Utii Kwa Mume

Kiswahili kina mameno machache, tafsiri ya ‘obey’ na ‘submit’ yote ni utii kwa Kiswahili, lakini kwa uhalisia ‘submit’ ni zaidi ya ‘obey’.’Submit’ ni kukubali kwa unyenyekevu kuwa chini ya mamlaka fulani, kuiamini hiyo mamlaka na bila kujaribu kuwa juu yake, na ‘obey’ ni kufanya kile unachoambiwa na mamlaka iliyo juu yako. Hivyo utii wa submit ni zaidi ya utii wa obey. Ni kuamua kuwa chini ya mamlaka hiyo na sio kusubiri kuambiwa kitu ndipo utii. Utii wa mke kwa mume ni ‘submit’, kuamua kuwa chini ya uongozi wa mume wako, kuuheshimu na kumwamini kuwa anaweza kuwaongoza bila kutaka kuingilia nafasi yake kama kiongozi.

Jambo hili limekuwa ni gumu sana kwa wanawake wengi hasa wale ambao wana kipato, wlimu, huduma au nafasi katika jamii zaidi ya waume zao. Biblia inawataka wake wote kuwatii waume zao bila kujali hali zao wala nafasi zao au kama wameokoka ama la.

Waefeso 5:22-24 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo na wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

Mistari hii katika biblia inatuonyesha jinsi gani inavyotupasa kuwatii waume zetu. Paulo amefananisha utii huu na utii wa kanisa kwa Kristo, utii wa kuamua toka moyoni kunakosukumwa na upendo na wala sio utii wa kulazimishwa. Ni utii katika kila jambo, dogo hadi kubwa kama vile kanisa linavyomtii Bwana Yesu. Ila tunapewa angalizo, “kama ipendezavyo katika Bwana”. Hivyo hatupaswi kutii pale ambapo tunaelekezwa kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

Kolosai 3:18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.

 Unaweza kusema kuwa mume wako hajaokoka na wewe umeokoka hivyo ni vipi sasa utajiweka chini ya uongozi wake? Biblia inalojibu kama tunavyoona hapa katika mistari hii ifuatayo.

1 Petro 3:1-2 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;

Kumbe utii wako kwa mume wako kunaweza kumfanya akaokoka bila hata mahubiri ya maneno mengi. Kutii sio utumwa, ni kuitambua nafasi ya mume wako na nafasi yako kama mke kwenye ndoa yenu. Unapoitambua nafasi ambayo Mungu amekupa utashangaa utii unakuja bila hata kujisukuma. Wewe ndiwe mlezi wa familia, mfariji wao, muangalizi, mfundishaji watoto na mengine mengi. Soma Mithali 31:11-31

Katika biblia tunaona jinsi Sarah alivyokuwa mtii kwa mume wake Abrahamu. Mume wake alipomuambia kwamba Mungu amesema watoke katika nchi yao na waende katika nchi atakayowaambia wasipopajua wao, sarah alimtii bila kubishana naye. Alikuwa tayari kuondoka mahali alipopazoea na kuenda na mume wake asipopajua kwa sababu alimuamini Mume wake na kuwa tayari kuongozwa naye. Mwanzo 12:1-9

Mume anajukumu kubwa sana la kumpenda mke wake kama Kristo kwa kanisa, upendo usio na sababu, upendo wa kujitoa kwa ajili yake, upendo wa kumtanguliza. Mume anapofanya haya ni rahisi sana kwa mke kumtii bila kuona uzito, ila hata kama mume wako bado hajafikia kiwango hicho cha upendo, wajibu wako wa kumtii upo pale pale na hapo utaziona Baraka za Mungu katika ndoa yako.

Ubarikiwe na Bwana Yesu.

Advertisements

9 thoughts on “Utii Kwa Mume

 1. mhhhhhh.kati ya mke na mume kunatakiwa kuwe na hali ya kutoa na kupokea,kwamaana mume ampende mke wake ndipo mke atamtii,tena inatokea aotomatically.upendo lazima uanze,Kristo alilipenda kanisa alifanya kila alivyoweza kuonyesha upendo kwa kanisa ,ndipo kanisa likamtii na kumwani kristo.nichangamoto kwa wanaume kuwapenda wake zao kama kristo na kanisa

 2. Ni kweli kabisa Grace mwanamke ni mlinzi wa mume wake.na Mungu atausaidie wanawake kusimama katika kusudi lake maana mwanamke anavishawishi vingi. kama Hawa alivyoweza kumshawishi Adamu hata akala tunda. Basi mwanamke wa leo simama kushawishi mambo ya Kimungu ili Adamu wako asimame Imara. Mungu anamwangalia mwanamke kama muombelezaji anasema niwapate wapi wanake wanaojua kuomboleza hata wakagusa moyo wangu. Taifa linapoangamia, ndoa zinapoingia matatani, watoto wanapoharibika Mungu anamtazama mwanamke kama muombolezaji. Hivyo wanawake tuwe watii tusimame katika zamu zetu kama walinzi na Mungu atakuwa pamoja nasi.

