusafari kwa ndege,haya ndio wengi wanatumika ili kutafuta na kupata haya,lakini sio kuwavuta watu kwa gharama yote na kuwafanya kuwa wanafunzi wa Yesu.

 2. Kanisani kuna matoleo makuu ya aina mbili,moja ni yale ya michango na yale ya sadaka.
  Tunaweza kutangaza matoleo ya michango ya aina yoyote kanisani lakini sio sadaka za aina yoyote,kwa sababu tunapitangaza sadaka lengo lake linakuwa ni nini.
  Kumbuka sadaka zote ni za Mungu,naye Mungu uona wakati wa kutoa sadaka hizo,ukitaka kuharibu kanisa anza kutangaza sadaka kanisani,ila michango na pengine maendeleo ya miradi fulani ya kanisa unaweza kutangaza mtu wa Mungu,lakini kamwe sio kabisa juu sadaka au dhabihu za watu wa Mungu.
  Je ni sababu gani ya msingi ambayo ilazamisha sadaka lazima zitangazwe kanisani???????????????????????
  cha muhimu kinachotakiwa kuangaliwa sana ni juu ya zile sadaka zote zinatumika kwa ajili ya kazi au jambo gani,je ni kwa ajili ya mchungaji au mtumishi tu,ukweli ni kuwa sadaka zote ni kwa ajili ya utumishi wa kazi ya Mungu ya mahala pamoja.hivyo mtandao wa matumizi ya sadaka ndio unatakiwa kuangaliwa sana na kuboreshwa au kuzingatiwa kama ilivyo kwa Bwana,ubarikiwe sana

 3. Wakristo wengi tunafeli kwasababu tunadhani tunachokitoa ni kikubwa sana kiasi kwamba tunahitaji kujua matumizi yake wakati hujui gharama gani Mungu anaitumia juu ya maisha yako, wengi wanaoongeaga ni wale wanaotoa hela ndogo. Wale wanaotoa hela kubwa wanelewa nini maana ya sadaka na Mungu anawaongeza na kuwabariki kwa maana mkono wao wa kulia hauangalii nini mono wa kushoto umetoa. Kamwe hatutakiwi kuwahukumu watumishi wa Mungu ni Mungu mwenyewe atawahukumu. Mchungaji wako anavyoamka saa nane usiku kuomba ulinzi na mafanikio juu ya waumini wake ukiwemo wewe na familia yako na kufunga unatembea juu ya neema aliyolipia gharama unahaja gani ya kupiga kelele akila hela yako? Baraka nyingine zinakuja pale hea yako inapomuudumia yule anayekuongoza katika mambo ya kiroho ndo maana si wote makuhani.Tunapoambiwa tunaangamia kwa kukosa maarifa hili nalo ni moja wapo. Mungu atujalie hekima. Tatizo hatuko rohoni tuko mwilini zaidi kwahiyo macho yetu siku yakifunguliwa hatutopigia kelele hizo sadaka. Wa madhabahuni atatkula madhabahuni mbona wanaoenda kwa waganga hawaulizii matumizi ya hela walizotoa?Fanya part yako the rest mwachie Mungu

 4. Mimi nadhani kazi ya Mungu ni ya kipekee sana,pia tunafanya kazi za Mungu kwa kufuata muongozo wa Mungu mwenyewe,hata kama wapo watumishi wabaya kwenye kazi ya Mungu,sio wakati wetu kuhukumu watumishi bali ni kazi ya aliyewaweka,endapo mtumishi hawezi kutumia kile anachopata kutoka kwenye aina zote za matoleo,sio wajibu wa washirika au waumini kufuatilia ili jambo.
  Je hamkumbuki jinsi ambayo yule mama alitoa mafuta mazuri kwa ajili ya Yesu,alafu Yuda alimpinga juu ya ule utaratibu wa utoaji na matumizi yake,mtumishi akitumia sadaka vibaya hata kama ni kwa kujilimbikizia mali ni yeye na Mungu,mimi na wewe hatuna nafasi ya kuingia uko na kuhoji,wengi waliojingiza kwenye kazi za Kikora waliangamizwa,hata kama wanakosea bado tuamini ni wapakwa mafuta wa Bwana au masihi wetu,wachukulie tu kama alivyofanya Daudi kwa Sauli.

 5. Rogers William,

  Siyo kweli ulichosema, kila toleo ni la Mungu, iwe zaka, sadaka, malimbuko, changizo, n.k.

