Nabii Flora

Nabii Flora akiwa kanisani kwake

Akimtabiria mtu

Hivi karibuni jijini Dar es salaam kuna nabii mwingine mpya ambaye amekuwa maarufu kutokana na wingi wa watu wanaohudhuria kanisani kwake na kupata huduma za kiroho. Anajulikana kwa jina maarufu kama Nabii Flora, watu wamekua wakiongelea kazi na shuhuda zinazotokea mahali anapohudumu, kwamba watu wanaponywa magonjwa yote sugu, vipofu wanaona, uvimbe na kila aina ya magonjwa na matatizo mbalimbali.

Mwaka 2011 pamekua na makanisa mengi ambayo watu wanakimbilia kupata huduma za kiroho na kimwili. Na Nabii Flora ni mmoja wa manabii ambaye amefanikiwa kupata watu wengi.

Advertisements

42 thoughts on “Nabii Flora

 1. Kujiita nabii wewe mwenyewe na kuitwa nabii na watu vyote lazima viwe matokea ya kazi au huduma unayofanya.

  Kwa hiyo huduma ndio kigezo cha wewe kuwa nabii. Uamue kujiita au watu wakuite, wewe bado ni nabii. Uamue kutojiita au watu waamue kutokukuita, wewe bado ni nabii

  Men

 2. Mimi naomba tu kuuliza swali.Hivi kuwa nabii ni mtu mwenyewe anajiita, watu wanamuuta au huduma anazotoa ndio zina-determine aitweje? kama nikimnukuu nd. Sungura hapo juu kwenye paragraph hii “Kama huyu dada angesema ni mwinjilisti, au mwalimu najua isingekuwa ishu. Kwa sababu tunadhani kuwa mtume na nabii ni watu wenye huduma kubwa zaidi kuliko mwalimu, na mwinjilisti, ndo maana kujiita kwake nabii kumekuwa ishu” napata picha kwamba ni kama mtu mwenyewe ndio anaamua na baadae kusema aitweje. Naomba kuelimishwa

  Mbarikiwe
  .

 3. Sungura, unasema, “Mimi nashindwa kuelewa nini hasa tunajadili katika hii mada: Je ni Flora kuwa nabii, je ni huduma ya nabii, au je ni manabii wa uongo?”
  Swali langu kwako ni kwamba, katika hayo uliyoyachangia, umelenga kipi kati ya hayo uliyosema huyaelewi kinachojadiliwa?

  Ubarikiwe

 4. Mimi nashindwa kuelewa nini hasa tunajadili katika hii mada: Je ni Flora kuwa nabii, je ni huduma ya nabii, au je ni manabii wa uongo?

  Kama Yesu alisema kuhusu manabii wa uongo siku za mwisho ina maana alimaanisha huduma ya nabii ipo bado.

  Nisichokipenda kwa wapendwa wengi, ni kwamba kikitokea tu kitu ambacho ni kigeni kwao utasikia; Oh tujihadhari hizi ni siku za mwisho, Oh baba tupe macho ya kuwatambua manabii wa uongo n.k. Kwa nini usimwombe Mungu akupe macho ya kuwatambua manabiiwa kweli kwanza?

  Sifa na kazi za nabii zinajulikana kwa yule anayesoma neno la Mungu.

  Nabii ni mtu anayesema mambo yatakayotokea. Kwamba anasema kwa taifa au kwa mtu binafsi hivyo ni viwango tu vya utumishi wake. Lakini kama yatatokea basi huyo ni nabii wa kweli, la hayatatokea basi huyo ni nabii wa uongo. It’s simple like that!

  Kuna manabii walimtabiria Paul (asomaye na afahamu), lakini hatuendelei kuona kama waliendelea na kutabiri mambo ya litaifa au kimataifa, lakini biblia imesema walikuwa manabii wale.

  Kama Flora anatabiri mambo yajayo na yakatokea kama alivyotabiri, basi huyo ni nabii bila kujali jinsia yake wala umri wake, wala utaifa wake.

  Lakini kama anasema tu mambo yaliyo ndani yangu, uvimbe alionao mtu, mpango wa Mungu juu yangu au hila za shetani juu yangu, basi siyo nabii ila ana karama ya ufunuo, neno la maarifa na karama ya unabii.

  Tatizo letu wapendwa ni vyeo.

  Kama huyu dada angesema ni mwinjilisti, au mwalimu najua isingekuwa ishu. Kwa sababu tunadhani kuwa mtume na nabii ni watu wenye huduma kubwa zaidi kuliko mwalimu, na mwinjilisti, ndo maana kujiita kwake nabii kumekuwa ishu.

  Wajinga sisi, Yesu hakuwahi kusema kuwa yeye ni mtume mzuri,wala nabii mzuri, bali alisema yeye ni mchungaji mwema, na aliitwa rabi – yaani Mwalimu.

  Asiyekuwa kinyume chetu huyo ni mmoja wetu, hata kama haambatani nasi!

 5. Nelson David,
  Je, si vema sana basi kusema kuwa tukiwa na shida tutamtafuta Kristo kuliko huyo nabii? Tufuate mkate?

 6. aisee nyinyi mnaombeza huyu nabii hamjapatwa na shida ila ukiwa na matatzo utamtafuta2.

 7. Bwana Yesu asifiwe mie ni mmoja wa watu wanaoshuhudia maajabu ya Flora huyu dada katumwa na mungu na kazi yake inaonekana mie kamwombea mwanangu akiwa amelazwa Agakhan hosp alikuwa hajitambui lakini leo anacheka namshukuru sana Mungu kwa kumtumia huyu nabii na isitoshe ana upendo na huruma ya hali ya juu sana Mungu ambariki sana.

 8. Jamani mimi naona tunatoka nje ya mipaka, manake kama sisi wenyewe kwa wenyewe tunakandiana na kutokuaminiana kihivi, je wasio wakwetu itakuwaje? wakitunyari tutalalamika?Kuna wengi wamesaidika sana * milion kwa hawa watumishi so naomba tuwe na imani kwani hakuna mtu anayelazimishwa kwenda kwa mtumishi yeyote ila shida nyingi na mahitaji mengi tuliyo nayo ndiyo yanayosababisha tutafute msaada, kwa maana hiyo basi naomba msihukumu msije mkahukumiwa kwani uwezo wa kumjua nabii wa ukweli na wa uongo ni mwenyezi mungu peke yake anao. Hata kama pazia lilipasuka bado kuna shida watu hawajui kuomba, hawajui kufunga, hawajui kukesha, wana imani haba, wamekata tamaa na mengine mengi mengi so naomba kila mtu anyamaze kimya aache watu watafute msaada.
  Shalom.

 9. Tufanye hukumu zisizoacha shaka kabisa(beyond reasonable doubt).
  Nabii ni yule mtu anayetabiri mambo yajayo nchini mwake au nje ya nchi yake na yakatokea kama vile alivyotabiri. Ni yule anayetabiri yanayokuja au yaliyojificha akayafunua kwa watu iwe yalishapita, yapo au yanakuja na yanatokea vile vile bila kupungua kitu. Nabii anayewatabiria waumini wake tu waliofika kanisani kwake huyo siyo Nabii bali ni Mwinjilisti mwenye karama ya Unabii na wala siyo Nabii. Nabii ambaye hajawahi kutoa unabii kwa Taifa lote au nchi yoyote Africa au kokote na yakatokea kama alivyotabiri, huyo siyo NABII? Huyo ni muhubiri tu wa kawaida mwenye karama za mafunuo, basi.

  Manabii wote tangu kale walitabiria taifa lote na siyo mtu mmoja mmoja tu kama ilivyo leo makanisani mwetu hasa Dar imezidi.

  Tunataka Nabii anayeweza kutabiri mambo yajayo hapa Tanzania au Afrika kuhusu uchumi, fedha, Uchaguzi, Viongozi wa taifa, hali ya hewa, nk.

  Lakini manabii wanaowatabiria watu kwamba wana uvimbe tumboni, wana matatizo ya ndoa, wana mapepo, wanaotabiria watu kwamba kesho watapata fedha kisha wakaishia makanisani mwao hao siyo Manabii. Ni wachungaji wenye vipawa vya ufunuo wa rohoni, na karama za unabii.

  Nabii Flora huenda akawa Nanbii au asiwe Nabii endapo tu vigezo hivyo na vile vya maandiko hataweza kuvitimiza.

  Definition of a True Prophet:
  A true prophet from God must bring forth prophecy that crosscuts a nation or nations on normal life issues and spiritual affiars as well. Hii ni tafsiri yangu. Niko tayari kukosolewa au kufundishwa.

  Nasubiri utafiti wa kiupelelezi (Investigative Research) kuhusu Nabii Flora.

  Milinga

 10. hakuna nabii anayechunga kanisa. kazi za kuchunga ni za wachungaji. ndani ya biblia hakuna nabii anayekaa nakuongoza kanisa la mahali pamoja. hawa wanaojiita manabii halafu wakachunga ni waongo hajui wanalofanya. kuponya wagonjwa sio ishara ya manabii, ni ishara ya mwamini yeyote. Thank you.

