Kazi ya manabii ni ipi?

Jamani hawa manabii wa Taifa wanashindwa hata kutuambia kuwa kuna janga la mafuriko tujiandae…….? Agabo katika Matendo ya Mitume alilionya Kanisa kuhusu Njaa itakayoshukia Jerusalem? Unabii wao uko kwa lipi hasa? Kwa nini wasikubali kuitwa Wachungaji tukajua moja?

Orbi

100 thoughts on “Kazi ya manabii ni ipi?

 1. Hakuna jambo baya linaloweza kutukuta bila kuwapasha habari watu wake ambao ndio hao manabii… lakini tatizo kubwa manabii wengi sasa wanaona walozi, maagano ya mababu, madhabahu za kiganga na kulishwa vitu ndotoni tu… tofauti na nabii mmoja nimemshuhudia Arusha akioneshwa mambo ya nchi za mbali na yanatyokea, ya hapa nchini pia ametabiri na nilipofuatilia nikakuta yanatokea… watu kama hawa duniani lazima wawe duni, na sometimes wataitwa free massons pale wanapoinuliwa zaidi. Ila kwa majanga kama haya ni lazima Mungu awapashe watu wake. Tatizo siku hizi pia manabii geresha wapo kibaaaaooo… Kwahiyo mambo kama hayo kwao ni hadithi, labda wabahatishe.

 2. Ndugu Orbi,sijui kwa nini sikuiona hii section mapema.anyway,unabii wote kuhusu majanga,ulishatolewa toka enzi za manabii wa kale kama Isaya.
  Swali:Je unabii utolewe mara ngapi?
  Unajua,manabii hutoa unabii pale wanapotumwa kufanya hivyo na Yesu.si kila kitu wanaambiwa kusema.vilevile,si kila kitu kinachotokea maishani mwako Yesu anakutaarifu hata kama unatembea katika mapenzi yake.Yesu alipomruhusu shetani kumtesa Ayubu,je Ayubu alijua au aliambiwa?Lengo ilikuwa ni kupima imani ya Ayubu.Na hiyo ni kwa yule mtu wa Mungu.
  Majanga pia,hutokea kama adhabu kwa wale walio kinyume na Yesu.mfano,Sodom na Gomorrah.hawa waliadhibiwa.Na mara nyingi hata leo,majanga yatawapata walio kinyume na Yesu.
  Hapo zamani kabla ya Yesu kuwepo,unabii ulitolewa sana kupitia manabii hata leo hii unabii bado unatolewa.Tatizo la vizazi vya leo ni kwamba, watu hatuna interest kabisa na mambo ya Yesu.Tunajifanya kuwa busy sana hivyo,hatumtafuti Mungu.
  Wengine wanapuuzia na kusema eti ni wa uongo na nabii husika ni muongo kwakuwa,jambo husika halijatokea kwa muda ambao tunaufikiria sisi.Nabii Isaya alipotoa unabii kuhusu Yesu,ulichua muda mwingi kutimia.Ina maana,hata waliousikia huo unabii wake,hawakuwepo tena duniani.
  Manabii wa leo ni wa muhimu sana,tusiwalaumu.Wanachotoa kama unabii,lazima waambiwe kukitoa.Hawafanyi vitu kwa akili zao ila,kwa kuongozwa na roho.
  Hata hivyo ndugu Orbi,labda kama hujampokea Yesu.Maana,wote walio wa Yesu wataambiwa mapema kuhusu yale yaliyoko mbele yao.
  Ujumbe:tafuta kukaa sana katika roho ili roho wa Yesu aongoze maisha yako.Ili,roho(Yesu)aongee na wewe individually.Maana,imeandikwa pia,mzipime hizo roho(zinazotoa unabii).
  Utazipimaje kama huna roho wa Mungu?
  Na kama ndo hizo unategemea zikutaarifu kila kitu.Utaweza kuipinga ile roho ya upotoshaji?Au,utaamini manabii wote duniani?!.

 3. Ndugu zangu katika Kristo ,

  Shalom!

  Asante kwa comment yako ndg Mabinza, kwamba kuna angalau asilimia 25 ya furaha uliyoipata, ni jambo la kumshukuru Mungu. Hiyo huzuni uliyonayo inawakilisha makabiliano uliyonayo aidha dhidi ya Neno la Mungu, au Mafundisho yaliyo kinyume na Neno la Mungu. Basi usiwe mbali na Biblia yako ili uweze kuwa na fursa ya kuyakagua mambo yote humo ndipo uwe na uamuzi wa kujiunga na JESHI lipi; jeshi la Mungu (Ufu 19:14 “Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, …”) au jeshi la Ibilisi (Ufu 19:19 “Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi na majeshi yao, …”).

  Basi hali ndivyo ilivyo, usajili wa majeshi hayo unaendelea, unapokutana na KWELI ya Mungu haswa inapoonekana kuwa ni tofauti na kile unachokijua, jaribu kuchukua wasaa kidogo kulipima hilo Fundisho lako na Neno la Mungu. Uamuzi utakaoufanya uwe juu ya uelewa kamili wa jambo hilo. Kama hujalielewa tafuta msaada na uendelee kuupima katika Neno, ndipo uamue kujiunga na jeshi lolote kati ya hayo mawili. Wengi wetu tuliandikishwa katika jeshi la Nabii wa Uongo bila ya kujijua, kama ilivyokuwa kwa Sauli (mt. Paulo), lakini nasi kama Paulo, Injili inatupa fursa ya kuchagua tena; kuendelea na mifumo ya ibada zetu zilizo nje ya Mafundisho ya Mitume, yaani kuendelea na yule Nabii wa Uongo au kuyakana hayo na kulipokea Neno la Mungu (Yesu Kristo kuwa Bwana), yaani kurudi katika Fundisho la Mitume. Wasajili wa majeshi hayo hawako mbali nasi, wote wawili wako jirani sana, hata tunapolitafakari Neno, nasi tukalipima na kusanyiko letu na wapendwa wote tuliowazoea labda na nafasi yako katika kusanyiko, nawe unaona ukilikubali Neno utakuwa umejitenga nao, basi kwa hali hiyo ukaamua uendelee kidogo na kusanyiko lako huenda pastor akaliona hilo huko mbele likarekebishwa; UMEJIDANGANYA! Fursa ni moja tu, naye Roho Mt. huwepo kando yako kulishuhudia Neno lake, hivyo unapolikubali basi hukuandikisha katika hilo Jeshi lake na ukilikataa, Ibilisi naye yupo kukuandikisha katika jeshi lake! Pande ziko MBILI tu hakuna neutral.

  Kwa hiyo Injili kama inatoa ahadi ya kuinuliwa kwa nabii wa huduma ya kinabii, ambayo inahusisha kulirejesha Kanisa katika NJIA ya KWELI, ambayo ndiyo hiyo ya FUNDISHO la MITUME, ambalo kanisa kwa kiasi kikubwa sana limeondoka kutoka fundisho hilo, kwa ushahidi wa Biblia ; basi wewe ukisema au kufundisha kanisa kuwa HAKUNA tena nabii ajaye, ni dhahiri kwamba umenasa katika utando wa yule Nabii wa Uongo. Nao wafuasi wa kundi hilo iwapo hawataondoa uvivu na kuikabili kweli ya Biblia na kufanya uamuzi juu ya jitihada zao binafsi za kumpeleleza Mungu, basi bila tashwishwi yoyote ile watakuwa wamepotea kwa uvivu wao wenyewe!

  Manabii wa karama ya unabii ndani ya makusanyiko yetu madogo madogo wapo. Nayo huduma yao ni ile ya kuwakamilisha watakatifu katika kusanyiko lililo katika FUNDISHO la MITUME tu, na si katika makusanyiko mengine, haya yaliyo katika mafundisho yao wenyewe. Karama hiyo ya unabii ikijiinua katika kusanyiko la aina hiyo, basi hiyo hutokana na roho anayeliongoza kusanyiko hilo maana Roho Mt. daima hukuelekeza katika Neno la Mungu. Basi karama hiyo ya unabii ya kweli hulisafisha kusanyiko uchafu wote kama uasherati, uzinzi, fitina na mambo mengine maovu ya mafichoni nk. Pia hulitaarifu kanisa kadiri Mungu anachotaka kuwajuza na hata kuwasifia katika vita wanayoendelea nayo. Lakini haya makusanyiko mengine, lo, karama zimo ndani ya makusanyiko yao, sasa zichunguze kwaya zao, zimejaa uasherati na uzinzi, na ‘utakatifu’ ndio unakamilishwa kwao kwa jinsi hiyo!

  Manabii wa Huduma wa KWELI, hawa leo hii hawapo. Hawa wote unaowaona wakijisifia na kujitangaza, hawa wa hapa kwetu Tz na wa nchi nyinginezo kama akina T.B. Joshua na wengineo wengi tu, wote hawa ni Manabii wa Uongo. Wengi wao wana roho za utambuzi tu, lakini SIRI ya Mungu hawana, bali UPAKO wa UONGO wanao, ambao ndio unaotuingiza katika kuukubali uongo wao kuwa KWELI, ukichanganya na nguvu ya miujiza iliyoachiliwa juu yao, basi sote tulio wa mwilini hatuna namna ya kupona!

  Manabii wa Huduma wa KWELI, tuwatarajie ili Huduma hizo zitufaidie katika kutuleta katika wokovu kamili na si huu wokovu wa kuigiza. Biblia inatuelekeza kumtegemea nabii Eliya tena kuja kumalizia ile Huduma iliyofanywa kwa nusu na Yohana Mbatizaji kama inavyoonekana katika Luka 1:17 “ Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, …” Huduma hiyo aliifanya Yohana Mbatizaji alipowageuza mioyo ya ‘baba’, hao walikuwa ni mafarisayo na wengineo waliokuwa katika Torati wakigeuzwa sasa kuwaelekea watoto – Kristo na mitume wake. Nayo dunia nzima ilichukua uelekeo huo mpya wa Kristo kupitia Mitume wake. Ahadi ya Mungu iliyotolewa katika Malaki 4:5-6 “Angalieni, nitawapelekeeni Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, …”, inatuonesha kuwa kulingana na kazi iliyofanyika, ile nusu iliyobaki bado haijafanyika, ile ya ‘Kuigeuza mioyo ya watoto kuwaelekea baba zao’ ambao watoto wenyewe ndio sisi tuliozaliwa kwa Injili ya mitume, kama mtume Paulo anavyolishuhudia hilo anapotuambia wazi wazi kuwa “ametuzaa”, na sasa tumeiacha na kushikamana na mafundisho ya mashetani, basi hiyo Huduma ya Eliya ajaye tena, ndiyo itakayo igeuza mioyo yetu kutoka katika hii injili potofu na kuwageukia baba zetu mitume yaani kurudi katika Injili waliyotuhubiria. Nao urejesho huo ndio utakaotufungua macho yetu hata kumuona yule ASI na uongo wake wote aliotudanganya kwa miongo yote tuliyodhania tunamuabudu Mungu kumbe tunamuabudu IBILISI (…ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akajionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.”)!!