  Kama ambavyo hakuna andiko linalosema serikali au mtu anaweza kuuliza (ku-audit) zaka na sadaka, ndivyo hivyohivyo hakuna andiko linamkataza mtu asifanye hivyo (asi-audit).

  Na migogoro mingi pamoja na matumiza mabaya ya fedha za kanisa iko sana ktk makanisa ya kipentekoste kwa sababu ndo yanashindwa sana kutengeneza misingi mizuri ya kiuongozi. Si rahisi ukakuta migogoro ya fedha kanisa Katoliki au kkkt, kwa sababu kila kitu kimewekewa utaratibu unaoeleweka.

  Kanisa ni taasisi, siyo chombo cha mtu binafsi, rasilimaliza za kanisa ni za taasisi siyo za mtu binafsi. Lakini leo kwa sababu ya kujificha kwenye kichaka cha kusema eti sadaka ni ya Mungu hairuhusiwi mtu kuhoji, tunashuhudia mapato ya kanisa yakitumiwa na mtu mmoja au kundi dogo tu la watu, na kuwaacha jamii kubwa ya kanisa wakiwa wahanga wa hali ngumu za maisha.

  Mitume walifanya vitu vyote shirika, hapakuwa na muhitaji kati yao, na huo ndo msingi twatakiwa kuufuata sisi kanisa. Hii tabia ya kukataa kuoditiwa ndo imesababisha watu matapeli kujipenyeza katika kanisa na kujipatia hela za aibu, kwa sababu wanajua serikali haiwezi kufika huko.
  Lakini hilo litafika tu, nyie subirini.

  Kama unajua kuwa mambo yako yako yako safi kwa nini unaogopa kukaguliwa?

  Na kama huamini kuwa hata machangizo ni mali ya Mungu kakiangalie tena kilichowapata Anania na Safira( Matendo 5:1-)

 6. Mtu yeyote hata serikali wanaweza kuuliza na kujua michango ya kanisa,lakini hakuna mwenye kibali cha kuuliza juu ya sadaka kama zaka na dhabihu au shukrani au malimbuko maana ni za Mungu,wala hakuna andiko usema serikali itauliza ili kujua ya sadaka za kanisa

 7. Hilo swala la kijinga sana.Kama watu hawataki kujenga kanisa si waache?Watu kama hao,wanaotaka kusomewa mapato ya kanisa; wasiposomewa ndo unakuta wanasema,mchungaji flani anatajirika kwa kula pesa zetu.wanataka tu wasiambiwe chochote kuhusu kutoa.tena kama ukiwambia,msali tu.msitoe sadaka,watafurahi sana.
  Tunapotoa,tujue kuwa tunamtolea Yesu!.
  Na sio mchungaji wala askofu.Msiwape shida watumishi wa Mungu kwa maneno yenu(hii ni kwa wale wote wenye tabia hiyo).

 8. ni vema waumini wajue mapato ili wajue ni wapi wamekwama ili waongeze juhudi ya utoaji kwa maendeleo endelevu ya kanisa.Lakini yote yafanyike kwa upendo si kwa mabishano wala kuhoji kwa manufaa ya kumuharibu mwingine kiroho

 9. Taarifa ya fedha ni ya muhimu sana ikiwa tunamtolea mchungaji. lakini kama tunamtolea Mungu tusijali sana namna mchungaji anavyotumia ile fedha kwa sababu yeye atahukumiwa na Mungu juu ya matumizi ya fedha ya Mungu. Kumbuka unapotoa sadaka ile fedha siyo ya waumini tena ila ni ya Mungu, na mtumishi mwenye ufahamu huwa hakimbilii kununua suti na mchele au kulipa malipo ya watoto kwa sadaka ila husubiri Mungu amkumbuke kwa ajili ya mahitaji yake. Watumishi wengi wa Mungu wako chini ya laana kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha ya Mungu, hivyo waumini msijiingize katika matatizo ya watumishi msije mkahukumiwa pamoja nao. Mungu ana nguvu na uweza mwingi wa kumuadhibu mtumishi tena kwa maarifa ya hali ya juu sana. Mbarikiwe sana.