 11. Strictly Gospel,
  Kazi yenu si ya bure, pia Ono lenu na kanuni mliojiwekea ya kulifikia hilo, nina uhakika inajitambulisha katika jina lenu!
  Basi ninawaombea Mungu awapeni nguvu zake zaidi ili msimame katika Ono lenu, awaongezeeni Hekima yake katika kutuhudumia na kutuvumilia haswa pale tunapojaribu kuwavutia katika upande wetu ambako hata Ono letu hamlijui! Pia fursa mliyoitoa ni changamoto kubwa sana kwa yeyote anayeujia Ukristo, maana kwa changamoto hizo atajua kuwa Ukristo ‘sio le le mama’!
  Bwana awabarikini katika yote yenye kumtukuza Yeye.

 12. Strictly Gospel,

  Asante kwa hilo, Nashukuru pia kwa kazi yenu ya Moderation, naona mnapenda kutuacha huru kutoa mawazo yetu…..lakini labda uhuru mliotuachia ni mkubwa mno….maana hata lugha zetu zinakua kali mno…zinaweza hata kuwakwaza wengi.

  Lakini jambo jingine ambalo naona ni la msingi kuwa hata ninyi mnatakiwa kutoa hitimisho la baadhi ya mada zisiachwe zinaelea! Kuna maswali yanaachwa bila kujibiwa au yanajibiwa kinyume na Maneno ya Mungu,Hivyo hitimisho lenu ni Muhimu sana…..kumbukeni baadhi ya wanaoandika wengine si Wakristo kwa maana ya kumjua Bwana kama Mwokozi, au wenye mitazamo tofauti….hivyo nyie wenye Blog mngekuwa mnaturidisha kwenye msimamo wenu…….hasa mnapoona mada inachukua muda mrefu.

  Na pengine kuhitimisha mada kama hii ya manabii , mngeweza kuleta hata waalimu wakristo wenye opposing views au balanced views ili kusaidia Wakristo kutambua mitazamo tofauti ambayo ingetusaidia kuliko kuwa na view moja to the exreme.

 13. Bwana Yesu Asifiwe ndugu Orbi na C K Lwembe. Mjadala au maelezo kuhusu huduma ya kinabii tumehamishia kwenye mada ya KAZI YA MANABII NI IPI? Ili iwe katika mtiririko unaoeleweka badala ya kujadili kwenye mada inayomhusu Nabii Flora. Mungu awape neema katika kuchangia, tujifunze kupitia ninyi. Shalom

 14. Ndugu Lwembe,

  Hivi kwa nini hujiulizi kwa nini Agano Jipya…….Tahadhari juu ya Manabii wa uongo ni kubwa?
  Kama utachukua Biblia yako na kuayaangalia Maonyo ya Bwana wetu Yesu utaona Maonyo dhidi ya Manabii wa uongo inachukuwa sehemu kubwa katika mafundisho yake…..Kuliko kuwasikiliza na kuwakubali…….kwa kifupi sioni mstari kutoka kwa Yesu unaonisisitizia niwasilikize Manabii……..Hebu angalia….

  1 Wapendwa msiziamini kila Roho……….1John 4:1

  2.Jihadharini na Manabii wa uongo wanaowajia wamevaa mavazi ya Kondoo…..Mathew 7:15

  3. Na Manabii wengi wa Uongo watatokea na kudanganya wengi…….Mathew 24:11

  4. Kwa maana wataondoka Makristo wa Uongo, na Manabii wa Uongo,watatoa Ishara…..Marko 13:22

  Kwa mistari hiyo tu hata kabla sijaja kwa mafundisho mengine ya Agano jipya na hasa kutoka kwa Paulo, kwa nini basi NISICHUKUE TAHADHARI KWA MTU ANAYEJIITA NABII? Nadhani aliye wa Kiroho na aliye na mwalekeo wa KUTII alichosema YESU atachukua Tahadhari….kwa sababu mafundisho ya Bwana wetu yanasema hivyo! Na yule ambaye ni mchanga Kiroho au asiye na Utii kwa Maneno ya Mungu ataonekana na kuyakimbilia yale na kuyaparamia yale yaliyoonywa na Yesu!

  Kwa kifupi kabisa ni afadhali kuchukua tahadhari kwa watu/Mtu anayejiita NABII kama anavyotufundisha Yeremia na Manabii wengine wa Agano la Kale kuliko kuwakimbilia Manabii hawa……Hebu angalia onyo kuhusu Manabii kutoka Agano la Kale

  1. Ndipo Bwana akaniambia, HAO MANABII wanatabiri uongo kwa JINA LANGU MIMI, MIMI SIKUWATUMA, WALA SIKUWAAMURU,WALA SIKUSEMA NAO,WAWAPENI UNABII WA MAONO YA UONGO…..Yeremia 14:14-15

  2.Nimesikia waliyosema Manabii, wanaotabiri uongo kwa jina langu…….Wakisema nimeota ndoto……nimeota ndoto……..Je mambo hayo yatakuwa moiyo ya manabii wanaotabiri hata lini…….Yeremia 23:25

  3. Tazama, mimi ni juu ya Manabii Asema Bwana….wanaotumia ndimi zao kusema Yeye asema Yeremia 23:31

  Sasa ndugu yangu Lwembe hii ni sehemu ndogo mno katika Maandiko ya Agano la Kale linaonya kuhusu Manabii……Hebu njoo basi na Mafundisho yako ambayo YANASISITIZA tuwasilikize Manabii kutoka kwenye Kinywa cha Yesu! Narudia tena kutoka kwenye andiko la Kitabu cha Waebrania……..

  “MUNGU AMBAYE ALISEMA NA BABA ZETU KATIKA MANABII KWA SEHEMU NYINGI NA KWA NJIA NYINGI NA KWA NJIA NYINGI, MWISHO WA SIKU HIZI AMESEMA NA SISI KATIKA MWANA ALIYEMWEKA KUWA MRITHI WA YOTE TENA KWA YEYE ALIUFANYA ULIMWENGU….(Heb 1:2)

  Ndugu yangu hebu angalia huyo Mwana aliyewekwa na Mungu anasema nini na sisi kuhusu hwa Manabii na mitume! Sauti ya Mungu ni hakika kwa kupitia Neno lake……sidhani ni hili lindi la Manabii…..ambao kila leo wanaumuka kama uyoga na wala hatuona sauti yoyote yenye mguso wa Kinabii toka kwa Bwana!

 15. Lwembe,

  Hebu ndugu yangu simama katika maandiko! Hicho kipimo chako cha DNA nini? Kumbuka unaweza kuchukua Maandiko ukayalazimisha yasema yasichosema! Na kufanya yasema unachotaka kusema! Na ndio unachofanya wewe kwa mtazamo wangu!

  Narudia swali lako la awali ….ambalo kwangu sasa linatilia shaka uelewa wako imani hii, na kunifanya kutilia mashaka mno Ukristo kwako una maana gani…….na umeshindwa kabisa kulijibu swali bali kulitetea pasipo hata kusimama katika Maandiko!

  “Basi mtu akikuambia yeye ni nabii, muulize kwanza iwapo yeye mwenyewe amebatizwa maji mengi kwa jina la Bwana Yesu Kristo ili kuziondoa dhambi zake hata sasa kapewa hicho kipawa cha unabii?”

  Kwa hiyo wewe ni zaidi ya Bwana wetu Yesu? Maana yake hakuja na hiyo DNA unayoizungumza…….alisema kwa lugha rahisi kabisa na inayoeleweka……”MTAWAJUA MANABII WA UONGO KWA KWA MATUNDA YAO” ……..Wewe unasema utawajua kwa UBATIZO WA MAJI MENGI” Ni nani tumsikilize basi …..wewe au Maandiko?

  Hebu nipe kwa urahisi kabisa listi ya manabii katika AGANO JIPYA……Na kwa lugha lugha nyepesi kabisa na tumia MAANDIKO kutetea hoja yako…….walifanya nini……..au Maandiko katika Agano yanawapa nafasi gani! Hebu jibu swala hili……mAFUNDISHO YA YESU yalikuwa yako wazi kwa kila jambo…….mbona maelezo yako ni very complicated? Au ndio kuwa wa Rohoni unakokuzungumza? Kwa kifupi naamini ulichoandika si kwangu tu….Naamini hata ukimuuliza msomaji yoyote ule unasema nini……sidhani unaeleweka!

  Halafu naona kwa maandiko yako unatisha kama sio kushangaza ….au Labda hujui unachoandika kina maana gani……hebu soma tena nukuu yako hii………

  “Tena ukaniona kama mtu ninayeleta mafundisho mapya, yaani kwa namna nyingine ukaniona kama nami ni mmoja wa hao manabii utitiri, hujayakagua tu Maandiko!”

  Hivi wewe ni nani hasa! Wewe ndio kipimo cha kuyafahamu Maandiko? Kwa hiyo tusipoyafahamu Maandiko kama unavyoyafahamu wewe……..tunakuwa hatujayakagua Maandiko? Wewe ndio kipimo cha kufahamu Maandiko?

