SABABU SABA ZA KIBIBLIA KWA NINI USIWE MGONJWA

Kati ya mambo ambayo yanampa mwanadamu wakati mgumu katika kipindi chake cha kuishi hapa duniani ni swala la kukosa afya…kuwa na udhaifu au kuwa na ugonjwa katika mwili wake.

Ukisoma Biblia inazungumzia habari ya uumbaji wa Mungu hapo mwanzo, na haioneshi hata sehemu moja ya kuwa Mungu aliumba magonjwa,udhaifu au mateso kati ya vitu alivyoumba. Magonjwa ni matokeo ya anguko la mwanadamu, alipokubali kutomtii Mungu na kumsilkiliza shetani. Akauza haki yake ya kumiliki na kutawala katika maeneo yote (ikiwemo afya).Akamuuzia Shetani haki ya kuwa ‘mungu wa dunia hii’ japo Mungu alimuumba mwanadamu awe ‘mungu wa dunia hii’…yaani awe mwenye kauli ya mwisho hapa duniani kwa niaba ya Mungu aliye hai.

Hata baada ya anguko la mwanadamu, bado Mungu aliweka ‘plan B’ ya urejesho wa kile tulichokipoteza kwa kutokutii kwetu…akaweka SHERIA, KANUNI na TARATIBU ambazo kama zikifatwa kwa usahihi na mwanadamu zitamtoa pale alipo na kumrejesha katika ‘KUMILIKI NA KUTAWALA’ japo si kwa urahisi na wepesi kama kabla ya anguko.

Nilipokuwa ninayapitia maandiko kwa muda wa miaka karibu 9 sasa tangu nilipopata ‘NEEMA’ ya kumjua Yesu kama BWANA na MWOKOZI wangu binafsi…Mungu amenifundisha ‘kweli’ nyingi sana na mojawapo ni hii ya kuwa na ‘AFYA TIMAMU’…Sababu hizi saba za kibiblia zinaeleza ni kwanini uwe na afya timamu(out of sickness and disease phase)…Zinafanya kazi katika maisha yangu…NA HAKUNA WAKATI WOWOTE NINAWEZA KUWA MGONJWA…HAIWEZEKANI NA HAITATOKEA…ni sehemu ya Mpango wa Mungu kwa maisha ya kila mmoja wetu…si kwangu tu…wala kwa baadhi ya watu wenye ‘IMANI KUBWA’ au ‘UPAKO’ sana. Ni kwa ajili yako na ni sasa….!

Ebu tuanze kuzichambua kweli hizi saba, kwa Jina la Yesu:

 1.KAZI YA MSALABA

Kama unamwamini Yesu we si mgeni wa neno hilo hapo juu…ina maanisha kufa na kufufuka kwa Yesu…na matokeo yake chanya juu ya maisha yetu.Wengi tunajua Msalaba umetupa kuwa wana wa Mungu, watu wa nyumbani kwa Mungu,umetupa Uzima wa milele,umetupa msamaha wa dhambi nk

Lakini hatuko tayari kukubali kwamba msalaba huohuo umeleta “AFYA YA KIMUNGU” ndani yetu! Biblia ktk 1Petro 2:24 inasema, “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu MWILINI MWAKE juu ya mti ili tukiwa hai kwa mambo ya haki tuwe wafu kwa mambo ya dhambi, NA KWA KUPIGWA KWAKE TULIPONYWA” Haisemi tunaponywa au tutaponywa…inasema ‘TULIPONYWA’  Andiko lingine linatoka katika Mathayo 8:17, “Yeye mwenyewe(Yesu) aliuchukua UDHAIFU wetu, amejitwika MAGONJWA yetu’…kama ameyachukua magonjwa yetu, kwanini sisi(Wakristo) tunayang’ang’ania? kama amejitwika magonjwa yetu kwa nini sisi tunalazimisha kujitwika Magonjwa? Utamsikia Mkristo aliyeokoka tena kajazwa na Roho wa Mungu lakini anasema…’Yaani hiki kichwa changu kinauma kila mara tangu nikiwa mdogo’…mwingine anasema…’Hili tatizo la kubanwa na kifua ni la familia yetu, hata mama naye analo…’ huku ni kujaribu kukana kile ambacho Yesu alishafanya MSALABANI…ALIYEKUSAMEHE DHAMBI ZAKO NDIYE ALIYEKUPONYA….”Akusamehe maovu yako yote akuponya Magonjwa yako yote” Zab 103:3

