Gwajima afungua tawi, London…Ashuhudia misukule inavyofufuka Tanzania!

Hivi karibuni mchungaji kiongozi wa huduma ya Ufufuo na uzima kutoka Dar es salaam nchini Tanzania, ameongoza ibada katika ukumbi wa shule ya sekondari Peak View maeneo ya Tottenaham, jijini London. Ambapo ni tawi la huduma yake alilofungua mwezi July mwaka 2011, Katika Ibada iliyofanyika amenunua vyombo vya muziki kwa ajili ya kanisa hilo na kuahidi kutuma wachungaji wengine kuja kanisani hapo kwa ajili ya kazi ya Bwana.

Ibada hiyo iliyofunguliwa na mchungaji Grace Gwajima aliongoza maombi na kumkaribisha baba mchungaji kufundisha Neno la Mungu, katika mafundisho yake alianza kwa kusema kuwa makini na uwepo wa shetani duniani “be aware of Satan’s presence in the world Mungu alimpa mwanadamu bustani ya Eden ili aitawale na kuitunza but man handed it over the devil after sinning, toka wakati huo dunia ikawa mikononi mwa shetani na ma agent zake,akitolea andiko kutoka Mat 4;8″

Pia amefundisha kuhusiana na Nyota inayowakilisha maisha yako inaweza kukingwa (A star of your life can be covered), amesema kuna astrologies, Sorcerer and the devil can know what you’re going to become in the future through your star, Matthew 2;1-2. Pia amezitaja shuhuda mbalimbali zikiwemo za jinsi Mungu anavyomtumia kufufua watu waliokufa, ukiwemo ushuhuda wa aliyekuwa mtabiri maarufu wa nyota Afrika Mashariki, alivyokuwa anatumia nyota za watu wengine kumng’arisha mtu mwingine na kumuonya kuacha tabia hiyo pamoja na kumpa masharti amabayo asipoyatimiza angekufa kitu ambacho kilitokea baada ya mnajimu huyo kukaidi. Shuhuda hizi ziliwagusa watu wengi waliohudhuria kwenye ukumbi wa ibada.
Akiendelea kusema “shetani anashikilia mihimili mikuu minne ya dunia ambayo ni Siasa, Jeshi,Dini na Uchumi, akasema kuna watu wanabaki wanahangaika na matatizo,wengine hawana amani, furaha kiasi kwamba wanadhani Mungu amewaacha la hasha.The devil can cover your star that your competence, ability, attraction cannot be seen. That is why people struggle a lot to make it in life because after the devil seeing your star and fore seeing what you’re going to become in your future he plans to kill it at an infant stage so what you need to have is Knowledge of the word of God kwasababu ufahamu wa Neno la Mungu ni nguvu ya kumshinda”
Akasisitiza kusema sehemu yoyote ulipo au kazi unayoifanya ili kupata mafanikio itategemea ni kwa jinsi gani unavyojishughulisha au “it depends on how you kick the ball, there is no dry place” akitolea mifano ya watumishi wengi na watu maarufu duniani akasema hapo walipo wamepambana sana kufikia mafanikio, pia alitoa ushuhuda kuhusu maisha yake, the devil can block or delay your miracle but he doesn’t have power to stop you from what God wants you to be. Daniel 10;12.
— Gospel Kitaa
Advertisements

17 thoughts on “Gwajima afungua tawi, London…Ashuhudia misukule inavyofufuka Tanzania!

 1. Huko London nako mmebanikwa juani (a blazing sun- a type of a miniature hell!) kama ndg zenu wa Kawe?!!

  Inasikitisha sana tunapowaona ndg zetu wakianikwa juani huku mchungaji akijirusha na chopper; Mwakasege makes the difference, anawaheshimu wateja wake, anawakinga na jua kwa maturubai, and in that coolness wapendwa huwa wanaielewa Injili vilivyo, tofauti na mfumuko wa hisia kali unaowapata walio juani over non issues!!!