  Kwa nini unawasiwasi na unachokiandika….kwa nini unafanya kigezo cha kuyajua Maandiko ni kukuelewa wewe? Nadhani kwa mtazamo huo Sitakuelewa…..na Labda kwa mitazamo kama hii inafanya waumini wengi leo washindwe kabisa Kuielewa huduma hii ya Manabii unayojaribu kuitetea! Na kama kweli wewe ndio kinywa cha Manabii…..basi Kanisa bado lina safari ndefu mno kuwaelewa “manabii” ambao Bwana atakuwa ametushia katika kizazi chetu!

 16. Ndugu yangu Orbi,
  Ninakushukuru kwa maelezo uliyoyatoa, ingawa kwa maelezo yako inaonekane swali lako la msingi uliloliuliza mwelekeo wa jibu lake ulikuwa nao tayari kibindoni. Hata hivyo jibu nililokupa lilikuwa ni la jumla katika kukujibu Nabii ni nani. Kutokana na maelezo yako mapya, inaelekea unahitaji muda zaidi wa kuyatafakari Maandiko ili kupata kina chake, yaani context funzo.
  Nilipokuletea mifano ya Agano la Kale, nia ilikuwa kukuonesha tofauti ya viwango vya manabii katika utendaji wao kulingana na umuhimu wa Neno walilolibeba. Kwamba hujaweza kuiona tofauti ya viwango vya manabii, hilo pekee litakulazimu kuchukua wasaa wa kulitafakari Neno la Mungu upya. Kwani iwapo hutaweza kuwatofautisha manabii katika viwango vyao vya utendaji, utasumbuka sana!
  Nilikupa mfano wa Nabii Elisha ambaye nilikueleza kuwa huyu alikuwa ni wa kiwango cha yule ndege ‘tai’ ili kwa uwezo wake wa kuruka juu, uwe mfano halisi wa kumtofautisha na wale manabii wengine wa kidhebu wale niliokwambia ni wa mfano wa yule ndege ‘mwewe’, waliokuwepo siku hizo ambao waliweza kutabiri kuondoka kwa Nabii Eliya sawasawa, lakini hawakuweza kujua amekwenda wapi hata wakajitolea kumtafuta milimani na mabondeni kwa siku tatu mfululizo wasimuone!
  Pia inaelekea hujayatazama Maandiko vizuri maana unaposisitiza kuwa Mungu katika Agano Jipya hakutoa prominence kwa manabii, unapaswa kwanza ujiweke katika uelewa wa uhalisia wa huduma iliyofanyika katika viwango vyote viwili: kiwango cha Kanisa la Kristo na kanisa la Mpinga Kristo. Haya ni makanisa mapacha. Kuyatofautisha utahitaji vipimo vya DNA!
  Kwa taarifa yako Mungu ametoa prominence kubwa sana ya huduma hii ya unabii katika Agano Jipya kama ilivyo katika Agano la Kale, katika makusanyiko yetu madogo madogo. Kama nilivyoelezea katika jibu langu la awali ambapo pia nilikuonesha na vifungu vinavyo wasimamisha manabii katika vipawa vinavyo paswa kuwepo katika kusanyiko lolote lile linalowakilisha Kanisa la Kristo. Manufaa ya vipawa hivyo kwa kanisa yako wazi. Huduma iliyofanywa na Mitume, kimsingi, ilikuwa ni huduma ya kinabii iwapo utaitazama katika jicho la kiroho. Manabii waliongozwa na Roho Mtakatifu kuyanena yote waliyoyanena kama ambavyo Mitume pia walivyoongozwa kuyafundisha yote waliyoyafundisha hata kuwekwa katika Biblia yakiwa na Nguvu ile ile. Kwa hiyo kudhani kwamba Mungu hajaipa umuhimu huduma ya unabii katika Agano Jipya ni kutokufahamu tu, Mitume walikuwa ndio Manabii wenyewe katika kiwango cha wale ‘tai’. Mambo makuu yote ya Mungu wametuletea hapa chini! Na wale manabii wa kiwango cha Agabo ndio hawa tulio nao katika makusanyiko yetu. Tazama Agabo alipokutana na Mtume Paulo, alimtabiria yatakayomfika lakini Paulo akiwa ni yule ‘tai’ aliendelea na safari yake kwenda kukabiliana na hali hiyo akiyajua yote; ya mateso na ya faida kwa kanisa!
  Hao ni manabii wa Kanisa la Kristo kwa upande mmoja. Kwa upande wa Mpinga Kristo, nako kuna kanisa kama hili la Kristo, likijitahidi kuigiza vipawa vyote. Huenda hili ndilo linalokuchangaya ndugu Orbi! Hili kanisa lina vitimbi vingi na kelele nyingi sana. Vikundi vya kanisa hili vina mashindano mengi sana, kwa hiyo misisimko yake ni mikubwa kidogo katika kuigiza na kushabikia mafanikio. Sasa, pia unapoyatazama Maandiko kwa jicho la mafundisho yaliyo nje ya mpangilio ni rahisi sana kuyaacha maonyo yote humo, ukitayatazamia kutimia kwake katika siku za mbele wakati yakikutimilia hapo hapo pasi wewe kujua! Mathayo 24:24 inasema: “Kwa maana watatokea makristo na manabii wa uongo … wapate kuwapoteza…”, basi ndio hawa hapa, huu utitiri wa manabii na wapakwa mafuta waliopo uwanjani leo hii wakilitimiza hilo Neno la Mungu kama lilivyosema, nao maelfu tunadanganyika . Wengi wetu tunapoambiwa ‘makristo wa uongo’ mawazo yetu hutengeneza taswira ya watu watakao jifanya ni Yesu Kristo kimwili kama yule ‘Yesu’ wa Urusi, halafu ndio watawadanganya watu, la hasha. Ukweli ni kwamba maana ya neno kristo ni mpakwa mafuta! Kwa hiyo hawa watakuwa na UPAKO. Nao UPAKO huo ndio unaowawezesha kuwadanganya watu na kufanya miujiza na kuleta unabii; bali hawakutumwa na Mungu. Tazama ilivyokuwa katika ile siku ya kutimia hukumu kwa Ahabu ilikuwaje. Ahabu alikuwa na manabii 400 waliomtolea unabii uliompeleka kifoni, wao walimwambia aende vitani, Bwana yu pamoja naye (2Nya 18:4-5). Lakini yule nabii ‘tai‘ Mikaya alimwambia hatarudi kutoka vitani kama ilivyotokea! Nayo makundi yetu ya manabii ya leo ndiyo hayo kama ya wakati ule wa Ahabu, itamchukua Yehoshafati wa leo mwenye ujuzi wa Neno kujua kuwa hawa SIO, vinginevyo makundi yote yanakwenda kutumbukia mtoni! Bwana, kuhusu hawa manabii waliorundikana leo hii uwanjani, anasema katikaYeremia 23:31-32 “Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema. Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi; lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA.” Hiyo ndio hasara tunayoiendea.
  Ndugu Orbi msururu ni mrefu sana ila sijui kama unaelewa. Yaani manabii wa uongo wapo, tena wanajulikana kama manabii hivyo hivyo, bali unapaswa uwe na kile kipimo cha DNA ambacho wewe yaonekana hukikubali, basi sijui hata utawatambuaje. Hebu mtazame huyu nabii mwingine aliyekuwepo wakati wa Nabii Yeremia, anaitwa Hanania Yer 28:1. Huyu alisimama akatabiri kinyume na Yeremia, akautoa unabii wake mbele ya Yeremia na mbele ya makuhani na watu wote akisema ‘BWANA asema’. Basi endelea mwenyewe kusoma uone yaliyomfika kama ambavyo hawa wa leo yatawafika katika siku yao!
  Nilipokupa kile kipimo cha DNA ili uweza kuwatambua manabii wa uongo mapema, umenishangaa kama vile nimeingia na chura sitting room kwako! Bali nimeingia na lulu! Ukristo wako unanitia mashaka kidogo maana UBATIZO ndio unao kuingiza katika Ukristo, yaani lile Kanisa la Kristo. Yaani kupitia Ubatizo ndio unakuwa “INITIATED into Christianity”. Hebu litazame lile kusanyiko la kwanza liliingiaje. Wao walipohubiriwa na Mtume Petro, waliipokea ile Injili na kufuata maelekezo aliyowapa. Nanukuu: Mdo 2:37-38 ‘Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili… na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie’. Vipawa vya Roho Mtakatifu vya kweli hupewa hao waliopitia mlango huo alioufungua Petro siku hiyo ambayo kulingana na hilo andiko jambo hilo hufanyiwa wote walioitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Sasa kwamba wewe hufahamu hata dhambi zako zinondolewa katika stage gani, hilo limenishangaza kuliko ulivyonishangaa wewe! Matunda Biblia inayoyaongelea ni mafundisho yao!
  Yeyote aliye na vipawa nje ya utaratibu wa Mungu, huyo ni dhahiri kuwa ni mtumishi wa lile kanisa jingine. Wote aliowaita Mungu wamjie wanapita katika ubatizo huo alioufundisha Petro na Mitume wote. Ndio maana nilikupa hicho kipimo ili uweze kukitumia kuyatenganisha makanisa haya! Mungu ametuwekea hapo katika urahisi. ‘Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto…’ (Rum 11:29), basi utitiri wa manabii hawa wasioongozwa na Mungu wapo hapa kwa ajili ya kuwapoteza wote ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo (Ufu 13:8).
  Halafu sehemu nyingine umesema huelewi kabisa nina maana gani niliposema:
  ‘Basi hali ndivyo ilivyo kwa wa kiroho atayapokea hayo na kwa mjinga naye atafanya analolijua mwenyewe, yaani kuendelea katika ujinga wake!!!’
  Tena ukaniona kama mtu ninayeleta mafundisho mapya, yaani kwa namna nyingine ukaniona kama nami ni mmoja wa hao manabii utitiri, hujayakagua tu Maandiko! Mungu katika Agano Jipya ametamatisha michezo yote ya kuigiza Injili, hali zote amezileta katika conclusion. Yaani, tunapoendelea na michezo yetu ya dini, tukiwa kwa makusudi tumeikataa Injili ya kweli, yale maagizo yatupasayo, Roho Mtakatifu kupitia watumishi wake mitume, ndiye aliyeikamilisha hali hiyo ambayo kwa wa kupotea hutaweza kutoka humo kwa upande mmoja na yule wa kiroho, yaani wa Ufalme wa Mungu pia huendelea mbele katika vinono vya Ufalme. Basi mtume Paulo akijenga Msingi wa Ufalme huo kwa mataifa, akitundisha mabo yote yahusuyo Ufalme kama wanawake kutokuongoza makusanyiko au kutawala wanaume, kanisa kutawala kunena kwa lugha nk, akatamatisha kwa kusema katika 1Kor 14:37-38: “Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.”
  Basi ndugu yangu Orbi hali ndivyo ilivyo!!!
  Mungu na atupe sote ujasiri wake!