Kama unamwamini Yesu…tena kwa moyo wako wote na unasema wewe ni raia wa mbinguni na unadai ya kuwa Mungu ni baba yako…HURUHUSIWI KUWA MGONJWA, DHAIFU hata mara moja…tembea katika afya timamu tangu sasa kwa Jina la Yesu wa Nazareth.

 2.WEWE NI NYUMBA YA MUNGU (MAKAO YA MUNGU)

Biblia inasema ya kuwa unapompa Yesu maisha yako na kumwamini, unakuwa ndani yake na Yeye ndani yako wewe, na pia MWILI wako unapata ‘HADHI’ au ‘HESHIMA’ ya kuwa NYUMBA/MAKAZI YA MUNGU ALIYE HAI….”Je hamjui ya kuwa MIILI yenu ni hekalu la MUNGU, na ya kuwa ROHO WA MUNGU anakaa NDANI yengu?” 1Kor 3:16-17, 1Kor 6:14-19

Biblia inaeleza ya kuwa Mungu anakaa sasa ndani ya MWILI wako…kwenye CELLS, TISSUE,ORGANS na System za mwili wako….Je unadhani vimelea vya MAGONJWA vitaweza kuishi katika uwepo wa Mungu uliotuama ndani yako…unaotiririka ndani yako? HAIWEZEKANI NA HAITAWEZEKANA

 3.UKO NDANI YA YESU

Biblia inasema katika 2Kor 5:17 ya kuwa “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo Yesu, ya kale yamepita na tazama yote yamekuwa mapya” Tangu siku ile ulipompa Yesu maisha yako…uliingia ndani yake!

Huo ndo ukweli wa mambo hata kama shetani anajitahidi kukuzuia usilifahamu hili.

Kama ni hivyo, ebu tembea na Ufunuo huu alionipa Mungu nilipokuwa ninafundishwa hili…Ili Ugonjwa uweze kukufikia wewe unapaswa kwanza umtoboe Bwana Yesu, kisha ndio ukufikie na ukupate…kwa hiyo unaamini kuna ugonjwa wenye nguvu ya kumtoboa Bwana Yesu? achilia mbali kuusogelea tu uwepo wake…KUWA NA AFYA NI SEHEMU YA MAISHA YAKO NDANI YA YESU.

 4.UMEZALIWA KWA NENO LA MUNGU

Biblia inasema ya kuwa tulio ndani ya Yesu, tumezaliwa mara ya pili(tumeokoka) kwa Neno la Mungu…Soma 1Petro 1:8, Yakobo 1:8… kwa maneno mepesi tu wana wa NENO LA MUNGU….na Biblia inasema ya kuwa NENO ni MUNGU (Yohana 1:1-3)…na kama unataka kupiga hatua yoyote kubwa kiroho au kimwili ni lazima ulitumie NENO na uliishi NENO, yaani uliweke NENO kwenye matendo (Yakobo1:21-24)

Mithali 4:20-22 Inasema, “Mwanangu yasikilize maneno yangu, tega sikio usikilize kauli zangu, zisiondoke machoni pako, uzihifadhi moyoni mwako, maana ni UHAI kwa walio nazo(waliozishika) na AFYA ya mwili wao wote”

 5.KUMTUMIKIA MUNGU

Biblia katika KUTOKA 23:25-26 inasema, “NAWE UTAMTUMIKIA BWANA MUNGU WAKO; NAMI nitakibarikia chakula chako na kinywaji chako…SITATIA JUU YAKO MAGONJWA YOTE niliyotia juu ya Wamisri(wasioamini)…kwa maana mimi ni BWANA MUNGU NIKUPONYAYE”

Kama unataka kufurahia afya timamu wakati wote hauna budi kuwa na muda wa kutosha wa kumtumikia Mungu, kwa nguvu zako, fedha au mawazo yako. Na kama ukiwa na bidii katika hili utayapiga teke Magonjwa maishani mwako…Utafurahia AFYA YA KIUNGU kila iitwapo leo!