 10. Shalom watumishi wa Mungu,
  mjadala ni mzuri na wenye kujenga, ni kweli watumishi wengi wamekuwa si waaminifu tena, ila kama anavyosema ndg Mwenda kwanini kukaa na mtu unayemuona kuwa si mtumishi wa Mungu bali wa tumbo? kwanini nipeleke sadaka yangu kwenye jengo au dhehebu ambapo ninajua wazi mtumishi aliyepo ni mpenda anasa na hana Mungu ndani yake. Mie nadhani kila mtu kwanza amuulize Mungu wapi akaabudu, kisha ukiishawapata hao washirika wenzio walio kweli na hofu ya Mungu dumu ktk upendo na umoja, mkiombeana, mkionyana, mkisaidiana ktk roho na mwili. kumbuka mtumishi nae ni binadamu na shetani anamuwinda maana akimpiga na kumshinda ameangusha kundi zima.
  Msemayo hapa kama yanatokea kwenye shirika zenu basi hao makuhani wenu wanapoinua mikono mbele za Mungu anaitika????????? Haitakiwi kabisa kupeleka sadaka yako kimazoea tu kwenye shirika ambalo unataka kufuatilia kimwli kwa kuhoji na kubana hadi penalti hivi kisha useme Mungu ameipokea? Yumkini wewe mwenyewe una matatizo ya kiroho kutohisi kuwa hapo hakuna Mungu au mie ndo nakosea?
  Kwa upande wangu mie shirika letu ninatoa kadri ninavyoguswa na ninaamini na ninamuona Mungu kwa kila nitoacho, sio kwamba mtumishi wangu ni malaika hasha ial kuna kamati za fedha za ujenzi na pia mwisho wa mwaka tunasomewa mapato na matumizi, mwisho wa mwezi tunasomewa mapato na madeni na bajeti za ujenzi. Kuna vitu kama sijui mchango wa suti ay hereni ay mtumishi ivyo ni juu yako wewe kama unayo hela na unayeroho wa Mungu ndani yako! kifupi ninaweza badala ya kuchangia sijui ujenzi nikaamua kufunga bahasha yangu nikaandika wajane na yatima (kuna wajane na yatima wanaosaidiwa kadri kanisa linavyoweza)
  Kwa kifupi siwezi kwenda kuabudu wala kutoa sadaka yangu kwa mtu ambaye inabidi nimfunge kengele nijue anafanyia nini hiyo sadaka! Mimi ninapotoa ninamshukuru Mungu na ninamtolea haja zangu, hata Eliya aliwaambia wale makuhani wa Baali watoe sadaka zao na yeye atatoa ya kwake kisha watu waamue nani ni Mungu wa kumfuata. Nasi tufanye hivyo! Mbarikiwe

 11. Nafikiri Mr Mlinga umechangia na umeelimisha kundi zima vizuri
  Katika Agano la kale wakati wanajenga hekalu Mambo ya Nyakati wa Kwanza 29 utaona namna mali zote zilivyoratibiwa na kuthamanishwa na watu wakaambiwa imepatikana nini na WAKAFURAHI
  Wachungaji msiogope kutoa hesabu maana hata mwisho wa kazi mtatoa hesabu siyo ya fedha tu bali hata ya majengo,muda, miili,na roho za waumini wote mbele za Mungu huyo huyo!

 12. Kuna wakati fulani nilikuwa Shemasi wa Kanisa katika kanisa moja mjini Dar es salaam.

  Kama ilivyo makanisa mengi, mashemasi ndio huhesabu sadaka na kumkabidhi Mchungaji. Wakimaliza kuhesabu wanampa fungu lote yeye ndiye atajua anatumia vipi. Akiamua kutoa msaada kwa wajane, yatima au wenye uhitaji kanisani au kutumia hela yote hilo ni juu yake.

  Kanisa hilo lilikuwa na utaratibu wa kutangaza mapato na matumizi pamoja na kwamba ni la Kipentekoste. Ila wakati mwingine hawatangazi. Sijui siku hizi maana kwa sasa mimi niko Kigoma. Hapa ninaposali kwa sasa sijawahi kusikia wakitangaza mapato na matumizi ya Kanisa kwa wiki mwezi au mwaka. Pale nilipokuwa nasali Dar walikuwa wanatangaza kwa wiki, mwezi, nusu mwaka na mwaka mzima. Inapofika mwisho wa mwaka kulikuwa kunafanyika mkutano Mkuu wa Kanisa lote ambapo Mchungaji ndiye mwenyekiti wa Kikao. Taarifa za maendeleo ya kanisa kiroho na kimwili yanatangazwa na Katibu wa Kanisa, waumini tunauliza maswali na kupata majibu na au tunatoa maoni ya kuboresha kazi ya Mungu na kurekebisha makosa yanayoonekana kutokana na taarifa ya fedha kutoka kwa Mtunza Hazina wa Kanisa na Katibu wa Kanisa. Utaratibu huu mimi niliupenda sana katika kanisa hili la Kipentekoste hapo Dar.

