Kutubu kwa ajili ya Tanzania.


Nehemia 1:6 “tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, ulizozifanya juu yako; naam mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi

Daniel 9:4-5 “Nikamwomba BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao na kuzishika amri zake. Tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi naam hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako

2 Nyakati 7:14 “Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya, basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao”
______________________________________________________________
Ikiwa imebaki siku chache Tanzania kusherehekea Uhuru wake kwa kutimiza miaka 50, kumekua na vikundi mbalimbali vinavyojipanga au vimekua vikijipanga kutubu kwa ajili ya ardhi ya Tanzania. Hii ni nzuri na inatia moyo kwamba kuna watu wana mzigo na Nchi ya Yetu. Lakini nimepata maswali kadhaa kuhushu hili suala la kutubu kwa ajili yaTanzania, Je ni Kibiblia?

Kwa mifano hiyo miwili ya Danieli na Nehemia wao waliomba kwa ajili ya Israeli wakiwa peke yao na waliishi maisha ya Utakatifu, Musa hakuiombea Israeli ila aliwaambia wana wa Israeli watubu, Gidioni alianza kwa unyenyekevu akifuata maagizo ya Mungu na baadae kuwa kiongozi.

Hili wazo Kutubu kwa ajili ya Tanzania, ni zuri lakini kwanini tusianzie kwa majirani zetu? au watu tunaofanya nao kazi? mfano mtu ni fisadi na mlevi unatubu kwa ajili yake, wakati huo huo bado anaendelea na ufisadi wake, Je umeokoa kitu? Hii ni sawa kabisa na jinsi tunavyoimbea nchi yetu. Hakuna mabadiliko ya watu, hakuna maendeleo tutazamie!!

Kwa sababu pamoja na kutubu huko tunahitaji watu watakaosimama na kusema wazi uovu wa viongozi wa Tanzania, Uovu wetu sisi na kufanya tuache uovu huo ndipo Mungu atasikia na kuiponya nchi yetu ya Tanzania.

MUNGU ANATAKA TUACHE MAOVU

Katika haya ni hakika Mungu anachotaka kwetu ni kuacha maovu, kila familia, kanisa na hata Taifa. Hatuna mamlaka ya kutubu kwa ajili ya dhambi ya mtu mwingine, jirani, kanisa au kundi la maombi kutubu kwa ajili ya Taifa, Ila ni mtu binafsi kuacha uovu wake ni kama kumwambia mfu alale mahali pema peponi. Wakati atasimama peke yake siku ya hukumu, hatuwezi kutubu kwa ajili ya dhambi za watanzania wakati watanzania wenyewe mioyo yao haiko tayari kutubu.

Utatubu kwa ajili ya kila fisadi? kila anayeharibu mimba? kila mzinzi nakadhalika? Ni suala la moyo wa mtu binafsi, tuombe kwa ajili ya Tanzania Mungu atupe watu, atupe macho tuone, tuingie Ikulu na kumwambia Raisi Acha A B C ili Mungu aokoe nchi yetu.

Kutubu sio tu kunyenyekea na kulililia Taifa kwa ajili ya matukio yanayotokea, lakini ni kuziacha njia zetu mbaya na kufanya mema. 2 Nyakati 2:17, 2 Wafalme 17:13, Yeremia 18:8, Ezekiel 18:21, Daniel 4:37, Joel 2:13, Yona 3:8, Zekaria 1:4, Luka 19:8, Matendo 8:22, Ufunuo 2:5

Katika 2Nyakati 2:17 mara nyingi inazungumza kama kanisa(au makundi ya wapendwa) watajinyenyekesha wenyewe, na kuomba, na kuutafuta uso wa Mungu na kuacha njia zao mbaya, Mungu ndio ataponya nchi.

Tutakapoziacha njia zetu mbaya, Mungu ataiponya Tanzania.

Geofrey

Advertisements

6 thoughts on “Kutubu kwa ajili ya Tanzania.

