Naomba maoni ya wasomaji!

Bwana Yesu asifiwe, naomba kupata maoni ya wasomaji. Mimi nimeokoka na nampenda Yesu niko safari ya kwenda mbinguni. Mimi ni mbunge mtarajiwa wa Urambo Mashariki kwa mwaka 2015 kupitia chama cha upinzani (Chama Cha Vijana). Katika jimbo la wapiga kura wangu, zao kuu la biashara ni Tumbaku. Nawaza nitaandaaje Ilani yangu ya uchaguzi kwa ngazi ya jimbo bila kuhusisha tumbaku. Na nikiipigia debe tumbaku nitakuwa namtenda dhambi Mungu wangu. Sitaki kukosa mbingu kwa ajili ya jambo hili. Je ungekuwa wewe unahisi ungefanya nini 2015?

John Maganga

Advertisements

8 thoughts on “Naomba maoni ya wasomaji!

 1. Mungu akupe hekima na kukufanikisha suala hili. Hongera kuwa na mawazo ya kugombea

 2. Shalom,
  Mungu akubariki sana, kwa kuingia ktk ulingo wa siasa.Kwa kweli ni muhimu wawepo akina Danieli ktk vyombo vya kutetea wananchi.Ushauri wangu ni huu, pamoja na kufanya utafiti wa zao mbadala, pia ungeshiriki kulilima zao hilo (mbadala), huku ukiomba Mungu akutokee hapo, ili utakaposimama kueleza sera kuhusu zao hilo waone mfano halisi, maana 2015 ni kitambo.Pia uwe muwazi ktk chama chako usije ukajichanganya, kwa sababu ktk kampeni ninaona kila anaesimama hugusia mambo yanayozunguka eneo husika, km maji, elimu, afya,miundombinu , kilimo, sasa watakapotaja kilimo uwe tayari umeliweka wazi na kuwaelimisha watu wa chama chako( wanaosimama ‘madhabahuni” au jukwaani kusindikiza kampeni). Katika yoote, YESU ANAWEZA.

 3. Shalom. Kwanza Mungu akubariki kwa uamuzi wako wa kugombea Ubunge kwani tunahitaji wawakilishi wanaomjua Mungu na wenye hofu ya Mungu. Tumbaku sio zao pekee la kuinua uchumi. Waeleze wananchi wako madhara ya tumbaku. Hii itakusaidia usimkosee Mungu maana ubunge sio sababu ya kumkosea Mungu. Mungu wetu ni mwaminifu atakutetea ukiwa mwaminifu kwake atakupa Ubunge na zaidi ya vile unavyovifikiria.

 4. Naomba nikushauri kwasababu nasema kwa ujasiri kwani hata mimi niliacha kazi katika kiwanda fulani kinachotengeneza pombe baada ya kuokaka tu.Hivyo naomba uwe wakili mzuri wa Mungu kwani cheo cha ubunge kama ni mpango wa Mungu utakuwa mbunge lakini ukitaka kujipatia mwenyewe lazima utumie zao la tumbaku katika kampeni.Sema madhara ya tumbaku na muombe Mungu akupe jambo ambalo ukilitambulisha kwao watakuelewa .Ingawa si wote watakubali lakini Mungu akikubali hakuna wakukataa.
  asante

 5. SHALOM.
  KATIKA 2 Kor 3:16-19, Biblia iko wazi kabisa kwamba miili yetu ni mahekalu ya Roho Mtakatifu, na mtu akiharibu hekalu la Mungu uwe na hakika Mungu naye atamharibu. Kwa hiyo mimi nasema uvutaji wa sigara na kulima tumbaku ni DHAMBI. Wengi wanadhanieti kwa sababu kilimo cha tumbaku kinaingiza pesa nyingi kwenye pato la taifa basi Mungu hana shida, Ukweli ni kwamba Mungu habadilishwi na taratibu zetu. Kuwa muwazi, itakuwa baraka iliyoje kuwa na mbunge anayeweza kuwashauri wale anaowaongoza juu ya uhusiano wao na Mungu.

 6. …Simple!

  Mashirika yote adiilifu yenye kujali Utu yanapiga vita UVUTAJI WA TUMBAKU kama kistarehesheo (sijuwi kama ni kiswahili sanifu). Hata hapa Tanzania huwa kuna fununu zakuwepo kwa mikutano ambazo kama sijasahau hata Wizara ya Afya ya Tanzania huwa inahusika kuhusiana na kutoa Onyo juu ya Uvutaji wa Sigara kwa kuanisha matatizo yanayotokana na uvutaji huo. Ndiyo maana hata kwenye pakiti za sigara wameandika kabisa, tena kwa shinikizo la wizara ya Afya, kuwa UVUTAJI SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO! Maelezo hayo machache tayari yanaweka msingi wa mahali pa kuanzia.