  Hata hivyo, changamoto kubwa ilikuwa (wakati nikingalipo) matumizi mengi hayakuwa yanawekwa wazi, hapakuwa na utaratibu wa manunuzi, baadhi ya pesa unakuta zimetumika isivyotakiwa au bila kanuni. Mfano, Uongozi wa Kanisa unaamua kutumia fedha za michango ya Ujenzi kwa matumizi yasiyokuwa ya ujenzi wa jengo au Fence ya Kanisa. AU Pesa ya Uinjilisti iliyochangwa kupeleka Injili mahala fulani au kusaidia wenye uhitaji unakuta haikutumika kwa matumizi hayo. Hali kama hii ilikuwa ikileta minongono sana kwa waumini hata kuwafanya wengine waseme maneno au mizozo kutokea baina ya Uongozi na Waumini.

  Kuna kipindi kanisani kwetu, kulifanyika harambee ya kuchangia ujenzi wa ukuta wa fence ya kanisa. Ilikuwa mwaka 2004. Waumini wengi waliahidi malaki ya fedha. Wapo waliofanikiwa kutoa ahadi zao zote na wengine walitoa sehemu ya ahadi zao. Pamoja na kwamba watu waliendelea kutoa kwa mujibu wa ahadi zao, Uongozi haukuweza kuonekana kuanza ujenzi wa Fence ya kanisa. Hadi sasa tunapoongea kanisa hilo halijaanza ujenzi wa fence ya kanisa tangu 2004 ilipoitishwa harambee hiyo. Juzi Oktoba 2011 nimetembelea kanisa hilo nikashangaa kuona hakuna hata nusu ya fence wala msingi au mawe yaliyokwishaletwa ili kujenga ukuta wa kanisa pamoja na kwamba watu wameendelea kutoa ahadi zao?

  Napenda kusisitiza kwamba utaratibu wa kutoa mapato na matumizi ya pesa yoyote inayotolewa kanisani ni utaratibu wa Mungu kabisa. Biblia inasema, Kila mtu atatoa hesabu mbele za Mungu. Yesu alitoa mfano wa Watu waliopewa talanta (kwa Kimarekani tungesema Dollar) kuna aliyepewa Dollar 1, Mwingine Dollar 2 Mwingine Dollar 5. Mkuu wao aliwapa ili wakaziwekeze au wakazizalishe kwa faida. Kuna waliozalisha na kuna ambaye hakuzalisha faida yoyote. Huyu alinyang’anywa hata ile moja aliyopewa akagawiwa yule aliyepewa Dollar 5 na kufanikiwa kuzalisha kwa asilimia 100% zikawa Dollar 10. Mfano huu ni mmoja wa mifano mingi inayotuonesha kwamba tunapaswa kutoa Hesabu ya kila kitu tunachopewa kutumia hapa duniani.

  Kama Wachungaji hawatajifunza zoezi la kutoa hesabu mbele za Waumini wanaoonekana kwa macho ya nyama, watawezaje kutoa hesabu mbele za Mungu asiyeonekana kwa macho. Kama wanaogopa kutoa hesabu sasa hivi, watawezaje kutoa hesabu siku ya mwisho?

  Kwa mfano kama Mtumishi unashindwa kutoa takwimu za pesa yote kanisani ikiwemo posho yako, Miradi ya Kanisa kama vile Vyombo vya Muziki, Ujenzi, Mikutano ya INJILI, Semina, Vikao, Safari za Viongozi wa kanisa, nk. hivi utaweza kutoa hesabu kwa Mungu kweli kuhusu Kondoo uliopewa na Mungu?

  Wachungaji wengi na Maaskofu wanasahau kwamba waumini waliopo makanisani mwao wamepewa na Mungu. Wanasahau kwamba ukitoa hesabu ya mapato na matumizi kwa waumini ni sawa na kwamba umetoa hesabu kwa Mungu. Hamjui kwamba Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu? Sauti ya waumini hata kama hawako na viwango vikubwa vya kiroho kama ninyi wachungaji bado wanawakilisha sura ya Mungu. Mchungaji hupaswi kuacha kutoa hesabu ya mapato na matumizi kwa hoja kwamba kuna waumini wengi hawatoi zaka au sadaka. Hata kama wanaotoa ni Watano tu katika kanisa la waumini 100, wewe unapaswa kuamini kuwa hiyo ni sadaka ya kanisa lote na siyo ya hao watu 5 tu. Kutoa hesabu ya mapato na matumizi haikuondolei heshima na utukufu bali hukuongezea zaidi.

