Mwambie Mungu, Asante

1 Wathesalonike 5:18Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu

Ikiwa zimebaki siku chache kuumaliza mwaka huu wa 2011. Je unalo jambo gani la kumshukuru Mungu? Je umewaza kwamba katika yote umepitia mazuri au mabaya, Bado mkono wa Mungu umekua pamoja nawe?

Kwa baadhi yetu umekua ni mwaka wa mafanikio, umejenga nyumba, umeponywa, kuongezewa mshahara, umepata mwenzi, biashara, umepata mtoto, umeinuliwa kihuduma nk.. hauna budi kumwambia Mungu asante, si kwa nguvu zako wala akili zako ila ni Mungu amekuona na kukukumbuka.

Kwa waliopita katika wakati mgumu ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba katika yote umepitia bado unaishi ingekua mbaya sana kama Mungu asingekusaidia, wengine wamekoswakoswa kuachishwa kazi, ajali, wameshindwa kulipa ada, kodi ya nyumba, kufukuzwa shule, magonjwa, kuondokewa na mpendwa wako… nk

Bado tunaishi,  bado tuko mikononi mwa Mungu kama anavyosema kwenye Neno lake katika Kumbukumbu 31:6 “Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu, kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha“. Na hata sasa hajakuacha, ukiangalia miezi kadhaa iliyopita haumini kama umepita kwenye moto ule. Huyo ni Mungu anayeenda pamoja nasi, hatuna budi kumwambia, Asante.

Kwa wale ambao bado wanapita kwenye wakati ngumu, bado mwaka haujaisha, kuna Neema ya Mungu kukuvusha katika hilo unapitia sio kwa nguvu zako, bali ni kwa nguvu za Mungu, mshukuru Mungu na uendelee kumwamini yeye anaweza kukusaidia. Kama amewasaidia wote hao nawe pia  subiri utauona mkono wake.

Mungu wetu anatenda mambo makuu mpaka hatuna maneno mengi ya kusema yeye pekee anastahili sifa na shukrani hizi kwa matendo anayotutendea. Hakuna Mungu kama Mungu wa Ibrahim, Isaka na Israel.

Zaburi 107:8-16, Zaburi 106:1-2

Advertisements

8 thoughts on “Mwambie Mungu, Asante

 1. Amen, Namshukuru sana Mungu kwa kunilinda kila inapoitwa leo,mwaka huu umekuwa mwema saana kwangu.

 2. Ni ngumu kuelezea kwa maneno, ila naweza kusema tu Mungu huyu ni kama amenichora ktk kiganja chake! Mwaka huu pekee nimeshuhudia matendo makuu mimi na mtoto wangu, mimi na huduma yangu, ktk kanisa ninaloabudu. Tukiwa tunaufunga mwaka sina cha kusema ila kama si Mungu huyu ninayemwabudu kila nilichokutana nacho sikutegemea wala kuwaza kukivuka bila Yeye. sifa na Utukufu ni kwako ee Mungu.

 3. Bwana asifiwe sana

  Kweli mimi namushukuru Mungu kwa yote anaponitendea yote enye inaoneka na zingine mimi sione na ndio na rudisha sifa kwake.Nina shukuru Mungu tena kwa kunilinda mwaka uyu kwa masafari ya mingi nilipofanya .na kunifikisha mwezi uju ya 12 jina lake lisifiwe .Na pia na mushukuru Mungu kwa yote anaponipa makubwa na madogo jina lake lipewe sifa.

  AKUNA MWENGINE KAMA YEHOVA NISSI UTUKUFU YOTE IMURUDIRIYE

 4. Asante Mungu kwa ulinzi unaponipatia kila siku. Ninasafiri sana, sana kwa kutumia njia mbali mbali za usafiri. Ajali nyingi nimeshuhudia zikitokea mbele yangu na zingine baada ya mimi kupita…..Sifa na utukufu ni kwako Mungu! Ni mengi mno ambayo umenitendea Baba, wa roho yangu, kuyaeleza moja moja ni vigumu kuyamaliza na kuyakumbuka yote….

  Mbali na hayo ninayoyaona na kuyafahamu lakini yako yale ambayo siwezi kuyaona wala kuyafahamu., Kuna mitego mingi ninayotegewa kwa siri lakini Bwana unaifyatua kabla sijafika. Kuna maadui wengi wanaopanga njama pasipo mimi kuwasikia wala kuwoana.. Lakini wewe Bwana Mungu, Baba wa roho yangu, unawatawanya na kubatilisha mashauri yao, yaliyojaa hila na uchungu….

  Nalitukuza jina lako Bwana kwa matendo makuu unayotenda. Umeniweka hai hadi mwisho wa mwaka mwingine ambao si kwa nguvu wala kwa akili zangu nimeweza kuufikia.

  Hakuna maneno ya kutosha kuelezea wingi wa matendo unayonitendea, lakini nauachia moyo wangu ukushukuru wa lugha yake wenyewe…

  “Umenibeba mbawani mwako,
  Umenichora mikononi mwako,
  Sitapotea, sitapotea,
  Nikishikamana naweee”

  Utukufu wote ni kwako Mungu. Amina!

 5. Ulikua mwaka mbaya kwangu lakini nashukuru kwa ujumbe wa kunitia moyo, bado ninaishi na yale yaliniumiza yamepita hata siamini japo kuna vidonda namwamini Mungu atasafisha kabisa. Mungu akubariki

 6. Hata mimi nakila sasa ya kumshukuru mungu kwani amenitendea mambo ya ajabu.na pia nawashauri ndugu zangu tukumbuke kutoa fungu la kumi mimi nimebarikiwa nilikuwa na mshahara wa 160000 nilitoa 16000 fungu la kumi ilikuwa siku ya jumapili.Juma tatu iliyofuata nikapigiwa simu nikafanye kazi sehemu nyingine na mshahara ukawa 300000.kutoka laki na sitini.Nikasema asante baba kwani nilipotoa nilimuomba mungu anipe kazi sehemu nyingine yenye mshahara mkubwa naye akajibu.
  Nawashauri kutoa fungu la kumi kuna baraka.

 7. Ni kweli nina kila sababu ya kumwambia Mungu asante maana mwaka huu 2011 nimemwona Mungu akifanya mambo makuu katika maisha yangu. Mungu alionekana kwangu pale nilipokuwa nimekata tamaa nilimwona alinishindia. Mwacheni Mungu aitwe Mungu.

 8. Shukrani yangu yote kwa Mungu muumba mbingu na dunia

  Na mimi na rudisha shukrani yangu yote mbele ya Mungu wangu kwa yote anapotenda ndani ya maisha yangu na miaka zote ninapohishi duniani anaponilinda na pia miaka niko nayo leo Mungu apewe sifa zake kupitiya damu ya Yesu Kristu iliofanya upatanishe kubwa ndani yangu EL-SHADAI

  Mungu unikamilishe nifike mwisho muzuri kwa IMANI yangu YESU NI BWANA

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s