 2. JESUS IS LORD AND MASTER IN THIS, BE CONCERNED, PARTICIPATE. BLESSINGS SHALL FOLLOW YOU ALL THE DAYS OF YOUR LIFE AND YOU SHALL DWELL IN THE HOUSE OF THE LORD FOREVER.

 3. jiji la London lawaka moto wa Roho Mtakatifu, hatimaye watu wanawapigia simu ndugu jamaa na marafiki walio nchi jirani waende kupokea parcels zao za kiroho kupitia mpakwa mafuta wa Mungu Mch. Josephat Gwajima. asante sana wewe unaeshirikiana nasi kwa maombi na tuzidi kuomba Mungu azidi kuokoa mataifa ya huko nje kupitia watumishi wake.

 4. haya haya…… Mikutano mikubwa ya injili kufanyika London Uingereza kuanzia leo tarehe 29/04 hadi 06/05/2012 na Mchungaji Josephat Gwajima atahudumu, hivyo omba kwa ajili ya huduma hiyo na Mungu akubariki

 5. Bwana Yesu Asifiwe. Songa mbele mtumishi wa Mungu, vita vipo lakini hawatashinda. Na utawezaje kutulia ikiwa Bwana amekupa agizo

 6. Bwana Yesu atukuzwe! Mtumishi Wa Mungu ndugu Asheri naomba kama utakuwa na nafasi kama unaishi dar njoo kawe kwenye viwanja vya tanganyika packers ntakuonyesha baadhi ya hao waliofufuliwa maana wengi wao wapo kanisani bado na upate muda wa kuwahoji mwenyewe then tutakuwa na muda wa kupitia mandiko pamoja. Naamini kwamba kwa kufanya hivyo tutajifunza vizuri ndugu ili tuwe askari imara wa Kristo na tuzidi kuujenga ufalme wake Kristo kwa umoja. Au tunaweza kupanga wote pamoja siku ambayo kila mtu aje akiwa na vigezo vyake naamini Mungu ni mwaminifu kwa Roho wake atatufundisha kwa kina, marefu na mapana yote. Ni kwenu wote hata kina Daniel na Lwitiko. Kiu yangu ni kutaka sana tusimame kwenye kweli ya Biblia na siyo maneno ya kwetu sisi wenyewe. Binafsi sipendi kuonekana tunabishana kwa ajili ya Injili bali napenda tufundishane tupate maarifa then tuweze kusimama imara kwenye imani yetu. Hayo ndo yangu.

 7. Ndugu Gershon Mwakila,

  Shalomu

  Naomba unisaidie maana ya neno msukule hasa kibiblia na unisaidie kuonyesha jinsi neno la Mungu linavyosema kuhusu Misukule.

  Pili, miaka ya 2008 mpaka 2009, suala la Misukule lilikuwa juu sana hapa Tanzania, kwasasa limepoa kabisa, ila limeibukia huko London, je hapa kwetu misukule imeisha?

  Tatu, wewe binafsi uliwahi kuona msukule uliofufuka? hivi sasa huyo msukule/mtu yuko wapi?