  Namalizia kwa kuwaomba Makanisa yote ya Kipentekoste na Kiprotestanti waanze upya kama walikuwa hawatoi hesabu ya mapato na matumizi ya kanisa kuanzia Jumapili ijayo waanze.

  Waumini wanahitaji kujua mambo yafuatayo (kwa maoni yangu):
  1. Mchungaji anaishije? Posho yake ni kiasi gani kwa wiki au mwezi
  kutokana na sadaka zinazotolewa kwa wiki au mwezi.
  2. Kanisa limekusanya kiasi gani kwa wiki au mwezi uliopita.
  3. Mkutano wa Injili uliopita uligharimu kiasi gani na ni kiasi gani waumini walitoa au wahisani(kama wapo) walitoa.
  4. Safari ya mchungaji au Askofu kwenda Jimboni, au kutembelea makanisa iligharimu kiasi gani?
  5. Vyombo vya kwaya vimegharimu kiasi gani kununua au matengenezo.
  6. Bill za Umeme ni kiasi gani
  7. Bill za maji na Simu ya Askofu au Mchungaji ni kiasi gani.
  8. Ujenzi wa Kanisa unaoendelea umeshagharimu kiasi gani. Watu gani wametoa michango yao na ni kiasi gani hadi sasa kimetumika na kwenye nini?
  9. Gari/Pikipiki ya Askofu au Mchungaji imegharimu kiasi gani toka kwa waumini au wahisani(kama wapo).
  10. Watoto wa Mchungaji wanasomeshwa na kanisa? Kama ni ndiyo, wanasoma shule gani na kwa gharama gani? Kanisa limetoa kiasi gani?
  11. Walinzi wa mali za kanisa, wahudumu wa kudumu wa kanisa wanalipwa kiasi gani au wamelipwa shilingi ngapi?
  12. Wajane na yatima na wasiojiweza wenye mahitaji maalum wamelipwa au kusaidiwa kiasi gani mwaka huu au mwezi uliopita?
  13. Kanisa lina akiba kiasi gani Benki, au kwa mwekahazina wa kanisa?
  14. Kanisa limepokea waumini wapya wangapi mwezi huu kutokana na mikutano ya Injili iliyofanyika wiki hii, mwezi huu, au mwaka huu?
  15. Ni waumini wangapi wamerudi nyuma kiroho au kiuchumi na kwa nini na ni hatua gani zimechukuliwa kuwasaidia?
  16. Kanisa lina mipango gani ya mwaka mmoja ujao, miaka 3 au 5 ijayo kiroho na Kimwili? Mipango hiyo itagharimu kiasi gani na kiasi hicho kitatoka wapi? Ni kwa Waumini au wahisani?

  Kama makanisa yote ya kiroho yangeendeshwa kisayansi namna hii, naamini makanisa yangeuteka ulimwengu.

  Sababu kubwa imbayo inawapaswa wachungaji kutoa hesabu ya mapato na matumizi ni kwamba MAKANISA YOTE YANASAJILIWA KISHERIA KAMA VYAMA VYA KIRAIA. Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya kiraia (Civil Society Ordinance Act) na sheria ya NGOs Act ya Mwaka 2004, kila chama kinapaswa kuwasilisha mahesabu yake kila mwaka kwa Msajili Mkuu wa taasisi za kiraia. Kutofanya hivyo kila mwaka ni kosa kisheria. Makanisa mengi yamekuwa wavunjaji wakubwa wa sheria iliyowapa usajili nchini na kujikuta wakijifanyia mambo yao hovyo hovyo bila kufuata sheria za nchi hii. Hii ni DHAMBI KUBWA. Yapo makanisa mengine tangu yasajiliwe hayajawahi hata mwaka mmoja kupeleka taarifa zao za mapato na matumizi wala hata kulipia ada ya usajili wa makanisa yao. HII NI DHAMBI MBAYA KWA MAKANISA. Yapo makanisa mengine badala ya kufuata katiba zao zile walizowasilisha ofisi ya Msajili wa Makanisa, hawafuati kipengere hata kimoja kama walivyomwahidi msajili. HII NI DHAMBI KABAMBE. Yapo makanisa badala ya kuhubiri Injili kama walivyoeleza katika katiba za makanisa waliyosajili, wameamua kuwa wafanya biashara tu kwa migongo ya makanisa na kukwepa kodi za serikali. Wengine wanatumia majina ya makanisa yao kununua magari, vifaa vya ujenzi wa majumba yao, mazahanati yao, nk. Wengine wanauza hata Bangi na Kokeini kwa kujificha ndani ya majoho na makoti ya madhehebu yao (inasemekana kuwa Rais Jakaya Kikwete na timu yake ya usalama wa taifa ana majina yao).

