Krismas ni sherehe ya Kikristo?

Bwana Yesu Asifiwe Wapendwa, hebu tujadiliane je Krismasi ni sherehe ya kikristo? Ama ya kidunia maana haipo kwa bibilia.

Paul Badia

Advertisements

59 thoughts on “Krismas ni sherehe ya Kikristo?

 1. Nimesoma sana maoni yenu ni mazuri na kweli inaonesha ni kwa kiasi gani mnafatilia mambo na haswa kuwa kweli ninyi ni wafuasi wa Yesu Kristo mkombozi wetu mbarikiwe sana. Lakini tunapolejea katika upande wa ile kweli kama biblia inavyosema ijue ile kweli nayo itakuweka huru, tunaweza kuona utofauti wa hoja kulingana na kielelezo chetu ambayo ni bibilia. Maana kuhusu Christmas bibilia yetu imekaa kimya na cha hajabu biblia inasema Yesu alipokuja duniani alikuwa mwanadamu %100 na hii inashangaza kuona watu wanasherekea kuzaliwa kwake mwezi wa 12 na wakati malaika Gabuliel anatumwa kwa mama yetu bikra Maria mwezi 6 lejea Luka 1:26. Kwa maana hiyo wanaoadhimisha kuzaliwa kwa Kristo Yesu mwezi wa 12 wanamudharirisha Mkombozi kuwa alizaliwa njiti maana kama wote mnaosuport kuwa Yesu alizaliwa mwezi wa 12 tarehe 25, mutakubaliana na mimi kuwa ili mtoto azaliwe hali akiwa amekamilika lazima mimba itimize umri wa miezi 9. Hiyo ni hesabu ya kawaida tu ukianza mwezi wa sita hadi wa kumi na mbili, ina maana Maria alikuwa na ujauzito wa miezi sita. Ndugu zangu mimi naamini sana lile lililoandikwa kuliko nyongeza au mawazo ya wachungaji na maasikofu au papa. Mungu ndiye kiongozi wetu na Yesu ndiye kielelezo wetu. Nimesoma sana maandiko ya bibilia lakini kamwe sijawahi kuona sehemu ya wazaz wa Yesu au mitume wake walipoadhimisha siku ya kuzaliwa kwake au kukufuka kwake. Marafiki katika siku hizi kuna kitu nyuma ya pazia kama alivyotabili Paulo
  katika ile 2Themotheo 2:2-12.juu ya yule muasi ambaye yeye kwa kujifanya kana kwamba ni Mungu atahazimu kutoa sheria zake na hivyo kuwapotosha wengi wale ambao hawakuipenda kweli. Soma Isaya pia 24:4-6.utaweza kugundua mambo haya. Ubarkiwe sana.

 2. Mi naona christmass tuisherekee,maana hata pasaka hatujaagizwa kuisherehekea kibiblia kwa maana tumepewa mamlaka yakuteka kila mawazo na fikra zipate kumtii Kristo,hivyo kusherehekea chrismass 25/Dec/ n sawa na kumwabudu MUNGU cku ya J2 badala ya J1. mpo hapo

 3. Bwana Yesu asifiwe, mimi naona 2jikite kwa kile chenye biblia inasema “tusiongeze Neno wala kupunguza” ni kweli kuzaliwa kwake masihi kumeandikwa lakini haijatajwa kwamba tusherekee ndiyo maana hata biblia yenyewe imekaa kimya, yale yatupasayo kufanya biblia haijakaa kimya mfano pasaka kwa ajiri ya ukumbusho wake wakati anapaa mbinguni imesema? kama kungalikuwa na uhaja wa sherehe hii mungu we2 angalitwambia maana ni wa upendo. mimi nashauri jambo hata kama linamhusu kristo kuogopa kuongeza au kupunguza neno katika maneno yake kama alivyoamuru!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

 4. Wapendwa,
  Shalom.
  Siku hii ni kama siku ya WAJINGA Duniani.
  Krismas ni SIKUKUU YA KIPAGANI.Hii ni mojawapo ya KARAMU ambayo MFALME
  KONSTANTINO aliwapa watu.
  Alichukua IBADA YA mungu jua na kuibadilisha kuwa ya Mwana wa
  Mungu.Badala ya Kuiadhimisha mnamo tarehe 21 DESEMBA, ambayo ndiyo
  waliyokuwa wakisherekea karamu ya mungu jua, waliiweka iwe Desemba 25 na
  kuiita siku ya kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu.
  Bali tunajua kuwa YESU alizaliwa APRILI.
  ****MTEULE HADANGANYWI ****

 5. NI UPAGANI TULIOUBATIZA UWE UKRISTO UKAGOMA,UKAINGIA KANISANI NA UPAGANI WAKE

  tumsikilize YEREMIA ANASEMAJE JUU YA MTI WA KRISMAS

  YEREMIA 10:3,4
  “MAANA DESTURI ZA WATU HAO NI UBATILI, MAANA MTU MMOJA HUKATA MTI MWITUNI,KAZI YA MIKONO YA FUNDI NA SHOKA. HUUPAMBA KWA FEDHA NA DHAHABU HUUKAZA KWA MISUMARI NA NYUNDO, USITIKISIKE”

 6. Na amani yake itutawale!. nakushukuru ndugu yangu lenda kwa kujitahidi kufafanua vitu usivyovifahamu vizuri kwani hiyo inatusaidia kuelewa udhaifu wako ili tukusaidie kama uko tayari maana unachanganya mambo sana na kunukuu misitali usiyoielewa. juu ya krismass soma ufafanuzi wa ndg. John poul. juu ya namna ya kusheherekea tunatofautiana taifa na taifa kabila na kabila. kwa hiyo hata kutoa heshima ya juu kabisa kwa machifu/miungu ya makabila kabla ya kumjua Huyu Mungu wa kweli inatofautiana. Baada ya kumjua Mungu wa kweli tunatakiwa kutoa heshima na sifa za juu ambazo tulizitoa kwa miungu ya kipagani ktk ujinga wetu tumtolee Mungu wa kweli ktk hekima ya kweli. ambacho hatuwezi kufanya ni kumtolea kafara yeyote ile ya wanyama/binadamu au vinywaji. kama heshima kwake. kwa sababu tumepewa kafara moja tu ambayo ni Yesu kristo. kwa hiyo mapambo kama mti wa Christmas siyo tatizo kama ukitumika kwa sifa na utukufu wa Mungu. kwa kuwa Mungu aliumba vitu vyote viweze kumtumikia yeye hata lusifa (,shetani) amsifu yeye. Sasa wewe unapotenga siku,vitu kwamba ni vya shetani wakati yeye hakuumba chochote je unamtetea shetani au Mungu? kwa maana shetani hana chochote cha kumsifu vinavyomsifu alivipola kutoka kwa Mungu. kwa hiyo sisi kama wakristo tunawajibu wa kumnyang’anya na kumrudishia Mungu. ambaye hafanyi hivyo anamsaidia shetani. nadhani Haya yatakuongezea hekima. Mungu atusaidie kuelewa.Amina

 7. TUJILINDE NA MITI YA “CHRISTMASS”

  YEREMIA 10:3-4
  “MAANA DESTURI ZA WATU HAO NI UBATILI, MAANA MTU MMOJA HUKATA MTI MWITUNI,KAZI YA MIKONO YA FUNDI NA SHOKA. HUUPAMBA KWA FEDHA NA DHAHABU HUUKAZA KWA MISUMARI NA NYUNDO, USITIKISIKE”

  YEREMIA 10:8
  “LAKINI WOTE PIA HUWA KAMA WANYAMA, NI WAPUMBAVU.HAYA NI MAELEZO YA SANAMU, NI SHINA LA MTI TU.”

 8. Bwana Yesu asifiwe!
  Ndungu kitu ambacho hakijaandikwa kwenye biblia si muhimu sana ktk wokovu. kwa hiyo tarehe na mwenzi sahihi wa kuzaliwa Yesu Kristo siyo yamsingi kwa wokovu. Maana ya christmas ni “christ’s mass” yaani “kusanyiko la Kristo”.kumbuka hakuna kusanyiko linalofanyika bila makusudi maalumu, kanisa takatifu katoliki la mitume liliweka kwa makusudi ya kukumbuka na kutafakari juu kuzaliwa kwa Yesu kulivyokuwa kila mwaka. “kilitrujia wanatafakari fumbo la UMWILISHO wa Mungu. yaani Mungu kuchukuwa mwili. Ambapo kimsingi siyo tarehe 25 Dec. tu Bali ni kwa kipindi cha majuma manne yaani mwenzi mzima wa Dec. na kuhitimishwa na kusanyiko kuu Dec. 25. linaitwa kusanyiko la kristo “christ’s mass” kwa hiyo kanisa liliweka kipindi hicho kwa nia njema Kabisa ili watu wote wasikie habari ya kuzaliwa kwa Yesu ili waachane na Ibada za kipagani. ndiyo maana waliteka hata Siku yao ya kipagani ya kusheherekea mungu mufu. na kuifanya ya Mungu mtu.Yaan Yesu kristo. maandiko yanasema wanaomjua Mungu wa kweli watateka wasiomjua wataenda uhamishoni. kwa hiyo tunamamlaka ya kuteka vyote Mali, muda, siku, miaka na vyote vilivyokuwa vimetegwa kwa ajili ya shetani ili vimtumikie Mungu wa kweli. kuzaliwa kwa Yesu kulileta mwanga /nuru pale palipokuwa na giza ndiyo maana zile siku zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kiza kanisa liliziteka kwa ajili ya mwanga, Na kristo yeye ndiyo mwanga wa ulimwengu. kama jua. pia yeye ni Jua la haki. kwa hiyo wengi wanaopinga shere he hizi ni kwa kutoyajua maandiko matakatifu, na wachache wao ni wapinga kristo wa tangu mwanzo na hao ndiyo wanao upotosha ulimwengu. wakristo wasasa wanashabikia pasipo kujua nia ovu ya watu hao ni kufuta ukristo duniani wakitumia kigezo hayajaandikwa kwenye biblia ndugu usiwe miongoni mwao. wengine wanajiita wachungaji, maaskofu, wasabato, mitume na nabii wanadanganya ulimwengu. ndugu jihadhari wewe msikilize Roho mtakatifu. ubarikiwe na Mungu wa lsrael.

 9. Sungura,
  Mungu akubariki.
  Nashukuru kwa maswali yako ambayo kimsingi sitayajibu kutokana na lugha uliyotumia. Mungu atusaidie sote rafiki yangu.
  Lwembe,
  Nashukuru kaka Lwembe kwa kuliweka vizuri swali lako. Naona sikulielewa hapo mwanzo ndiyo maana nilisita kulijibu moja kwa moja. Sasa, naomba nijibu kwa ufupi kama ifuatavyo;
  Umri wangu, mbwa au paka wangu, kimsingi unatawaliwa kwa kumbukumbu za sekunde, dakika, saa, siku, mwezi na kwa wengine hata mwaka ambao ndiyo mtu au kiumbe alizaliwa. Kama nakumbuka sekunde, dakika, saa, siku, mwezi au mwaka nitaadhimisha kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo. Na hapo, sitakuwa, naadhimisha siku, bali ni lile tukio la kuzaliwa kwangu au mnyama(paka/mbwa) wangu. Mamajusi walilisherehekea lile tukio la kuzaliwa kwa Kristo siku ile tu. Na hawakuonekana tena kusherehekea mwaka uliofuata au/na Yesu mwenyewe pamoja na wazazi wake, hawakusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mtoto wao – Yesu.
  Wazazi wa Yesu waliifahamu vizuri tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu lakini hawakusherehekea kwa kipindi chote walicchokuwa na mtoto wao (takribani miaka 33+). Na ndani ya Biblia, kuzaliwa kwa Kristo kwa maana ya sekunde, dakika, saa, siku au mwaka havikujatajwa. Tunaposoma kwenye historia ndipo tunakumbana na ukweli wa tukio hili, tena kwa upande wa mwaka peke yake aliozaliwa Kristo.
  Hivyo, Wakristo wote kama kweli ni wafuasi wa Kristo na wanaamini kile Kristo alichokisema (neno lake), wangelifuata hicho. Kristo hakusema watu waadhimishe siku yake ya kuzaliwa. Nami kama Mkristo, najitahidi tu kuamini na kufuata kile alichosema Kristo peke yake. Kufanya mambo mengine ya kiimani beyond the truth of the Bible, ni kujitahidi kumsahihisha Mungu juu ya kile alichotupa – Neno lake. Hatujalidhika na neno lake ndiyo maana tunaongeza hata kile kisichoandikwa ndani. Ndiyo, yaelekea siku hizi, tumekuwa na akili sana kiasi cha kumsahihisha Mungu. Mungu atusaidie kaka Lwembe.
  Ubarikiwe

 10. Siyi, si kwamba eti nataka kuujua umri wako, hapana; nataka kuijua namna unayoitumia kuuelezea umri wako bila kuhusisha kuzaliwa kwa Kristo; niambie tu hata umri wa mbwa wako kama unaye au hata paka wako!

  Asante, Mjoli Siyi!

 11. Kwa Siy na Lwembe,

  Siku zote huwa najiuliza huku nikifurahia lakini, swala la kwa nini Yesu hakuwa na majibu ‘straight’ kwa maswali mengi aliyoulizwa? Eg, Yohana anapotaka kujua kam yeye( Yesu ) ndiye Masia, hakujibu kama yeye ndiye au siyo, bali anawaambia ‘kawmwambieni Yohana haya mnayoyaona…..

  Mafarisayo wanapomuuliza ”unafanya haya kwa mamlaka ya nani?” badala ya kuwajibu tu, naye anawauliza swali,tena ” ubatizo wa Yohana ulitoka kwa nani?

  Sasa kwa kuwa Lwembe umeamua kumjibu Siyi sawasawa na mwelekeo wake, amini nakwambia, utakesha unamjibu.

  Ona hapa chini uwezo wake (Siyi) wa kufikiri na kuelewa mambo. Namnukuu:

  ”Ninaposoma aya hizi hapa, naona habari za furaha kwa sababu ya dunia nzima kupata mkombozi. Sijaona kama kuna aya yoyote inayosema watu waadhimishe siku ya kuzaliwa Masihi”

  Yeye bado anaona kinachoazimishwa kwa habari ya kuzaliwa kwa Yesu ni siku, wala siyo suala la kuzaliwa kwake. Japokuwa kuna majibu mengi sana huko nyuma umemjibu kuwa ishu siyo siku bali ni kilichofanyika.