  Shalomu,

  Mungu akubariki

 8. Shalom, Lwitiko hapo ndipo penye tatizo pale ambapo watu wanatengeneza hoja hata hawajasikiliza ujumbe wenyewe, fasihi simulizi inapoteza ujumbe kwa kadri inavyosimuliwa. 2Tim 3:16, kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao na kwa KUWAONGOZA…… Kama ni hivyo basi, habari ya nyota tuangalie Mathayo 2:2b, …..kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia, nyota ya Yesu ilionekana na wale wataalamu wa kusoma nyota(mamajusi), nyota ni nini? Ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha wewe utakuwa nani baadae. Mariam na Yusufu walijua wana mtoto mchanga, ila wale mamajusi waliona aliyezaliwa ni mfalme, (yuko wapi aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi). Mungu ndiye anapanga hatma za maisha ya watu, lakini shetani ni mharibifu ambaye anaweza kuharibu hatma njema, Yoh 10:10, kazi ya shetani ni kuua, kuchinja na kuharibu hivyo anaweza kufunika uhalisia wa maisha yako. Kama nyota ya Yesu ilionekana hivyo upo uwezekano wa kila mtu kuwana kiashiria cha maisha yake ambacho ndo kinampa mtu kibali cha kufikia hatma yake. Gwajima hafundishi nyota kusema kuwa watu waishi kwa kuongozwa na nyota na wanajimu wasoma falaki kama Biblia inavyokataza Isaya 47;13, kwa kifupi kuhusu nyota ndo na umesema anafundisha elimu ya wafu. Hiyo siyo kweli maana Mungu wetu si Mungu wa wafu bali walio hai. Yeye anafufua wafu mtu aliyekuwa amekufa akafufuliwa kuna ubaya gani Lwitiko? Na mch Gwajima si wa kwanza kufanya hivyo maana Eliya alifufua 1falme 17:17-22, Elisha alifufua 2falme 4:18-35, mifupa ya Elisha ilifufua 2Falme 13:20, Yesu alifufua binti yairo luka 8:49, Yesu alifufua kijana kwenye lango la naini Luka 7:11, Yesu alifufua Lazaro Yoh 11:38-44, imeagizwa hivyo kwenye biblia mathayo 10:8, pia kwa faida soma Yohana 14:12, ukisoma 1yohana 3:8b …kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi. Sasa swali kwako, unaamini kuwa watu wanachukuliwa msukule! Kama jibu ni ndiyo hiyo ni kazi ya nani? Sasa kuwarudisha kuna ubaya gani. Mi naamini anayechukia akiona kazi za shetani zinaharibika najua ni wa shetani. Naomba jengeni hoja kwenye mandiko tafadhali. Pia mtumishi Lwitiko umesema mnatetea Injili halisi, naamini injili halisi ni ile inayotangaza uhuru kwa waliofungwa, inayothibitishwa na uweza wa Mungu na si maneno yenye hekima za kibinadamu. Mungu wangu awabariki kwa Kristo Yesu.

 9. Gershoni, Mbona unanichekesha? tungekuwa tunawapoteza watu wachanga kiroho kama tungekuwa tunapotosha mafundisho ya Kristo au tunakwenda kinyume cha neno la kristo au kufanya kuizuia injili halisi ya Kristo. Daniel kutoa changamoto ya watu kumuhubiri Kristo kuliko elimu ya wafu au kuwarudisha wafu hapo kwa mtazamo wako tunawapotosha wachanga kiroho, ungeninambia tunawapotosha wachanga kiroho kama wewe ambao wamekaa kwenye elimu ya misukule ambayo Daniel anatakiwa ajibiwe kimaandiko zaidi. sio kiushabiki, halafu hayo mafundisho ya shetani kushikiria nyota ya mtu yanatoka wapi, uenda mtumishi Gershoni unaweza kufafanua elimu hii ambayo watu tusiokuwepo London hatukuweza kuipata vizuri kama post au mada kuu inavyoonyesha. tunamfuata Kristo Gersgoni, yeye aliye mtangulizi wetu,

 10. Bwana Yesu asifiwe, bwana Lwitiko umesema Daniel John ame raise maada inayohitaji mchanganuo wa kimaandiko, naomba uniambie kwanza wewe kama maneno ya Daniel yamekaa kimaandiko au naye anashabikia kupinga huduma ya ufufuo na uzima. Alisema angepewa ruhusa kumsahihisha mch. Gwajima angempa 0.001%, imeandikwa wapi? Hajasoma somo la Hermanutics, hilo somo lipo kitabu gani cha biblia? Yesu wameshawahi kumsikia, Roho wameshawahi kumsikia, Mungu wameshawahi kumsikia…… ‘twendeni ulaya kumtangaza Yesu’ uende ukafanye nini hali umesema wamesikia? Bwana Lwitiko na Daniel ni bora mkawaacha kondoo wa Mungu waingie zizini, kuliko kuwazuia kama mfanyavyo. Hiyo ni roho ya ufarisayo ambao Kristo alitoa ole nyingi juu yao. Mnategemea tutaingia mbinguni kwa kujadili fulani anakosea au fulani yuko sahihi? Kazi zako binafsi, jueni mnavyofanya mnapoteza wengi hasa wale walio wachanga kiroho. Daniel usimdharau mtumishi wa Mungu yeyote eti kwa kuwa wewe humkubali, wewe si Mungu, kama utaweza nitafute kwa 0655564445, tuwekane sawa zaidi.Mungu awabariki wote pia nami