  Mpendwa msomaji wangu nadhani nimekueleza vya kutosha ni kwa nini makanisa yatoe hesabu zao za fedha kila Mwaka. Ni matumaini yangu kwamba kama wewe unayesoma maoni yangi ni Mchungaji au Askofu utaanza utaratibu mpya wa kutoa hesabu kwa kanisa lako kana kwamba unatoa HESABU KWA MUNGU. Kila senti unayopokea kama Mchungaji unapaswa kuelewa kwamba umeipokea kwa niaba ya Kanisa lote na kwa muungwana kama wewe unapaswa kutoa Hesabu yake siyo kwa Mungu tu bali na kwa kanisa lako pia.

  Nategemea kwamba makanisa mengi yataanza kutoa hesabu za kila wiki, mwezi, miezi 3, miezi 6, 9 na 12. Ifikapo Desemba 2012, kanisa lako litakuwa na hesabu zilizo wazi na bila mashaka mbele ya Mungu na waumini.

  POKEA UJASIRI WA KUTOA HESABU YA FEDHA KATIKA JINA LA YESU KRISTO?

 13. Mie huwa najiuliza sana..mbona katika hili jambo yale makanisa tunayoita sio ya kiroho wanatangaza mapato na matumiz ya kanisa wakati haya ya kiroho yanaficha?kuna uficho gani katika jambo hili?je wakirsto yawapasa kufanya mambo darini?kama sivyo mbona kanisa linafanya?iweje unatoa sadaka lakini hujasikia kanisa likisaidia wajane na masikini kama matendo ya mitume inavyosema?iweje makanisa yasiyo ya kiroho yazidi yaliyo ya kiroho katika uwazi?
  naomba tuelimishane tusisingizie usiri na utiiifu kwa wachungaji…

 14. Shalom watu wa MUNGU.
  Ninaomba nami nitoe mchango wangu juu ya mada hii kama ifuatavyo;-

  Kabla ya yote ni kwamba, mwelekeo wa kiimani wa makanisa ya nyakati hizi umekuwa tofauti kabisa na mwelekeo ulivyokuwa wa kanisa la nyakati kwanza. Makanisa ya nyakati hizi washirika wanaokuwa katika makanisa kwa sehemu kubwa hawawaamini wachungaji wao, na pia wachungaji wao hawawaamini washirika wao.

  Hali hii ndiyo inayopelekea washirika watake kujua mapato na matumizi ya kanisa kwa sababu bado wanaamini kuwa wachungaji wao wanaweza kuwa wezi wa fedha zao au hata wakazitumia vibaya.

  Tukitazama baadhi ya maandiko yanayozungumzia maisha ya watu wa kanisa la kwanza, tunaweza kugundua kuwa waumini wake walikuwa na hofu ya Mungu halisi, hakuna aliyethubutu wala kufikiri kuwa viongozi wa kanisa wangeweza kuiba pesa za kanisa. Kila mshirika wa nyakati hizo alimwona mtumishi wa Mungu kama wakili wa Mungu. Maisha ya Wakristo wa nyakati hizo waliishi shirika, vitu vyote viliwekwa miguuni pa mitume, na mitume ndio waliokuwa wakiwagawia washirika kadiri ya mahitaji ya kila mmoja mmoja. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume 4:32-35 tunasoma, ”Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja wala hapana moja aliyesema ya kuwa kitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika……..Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaiweka MIGUUNI PA MITUME; kila mtu akagawiwa kadiri ya alivyohitaji”. Unaona? Hali hii kwa ujumla wake inatuonesha kuwa nyakati hizo isingekuwa rahisi mmoja wa washirika asimame mbele ya mitume na kusema eti anataka matumizi yanavyoendeshwa juu ya zile mali walizokusanywa, mtu huyo angeonekana kuwa si mwenzao.