  Sasa uwepo wa Manabii hawa wa Uongo, na kuzagaa kwa Huduma yao, kwani kwa kiwango ilichojichimbia leo hii si rahisi kwa mtu kujua ni kusanyiko gani lina fundisha kweli ya Mungu maana kila kusanyiko linadai kuwa wao ndio wako sawa. yaani kama hapa Tz kwetu, kuna makusanyiko yaliyo katika mafundisho tofauti zaidi ya 5,000, na yote, kila mmoja anasema yeye ndiye yuko sahihi! Je, katika hali kama hii, haimpasi Mungu kuja kuamua? Naye ataliamuaje hilo? Yeye daima huamua kwa Neno lake. Nao uamuzi huwa ni Hukumu! Basi Neno lake lenye kuhukumu laja. Naye Mungu kama alivyoahidi kuwa hafanyi lolote bila kwanza kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake (Amo 3:7). Basi na tuutegemee ujio wa nabii atakaye kuja na Huduma ya Urejesho ili tupate kuwa sawa na Neno la Mungu na kumfanyia Mungu Ibada iliyo safi badala ya hizi ibada lukuki zilizojaa uharibifu. Hizi ibada zetu ni sawa kabisa na ile ibada ya Kaini. Ndio maana unaziona leo hii zinawatukuza watu badala ya Mungu, makundi yetu yanajitambulisha na maaskofu wao au manabii wao au mitume wao au madhehebu yao na si Kristo tena! Utawasikia, ah, siku hizi niko kwa nabii na mtume Lwembe! Basi kama jambo hili silo alilolikemea mt. Paulo, ni nini basi?

  Basi ndg yangu Mabinza na ndugu wote wengine, chukueni wasaa kidogo mlikague Neno la Mungu, mkiitazama na hali ya Kanisa ilivyo leo hii, kisha ninyi wenyewe muone iwapo mnapaswa mumuombe Mungu awaletee nabii leo hii ili kanisa lipate macho ya kuiona njia ya kweli au kama mmeridhika na hali hii iliyopo na mnaona mnaweza kujitegemea ninyi wenyewe kwa kujiongoza au kuongozwa na wachungaji wenu na mkaiona ile NJIA, basi Mungu katika Rehema yake, awapeni hayo kulingana na mioyo yenu. Jinyenyekezeni mnapoliendea Neno maana ndiye Mungu mwenyewe, jiwakilisheni mkiwa na mioyo mieupe mkiyaacha mafundisho yenu nje kama Musa alivyovua viatu vyake, Mungu atawasikiliza. Mkiingia na viatu vyenu, basi atawazawadia ile : “… nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.” (2The 2:11-12).

  Nawashukuruni nyote, nikiwasihi tuzidi kuombeana,
  Rehema ya Bwana itufunike!

 4. Ndg yangu Lwembe,leo umenifurahisha asilimia 25 tu,na hivyo robo tatu yote ni huzuni! kaka yangu,mara zote hupata furaha ninaposoma komenti zako, ambazo huwa na mafundisho yanibarikiyo sana,tafadhali changia kwa kirefu, je, ni kweli kwamba unabii na vyeo vya manabii, kwa sasa, HAKUNA? Maana nasikia ati YOHANA MMBATIZAJI alifunga Huduma hiyo? yaani hakuna Ishu kama hiyo tena?…sababu ni kwamba watu wanaweza kuomba moja kwa moja kwa Mungu, hivyo nabii wanini kuwepo pamanenti tena?! – ATI,KWAMBA HUYU HAPA NABII! Nitafurahi kusikia toka kwako mapema,lakini pia kwa yoyote mwenye ufahamu juu ya hilo. UPATE ZAIDI BARAKA ZA BWANA,KAKA LWEMBE!

 5. Wapendwa ndg Mabinza na dada Rosemary,

  Shalom!

  Tukiwa pamoja katika mjadala huu tunaoendelea nao katika kujifunza, nilipoisoma michango yenu, nimeona kuna jambo moja dogo tu ambalo tukiliweka vizuri yaweza kutusaidia sote katika kayaelekeza macho yetu ya kiroho mbele kidogo ya jambo hilo dogo ili twende sote katika hatua moja tunaposonga mbele.

  Nadhani sote kimsingi tunakubaliana kuwa manabii kama manabii, wapo, wa KWELI na wa UONGO. Uwepo wao wote huendana na Huduma wanayoitimiza kulingana na NGUVU iliyowaachilia! Kwa hiyo mjadala wa kujua iwapo leo hii kuna manabii au la, kimsingi unakuwa umevukwa kwa kule kujua kuwa wapo, maana hata matangazo yao yenyewe ya manabii hao hushuhudia kuwepo kwao. Hatua tuliyonayo sasa hivi ni kuwatazama hawa manabii, iwapo ni wa KWELI au ni wa UONGO? Kama ni wa kweli, je, Maandiko yanawathibitisha? Au je, Maandiko yanatupa ahadi ya kuletewa nabii yeyote katika kipindi hiki, na kama iko ahadi, huduma yake itakuwa ni nini? Na kama hatuna ahadi ya nabii, je, nini hatima yetu ilhali migawanyiko ni mingi sana yenye mafundisho tofauti tofauti na kila fundisho likidai kumwakilisha Kristo? Na mambo mengine yatakayo tuongoza kuufikia ule Wito wetu Mkuu!

  Mjadala umepamba moto,

  Nawatakieni nyote Furaha ya Bwana!

 6. Nikushukuru sana Dada yangu Rose,kusema kweli maneno mengi yalilazimika ili uelewe,hata hivyo pole kwa usumbufu ulio upata.Leo nitatumia mistari kadhaa itokayo katika Biblia takatifu na kwa maelezo mafupi,ili uelewe kwa kuipitia mwenyewe polepole.Umesema hivi “……..cheo au Title ni Dhamana, kwamaana hiyo Mtu huyo anatumika maalumu kwa na anawajibika kwa kazi hiyo tu” (Mwisho wa kunukuru) Dada, kwa maelezo yako niliyoyanukuu hapo juu, jibu lake ni NDIYO! Tunapojaliwa Neema ya kukilimiwa karama yoyote,karama hiyo huwa Dhamana maalumu kwa ajili ya Kanisa la Yesu Kristo, kwa maana nyingine ni TALANTA KWA ALIYEJALIWA KARAMA HIYO,Kwa kifupi talanta ni kama fedha,mtu aliweza kulipwa kwa Talanta au kupewa mtaji wa kibiashara kwa Talanta,utaweza kuona kuwa,ukipewa kipawa cha karama yoyote ni kwamba umepewa mtaji wa kufanyia biashara yenye faida! Utadumu na Talanta yako uliyopewa kwa kuitunza na kuifanyia kazi kama mwenyekukupa alivyoagiza, ukiipoteza tu hovyo au ukakaa nayo bila kazi iliyokusudiwa, kama Lugha ya vijana waleo wanasemavyo, itakuwa “IMEKULA KWAKO!” Kwa kifupi, ukipata Karama ya UNABII hiyo ni Talanta yako, utapaswa kuidumisha,itapsa pia uitumie kwa mjibu wa maelekezo ya mwenye kukupa! – kwa hiyo, Unabii ni cheo,unapaswa kukitumia ipasavyo,kwa kadri ya maagizo ya aliyekupa,na kipawa hicho huwa ni kazi yako ya KUDUMU,HADI UTAKAVYOELEKEZWA NA MWENYEKUKUPA VINGIMEVYO! – ujue utakuja kuitolea hesabu yake (CHEKI;math,25:20, na 2timo1:9) Tatizo watu kwa kutoujua wajibu wao huzijichimbia chini Talanta (KARAMA) zao,watajivuna nazo kana kwamba ni Mali ya jasho lao,watanyanyasa nazo weeee,hadi mwenyewe anawanyang’anya! – Na shetani akisha ona vile, huwaendea haraka na kuwapa karama za kwake,ndipo wenye macho na masikio ya kiroho, hugundua kuwa, wale si manabii wa kweli bali waongo,ingawa matukio wanafanya na kufanana na ya kweli-kama ilivyokuwa kwa wachawi wa Misri!. (cheki;kuto;7:10-12, mt;25:14-21,) Uliendelea pia kusema kuwa (nanukuu)”………..wakati karama ni kitu kitolewacho kwa Roho kupenda kwa kulifaidia kanisa,….”Jibu lake katika sentesi hiyo ni KWELI Roho hutoa karama kwa kupenda yeye mwenyewe,anafanya hivyo kwakuwa anatujua tulivyo Yeye huangalia Rohoni.Kama sikosei kwa sentesi yako kuwa “………kitolewacho kwa Roho kupenda…..” unamaanisha kuwa ,kwakuwa Roho hutoa karama kwa kupenda, basi huwapa watu ”KWA MATUMIZI YA HAPO HAPO TU basi!,yaani – kwa mahitaji ya muda huohuo tu,na hitaji hilo likiisha,basi, na upako huo hakuna tena,hadi siku nyingine! (nilivyo kuelewa mimi,kuwa una maana hiyo)” kama unamaana hiyo, Nakujibu kuwa SIYO! Kwa wakati wa Torati ilikuwa kama leo -tofauti yake tu ni kwamba wakati wa Torati mambo yote yalifanya kwa uwazi “WA KIMWILI” ili kuja kuikamilisha Injil kwa uwazi “WA KIROHO”, kwa sababu mpango ulikuwa,Yesu ndiye alipaswa kutukabidhi huyo Roho,ambaye ndiye mtoa karama,yaani ilipaswa Yesu aje kwanza,ndipo roho aje,kwa maana nyingine,Yeye Yesu, “ajibadili kuwa ROHO,abaki daima kwetu (cheki,math;28:20),ili alijenge kanisa lake,kwa kutoa hivyo vipawa mbali mbali (cheki,1kor; 7:7),viwe kama Zana au vfaa vya ujenzi wa hilo kanisa” (cheki, 1kor; 12:4) Wale wote watakaotumia karama hizo kwa manufaa yao (KUFANYA UCHAKACHUAJI), ingawa wamepewa wadumu navyo kwakuwa ni vyeo vyao – watajaribu kujitetea kuwa,Bwana aliwapa karama hizo,ukiwemo unabii,nao walitumika kwa kutoa unabii KWA JINA LA YESU!,iweje hawafai? Kwa andiko hilo ina thibitisha kuwa UNABII kwa wakati wa injili utakuwepo (cheki,math;7:22),”………wengi wataniambia siku ile,Bwana, Bwana, hatukufanya UNABII kwa jina lako,…….. (jina la Yesu)” Labda nisiseme maneno mengi sana niishie hapo kwa kusema tu kwamba,MANABII NA VYEO VYA MANABII VIPO HADI LEO! Ujue,watafika na vyeo vyao mbele ya hukumu,na Jaji Bwana Yesu Kristo, ataviona vyeo hivyo na kwamba bado wanavyo,lakini vipo kivingine,si kama alivyowakabidhi – kwa maana hiyo si manabii wake,walisha jifutisha kazi kwa ujinga,ni kweli ni manabii na walifanya hivyo kwa jina la Yesu,lakini kwakuwa waliacha kumsikiliza Boss wao (Yesu),wakatumia akili zao, sasa hapo Yesu bila kujali hapo mwanzo, walikuwa manabii,na kwamba walifanya kazi hiyo kwa jina hilo kuu la Yesu – Yesu hata yabishia maelezo yao kuwa kweli ni manabii,na walitoa unabii kwa jina lake,UNAONA? YESU HAJAKATAA,KUWA HAWAKUWA MANABII,NA KWA MAANA HIYO,WALIKUWA NA HUDUMA HIYO KWA MUDA WOTE,HADI WANAFIKA MBELE YA HUKUMU! INGEKUWA HUDUMA ILE WALIIPATA SI KWA PAMANENTI, WASINGEITOA KAMA SABABU YA UTETEZI WAO – WANAMWAMBIA YESU,KUWA WALIKUWA NA JUKUMU HILO MUDA WOTE! “Tulitoa unabii kwa jina lako” (hiyo ni sentesi inayoonyesha tendo endelevu) hata kama watafika na vyeo vyao hivyo,Yesu hatakuwa na lingine ila kuwakataa, kwa vile hawakufuata Itifaki ya kazi waliyopewa! (Yaani watakaokuwa wametumia madaraka ya VYEO vyao hovyo, Yesu, kwa mjibu wa msitali huo wa mathayo, 7:22 – atawatimulia mbali!) – Ndg yangu,Kama kunatashwishwi yoyote usiache kabisa kuuliza.Mpendwa Rose, Bwana Yesu Kristo Akutunze.