 17. kwako Yohana, hivyo tatizo lako kuu kwavile ni mwanamke?????? uache wivu. Mungu hana upendeleo nani amtumikie nani asimtumikie, kwa Mungu hakuna huyu ni mtu mke au mume wote ni sawa kwenye ulimwengu wa roho.

 18. Jamani hawa manabii wa Taifa wanashindwa hata kutuambia kuwa kuna janga la mafuriko tujiandae…….? Agabo katika Matendo ya Mitume alilionya Kanisa kuhusu Njaa itakayoshukuia Jerusalem? Unabii wao uko kwa lipi hasa? Kwa nini wasikubali kuitwa Wachungaji tujajua moja?

 19. Ndugu Lwembe,

  Umezungumza mengi lakini vigezo ulivyotumia kuwachambua Manabii na kuwagawanya kwangu mimi naona havisimama vyote katika wigo wa Maneno ya Mungu……Sina haja ya kurudi tu Agano la Kale na kuona kila Nabii aliitwa na Mungu kwa njia ya pekee na kusudi la pekee nikiweka Orodha na kwenda na Nabii mmoja mmoja hapa ambao wameorodhesha Agano la Kale utaona kabisa vigezo ulivyotumia wewe ni hafifu MNO.

  Na sijaona kabisa ukitumia AGANO JIPYA kutetea huu UTITIRI wa manabii uliopo leo! Hebu rudi katika Kitabu cha Matendo ya Mitume na uangalie Kazi ya Manabii katika kitabu hicho katika hatua za awali na za msingi za kulianzisha na Kulijenga Kanisa, Je unaona Mchango wa Manabii hapo? Kama Roho Mtakatifu mwenyewe hakuwapa prominence manabii katika Maandiko haya ya Msingi ya kuanzisha Kanisa sembuse sisi? Hebu nipe orodha ya Manabii katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ni AGABO pekee katika hilo “KUNDI LA MANABII” aliyeandikwa, Wako wapi wengine? Nini walifanya? Na pengine ndio maana Kitabu cha Matendo ya Mitume kimeitwa hivyo badala ya “MATENDO YA MANABII” Kwa kifupi ndugu Lwembe Kanuni mojawapo ya msingi katika kulisoma Neno la Mungu na kulielewa ni kuwa Lisome kwa kuangalia Roho Mtakatifu aliruhusu nini Kiwepo kwenye Maandishi! Alichokiandika ndio na sisi tuhahitaji kukifundisa na kukifuata! Neno la Mungu katika Agano jipya halijatoa Prominence (umuhimu mkubwa wa manabii) Katika kuliongoza Kanisa, Hakufanyika kipindi cha Matendo ya Mitume…..na HAKIJABADILIKA LEO! Kinachofanyika leo na utitiri wa Manabii ni si kile kilichofanyika katika Kanisa la Mwanzo na maadamu hakijasimama katika mafundisho ya Neno la Mungu hakitafanya chochote kuisukuma kazi ya Mungu Tanzania bali kuwaaacha waumini wazidi kuzunguka Jangwani!

  Lakini uliponishangaza zaidi ni pale uliposema jinsi ya kuwatambua manabii na mimi Nakuu hapa chini……..

  “Basi mtu akikuambia yeye ni nabii, muulize kwanza iwapo yeye mwenyewe amebatizwa maji mengi kwa jina la Bwana Yesu Kristo ili kuziondoa dhambi zake hata sasa kapewa hicho kipawa cha unabii?”

  Kwa hiyo vigezo vya kumtambua Nabii ni Ubatizo wa Maji Mengi? Na ubatizo wa Maji mengi unaondoa dhambi? Naona haya ni mafundisho mageni kabisa kwangu…..!Je unaweza kutumia ubatizo uwe wa maji mengi au machache kupima uhusiano wa Mtu na Mungu? Na hasa katika kumtambua Nabii? Je Yohana mbatizaji alibatizwa? Maana alikuwepo kipindi cha Yesu…….Kwa kutobatizwa kunafanya kazi yake ya kinabii kuwa batili?

  Hebu angalia Yesu alisemaje kuhusu kuwatambua manabii wa uongo

  “JIHADHARINI NA MANABII WA UONGO WANAOWAJIA WAMEVAA MAVAZI YA KONDOO…LAKINI KWA NDANI (sio kwa nje ambako unaweza kupapima au kupatambua kwa vitu kama ubatizo/Kuhubiri/kuponya wagonjwa nk) NI MBWA MWITU WAKALI…..MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO” Mathew 7:15

  Halafu sielewi kabisa una maana gani unaposema hivi….nanukuu……

  Basi hali ndivyo ilivyo kwa wa kiroho atayapokea hayo na kwa mjinga naye atafanya analolijua mwenyewe, yaani kuendelea katika ujinga wake!!!

  Sielewi hapa una manaa ipi hasa…..una maana atakayeyapokea mafundisho yako? Au maelezo yako kuhusu manabii? Siamini kabisa mafundisho yako nayo yamevuviwa kama Maandiko? Labda uiweke sawa nukuu yako, kwangu mimi mjinga mtu yoyote yule anayemeza kila kitu chochote anacholetewa maadam maandiko Matakatifu yamenukuliwa! Waberoya katika matendo ya Mitume hawakufanya hivyo!

  Labda nimalizie kwa nukuu hii kutoka kwa Mwandishi tusiyemjua…….ambaye hata kwa kutojulikana kwake Maandiko yake yamepewa nafasi kama maneno ya Mungu

  ” MUNGU AMBAYE ALISEMA NA BABA ZETU KATIKA MANABII KWA SEHEMU NYINGI NA KWA NJIA NYINGI.MWISHO WA SIKU HIZI AMESEMA NA SISI KATIKA MWANA ALIYEMWEKA KUWA MRITHI WA YOTE TENA KWA YEYE ALIUFANYA ULIMWENGU”

  Hivyo kwangu mimi huu utitiri wa Manabii ambao umejazana Tanzania Leo ambao kwa kweli hatusikii hata LOLOTE MAALUMU TOKA KWA BWANA, Hatuoni tofauti zao na huduma za kazi za kichungaji na kulisha kundi la Bwana Neno lake! Hatuoni ujumbe wowote unaweza kuuita wa KINABII kuligeuza Taifa limrudie Mungu tofauti na Wainjilisti wengine wa kawaida tu wanaopiga kelele watu Watubu na Kuamini INJILI! Je manabii hawa kweli wametoka kwa Bwana?

  Hivyo ndugu yangu Lwembe,kwangu mimi hujanigusa kwa Maandiko kutetea hoja yako ya Kinabii……….Mungu na Akubariki…..na tuzidi kujfunza.

  UBARIKIWE.

 20. Ahsante C k Lwembe kwa kugusia andiko ambalo mie nilikuwa nikilifikiria:

  “wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena; bali watii, kama vile inenavyo Torati nayo…”

  Ndugu wapendwa,

  Sasa kwa mujibu wa hili andiko, nabii Flora yeye kama mwanamke anatumia Biblia ipi inayomruhusu kunena/kufundisha/kuongoza kanisa/kusanyiko?