  Unahangaika na mtu mwenye ‘mindset’ ya kushika mambo katika mwili, mtu mwenye kuazimisha siku ya sabato na si sabato, mtu mwenye kumwelewa Mungu kwa agano la mwilini.

  Sijui nikimuuliza swali linalohusu uzalendo wetu kwa nchi yetu atajibuje; kwamba tunapoazimisha siku tulipopata uhuru wetu( Tanganyika huru), tunachokiazimisha huwa ni ile tarehe 9/12, au huwa ni lile suala la sisi kupata uhuru?

  Tarehe huja kwa sababu kuna majira na nyakati, bali tukio au suala lenyewe halijali majira wla nyakati katika kutokea kwake. Kwamba hata kama kusingekuwa na kalenda, bado tungepata uhuru na tungesherekea kupata uhuru, na sherehe tungezifanya siku na wakati wowote tunaoona kuwa ni vema kufanya hivyo.

  Kwani pasaka ilikuwa inasherekewa siku waliyotoka Misri au walikuwa wanasherekea kile kitendo cha malaika kutoangamiza katika nyumba zao, na wao kutoka Misri?

  Kwani mamajusi waliosherekea kuzaliwa kwa mtoto na mtoto mwenyewe, waliambiwa na Mungu kwamba wakamsherekee na kumpelekea zawadi, au ni wao waliona kuwa suala hilo lafaa kusherekewa maana ni kuu mno?

  Halafu mimi siamini sana kuwa siku/tarehe aliyozaliwa Yesu Mungu aliificha. Sioni ni kivipi niamini kuwa aliificha alhali kuna watu walishuhudia kuzaliwa kwake, na jinsi tukio lilivyotokea-yaani kuzaliwa kwenye hori la kulia ng’ombe, na mamajusi pia walikwenda kumwona kwa sababu tukio halikuwa la kificho, pamoja na wale wachungaji waliopashwa habari na malaika. Hapakuwa na siri hapo.

  Tatizo tu ni kwamba kumbukumbu hazikuweza kutunza vema, au zilipotea kwa sababu ya utunzaji hafifu wa kumbukumbu, lakini lazima kulikuwa na kumbukumbu za siku aliyozaliwa.

  Mbarikiwe.

 12. Lwembe,
  Mimi nakushukuru sana ndugu yangu kwa kuyajibu maswali yangu. Kimsingi yalikuwa ni maswali ya Seleli ( hasa yale ya sehemu ya kwanza), lakini kwa sababu ya ari kubwa na njema uliyo nayo moyoni mwako, umeamua kujitosa kuyajibu, mimi nasema ubarikiwe. Maelezo yako ya siku ile, ndiyo yaliyoongeza maswali hayo ambayo kwa kweli nilikutwika zigo la kuyajibu yote kwa pamoja. Nakushukuru sana kwa moyo huo wa kujitoa na kuwa tayari kutumika. Yaelekea wewe, ni kiongozi mzuri huko kanisani kwako. Nimenotice vitu. Bwana akubariki sana. Sasa twende kwenye majibu yako ya msingi.
  Jibu la swali la kwanza, ni jibu zuri sana. Ni kweli kuwa, kwa hali ya kawaida, mambo yote yanayohusu ibada, shetani hanalo la kwake hata moja. Yote ameyaiga kutoka kwa Mungu na kisha kuyageuza kwa namna alivyoweza yeye. Na kwa sababu mambo hayo (ibada) yalikuwa ya Mungu na sasa shetani akayegeuza, wewe unafikiri mambo hayohayo yakifanyika kwa mtindo wa shetani, Mungu atayakubali pamoja na kwamba hapo mwanzo yalikuwa ya kwake? Biblia inasema, Mungu anapoona mambo yake hayafanywi kama alivyoagiza YEYE, au sehemu yake ya ibada, haitunzwi na kuiheshimu kwa kufanya yale tu aliyoagiza, Mungu anasema YEYE huwa hakai karibu na sehemu hiyo au watu hao. Hujitenga kabisa tena kwa mbali maana kufanya hivyo mbele za Mungu ni machukizo. “Akaniambia, Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, hata niende zangu mbali na patakatifu pangu?” – Ezekieli 8:6. Patakatifu pa Mungu leo, paweza kuwa ndani ya mioyo ya watu, sehemu ambayo RM anakaa. Ukipata muda tafadhali endelea kuisoma sura hii ya Ezekiel 8.
  Hayo ni kwa upande unaohusu matakatifu ikiwemo na ibada. Ukiangalia kwa upande wa mambo mengine mf. wizi, tamaa mbaya, ufisadi, chuki nk, hivi haya nayo ni ya Mungu kwa asili yake? Nimeileta kama changamoto, ili tuitafakari sote!!
  Jibu la pili, nalo ni zuri sana. Mbinu zetu za kumwabudu Mungu sharti zifuate utaratibu kama Mungu alivyoagiza. Tukifuata uchakachuzi wa ibilisi, Mungu hatasikia ibada zetu.
  Jibu la tatu, umenipa aya za kurejea. Lakini ninavyozisoma, nakutana visa vya akina Magdelena. Nafikiri ulimaanisha luka 2:8-20. Ninaposoma aya hizi hapa, naona habari za furaha kwa sababu ya dunia nzima kupata mkombozi. Sijaona kama kuna aya yoyote inayosema watu waadhimishe siku ya kuzaliwa Masihi. Hata hivyo, umejaribu kulitafsiri beyond the Bible. Yaani umesoma aya hizo ukazielewa zaidi ya vile zinavyomaanisha kwenye Biblia, jambo ambalo mimi linanipa changamoto ya kuweka mipaka kati ya mtazamo wako na uelewa halisi wa Biblia kwa njia ya RM. Mimi ninavyofahamu RM yupo kutuongoza kwenye kweli yote tu na siyo beyond ya hiyo kweli. Labda ukinipa biblical hoja za ku-refute uelewa wangu huu, nitafurahi kusikia kutoka kwako pia.
  Jibu la nne, ni zuri sana. Linajitosheleza.
  Jibu la tano ni zuri sana pia. Jinsi ulivyoliunganisha, linatia hamu ya mtu kujifunza zaidi. Nimefurahi sana. Umetetea vizuri hoja. Lakini hoja yenyewe, haina mizizi ya kibiblia. Ungekuwa wakili (na huenda ndivyo ulivyo), mteja wako licha ya kuhusika na kosa kabisa, mahakama ingempunguzia adhabu kutokana na utetezi wako mzuri. Strong premises, but hoja yenyewe, kibiblia inapwaya kaka. Ila kwa sababu tu na wewe umeithibitisha kuwa ni unbiblical na ilhali unaisherehekea, ndiyo maana unajenga ukuta imara hapa bila ya kuwa na msingi mathubuti kwanza .
  Jibu la sita, naomba kutofautiana na wewe kwa kiasi fulani. Nafanya hivi kwa nia njema sana. Kama kujifunza hakuhusishi ushahidi, watu wangemfahamuje Kristo isipokuwa kwa lile neno la manabii ambalo lilimshuhudia? Au umesahau kaka kuwa shahidi ni mtu wa muhimu sana sehemu yoyote ile? Hivi, sisi tungemfahamuje Kristo isipokuwa kwa mashahidi wake wawili – Agano la kale na jipya? Imani au taaluma ya kujifunza tu bila ya ushahidi, binafsi sikubaliani nayo. Tunapoambiwa habari za Yesu, tukaziamini, ni kwa sababu zimeandikwa na tunazisoma. Tunapoambiwa Yesu atarudi tena muda si mrefu na tukaamini, ni kwa sababu tunasoma na kuangalia dalili zilizopo na kisha tunaamini. Hata kwenye fizikia, kemia na biolojia, tulijifunza kwa majaribio – ushahidi!!
  Jibu la swali la saba, nalo natofautiana na wewe kiasi fulani. Kwa uelewa wangu, sidhani kama ni kweli Mungu aliyaficha baadhi ya mambo ili watu wasiyo na akili wayang’amue. Yale aliyoyaficha, aliyaficha kwa faida zake Mungu mwenyewe. Na ana makusudi maalumu kwetu kwa nini aliyaficha. Sikukuu ya Krismas, Mungu hakutaka iwemo ila watu wamejifanyia wao wenyewe chini ya mamlaka ya yule adui na kuihalalisha kuwa sikukuu ya kidini – sehemu mojawapo ya ibada. Kama Mungu angedhamiria Krismas iwepo, basi hata siku ya kupaa kwa Yesu mbinguni, leo tungesherehekea, kifo cha Yesu tungesherekea, naam wapo (waj2) wanaosherehekea kufufuka kwake na wamekufanya kuwa siku ya ibada japo ni mawazo na mitazamo ya watu tu isiyo na mizizi ya kibiblia.

  Mimi kaka Lwembe naamini sana Biblia kuliko kitu kingine. Naamini sana kuwa RM huwaongoza watu kuelewa yaliyomo ndani ya Biblia peke yake na si zaidi ya hapo. Naamini kuwa, yale Mungu aliyoyafunua kwetu, yanatutosha kabisa kutupeleka mbinguni na si zaidi ya hapo.
  Kuhusu umri wangu, nitakujibu kwa baruapepe yako binafsi. Nitafanya hivyo kwa maana sijaona umuhimu wa kusema umri wangu hapa SG.
  Ubarikiwe sana

 13. Siyi,
  Nami nakushukuru kwa kuyapokea maelezo yangu, ni kweli ni marefu kidogo, lakini ni kwa ajili ya kujaribu kuliweka jambo katika urahisi zaidi tu!

  Nikiyajibu maswali yako:

  1: Mfano wa kitu au jambo la Ibilisi lililogeuzwa kuwa Mungu hakuna! Ibilisi hana kitu wala jambo ambalo ni la kwake, yeye huyapindisha ya Mungu na kuyadai kuwa ni yake anapowadanganya wasio na RM! Alijaribu kumdanganya Kristo kuwa atampa himaya zake akimsujudia; unaona mwizi akijidanganya kumpa zawadi mwenye mali yake!!!

  2: Mungu si masikini wa chochote, hata ikiwa ni Ibada, bali watu wamedanganyika na uongo wa Ibilisi mpaka wanamuabudu na kuendelea kueneza uongo wake wa kumiliki visivyo vyake, na hivyo kuishia kumsujudia bila kujijua!

  3: Ibada ya Krismasi nimekuonesha katika Luka 8:2-20, utakuwa hujaelewa tu! Soma tena vifungu hivyo Mungu atakupa kuyaona rohoni yaliyotendeka katika siku hiyo Mbingu na Dunia vilipoungana yaani watakatifu, si kila mtu, hata hiyo Furaha!!!

  4: Mungu analiangalia Neno lake na si hisia wala nia zetu! Nia ya Kristo ndio pekee inayotubidi kuwa nayo. Kama Malaika walishuka na matarumbeta kupulizwa katika tukio hilo, basi siijui Nia inayoweza kuizidi hiyo!

  5: Kuhusu dunia kukutukuza Kuzaliwa kwa Yesu, hili liko katika urahisi kama unavyolitumia siku zote, hapo unapoidhihirisha imani uliyonayo katika kuzaliwa kwa Kristo, mnyororo wa maisha yako unapouvisha Nanga ya Kuzaliwa kwake, ndipo maisha yako yoote hurejea hapo kwanza kila siku unapoikiri tarehe ya siku hiyo! Hata Waislamu, kalenda yao ina mzizi wa kuzaliwa kwa Kristo, hapo mtume wao alipozaliwa, ule mwaka wa 570 Baada ya Kuzaliwa kwa Kristo!!!! Miaka yote imefungwa Nanga ya Kuzaliwa kwa Kristo, aidha B.C. au A.D; Imani ya siku hudhihirisha kwamba wewe ni mzima wa akili na hivyo unao wajibu, basi kukukiri Kuzaliwa kwa Kristo kunawatia Hukumuni wote wasiompokea licha kumkiri kwao!!! Na hata kesho usiku dunia nzima tutakutukuza kuzaliwa kwake hapo tunapoingia katika Mwaka Mpya!!!

  6: Kujifunza kunawezekana tu iwapo utakuwa na katika usikivu ulio katika unyenyekevu. Kutafuta Ushahidi katika Maandiko si kujifunza, huko kuna mhusu mtu aliyekomaa. Lakini kwa mtu anayejifunza, Mungu huwajibika zaidi kumfunulia aliyowaficha watafiti, akiwafunulia hao watoto wenye kujifunza! Lk 10:21 “Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza.”

  7: Kuyaficha mambo ninakokuzungumzia mimi, ni kwa ajili ya kuikata hulka ya watu ya kupenda kuabudu vitu na siku. Ukitazama vizuri utaona huwa anayaficha mambo mara nyingi ni kwa ajili ya ya kuwashusha hao “wenye hekima na akili” akiwafikisha mahali ambapo hubaki waki waya waya na kulazimisha kujishikiza katika aya za Biblia kwa nguvu! Hebu utazame uongo wa tarehe 25, si unawaona Wakatoliki wanavyojikausha? Hayo ya Siri yanabaki kama ulivyokinukuu hicho kifungu, ila ya kuficha ndio haya tunayoyacheka leo hii ukweli anapoufunua mwenye kuyaficha!!! Kuna mahali nimekusoma ukisema unafanya kazi siku sita na saba unapumzika, BIG UP kwa kufika ktk real understanding ya issue, badala ya kujiungia tu mambo kwa akili, kama hao akina Vai wanao hesabu mwezi wa sita wa mimba kuwa ndio June!!!

  Nako kufunuliwa kwa jambo hili ndiko huko unakokusoma ktk Luka katika maana ya kuadhimisha, yaani ulikuwaga unasoma tu na huoni chochote kwani ulikuwa hujafunuliwa kuhusu hiyo Sherehe iliyofanyika Mbinguni na Duniani kwa PAMOJA wakiungana; bali leo hii macho yako YAMEFUNULIWA!!!!

  Halafu Siyi hebu niambie umri wako, bila kumuhusisha Kristo, nitafurahi kuijua hiyo namna!