 6.UMEINGIA SAYUNI NA YERUSALEM WA MBINGUNI

Ukisoma katika Isaya 33:21-24 utaona ahadi za ajabu walizonazo wale wanaoishi katika Sayuni…amani, usalama, kumiliki,nk lakini zaidi ni ile iliyoko mstari wa 24 isemayo, “Wala hapana MWENYEJI wa mji huo atakayesema mimi Mgonjwa”…yaani watu wa Sayuni hawana habari ya magonjwa maana Mungu ndiye Mfalme wao na pia ndiye mtetezi wao!

Ukisoma Waebrania12:22 Biblia inasema ya kwamba sisi(tuliokombolewa na Yesu) tumeufikiria mlima Sayuni na Yerusalem wa mbinguni, mji wa Mungu aliye hai, ambako kuna majeshi ya malaika (malaika wa vita/wapiganaji) maelfu elfu…Huku ndiko tuliko, ambapo Mungu ni baba yetu… na sie ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa NYUMBANI KWA MUNGU(Waefeso2:19)

Kama uko ndani ya Yesu, unaishi Sayuni, na HAURUHUSIWI KUWA MGONJWA…maana hapana mwenyeji hata mmoja atakayesema mimi mgonjwa!

 7.KAA UWEPONI MWA BWANA

Zaburi 91:1-16 Inasema “Aketiye uvulini(uweponi) mwa aliye juu atakaa salama…Hauaogopa TAUNI(UGONJWA WA MLIPUKO)iliyo gizani  wala UELE uharibuo adhuhuri…ijapokuwa watu elfu wataanguka(waakufa kwa sababu ya Magonjwa) mkono wako wa kushoto, naam kumi elfu mknono wako wa kuume,lakini hautakukaribia wewe…maana Bwana atakufunika kwa manyoya yake na chini ya mbawa zake utapata kimbilio…”

Ukitaka kuongeza miaka yako ya kuishi, ukitaka kuwa na Afya ya Kiungu, kulindwa na Nguvu za Mungu, kustawi, kutukuzwa na kuinuliwa na Mungu, yote haya yako katika UWEPO WAKE.

Lazima ujifunze kukaa mbele za Bwana, kupitia maombi, kulisoma NENO, Kumtafakari Mungu, kwa Kusifu na kwa kuabudu pia…TUMIA MUDA WAKO MWINGI UWEPONI KWA BWANA.

Ni maombi yangu kwa BWANA kwamba Mungu aliye hai atayafungua macho ya moyo wako, na Nuru ya Kristo itang’aa ndani yako mara tu umalizapo kuusoma ujumbe huu…Ni ujumbe wa Mungu kwako!

Wako katika Ndani ya Kristo Yesu,

—Dickson Kabigumila

20 thoughts on “SABABU SABA ZA KIBIBLIA KWA NINI USIWE MGONJWA

 1. Amina. Hiyo ni kweli tupu, chanzo cha magonjwa yote ni dhambi na uasi, ndiyo maana ikaandikwa, “mtaifahamu kweli na iyo kweli itawaweka huru,” ,,,yohana 8:32) MAANA YAKE TUKO HURU MBALI NA MAGONJWA, VITA, UMASKINI, NK,… Kikubwa apa ni kufuata tu kanuni na sheria ya Roho wa Uzima ,,,warumi 8:2) hiyo ndiyo inayotuweka huru mbali na sheria ya dhambi na (magonjwa) “mauti” ,,, kwani YESU alikuja ili tuwe na “uzima,” (si magonjwa) na kisha tuwe nao TELE,,,TELE,,,TELE,,,
  … endelea kubarikiwa”
  *** freddjj

 2. mr Milinga? Bwana Asifiwe? nauliza kama hatuko chini ya Adam au musa ati tuko chini ya Yesu.na juu ya 10comd na na Musa alipewa juu ya watu.Tuko chini ya 10comd?

 3. Hapana Milinga, ndugu Dickson yuko sawa.

  Maandiko ya Isaya 33:21-24 yanahusu wakati huuwa agano jipya wala si wakati ujao wa millenium kingdom kama unavyosema.

