Mtu aponywa UKIMWI kwa kusikiliza Album ya nyimbo za kuabudu!

Mungu apewe sifa kwa matendo makuu anayotenda kwa kupitia mtumishi wake Mwinjilisti Milca Katete anayefanya kazi ya uimbaji nchini Canada. Muimbaji huyu mzaliwa wa Arusha Tanzania, amesikika sana na nyimbo kama NATAMANI SOGEA na KABLA SIJAKUUMBA ambazo zote zinapatikana kwenye album ya YESU NIKO MBELE ZAKO.

Akiongea jinsi Mungu alivyotenda kupitia album yake, anasema anamuheshimu na siku zote kumtii anachosema ili yeye ndiye afanye kazi na maisha ya watu, akielezea jinsi alivyorekodi album yake ya YESU NIKO MBELE ZAKO Anasema ” Nilisikia Mungu akisema nami nitoe album hiyo, katika hatua ya kumsikiliza Bwana, Nikaingia kwenye maombi na kupata hakika wa kuendelea na hatua hiyo ndipo nilipoingia studio na kusikia nguvu ya Mungu ikisimamia album ile hata ilipokamilika.

(Chini ni moja ya wimbo ulio kwenye album ya YESU NIKO MBELE ZAKO, NATAMANI SOGEA)

Anaendelea kutoa ushuhuda baada ya album yake kutoka alipata ujumbe kwa ndugu aliyekua amejawa furaha na shukrani akieleza mambo ambayo Mungu ametenda kupitia album hiyo, Alikua kwenye maombi ya siku mbili akimsihi Mungu amponye, akiwa ndani ya maombi Mungu alisema naye kuuwa atulie asikilize kanda hiyo ya kuabudu yenye jina YESU NIKO MBELE ZAKO.

Akiwa katika kuabudu alikuwa katika hali kama ya kupoteza fahamu kama nusu saa kisha akaamka akasikia sauti ikisema mshukuru Mungu maana umepona.

Alienda hospitali kupima alikua na UKIMWI, akakutwa hana tena. Ndipo nikakumbushwa kwanini niliambiwa niitoe hiyo album, ni kwa Utukufu wa Mungu, sio Burudani tu. Namtukuza Mungu kwa ajili ya Utumishi aliouweka ndani yangu.

Milka Katete

10 thoughts on “Mtu aponywa UKIMWI kwa kusikiliza Album ya nyimbo za kuabudu!

 1. hiyo ndiyo tabia ya Mungu akiabudiwa katika roho na kweli. Mungu awasaidie waimbaji wengine wa injili wasiimbe kibiashara zaidi ila wamaanishe kuabudu na kusifu kwa nia ya kumpenda Mungu sio pesa

 2. Hakuna Mungu mwingine wa kuabudiwa peke yake aliye juu mama endelea kushuka mbele za Bwana uzidi kuona Baraka zake nazipenda nyimbo zako Mungu azidi kukuinua.

 3. NIME BARIKIWA SANA KUSIKIA WATU WANAO SHUHUDIA MATENDO MAKUU YAMUNGU KWELI MUNGU IKO NA VYOTE VIMEFANYIKA NA YEYE,MUNGU ANA SEMA NW WATU KILA SIKU KILA SAA ILA WATU NIVIGUMU KUSIKIA SAUTI YA MUNGU.ILA NENO LINA SEMA,WALIO WANGU HUISIKIA SAUTI YANGU.PIA NDOO HUMJUA BWANA WAO KWA SAUTI.MUNGU APEWE SIFA ALIE SIKIA SAUTI YA DADA HUYU ALIPO SIKIA TU NYIMBO ZA KUABUDU.SIRI MOJA KWA WANAO TAFUTA MUNGU MSIKOSE KUTUBU KWELIKWELI,BAADAYE SIFU NA KUSHUKURU,KISHA ABUDU KWAKU MIMINA MOYO WAKO WOTE KATIKA UWEPO WA MUNGU BILA KUFIKIRI KITU CHOCHOTE KILE KINACHO WEZA KUKUONDOLEA UTAMU WA UWEPO,UKIZAMA SASA KATIKA MAOMBI YAKUABUDU HAPO MUNGU ANA SHUKA KARIBU NAWE.NA KUTENDA CHOCHOTE UNACHO KIHITAJI,KATIKA MAISHA YAKO

 4. ni kweli nyimbo ni huduma kamili.ukiwa na huzuni zinaleta furaha, ukiwa na hofu zinatia ujasiri. ukiwa katika uhitaji wowote sikiliza nyimbo za dini lazima utapata nuru!!!

 5. Acheni Mungu aitwe Mungu. Hata mimi naupenda sana huo wimbo wa NATAMANI SOGEA. Wimbo huu unanibariki sana na kunijaza nguvu za ajabu za Mungu kila niusikiapo katika praise power radio. Naitafuta sana album yako dada. kwa kuwa nimejua jina la mwimbaji na album, ntaitafuta haraka sana. Dada Mungu azidi kukutumia katika huduma ya uimbaji lakini kumbuka siku zote anayefanya haya ni Mungu tu. hivyo tuzidi kumpa sifa na utukufu yeye Mungu maana yeye humchagua yeyote yule ili amtumie kwa kazi yake.

  BARIKIWA!

 6. Dada Milka namshukuru Mungu kwa ajili yako kwamba hata huku uliko bado unaendelea kumtumikia Mungu, ni miaka mingi imepita tangu ulipo ondoka arusha, nilipenda nyimbo zako na nilitarajia kununua album ya nyimbo zako, nilisikitika kusikia umeondoka bila kutoa album, nyimbo zako zinatia nguvu sana, nakumbuka kipindi tunafanya huduma ktk kanisa la Kimahama Arusha na mara kadhaa kuja kututia moyo Technical college Arusha, ulifanyika baraka. Mungu wa mbinguni akuzidishie, Kiu yangu bado nitaipataje nakala ya album yako? it’s me Ima wa Arusha.

 7. Bwana Asifiwe Wapendwa, acheni Mungu aitwe Mungu yeye ni mweza yote hakuna kinachomshinda. Pia naamini ya kwamba Mungu hunena nasi kupitia ndoto na njia nyingi. Hatuwezi kumwona Mungu lakini tunahisi uwepo wake.

 8. BWANA YESU ASIFIWE!
  HAKIKA MUNGU ANAWEZA.TUZIDI KUOMBA ILI TUZISIKILIZE NYIMBO ZA INJILI KWA NAMNA AMBAYO MUNGU AMEIKUSUDIA ILI UJUMBE UNAOTOLEWA KATIKA NYIMBO HIZO UBADILISHE MAISHA YETU KAMA TULIVYOSHUHUDIWA HAPO JUU.
  JINA LA YESU LITUKUZWE!

 9. Mungu anabaki kuwa Mungu mwenye ajabu Mungu wa miujiza amejaa upendo nakadhalika.

  Ndipo na muita mwenye Rehema na Neema

  Amina

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s