 11. Ndugu stina, Daniel ame raise hoja ambayo inatakiwa iangaliwe katika kipimo cha maandiko ambayo ni neno la Mungu lakini wewe umeenda moja kwa moja kuangalia katika kipimo chako mwenyewe cha akili zako na utashi wako wa kishabiki inawezekana ni muumini wa Mchungaji Gwajima, hilo hatukatai na wala hatulibishanii ila ulitakiwa kumjibu Daniel kwa kuonyesha kimaandiko zaidi kile ambacho Daniel ameonyesha kuwa na shaka nacho, hivyo ndivyo tunavyojifunza lakini wewe umekwenda moja kwa moja kutoa duku duku lako la kishabiki, Daniel hajaonyesha kuwa concern na kufunguliwa kwa hilo kanisa huko London ila ameonyesha concern ya kimaandiko ya kile kinachofundishwa katika doctrine ya ” misukule” mimi nilitegemea utaweza kuja na hoja ambazo ziko kimaandiko badala ya kuja na ushabiki ulioutanguliza mbele kuliko neno la Mungu.

 12. Majeshi majeshi,yakowapi majeshi,yanapiga majeshi,yanauwa majeshi,ni majeshi ya nani?ni majeshi ya Bwana,songa mbele baba wanao tuko nawe.

 13. Ndugu Daniel. Kama wewe unayajua yote hayo, kwanini usiende huko London na ukawapa kile unadhani kinafaa. Acheni kusubiri wengine watende jambo nanyi ndo mjitokeze kukashifu. Fanya jambo tuone, usisubiri kupinga vile wengine wanatenda. Gwajima, songa mbele katika kulihubiri neno la Bwana….

 14. shalom! mimi sikuzote ni mdadisi, sipokei kitu kirahisi rahisi tu hivi bila conviction ya Roho Mtakatifu, hata hivyo sipingani na watumishi wa Mungu! lakini juu ya huyu Gwajima yuko juu sana kupita maelezo! namna ambavyo anayahusisha maandiko na maisha ya watu wa kawaida mimi binafsi sijaelewa hata kidogo. katika ile hotuba ya London kama ingekuwa ni kwa kumpa makisi ningempa 0.001% kwa sababu ambazo nazitoa katika hotuba yake na jinsi anavyoyatafsiri maandiko matakatifu.nadhani Mch Gwajima hajasoma somo la HERMANUTICS linalohusu kuyafasiri maandiko matakatifu? ameacha kabisa kuangalia mazingira ya uandishi wa NENO la Mungu na kulipeleka moja kwa moja kwenye APPLICATION! na hivyo alipo-inject Elimu ya Misukule kule London ilibidi wamsikillize kwa makini kwa sababu: KAMA NI YESU=WAMESHAWAHI KUMSIKIA, KAMA NI ROHO=WAMEWAHI KUMSIKIA, KAMA NI Mungu= wamewahi kumsikia? so JE HAWA MISUKULE NI AKINA NANI JAMANI? Nadhani wazungu walishangaa ikabidi watumie muda wao mrefu kumsikiliza mtanzania akiwapa Elimu Mpya ambayo hawaijui kabisa! wazungu wako tayari kumpa kiwanja cha kujenga hata kanisa kwa namna alivyowaendea kwa kuwa hawajui maana ya misukule, hivyo wanaona ni elimu mpya kwao! jamani tuamkeni katika hili! Twendeni Ulaya kumtangaza Yesu!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s