  Ukitaka kupata tafsiri halisi ya maandiko ya mbweha kucheza na kondoo, na simba kulisha pamoja na ndama n.k, lazima ujue katika ”metaphor” (lugha za picha) za biblia tangu mwanzo simba, kondoo, mbuzi, mbweha,chui zilimaanisha nini.
  Believe me, hao simba wanaosemwa si simba wanyama.

  Ukisoma tu hii Isaya 11:1-5 utagundua kuwa inaongelea habari za kuzaliwa kwa Yesu wala si kuja kwa Yesu mara ya pili.

  Tukubali tu ukweli kwamba tukimlingana Mungu sawasawa, na kuzingatia kanuni za afya( kama ulivyosema Milinga) hatutakuwa chini ya magonjwa maana ni moja ya mambo yaliyompeleka Yesu msalabani.

  Tujiulize sana kwa nini mitume hata Yesu mwenyewe hatusomi kama waliwahi kupatwa na magonjwa, zaidi ya Paul ambaye hata hivyo haijaainishwa wazi kama kweli huo mwiba ulikuwa ni ugonjwa.

 4. Wapendwa, Heri ya mwaka Mpya?

  Mtumishi wa Mungu Dickson Kabigumila ameleta mada ambayo huwa ni tata. Mafundisho ya kwamba ukija kwa Bwana huna sababu ya kuugua nadhani ni miongoni mwa mafundisho yenye dhana potofu sana.

  Napenda kuwakumbusha kwamba makanisa yetu mengi yenye mwelekeo wa Kipentekoste yamejaa mafundisho mengi potofu kuhusu maswala kadhaa ikiwemo hili la Magonjwa.

  Wapo wapendwa wengi wanaoshindwa kuelewa mgawanyo wa nyakati za Mungu.

  Hatuna budi kuelewa kwamba tangu Adam na Eva hadi sasa Mwanadam amepitia nyakati mbalimbali na katika Ufunuo, Daniel na Isaya kuna nyakati nyingine ambazo wanadamu hawajaanza kuziishi. Hapa ndipo hata Dini ya Mashahidi wa Yehova na Sabato wanapojichanganya.

  Wapendwa tunapaswa kuelewa kwamba mafundisho aliyoyatoa Mtumishi huyu Dickson hayahusu nyakati tulizonazo. Haya yanahusu wakati ujao ambao unasemwa pia katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana na kile cha Nabii Daniel kitakachokuwa cha miaka isiyopungua Elfu Moja. (Sion Millenium au Jesus Christ reigning Millenium).

  Kuna nyakati mwanadamu amepitia kama ifuatavyo kwa wasomi wa Biblia wataelewa:

  1. Adam na Eva waliambiwa kula Matunda ya Miti tu na wazae waijaze dunia ikaliwe na watu. Hilo lilitimia hadi Gharika ilipotokea.(Wakati huu ulishatoweka)

  2. Baada ya Gharika Kuu ya Dunia, Nuhu na Kizazi chake waliagizwa kula matunda, Nyama na majani kasoro damu ya wanyama. Aidha waliagizwa kuzaana upya ili kuongezeka watu duniani.

  3. Enzi za Musa nazo zinaanzia Misri hadi Yesu alipozaliwa. Enzi za Musa na Manabii wanadamu wamchao Mungu walikatazwa kula baadhi ya vyakula tu vitokanavyo na wanyama kama vile kutokula Nguruwe, sungura, Ngamia, Punda, Kumbikumbi, samaki kambale, nk. Hizo zilikuwa enzi za Musa ZIMEPITA kabisa hazipo. Imebaki ni historia iliyoandikwa katika Maandiko na vitabu vya historia tu. Enzi hii haitarudi tena. Enzi za Musa talaka ya ndoa ilikubaliwa, kula mboga za majani, kula nyama na kunywa vilikubaliwa. Enzi hizo za Musa watu walikuwa wanapata tiba kwa kula mizizi, matunda, maji na kujichovya katika mabwawa kama vile Sloam, Mto Yordani, nk baada ya maji kutiwa dawa na malaika wa Mungu. Enzi hizo madaktari kama waliopo leo hawakuwepo. Tiba kubwa ilipatikana katika vyakula vya mazao ya miti na wanyama walioruhusiwa na Mungu. Lengo la Mungu kuwakataza wanadam wasile baadhi ya vyakula na ikawa hivyo kama sheria ya Mungu ilikuwa ni “Natural Healing techniques” za Mungu kwa watu wake. Kama Mungu asingewakataza watu wake kuacha kula baadhi ya vyakula hasa nyama zenye mafuta sana kama vile nguruwe, nk wangeugua mara kwa mara magonjwa mengi sana. Hivyo Mungu alikataza watu kula nguruwe kwa sababu za kiafya zaidi.