 7. Dada Rosemary,

  Shalom!

  Asante kwa maelezo uliyoyatoa.

  Mimi nadhani kuna kujichanganya kidogo katika michango inayoendelea. Suala la kuwatenganisha manabii wa cheo na manabii wa karama, maelezo yake yametolewa sana katika michango iliyotangulia. Huenda ndugu Mabinza hakuiona hiyo ndio maana naona hilo likirudi tena. Ushauri wangu kwa ndg Mabinza, ajaribu kuchukua wasaa kidogo kuipitia michango hiyo ili awe updated kwanza, ndipo aendelee.

  Mimi, katika jibu lako, nilitegemea utakuja na Andiko linalofunga ujio wa manabii (cheo). Lakini sijaliona hilo, naona maelezo yako kuhusu Yohana Mbatizaji kuwa ndiye nabii wa mwisho ni yale yale yaliyozoeleka ambayo yamejikita katika tafsiri za kiteolojia badala ya Neno la Mungu kama unavyodai. Nimekuonesha manabii wawili katika kitabu cha Ufunuo, sijaona jibu lako kuhusu hao, au kitabu cha Ufunuo si cha Agano Jipya?

  Kuhusu manabii (cheo), hawa hutambulika kwa Huduma. Wao huja na Upako wa Mungu ili kuyatimiza yale ambayo Mungu aliyaahidi kwa kipindi hicho. Maandiko yanayo muongelea Yohana Mbatizaji ndiyo hayo niliyoyarejea na Huduma aliyoifanya ndiyo hiyo hapo kama ilivyowekwa wazi katika Luka 1:17 “ Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, …” Sasa kuna haja gani kuongeza ambayo hayapo, kwa faida gani? Mimi nadhani ni vizuri kuyachunguza Maandiko kwa kituo bila jazba. Maana humo ndani kuna mambo mengi Mungu ameyafunga yasieleweke katika wakati fulani mpaka wakati alioukusudia mwenyewe.

  Jambo jingine ambalo ningependa nikuulize : Je, kulingana na hali ya kanisa ilivyo, yaani hizi tofauti za mafundisho zilizopo katika kila nyanja, Kristo akishuka leo hii, ni kundi gani atakalo linyakua? Waadventist, au Mormon au Mashahidi wa Yehova au TAG au EAGT au …?? Au wanaFellowship????
  Ndio maana Kristo anasema huyo Eliya atayarejeza yote, nayo yakiisha kurejezwa ndipo IMANI itakuwa MOJA badala ya hii vurugu iliyopo. Basi Roho ya Eliya Mungu anaitumia mara ngapi hilo ni lake yeye. Nao urejesho huo sio Injili mpya ni Injili ileile ya Mitume ambayo makundi yetu yameiacha.

  Ushauri wangu kwako dada Rosemary, ipitie tena Biblia yako polepole. Biblia inajitafsiri yenyewe. Mungu hanihitaji mimi Lwembe wala mtu yeyote yule kumtafsiria Neno lake. Yeye huichunguza mioyo yetu ili kuiona shauku tuliyonayo, naye huijibu hiyo na kutufunulia Maandiko yake ili tuwe na Uzima tele.

  Bwana na akupe kiu zaidi ya Neno lake!

 8. Shalom ndg Mabinza na Lwembe
  asante kwa majibu yenu mazuri, ila naomba nijibiwe kwa mujibu wa Neno nimeona maelezo mengi. naomba tu kujibu kuwa cheo au title ni dhamana na kwa maana hiyo ni kuwa mtu huyo anatumika maalumu kwa na anawajibika kwa kazi hiyo tu wakati karama ni kitu kitolewacho kwa Roho kupenda kwa kulifaidia kanisa, sio cheo kwa hiyo leo karama ya muujiza anayo mwalimu, mchungaji na hata mkristo yoyote mwenye huyo roho akipewa kwa kulifaidia kanisa. Naomba tu ufafanuzi wa hiyo mistari niliyoweka naona tunazunguka, hata hiyo Malaki 4 ni Yohana huyohuyo aliyekuwa akitabiriwa, Samahani sina Biblia ila ni Yesu pia alirudia hayo hayo maneno ….kuigeuza mioyo ya watoto kwa baba nk kwani naye alisema sijaja kuleta amani…na inaeleweka kuwa yeyoto aliyempokea Yesu wakati ule alikuwa anaonekana anaikosea Torati na hivyo kutengwa na sinagogi ambao ndio mababa

  napenda kufuta kauli ya kuwa mafundisho fulani ndio yamepelekea niandike hivi, ni uelewa wangu tu wa Neno na uzoefu wangu kwa baadhi ya wanaojiita manabii na mafundisho yao. Hivyo naomba majibu yetu tuweke udhehebu, mila na desturi pembeni na tutumie Neno kujadiliana. Asante na Mungu awabariki nyote

 9. BWANA YESU,ASIFIWE DADA ROSE,Nikushukuru sana kaka Lwembe kwa kuendela vizuri na Dada yetu Rose,kusema kweli hujabakiza kitu,tena kuna mambo mapya nimejifunza,Uendelee kubarikiwa kaka.Kwetu kuna msemo kwamba, ukikuta wanamchuna Ng’ombe usiondoke bila hata kipande cha kuchoma,maana ukifika nyumbani kwako ambako kuna mboga za majani,na ukajaribu kusema,ati nimechelewa kidogo,nilikuwa ninamsaidia Mabinza kuchuna,kachinja Ng’ombe pale kwake,WATAKUONA MWEHU! Kwakuwa, nimekukuta unachuna,basi nami nikate kidogo,kwa mjibu wa mila ya kwetu, cha kuchoma kama ifuatavyo;Labda nianzie na neno CHEO CHA UNABII – Labda tujiulize kuwa,neno CHEO lina maana gani? kwa tafri isiyo lasimi, cheo ni sifa inayotokana na kazi husika,kwa kifupi cheo si jina.kwa maana hiyo haiwezekani kuwa na kazi furani na pasiwepo mwenye cheo cha kazi hiyo – maana nisawa na kusema kazi furani kweli ipo.ila mfanyaji kazi hiyo hayupo! Sielewi kama inaingia Akilini mtu kaenda kutibiwa Hospital fulani,kamkuata mtu aitwaye Joh. Na huyo John, ndiyo kaajiriwa katika hospital ile kutibu wagonjwa,John akamwabia mgonjwa yule njoo nikutibu,naye kweli katibiwa na huyo john,….itashangaza kidogo, akisema nimetibiwa na JOHN mwala sijatibiwa na TABIBU! kwa tafsiri fupi mtu anaye fanya kazi ya kutabili cheo chake ni NABII,MTU AKISHINDA MBIO,CHEO CHAKE HUITWA MSHINDI,maana hayupo mshindi bila kushindana! Neno la Mungu linasema kutakuwepo na MANABII,na ikiwa neno ni lilelile halibadilki,sasa itakuwaje lijipinge?Yesu alisema, sikuja kuitangua torati,natorati tunakubali kuwa ni Neno la Mungu lisilo badilika,na hiyohiyo torati ndiyo inataja na kutambua manabii na vyeo vyao,unadhani kwanini injili itangue kuwepo kwa cheo cha unabii,ila ikubali kuwepo kwa manabii?! Maana kama sikosei, Dada Rose,amenukuu maandiko kadhaa yakikubali kuwa roho ya unabii katika Agano jipya itakuwepo,kwa maana hiyo anakubali kuwa watakuwepo manabii,ila nashindwa kujua anamaana gani,anaposema kwa sasa inatia shaka kuwepo watu wnajiita manabii,yaani wana vyeo vya manabii! Mimi binafsi, namshauli Dada Rose,ayasome na kuyaweka kwa wingi maneno ya Mungu,na kumruhusu Roho mtakatifu,ambaye ndiye mwalimu kwa unyenyekevu amfundishe. CHEO cha MANABII na Manabii WAKWELI WAPO.NA BOSS WAO NI ROHO MTAKATIFU! Kama ilivyo kuwa manabii wa kweli wapo,basi na wa uongo wapo! Neno la Mungu linasema, WATAKUWEPO MANABII WA UONGO,kama Neno limesema,kuna ujasiri gani wa kukubaliwa kwa kusema kuwa HAWATAKUWEPO? Kuwepo lazima wawepo.maadamu NENO linakili hivyo, sasa wawe wa uongo au wa kweli hiyo ni ishu nyingine.Nimalizie kwa kusema hivi,KAMA MANABII WA KWELI HAWATAKUWEPO,BASI NA ROHO MTAKATIFU AMBAYE NDIYE MUNGU BABA,NA NDIYE MUNGU MWANA(Yesu) HAYUPO! Kitu ambacho hakiwezekani,maana tunaamini na kujua kuwa Mungu yupo……Biblia inasema, Mpumbavu husema moyoni mwake kuwa Mungu hayupo!……na sehemu nyingine imeandikwa, Mungu hatafanya jambo lolote bila kuwajulisha watumishi wake MANABII, Biblia inaendelea kusema,……siku za mwisho nitaimimina Roho yangu……watatabili (Mtabili ni watabili) Bwana atujalie Neema yake.ili tuelewe mapenzi yake.

 10. Dada Rosemary,

  Asante kwa maoni na rejea nzuri za Maandiko katika hayo uliyoyaeleza. Ninaamini kwamba maelezo yote uliyoyatoa msingi wake ni Biblia na si kanuni au dogma. Ni katika mtazamo huo ambapo nina mambo mawili matatu juu ya mambo hayo kulingana na mada kama ulivyoyaweka.

  Katika maelezo yako katika post hizi mbili za mwisho, umeainisha kwa uhakika kabisa, kwa kuyanukuu Maandiko, ya kwamba hakuna tena nabii ajaye baada ya Yohana Mbatizaji. Katika jambo hili, mimi nadhani dada yangu hujayatazama Maandiko vizuri au umechukua ushawishi wa mafundisho ya waalimu ambao katika kujikweza kwao, wamekuwa wakiwafundisha watu kukoma huko kwa manabii ili kuzifanya huduma zao kuwa ndizo kikomo cha mambo yote yamhusuyo Mungu kama alivyowakabidhi wao.

  Kwanza Biblia, haswa Agano Jipya, ambalo ndilo tunalolizungumzia, halijafunga ujio wa manabii baada ya Yohana Mbatizaji. Manabii bado wanayo nafasi katika Programu ya Mungu kama alivyoitayarisha na kwa manufaa yaliyokusudiwa. Kwa mfano, kuna manabii wawili ambao wanatajwa katika kitabu cha Ufunuo 11:3-6 “Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini …” Basi iwapo hakuna tena manabii baada ya Yohana Mbatizaji, Je, Andiko hili tutalifanyaje? Tukizikubali tafsiri zinazo tuambia kuwa hakuna manabii, maana yake ni kwamba ufahamu wetu wa kiroho utakuwa umefungwa. Kwa hiyo hata akija huyo nabii tutamkataa kama walivyomkataa Kristo huko nyuma kwa tafsiri kama hizi, jambo ambalo litatutia hasara! Kristo anasema twapotea kwa kuwa hatuyajui Maandiko wala uweza wa Mungu (Mt 22:29).