 21. Nabii ni kinywa cha Mungu, ndugu Orbi!!!!

  Mungu huwatumia manabii kila anapotuletea ujumbe wake, tena hafanyi lolote lile bila kuwajulisha watuishi wake manabii kama anvyoliweka wazi jambo hilo katika kitabu cha Amos 3:7, ““Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote, bila kwanza kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.”

  Mungu ameigawa karama hii ya unabii katika mafungu mawili: Fungu la kwanza ni Manabii ambao husimamishwa mwisho wa kipindi au msafara unapofika katika njia panda ya wakati. Kundi hili husimamishwa hapo ili kuuchambua msafara huo, yaani kanisa, ili wale “… waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, …”(Yuda 1:4), hawa hupepetwa na hilo Neno nabii anaposimamishwa hapo. Yaani nabii wa kundi hili huja na Neno linaloifunga dunia yote katika mafurushi mawili; moja la kuokolewa na jingine la kupotea. Nao manabii wa kundi hili Mungu anawafananisha na yule ndege tai ambaye huruka juu sana kuliko ndege wengine wote, nao huko juu hulichukua hilo Neno na kushuka nalo hapa chini kwa ajili ya kusanyiko, hata hulionya kuhusu ghadhabu ya Mungu ijayo (Yer 48:40) au Neema.

  Basi Mungu, inapofikia kipindi hiki, humsimamisha nabii mmoja tu uwanjani kulileta hilo Neno ambalo huwa ni Neema kwa wale wa kuokolewa na pia huwa ni Hukumu kwa wale wakupotea. Mfano wa manabii wa kundi hili ni kama Musa, Eliya, Elisha, Samweli na wengineo tunao waona katika Biblia ambao Neno walilopewa na Mungu hata sasa lingali likituongoza. Manabii wa kundi hili huja na Neno lijengalo msingi wa kumjua Mungu, maana haiwezekani kumjua Mungu nje ya manabii ambao hutuletea mafundisho kumhusu Yeye kwa uongozi wa Roho Mtakatifu kama Maandiko yanavyotuonesha; 2Petro 1:21-“Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”. Na pia huja na Neno la upatanisho kwa kanisa lililoondoka katika njia ya wokovu na kuelekea kusiko, basi inapofikia hapo katika njia panda ya wakati Mungu humleta nabii kuwarudisha katika njia iliyo sawa. Kamwe Mungu hasimamishi manabii wa kundi hili zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja uwanjani! Nao manabii wa kundi hili hawatokei vyuoni bali wao Mungu huwatayarisha kwa kazi hiyo maalumu tangia tumboni mwa mama zao (Yer. 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”). Kwa mfano Yohana mbatizaji na Bwana Yesu Kristo walipokutana uwanjani, tunaona Yohana akitutangazia kuwa yeye inambidi apungue ili Kristo aongezeke

  Fungu la pili, ni manabii wanao hudumu ndani ya makusanyiko yetu madogo madogo ambao pia Mungu huwapa Neno la kulitakasa kusanyiko kulingana na shida iliyomo ndani ya kusanyiko hilo, kama ni uzinzi au uasherati au uongo au unafiki na uchafu mwingineo ambao hujificha ndani ya makusanyiko yetu. Na pia iwapo kuna neno la kuwatia moyo basi Mungu pia hulipitishia katika kundi hili. Hawa wanaweza kuwepo hata zaidi ya mmoja ndani ya kusanyiko, nao Mungu huwatumia katika kiwango hicho. Hawa, Mungu huwatumia wanawake kwa wanaume. Bali ieleweke kuwa wigo wa kundi hili ni makusanyiko yao tu, tena hawa iwapo watakuwa ni wanawake, basi hawasimami madhabahuni kuongoza ibada. Nao unabii wao huangukia katika lile fungu la vipawa (gifts), 1Kor. 12:28 “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, watatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.” Hata kwa Andiko hili, kusanyiko ambalo halina vipawa hivi lapaswa kujikagua au kufunga biashara hiyo au waumini wake wanapaswa kulikimbia maana halitawasaidia chochote.

  Ukisoma kuanzia mstari wa 4 utaona ya kwamba vipawa vyote hivi ni vya Roho Mtakatifu. Basi kwa vile karama hizo zote huongozwa na Roho yule yule makusanyiko yetu madogo madogo yalipaswa kudumu katika upendo na umoja wa mafundisho na vyote, kama madhehebu yetu yanavyo dumu katika umoja wa mafundisho kwa mafungu yao. Yaani waLuteri kivyao, wasabato kivyao, nk. kulingana na Roho anayewaongoza. Basi kulingana na tofauti zetu za kimafundisho zikidhihirisha utofauti wa Roho zinazoongoza makusanyiko yetu, nazo Roho hizo zikihudumu katika makusanyiko yetu katika kiwango cha hivyo vipawa, inakuwa ni vigumu sana kwa yeyote asiye na ujuzi wa Neno la Mungu kuweza kupambanua huduma hizi za leo za kinabii zinazochipuka kutoka makusanyiko yetu madogo madogo na kujitangaza kama wa lile fungu la kwanza wakivuna juu ya udhaifu uliotokana na migawanyiko iliyozalishwa kwa makusudi na zile Roho zinazohudumu katika madhehebu yetu.

  Jambo kuu linalo watofautisha haya makundi mawili ya manabii, ni kwamba manabii wa kundi la kwanza sifa yao kuu ni kuambatana na Neno la Mungu. Nabii yeyote ajaye huwa ni muendelezo wa nabii aliyeondoka. Hakuna nabii wa kweli anayepinga Neno alilopewa nabii aliyemtangulia. Wao huyarejea hayo katika kudhihirisha muendelezo wa lile Neno. Naye Mungu kulingana na program yake ya Ukombozi ameliweka hapo katika Biblia ili kuwa Nuru kwetu katika vizazi vyote. Nabii Isaya alitabiri ujio wa Yohana Mbatizaji, Isaya 40:3; pia kuzaliwa kwa Kristo, Isaya 7:14. Naye Musa, akiwa alikwisha tabiri ujio wa Masihi, Isaya alipouleta utabiri huo wa kuzaliwa kwa Kristo, ilikuwa ni muendelezo wa lile Neno lililokuja na Musa. Yoeli alipotabiri kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, jambo hilo lilipotimia Petro aliurejea huo utabiri na kuudhihirishia ule umati wote uliokuwa ukiwashangaa kuwa hilo lililotabiriwa huko nyuma limewatimilia siku hiyo! Hilo linadhihirisha ya kuwa Roho aliyekuwa juu ya Yoeli ndiye yule yule aliyeko juu ya Petro! Nao unabii huu huufunga ulimwengu wote katika kuuleta katika Njia ya Wokovu au kuupeleka kuzimu.

  Lakini unabii wa lile kundi la pili, ule unaohudumu katika makusanyiko yetu madogo, huo hauvuki wigo wa makusanyiko yetu. Unabii huo mara nyingi hutolewa kuwahusu watu waliopo katika kundi hilo. Kwa mfano unabii alioutoa Agapo kuhusu Mtume Paulo, Mdo 21:10-13. Tunaona Maandiko yanamtaja Agabo kuwa ni nabii kati ya kundi la manabii, Mdo 11:28, ukisoma mbele utaona licha ya kwamba njaa aliyoitabiri ilikuwa kwa dunia nzima, bali utabiri ule uliwainua wanafunzi kuwapelekea misaada ndugu zao walio Yerusalemu. Hao ni manabii walio katika uongofu, karama hiyo huwafaidisha kusanyiko. Wakati mwingine manabii wa kundi hili hujaribu kuvuka mipaka yao na kuingia katika Anga Kuu iliyo nje ya uwezo wao kwa ushawishi wa Ibilisi bali Mungu huwarekebisha kama walivyo jaribu Miriamu nabii na Haruni nduguye (Hesabu 12:2-10).

  Sasa, katika ile migawanyiko ya dini pia huzalishwa manabii wengi sana. Mara nyingi manabii wanaozalishwa na Roho hiyo ya migawanyiko hupenda kujitwalia nafasi za wale manabii ‘Tai’ huku wenyewe wakiwa ni ‘mwewe’ tu katika anga za kinabii. ‘Mwewe’ pia huruka juu sana lakini hawezi kukifikia kimo cha Tai kutokana na maumbile yake. Kwanza akienda juu zaidi asingaliweza kuona chini kuna nini, hilo pekee lingemteremsha chini ili ayaone matawi ya miti ya kupumzikia akichoka kupiga mbawa zake. Yaani hawa ni manabii wa makundi, hivyo kwao ukiliondoa kundi, basi unakuwa umemuua, ndio maana ukubwa wa kusanyiko ni jambo kubwa sana kwao! Wao hujitahidi kuwavuta watu wengi waje kwao ikwezekana wote! Jambo hili ndilo linalozalisha mivutano, kuchukiana, wivu, masengenyo, kuchambana na mwishowe Roho yule huwatumbukiza katika ushirikina. Nao huyafanya yote haya bila kujua! Mungu aliahidi kuwapa Roho ya kuamini uongo tangu walipoikataa ile kweli, ndio maana wanazidi kutokomea, hata kwa yanayotendeka, ndiko kunako leta maswali mengi kuhusu unabii wao.