  4. Enzi za Kristo Yesu zilianza sasa yapata zaidi ya miaka 2000 hadi sasa. Katika Enzi hizi za Kristo (2012 BK) mambo ni tofauti sana. Magonjwa mengi bado yapo hata kwa wapendwa kwa sababu mbalimbali za kiroho, kiukoo, urithi, na ukosefu wa elimu ya afya na usafi wa mazingira.

  Enzi za Musa, Mungu aliwakataza watu wasiende kujisaidia haja kubwa au ndogo hovyo hovyo. Waliamuriwa kwamba wahakikishe wanachimba shimo na wamalizapo kujisaidia wafunike kinyesi. Tabia hii wanayo hata baadhi ya wanyama kama vile paka. Leo hii watu hawafuati kanuni za Mungu zihusuzo afya zetu. Hata wapendwa wengi pia. Hebu angalia Jiji la Dar es salaam lilivyoshindikana kwa usafi. Watu wanakula ovyo. Wanajisaidia ovyo. Mazingira ya kuandalia chakula majumbani mwetu au kwa migahawa ya chakula. Vyoo vyetu na mabafu yetu yako vipi? Utunzanji wa mazingira wapendwa umetushinda hata makanisani ukienda vyooni siku ya Jumapili ndipo utacheka wewe mwenyewe!!!!!! Vyoo havina Usafi kabisaa makanisa mengi. Fanya utafiti siku moja uone.

  Enzi hizi za Kristo (Agano Jipya), Watu wameongezeka sana. Inakisiwa kwamba wakati ule Kristo Yesu alipokuwepo duniani watu walikuwa hata hawafikii idadi ya bilioni moja. Lakini leo hii watu wameshafika zaidi ya bilioni Saba. Tanzania wakati wa Uhuru 1961 kulikuwa na watu wasizidi miloni 9 tu. Leo hii kuna watu zaidi ya milioni 40.

  Katika Enzi hii ambayo kuna dini nyingi, nyakati ambazo kuna makabila mengi na tamaduni nyingi sana zenye kufuata mitazamo na mafundisho tofauti kuhusu Usafi wa mazingira, Afya ya mwili, Mpango wa Uzazi, Tiba za kisasa au Kizamani, katika kizazi ambacho wahubiri ni wengi sana wenye mbwembwe kila aina na wenye kutafsiri maandiko katika milengo tofauti, dunia ambayo ina madaktari wengi waliosomea vyuo tofauti, katika dunia ambayo kuna vyuo vya Biblia tofauti SIYO SAHIHI KUSEMA KWAMBA WATU HAWATAUGUA.

  Wapendwa tunapaswa kuelewa kwamba tunaugua magonjwa mbalimbali kama vile Kuharisha, Kichocho, Kipindupindu, homa, minyoo, nk kwa sababu ya kutofuata kanuni za Usafi. Nchi kama ile za Ulaya na Amerika swala la Kipindupindu, kuugua malaria, minyoo au kichocho vimebaki katika vitabu vya Historia tu wakati sisi ndiyo wimbo wa kila siku. Magonjwa haya hata kama ungekuwa umeokoka kivipi, unafunga na kusali, unatoa zaka, unaimba kwaya, unahubiri, nk utayapata tu kama wewe huzingatii Usafi wa mwili, mazingira na unawaji wa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni. Magonjwa kama vile fangasi sehemu za siri, vidole vya miguuni, mapajani na kichwani, wanawake wengi na wanaume wanayapata kwa sababu ya kutokuwa wasafi au kutokufuata masharti ya Afya Bora. Magonjwa kama BP, TB, CANCER, HIV, nk yanatokana na kutofuata kanuni za Afya. Biblia imeeleza kwamba usikiite najisi kitu kilichotakaswa na Bwana na kwa kusema hivyo Yesu alivitakasa vyakula vyote. Lakini tuelewe kwamba Yesu alivitakasa vyote haina maana kwamba tule mazao ya wanyama au miti bila kufuata kanuni za usafi na ulaji.