  Asante na karibu ndg yangu!

 14. Lwembe,
  Nashukuru kaka kwa maelezo mengi kiasi lakini yasiyojibu maswali yangu na badala yake, yameongeza maswali. Maswali yaliyoongezeka ni haya;
  5. Naomba unifafanulie vya kutosha namna dunia inavyokutukuza kuzaliwa kwa Yesu kwa kuangalia kalenda zetu. Huenda kweli sielewi hapa.
  6. Maelezo yako haya, sijayaelewa, nanukuu, “Pia, katika kuyafuata Maandiko, ni vizuri tukajiweka katika nafasi ya kujifunza kuliko kutafuta ushahidi!” Tunawezaje kujifunza Biblia bila ya kuwa na ushahidi wa Kibiblia?
  7. Halafu umesema kweli kuwa, “Mungu aliificha siku aliyozaliwa Mwokozi kwa makusudi kama alivyolificha kaburi la Musa.” Kama Mungu alifanya hivyo, kwa nini sisi tunataka kujua mambo ambayo Mungu hataki sisi tuyajue? Zingatia aya hii katika kujibu swali hili, “Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.” – torati 29” 29.

  Ubarikiwe kaka. Nakungoja kwa majibu mazuri yenye ushahidi wa kibiblia maana tunajifunza Biblia hapa na si kinginecho chochote.
  Nakungoja!

 15. …..Tunapoendelea,

  Siyi,

  Jambo la kwanza na la Msingi ni kuelewa na kukubali kwamba Kristo alizaliwa, na siku aliyozaliwa Dunia wala Mbingu havikukaa kimya, bali VILIUNGANA katika SHANGWE ya jambo hilo, nayo Shangwe hiyo ingali iki reverberate katika makusanyiko yetu ya Kikristo hata leo hii, huko ndiko kuwa tukio endelevu katika maisha yetu mapya!

  Kuhusu ushahidi wa Kimaandiko unaotuambia “Tukuadhimishe Kuzaliwa kwa Kristo”, nadhani utakuwa tu hujalielewa jambo hilo kimaudhui katika ujumla wa kuyapokea maagizo hapo yanapotolewa. Kuadhimisha Kuzaliwa huku, kunamtokea huyo aliyeijua maana ya kuzaliwa huko, maana ambayo inaambatana na furaha ya jambo hilo kulingana na Neno la Mungu lililoiamuru “Furaha Kuu” hiyo iwe kwa watu wote which includes me and you if at all umekielewa anachosema Mungu; yaani Neno hilo ndilo lililoiumba hii “Furaha Kuu” unayoiona leo hii ndani yetu!!!

  Mungu aliificha siku aliyozaliwa Mwokozi kwa makusudi kama alivyolificha kaburi la Musa. Kwahiyo Uongo wa Wakatoliki hauubadili Ukweli na kuufanya ukweli huo uwe si muhimu, otherwise UNATAKIWA uyarejeshe na uyamiliki yote hata yaliyoibiwa na watu wa dini na si kuwasusia! Hakuna siku wala tarehe inayomuhusu Shetani, siku zote ni za Mungu, nao walio katika Ufalme wake huzitawala siku hizo ndio maana unamuona Joshua akilisimamisha jua bila kufanya maombi! Pia jambo la Furaha ni la starehe, kwahiyo kumbukumbu hiyo inaishia katika Furaha ya Udhihirisho au manifestation ya Hatua ya Kwanza ya Mungu alipofanyika Mwili ili kuukamilisha Wokovu wangu!!!

  Ukitaka kulifananisha jambo hili la Kuzaliwa na Agizo la Meza ya Bwana na Pasaka yake, utakuwa umeikosa hata maana ya Agizo la Pasaka! Hauwezi ukawa na Mwanakondoo wa kumtoa katika Pasaka bila ya Mwanakondoo huyo Kuzaliwa! Tena kondoo wa kumtoa humchagui randomly, hapana, unavikagua vigezo ulivyopewa tangu siku anazaliwa, na kisha unamtunza kwa ajili hiyo; usifanye kama wale wafanya biashara wa Hekaluni waliokuwa wakiwauzia watu wasiyoijua maana kwa kuongozwa na dini zao, kondoo ovyo ovyo mpaka wakatimuliwa!

  Uadhimishwaji wa Pasaka kwetu hulikamilisha jambo hilo kwa kumtoa Mwanakondoo huyo aliyezaliwa kwa ajili hiyo, ndipo sisi hukuadhimisha kutolewa kwake katika jinsi halisi ya namna anavyotolewa, ni Mwanakondoo tunayemjua, nasi kama ilivyokawaida, humshika Mwanakondoo huyo hapo anapochinjwa ili kuungana naye ule uhai unapomtoka, nasi huinywa Damu yake na kuula Mwili wake, ili kuupokea ule Uzima uliomtoka!!! Kwahiyo sisi huliadhimisha jambo hilo katika maana hiyo HALISI ambayo HAIAMBATANI na Furaha kamwe, bali kuyajutia yaliyotushinda tukiya renew maisha yetu na Vows zetu hata kupata Ujasiri wa kuendelea na Injili, ndipo mzunguko huo hujirudia na kuturejeshea Furaha ya Kuzaliwa kwake ikiifunika Huzuni inayofuata ambayo hulipukia katika FURAHA KUU zaidi katika ile Siku ya Bwana hapo tunapofufuka naye siku ile ya Jumapili ya Pasaka inayotuingiza katika Pumziko la Milele kiroho, ndipo kusanyiko hilo huwa ni tofauti, maana hao wamefufuka, si wafu tena wasio na ijara!!!!

  Ubarikiwe!

 16. Siyi ndg yangu,

  Ni jambo jepesi lakini linafanywa kuwa gumu kwa sababu ya dini! Watu wengi wako hapa kutetea misimamo ya dini zao kuliko kujifunza, wanaiogopa saaana Kweli!!!

  Kwa mfano, ni kwa kukosa ufahamu tu ndio hatutambui kwamba katika maisha yetu, waaminio na wasioamini, kwa pamoja hukutukuza kuzaliwa kwa Kristo kila tunapoirejea kalenda kujua leo ni siku gani; ndipo tungesema, labda ni siku ya 27 ya mwezi wa Desemba, mwaka wa 2013 “Baada ya Kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo”!!! Umeona Siyi, dunia nzima inalitukuza jambo hilo kila siku!

  Ki Maandiko kuzaliwa kwa Yesu kuliadhimishwa kama unavyoyaona Maandiko yanavyojishuhudia ktk Lk 2:8-20. Sehemu ya tangazo hilo inasema, “…kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya FURAHA KUU ITAKAYOKUWA KWA WATU WOTE”; kwahiyo inategemea hali yako ya kiroho ilikuwaje ulipoipokea habari hii ya kuzaliwa kwake. Maana katika wote walioletewa taarifa za kuzaliwa kwake, hakuna hata mmoja aliyejituliza kimya kana kwamba hakuna kitu kilichotokea, wema kwa wabaya, wote waliinuka kufanya jambo fulani. Wema waliondoka kwenda kumuabudu wakimtolea sadaka, na wabaya waliinuka kulipinga jambo hilo kwa nguvu zote, pamoja na umwagaji wa damu!!!

  Kwahiyo tukio hilo la kuzaliwa kwa Mkombozi, liko hivyo, yote yaliyotokea si ya kawaida, na hayajawahi kuwa ya kawaida kwa yeyote yule, hata ajibaraguze vipi, ukweli ni kwamba kiroho anakuwa ameungana na kundi mojawapo ya hayo mawili, lile linalotafuta kukiangamiza “Kitoto” hicho cha Ajabu, au kundi lililosherehekea huko Kuzaliwa Kwake; nalo jambo hilo linaendelea mpaka leo!!

  Katika ulimwengu wa kikristo, Warumi walipoupokea Ukristo, ni kwamba waliipokea Injili kwanza, na baada ya kuipokea ndipo wakaipindisha, maana hauwezi kukipindisha kitu usichonacho!

  Pia, katika kuyafuata Maandiko, ni vizuri tukajiweka katika nafasi ya kujifunza kuliko kutafuta ushahidi! Haya yote tunayoyasoma, ni matukio yaliyorekodiwa kwa ajili yetu, yanayotuonesha mapito ya Kanisa katika nyakati Ngumu sana hapo Msingi ulipokuwa ukijengwa!! Paulo anatuhakikishia HAKUNA Msingi mwingine zaidi ya huo walioujenga!! Kazi ya Msingi ikiisha kumalizika, basi yanayofuata ni mepesi, ndipo katika wepesi huo Katoliki wakaliona na la Kuzaliwa kwa Mwokozi, wakalichukua na kulijumuisha ktk Mpindo wao!

  Spiritually, hilo jambo la Mpindo, lilikuwa na nguvu na starehe kubwa kwa yule ‘roho’ anayewaongoza ktk uongo huo, pale anapoyaona makundi makubwa ya wakristo yakishiriki uongo huo wa tarehe inayomuhusu shetani, ktk JAMBO LA KWELI! Tena si kwa wanaoshiriki tu, bali hata hao wengine, ambao kutokana na kuugundua kwao uongo huo wa siku, wanakataa kata kata kulikubali jambo la kuzaliwa huko katika maana ya kumbukumbu ktk jinsi yoyote ile, wakijitahidi kukaa mbali na jambo hilo la Kweli linalopaswa kuwapa FURAHA KUU, bali wao huishia kujibanza pembeni kama wafiwa, hili humpa starehe zaidi yule roho!!!

  ………. nitaendelea!

  Ubarikiwe!!

 17. Seleli,
  Mtazamo wako mtu akiusoma, anakuwa na maswali mengi sana. Mimi nikuulize machachetu.
  1. Kuna mfano wowote ndani ya Biblia wa kitu au jambo ambalo kwa asili yake lilikuwa ni la ibilisi, halafu watu wakaligeuza kuwa la Mungu na Mungu akalikubali?
  2. Hivi ni kweli kabisa kuwa Mungu siku hizi amekuwa masikini sana wa mbinu au njia za kumfanyia ibada hadi tuige kutoka kwa ibilisi?
  3. Kama jambo hili la Krismas halipo ndani ya Biblia, mnatumia vigezo gani kuweka mipaka ya jinsi ya kulisherehekea ili msitende dhambi?
  4. Unaweza kunipatia mfano wowote ndani ya Biblia, wa watu waliokuwa na NIA tu lakini hawakufuata taratibu za kutimiza NIA hizo, lakini walifanikiwa na Mungu aliwasikia?

  “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi” – Isaya 8:20

 18. By the way, TUWE NA UFAHAMU HUU…si kila kitu ambacho hakiko ktk andiko ni dhambi tukikifanya eg tunasherehekea siku ya Uhuru wa Nchi, Ndoa Miaka kadhaa, Utumishi miaka kadhaa, Kumaliza masomo baada ya muda fulani, YOTE HAYA hayapo ktk Biblia but tunayayafanya, where is sin or pepo in that? vitu vingine ni by common senses we make clear and perfect judgement hapa CHINI na JUU wako fine kabisa hawana shida, as long as tuvifanyavyo, haviharibu KWELI ya Neno-life is that simple basii, mengine ni religious dead complications kama vile zinamtetea Mungu sana au za kiroho kweli au zia uhai kweli kumbe walaa mbinguni hawana time wala tija na hayo, ni tabu tu ya ufahamu au masumbufu ya Wana dunia hii ya ufinyu wao wa mambo mazito na ya kweli ya rohoni na kujikita kwa ya mwilini na taratibu tupu patupu!

  Kwamba siku na tarahe au majina ya miezi au historia ya sherehe izi ni paganism, so what? hii nayo ni lack of real issues and sleeping on the negligible. Kitu hata kama kilikua devilish formerly but sasa kikageuzwa kwa utukufu wa Mungu eg Mfalme Nebukreza, sisi kabla ya kuokoka tulivyokua full devo na laga, mali zetu-viwanja, migodi, nyumba 100, magari 200, tulizopata wakati wa devo times in our life/jobs/dealings kisha TUNAOKOKA, je hatuwi wapya SISI na WOTE na VYOTE tulivyonavyo?

  Tukiamua out of one’s joy kama Zakayo kurudisha, its fine but not God’s commands. Ndio maana hata ktk ndoa, Paul anasema ukiwa na Mume hajawa mwamini, kwa kukaa naye na kama naye anaridhia, basi watoto wazaliwao wametakaswa hata kama wanatokana na Mzazi mmoja bado yuko full devo. Kama Mtu full imani kwa devo-isiyo ya kwa Kisto Yesu, anahesabiwa haki mpaka kwa watoto wake kwa kua/kuishi na Mwamini sembuse siye kuinyakua siku/mwezi wa formerly used for devo, sasa tunamkandimiza devo chini na kuvitwaa vilivyokua vyake(as a matter of fact-si vyake maana hana vitu hapa duniani) bali utumia vya Mungu kufanya yake).

  Mbona ni rahisi kabisa kuelewa kwa logic iyo kiroho, shida iko wapi? ni dini ya mtu imemuniga koo la rohoni au serious kuna kukosekana ufahamu wa mambo innocently and sincerely kunahitajika shule hapa au?

  Enjoy spiritually and physically X-Mass season always conceptually and not peanut dates/days/months thing/mentality.

  Press on.

 19. Kama ni ya Kikristo au siyo, nina majibu 2

  Moja, Inakua ya Kikristo kwa sababu ya Yule aliyezaliwa-Yesu Kristo na wala si day yenyewe, tungeweza kuamua mwezi wa kukumbuka kuzaliwa Bwana uwe June na tunasherehekea kimwili-pilau na pork kwa sana tu na kiroho-ibada ya sifa, kuabudu na shukrani kwa sana kabisa NA BADO MBINGUNI tungekua sahihi hata kama mwezi tulioamua haupo ktk Neno-haitakua dhambi- Mbinguni hawako interested eti tunakua smart sana kupata day/mwezi ambao Mwana wa Mungu alizaliwa! mmh! hawana time, appitite wala haja iyo na nadhani wakiona Wanadamu wana fight ipi ni day/mwezi..wana-conclude ktk file na folder kua.. wako fools kwa sababu wako after chicken and not ostrich!!!!!!!