  Nikiyarejea maelezo yako, katika kuainisha kazi ya nabii (cheo), umesema kuwa huyu huweza kubadili muelekeo wa kanisa, nanukuu: “… nabii alikuwa na sauti au tuseme ni uamuzi wa mwisho na hivyo alikuwa na uwezo wa kubadili muelekeo wa kanisa kabisa mfano Yohana kuwaambia watu watubu na wabatizwe ilikuwa ni injili mpya na tofauti kabisa na mfumo wao wa makuhani wa kuwatakasa kupitia dhabihu za kuteketezwa.” Hili ni jambo la kweli, ambalo kimsingi, ndilo linalowafanya hawa wanaojiita manabii wa leo, kwa mwenye ufahamu huu, awajue kuwa ni manabii wa uongo.

  Sasa, nabii anapokuja huja na Neno la Bwana, yaani, “BWANA ASEMA!” Nalo Neno hilo ndilo lenye nguvu ya kuligeuza kanisa mwelekeo, likiwatoa kutoka njia ya mauti linakokwenda bila kujijua, na kuwarudisha katika njia ya wokovu waliyoiacha kwa kudanganywa. Udanganyifu unapoliteka kanisa na kuliongoza kuelekea upotevuni, ndipo hitaji la nabii (cheo) huhitajika. Kumbuka, Mungu hajawahi kuliacha kanisa lake utupu, si la Agano la Kale (ambalo lilikuwa la mwilini, lilikuwa nao wale manabii wa Karama – wana wa manabii, makuhani nk); wala kanisa la Agano Jipya – ambalo ni la kiroho, humo tunaziona karama za Roho Mtakatifu nyingi tu kama ulivyoziorodhesha, zikiwa zimewekwa ndani ya kanisa kwa ajili ya kuliongoza katika mapenzi ya Mungu ambayo ni Neno lake.

  Lakini kanisa, ambalo ni mfano wa mwanamke, ndani yake kuna udhaifu ambao ibilisi huutumia kama alivyofanya kwa Hawa mama yetu. Kanisa linapo venture bila kuongozwa na Neno, Ibilisi hulikamata kwa urahisi na kuliingiza kwenye program yake ya uharibifu. Sasa, jambo la kusikitisha ni ile hali ya kudanganywa linayokuwamo kanisa pasi kujijua. Kanisa hilo huendelea katika udanganyifu likiyashika mafundisho ya uongo na kujitoa dhabihu katika ibada za jinsi hiyo likiamini kuwa liko katika NJIA ya KWELI! Naye Mungu akiwa ni mwenye kuyajua yote, alikwisha litayarishia jinsi ya urejesho ambavyo humleta nabii ili kuikamilisha kazi hiyo.

  Kwa hiyo, tunapolitazama kanisa leo hii katika ujumla wake, tukiwa ni wale tulioiamini hii injili ambayo dada yangu Rosemary anaihubiri, ya kwamba hakuna hitaji la nabii (cheo) katika siku yetu ya leo maana Roho Mtakatifu anahudumu katika makusanyiko yetu; jambo hilo linatuhakikishia kuwa kanisa liko imara na katika NJIA ya KWELI kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo kanisa hilo ni ‘barua inayosomwa’ na watu wote, kwa UTAKATIFU lilionao! Kwa upeo mdogo wa kuwaza nilio nao, hata hii mada itakuwa imepotea njia tu, maana inajadili jambo lililo kinyume kabisa na tabia na matendo ya kanisa hilo lililo katika utakatifu, maana mada hii inalihusu kanisa lililo katika mkanganyiko! Tusiishi katika nchi ya kufikirika huku nchi HALISI ikiwapo. INJILI si HADITHI ni HALISI!!!

  Mada hii tunayoijadili ndiyo inayotoa taswira halisi ya kanisa, kwamba limefika katika umbali usioeleweka. Leo tunawapigia kelele manabii na mitume ambao nadhani hawazidi hata mia moja kwa idadi. Hao ni wale waliojitangaza hadharani kuwa wao ni manabii. Hawa ni individuals ambao wamejisimamisha hapo wenyewe na kupiga yowe ya kuwaita watu waje watabiriwe mambo yao na kuvunjiwa laana nk. Lakini liko kundi jingine kubwa zaidi la manabii wa jinsi hiyo hiyo ambao wanaendesha jambo hilo hilo katika mifumo maalumu, yaani systems. Mifumo hii ni madhehebu. Haya kwa Tz yanavuka elfu tano kwa idadi. Hiyo ina maana hizo ni jinsi 5,000 za mitazamo tofauti ya Injili. Kama utafika katika njia panda hiyo, mbele yako kutakuwa na barabara hizo 5,000 zikikuitia katika njia zao kila moja ikikuhakikishia kuwa yenyewe ndiyo njia ya KWELI itakayo kufikisha uzimani! Hiyo ndiyo hali halisi. Makundi yote haya, kila mmoja anakiri kumuwakilisha Kristo. Mwishowe waumini ndani ya madhehebu hayo, katika kukabiliana na mapungufu yaliyomo humo ndani ya makusanyiko yao, haswa haya yasiyo ya Kipentekoste, wamejikusanya na kutengeneza kundi jingine, ambalo ni interdenominational wanaojiita ‘Fellowship’. Hawa wamegundua udhaifu wa madhehebu yao, kwa hiyo wao hujitenga katika nyakati maalumu ili kufanya ibada ambayo wanaamini ndiyo inayokufikisha Uzimani, kwani wao hutangaza kuwa ‘dhehebu halikufikishi mbinguni’ licha ya kwamba bado wako humohumo katika madhehebu hayo hayo ambayo wanasema hayakufikishi mbinguni; Je, kuna unafiki unaozidi huu wa wanafaragha???

  Yeyote anayedai kuwa anayo ‘Bwana Asema’ huyo ni nabii. Nayo madhehebu hayakuanzishwa kwa kuimba pambio, bali kwa ‘Bwana Asema’ iliyojikita katika tafsiri ya Neno la Mungu katika namna ya ufunuo wa jambo hilo. Basi leo unaposema kanisa linaongozwa na Roho Mtakatifu katika kiwango lilichomo cha kusimika mashoga, hilo laonesha mapungufu makubwa kwa uongozi huo hata kudhihirisha kuwa kuna mahali tulipomsikitisha Roho Mtakatifu kwa kuikataa kweli, akajiondokea zake, “Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.” (2The 2:11-12). Unaweza kuwaza kuwa mimi si dhalimu; bali chochote kilicho kinyume na Neno la Mungu ni dhalimu! Basi ni vizuri kuyachunguza mafundisho yetu ili kuona kama yanawakilisha ile kweli ya Mungu. Hebu litazame kanisa letu, leo hii madhehebu yetu mengi yanatuweka katika utayari wa kumpokea Bwana wetu Yesu Kristo, kama alivyoahidi kuja kutuchukua, yaani kutunyakua. Sote tunamsubiri Bwana nje ya utaratibu! Tunapelekwa tu kama mazuzu na Biblia zetu tumezibeba mitaani hata watu wakituona wanasema, “…eh siku hizi Lwembe hutaki utani na Ibilisi, naona unatembea na kipande cha Nondo tayari kumponda kichwa!” Maskini mimi, kumbe ibilisi mwenyewe ndiye aliyenibebesha hiyo Nondo akijua kabisa kuwa simjui, naye ananitafutisha mijusi badala yake! Maandiko yanasema siku hiyo, “… haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akajionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” (2The 2:3-4). Jamani tuzichunguze hizi roho zinazo kaa ndani ya hekalu la Mungu (miili yetu) zinatuabudisha visivyo. Kanisa lingeipokea kweli lingekuwa katika ufahamu huo. Unamuuliza askofu mkuu au mtume na nabii, hivi huyu mtu wa kuasi ni nani? Anakuambia, huyo ni Yuda Iskariote, wako wengi sana kanisani! Hapo anakuelekeza kwa wanaompinga!

  Nimekuonesha mapungufu hayo machache ya kanisa na pia Ahadi waliyo nayo Kanisa, ili uweze kupima mwenyewe iwapo vurugu hii tuliyomo, je, tunahitaji Mungu atuletee nabii ili atutoe katika hili dimbwi la matope, au tuendelee kupakana matope machoni?

  Sasa, macho yenye matope si rahisi kuona vizuri. Sioni jinsi gani mtu aliyejifunga katika mafundisho yanayoikataa KWELI, atakavyoweza kuyaona yanayohusiana na KWELI hiyo. Basi hata tunapo uzungumzia ujio wa Eliya nabii ili kuja kuikamilisha ile nusu ya Andiko la Malaki 4: 6, kule kuigeuza mioyo ya watoto iwageukie baba zao; tukiainisha kabisa kwamba hili kanisa lililopo juu ya nchi, Mungu akiliacha liendelee katika mafundisho haya ya uongo HAKUNA atakaye OKOKA. Hili kanisa lililopoteza muelekeo, baba yake wa Imani ni mitume, ndio waliolizaa kiroho. Nayo huduma hiyo ya kinabii ndiyo inayoweza kupambana na ‘mtu huyo wa kuasi’. Basi unaposema ujio wa Eliya nabii ulikamilika katika huduma ya Yohana Mbatizaji, ulipaswa utueleze hao waliokuwa wakigeuzwa ni akina nani, hao baba (ni nani) walio wageukia watoto (ni nani) ; na hao watoto (ni nani) waliowageukia baba zao ni nani. Na hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na kuogofya ilikuwa lini maana leo ni miaka zaidi ya 2000 toka Yohana Mbatizaji aje, na hali ya kanisa ni mbaya kuliko wakati wowote ule, maana leo mashoga wanahudumu ndani ya kanisa, ndoa za jinsia moja zinaenea kwa kasi kubwa, kanisa likiwa katika mambo haya, halafu linangojea kunyakuliwa na vichekesho! Ndio maana Mungu anatuahidi urejesho wa Neno lake la kweli ili lituongoze na si injili hizi zisizo na mwelekeo wowote ule wa kueleweka.

  Tunamngojea huyo, Mungu ametuahidi kumleta basi atamleta. Naye atakapokuja, kama kawaida atakuja katika nguvu za Eliya azikusanye injili zote za uongo zilizozagaa, hadi kijito cha Kishoni na kuzichinja zote kwa Upanga wa Neno la Bwana! (1Fal 18:40).

  Rehema ya Bwana itufunike sote!

 11. Ndugu Kinyau Haggai,

  Shalom!

  Ninakushukuru kwa fellowship ambayo tumekuwa nayo pamoja na ndugu wengine tulioungana nao katika kuijadili mada hii, hususan ndugu yangu Orbi, ambaye ndiye aliyetuletea mada hii kama alivyosukumwa na Roho wa Bwana. Ninaamini kumekuwa na mapungufu ya hapa na pale hata ndugu wengine wakaona jambo tunalolifanya, yaani katika jinsi tunavyolijadili, wakatuchukulia kama ni waasi au renegades, jambo ambalo si kweli. Ninaamini tumelijadili Neno katika wakati wote, huenda ni makali ya hilo Neno ndiyo yaliyowastua, maana hayajazoeleka kwa wengi. Basi niwasihi wote walioingia woga, wasiwe “Waoga Jasiri”, maana hilo huwafanya wawe majasiri wa kuogopa kulichunguza Neno, jambo ambalo laweza kuwadumaza.