  kUMBUKA kuwa kula nyama sana iwe nguruwe, mbuzi, ng’ombe, samaki, kuku, bata, nk huleta madhara kiafya. Majani ya chai huleta magonjwa, Kahawa huleta magonjwa, Kunywa maji yasiyochemshwa na kuchujwa huleta magonjwa, Kunywa pombe, kuvuta moshi wa sigara unapokuwa karibu na mvutaji nayo pia huleta magonjwa.

  Kumbuka pia kwamba Kulala au kuishi nyumba isiyokuwa na madirisha yanayopitisha hewa huleta magonjwa mengi kwa afya zetu. Kulala nyumba moja watu wengi zaidi ya uwezo wa nyumba hiyo huleta magonjwa. Kushirikiana mavazi huleta magonjwa. Kuvaa nguo moja au soksi za viatu kwa muda mrefu huleta magonjwa.

  Kumbuka kuzaa watoto wengi zaidi ya uwezo wa rasilimali ulizonazo nayo huleta magonjwa mengi kwa watoto na wazazi wao. Kama mwanamke atazaaa watoto zaidi ya 5, wengine wamezaa mpaka watoto 12, ukweli unabaki kwamba familia hiyo kama haina rasilimali nyingi(fedha, mashamba, mifugo, elimu, nyumba, nk) itakumbwa na maginjwa mara kwa mara na hawatapona kabisa. Watoto watakufa sana.

  kUMBUKA kutokufanya kazi za mikono na au kutokuufanyisha kazi mwili huu nayo huleta magonjwa. Kusema kweli wanadamu tumezungukwa na Ulimwengu wa magonjwa.

  Napenda kuhitimisha kwa kusema kwamba, maisha ya kutokuguua yanawezekana ikiwa tu watu tutafuata kanuni za afya kwa kuepuka kufanya mambo yasiyoendana na Biblia wala Afya.

  Ulimwengu ujao wakati Yesu atakaporudi kutawala dunia hii (Jesus Chrsit’s Millenium Kingdom) hapo ndipo litakatimia neno la nabii Isaya kama alivyoandika Bwa. Dickson, nanukuu, “Ukisoma katika Isaya 33:21-24 utaona ahadi za ajabu walizonazo wale wanaoishi katika Sayuni…amani, usalama, kumiliki,nk lakini zaidi ni ile iliyoko mstari wa 24 isemayo, “Wala hapana MWENYEJI wa mji huo atakayesema mimi Mgonjwa”…

  Andiko hilo na mengine yanayofanana nayo hayahusu Nyakati hizi za Agano Jipya bali yana husu wakati uajao wa utawala wa Kristo hapa duniani ambapo, watu hawatakufa, wanyama kama simba watacheza na mbuzi, watu wote wataenda Sayuuni kuabudu, hakutakuwa na kuugua tena wala kufa kwa wale watakaokuwa na Yesu katika utawala wake wakihukumu kabila za Israel na dunia nzima. Dunia nzima itakuwa sehemu nzuri ya kuishi na wala hapatakuwepo atayeugua kabisaaa.

  Nawatakia baraka tele.