  Hebu tazama mifano hii miwili mitatu ili uweze kuona utendaji wa nabii ‘Tai’ na nabii ‘Mwewe’ wanapokutana uwanjani inakuwaje.

  Tumwangalie nabii wa Mungu, Eliya, alipopambana na manabii wa kidhehebu; manabii 450 wa Baali na 400 wa Asheria pale katika mlima wa Karmeli, (1Wafalme 18:19-28). Hawa manabii wa kidhebu walijua jinsi ya kutoa sadaka na mambo mengi mengine. Waliweza kukamata mambo yaliyo katika anga za chini katika kiwango kilichowafanya watu wawaheshimu kama manabii. Kama nilivyo sema hapo awali kuwa, bila ujuzi wa Neno ni vigumu kupambanua manabii wa kweli na wa uongo maana wote huyaleta mambo yaliyo katika anga za kiroho. Hebu wazia jambo hili Israeli, ambayo ni mfano wa kanisa, ilikuwa na manabii 850 kwa wakati mmoja ndani ya kusanyiko moja, ‘… walao chakula mezani pa Yezebeli’!! Dini zilikuwa na manabii hao 850, lakini Mungu alikuwa naye Nabii mmoja tu yule ‘Tai’, Eliya. Ilipofika saa ya mpambano, Mungu alizifunga anga zote. Soma mwenyewe Mlango wa 18 wa kitabu hicho cha 1Wafalme uone jinsi nabii Eliya alivyowachezea na kuwadhihaki. Pia jionee mwenyewe hao waliojitukuza na kujikweza hata kukaa kwenye meza moja na mfalme kama hawa wa leo wanavyopigania kutambulika na viongozi wa serikali wakipigana madongo kwa ajili hiyo walivyoadhirika.

  Mungu alizifunga anga hata wasijue kuwa sadaka huoshwa kabla ya kuteketezwa, kama ambavyo wakristo wa leo tunadanganywa kuwa nasi pia tumekufa na kuzikwa na Kristo, yaani nasi tumezitoa nafsi zetu kuwa sadaka, hizi nafsi ambazo hazijaoshwa kama alivyooshwa Kristo katika ubatizo wa maji mengi kabla ya kutolewa sadaka, Mungu hatazipokea nafsi chafu! Licha ya wale manabii kujua jinsi ya kutoa sadaka, kama yule nabii wa uongo Balaamu alivyojua na kutoa unabii siku zote, lakini Musa alipowasili akaingia matatani kama ambavyo manabii wa Baali na Asheria walivyoingia matatani katika ujio wa Eliya. Mungu hakuipokea sadaka yao isiyooshwa. Ilipofika zamu ya nabii Eliya kuitoa sadaka, yeye aliiosha kwanza, “… Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni. Akasema fanyeni mara ya pili … Wakafanya mara ya tatu. Yale maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji”. Sasa hebu isikilize Sala ya Eliya: “… nimefanya mambo yote haya kwa Neno lako. Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu wajue ya kuwa wewe BWANA ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie.” Maandiko yanasema baada ya sala hiyo moto wa BWANA ukashuka ukaiteketeza ile sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. Yaliyowakuta manabii wa kidhebu yasome mwenyewe!

  Elisha pia katika 2Wafalme, alikutana na kundi la watoto wa manabii wa kidhehebu, bila shaka waliokuwa katika mafunzo ya unabii. Nao waliweza kukamata mambo yaliyokuwepo katika anga za kiroho hata wakamwambia Elisha yatakayomtokea kuwa “…BWANA atamuondoa bwana wako leo …” Hao walikuwa wa Betheli. Walipofika Yeriko wakawakuta wana wa manabii wa huko. Pia wakamuuliza swali lile lile, naye akawapa jibu lile lile alilowapa wale wa Betheli: “Naam, najua, nyamazeni.” Sasa angalia kituko kinachofuata baada ya Eliya kweli kuondoka kama walivyomtabiria dogo mwenzao Elisha.
  Baada ya Eliya kuondoka, Maandiko yanasema; “… alipanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli”, naye Elisha alipokuwa akirudi, akakutana nao tena wale wana wa manabii wale wa Yeriko, walipomuona wakasema Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Unaona, wao waliweza kukamata hilo lililotokea kwa Elisha katika anga ya kiroho upeo wa mwewe. Wakainama kifudifudi mbele yake (maana sasa sio dogo tena!). Wakamwambia, Angalia, wako hapa pamoja nasi watumishi wako watu hamsini walio hodari; waende, twakuomba, wamtafute bwana wako; isiwe labda roho ya BWANA imemtwaa na kumtupa juu ya mlima mmoja, au bonde moja. Elisha akawaambia msiwatume. Walipong’ang’ania akawaruhusu. Wakatafuta siku tatu, wasimwone. Umeona, manabii wa kidhebu wasivyoweza kupanda juu upeo wa ‘Tai’, Eliya alipopelekwa juu mbinguni wale manabii hawakujua kaenda wapi, bali Elisha alijua. Hebu fikiria kama nawe ungekuwa miongoni mwa wale hamsini hodari wa dhehebuni kwenu, bali leo hii mkienda kumtafuta hamna njia ya kurudi bali mnaendelea hadi kiyama, itakuwaje?

  Tena Elisha akawakuta wale wana wa manabii wa Gilgali, 2Wafalme 4:38-41. Walipotayarishiwa chakula, matango mwitu, wakakiona kifo ndani ya sufuria ikawabidi wamlilie Elisha ili aje akabiliane nacho, wao uwezo wa kukabiliana na kifo hawanao!

  Basi, licha ya Neno la Mungu kuwapo hapo katika Biblia, bado manabii wa kidhehebu hawawezi kulifikia hilo katika ukamilifu wake. Wao hujaribu kutumia akili zao katika kuyajua mambo ya kina ya rohoni na matokeo yake hutoka nje upotevuni na makundi yao wanayoyaongoza. Wengi kwa kukosa uelewa, humlaumu mtume Paulo kana kwamba alikuwa na Injili yake binafsi. Tazama katika Wakorinto 14:34 Maandiko yanasema; “wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena; bali watii, kama vile inenavyo Torati nayo…” Tena katika 1Tim 2:12 “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, … Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” Basi unapoona mwanamke analitawala kanisa, hilo huonesha dhahiri kuwa kusanyiko hilo liko chini ya uongozi wa Roho aliye tofauti na yule ROHO aliyemuongoza mtume Paulo. Bila shaka katika dhihaka ya Roho huyo, amewafundisha kwa kuwaletea unabii ulio kinyume na Maandiko ili kuikamilisha starehe yake! Tena katika kuendeleza michezo yake hiyo ya dhihaka, nimeona katika magazeti majuzi walipokuwa wakisimikana uaskofu, sasa hivi amewapeleka wapentekoste mbali kidogo; nao amewavisha maaskofu wao yale makofia makubwa kama ya maaskofu wa kikatoliki au kiluteri wanapohudumu, kinyume na Andiko linalowataka wanaume kutokufunika vichwa vyao wasalipo! 1Kor 11

  Kwa kumalizia, katika ujumla wa manabii, mwisho wote hao wa fungu la kwanza, yaani wale ‘tai’, na wale wa fungu la pili ‘mwewe’, wote wanakusanywa pamoja na kisha kugawanywa katika mafungu mawili. Fungu la kwanza ni wale wanaotumika kwa ROHO wa Mungu ambao hutokana na Neno la Mungu nao huambatana nalo hilo katika hali zote. Na kundi la pili ni wale wakidhehebu ambao wao hulipindisha Neno la Mungu kukidhi haja zao. Kama unavyoona wachungaji kibao wanawake wakiyatawala makusanyiko yao yaliyojaa wanaume kwa wanawake, kinyume na Mwanzo 3:16 inayomuweka mwanamke kutawaliwa na mwanamume. Basi ule uasi ulioanza na Kaini ndio huo unaoendelea ukiwapandisha wanawake mimbarani bila ya uoga wala heshima kwa Neno la Mungu. Hata katika makusanyiko yao hawa manabii wa kidhehebu, asilimia 90 ya mafundisho yao hushughulika na mambo ya kidunia na utajiri. Hawajali kabisa hali za kiroho za waumini wao. Basi mtu akikuambia yeye ni nabii, muulize kwanza iwapo yeye mwenyewe amebatizwa maji mengi kwa jina la Bwana Yesu Kristo ili kuziondoa dhambi zake hata sasa kapewa hicho kipawa cha unabii? Kama hajafanyiwa hilo ikimbize roho yako! Ndio maana mtume Paulo akizijua roho hizo zisizoweza kuongoka, basi akatamatisha kwa kutuonya kuwa ; “Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni na ayatambue hayo ninayo waandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga na awe mjinga”! Basi hali ndivyo ilivyo kwa wa kiroho atayapokea hayo na kwa mjinga naye atafanya analolijua mwenyewe, yaani kuendelea katika ujinga wake!!!