  Pili, haiwi ya Kikristo hata kama kweli tarehe na siku ni accurate kua ndio alizawaliwa. Tukisherehekea, kukumbuka kuja kwa Mwokozi wetu live duniani kwa msukumo/mentality/joy/pride out of our capture ya accuracy ya date/days/months na si mantiki ya why his coming-regardless ya timings calculations, bora Watu wakalime tumbaku na bange Mashamba ya Mtera na Turiani mpaka Mkinga kuleee.

  Yote tisa, kumi Christmass hata kama tunandika X-mass, ehe ndio nini kwani au kuna soo gani kwa Baba? mmmmmh! walaa hakuna shida maana what always matters ambacho kwa icho Mungu huukumu Wanadamu ni nia. Kama naandika xmass niki maanisha very simply kua nimefupisha tu neno hilo, JUU wana noma gani? hamna lolote, ayo ni beyond needs conceptualization of very light matters

  Press on

 20. Nelson,
  Wewe, ni mkristo- mfuasi wa Kristo. Unapaswa kuishi kwa kufuata neno la Mungu na si vinginevyo. Ni ukweli kuwa, kufanya jambo lolote nje ya neno ni dhambi. Na kama umesoma kile kitabu, umeambiwa kuwa, Krismas chanzo chake ni upagani. Sasa rafiki, tangu lini upagani(giza) na nuru(Kristo), vikapatana? Je, umeshaishi kwa mujibu wa neno hadi ukalimaliza na kudandia yale yasiyokuwemo kwenye neno kama Krismas?
  Nakutia moyo kama mkristo unayepanga kwenda mbinguni, uachane na krismas, maana ni upagani – ibada ya shetani iliyovikwa vazi la kikristo.
  Ubarikiwe kaka

 21. Sasaa!tatizo ni tarehe na mwezi au haitakiwi kabisaaa kuadhimisha ckuku yenyewe?je kama mitume hawakuadhimisha na biblia hajaongea kuhusu hilo je imehalalishwa ni dhambi kuadhimisha cku hiyo?shida iko wapi?

 22. Lwembe,
  Binafsi, nimefurahi sana kukuona mtu usiye Siyi wala Lenda, ukipinga sikukuu ya Krismas. Na umesema kweli kabisa, uadhimishaji wa Krismas, ni uongo wa wakatholiki. Hilo liko bayana.
  Sitaki niende mbali ya hapo, nataka nikurudishe Lwembe kuwa, tukio hili hata kama lisingegeuzwa na waroma, bado hatupaswi kuliadhimisha. Maana tofauti na sherehe ya kuzaliwa kwa Kristo, sherehe iliyokuwa imelenga kwenye WOKOVU wa mwanaamu, hakuna hata aya moja ndani ya maandiko ya injli yanayoonesha kuwa Yesu aliitukuza siku yake ya kuzaliwa. Wala hakuna hata mtume mmoja wa Yesu aliyefanya hivyo kwa ajili ya Bwana wake kuzaliwa.
  Aidha, kuzaliwa kwa Kristo ndani ya mioyo ya watu, hakuna muda maalumu. Pale mtu anapompokea Yesu ndipo kuzaliwa kwa Yesu mtu huyo hudhihirika ndani ya moyo wake. Hivyo, hata kama waroma wasingeligeuzageuza tukio hilo, HATUNA HATA AYA MOJA NDANI YA BIBLIA INAYOTUAMBIA TUADHIMISHE KUZALIWA KWA KRISTO KILA MWAKA TOFAUTI NA KULIFANYA TUKIO HILO ENDELEVU NDANI YA MAISHA YA MWANADAMU.
  Na hata kama lingekuwa sahihi kibiblia, kwa sababu waroma waliligeuza, basi tulipaswa kuifuata Biblia na si uongo wa waroma. Maana kuendelea kufuata ufedhuli wa waroma, Mungu asingekuwa tayari hata kidogo kusikia sala na shukrani zetu. Intention na modality ya kufanya mambo ambayo Mungu ameagiza, sharti viende pamoja. Ukipuuza kimojawapo, Mungu huwa hayuko tayari kukubaliana nawe. Intention ya Kaini, ilikuwa ni njema sana – kutoa sadaka. Lakini alipokiuka modality, Mungu hakuzipokea sadaka zake. Kama Mungu hakusema tuadhimishe siku yake ya kuzaliwa, hatuna budi kutii hilo. Kama Mungu alitoa utaratibu wa kumwabudu, hatuna budi kuutii huo. Tofauti na kufanya hivyo, tunatafuta matatizo mengine tu.
  Hatupaswi kuongeza mambo ambayo Mungu hakuyasema, wala hatupaswi kuyapunguza yale aliyoyasema. Na kwa kufanya hivi, Mungu anatuita kuwa ni watii wa neno lake.
  Ubarikiwe sana.

 23. Siyi, Lenda & all,

  Ukweli wa Biblia kuhusu kusherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo, hilo liko wazi sana kwa asiyefungwa ufahamu kwa dini na mapokeo yake: Lk 2:8-20
  “Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; KWA KUWA MIMI NINAWALETEA HABARI NJEMA YA FURAHA KUU ITAKAYOKUWA KWA WATU WOTE; maana LEO katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe. MARA WALIKUWAPO PAMOJA NA HUYO MALAIKA, WINGI WA JESHI LA MBINGUNI, WAKIMSIFU MUNGU, NA KUSEMA,
  ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI,
  NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA.
  Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, … Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.”

  Sherehe ya jambo hili inawahusu hao watu wote walioipokea hiyo “HABARI NJEMA YA FURAHA KUU ITAKAYOKUWA KWA WATU WOTE” nao udhihirisho wa kuipokea habari hiyo ndiyo hii furaha tuliyonayo kulihusu jambo hilo, uongo wa dini notwithstanding!

  Kwamba Kristo alizaliwa Decemba, hilo si kweli, maana katika mwezi huo ni majira ya baridi huko mashariki ya kati kwahiyo usingetegemea uwakute wachungaji huko makondeni! Pia Kristo ni Mwanakondoo, kwahiyo asingezaliwa nje ya majira wanayozaliwa kondoo ambayo ni mwezi wa tatu/nne; tena yeye ni Mkombozi, basi mwezi wa Ukombozi ni Abib (April), ndivyo mambo yanavyokwenda, ktk mpangilio!

  Halafu kuna kundi kama Siloamu na wengineo, wao wameichukua kauli ya Biblia ktk Lk 1:26-27 “MWEZI WA SITA, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.”
  Ndipo wakachukulia kwamba mwezi wa sita unaotajwa hapo ni mwezi June! Lakini huo ni mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeth!!! Maelezo yanayoonekana ktk kifungu cha 26 yameanzia huko juu, yakimhusu Elizabeth huyo aliyetawa miezi mitano, na katika mwezi wa sita ndipo malaika Gabrieli akamtembelea Mariamu, unaweza kuyaona maelezo yanayolidhihirisha jambo hilo ktk kifungu cha 36 “Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na MWEZI HUU NI WA SITA KWAKE YEYE ALIYEITWA TASA”!!!

  Kwamba Wakatoliki wameipachika sikukuu hiyo mwezi Decemba kulingana na sikukuu zao za kipagani za Kirumi, hilo ni kweli inayojulikana na ndio maana tunaisema hivyo; kwamba inajulikana! Basi ukiujua ukweli wa jambo, licha ya kwamba limegeuzwa, Je, hilo laweza kulibadili jambo la msingi? Labda uwe umekosa mwelekeo, lakini uongo wa Wakatoliki hauwezi kuibadili kweli ya Injili na Uhuru unaoambatana nayo, maana haturudi kuzitukuza siku wala tarehe, bali tunalitazama tukio katika hali yake Halisi, kwamba katika majira fulani Mwokozi alizaliwa nayo furaha ya jambo hilo ndio hii, kama nawe u mmoja wapo wa hao walioletewa habari njema hizo!!!!

  Basi tumeichukua siku hiyo ya uongo wa Kikatoliki tumeifanya Kumbukumbu ya Kweli ya Kuzaliwa kwa Mwokozi katika majira aliyozaliwa, nasi tukikuadhimisha kuzaliwa huko katika maana hiyo tu, bila kuujali uongo uliokufa!!!

  Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia!!!

  Nawatakia Xmas njema, Kristo anapozaliwa ktk mioyo yenu!!

  Gbu all!

 24. Tumaini Nelson,
  Kifupi nikwambie tu rafiki kuwa, KRISMAs ni sherehe ya kiPAGANI. Licha ya kuisoma Biblia, mwulize mchungaji yeyote atakwambia ukweli wa mambo. Mpaka sasa, hakuna mtu asiyejua historia na malengo ya Krismas kuingizwa ndani ya ukristo.
  Mimi nakutia moyo, uchimbe kuhusu hilo.

  Soma kitabu hiki cha Christmas, Easter, and Halloween pdf by Vance Ferrell.
  Google tu kipo na utanufaika kwa uelewa tele.
  Ubarikiwe sana

 25. CHRISMAS -CHRIST+ MASS NI FURAHA

  MASS NI MISA MAANA YAKE KIFO – IBADA YA KIRUMI INAYOTOKANA NA KUTOA DHABIHU MWILI WA KRISTO KWA KUUKATA VIPANDE VIPANDE.

  SIJUI KAMA WAKRISTU WENGINE IBADA ZAO ZINAITWA MISA/MASS.

  IBADA YA MISA WATU HUGAWANA HOST-VICTIM “hostial”
  DHABIHU HIZO HUTOLEWA KILA MISA KUONYESHA DHABIHU ISIYOTOSHEREZA.
  KWA KUSEMA WANAUWEZO WA KUMSHUSHA YESU TOKA JUU NA KUMTOA DHABIHU.

  WAEBRANIA 10:12
  “LAKINI HUYU, ALIPOKWISHA KUTOA KWA AJILI YA DHAMBI DHABIHU MOJA IDUMUYO HATA MILELE, ALIKETI MKONO WA KUUME WA MUNGU”

  KAMA DHABIHU YA YESU YANITOSHA SIHITAJI MASS/MISA

  Shida ya pili ni tarehe hiyo/KWA NINI BABELI WALIACHIA WAFUNGWA SIKU HIYO?

  YEREMIA 52:31
  “HATA IKAWA, KATIKA MWAKA WA THELATHINI NA SABA WA KUHAMISHWA KWAKE YEHOYAKIMU, MFALME WA YUDA,KATIKA MWEZI WA KUMI NA MBILI, SIKU YA ISHIRINI NA TANO YA MWEZI, EVIL-MERODAKI, MFALME WA BABELI, KATIKA MWAKA WA KWANZA WA KUMILIKI KWAKE, AKAMWINUA KICHWA CHAKE YEHOYAKINI MFALME WA YUDA, AKAMTOA GEREZANI.”

  KWA NINI MKUTANO JUU YA SHEREHE HIYO ULIACHA KUNDI JINGINE LIKIKANA TAREHE YA SHEREHE HIYO/ NA JINA LAKE?

  UFUNUO 17:4
  “NAYE ALIKUWA NA KIKOMBE CHA DHAHABU MKONONI MWAKE, KILICHOJAWA NA MACHUKIZO, NA MACHAFU YA UASHERATI WAKE”

 26. Eeehe!kuna shule gani tena kuhusu krismas?maana naona wengine wanapinga wengine wana support!Bro Sungura na wa wana S.G nipe shule mdogo wenu wa kiroho nami nijue kweli.

 27. Bwana nimwema sana wependwa hebu tupende kuchangia vitu ambovyo vipo kwenye Biblia tusije tuka poteza watu wa MUNGU na kitabu kinochotoa uhalisia ni Biblia tu kwa hiyo kama kuna sehemu biblia inazungumzi xchrismass is ok lakin kama hamu tufanye YESU azaliwe upya kila siku ktk maisha yetu MUNGU Awabarik sana zaid atupe hekima ya kutambua mafundisho yeke husan ktk nyakat hizi za kuridi kwake

 28. Ivi mnajua kuwa hatusherekei siku ya krismas bali tunasherekea kuzaliwa kwa Yesu? Kwa hiyo kama kuzaliwa kwa Yesu kunapendeza kusherekewa basi hata kama tutaamua iwe tarehe 30January sawa tu.

  Kumbukeni hata pasaka tunayosherekea haijasemwa kwenye biblia kuwa tuisherekee. Wengi watasema imeandikwa na ilisherekewa tangu agano la kala. Ya agano la kale siyo tunayosherekea sisi. Ya agano la kale iliitwa ‘PASSOVER’ ya kwetu ni Easter, tukimaanisha kusherekea kufufka kwa Yesu ambako biblia haijaandika popote kuwa tukusherekee, wala siyo pasaka ya malaika wa kuharibu alipoziacha nyumba za wayahudi waliopaka damu miimo ya milango yao pale Misri.

 29. Wapendwa,

  Mada hii imenigusa sana hadi nikasema haiwezi kupita bila kuchangia chochote. Ukweli napenda kuwahakikishia wapendwa wote kwamba:

  YESU ALIZALIWA TAREHE 25 DESEMBA. Kama kuna mtu anabisha hajui maandiko. Kwa watu wanaoyajua maandiko watakubaliana na mimi kwamba YESU ALIZALIWA TAREHE 25 DESEMBA.

  Nashangaa kuona hakuna hata mchangiaji mmoja anayelitaja au kulieleza hilo vyema. Wachangiaji karibu wote wanazunguka tu wapo wanaosema kwamba pamoja na kwamba haijaandikwa siyo vibaya kuisherehekea na wapo wanaoona kwamba ni upuuzi kabisa kuisherehekea siku ya kuzaliwa Yesu kuwa ni Desemba 25.

  Kwa wote wanaokubali kwamba Kalenda ya sasa tunayoitumia ni ya uhakika na huwa haikosei, basi lazima akubali kwamba Yesu Kristo alizaliwa Desemba 25. Wala huna haja ya kubisha.