  Basi ndugu yangu Haggai, kimsingi nimekuelewa vizuri sana katika yote uliyoyasema. Ni sawa kabisa! Hata ile presentation tuliyokuwa tunatofautiana, naona sasa umeileta vyema katika maana kamili ya matumizi ya Jina la Bwana Yesu Kristo, ingawa nimeona mkoroganyo kidogo tu, nami ninalimalizia jambo hilo vizuri na kuyakamilisha uliyoyasema ili na wasomaji wengine wanaolifutilia jambo hili waweze kunufaika, aidha kiuelewa au kama litazalisha maswali, basi wajue waulize kipi. Iwapo umeisoma post ya ndugu Otieno Dullo ya tarehe 19/01/2012, unaweza kuona ninachokisema.

  Hebu na tulitazame tena jambo hilo, ninanukuu kutoka post yako ya mwisho: “Utakumbuka kwamba nilisema wazi kwamba Jina YESU ndilo Jina u-Baba wa Mungu, ndilo pia Jina la Mungu Mwana na ndilo pia Jina la Mungu Roho Mtakatifu. Ingekuwa ni Hesabu tungesema, BABA= MWANA= ROHO MTAKATIFU= (jina) YESU, (angalia sijaweka alama ya kujumlisha kwa sababu ukiweka alama ya kujumlisha itaonekana kama vile ni vitu vitatu tofauti, wakati ni kitu hicho hicho kimoja). Kwa hiyo mtu anapotaja Mungu Baba maana yake ametaja Jina YESU, au anaposema Mungu Mwana maana yake ni Jina YESU, vivyo hivyo kwa Mungu Roho Mtakatifu. Kwa maana hiyo mtu akisema ‘kwa Jina la Yesu’ maana yake ameshataja Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kwa pamoja ndani ya Jina hilo. Sasa inakuwaje mtu mwingine anaposema ‘kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu’ anaonekana kama vile ametaja majina matatu tofauti?”

  Kama nimekuelewa vizuri, kwa maelezo haya uliyoyatoa, katika maana ya kile kifungu cha Mathayo 28:19-20, fumbo hili la ‘Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”, nawe naona unaunga mkono jinsi lilivyo fumbuka kwa mitume baada ya kujazwa Roho Mtakatifu, kuwa JINA hilo ni YESU; kama unavyo liweka wazi katika urahisi kwa mtu yeyote mwenye nia ya kujifunza kulielewa, ingawa inahitaji ujasiri kuweza kuliamini hilo. Hesabu uliyoiweka ni sahihi kabisa kadiri ya Maandiko yalivyo jifunua katika jambo hili: BABA= MWANA= ROHO MTAKATIFU= (jina) YESU.

  Basi, kwa ule mfano ulioutoa wa Mhe Mrema, ndio unao lifunga jambo hili katika kutuleta kwenye uelewa sahihi, nanukuu: “Hata katika hali ya kidunia mtu anaweza kuwa na cheo zaidi ya kimoja, kama ilivyokuwa kwa Mhe. Augustine Lyatonga Mrema (Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani), lakini jina lake linabaki kuwa hilo hilo moja. Wakati huo, mtu akisema ‘Augustine Lyatonga Mrema’, na mwingine akasema ‘Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani’, siamini kama watu hawa wangekuwa wanazungumzia watu wawili tofauti!” Hili ni kweli, hao si watu wawili bali ni mtu mmoja! Katika mantiki hii, kimaelezo na kiuelewa, basi, mathalani, tumealikwa harusini, mwalikaji ametuambia kundi la watu, Jamani mkifika getini tajeni code ambayo ni jina la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani, mtaruhusiwa kuingia ukumbini. Je, ukifika katika lango hilo, nao walinzi wakakwambia tupe code, sina shaka ukisema eti, ‘Jina la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani’, bila kuchelewa utajikuta umebebwa juu juu na kutupwa huko barabarani na suti suti zako! Hilo linadhihirisha kuwa wewe hukukusudiwa katika waalikwa ndio maana hata jina hulijui au mambo yenyewe hayakuhusu umeyarukia tu, yaani wewe ni ‘gate crasher’! Basi, ikiwa code inayolifungua lango la UFALME ndio huo ubatizo kwa JINA LA BWANA YESU KRISTO, ni vizuri tukafanya hima kuuendea huo nasi tupate kuwemo katika ule ufufuo wa Watakatifu unao tukusanya kwa ajili ya kunyakuliwa. Huu ubatizo tulioupitia, huu wa ‘Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu’ ni ukariri wa maelezo ya ile code tu si code yenyewe kwa hiyo lango halifunguki! Ubatizo huu ulituingiza madhehebuni mwetu na utatubakiza humo kusiko na ufufuo!!!

  Hilo ndilo lililonifanya niseme wanaoutimiza ubatizo kwa “Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”, hao ni dhahiri kuwa hawajaelewa kinachoagizwa maana hawajajengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, kwa hiyo kwao si rahisi kuelewa. Basi wanachokifanya ni kumimic Maandiko bila kuwa na context yake. Hao ndio wale wenye mfano wa utauwa (hili linakufanya ubaki mpagani!).

  Jambo jingine lililomchanganya ndg Otieno (ingawa yeye kasema mimi ndiye niliyemchanganya), ni pale uliposema, “(angalia sijaweka alama ya kujumlisha kwa sababu ukiweka alama ya kujumlisha ITAONEKANA KAMA VILE NI VITU VITATU TOFAUTI, WAKATI NI KITU HICHO HICHO KIMOJA).” Nadhani hili ndilo lililomchanganya zaidi, maana mimi, ili nisitoke nje ya mada, nilipozungumzia Jina la Yesu katika uwiano wa ile Mat 28:19-20, nilisema kuwa hizo nafsi tatu zimeamua kutumia jina moja na nikanukuu Maandiko yanayoelekeza hivyo. Sasa kwa conclusion hii uliyoileta, hebu ilinganishe na tafsiri ya UTATU MTAKATIFU ndipo unaweza kumuelewa Otieno anachokishangaa, maana ‘nadharia’ nzima ya UTATU umeivunja!

  Tafsiri ya neno TRINITY kulingana na The Concise Oxford Dictionary ni: “Union of three Persons (Father, Son, Holy Spirit) in one Godhead.” Hiyo ni Dictionary. Kuna wakati nilikuwa na shauku ya kumjua Mungu vizuri, haswa UTATU. Wengi niliowauliza kuhusu hilo, kila mtu alikuwa na jibu lake. Baadaye nilifanikiwa kuongea na wanatheolojia ndipo nikapata tafsiri sahihi ya jambo hilo ambayo inaoana na hiyo iliyomo katika kamusi/dictionary. Nayo tafsiri hiyo kama ilivyo katika anga za kidini ni: “Mungu mmoja mwenye nafsi tatu dhahiri zinazojitegemea tena zenye mamlaka sawa. Nafsi hizo tatu ni 1. Baba 2. Mwana 3. Roho Mtakatifu Baba ni Mungu na Mwana ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu na hawa Watatu si jinsi tatu za Nafsi Moja (mtu mmoja ) bali ni Nafsi Tatu dhahiri (yaani watu watatu) zikiwapo hapo katika ushirikiano wa dhati baina yao.”

  Ndipo katika ufafanuzi wa kujitegemea na udhahiri wa Nafsi hizo Tatu wao wameweka wazi udhahiri wa hali hiyo kama hivi:- “Baba si mwana , wala si Roho Mtakatifu naye Mwana si Baba wala si Roho Mtakatifu; pia Roho Mtakatifu si Baba wala si Mwana.” Yaani hawa ni ‘Three distinctive personalities’, bali ni Mungu mmoja!

  Kwa hiyo ndugu Haggai au mpendwa yeyote yule aliye na ufahamu au ufunuo wa jambo hili la UTATU MTAKATIFU, basi atusaidie ili atuondoe kutoka katika mkanganyiko huu tuliomo pamoja na ndugu wengine kama akina Otieno. Mimi kimsingi nimeshindwa kuliendea hilo, maana kadiri nilivyojaribu kulitafuta katika Biblia sikuliona humo. Mwishoni nilitaka kufika katika uamuzi kuwa hilo lawezekana kuwa ndiyo yale yaliyo katika zile EXTRA BIBLICAL REVELATIONS , nikimkumbuka ndugu yangu Orbi, lakini pia nikakukumbuka ndugu yangu Haggai, nikaona ni bora nikusubiri kwanza wewe, maana huenda kule kutokuliona kwangu ikawa ni kutokana zile tofauti za Biblia tena, basi ndugu zangu tusichoke katika kulitafakari Neno la Mungu. Mungu akitujalia tukamaliza safari vizuri, basi tutakaa na Hilo Neno milele, basi tukijizoeza mapema kulipenda, itatufaidia sana.

  Bwana na atufunike kwa Mbawa zake!

 12. Mpendwa Lwembe,
  asante, kwa majibu yako,Niko safarini ndani ya nchi, Nimepata wasaa mdogo kupitia hapa kwenye internet cafe link ipo slow sana,kumbe Mimi nimeokoka na nimetimiza haki yote sawasawa na walimu walionifundisha imani..Kwa jumla nachunguza sana maandiko,Nikipata kibali nitapitia vizuri hii tafakari yako.ninakushukuu unapoandika kwa kiwango cha wale watoto wachanga wa Bwana ili nao wapate ufahamu.Nina mengi ya kusema nanyi ktk hii tafakari,nimesoma kwa haraka nikipata huo wakati nitasema nawe/nanyi ndugu zangu ktk Bwana

  Bwana atuzidishie neema na amani ile izidiyo.

  Amen

 13. Shalom ndg Mabinza
  nashukuru kwamba hata umepata muda wa kupitia maoni yangu naomba nikujibu kufuatana na maswali yako
  1)- kulingana na maelezo yako,wewe unajuaje, Nabii na huduma za kinabii zilikomea mwisho kwa Yohana yupi, mbatizaji?
  Naomba rejea maelezo yangu, nabii wa agano la kale alikuwa ni cheo na alitumwa na Mungu maalumu kwa ajili ya kazi hiyo, alikuwa ni kiungo kwa Mungu na wanadamu maana kulikuwa hamna njia nyingine, ilikuwa ndio sauti pekee ya Mungu, waisraeli walipaswa kwenda kwa mfano Samweli na aliwaulizia kwa Mungu wafanyeje mfano vitani, njaa nk
  nabii alikuwa na sauti au tuseme ni uamuzi wa mwisho na hivyo alikuwa na uwezo wa kubadili muelekeo wa kanisa kabisa mfano Yohana kuwaambia watu watubu na wabatizwe ilikuwa ni injili mpya na tofauti kabisa na mfumo wao wa makuhani wa kuwatakasa kupitia dhabihu za kuteketezwa. alikuwa anawaanda watu kwa ujio wa Yesu na utakaso kupitia damu ya Yesu na sio tena damu za wanyama…
  Marko 1:3-4
  Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
  Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.
  Mathayo 11:10-15
  Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako. Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja. Mwenye masikio, na asikie.
  Marko 9:11-13
  Wakamwuliza, wakisema, Mbona waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza upya yote; lakini, pamoja na haya, ameandikiwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharauliwa? Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa.
  Yohana mb alikuwa ndiye nabii aliyekuja kwa Roho ya Eliya na kubadili mwelekeo mzima wa injili ya toba…