  Obed Venerando Milinga

 5. Swali alilouliza Mr Orbi ni la msingi sana. Kwa sababu watu wengi wanaishi kabisa kwa kufuata hizo sababu 7 lakini magonjwa hayakuwaacha. Walokole wengi wanasumbuliwa sana na magonjwa tena mengine mabaya kabisa mfano saratani, vifafa, madonda ndugu nk. Hivi ni kweli ukiishi kwa kufuata hizo sababu saba utaishi pasipo magonjwa? Mbona watu wana magonjwa na hata wale waliookoka na wanasema wanakwenda mbinguni? Nenda hospitalini hutakosa mlokole aliyelazwa!! Mimi ninadhani hiyo ni “too theoretical!!” “The practical side of it” kwa maoni yangu ni hii.
  Asili ya magonjwa yote ni dhambi tu na dhambi yenyewe amesema Mungu katika Kutoka 15:26.; Kumbukumbu 28:15-69; Walawi 26:14-16. Hapa kuna tatizo moja kubwa nalo ni “kusikia sauti ya Mungu”. Watu wengi wanapoamka asubuhi kwenda kwenye shughuli zao huwa hawaelewi kama leo Mungu amewakasirikia au amesema nao nini kwa ajili ya siku hiyo au siku zijazo. Kwa sababu hiyo Mungu huona kama wamemfanyia kiburi kwa sababu Yeye anaongea lakini watu hawatii ufahamu (they perceive not) Soma Ayubu 33:14-16. “ajapokuwa mtu hajali” Biblia ya kiingereza inasema “he perceives not yaani hatii ufahamu katika yale anayosema”. Matokeo yake Mungu hupata hasira na kumtia adabu (kumletea magonjwa) mtu kwa kutokuisikiza sauti ya Ayubu33:19-22. Kwahiyo binafsi sifikirii kuwa inatosha kutumia approach ya hizo njia 7 ili kuishi pasipo magonjwa. Ni vema pia, pamoja na hizo njia saba, kuhakikisha mtu anayeamini anatumia principle hii ya kumsikiliza Mungu anachoamuru na hakika utakuwa salama pasaipo magonjwa.

 6. Amina ndg Nengai hapo umenena vema, mfano mwingine ni mtume Paulo na mwiba wake… ili Mungu adhihirike ktk udhaifu wake…
  sipo kufagilia vifungo wala magonjwa nami nimepona mengi kwa jina la Yesu, ila karibuni kumekuwa na mafundisho yanayosisitiza kupokea kila uombacho…mfano njoo kwetu hakuna anayevaa miwani, hakuna wagonjwa, ukiombewa sijui ukimwi, kansa ukapata amani ya Kristo ndani yako ukijasema nasikia maumivu tena….ahhaa amerudi nyuma huyu
  Jamani wapendwa nimeishakosana na wengi kwa imani kama hizi, majaribu ni mengi ktk safari yetu hii, lakini tunayashinda na kikubwa hayatuangamizi, sio vizuri kumuona mwenye ugonjwa kama kansa sijui ukimwi, ulemavu ohooo hana imani, karudi nyuma huwezi kujua amani aliyonayo na pili Mungu akikutupia wewe hilo jaribu naona ndio itakuwa mwisho wa wokovu wako. Tusimame ktk neno hata ktk majaribu yote iwe uhitaji au umaskini, ugonjwa, vifungo hata kifo. Mbarikiwe

 7. bwana Yesu Asifiwe wapendwa.
  naomba kumjibu orbi swali lake.”Kwa hiyo ina maana nikufuata hayo uliyosema sitakuwa na magonjwa?”somo alilofundisha mwalimu ni zuri sana lakini tujue kwamba tukiwa ndani ya Yesu na maneno yake yawe ndani yetu tunaweza kuumwa lakini ugonjwa tutakaoumwa sio kwaajili ya kutuangamiza ila ni kwaajili ya kutuimarisha.namaanisha hivi ugonjwa wetu sio trial bali ni test ili kwamba tuweze kupandishwa cheo tutakapo shinda.mtu wa duniani akiumwa anaangalia zaidi ule ugonjwa alionao ila wewe mkisto ukiumwa unatakiwa umuangalie yule ambaye ni mponyaji.kumbuka habari za yule nyoka wa shaba ambaye alipandishwa,waisrael walitakiwa wamuangalie tu yeye na wala sio wale nyoka wadogo ambao walikuwa wakiwauma.mfano mwingine ni wa ayubu,Mungu aliruhusu apate ule ugonjwa ili kwamba akishinda katika hilo yaani kutokumkana Mungu basi atapandishwa cheo.mtihani mwingine ni ule alioupata Ibrahim,mke wake alikuwa tasa si ili kumuangamiza ila kumpandisha cheo siku atakapo shinda huo mtihani. kwa hiyo cha msingi sana ni kwamba ugonjwa unapokuja ni kutafuta kujua mapenzi ya Mungu katika huo ugonjwa,kwasababu kama Mungu ameachilia huo ugonjwa kwa kusudi lake hata uombewe vipi hautapona kwa muda unaoutaka wewe ila mpaka mapenzi ya Mungu yatakapotimia katika hilo.