 22. Ninaungana na bro Marko Majura hapo juu,ni vyema tumuachie Mungu kazi ya kujudge yupi wake na yupi c wake,maana huyu ni mtumishi wa MUngu na km ni nabii wa uwongo hiyo atajibu yeye siku yake ikifika.

  Naona watu wengine wanakosoa mpaka rangi,jamani tuwe makini na watumishi wa Mungu,kumbukeni Mungu anaweza kumchagua yeyote akafanye kazi yake na pia ana uwezo wa kuwabadilisha watu wake pia.Msimuhukumu mtu kwa muonekano wake wa nje.

  Bwana anaweza

 23. Kujua huyu ni nabii wa kweli au nabii wa uongo itategemea sana ujuzi wako katika Neno la Mungu, yaani Biblia. Ujuzi huo hukupelekea kujua position yako katika ujumla wa uhusiano wako na Mungu. Sisi wa Mataifa tumemjua Mungu kupitia Huduma ya Mitume. Basi ufahamu huo hutarahisishia kujua wajibu wetu kulingana na nafasi yetu tuliyotengewa katika Ufalme wa Mungu. Mtume Paulo ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kutuletea sisi Injili. Kazi hiyo hakuifanya yeye kama yeye bali kwa uongozi wa yule aliye mtuma. Basi Injili aliyotuletea inamkataza mwanamke kuwa mchungaji/kufundisha, yaani kuongoza kusanyiko! Basi aliyeipokea Injili hiyo akiwa ni mwanamke, basi yeye husubiri kuoneshwa nafasi yake katika kusanyiko! “Vipawa havina majuto”, hata wengine hupewa hivyo kwa ajili ya kupotea! Yachunguzeni Mapenzi ya Mungu. Katika siku yetu ya leo, nafasi ya mwanamke imewekwa wazi katika mafundisho ya Mtume Paulo, naye anatuhakikishia kuwa Mungu atahukumu kwa Injili yake! Basi jihadharini na matango mwitu!

 24. Ewe MWENYEZI MUNGU tunaomba utupe macho ya rohoni ile tuweze kuwatambua manabii wa uongo

 25. Shalom watakatifu wa Mungu.

  Nimesoma ‘comments’ za wengi hapo juu, nimebaini kama wanam-beza huyu mama kuwa hawezi kuwa mtumishi wa Mungu, kwa maana kuwa hafanyi kazi za Mungu.

  Mimi binafsi sijaijua kabisa historia ya huduma ya huyu mama, wala sijaiona hata kwenye video au TV. Kutokana na hilo, ningependa yeyote kati yetu tunaotumia blog hii, ambaye kwa namna moja ama nyingine anazo taarifa za huduma ya nabii huyu aweze kutuelewesha juu ya huduma yake. Tunaweza tukawa tunaendelea kuipinga huduma hii wakati hatuna uhakika na namna yake ya mafundisho.

  Watu wa Mungu tunaye Roho Mtakatifu, ninaamini kuwa iwapo tunaona huduma ya ibada ya imani yoyote inayojiita ya ki-Kristo, tunao uwezo wa kutambua iwapo ni ibada inayotokana na Mungu au la.

  Kuna mapungufu mengi ya mafundisho katika madhehebu mbalimbali ya ki-Kristo. Hilo halitufanyi moja kwa moja tuseme kuwa dhehebu husika kwa sababu ya upungufu wake basi mafundisho yake ni potofu.

  Mahali panapoitiwa jina la Yesu Kristo ili watu watubu dhambi zao na kuokoka, tayari mahali hapo Yesu yuko kazini. Mapungufu yaliyopo katika kanisa hivi sasa ni tatizo la kanisa la Mungu kote Ulimwenguni. Makanisa mengi hayatafuti kufundisha utakatifu, yanatafuta miujiza na watu kuokoka basi!.

  Kutokana na hayo yote, kwa upande wangu ninaona ni heri huyo mama ambaye anajiita nabii tumsikilize; anahubiri nini, anafundisha nini,kisha tuseme iwapo ni nabii wa uwongo au vinginevyo. Tusipofanya hivyo tunaweza tukawa tunahukumu huduma ambayo kimsingi haipo tofauti na huduma zilizopo ambazo tumezizoea.

  Haya ni mawazo yangu tu, shalom.

 26. Mungu wetu ni mkuuuuuuuuuuuu tusihukumu mambo kabla ya wakati wake tusije tukakuta tumewakataa wale waliotumwa na yule tunaemwamini yaani Yesu. Kila jambo ni kwa kuomba na kusali na mungu atafunua.ni jambo zuri watenda kazi wa kirsto wakiongezeka tuwatie Moyo wa kuendelea wala sio kuwakatisha tamaa.kama Roho wa bwana yumo ndani yetu yeye huyafunua yote .tuzidi kuomba na kuwaombea Watumishi-

 27. Bwana Yesu asifiwe wapendwa, jambo la msingi kabisa Mungu anataka watu waokoke kwanza wamkubali kwanza ndani yao haya mengine uponyaji, baraka zitashuka tu,ukitabiriwa na mtumishi flani kuwekewa mikono sio kwamba umefunguliwa mpendwa , kufunguliwa kwa mtu ni kazi ya Roho Mtakatifu ndo ajuae kuponywa kwako kabisa, mimi ni shahidi wapendwa nilikuwa nimefungwa na roho za uchawi kwenye kizazi changu,niliombewa sana na watumishi lakini siku moja naenda kazini roho mtakatifu alishuka kwa nguvu akaniambia nakusafisha sikuelewa rahis maana yake ilipita kama miezi 9 badae ndo nikaanza kuona natapika vitu vya ajabu kutoka tumboni mwangu, nikaanza serious maombi ya vita mnaelewa watu wa rohoni,kila nikiomba naomba wakat flani masaa 2 ikipungua sana dk30 na wakat wote huo natapika si kawaida nilikuwa na kopo rasmi nimetengeneza la kutapikia na hali hiyo iliendelea kwa mda wa miaka 2 nadhani nikikadiria huenda nilitapika kama ndoo kubwa na lita 20.

  jamani tuwe watii kwa neno tusome neno tuombe mambo yetu yatanyooka tu haya mambo ya manabii kutabiriwa siyapendi maana hayafungui isipokuwa tu ukiwa msikivu wa Roho Mtakatifu.

  mbarikiwe sana

 28. Wapendwa,

  Bado naomba kusaidiwa……Je Nabii ni nani hasa Kimaandiko…..naamini maandiko matakatifu yana majibu……Je ni uponyaji? Wingi wa watu? Watu wanaokoka? Ni nini hasa kinamfanya mtu akaitwa Nabii? Hebu nisaidieni kwa Kutumia Maandiko?

 29. Jamani wapendwa ninaomba kutoa angalizo, chochote unakiandika usikiandike ukiwa moved na hisia zako tu juu ya kitu kilicho kwenye mada, wengi sana wanaweza wakasukumwa na hali fulani ndani ya roho zao tu kuandika jinsi wanavyojisikia, unaweza ukasukumwa na wivu au ukaandika kwasababu ndani ya moyo wako unaona unakosa amani na kujisijia vibaya tu juu ya huduma ya huyu dada.

  Msisitizo wangu ni kwamba tutafuta maongozi yote katika hekima, ufahamu, maarifa na ujuzi wote wa rohoni kutoka kwa Roho Mtakatifu, kama Roho hajafunua kitu chochote kinachoonyesha uhalisi wa huduma yenyewe basi angalia sana usisukumwe na hisia zako, kwasababu hisia zako nazo zinaweza zisiwe sawa asimia mia moja, na hisia zinapokusukuma unaweza ukatoa na vifungu vingi sana vya biblia ukasimamia hapo ukasema hata Yesu alisema siku za mwisho manabii wengi watatokea, hili andiko lisianishwe katika hisia zako tu au msukumo wa Moyo wako, lakini unahitaji Roho Mtakatifu akupe ufahamu wa ndani zaidi, hapo ndipo unaweza ukawa na msingi Imara wa kuandika unachokiandika, sina lengo la kurusha lawama juu ya huduma hii wala kutoa neno la heri wala shari ninachokisema ni kwamba kazi zote zitakuwa dhahiri na kuonokena wazi bila kificho kama zinatendwa katika Mungu au kuna hila nyingine za wanadamu ambao wanaweza kabisa kuvaa vazi la unabiii au utume ili kufanikisha malengo ya shetani, yote hayo tunahitaji uongozi na guidance ya ndani kabisa toka kwa Roho Mtakatifu, kwasababu pasipo hivyo tunaweza tukajikuta tunaupiga teke mchokoo. Kama Roho mtakatifu atatuonyesha zile huduma ambazo hazitoki kwake au hazina lengo lake, basi atatuonyesha pia na huduma zake ambazo ameziweka mbele yetu na ambazo anataka tuenende katika hizo.