  2)-Kwa hiyo, hakuna manabii tena kwakuwa watu wanaweza kuwasiliana na MUNGU moja kwa moja?
  naomba rudia tena maelezo yangu unabii kama sehemu ya kanisa upo ila sio cheo cha nabii, maana Roho mt anamgawia yoyote kwa kufaidiana sio tena mpakwa mafuta tu, ni kwa yeyote kwa kufaidiana….sio kuleta mageuzi au mabadiliko makubwa kama wale manabii waliokuwa wanateuliwa maalumu kwa kazi maalumu kama kiuongo na sauti pekee ya Mungu
  1Korintho 12:4-14
  Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.
  Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
  Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
  Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
  Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.
  Matendo 1:8
  Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
  Matendo 2;17-18
  Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
  Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.
  Ndugu yangu hii inaonyesha ni tofauti na ilivyokuwa kwa manabii wote waliotangulia Yohana, basi hawa wote kama wanaweza kutabiri na wawe manabii na wenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa injili itakuwaje? si ni machafuko!
  kazi ya manabii ktk agano jipya ilikuwa ni ndogo kama kwa Agabo, kuonyeshwa njaa, maafa nk ili kanisa lijiandae ili liweze kuwafaidia waadhirika, utaona ni wa vipindi maalumu kwa kufaidiana, kuujenga mwili wa Kristo na si kubadili mwelekeo kama ilivyo kwa hawa…na hiki ndicho ndg Orbi nadhani alichouliza, uwezo wa karama ya unabii ktk kanisa kwenye mambo kama haya….kule Nigeria kuna TB Joshua ndiyo ana maono na utabiri hata kutafsiri, je naye tayari tuseme ni Eliya? na hawa wa Tanzania je? au Mungu yuko vipandevipande kila nchi ina Mungu wake anayetuma manabii kila leo?
  Binafsi ninatambua sana uwepo wa karama hii na ninaposema kuomba kutafaa nina maana kuwa karibu na Mungu karama hujidhihirisha zaidi, nadhani wengi wetu mmeisha kuwa ktk kambi au maombi maalumu jinsi udhihirisho wa karama na nabii mbalimbali unavyokuwa dhahiri kuliko ktk hali zingine zozote
  Matendo 11:27-30
  Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio.
  Matendo 13:1-2
  Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

  3)Unamaana kuwa maombi yanatosha -sana tu- hivyo hakuna haja ya Huduma za kinabii na vyeo vya manabii?
  kwenye swali namba nimejibu hapo, uwepo wa Mungu utatoa udhihirisho wa karama mbalimbali ndani ya kanisa ikiwemo hiyo ya unabii,
  tatizo watu wanataka kuwa wapendavyo na wapewe unabii hata kwa vitu ambavyo Mungu anaweza kusema nasi moja kwa moja au kupitia kanisa kwa kufaidiana miongoni mwetu, sasa hapa ndio wanapotokeza manabii wa uwongo au wenye karama kuitumia isivyo….

  4)- au je,unakubali au unakata pia kuwepo kwa Roho mtakatifu?
  nadhani toka mwanzo nimetaja unabii kama cheo na kiungo pekee kwa Mungu vimekoma kutokana na ujio wa Roho mt. hapa ndio naona tunashindwa kuelewana unabii ni karama na si cheo maana Yesu mwenyewe alitamka hivyo (rejea hapo juu). Ninatambua na ninawaheshimu sawa na watumishi wengine wote wenye karama hii na nimefaidika sana kwa nabii zao mbalimbali isipokuwa ninawakataa wanaokuja na cheo cha unabii chenye lengo na nia ya kuleta mabadiliko ktk Injili ya Yesu Kristo mfano kubadili baadhi ya vitu ktk Biblia, kujipa vyeo vya manabii waliokwisha kuja au kujiita ndio Yesu mwenyewe! Labda utashangaa kwa nini? naomba tu angalia huo mlolongo wa manabii ktk agano jipya na uone role au kazi yao ktk uelekeo wa Injili…. hakuna ispokuwa kama tu huduma nyingine ktk kuujenga mwili wa Kristo. Hii ni tofauti na Musa na torati, Yohana na Injili ya ubatizo wa toba, Au mtume Paulo na injili kwa mataifa…

  Ndugu ninashukuru sana kwa muda wako kusoma maelezo yangu na uchanga wangu kwani ktk kutoa niliyonayo ninajifunza kwa kusahihishwa na kuelekezana, Mungu awabariki na kuzidi kutujenga ktk umoja wa Kristo.

 14. Mpendwa John Haule,

  Kama ulivyotutaka tutafakari, nami tafakari yangu juu ya mambo hayo uliyoyaleta, ninaileta katika jicho la ubatizo kulingana na hicho kuwa kigezo kimojawapo nilichokiweka katika kuwatambua manabii wa uongo. Basi unapokuja katika suala la kujazwa Roho Mtakatifu na Ubatizo wa Moto na Kunena kwa Lugha na ishara nyinginezo, mambo haya ndiyo yanayotuacha njia panda wengi wetu hata tunaishia ku compromise Neno la Mungu.

  Kwanza, kuhusu habari ya Petro na watu wa mataifa (Kornelio). Petro alikuwa ni Myahudi katika mila na tabia. Wayahudi walikuwa ni watu waliokuwa wakiongozwa na Torati katika maisha yao. Wao walikuwa ni watu waliotengwa na Mungu kwa shughuli maalumu, hata wakawa hawajichanganyi na makabila mengine. Kwa hiyo, linapokuja suala la mmataifa Kornelio, hili lilimhusu Mungu zaidi kwani ndiye aliyekuwa akiwasiliana naye na si Petro myahudi.

  Tunachokiona hapa ni Mungu akimtayarisha Petro (ule mwili wa Kristo), aende akamhudumie Kornelio ili kumuingiza katika Programu yake ya Wokovu apate kuwa salama. Kwani Mungu akiisha panga jambo huwa halivunji wala kuigeuka program aliyoiweka, ndio maana licha ya sadaka za Kornelio kupokelewa, bado asinge stahili wokovu mpaka awe amepitishwa katika njia hiyo ya wokovu. Nayo njia hiyo alikuwa amekwisha kuiweka tayari na kuwakabidhi akina Petro : “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Ukisoma Mungu alivyomtayarisha Petro kwa ajili ya huduma hiyo ya Kornelio, utaona alianza naye kwa kumpa maono ya kuchinja mnyama aliye najisi kwa mafundisho ya Torati. Na mwishowe akafikishwa kwa Kornelio, Mungu akajithibitisha katika jambo hilo kwa kuwafanyia kama Maandiko yanavyojionesha. Hayakuishia hapo, kwani Mungu angekuwa amelikiuka Neno lake, ndipo katika kuitimiza Haki yote, tunawaona Kornelio na nyumba yake wakibatizwa. Tena, mtume Petro hakuwa ametayarishwa kwa huduma ya watu wa mataifa bali mtume Paulo. Ndio maana Mungu, ili kumleta Petro katika kiwango cha kumhudumia mmataifa, ilimbidi afanye jambo hilo katika jinsi hiyo ambayo ushuhuda wake tunauona katika Mdo 11:14-15 kama ulivyokinukuu, “Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo. Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu”. Nao Israeli (Wayahudi) kwa ushuhuda huo, wakafahamu kuwa mataifa nao Nuru imewazukia!

  Kwa hiyo mfano huu wa Kornelio hauuondoi umuhimu wa ubatizo tukijitegemeza katika ubatizo wa Roho Mtakatifu na kwa moto, tukimtegemea Mungu atufanyie hayo kwa sababu tu hatutaki kufuata jambo fulani kadiri Mungu alivyotuwekea hapo nasi tumeamua kuzifuata TAFSIRI ZETU za jambo hilo.

  Ubatizo wa Roho Mtakatifu, anayekufanyia ni Mungu mwenyewe. Hakuna yeyote mwingine awezaye kukufanyia jambo hilo! Hili liko mikononi mwa Mungu, kwa maana ni TAJI ya utii na uaminifu wako kwa Neno lake, yaani Injili kama ilivyohubiriwa na Mitume. Injili iliyohubiriwa na Mitume ndiyo inayobeba Ahadi hiyo, hauwezi kuyapata hayo nje ya Injili hiyo. Mitume walipewa mamlaka ya kufunga na kufungua. Sasa iwapo Mungu katika kuyajua yote; kuwa watakuwepo wabishi huko mbele, wajeuri, wasio na adabu, watakaowadhalilisha watumishi wake, basi akawatega kwa Neno hilohilo ili wapate kuanguka. Akakiweka hicho kifungu cha Mathayo 28:19-20, akijua amewapa yale mamlaka tayari, na akijua watayatumia wapi. Kwa hiyo, Petro kwa MAMLAKA aliyopewa, anafungua lango la kuingilia katika UFALME wa Mungu katika siku ile ya Pentekoste, kuwa kuanzia siku hiyo MLANGO wa kuingilia ndio huo, yaani: Unatubu, halafu Unabatizwa (maji mengi) kwa jina la Bwana Yesu Kristo. Hapo ndipo unapata Ondoleo la Dhambi, ukiisha litimiza hilo, kuonesha Utii wako kwa Neno lake, basi unakuwa na Haki ya kumgojea Mungu naye atimize sehemu yake kama alivyo ahidi. Jambo ambalo hulitimiza. Ukijidanganya na njia za mkato, utaishia kupata ubatizo wa ‘ROHO MTAKAKITU’. Nawe ukiisha jazwa na Roho huyo Mtakakitu, maisha yako yote utakuwa unakimbizana na mitume na manabii ukizikimbilia na kuzisubiri ahadi zao za utajirisho na mambo mengine mengi wanayoyachomoza kila kukicha kuhakikisha kuwa hutakaa usikie INJILI ya kweli tena. Yaani Roho Mtakakitu huiingiza roho yako kifungoni!

  Unajua, Biblia inatufunza kuzipima ROHO, maana ndizo zinazo hudumu. Kwa upande wa ROHO MTAKATIFU, yeye ndiye Mwandishi wa Biblia. Basi yeye ni dira au compass. Nalo Neno ni ile Nyota ya Magharibi. Unajua nyota nyingine zote huhama hama na dunia, lakini ile North Star, yenyewe haihami ndiyo maana yaweza kukuongoza katika safari yako na ukafika ilimradi UNAIJUA. Manahodha wa meli na marubani huitegemea sana hiyo kuwaongoza, maana ukiwa katikati ya bahari au juu angani, hakuna mlima wala bonde la kulirejea ili liwe ishara ya kukuonesha mahali ulipo, basi dira ndiyo tegemeo lao, nayo ile Nyota ya magharibi ikiwa imetulia katika sehemu yake kwa uaminifu, basi wao huimaliza safari yao vizuri. Naye Roho Mtakatifu akiwa ndiye ile dira, nalo Neno likiwa ndiyo hiyo Nyota ya Magharibi, basi Roho Mtakatifu hutuongoza kwenye hilo Neno wakati wote! Ukiona ROHO uliyenaye anakuongoza kulitilia shaka au kulikataa Neno la Mungu (ooh, huyu Petro naye, au oh, Paulo alikuwa anachukia wanawake, nk) basi jua huyo ni ROHO MTAKAKITU. Huyu, hiyo ndiyo kazi yake, kupindisha Neno la Mungu. Huyu pia huigiza mambo yote ya Roho Mtakatifu, isipokuwa yeye huishia mwilini.