  mbarikiwe

 8. asante sana kwa ujumbe huu mzuri! Mungu azidi kukulinda, Mungu akubariki sana

 9. Shalom jamani
  mbona hamumjibu kaka Orbi, nikiwa na magonjwa je sifuati Biblia au magonjwa mengine ni kujaribiwa imani yako, iwapi neema yangu yakutosha hapa?

 10. Ubarikiwe sana kaka, nimebarikiwa sana na somo hili kwakweli limenifariji sana. Mungu na azidi kukufunulia zaidi. barikiwa

 11. Nimebarikiwa sana na ujumbe huu wa uponyaji. Mungu akuabariki na kukufunulia mengi zaidi

 12. Aisee nashukuru Mungu kwa ajili ya Blog hii, pia nashukuru Mungu kwa Jinsi alivyomtumia Mtumishi wake Kabigumila, aisee hii ni kweli tupu sina kipingamizi.Nashukuru Roho Mtakatifu kwa kuwa alikuwa pamoja na mtumishi wake Kabigumila. Mungu na aendelee kukutumia katika masomo mengine mbali mbali, hasa katika kipindi hiki cha siku za mwisho mwisho, kwa kanisa likiwa linakaribia unyakuo.Somo ni zuri sana endelea kukaa uweponi mwa Bwana ili akutumie zaidi na zaidi. BARIKIWA MTUMISHI WA BWANA !!!

 13. m mwenyewe binafsi kwa ushuhuda wa biblia sishawishiki kuwa sisi kama wakristo tunapaswa kwenda hospital ambazo uponyaji wake si wa kumtegemea Mungu au tunaweza kusema haukuagizwa ndani ya biblia.
  tunalotakiwa kufanya ni kuamini juu ya Mungu kwa udhaifu wowote ule yakiwemo na magonjwa yote.
  MAOMBI NDO IWE SILAHA KUU!

 14. NASHUKURU KWA UAMSHO HUU,NINA USHUHUDA WA MAMA YANGU AMBAYE KUUMWA KWAKE IMEKUWA KAMA SEHEMU YA MAISHA YAKE,SIKU ZA FURAHA KWAKE NDOGO KULIKO UDHAIFU WA MWILI,NAOMBA MUUNGANE NAMI KATIKA MAOMBI ILI KUMBADILI MITAZAMO YAKE MAANA YUKO KIMWILI ZAIDI KULIKO ROHONI. BADO HAJAJUA KWELI ILI IMUWEKE HURU.LAKINI NEEMA YA MUNGU INAZUNGUKA KWA AJIRI YAKE MAANA TULIO WATOTO TUNAOKOKA(TUMEMKILI YESU KRISTO KUWA BWANA NA MUOKOZI WETU) WAO WANABAKI KUONA BARAKA ZA MUNGU KWENYE MAISHA YETU.

  NASHUKURU KWA KUNIONGEZEA MANENO MENGINE YA KIBIBILIA KWA AJIRI YA NENO LA MUNGU KUKAA KWA WINGI MOYONI MWANGU.MAANA PASIPO IMANI HUTUWEZI KUMPENDEZA MUNGU waebrania 11.6

 15. Bwana YESU kristo asifiwe ndugu katika bwana nashukuru kwa makala mnayonitumia kila wakati na yamekuwa msaada mkubwa sana kwangu mimi kwani nimepata kujua vitu vingine vingi ambavyo sikuwa na vijua, ikiwemo sababu saba ….. nimejifunza mengi sana ,MUNGU WA BABA ZETU MUNGU WA ELIA IBRAHIMU MUSA,YAKOBO NA BWANA WETU YESU KRISTO AWABARIKI SANA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s