  Soma Maandiko vizuri. Maandiko yanaonesha kwamba wayahudi walikuwa na desturi ya kuwatahiri watoto siku ya nane baada ya kuzaliwa. Ukisoma maandiko yanaoenesha kwamba Yohana Mbatizaji alitahiriwa siku ya nane baada ya kuzaliwa. Watoto wote wa kiyahudi walitahiriwa SIKU YA NANE. YESU NAYE ALIPELEKWA KWENYE TOHARA SIKU YA NANE BAADA YA KUZALIWA. (Luka 1:59, 2:21)

  Nanukuu, ” Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri aliitwa jina lake Yesu……..” Luka 2:21

  Wote wapendwa mtakubali kwamba siku ya nane ambayo imetajwa huwa ni tarehe moja mwezi wa kwanza. Hii kusherehekea sikuu kuu ya mwaka mpya kwa ufupi ni sherehe iliyopaswa kusherehekea KUTAHIRIWA KWA YESU. Kwani alizaliwa tarehe 25 Desemba na ukihesabu kuanzia tarehe 25 Desemba hadi tarehe moja mwezi wa Kwanza ni siku nane.

  Kwa hiyo, ukweli ni kwamba YESU ALIZALIWA DESEMBA 25 NA AKAFANYIWA TOHARA JANUARI MOSI. YAANI SIKU YA NANE KAMA YANENAVYO MAANDIKO.

  Kama ukweli hauukubali basi hata kalenda hii tunayoitumia naomba usiikubali wala usiitumie kwenye kuwekeana miadi na mtu. Labda kama unatumia kalenda ya kiislam. Tukumbuke kwamba kalenda hii inayotumiwa na dunia nzima ukiacha kalenda zingine kama zile za kiislam au imani zingine hii ni kalenda ya Kikristo kabisa.

  Mwisho, Yesu alizaliwa tarehe 25 Desemba na akatahiriwa tarehe 01 Januari. Na siku zote hizo ni shangwe duniani kote wanakomwamini Yesu kuwa ndiye mwanzilishi wa kalenda hii.

  Ufanye sherehe au usisherehekee Krismas tarehe 25 Desemba utasherehekea kwa lazima tarehe ya kufanyiwa tohara Yesu Kristo siku ya Nane yaani Januari Mosi upende au usipende. Mbona unawaambia watu HERI YA MWAKA MPYA?

  Kuanzia leo usiseme kwamba maandiko hayajasema wazi Yesu alizaliwa tarehe ngapi, labda wewe ndiye husomi maandiko kwa uwazi.

  Mr. Milinga.

 30. mi-maada hii imenigusa sana lakini sina mengi sana ya kuchangia.kwa ufupi ninavyofahamu mimi:tarehe hiyo ilikuwa ni ya mungu wa jua katika historia za kale,pia katika tarehe hiyohiyo,waisrael walikuwa wakikusanyika katika magulio yao (masoko)katika kununua bidhaa mbalimbali kama vile weekend kwa huku kwetu..kiufupi ilikuwa ni siku maalum kwa israel wale walioamini mungu jua.katika kumsimamisha yesu kristo waisrael waliangusha imani ile ya mungu wa jua na kumsimamisha mungu wa kweli kama kumbukumbu ya ushindi ili siku ile iwe siku ya kuangushwa na kusimamishwa kwa mungu wa kweli.kwa hiyo tarehe ile sio tarehe haswa ya kuzaliwa kwa mwokozi wetu bali tunaiadhimisha kama kumbukumbu ya ushindi wa kuangushwa kwa mungu wa uongo na kusimamishwa kwa kristo…ndio maana tunasema siku ya kuzaliwa kwa kristo.ndiyo maana wakristo leo tunaisheherekea siku ile kwa kumkumbuka kristo na wala hatumkumbuki yule mungu wa jua kwa kuwa aliangushwa na mungu wa kweli. Kama tungemkumbuka mungu yule wa jua lingekua tatizo kubwa sana la kiimani…lakini si hivyo kabisa…mungu anaangalia roho na roho zetu ni ushuhuda tosha mbele za mungu na wala si hila za ibilisi na mawazo ya kingundi fulani ndivyo vitutenge na kristo.ushuhuda kwa mungu katika kristo ni roho na wala si mwili siku na akili za watu fulani katika kuchafua imani…hata tukimfurahia kristo siku ya WAJINGA DUNIANI… bado mungu wetu atakuwa shuhuda roho zetu katika kristo na wala si siku hiyo ya wajinga…WAJINGA WATAWAZA UJINGA KATIKA SIKU HIYO NA WAKRISTO WATAWAZA KRISTO SIKU HIYO.kumbuka tunakwenda kwa imani na roho sio kwa siku na sabato kwa kuwa sisi sio watoto wa mtumwa tena bali ni watoto wa muungwana.

 31. Kwa ufahamu wangu mimi kati ya tarehe 15 mwezi 12 hadi tarehe 15 mwezi january kipindi hiki chote kinaitwa majira ya christimas kwa maana kwamba siku mojawapo yeyote kati ya kipiondi hicho Yesu alizaliwa.Jambo hilo ni kweli kutokana na sababu hii kwamba Injili ya Luka imeandikwa na Dr.Luka ambaye alikuwa anamuandikia kiongozi mmoja mkubwa wa kirumi aliyeitwa THEOFILO MTUKUFU yaani mheshimiwa ambaye alimuomba Luka amuelezee kwa ufasaha habari za Yesu tangu wakati wa kuzaliwa Kwake hadi Kufufuka na kupaa! soma Luka 1:3-4. Kipindi hiki kulikuwa na Kalenda za aina mbili kama ilivyokwetu leo kwamba mathlani hapa kwetu kuna kalenda mbili ya kwanzani ya kiserikali ambayo inaanza tarehe 1/7 na kuishia tarehe 31/6, kalenda ya pili ni hii inayotumiwa na watu wote inayoanza tarehe 1/1 hadi 31/12.Hali kadharika wakati huo kulikuwa na kalenda mbili ya kwanzailikuwa ni ya kirumi ambayo tofauti na sisi kidogo yenyewe ilikuwa inaanza katikati ya mwezi wa 10 hadi katikati ya mwezi wa 9 ambayo ilikuwa ni kalenda ya kiserikali, halafu kulikuwa na kalenda ya kiyahudi ambayo yenyewe haipishani na hii ya kawaida tofauti yake kidogo yenyewe inaanza katikati ya mwezi 1 na katikati ya mwezi 12.Luka wakati anaandika injili yake alitumia kalenda ya kirumi jambo hili unaweza kulipata katika ufuatiliaji wa historia ya kitabu hicho katika mtandao, sasa ukisoma katika Luka1:26 maandiko yanasema kwamba MWEZI WA SITA malaika alimtokea mariamu na kumueleza kuwa atachukua mimba kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Mwezi huu wa sita tukumbuke kwamba ni kwa kalenda ya kirumi ambapo ukileta katika kalenda ya kiyahudi ni MWEZI WA TATU ambapo ukihesabu miezi TISA ambayo ni hali ya kawaida tangu mimba kutungwa hadi kuzaliwa utagundua kuwa inaangukia MWEZI WA KUMI NA MBILI ambapo sasa kwa kalenda ya kiyahudi ambayo haipishani sana na hii ya kwetu ni KATIKATI YA MWEZI WA 12 NA WA 1.Ndio maana kuanzia tarehe 15/12 hadi 15/1 yanaitwa ni majira ya krismass, kwa hiyo kwa upande wangu mimi sina mashaka juu ya hili kwa sababu ni HAKIKA.
  Kuhusu neno Christmass, ukweli ni kwamba kule mashariki ya kati katika majira ya kati ya tarehe15/12 hadi 15/1 kutokana na hali ya hewa ya kipindi hicho kulikuwa na aina fulani ya miti ambayo ilikuwa ikiota katika majira haya ambayo ilijulikana kwa Jina Christmass trees yaani mi-christmass na kulikuwa na tabia ya watu wa nyakati hizo ambao hawakuwa wakristo kufanya sherehe majira haya mpaka alipoongoka mfalme mmoja wa nyakati hizo aliyeitwa konstantino na kufuta sherehe za kipagani zote akaamuru kwamba majira hayo yawe ya kukumbuka kuzaliwa kwa yesu yaani majira ya mi-christmass!
  Wako baadhi ya wakristo ambao wanapinga vikali kusherehekea christmass kwa kusema kwamba hakuna mahali ambapo Biblia imeagiza tufanye hivyo wenzetu hawa ni kama wasabato na mashahidi wa jehova wanapinga sana! Ukweli ni kwamba HAKUNA KOSA KUSHEREHEKEA CHRISTMASS ni kukosa ufahamu kimaandiko ni muhimu kuelewa kuwa wa kwanza kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu alikuwa ni Mungu mwenyewe na malaika mbinguni angalia Luka2:13 inasema hivi………Mara walikuwepo pamoja na huyo malaika WINGI wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema atukuzwe Mungu juu mbinguni na na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Vile vile Luka 2:10 inasema…….Malaika akawaambia msiogope kwakuwa mimi ninawaletea HABARI NJEMA YA FURAHA KUU ITAKAYOKUWA KWA WATU WOTE!
  Furaha kuu ni pamoja na kusherehekea, furaha kuu ni KUU kweli kwani haijawahi kuwepo sherehe yeyote duniani inayosherehekewa kwa ukuu kama Christmass.
  Mungu awabariki sana wapendwa!

 32. Mr Lwitiko ndiyo maana nilitangulia kusema “sijui kama utaamini hili nitakalosema juu ya ushuhuda wa Nam Choo”. watu wengi hawaamini shuhuda kwakuwa sio wao walioshuhudia hayo yaliyotukia. Ndiyo maana hata Tomaso akawaambia wanafunzi wenzie, “mimi nisipoziona alama za misumari mikononi mwa Yesu na kuona ubavu waliomchoma mkuki sitaamini kuwa Yesu amefufuka.” Hapa hatuongei suala la mavazi ya Yesu maana haiwezekani kuwa huko mbinguni hawavai mavazi kwa vyovyote vile wanavaa, wanabadilisha au hawabadilishi mavazi hiyo si issue.
  Tunazungumza uhalali wa kusherehekea Christmas (sio X-mas), mimi ninasema ikiwa wanadamu tunasherehekea siku zetu za kuzaliwa si zaidi sana siku ya kuzaliwa Masihi? Achana na huo ushuhuda wa Nam Choo maana wewe hautakusaidia!

 33. Kuna utata mwingi sana,mimi nashindwa kuelewa? hasa kile kitu unachosema Ndugu John, ina maana huwa Yesu anabadilisha mavazi? kuna siku nyingine ambayo huyo mama aliwahi kwenda mbinguni akamkuta Yesu ana mavazi mengine? mpaka amuulize mbona leo “mbona leo umevaa vazi zuri na la ajabu sana” ina maana anayajua mavazi anayovaa kila siku? wapendwa hebu tuache uchuro huo? Huu ni wakati wa kujiangalia sana walimu na watu wengi wanakuja na kusimamisha mafundisho yao katika maono au hoja zao katika maono. Hizi ni nyakati mbaya

 34. Mr Paul Badia, sherehe ya bithday yako ni ya kikristo au ya kipagani? Kukumbuka siku uliyozaliwa ni upagani kweli? Furaha ya kukumbuka siku ambayo Mungu alikuleta duniani ni ya kikristo au ya kipagani? Basi hatuna sababu ya kufurahia kuzaliwa kwetu duniani ikiwa ni upagani. Mtu mmoja anapokuja duniani familia zinafurahi sana si zaidi sana kukumbuka ukombozi wa dunia ulipokuja duniani? Ni nini chanzo cha imani ya ukristo? si kuzaliwa kwa Yesu duniani? Tusipokumbuka kuzaliwa kwa Yesu imani yetu ni bure. Hatuhitaji andiko la biblia ili kumkumbuka Yesu na kuzaliwa kwake. Sijui kama utaamini hili nitakalosema juu ya ushuhuda wa mama mmoja wa ki-Korea anayeitwa Nam Choo. Yeye ameandika kitabu kinachoitwa “Kweli mbingu ipo.” (ninakushauri ukakisome ikiwa unaamini shuhuda maana hata yule ibilisi nyoka wa zamani Malaika Mikaeli alimshinda kwa Neno la ushuhuda). Tarehe 25/12 siku Nam Choo alipochukuliwa katika ulimwengu wa roho na Yesu Kristo hadi mbinguni, alishangaa sana siku hiyo alipomwona Yesu amevaa vazi la dhahabu na taji nzuri sana. Ikabidi amuulize “mbona leo umevaa vazi zuri na la ajabu sana?” Yesu akamjibu “leo ninasherehekea siku ya kuzaliwa kwangu duniani” Ikiwa Yesu mwenyewe anaikumbuka siku ya kuzaliwa kwake huko mbinguni si zaidi sana sisi tuliopokea ukombozi kwamba tunahitaji kusherehekea kuzaliwa kwa mkombozi wetu? Mkumbuke sana Yesu katika maisha yako ukianza na siku yake ya kuzaliwa, ikifuatiwa na siku ya pasaka yaani kufa na kufufuka kwake maana hivyo ndivyo vyanzo vya imani ya Kikristo. Mungu akubariki sana.

 35. Mimi ninavyojua kuhusu xmas ni kuwa:

  1. chanzo chake ni kutoka katika dini za kipagani ambazo zilisherekewa katika karne ya nne.
  2. Ikumbukwe kwamba Yesu Kristo hakuzaliwa tarehe 25/12/ bali haijulikani ni katika kipindi kipi, lakini historia inaonesha kwamba ni kama mwezi wa nne hivi.
  3. kuhusu kuadhimisha Xmas na kuwa sherehe ya kikiristo ni sahihi kabisa kwa sababu zifuatazo:
  1. Kanisa liliona badala ya kusherehekea dini za kipagani ulimwengu mzima ulielekezwa katika kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo badala ya kuabudu miungu.
  2. tarehe 25/12 ni karibu na mwisho wa mwaka, hivyo kanisa liliona ni bora watu wa Mungu wakakumbuka kuja kwa mwokozi wao hapa duniani.

  binafsi naafiki Kuwa Xmas ni sherehe ya Kikiristo! nitaendelea zaidi kuelezea baadae

 36. Bwana Yesu wapendwa

  mimi naona kuadhimisha na kutoadhimisha vyote ni sawa kwani tunasoma hivi ktk kolosai 2:16…..”Basi mtu asiwahukumu ninyi ktk vyakula au vinyaji,au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato” Hata hivyo anayeadhimisha anaazimisha kwa BWANA naye asiye adhimisha haadhimishi kwa BWANA. Najua kuwa kila tendo lisilo tokana na imani ni dhambi.hivyo wote wawili KRISTO alikufa kwa ajili yao!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 37. bwana asifiwe wapendwa!!
  i agree that christmass haipo in bible but whe have to celebrate!