  Basi ndugu yangu John Haule, Ubatizo wa Roho Mtakatifu, mtu huupata iwapo atakaa chini ya mafundisho ya mitume. Mungu anawajibika katika hilo tu, ndio maana anasema “Asiyeamini atahukumiwa”. Basi asiyeamini nini, injili ya dhehebu fulani, au fellowship au karismatic, au nabii na mtume fulani? Ambaye hataamini walicho kihubiri mitume, huyo ataangukia katika mkono wa Mungu wa Hukumu, hata awe mwaminifu vipi kwa hiyo ‘injili nyingine’ inayohubiriwa, hiyo ambayo mtume Paulo anasema na ALAANIWE huyo anayeihubiri, je ukisha jiunganisha na yule aliyelaaniwa, itakuwaje kwako?

  Ukisoma katika kitabu cha Ezekiel 36:26-27 utaona jinsi ya Programu ya Mungu inavyofanya kazi, tokea Mungu anakuita mpaka anakupa Roho Mtakatifu. Kuna hatua tatu anazokupitisha tokea siku unapoisikia Injili.
  Hatua ya Kwanza: Kwa imani (unapoipokea ile Injili), Mungu hukuhesabia Haki. Yaani Mungu anautoa ule moyo mgumu wa jiwe ule uliokuwa nao zamani ambao Neno la Mungu lisingeweza kupata nafasi ya kukaa humo, naye hukupa badala yake MOYO WA NYAMA .
  Hatua ya Pili: Mungu hukutakasa kwa Neno lake. Utakaso huo ni pale Mungu anapokupa ROHO MPYA. Yaani matamanio mapya. Zamani usingekuwa na muda wa kupoteza kusoma mambo kama haya ya dini, au kwenda kwenye mkutano wa Injili, zamani usingeweza hata kusema ‘Bwana Yesu asifiwe’, lakini leo bila ya aibu unapaza sauti kabisa nk. Sasa katika hatua hii ya pili ndipo shetani ameweka mtego wake. Hapa tunapokuwa tumepewa Roho Mpya maisha yetu hubadilika sana, furaha yetu huwa kubwa hata ungeweza kutuona tukiruka ruka na kulia kwa furaha na mambo hayo yenye kumtukuza Mungu! Tuwapo katika hatua hii, ndipo ibilisi akauingiza ule Uongo na kutuhakikishia kuwa huyo Ni ROHO MTAKATIFU, akatufundisha na Kunena kwa Lugha, akafanikiwa kututoa katika ile njia ya Kweli! Katika hatua hii hata vipawa hutenda kazi (kwanza vipawa vyenyewe havina majuto), kwa hiyo katika mkoroganyo huo, wa furaha inayoambatana na Moyo Mpya na kujitokeza kwa vipawa, hayo huufunga uelewa wetu na huwa ni vigumu kusikiliza chochote nje ya hayo! Kwa hiyo makusanyiko yetu mengi yamekwamia katika hatua ya pili yakiamini kuwa yamejazwa Roho Mtakatifu kumbe sivyo, bali yamepewa Roho Mpya tu! Hiyo ndiyo hatua aliyofika Yuda Iskariote pia. Kama ni vipawa, naye anavijua! Lakini Ibilisi ilibidi amtumie katika hatua hiyo kabla hajafika katika hatua ya Tatu ambayo asingeweza kumtumia tena maana angekuwa amekwisha tiwa Muhuri, yaani amepokea ubatizo wa Roho Mtakatifu nao moto unaoambatana nao usingemsaza kitu Ibilisi ndio maana akakimbia nae mapema!!!

  Hatua ya Tatu: Mungu hukubatiza kwa Roho Mtakatifu, yaani hukupa ROHO WAKE. Huko ndiko kule kujazwa ROHO MTAKATIFU. Basi ukiisha kujazwa na huyo, yeye hukaa katikati ya ule MOYO wa NYAMA uliowekewa, na ile ROHO MPYA uliyopewa, basi Huyo Roho Wake hukaa katikati na kuvimiliki vyote naye huyaendesha maisha yako mapya hata ukawa chumvi. Kristo huonekana katika maisha yako. Roho wake hukufunika hata huushinda ulimwengu. Leo wamekufanyia fitina hata wamekuondoa katika nafasi ya Ushemasi, badala ya kujifungia chumbani kwako na kumuomba Mungu ashushe Moto uwararuwe wale wanafiki, au alifungilie mbali lile kanisa, siendi tena huko! Hapana, hufanyi hivyo; bali unaibeba ile mizigo ya shutuma za uongo hadi kilima cha Golgota, pale Kalvari, nawe unaitua ile mizigo pale, na kuwaombea Amani ya Bwana iwafunike!

  Kuhusu swali lako la pili, ni kwamba mitume walikuwa wanafunzi wa Yohana Mbatizaji. Kwa hiyo walibatizwa ubatizo wa Yohana. Walipokuwa tayari walimfuata Kristo, huko waliendelea kutoa huduma hiyo ya kubatiza. Baada ya ubatizo huo wao waliipokea ile ahadi ya Mungu iliyokuja kwa Neno la Yohana kuwa Yeye ajaye nyuma yake atawabatiza kwa moto kama ilivyokuwa siku ya Pentekoste.

  Kuhusu ubatizo kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, mitume hawakubatizwa hivyo wala wao mitume hawakuwahi kumbatiza mtu yeyote kwa jinsi hiyo na wala hakuna mtu yeyote yule katika Biblia, aliyewahi kubatizwa hivyo! Huu ni ubatizo unaofanywa na makundi yetu tuliokwamia katika ile hatua ya pili, ambao ubatizo huu, hutuingiza katika madhehebu yetu tu. Yaani kiulinganishi tungeweza kusema, katika hali tuliyomo, tunaweza kuufananisha na ule wa Yohana Mbatizaji, maana nasi ubatizo huo ulituingiza madhehebuni kwetu ambako tumetambulishwa kwa Kristo. Kwa hiyo nasi tunapokiri Kumpokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi Wetu, tunapaswa kulishuhudia jambo hilo kwa kulikubali Neno lake kama linavyo tufunulia kuwa tunakamilka kwa ONDOLEO la DHAMBI, basi nasi tuuendee huo ubatizo wa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili tuungane na wenzetu waliotutangulia kama wale aliowakuta mtume Paulo katika Mdo19:3-5 “Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema,… Waliposikia haya wakabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu.” Paulo aliwakuta hawa katika furaha ya Moyo wa Nyama na Roho Mpya, ukijichanganya ni rahisi sana kudhania ni Roho Mtakatifu mpaka uwe naye ndipo atakuonesha zile tofauti. Kanisa linapaswa kuwa humble kama hao tunao waona hapo, tukiendekeza kumjeuria Mungu, inasikitisha sana, maana wengi wetu, hawa manabii waliojaa kwenye sura ya nchi wametufunza vibaya mpaka tunamuona Mungu kama Babu yetu, na wakati mwingine tunamgeuza houseboy atuletee hiki, na kutufanyia kila kitu, mpaka mwisho wake tunatake Yeye ndiye atusikilize namna tunayoitaka na atubariki kwa jina la maombi!!

  Kwa kweli, Kanisa linapaswa kuchagua leo hii, litaongozwa na nani, Injili ya Mitume au Tafsiri za Kidhehebu?

  Mbarikiwe!

 15. Rosemary,uendelee kubarikiwa.naomba usione usmbufu. Dada, ili tuweze kusaidiana,naomba kujua yafuatayo:- 1)- kulingana na maelezo yako,wewe unajuaje, Nabii na huduma za kinabii zilikomea mwisho kwa Yohana yupi, mbatizaji? 2)-Kwa hiyo, hakuna manabii tena kwakuwa watu wanaweza kuwasiliana na MUNGU moja kwa moja? 3)-Unamaana kuwa maombi yanatosha -sana tu- hivyo hakuna haja ya Huduma za kinabii na vyeo vya manabii? na 4)- au je,unakubali au unakata pia kuwepo kwa Roho mtakatifu?Nifafurahi kupata majibu ya maulizo hayo kwa uchache au kwa kirefu kadri uwezavyo – ili tuone kwa pamoja inakuwaje,na usiogope kumkwaza mtu,maana tupo kujifunza. kumbuko sisi ni ndugu Dada Rose.

 16. Hapa kuna pumba na ngano, Mungu atusaidie kuchambua maana kazi ipo kwa watumishi wa Mungu. Wengine wanabugia tu.

 17. Shalom shalom!
  naona mjadala unapamba moto, kwa kweli hili suala la manabii lina utata mwingi…samahani kama nitawakwaza wengine ila ndani ya moyo wangu na ufahamu wangu wa neno huwa sina imani na kinachoitwa cheo cha nabii ktk agano jipya sijui ni kutokana na wengi niliokutana nao kuwa na huduma zenye utata kulingana na neno na hivyo kwangu hayo ndio matunda anayosema ndugu John Paul.
  Kwa ufahamu wangu mimi (naomba kusahihishwa kulingana na Neno)
  !. manabii waliishia na Yohane mbatizaji (huyu sio tu alitabirii ujio wa Yesu bali aliwaweka watu tayari kwa ajili ya ujio wake)
  Baada ya Yesu kuja, tunaambiwa uwezo wake ulipaswa kupungua hadi kwisha na toka hapo hakuna nabii aliyetabiriwa kuja tena ktk Biblia ….”maana huyu ndiye Eliya ajaye…..Eliya ameishakuja hamkumwamini….namtuma mjumbe wangu atakayetangulia kwa roho ya Eliya kunitengenezea njia….” au yupo mwingine?
  2. Cheo cha nabii kiliishia hapa (tangu Yohana ufalme wa Mungu utaingiwa kwa nguvu (Roho Mt) na wale wenye nguvu ndio watakaouteka….. hapa nilijua anamaanisha unabii umeishia hapa nami kwa kuangalia kazi zao kama alivyotaja Anthony kama kiungo kati ya Mungu na wanadamu iliishia hapa, kuanzia hapa ni kuwa Roho Mt anakuwa ndani ya waumini wote kutuwezesha kuwasiliana na Mungu moja kwa moja.
  3. Kuna karama ya unabii: Sikatai kuwa kulingana na karama kila mmoja aliyopewa kuna unabii kama karama na si cheo …”.lakini kila mmoja apewa karama kwa kufaidiana, mwingine unabii, neno la maarifa, matendo ya miujiza nk ” hivyo kwangu mimi cheo hiki baada ya kuwa na Roho Mt kwa kila amwaminiye Yesu sioni kazi yake, isipokuwa ninatambua karama hii kuwepo kwa watu kwa kipindi au muda muafaka kwa kufaidiana,
  4. Utawatambua kwa matunda yao…. matunda ya huduma hizi ninaona kuwa sio mema: kunakutabiri na kupindisha neno kwingi kulingana na nabii anavyoona……kuna vitisho na kutiishana kwingi bila kutaka kuhojiwa wala kushauriwa….na kuna kujiinua kwingi hadi kuchukua utukufu aliopaswa kupewa Mungu kupitia Bwana wetu Yesu Kristo aliyetuokoa, kwao watu wanafata kutabiriwa: nani mwizi wake, mbaya wake, mke mtarajiwa nk na wala hawahubiriwi neno wamrudie Mungu….
  samahani ila experience yangu na hawa watu sio nzuri kwa kweli.
  najua nitawakwaza wengi ila naomba tu kusema tumeishapewa kila mtu nguvu kupitia Roho mt, miongoni mwetu ndio kuna hao wenye hizo karama za unabii, lakini tukumbuke hata sisi tukiomba Mungu atatuonyesha yale anayopenda tujue mfano wenza wa maisha, ktk huduma, ktk biashara. atatuonyesha yajayo ktk kazi zetu, ktk familia zetu lakini zaidi atatupa nguvu ya kustahimili hata yale ambayo hajatuonyesha na yanatusumbua…”neema yangu yakutosha… niwapo dhaifu ndipo uwezo wake hutimilika zaidi….” ….” nao wakiwa ktk kuomba siku ya tatu Bwana alisema nao mnitengee Barnaba na Sauli kwa ile kazi….”
  Inatupasa kila mmoja au kama kanisa kuwa karibu na Mungu hivyo tu tutaweza kuongea nae, tutaweza kuisikia sauti yake, tutaweza kujua mapenzi yake…..
  Hivyo ombi langu mie ni kuwa ndg alipouliza wenye karama ya unabii hawakuliona hilo sio kosa nadhani alimaanisha uwezo wa kanisa kuongea au kusikia sauti ya Mungu, je hili linamaanisha nini? alitaka kujua miongoni mwa wenzetu wenye karama hii, Mungu anasema nini ktk hili tukio kubwa….
  Mungu wetu wa amani atuwezeshe kujifunza kupitia neno lake.