 30. Bwana Asifiwe wapendwa, naona wengi mnaongea kama kwa wasiwasi, Muwe makini kabla ya kuwasema watumishi wa Mungu, Jina la Yesu linahubiriwa iwe kwa hila au kwa haki watu wanaokoka tu. mambo mengine yawe ya kweli au uongo atasimama mwenyewe siku ya hukumu na kujibu, pengine wewe unayemyooshea kidole mtumishi utabaki mlangoni yeye unamkuta na Musa. msiwaseme masihi wa Bwana.

 31. kwa kweli inatubidi tuwe makini na hao wanaojiita manabii, mwisho

  tutakuwa na viongozi ambao hawakutoka kwa Mungu bali kwa shetani wakitumia jina la Yesu

  kutudanganya na miujiza ya kiushetani na majini.Mungu tusaidie sana tuwe na utambuzi juu ya watu hawa.nina wasiwasi na manabii wanaozuka hizi ni siku za mwisho kama ilivoandikwa katika biblia

 32. Bwana Yesu asifiwe!
  Wapendwa naona kufungiwa kwa Mtumishi Nabii Flora kwasababu ya majirani kusema kuwa anawapigia kelele au sio eneo la kufanyia huduma, ni mambo ambayo yanasuruhisho kwani hata katika nyumba zetu za kupanga uwezi kupata uhuru wa kukusanyika na kuomba kwa pamoja na wapendwa wenzako labda mwenye nyumba awe ameokoka.

  Cha msingi naona aende akamilishe usajiri na huduma itaendelea kama kawaida kwani si yeye wa kwanza kuweka huduma katikati ya makazi ya watu. Mangapi petrol station zinakuwa karibu na makazi ya watu itakuwa huduma ya kiroho?
  Mungu ampe nguvu katika kufuatilia usajili. Pamoja na Roho Mtakatifu ampe kusimama imara na kuwa na moyo mkuu atashinda kama alivyotumwa na Mungu. AMEN

 33. Mungu atusaidie sana wapendwa maaana hizi ni siku za mwisho na biblia inatuonya kabisa kuhusu haya mambo

 34. Hata kidogo mm simkubali huyu anayeitwa Nabii,muonekano wake wa nje tu haumtambulishi kama mtumishi wa Mungu,sasa huo wa ndani atajua mwenyewe!! Biblia inasema mtu alivyo nje ndivyo alivyo ndani!! EEEH MUNGU TUSAIDIE

 35. Napenda na mimi kutoa mchango wangu katika hili,Tunamshukuru MUNGU kwa YESU KRISTO aliyetupa ahadi ya kumwagia roho wake wale wote wenye mwili,lakini tunapewa agalizo katika Mathayo 7:8- kuwa tuwe makini na kutatokea na manabii wa uongo na waalimu wenye mafundisho ya kidunia,wenye mfano wa utauwa lakini wakimkana YESU (2tim 3.1-8)

  Nyakati za mwisho ibirisi atajiinua juu afanane na aliye juu na kutenda kazi kama YESU alizozifanya na atajigeuza kama malaika wa nuru

  kwa maneno hayo,nabii wako wa uongo na wa kweli kumtambua tutatumia vigezo vya YESU kuwa mtawatambua kwa matunda yao.

  hata hivyo Je Nabii Frola anayomaswali ya kutujibu kaanzia wapi tuko alipoibuka na huduma yake ya unabii? anatumia jina la YESU KRISTO au la YES? maana ibirisi yuko kazini sasa maana anajua muda wake ni mchache anatafuta watu awameze.

 36. Mambo ya Ndani nayo yapiga ‘stop’ Kanisa la Nabii Flora
  Na Edmund Mihale

  MSAJILI wa Vyama Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amevitaka vyombo vya dola kutekeleza agizo la ofisi hiyo kusitisha shughuli za Kanisa la Huduma za Maombezi zinazotolewa na Nabii Flora Peter Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
  Agizo hilo linatokana na ofisi hiyo ya msajili kubaini kuwa kanisa hilo limekuwa likiendesha shughuli zake kinyume cha sheria ya vyama namba 337 ya mwaka 2002.

  Akizungumza katika mahojiano maalum Majira wiki hii, Mkurugenzi wa Sheria na Malalamiko ambaye pia anashughulikia usajili wa vyama, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Augustine Shio, alisema ofisi yake haijapokea maombi yeyote wala kutoa kibali kwa kanisa hilo kuendesha shughuli zake.

  Alisema kuwa kanisa hilo pia limekuwa likiendesha shughuli zake kinyume cha sheria kwani lipo katika eneo ambalo ni la makazi ya watu.

  Kwa mujibu wa Bw. Shio, ofisi yake imepokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa eneo hilo wakilalamikia usumbufu unaotokana na shughuli za kanisa hilo kwenye makazi yao.

  Hata hivyo, msajili huyo alisema kuwa amesikitishwa na hatua ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kiniondoni Kitengo cha Ardhi kukiuka maagizo ya yaliyotoka Wizara ya Ardhi kwa kuruhusu shughuli za kanisa hilo kundelea ndani ya makazi ya watu.

  “Nimeshangazwa na kitendo cha Mkurugenzi wa Manispaa kukaidi mamlaka ya juu yake, maagizo yakishatoka wizarani haiwezekani wilaya kuyatengua,” alisema.

  Kwa mujibu wa barua ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kiniondoni ya Oktoba 31 mwaka huu, kanisa hilo lilipewa ruhusa ya kuendelea na huduma zake kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 31 mwaka huu kinyume na barua ya Wizara ya Ardhi ya Oktoba 21 mwaka huu iliyomtaka kiongozi wa kanisa hilo, Nabii Flora Peter kusitisha huduma hiyo mara moja.

  Katika barua yake ya Novemba 18 mwaka huu kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Bi Albina Burra, amesema kuwa kibali hicho cha manispaa ni batili kwa kuwa kimekiuka sheria ya Ardhi namba 8 ya mwaka 2007, kifungu cha 6(3)

  Alisema kuwa kifungu hicho kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Mipango Miji kubadilisha matumizi ya ardhi.

  Kutokana na hali hiyo, Msajili wa Vyama Wizara ya Mambo ya Ndani alisema haitambui huduma hiyo kwa vile haipo katika vitabu vyake vya usajili.

  Alisema katika barua yake ametoa nakala kwa uongozi wa Jeshi la Polisi na amewataka wakazi wa eneo hilo kutoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni ikiwa kanisa hilo litaendelea kukaidi maagizo ya ofisi ya msajili.

  Aidha katika barua yake Msajili amevitaka vyombo vya dola, ikiwemo Idara ya Uhamiaji kuhakiki uraia wa viongozi wa kanisa hilo.

  Hata hivyo, alipohojiwa kuhusu suala hilo, Nabii Flora alisema kuwa kanisa lake litaendelea na huduma zake kwani huduma hizo zinahitajika na watu wengi na imesaidia kubadili tabia za vijana wengi ambao walikuwa wakijihusisha na masuala ya uhalifu.

  “Haya nayaona kama ni majungu tu ya watu wachache, lakini tutaendelea kutoa huduma na katika jina la Yesu tutashinda,” alisema.

  source:

  Gazeti la Majira

  Tarehe 7 December 2011

 37. ………………….
  cha msing ni kujiangalia mtu binafsi ni jinsi gani una uhusiano mzuri na Mungu.

 38. Lihimidiwe jina kuu lipitalo majiana yote jina la Yesu Kristo.
  Ni jambo la kumshukuru Mungu sana pale tunapoona injili inaenda mbele na makanisa mengi ya kiroho tena yenye upako na miujiza mingi yanaibuka na kuwa na wafuasi wengi.
  Roho mtakatifu azidi kukaa juu ya hao wanaoanzisha hayo makanisa/huduma ili injili ya kristo iende mbele na uponyaji na miujiza yote itoke kwa kristo ili utukufu wote umrudie Mungu.
  Mimi natoa angalizo kwa hao manabii,mitume nk wanaonzisha hizo huduma /makanisa.waangalie wasije wakadanganywa na wale waumini wao wakawapa utukufu baada ya kuponywa nakuanza kuwaita majina makubwa kama katapila ,transforma nk.Kama muujiza umetoka kwa Mungu basi utukufu urudi kwa Mungu.
  Pia tuangalie sana matangazo yetu yana beba ujumbe gani ,mara nyingi utakuta picha ya mtumishi ndio imejaa kwenye tangazo au kama ni la redio utashangaa kuona jina la yule mtumishi linatajwa mara nyingi sana kuliko jina la Yesu ambaye ndiye mwanzilishi
  Mbona huduma za kidunia hawafanyi hivyo ? makapuni ya kidunia mbona wamiliki wake hawabandiki picha zao kwenye matangazo yao ya biashara ? kwa nini sisi watu wa Mungu tunakua malimbukeni hivyo?
  JINA LABWANA LIBARIKIWE NA UTUKUFU WOTE UBAKI KWA MUNGU

 39. Ni habari njema………!!Lakini napenda kuuliza, Je Hivi Nabii ni nani hasa tukiangalia Maandiko? Je ni huduma ya uponyaji? Kuponya magonjwa sugu? Kukimbiliwa na watu wengi? Kunafanya mtenda kazi ya Bwana Kuitwa (Kujiita nabii)?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s