 1. Shalom thanks my brother,
  nimelielewa swali lake lakini issue ni watatubuje wasipohubiriwa?…Ebrania ndo ninaposema utakatifu uanzie kanisani, kujitoa, upendo wa kweli ndani yetu itafanya hata wanaohubiriwa wasikie na watubu…”mkipendana watu watajua nyie ni wanafunzi wangu…Yohana” Huwezi kumwambia mtu asiwe mwizi, asiwe fisadi awe na upendo wakati hamjui Yesu. Injili itamfundisha yote hayo, huwezi kuvuna zabibu katikati ya michongoma (kati ya taifa lisilookuwa na waokovu wa kutosha) na kikubwa sio kwamba hakuna hata mkristo aliye karibu na raisi, aliye waziri, aliye mbunge? wote hao wakiwa karibu nae wanamhubiria neno au wao ndio wanapokea tu yake? kanisa tuamke tuombe utakatifu upya, toba kisha turudi kupeleka injili tukiomba ipokelewe. Ubarikiwe

 2. Yes sister Rosemary, there is a “secret” in Jubilee (50 yrs).
  I agree with you on steps to take regarding Tanzania.

  What ever the matter, characters or situation; “WE HAVE TO ASK GOD FOR HIS MERCY”
  As per original post; “Utatubu kwa ajili ya kila fisadi? kila anayeharibu mimba? kila mzinzi nakadhalika? Ni suala la moyo wa mtu binafsi, tuombe kwa ajili ya Tanzania Mungu atupe watu, atupe macho tuone, tuingie Ikulu na kumwambia Raisi Acha A B C ili Mungu aokoe nchi yetu.” – I advice you brother Geofrey to start looking for appointment with the president of URT, Mr. J.M. Kikwete and tell him “the message”. Before doing that you may call a press, write to newspapers, books etc.

  With considerations of my comments we should not forget “WHO CONTROLS WHAT, WHEN, HOW AND AT WHICH AUTHORITY”.

 3. Leo ni mkesha wa miaka hamsini ya Tanzania kujitawala:
  Mambo ya Walawi 25:10-14 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile….Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. ..Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa.

  Jamani naomba tumwombe Mungu toba tulipomkosea, pili tuombe huu mwaka uwe mtakatifu (kuanzia 9 december 2011)
  …..kuwa huru, kuirejea milki yetu ni kuwa na uwezo wa kujitawala na kumiliki.
  Tumwombe Mungu kwa ajili ya kanisa kutawala na kumiliki si kiroho tu bali kimwili pia. nipo Zanzibar muda, jinsi kanisa linavyotendewa huku ni kwamba haliko huru kimwili ingawa kiroho tunatawala na kumiliki lakini kimwili wananyanyaswa sana, tuombe na maeneo yote ya Tanzania ambako injili ya Mungu haijafika iwafikie.
  Katika yubilee Mungu anatuasa kuishi ktk upendo kwani Yeye alitukomboa utumwani: tuwaachie wadeni wetu, watumwa au wajakazi ambao tunaweza wasaidia wakaanza maisha huru, ndugu ambao hawana uwezo. Tuombee hili ktk kanisa la leo ambapo upendo wa Mungu umepoa mno, hakuna kujaliana wala kusaidiana kama kanisa la Mwanzo,
  Tuombee injili (uhuru) uenee nchi yote, tusijazane mijini au ktk maeneo ya kabila zetu tuwakumbuke watanzania wavisiwani kwa hali na mali wanapohangaika kupeleka injili.
  Tumwombe Mungu azidi kuliweka huru taifa letu kutoka mikononi mwa shetani na kuwa taifa huru lenye amani chini ya utawala wake (Injili ienee Tanzania yote). Ee Mungu Ufalme wako uje! Mbarikiwe

 4. ni 2nyakati 7:14,sio 2nyakati 2:17. ubarikiwe kwa somo ila naomba tuwe watendaji wa Neno na sio kusifia tu kwamba somo ni zuri.tuanze sisi watu tuliookoka kuingia ikulu na sio kusubiri watu wasio mjua Yesu.
  ubarikiwe mwandishi na watoa maoni

 5. “Tutakapoziacha njia zetu mbaya, Mungu ataiponya Tanzania”

  Ni kweli kabisa mpendwa Geofrey: Tukiacha woga, wizi, uvivu, uongo, ufisadi, uchoyo, chuki, fitina, hila, ubinafsi na mambo yanayofanana na hayo, hapo ndipo nchi yetu itasitawi na hapo ndipo uponyaji wa nchi utakuwa umeingia!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s