  Sasa, kama Ningekuwa ni mimi: Ningeanza kwa kuwaambia watu kuwa uchaguzi wanaokwenda kuufanya unakwenda kubadilisha maisha yao kwa namna ambayo hawajawahi kuona tangu waanze kuchagua viongozi! Kwamba kingozi wanayekwenda kuchagua siyo tu atasaidiana nao kutatua matatizo ya kiuchumi bali anakwenda kuwawekea msingi mpya na sahihi wa kutatua matatizo hayo ka kubuni njia mbadala tofauti na ambazo wamekuwa wakifanya tangu enzi na enzi lakini umasikini uko pale pale.

  Pamoja na mambo mengi ambayo kama ningekuwa mimi ningesema, suala la Tumbaku ningeliwekea msisitizo mkubwa kuwa SIYO ZAO LINALOFAA kwa uchuki kwa kuwa lina madhara mangi yanayobakia baada ya zao hilo kuzalishwa. Suala la madhara ya kiafya ni moja lakini kuna suala la Uharibifu wa mazingira kutokana na miti mingi inayokatwa kwa ajili ya kukaushia zao hilo. Urambo ilikuwa ni moja ya maeneo yenye uoto mwingi wa asili, huku mvua na mahitaji mengine ya mali asili yakiwa yanapatikana kwa kutoshelevu. Lakini zao hilo limeleta madhara makubwa, huku kiwango cha ukuaji wa uchumi hakiendani na uzalishaji na kazi ngumu inayofanywa katika kuzalisha tumbaku.

  Ziko data nyingi za kuelezea jinsi nguvu kubwa sana inatumika kwa uzalishaji wa tumbaku lakini kipato ni kidogo na nchi/ardhi inabakia jangwa, huku akina mama na watoto wakiwa wanaathirika sana katika utafutaji wa kuni na mahitaji mengine yanayotegemea uoto wa asili. Mambo ni mengi sana ya kuwaelezea wanachi ili WACHUKIE KABISA zao la tumbaku.

  Baada ya hapo ndipo wanapaswa kuelezwa utaratibu mpya wa kufanya kilimo cha biashara. Kilimo kisichoathiri afya zao wala ardhi na mazingira haviathiriki. Kuna mazao mengi yanayoweza kulimwa kule ambayo yanafaa kwa chakula na biashara na faida yake ni nzuri. Hata kama faida yake ni kidogo lakini hakuna madhara mengine yanayozalishwa ambayo hulazimisha sehemu kubwa iliyotokana na faida ya tumbaku itumike katika kukabiliana na matatizo yaliyosababishwa na uzalishaji wa tumbaku.

  La muhimu tangu sasa fanya utafiti, au chukua data za kitafiti katika ofisi zinazohusika kuhusiana na mazao mbadala yenye faida na tija ambayo yanaweza kuzalishwa wilayani humo. Yako mengi tu mazuri na andaa mkakati wa namna ya kufikisha elimu hiyo kwa umma. You tell them kwa kukuchagua wewe wategemee maisha mapya yasiyo na jasho jingi, bali akili zaidi jasho kidogo lakini maisha yao yatakuwa bora!

  Uzalishaji wa tumbaku huchukua muda wa miezi karibu 10 hadi kuuza. Lakini kipato kinachopatikana kikigawanywa kwa muda uliotumika plus jasho linalotoka katika kuzalisha zao hilo utakuta faida ni ndogo mno!

  You tell’em ni wakati wa watu kuacha mzaha na kuzingatia kila kitu kinachoelekezwa iwe katika uchumi, afya, na mambo mengine. Hivyo kuwaambia watu “UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO” halafu bado unawahamasha KUVUTA huo ni mzaha, na Bible imekataa!

  Yako mengi sana ya kuandika kuhusiana kuacha kuzalisha zao hilo na kisha kuwa na mazao mbadala yenye manufaa zaidi kwao na kwa vizazi vijavyo maana ardhi itahifadhiwa kuliko sasa ambapo inazidi kuharibiwa!

  Kama umeona kuna la muhimu nimeandika na Ukihitaji zaidi kutoka kwangu usisite kuwasiliana nami.

  Kila la heri katika mkakati huo!

 7. mtumishi hongera kama unasikia wito wa siasa!sasa ninafikiri ni wakati mzuri wa kupima kiasi cha amani ndani yako juu ya swala kama hilo,kama ni suala la kimungu utajisikia amani nalo and you will find a starting,…..amen

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s