 38. Bw asifiwe wandugu,

  Ni kwei christmass haipo kwa biblia lkn kuna ubaya gani kuiadhimisha kwa kukumbuka kuzaliwa kwa bwana na mwokozi wetu?hakuna ubaya,unless unaiadhimisha otherwise.

  But to me naona kuna umuhimu wa kuiadhimisha siku hii.
  Tunajifunza

 39. Amani iwe nanyi wapendwa wa Mungu!
  Christmas naweza kuifananisha na birthday ya baba yangu…je! itakuwa hainihusu?La hasha!Ninachoamini hapa Christmas ni ya wale wanaoamini kuwa Yesu Kristo ni Bwana na mwokozi wa maisha yao na kuiadhimisha si kwa mavazi mapya na sherehe lakini zaidi sana mioyo yetu kumshangilia mkombozi wetu.Watu wengi tunaojiita wakristo tumekuwa tukienda kinyume na sikuu hii kwa sababu wengi tunadhani tukinywa,kula na kuvaa vizuri siku hyo ndio kuiadhimisha.Yesu Kristo azaliwe katika mioyo yetu kwa upya nasi tuenende sawasawa na yeye anavyotaka hapo tutakuwa Wakristo kamili.Yesu Kristo ni njia,kweli na uzima,mchungaji mwema,mlango wa kondoo,ufufuo na uzima,nuru ya ulimwengu,chakula cha uzima,rafiki mwema,n.k hivyo ndugu zangu wote karibuni muuonje upendo wa huyu Yesu ambaye anasema hatamtupa nje kamwe yeye anayemjia.

 40. Kwa kuchangia kidogo tu…….Kuna siku moja maalumu Yesu alizaliwa Ulimwenguni……Yesu alifanyika Mwanadamu…………Yesu aliingia ulimwenguni…….Tunaweza kabisa kutojua ilikuwa siku gani…..Lakini ni Hakika iko siku hiyo……Ni hiyo ndio tunayoisherekea/Kuikumbuka…..na haina manaa kabisa kwetu kama walivyosema wengine pasipo kuwa na uhusiano binafsi na Yesu…..ambao tunaupata kwa kutubu dhambi…..na kukubali kifo chake kama sadaka ya dhambi….na kuukubali msamaha wake na kumpokea ili kupata maisha mapya (maisha ya milele) na kuishi maisha yetu hapa duniani kwa kumtii na kumpendeza (utakatifu) na hasa kuyatoa maisha yetu ayatumie kwa ajili ya kusudi lake……hapo ndipo Krismas inakua ni Sherehe yenye maana……

 41. Bwana Yesu Asifiwe sana, Mimi naomba kabla hajutaendelea tujiulize jambo hili kwanza. Je katika Maandiko Matakatifu Ya Mungu toka kile Kitabu Cha Mwanzo mpaka Kitabu Cha Ufunuo wa Yohana. Kuna miezi hii inayoitwa January,February,…..December? Maana tukimpata huyo December na wenzake ndipo jibu lilipo. Ndugu zangu tukilielewa hili ndipo tutakuja na jibu zuri juu ya majira haya ya kuzaliwa Kwa Bwana Wetu Yesu Kristu wa Nazaireti.

  Asante sana kwa kiu iliyopo kuelewa na maandiko. Bwana Yesu Awabariki sana.

 42. Sijamalizia kusoma maoni yote, lakini John Paul, amesema mengi ambayo vilevile ndio msimamo wangu.

  1. Mjadala kuhusu siku sahihi aliyozaliwa Yesu Kristo mwokozi wangu, hauwezi kupata suluhu, inawezekana mpaka anarudi kulichukua Kanisa mwafaka utakuwa bado haujafikiwa. Mimi, Sikukuu ya Krismasi kwa wakristo ni tendo la Kikristo kwa sababu nashangilia tendo la kuzaliwa Mwokozi wangu, hata kama nisherehekee kila siku, ni sawa. Kama alivyosema John, tunachosherehekea ni tendo la kuzaliwa Yesu Kristo sio siku aliyozaliwa, Kwa sababu hatujui “exactly” ni siku gani alizaliwa, na hata kama tungekuwa tunajua ni siku gani alizaliwa, bado ingekuwa sio sahihi kushangilia siku, bado tungesherehekea tendo na sherehe ingeweza kufanyika hata siku tofauti na ile aliyozaliwa. I will never mind about the day He was born, my business is to celebrate Him everyday, all the way.

  2. Kuna watu wamejenga hoja kwamba asili ya Krismasi ni paganism, ninachojua mimi ni kwamba kuna maadhimisho yaliyofanywa/yanayofanywa na wapagani kwa ajili ya kusherehekea kuzaliwa kwa miungu au watu fulani labda kutokana na umaarufu wao, na hizo sherehe zikawa na “asili, mazingira/mandhari, matukio, matendo” yanayofanana na kusherehekea kuzaliwa Kristo. Hizo ni sherehe kama zingine zote kwa mfano “birthday” ya mtu yeyote yule.

  Kwa hiyo kuwepo kwa ufanano kati ya sikukuu za kipagani na Krismasi haina maana Krismasi ni sherehe ya kipagani. Mpagani ambaye “simply” ni mfuasi wa shetani ataadhimishaje tendo linalomhusu Kristo Mesiah? Mambo yote yanayomhusu Kristo yanafanywa kwa ajili yake tu. Mpagani anaweza kuonekana anashangilia kuzaliwa Kristo kwa sababu amekuwa “influenced”, na akajikuta anashangilia tu kama desturi au utamaduni au mazoea au kujiburudisha au anafanya hivyo ili kutumia kivuli cha Kristo kufanya mambo yake mengine. Ni sawa na wafanyavyo manabii wa uongo, yaani huwa wanaonekana kama vile wanamhubiri Kristo lakini hiyo sio nia yao, nia ni kufanikisha malengo yao kwa kumtaja Yesu.

  KUFANANA KWA MAMBO FULANIFULANI KATIKA SHEREHE ZA KIPAGANI NA KRISMASI NI JAMBO LA KWAIDA! “Logic ni simple”:

  KWA SABABU ZOTE NI SHEREHE, KWA HIYO KUNA VITU AMBAVYO NI “common”. Kwa hiyo kufanana Krismasi na sherehe za kipagani isichukuliwe kwamba upagani ni asili yake.

  Angalizo: Haiwezekani Krismasi ya Kikristo (ukristo aliouongelea John, siongelei dhehebu au kuhudhuria kanisani au kusalisha au kuwa mchungaji au nabii au mzee wa kanisa au kubatizwa au kutoa sadaka sana na mengine yafananayo na hayo) ikafanana na sherehe ya kipagani, ila sherehe ya kipagani inaweza kuwa na mambo ambayo pia yanaweza kuonekana kwa wakristo kama Kuimba, kula, kushangilia, kupamba. Hapa naongelea “contexts” sio “contents”. “Contexts” zaweza kufanana lakini sio “contents”. Halafu pia nia za sherehe za kipagani na Kikristo huwa ni tofauti kabisa.

  Krismasi asili yake ni wakristo ambao wameamua kuadhimisha tendo la kuzaliwa Yesu Kristo, “don’t mind the day”, sherehekea kila siku ukitaka kama unaweza, kwa namna ambayo inampendeza Mungu.

  4. Zaidi tuongozwe na Roho mtakatifu kufanya yale yanayompendeza Mungu, historia, na elimu nyingi na uwezo wa kuchambua bila kumshirikisha Roho mtakatifu ni kazi bure.

  Kwa mfano, sote tunatumia hela ukiambiwa hizi hela asili yake ni upagani, na wanaozitengeneza ni wapagani, au ili uogopeshwe zaidi ukaambiwa ni “Antichrist” ndio wanaotengeneza, utaacha kuzitumia? Au utafanyaje?

  Mungu awe nasi.

 43. tatizo si ukristo maana hata shetani hujiita kristo, ndo maana watu na makanisa yanayojiita ya kikristo ndani yao hakuna ukristo just watoe fungu kubwa sawa na tanzania na dhana ya ushoga NA MISAADA YA CAMEROON. Huyo kiongozi kaja kufanya nini kama si MNATAKA FUNGU TOKA KWAKE? mi naona 90% ya makanisa yanajiita ya kikristo hayana ukweli ndani yake. ukristo si kusema BWANA YESU ASIFIWE bali ni juhudi zako kujifunza BIBLIA kwa bidii.

 44. Wapendwa watu wa Mungu,

  Kimsingi, naungana na Ndg John Paul kusema kwamba Krismasi ni sherehe ya Kikristo. Shida iliyopo kwa watu wengi wanaiangalia tarehe ya sherehe hiyo badala ya maana na umuhimu wa sherehe hiyo.

  Yesu ambaye tunasherehekea siku ya kuzaliwa kwake hiyo tarehe 25 Desemba, alikuwepo kabla hata kuumbwa kwa dunia hii kwa kuwa Yeye ni Mungu, ndivyo Mithali 8:23-31 na Injili ya Yohana 1:1-4,10-14 zinatueleza. Kitendo cha huyo Neno kufanyika mwili na kuzaliwa na Bikira Maria na kukaa pamoja na wanadamu na wanadamu kuuona utukufu wake baada ya kukombolewa dhambi zao kwa kifo cha aibu pale msalabani cha huyo Neno, context nzima hiyo ndiyo inayofanya sherehe ya kuzaliwa kwa Yesu kuwa ni sikukuu ya Kikristo. Kama mtu anajua ukristo ni nini, basi hawezi kuutenganisha na sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa huyo ambaye ndiye muhimili wa huo ukristo. Thamani na umuhimu wa kitu huja pale yule anayekithamini kitu hicho anakijua vizuri na kukipenda. Kama hukijui wala hukipendi kitu, huwezi kamwe kuona thamani yake kwako!

  Sherehe ya Krismasi haiwezi kuonekana kama sherehe ya Kikristo pale wale wanaosherehekea hawamjui Kristo ni nani kwao na ana umuhimu gani kwenye maisha yao. Ndio sababu sherehe ya Krismasi kwa watu wengi imekuwa ni wakati wao kunywa vinywaji vya kulevya na kufanya mambo mengine mengi ambayo ni kinyume kabisa na maana hasa ya ukristo. Na hili limefanywa au linafanywa na hao wanaojiita wakristo ambao kwa kweli tulitarajia wao wawe mfano na nuru kwa wasio wakristo kuhusu sherehe hii.

  Kwa mkristo wa kweli ambaye Yesu Kristo amefanyika Bwana na Mwokozi wa maisha yake, sikukuu ya Krismasi ni wakati muhimu sana wa kukaa na kumtafakari jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu huu kiasi cha kumtoa Mwana wake wa Pekee (Yohana 3:16) auvae huu utu wa nyama na damu ili aweze kuwakomboa wale walio katika mwili wa nyama na damu kutoka katika nguvu ya mauti (Waebrania 2:14). Kwa hiyo ni sherehe muhimu sana kwa ustawi wetu kiroho na kimwili pia.

  Baraka kwenu nyote na Heri ya Krismasi.

 45. Dada Aiyalon,

  Ninaandika haya kufuatia maoni yako ya tarehe 9, December:

  Kumwalika mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa album ya mkristo si tatizo. Tatizo ni mgeni GANI anayealikwa. Mimi niliandika nikasema kuwa kumwalika mtu ASIYE MKRISTO katika tukio la Kikristo kisha kumpa uhuru wa kusema ANAVYOJISIKIA si jambo zuri kwa UKRISTO.

  Angalia mfano ulioutoa wewe: Mlimwalika mheshimwa waziri huyo, kisha mkamruhusu aseme aliyo nayo naye akawaambia DINI ZOTE NI SAWA na watu wakapiga makofi? Hivi huoni kuwa MLISHIRIKI katika kuupoteza Ukristo?

  Kama dini zote ni sawa, yaani hata zile zinazompinga Kristo nazo ni SAWA na Ukristo? Tukifika hapo ukristo utaonekana WAPI [kwa maana umechanganyikana na dini zisizo ukristo]?

  Ndiyo maana niliandika kuwa KAMA HATUKAI VIZURI na huu Ukristo, inawezekana kabisa ikafika huko mbele tusijue Mkristo ni Yupi na Asiye Mkristo ni yupi kwa SABABU WAKRISTO WATACHANGANYIKANA na WASIO WAKRISTO?

  Ni tatizo sana kumualika mtu asiye Mkristo kisha KUMKABIDHI MADHABAHU ASEME ALIYONAYO!

  -Agizo la Bwana Yesu kuhusu kueneza Injili ni KUWAHUBIRIA watu, kwa kuwafuata huko waliko, na wala siyo hii staili ya sasa ya kuwakaribisha ndani kisha wao ndio wakawa WASEMAJI WAKUU kwenye matukio ya Kikristo. Si unaona kama hapo kwenu, badala ya yeye KUMHUBIRIA, ninyi ndiyo aliwahubiria na mahubiri yake umesema “Kila mmoja alisisimka”. Hivi hata wewe Ulisisimka kusikia kuwa DINI ZOTE NI SAWA?

  -Kuwaheshimu viongozi wa nchi ni jambo la Kibiblia. Lakini mpaka wa heshima hiyo unakoma pale kiongozi huyo ATAHATARISHA mwelekeo wa imani. Wakati Biblia inaelekeza kutii mamlaka ya uongozi wa Nchi VILE VILE imeelekeza juu ya KUMTII MUNGU KULIKO WANADAMU itakapotokea kiongozi wa nchi anaharibu mwelekeo wa imani. Kuna watu kwenye Biblia ambao HATA KABLA YA KUWEPO KWA BIBLIA walichagua KUMTII MUNGU kuliko WANADAMU pale kiongozi wao wa serikali aliwaambia WAABUDU SANAMU! Nasi tunaweza kuwaheshimu na kuwatii Vingozi wa nchi lakini SI HADI KATIKA Kutuelekeza kumuasi Mungu!

  Nimeoana niandike hayo machache lakini mada iliyopo ni Kama Krismasi ni Sherehe ya Kikristo Au Siyo ya Kikristo. Nami nimeshatoa maoni yangu pamoja na majibu/ufafanuzi kwa yale uliyoniuliza.