 3. Bwana Yesu asifiwe kaka ROYA , umechangia vizur, ila sikuungi mkono unaposema mwanamke ni chombo dhaifu, mwanamke ni jeshi kubwa, mwanamke ananguvu sana aliweza pambana uso kwa uso na nyoka bustani ya edeni, mkombozi wa taifa, familia mfano esta, abigail, pia Mungu amemuweka mwanamke kuwa mlinzi wa mume, ya kwamba mwanamke atamlinda mwanamme, mlinzi mi mtu anaepambana na majambazi, wezi, wanyama etc. tatizo wanawake wengi hawajitambui nafasi waliopewa na Mungu, lkn kama wanawake wote tungetambua nafasi yetu ktk ulimwengu wa roho na uwezo tulionao hata makahaba wasingeweza kukamata ndoa za wakristo.

  mbarikiwe

 4. Bwana asifiwe

  Kweli ndugu YOHANA kama ujahowa uwezi kujuwa mambo ya Mme na Mke iko mambo mingi sana na iko tafauti kwa kila mutu. Kama vile inaposema ku Waefeso 5:22-24 kwa wengine inatumika na kwa wengine ni UPUHUZI mutupu kwa kweli tabiya ya Mme inaweza kubadirisha tabiya ya Bibi ama tabiya ya Mke pia inaweza kubadirisha Mme kwa njia mengi pamoja na ufumilifu mno.Mungu alijuwa kama Mke ni chombo zaifu sana . Na ndio alisema sana juu ya kueshimu kwao.kama tukiangaliya mambo iko mingi sana ndani ya unyumba ingine kutoka kwa washemeki ya Bwana ama ya Bibi na pale tayari Upendo inapoa wakati Upendo Unapoa tayari eshima inatoka automatique.

  Mungu alisema ukipata Bibi muzuri ni baraka kutoka mbingu.Akusema juu ya Bwana Sisi kweli tuwapende wake wetu kama nafsi yetu mwenyewe iko na mahana sana .na zaidi juu ya elimo ama pesa ama jamaa ya bibi wako ya Pesa koliko ya Bwana NK.

  NB…. wandugu kweli mambo ya eshima ni apa Afrika ndio tunasimamiya . lakini vile mimi naishi ULAYA nitafauti saaaana kule wa bibi mambo wako na fanya iko ya kutisha sana juu ya pesa ya watoto na sheria ya Wazungu iko atari ata nalishidwa kuelewa kitu inabaki tu ni kuwaombea sana

  Kumbuka wandugu Mungu alisema na jamaa ya LOTHI watoke Sodoma Na Gomora na akasema ata mutu asitazame nyuma Bibi ya LOTHI alitazama nyuma aliendelea ama La
  History iko mingi sana juu ya wamama Heshima tu Mungu aliwapa kuzaliwa kwa Bwana wetu YESU kupitiya wao ndio Heshima ikarudi sana tena

  Basi ile tu machache muchango yangu
  Mubarikiwe

 5. ni kweli ndugu zanguni,Ndoa ni kusudi la Mungu kwa 100% ila wengi hupenda kuziongoza kwa akili zao binafsi,na huaanza vibaya tangu mwanzo wa ndoa hizo,lakini ukianza vizuri tangu uchumba hadi ndoa kwa kumhofu na kumwogopa Mungu,kisha kumtanguliza HAKUNA LISILOWEZEKANA KWAKE,ninyi vijana msioooa msiogope kwani ndoa ni mpango kamili wa MUNGU,na matatizo uyaonayo katika ndoa ya mwenzio sio yatakuwa kwako cha muhimu ni kujua chanzo cha matatizo yao nawe kuepuka usifuate nyayo hizo
  barikiweni kama mimi nilivyobarikiwa katika somo hilo

 6. Naamini mno katika wajibu na haki.Kwa uelewa mdogo,kumbe Mume ana WAJIBU wa kumpenda MKEWE,kutunza FAMILIA na hta KUJITOA(kama Kristo alivyolipenda KANISA hata AKALIFIA)

  Kwa maoni yangu kumbe mume akitekeleza wajibu huo hapo juu SUBMISSION ya MKE , HONOUR ya WATOTO na VINGINE VITAFUATA
  JIULIZE KAMA MKEO ANAKUTII NA WEWE HUONESHI HATA CHEMBE YA UPENDO utii huo ni wa kweli au ni changa la macho?

 7. Ni kweli ni lazima mke na amtii mume wake vivyo hivyo na mme amtii mke wake ndivyo lilivyo kusudi la Yesu kwao katika ndoa yao.Haijalishi mme wako ni mlevi ama ni mtu wa mataifa ni lazima ujue kuwa anayepaswa kuvumilia ni ww mke,anayepaswa kuomba kwa ajili yake ili awe na apate nuru ya Yesu ni ww mke,na sio wakati wa kuanza kumsema vibaya mme wako.Tambua kuwa ukimsema vibaya mme wako ni sawa na unajisema wewe mwenyewe maana wewe na yeye ni mwili mmoja.
  Kwa maombi ya mke na mme ataponywa kadhalika na kwa maombi ya mme na mke atafunguliwa.Kwa kuheshimiana ktk ndoa mtakuwa mnaitengeneza kizazi cha watoto wenye utii na uadilifu ktk jamii wenye adabu nzuri

 8. Waefeso 5:33: Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.

  Ila siku hizi swala la upendo na staha katika ndoa nyingi ni nadra kama madini ya alimasi, pamoja na kwamba wanandoa hao ni wakristo. Tatizo ni watu kuruhusu ndoa zao ziongozwe na elimu za kidunia na sio neno la Mungu.

  Elimu kama Gender equality, gender mainstreaming, gender integration, gender dimension na kadhalika, hasa vyuo vikuu kama UDSM (DS), watu hasa wanawake, wakizichukua kama zilivyo bila kuchanganya na akili zao zitaendelea tu kuwagharimu. Hii inatuvunja mioyo sana sisi vijana ambao hatujaoa au kuolewa tunapoona mioto ikiwaka ndani ya ndoa nyingi, mpaka mtu unaanza kuhisi inawezekana maisha ya ndoa ni magumua sana, Mungu atusaidie.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s