  Imani ya wenzetu wa nyakati hizo ilikuwa imani kweli, hapakuwa na mwenye kumfikiria mwingine vibaya eti angeweza kuwa mwizi. Wote walikuwa na hofu ya Mungu iliyo ya kweli, kila mmoja alishuhudiwa na roho wa Mungu ndani yake kuwa hapakuwepo ujanja wa namna yoyote wa kuweza kuwaibia. Kila mmoja alimtazama mwenziwe kwa jicho la Mungu; hapakuwa na udanganyifu.

  Siku hizi ni tofauti sana, kila mmoja anatafuta mali hakuna wa kuaminiwa tena. Mchungaji anatazama mali inayopatikana katika kanisa na pia anatazama namna ya kuipata iwapo atapata nafasi. Washirika nao wanachunga mali wanayoichanga ili isiporwe au kuibiwa na wajanja katika kanisa, ndiyo maana tuna mjadala huu, “Washirika kusomewa /kutangaziwa mapato ya kanisa je inafaa?” Shina la mabaya ya kila mana ni kupenda fedha; “ 1Timotheo 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo, wamefarakana na imani……

  “ Nionavyo mimi, kila mmoja akae katika kanisa ambalo atamwamini mchungaji wake kwa viwango vyote, ili anapotoa pesa atoe kwa kujua na kuamini moyoni kuwa anatoa kwa ajili ya Mungu wala si kwaajili ya mwanadamu. Mtoaji asitoe huku akiwa na shaka kuwa pesa yake inaweza kumezwa na wengine, mahali pa namna hiyo ni afadhali tutoke tukatafute pengine, kama inashindikanakabisa kupapata pengine, basi kama sisi wenyewe tunajiamini kuwa tunaweza kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu kuliko hao tunaowaona, basi ni heri tuanze na sisi huduma zetu ambazo tunaamini kuwa zitakuwa na uaminifu kwa viwango vyote.

  Mchungaji kama mchungaji wa kanisa linalosimamia kweli yote ya Neno la Mungu, hana ulazima wa kutangaza mapato na matumizi ya kila kipatikanacho kanisa. Matangazo ya mapato na matumizi yanaweza kutolewa kwa mazingira maalumu, mfano; iwapo kanisa litakuwa limeazimu kuchangisha pesa kwa ajili ya kazi maaluma ya Mungu, hapo matangazo ya mapato na matumizi yanaweza kutangazwa. Katika mazingira kama hayo kanisa linaweza kutangaza mapato na matumizi ili kujua iwapo lengo lililokusudiwa juu ya uchangiaji huo limetimia, na pia ili kujua iwapo kazi iliyokusudiwa kufanyika imekamilika na kama bado ni kwa kiasi gani. Vinginevyo kama kweli kanisa ni la Mungu wa kweli sioni sababu za kila mshirika kujua kila kinachokusanywa na kila matumizi yanavyotumika. Lakini siyo kila kinachofanyika, hiyo itakuwa ni kazi ya wajumbe maalum au kamati maalum. Kanisa likiwa na hofu ya kutaka kutangaza kila kinachoendelea kuna walakini ndani yake, ni kwamba hakuna uaminifu.

  Huu ni mchango wangu tu na pia ni mwawazo yangu tuend

 15. Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu. Ni muhimu tena ni vizuri mapato na matumizi kusomewa na washirika, ili kuondoka na minong’ono ya kutuhumiwa kufuja mali za kanisa. Kama unaweza kukusanya kwa nini usitoe taarifa?

  Tena ikiwezekana mara mbili kwa mwaka ,yaani taarifa ya miezi sita sita. Asante

 16. Unajua zamani fedha iliyokuwa inatolewa, ilikuwa ni kwa ajili ya kuwatunza Makuhani. Lakini kadiri siku zilivyokwenda, badala ya kuwa sadaka, imekuwa MICHANGO. Ambayo watumishi wanapewa sehemu tu ya Michango hiyo. Kwa kweli sasa hivi hatuwezi kuiita Sadaka, bali ni michango, hivyo kama ni michango tuna ulazima wa kutoa ripoti ya mapato na matumizi. Ili kusiwepo na ripoti, turudi kwenye utaratibu wa zamani wa kuitwa SADAKA.

 17. ipo haja ya kujua mapato ya KANISA kwa ajili ya kujua jinsi mtakavo tumia kile MUNGU alicho wa bariki nacho.