  Asante na tuendelee kujifunza!

 46. Bwana Yesu asifiwe sana , mi napenda kusema mkristo sio kuwa ktk dhehebu flani au kuwa na jina john, matayo. esta na n.k, wapo wengi wanamajina kama hayo yasemwayo ni ya kikirsto lkn, ni wapagani haswa, waenda wa waganga wa kienyeji ndo wenyewe, walevi ndo wenywe na makahaba ndo wao lakini maana halisi ya kiroho mkristo ni yule aliemua kuacha dunia na tamaa zake na kumkubali Yesu kristo aishi ndani yake kama bwana na mwokozi, tofauti na hapo ni kristi fake.

  hata mie siku ya christmas huwa nakumbuka tukio la kuzaliwa bwana Yesu kristo kama mwokozi wangu, na ni siku ya kupeleka hoja zangu zenye nguvu mbele zake ili Yesu kweli azaliwe kwenye lile nampelekea.
  ubarikiwe

 47. Kuna maelezo kutoka Wikipedia, yanayohusu historia ya Krismasi kwa ufupi na suluhisho na nimeona niyaweke hapa maana yaona yanasaidia kuelezea msimamo nilionao kuhusu Krismasi:

  DATE OF CELEBRATION

  On Christmas Day, the Christ Candle in the center of the Advent wreath is traditionally lit in many church services.

  For centuries, Christian writers accepted that Christmas was the actual date on which Jesus was born. John Chrysostom preached a sermon in Antioch c. 386 which established the date of Christmas as December 25 on the Julian calendar since the conception of Jesus (Luke 1:26) had been announced during the sixth month of Elisabeth’s pregnancy with John the Baptist (Luke 1:10-13) as dated from the duties Zacharias performed on the Day of Atonement during the seventh month of the Hebrew calendar Ethanim or Tishri (Lev. 16:29, 1 Kings 8:2) which falls in September–October.

  In the early 18th century, scholars began proposing alternative explanations. Isaac Newton argued that the date of Christmas was selected to correspond with the winter solstice,which the Romans called bruma and celebrated on December 25. In 1743, German Protestant Paul Ernst Jablonski argued Christmas was placed on December 25 to correspond with the Roman solar holiday Dies Natalis Solis Invicti and was therefore a “paganization” that debased the true church.In 1889, Louis Duchesne proposed that the date of Christmas was calculated as nine months after the Annunciation, the traditional date of the conception of Jesus, which itself was based on a traditional belief that he was conceived and crucified on the same date, 15 Nisan.

  In the early 4th century, the church calendar contained Christmas on December 25 and other holidays placed on solar dates: “It is cosmic symbolism…which inspired the Church leadership in Rome to elect the winter solstice, December 25, as the birthday of Christ, and the summer solstice as that of John the Baptist, supplemented by the equinoxes as their respective dates of conception. While they were aware that pagans called this day the ‘birthday’ of Sol Invictus, this did not concern them and it did not play any role in their choice of date for Christmas,” according to modern scholar S.E. Hijmans.

  However, today, whether or not the birth date of Jesus is on December 25 is not considered to be an important issue among mainstream Christian denominations; rather, celebrating the coming of God into the world in the form of man to atone for the sins of humanity is considered to be the primary meaning of Christmas”

  …unaweza kurudia tena kusoma paragraph ya mwisho ili kuelewa ninachomaanisha katika maoni yangu:

  Kwa hiyo Wakristo tukiichukulia Krismasi kama siku ya kukumbuka Kuja kwa Yesu Ulimwenguni, na kuyatupilia mbali mambo mengine ya kipagani yaliyokuwepo na yanayoingizwa katika sherehe hizo naamini kabisa tunaweza kuifanya Krismasi kuwa ni sherehe ya Kikristo!

 48. Dada Aiyalon,

  Nashukuru kwa maoni yako juu ya yale niliyoandika mimi. Nakubali kuwa “UNADHANI” kuwa nimekosea kuandika orodha ya ambao “huwa” hawasherehekei Krismas. Nami nakubali kuwa “inawezekana” nimekosea orodha ya wale ambao huwa hawasherekei Siku kuu ya Krismasi. LAKINI NATUMAINI SIKU TUKIICHAMBUA ORODHA HIYO KIBIBLIA TUTAPATA UHAKIKA! Lakini kwa kuwa mada hapa ni kama Krismas ni jambo la Kikristo au Si la Kikristo, basi sitajikita sana katika orodha hiyo na wala sishauri tuendelee kuichambua bali tujali zaidi ni kwa vipi ni ya Kikristo au Si ya Kikristo. Nadhani hilo ndilo muhimu!

  Dada Aiyalon, kuna maneno makali umeandika, ambayo nayanukuu:

  “shida yako ninayoiona hapa ni kuona kwamba dhehebu lako ni sahihi zaidi ya mengine.kumbuka sio wote wamwitao bwana bwana watauona ufalme wa mbinguni,Biblia inasema tutashangaa kuwaona wale tusiowategemea huko paradiso,unamkumbuka yule nyang’anyi pale msalabani aliyesulubiwa pamoja Yesu? je unakumbuka aliahidiwa nini?”

  …dada yangu mpendwa, nikuambie tu kuwa wewe ni mgeni katika blog hii [na ninakukaribisha] kwa hiyo maneno hayo niliyoyanukuu hapo juu umepata nguvu ya kuyaandika kwa kuwa hujafahamu vizuri MISIMAMO ya wachangiaji, nikiwemo mimi. Lakini natumaini kadri tunavyoendelea pengine utakuja kuona kuwa maneno hayo hayanipasi mimi. Kwa sababu hiyo nakusamehe tu ili tuendelee na mada!

  Nanukuu tena:

  “unaposema jambo lolote ambalo linamtangaza Yesu ni sahihi kufanywa nje ya maandiko nadhani si kweli,na ndio maana wakristo wengi hasa wa Afrika wamejikuta wakipoteza uthabiti wa imani zao kwa mambo ya kuiga”

  Dada, nilichoandika mimi ni maneno yafuatayo:

  “kitendo chochote kinachomhusu Yesu Kristo, kikifanyika na waKristo, tayari kinatosha kuwa ni tukio la Kikristo”

  Ulivyofafanua wewe ni TOFAUTI na nilivyoandika mimi. Ninalojua ni kuwa HAKUNA JAMBO LINALOMHUSU KRISTO AMBALO HALIKO KWENYE MAANDIKO. Suala la kuzaliwa kwa Kristo liko kwenye Biblia. Hivyo sioni ni kwa nini kukumbuka TUKIO [si kukumbuka SIKU] la KUZALIWA KWA KRISTO lisiwe tukio la Kikristo!

  Ona ulivyoandika wewe: “mfano ndio maana siku hizi tunaona vikundi vinavyojiita vya injili hapa chini kwangu Tanzania vijana wa kiume wanaimba huku wamesuka,na wamevaa milegezo eti wanamsifu Mungu,Mungu wetu ni ustaarabu sana”

  Hivi KUSUKA ni TENDO linalomhusu Kristo?…., Kuvaa MILEGEZO ni Tendo linalomhusu Kristo?

  Tafsiri yangu ya WAKRISTO ninayotumia ni “Watu wanaoishi kama Kristo” au “Wafuasi wa Kristo”. Mfuasi wa Kristo hawezi fanya tukio linalopingana na Kristo. Hebu tutumie “WAKRISTO” kwa Tafsiri ya Biblia na SI kwa Tafsiri tunazofundishwa katika MADHEHEBU, ambako naona umekimbilia huko mapema sana!

  Ninakushauri tu unaposoma usome ukiwa umetulia, utafakari kwa makini. Bila kufanya hivyo unaweza kuandika mambo ambayo hukuyaelewa vizuri.

  Kuiga si tatizo, Tatizo ni kile Kinachoigwa. Hakuna Tatizo kuiga mambo ya Kikristo toka kwa mtu mwingine, kama hayo yametoka kwenye maandiko. Tatizo ni kuiga mambo YASIYO YA KIKRISTO, mambo YASIYOMHUSU KRISTO, mambo yasiyokuwepo kwenye maandiko! Ndiyo maana mtume Paul alisema “nifuateni mimi kama ninavyomfuata Kristo” na kuna mahali pengine Biblia inasema maneno kama “igeni mwenendo wa watu waliowatangulia”.

  Kuhusu Historia ya Krismasi WAWEZA SOMA MAONI YALIYOWEKWA NA NDUGU MAZOGOLA SAMWELI hapo juu! Lakini Krismasi ninavyofahamu mimi siyo kukumbuka SIKU aliyozaliwa Yesu ni siku ya kukumbuka TUKIO la kuzaliwa Yesu. Tarehe si muhimu bali Tukio/Tendo. Hatupaswi kukumbuka SIKU bali tunapaswa kukumbuka TUKIO na UMUHIMU wake. SIKU haina LOLOTE maana siku zote ZINAFANANA tu. Muhimu ni TUKIO lililotokea katika SIKU fulani. Kwa hiyo kama kinachotafutwa ni TUKIO basi laweza kukumbukwa katika SIKU YOYOTE!

  Mfano: Hivi unafikiri Siku ya Ukimwi duniani ni siku ya kuadhimisha SIKU au TUKIO?
  Siku ya Kifua Kikuu, ni siku ya kuadhimisha Siku au Tukio? Siku ya Malaria, Siku ya Unywaji wa Maziwa nk. Kwa hiyo hapo muhimu siyo SIKU bali ni TUKIO linaloadhimishwa na ndiyo maana nikasema linaweza kufanyika katika SIKU yoyote!

  Hayo ndiyo maoni yangu kwa sasa.

 49. huenda ingekuwa vyema kama utanieleza historia hasa ya kuadhimishwa xmass ilianza vipi na mwansilishi wake ni nani? maana naperusi kwenye Biblia sioni majira Yesu aliyozaliwa kwa hesabu,wana historia hupenda kusema neno kabla ya Yesu Kuzaliwa lakini na wao hawana usahihi kwa jambo hili.ila wenzetu muslim wao wanaijua taerehe maana huadhimisha siku hiyo ya mtume wao kwa kufuata maandiko sasa ili nielewe naomba unipe historia ya xmass.

 50. Hivi kumwalika mgeni rasmi kuwepo kwenye sherehe ya uzinduzi wa album ya mkristo kuna shida gani? Sasa ni kwa vipi tutaeneza injili kwa watu wasiomjua? inawezekana siku uliyoamwita huyo mgeni rasmi ambaye ni mmtaifa au si mkristo mahubiri yanaweza kumvutia na akaokolewa! sasa tukialikana sisi ambao tayari tunamjua Yesu kweli injili itaenea? nadhani hata Biblia inazungumzia umuhimu wa kumheshimu kiongozi wako wa nchi.hapa visiwani Zanzibar askofu Dickson Kaganga alipokuwa anapata uaskofu mgeni rasmi alikuwa ni waziri wa nchi ofisi ya rais. na kwakweli alizungumza maneno mazuri sana ambayo kila mmoja alisisimka,alisema neno moja ambalo silisahau akasema “sikujua kwamba kumbe wakristo wanapokuwa kwenye ibada zao kuna kuwa na ustaarabu wa aina hii kila mtu namuona yuko makini kwa kufuatilia kile muhubiri anachosema mimi nilijua wanaimba imba tu basi na sasa nimetambua kwamba dini zote ni sawa kwa kuwa zinamkiri Mungu ambaye sote ni tegemeo letu”.

  Mheshimiwa huyo alitoa ahadi ya kufuatilia nyendo za wale ambao wanachoma makanisa moto na akasema atahakikisha watu hao wanachukuliwa hatua za kinidhamu maana hapa kwetu uliingia mtindo wa kuchoma moto makanisa,kuvunja na kuiba hususani kwenye makanisa ya kilokole,makanisa ambayo hayajawahi kufanyiwa unyama huo ni Aglikan,Roman na Sabato. Yaliyosalia kwa kweli hali ilikuwa inasikitisha lakini tunashukuru Mungu amesikia kilio hicho tunasali kwa amani. Ama khusu kanda za nyimbo injili kuchanganywa na nyimbo za kidunia sijawahi kuona na kama lipo naunga mkono kwa kweli sio sahihi kabisaaaaaaaaa! haifai maana NURU NA KIZA HAVITANGAMANI! lakini hapo hapo Rose muhando ana award ya bia ya Kilimanjaro ambapo alipata ni tuzo zinazoandaliwa kila mwaka ambazo zinahusisha waimbaji wa nyimbo za kidunia na magazeti yalimshangaa unawezaje kwenda kuchukua tuzo ya BIA? MVINYO?

  Aiyaloni.

 51. nadhani umekosea katika orodha yako ya watu ambao hawapaswi kusherehekea XMASS pale uposema na wabato hawastahili maana dini yao haijaja kwa ukombozi wa Yesu Kristo mimi sio msabato lakini wasabato wanamkiri Yesu ni Bwana na mwokozi wao.shida yako ninayoina hapa ni kuona kwamba dhehebu lako ni sahihi zaidi ya mengine.kumbuka sio wote wamwitao bwana bwana watauona ufalme wa mbinguni,Biblia inasema tutashangaa kuwaona wale tusiowategemea huko paradiso,unamkumbuka yule nyang’anyi pale msalabani aliyesulubiwa pamoja Yesu? je unakumbuka aliahidiwa nini? na unaposema jambo lolote ambalo linamtangaza Yesu ni sahihi kufanywa nje ya maandiko nadhani si kweli,na ndio maana wakristo wengi hasa wa Afrika wamejikuta wakipoteza uthabiti wa imani zao kwa mambo ya kuiga.mfano ndio maana siku hizi tunaona vikundi vinavyojiita vya injili hapa chini kwangu Tanzania vijana wa kiume wanaimba huku wamesuka,na wamevaa milegezo eti wanamsifu Mungu,Mungu wetu ni ustaarabu sana.sasa sikubaliani na wewe kuhusu wasabato eti dhehebu lao halijazaliwa kwa mfumo wa masihi Yesu.japo najua uko sahihi kutoa mawazo yako.

  Aiyalon

 52. Here are 4 major reasons for not celebrating Christmas:

  1. Jesus wasn’t born on or near December 25

  Most experts agree that December 25 has nothing to do with His birth. The first reason why Christ could not have been born in December is found in a fact mentioned by Luke relating to those shepherds who were “living out in the fields, keeping watch over their flock by night” (Luke 2:8). There is no way any shepherd would be found keeping his flocks outside at night in the kind of weather (very cold and rainy) that is know to exist in and around Bethlehem in December. Such weather argues strongly against the birth of our Lord on December 25, as the weather would have prevented the shepherds to be out in the fields attending their flocks.

  Furthermore, there is no logic at all for the administratively skilled Romans to undertake census during the coldest season of the year. Luke informs us that our Lord was born in Bethlehem because his parents needed to register for the Roman census. It makes much more sense to conduct such senses when it is most convenient for the people to travel around, and not be hampered by severe weather conditions. Thus, precludes any birth of Christ on the Month of December.

  2. Christmas is not mentioned in the whole New Testament

  No where in the whole New Testament do we have a single recorded instance of Christians celebrating the birth of Christ on December 25, or on any other date. Yet the New Testament does mention several details about His birth. More importantly, there is no command by our Lord or our heavenly Father to celebrate His birth. While it is true that celebrating the birth of Christ is not condemned in the Bible, but the absence of any recorded instance of such celebration in the New Testament should not be overlooked or ignored. In addition, it is a proven fact that the early Christian church did not celebrate the birth of Christ on Dec 25 or on any other date.

  “Christmas was not among the earliest festivals of the church … the first evidence of the feast is from Egypt.” (Catholic Encyclopaedia 1911 edition)

  3. Christmas is a PAGAN festival and has nothing to do with Christianity

  The 25th December was anciently celebrated as the birthday of the invincible SUN god, (variously know as Tammuz, Mithra, Saturn, Adonis or BAAL) long before our Lord was born in Bethlehem. It is interesting to note how December 25 became the birth date of Christ. Historians Gerard and Patricia Del Re state the following:

  “The tradition of celebrating December 25 as Christ’s birthday came to the Romans from Persia. Mithra, the Persian god of light and sacred contracts, was born out of a rock on December 25. Rome was famous for its flirtations with strange gods and cults, and in the third century the unchristian emperor Aurelian established the festival of Dies Invicti Solis, the Day of the Invincible Sun, on December 25.

  “Mithra was an embodiment of the sun, so this period of its rebirth was a major day in Mithraism, which had become Rome’s latest official religion . . . It is believed that the emperor Constantine adhered to Mithraism up to the time of his conversion to Christianity. He was probably instrumental in seeing that the major feast of his old religion was carried over to his new faith” (The Christmas Almanac, 1979, p. 17).

  The pagan origin of Christmas can be further seen with the many customs associated with it–Christmas lights and candles, Santa Claus, Santa’s Elves, The Christmas tree, Holly and Ivy and Mistletoe and the Yule log. These traditions have nothing to do with the birth of our Lord, but have their origin in ancient pagan festivals..

  We cannot avoid concluding that Christmas is rooted in ancient religious customs and established by the Roman Catholic Church to ease the pagan converts’ transition to Christianity. Today Christmas is driven by commercialism, and the original celebration of Christ’s birthday is today more regrettably replaced by the tradition of Santa Claus.

  4. Christmas is a Roman Catholic institution: sufficient reason to reject it

  As with Sunday worship origin, Christmas is the child of the Roman Catholic Church.

  “The festivals of Rome are innumerable; but five of the most important may be singled out for elucidation -viz., Christmas-day, Lady-day, Easter, the nativity of St. John, and the Feast of the Assumption. Each and all of these can be proved to be Babylonian.” (The Two Babylons, by Alexander Hyslop, page 91)

  “… within the Christian Church no such festival as Christmas was ever heard of till the third century, and that not till the fourth century was far advanced did it gain much observance. How, then, did the Roman Church fix on December 25th as Christmas-day? Why, thus: Long before the fourth century, and long before the Christian era itself, a festival was celebrated among the heathen, at that precise time of the year, in honour of the birth of the son of the Babylonian queen of heaven; and it may fairly be presumed that in order to conciliate the heathen, and to swell the number of the nominal adherents of Christianity, the same festival was adopted by the Roman Church, giving it only the name of Christ. This tendency on the part of the Christians to meet Paganism half-way was very early developed … Upright men strove to stem the tide, but in spite of all their efforts, the apostasy went on, till the Church, with the exception of a small remnant, was submerged under Pagan superstition. That Christmas was originally a Pagan festival, is beyond all doubt. The time of the year, the ceremonies with which it is still celebrated, prove its origin. In Egypt, the son of Isis, the Egyptian title for the queen of heaven, was born at this very time, ‘about the time of the winter solstice.'” (Ibid. page 93)

  Participation, therefore, in Christmas would be another way of paying homage to the Beast of Revelation, something that will be most displeasing to our heavenly Father. His people should never be found endorsing any institution which is pushed and promoted by the anti-Christ

  Amen

 53. Question: “Should Christians celebrate Christmas?”

  Answer: The debate about whether or not Christians should celebrate Christmas has been raging for centuries. There are equally sincere and committed Christians on both sides of the issue, each with multiple reasons why or why not Christmas should be celebrated in Christian homes. But what does the Bible say? Does the Bible give clear direction as to whether Christmas is a holiday to be celebrated by Christians?

  First, let’s look at the reasons why some Christians do not celebrate Christmas. One argument against Christmas is that the traditions surrounding the holiday have origins in paganism. Searching for reliable information on this topic is difficult because the origins of many of our traditions are so obscure that sources often contradict one another. Bells, candles, holly, and yuletide decorations are mentioned in the history of pagan worship, but the use of such in one’s home certainly does not indicate a return to paganism. While there are definitely pagan roots to some traditions, there are many more traditions associated with the true meaning of Christmas—the birth of the Savior of the world in Bethlehem. Bells are played to ring out the joyous news, candles are lit to remind us that Christ is the Light of the world (John 1:4-9), a star is placed on the top of a Christmas tree to remember the Star of Bethlehem, and gifts are exchanged to remind us of the gifts of the Magi to Jesus, the greatest gift of God to mankind.

  Another argument against Christmas, especially having a Christmas tree, is that the Bible forbids bringing trees into our homes and decorating them. The passage often cited is Jeremiah 10:1-16, but this passage refers to cutting down trees, chiseling the wood to make an idol, and then decorating the idol with silver and gold for the purpose of bowing down before it to worship it (see also Isaiah 44:9-18). The passage in Jeremiah cannot be taken out of its context and used to make a legitimate argument against Christmas trees.

  Christians who choose to ignore Christmas point to the fact that the Bible doesn’t give us the date of Christ’s birth, which is certainly true. December 25 may not be even close to the time Jesus was born, and arguments on both sides are legion, some relating to climate in Israel, the practices of shepherds in winter, and the dates of Roman census-taking. None of these points are without a certain amount of conjecture, which brings us back to the fact that the Bible doesn’t tell us when Jesus was born. Some see this as proof positive that God didn’t want us to celebrate the birth, while others see the Bible’s silence on the issue as tacit approval.

  Some Christians say that since the world celebrates Christmas—although it is becoming more and more politically correct to refer to it as “the holidays”—Christians should avoid it. But that is the same argument made by false religions that deny Christ altogether, as well as cults such as the Jehovah’s Witnesses who deny His deity. Those Christians who do celebrate Christmas often see the occasion as an opportunity to proclaim Christ as “the reason for the season” among the nations and to those trapped in false religions.

  As we have seen, there is no legitimate scriptural reason not to celebrate Christmas. At the same time, there is no biblical mandate to celebrate it, either. In the end, of course, whether or not to celebrate Christmas is a personal decision. Whatever Christians decide to do regarding Christmas, their views should not be used as a club with which to beat down or denigrate those with opposing views, nor should either view be used as a badge of honor inducing pride over celebrating or not celebrating. As in all things, we seek wisdom from Him who gives it liberally to all who ask (James 1:5) and accept one another in Christian love and grace, regardless of our views on Christmas.

  Recommended Resource: The Case for Christmas by Lee Strobel.

 54. Maoni yangu mimi ni haya:

  Krismasi ni sherehe ya KIKRISTO kwa sababu ni tukio la kukumbuka kuzaliwa kwa Kristo, Yesu, mwokozi wa Ulimwengu! Kwa hiyo hata kama si agizo katika Biblia, lakini kitendo chochote kinachomhusu Yesu Kristo, kikifanyika na waKikristo, tayari kinatosha kuwa ni tukio la Kikristo.

  Kwa hali ya kawaida Siku hii haiwezi kuadhimishwa na waislam, wabudha, wahindu, wasabato, na wengine ambao msimamo wa imani zao haupo katika UKOMBOZI ulioletwa na Mungu kupitia Yesu Kristo.

  Tatizo lililopo SASA ni kuwa ile ncha, [the cutting edge] ya wakristo imekuwa butu. Kama ni kisu kilichokuwa kinakata kwa ukali sasa ni butu. Kama ni panga au shoka lililokuwa linatumika kukata sasa ni butu. Ncha inahitaji kunolewa. Maana yangu ya kuandika haya ni hivi:

  Ukristo umeshaigiliana na dunia. Yawezekana ni Wakristo wameingia duniani au Dunia ndiyo imeingia katika Ukristo. Mambo ambayo yalikuwa na nguvu ya kutenganisha giza na nuru sasa hayatenganishi tena! Mambo yaliyokuwa yanatenganisha mkristo na asiye mkristo sasa hivi ni vigumu kuyaona tena. Ukristo wa sasa hauna makali wa kukata na kujitenga kutoka katika hali isiyo ya kikristo.

  Nakumbuka sherehe za Krismasi za miaka ya 80, mahali nilikokuwa miaka hiyo nikiwa kijana mdogo, zilikuwa ni sherehe tofauti sana na sasa. Wakati ule wakristo tulikuwa tunakutana kumshangilia Mungu, kuomba, kusifu kuabudu na Mungu alikuwa anajitokeza kwa namna ya ajabu mno, mno, kiasi ambacho sidhani kama hali hiyo inaweza kurudi tena!

  Kilichopo sasa ni kitu cha ajabu maana Wakristo wanakimbilia kufanya mambo wanayoyafanya wasio wakristo HALAFU wasio wakristo nao wanakimbilia kufanya mambo wanayoyafanya wakristo. Katika nchi zenye uhuru wa kuabudu Wakristo hawazongwi zongwi sana tena na maneno ya kejeli, kutukanwa kwa kuwa wanaonekana SI WATU WA TOFAUTI. Halafu na wakristo hawana tena muda wa kuwahubiria wasio wakristo ili wawe wakristo kwa sababu WANATAKA KUFANANA NAO.

  Wakrito wanataka kufanana na wasio wakristo katika namna ya kuishi: mavazi, vipaumbele katika maisha, maongezi yao, starehe, namna wanavyokabiliana na matatizo kama vile kukimbilia mahakamani, nk. Mambo hayo yamefanya ule mstari unaotenganisha mambo ya kikristo na yasiyo ya kikristo UFUTIKE. Mstari ulipofutika MAMBO YAMEINGILIANA.

  Mambo yalipoingiliana SASA NI VIGUMU KUBAGUA JAMBO LIPI NI LA KIKRISTO NA LIPI SI LA KIKRISTO KWA KUWA WAKRISTO NA WASIO WAKRISTO WANAFANYA MAMBO KWA PAMOJA!

  Angalia katika nyimbo; Sasa ni matamasha mengi tu ya Nyimbo ambayo waimbaji wanaoimba Nyimbo za Kikristo wanafanya kwa Pamoja na wale wanaoimba Zisizo za Kikristo! Unafikiri ni kwa kiasi gani tunaweza kuwa na uhakika wa kusema matamasha hayo ni ya Kikristo au siyo ya Kikristo?

  Fikiria tukio la kuzindua kanda za nyimbo za Kikristo halafu mgeni rasmi anaalikwa ASIYE MKRISTO na kuachiwa mamlaka ya KUSEMA ATAKAVYOJISIKIA. Je, ni kwa kiasi gani tunaweza kusema kuwa tukio la kuzindua kanda hizo ni la Kikristo au siyo la Kikristo?

  Fikiria suala la Nyimbo; Sasa nyimbo zisizo za Kikristo zinawekwa katika kanda moja, flash discs, DVD, CDs nk, pamoja na zisizo za Kikristo na watu huzisikiliza hivyo hivyo kwa kuchanganya. Je, ni kwa kiasi gani tunaweza kusema kanda zile ni za Kikristo au siyo za Kikristo?

  Wakati sasa tunashindwa kuelewa kama Krismasi ni tukio la Kikristo au lisilo la Kikristo kuna nyakati zitafika ambapo TUTASHINDWA KUTAMBUANA YUPI NI MKRISTO na YUPI SIYE! kwa sababu maisha WATAKAYOKUWA WANAISHI WAKRISTO SI YA KIBIBLIA!

  Ndiyo maana Bwana Yesu akauliza “..walakini, atakapokuja mwana wa Adamu, Je! Ataiona Imani duniani?” Luka 18:8

 55. MIMI SIAMINI KUWA XMASS NI SHUGHULI YA KIKRISTO AU SHEREHE.LAKINI NAOMBA NIJIBIWE KWA NINI WAKRISTO WANAIADHIMISHA SIKU HII,UKIACHILIA MBALI WASABATO AMBAO HAWAITAMBUI SIKU HII?

  WANA WA MUNGU NIJIBUNI

  AIYALON.
  ASANTE.

 56. sherehe hii sio ya kikrisro na ni kweli kua haina ushahidi wowote wa kibiblia.Ni sawa na sherehe nyingine za kawaida kama vile birthday na kubariki ndoa ambazo zimehalaliswa makanisani na kanisani kwa ujumla bila ushahidi wa kibiblia.

  Watu wanatumia kifungu kinachosema chochote mtakachobariki duniani na mbinguni kitabarikiwa, vibaya hadi kubariki mambo ya kishetani.

 57. Christmas is now spelt—Xmas, Christ has been replaced with the letter”X”the sound of snake –XXX, and christians do not ask questions about what anything stands for, we just copy and adopt things because it looks cool, is there restrictions anymore in christianity, or anything goes this days? Judges 21:25– In those days there was no king in Israel:every man did that which was right in his own eyes

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s