 18. umuhimu upo kwani kwa watu wengi wanapenda kujua hela zilizopatikana zimetumika ipasavyo au wamechakachua

 19. Taarifa ya Mapato na Matumizi ni jambo la lazima, wala hapo hatuhitaji kujiuliza kama ni muhimu au sio muhimu. Sisi Makanisani tunaitwa washirika (kwa lugha ya kiingereza “Members”). Jambo ambalo ,mimi nalifahamu kwa habari ya mtu kuwa member ni hili; unakuwa na WAJIBU kama member, na unakuwa na HAKI kama member. Ni wajibu wangu kutoa sadaka na michango kwa ajili ya kazi ya Mungu, lakini pia nina haki ya kujua zinatumikaje.
  Jambo baya sana, ambalo siku za leo linaonekana kutiliwa msisitizo mkubwa Makanisani ni wajibu wa mshirika, hasa kwenye suala zima la utoaji wa sadaka na michango, lakini hutakaa usikie taarifa ya Mapato na Matumizi. Udhaifu huu ni hasa kwa Makanisa yanayotambulishwa kuwa ni Makanisa ya Kiroho.
  Uzoefu unaonyesha; mtu akitokea akaanza kuuliza maswali juu ya mapato na matumizi, anaanza kufanyika adui wa Mchungaji. Hapo utasikia yanasemwa mengi juu ya huyo mtu. Utasikia anaitwa:
  1. Mpinzani wa kazi ya Mungu.
  2. Mchafuzi.
  3. Wakala wa Shetani.
  Kitu ambacho kimefanyika ni kibaya sana. Wachungaji wametumia maneno ya Mungu kuwatisha watu wasiwe na maswali ya kweli.
  Naona nisiendelee sana, ila kwa mtazamo wangu taarifa ya Mapato na Matumizi inawalinda WATUMISHI wasiingie lawamani na kuchafuka.
  Nitaendelea, kutegemeana na maoni yatakayotolewa.

 20. NDUGU UBARIKIWE SANA

  IYI NDIO MAMBO INALETA SHIDA KWA MAKANISA LEO JUU YA PESA. AO VIFAA YA KANISA NA VILE BIBLIA INASEMA SHINA KUBWA YA ZAMBI NA TAMA NI KUPENDA
  PESA.

  KAMA VILE UNAPOSEMA MAPATO NA MATUMIZI YA KANISA SIO YA MUTU BINAFSI .KWANGU MIMI YAFAA ITANGAZWE KANISANI WAHAMINI WAJUWE VILE KAZI NA MAENDELEO LA KANISA LAO.

  KUANZA MWANZO YA BIBLIA MUPAKA MWISHO KWA UFUNUO AKUNA SIRI MUNGU ANAPOFICHA WANA WAKE YOTE NI WAZI

  ILE KWA MAFIKIRI YANGU

  MUNISAIDIYE

 21. Prise GOD!Hakuna haja ya kusomewa washirika mapato na matumizi kamaunafundisha washirika wako umuhimu wa kumtolea MUNGU ktk zaka sadaka malimbuko na kadhalika hawatakuwa na mashwali juu ya mapato na matumizi na uongozi wa kanisa linalojua kufundisha juu ya kumtolea MUNGU linajua pia matumizi na jinsi ya utumiaji mzuri wa pesa maana wanajua MUNGU anahusika na anaonaukitumia vibaya utawajibika kwa MUNGU sio kwa mshirika,na washirika wengi wasasa wamekufa kiroho ktk utoaji kwa kutaka kujua / kuangalia hela wanayotoa inaendawapi wanajigeuza wao MUNGU kuhukumu bila hata kuangalia yeye binafsi anatoa nini?wengi wa wasemaji watumishi niwale wanao piga panga zaka zao (hawatoi zaka kamili) wakidhani hakuna anayewaona! wanasahau anania na safira!kila mtu anavyokuwa mgumu ktk utoaji ndivyo anavyokuwa mgumu kufanikiwa,kwakutoa tunapokea kwakubania tunaishiwa / umaskini unakuwasehemu ya maisha yako!toa achatabia ya uchoyo mchoyo hujiuliza niki mpa huyu mchungaji atanunua gari ingine atavaa kuliko mimi watoto wake watasoma shulenzuri we toa hatausipotoa yule lazima MUNGU atambariki tu!usijiulize mawazo mabaya yanatoka kwa mwovu iliusibarikiwe sawa sawa na ahadi za MUNGU!fanya sehemu yako upate nafasi ya kumhoji MUNGU!
  mbarikiwe by Frederick Marandu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s