 18. Ndg zangu,mimi nipo pamoja nanyi nyote,nimesoma hitimisho la ndg kinyau nikaona kuwa uko pamoja nami karibu kwa mambo yote,ila labda kwa lile la ……”KWA JINA LA BABA NA LA MWANA LA ROHO MTAKATIFU…” Kuwa ni la KIPAGANI…,Mimi kwa upande wangu nilivyoelewa (si mjibii Lwembe) ni kwamda Neno au sentesi kama ilivyonenwa na Bwana Yesu Kristo, na au kama inavyosomeka ..NI SAHIHI,yaani hapo ndivyo lilivyo kwa kutamkika na kwa maana yake.Lakini jambo huwa jema au baya kwa MATUMIZI YAKE,ikumbukwe kuwa si jambo la kutilia shaka kuwa agizo hilo ni la Bwana Yesu Kristo mwenyewe – Wakabatizwe kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu,…hapo anawaagiza Mitume wakafanye sawa na alivyosema, na kama tu watu tunaoamini Neno la MUNGU kuwa ni la kweli, nakama pia tunaamini kuwa tupo chini ya mafundisho yaliyojengwa na YESU mwenyewe kupitia Mitume wake. Basi ni wazi kuwa walivyobatiza mitume ndiyo tafsiri sahihi ya agizo hilo la Yesu. paulo ktk 1kor.13:9-10,anasema upo wakati kila jambo litaeleweka wazi…watu watakapo taka sana karama za Rohoni,…..soma pia 1kor.14:10-12.Kama namuelewa vizuri Lwembe CK, NENO au sentesi au tamko au agizo hilo la Yesu,halina tatizo NENO kama neno SI UPAGANI, BALI JINSI WATU WALIVYOLITUMIA,Neno linasema watu wataacha mafundisho na maagizo ya MUNGU (MAFUNDISHO KUPITIA MITUME WAKE AKIWEMO PAULO) na kufuata mafundisho yaliyo ya wanadamu!!!……..Neno ni lilelile lakini shetani amelipanda “kivyake!” Au nakosea kaka Lwembe? nikosoe tu ndg yangu kama hukuwa na maana hiyo ili nami nikuele zaidi, MMZIDI KUBARIKIWA NA BWANA!

 19. Wapendwa!

  Ninaingia katika mjadala huu kwa mara ya kwanza, baada ya kuvutiwa na mijadala yenyewe. Kwanza nianze kwa kusema Mungu awbariki katika Maisha yenu na awajalie afya njema mnapoondelea kusoma kwa bidii neno la Mungu ili kuweza kumfahamu vyema, nia ikiwa kila mmoja siku YESU akirudi atupaie nafasi katika makao aliyoenda kuandaa (Yn 14)

  Lakini pamoja na hayo Mr. Lwembe amenichanganya kidogo. Hivi tukisema BWANA YESU KRISTO, tuna maana ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu? Labda mi sikuwa naelewa vizuri…., lakini pamoja na hayo nafahamu neno KRISTO ambalo kwa lugha ya kiingereza ni CHRIST ni neno la kiyunani lenye maana ya MESIAH na tafsiri yake ni MPAKWA MAFUTA WA BWANA…..,

  Na mpakwa mafuta wa Bwana ni jina alilopewa mtu aliyechaguiliwa na Mungu kwa ajili ya utawala au kazi maalumu…, eg. Mfalme Daudi, Sauli na wengineo. hapa nashindwa kuelewa ni kwa vipi KRISTO imaanishe Roho Mtakatifu? kama ndivyo basi nafsi tatu za Mungu TRINITY ni nadharia ngumu. Kama jina la Mwana ni YESU, na jina la Roho ni Mtakatifu ni KRISTO, jina la Baba ni lipi? Maana tunajifunza katika utatu mtakatifu wana “share” jina MUNGU, logic ya kawaida Baba ana jina lake. Naomba nisaidiwe!

 20. Ndugu Lwembe,

  Nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri na wa kina kuhusu kile kifungu namba 11. Mungu akubariki sana. Kimsingi umeeleza na kueleweka vizuri sana, na karibu sehemu kubwa tunakubaliana (yaani wewe na mimi) labda tofauti ni presentation ya hicho ninachokielewa na unachokielewa kutoka kwenye maandiko.

  Utakumbuka kwamba nilisema wazi kwamba Jina YESU ndilo Jina u-Baba wa Mungu, ndilo pia Jina la Mungu Mwana na ndilo pia Jina la Mungu Roho Mtakatifu. Ingekuwa ni Hesabu tungesema,
  BABA= MWANA= ROHO MTAKATIFU= (jina) YESU, (angalia sijaweka alama ya kujumlisha kwa sababu ukiweka alama ya kujumlisha itaonekana kama vile ni vitu vitatu tofauti, wakati ni kitu hicho hicho kimoja). Kwa hiyo mtu anapotaja Mungu Baba maana yake ametaja Jina YESU, au anaposema Mungu Mwana maana yake ni Jina YESU, vivyo hivyo kwa Mungu Roho Mtakatifu. Kwa maana hiyo mtu akisema ‘kwa Jina la Yesu’ maana yake ameshataja Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kwa pamoja ndani ya Jina hilo. Sasa inakuwaje mtu mwingine anaposema ‘kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu’ anaonekana kama vile ametaja majina matatu tofauti? (kufuatana na post yako ya tar. 16/1/2012 inavyosema;
  “…….kama hizo nafsi tatu zingekuwa zinajitegemea katika majina, basi kifungu hicho kingesomeka hivi: “ Jina LA Baba na LA Mwana na LA Roho Mtakatifu” bali sivyo! Nao ubatizo wa vyeo haujaagizwa katika Biblia, ni UPAGANI!)”

  Hicho ndicho kilichonipelekea mimi kukuliza kwamba ni kweli kwa biblia zingine kuandika mstari huo kwa kuweka kiambishi ‘la’ ni za kipagani? Au zina maana kwamba ufanyike ubatizo kwa kutumia vyeo vya Mungu? Au mtu akisema, ‘kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu’ atakuwa na maana ya kutaja majina matatu tofauti?

  Hata katika hali ya kidunia mtu anaweza kuwa na cheo zaidi ya kimoja, kama ilivyokuwa kwa Mhe. Augustine Lyatonga Mrema (Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani), lakini jina lake linabaki kuwa hilo hilo moja. Wakati huo, mtu akisema ‘Augustine Lyatonga Mrema’, na mwingine akasema ‘Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani’, siamini kama watu hawa wangekuwa wanazungumzia watu wawili tofauti! Inaweza kuwa mfano huu hauna maana sana, lakini ndivyo nilivyoelewa mimi kutokana na agizo lile la Bwana Yesu kwenye ile Math.28:19 na kile walichofanya mitume.

  Kama ambavyo umesema mwenyewe kwenye post yako ya tar. 18, yaani jana kwamba;
  “….Lakini kwa upande mwingine, tukiyaacha Maandiko yatuongoze katika jambo hili, itaturahisishia kufika katika kuelewa ni kwanini Mitume waliutimiza ubatizo walioagizwa waufanye “kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”, lakini wao wanalitimiza Agizo hilo kwa kuufanya ubatizo huo “kwa jina la Bwana Yesu Kristo” jambo ambalo limetutatanisha wengi, hata kutupelekea kuwatilia shaka mitume.”

  …basi ina maana tunaongelea kitu hicho hicho kimoja kutoka angle mbili tofauti! Kilichonishtua kwenye kile kifungu namba kumi na moja ni kile ulichokisema kwamba ‘kwa kusema JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU ni upagani wakati ni Agizo na ni maneno ya Bwana Yesu (Mungu); hicho ndicho kilichonipelekea kuuliza haya yote.

  lakini pia ndugu yangu Lwembe, kwa kuuliza maswali yote hayo sio kwamba tunabishana ili apatikane mshindi wa kujua sana kulitafsiri Neno la Mungu au kwa kufanya hivyo naomba isionekane kana kwamba mimi nawafanya Mitume kuwa waongo na mimi ndiye mkweli sana (kwa sababu sisi sote tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii), au najua sana kuliko Roho Mtakatifu aliyewawezesha kuandika yaliyoandikwa, BALI (nasisitiza BALI), nia yangu ni kujifunza zaidi ili nifikie hatua ya kutoka imani hadi imani na utukufu hadi utukufu.

  Kwa maswali yangu niliyoyaweka mbele yako huwezi kujua majibu au maelezo uliyoyatoa yamewasaidia watu wangapi kukua kiroho kwa kiasi gani!!! Lakini mtu mwingine ambaye ni bado mchanga kiroho anaposoma kwamba kwa kusema ‘Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu’ ni upagani bila kufafanua una maana gani, huwezi kujua anaathirika kiasi gani pia kiimani!

  Kwa sababu hiyo basi naomba mjadala juu ya kifungu hiki cha kumi na moja kati yangu na ndugu Lwembe ufikie tamati, LAKINI kama kuna mwingine anataka kuuliza zaidi, basi afanye hivyo ili tuendelee kufundishana zaidi. Aliyemuelewa ndg Lwembe anachokisema na kama kimemtoa hatua moja kwenda hatua kubwa zaidi kiroho basi sifa na utukufu zimrudie Mungu. Kwangu mimi kile kifungu nilichokinukuu hapo juu (cha ndg Lwembe cha tar.18/1/2012) naona kuwa hilo ndilo hitimisho la maswali yangu kwa ndugu Lwembe. Kama ni lazima basi nitarudi tena kuuliza juu ya vifungu vile vingine 10 vilivyobaki, yaani namba 1-10.

  Roho Mtakatifu, aliye ndani yetu na juu yetu, aendelee kutufungua macho na masikio ya rohoni ili tuendelee kuona na kusikia wazi wazi yale aliyoyakusudia tuyaone na kuyasikia kutoka katika maandiko yake.

  Barikiweni sana!

 21. Wapendwa,hapana kitu kizuri kuliko hiki yaani hamu ya kuyaweka maneno ya MUNGU kwa wingi ndani yetu,nimefurahishwa na jinsi mnavyozidi kufanya watu wakeshe wakitafakali namna ya kuitimiza “Haki yote!” Ndg zangu kwa upande wangu naona mjadala juu ya namna ipasavyo mtu kubatizwa ni kama umekwisha,nataka nikubaliane na Ndg Lwembe,pengine watu watasema nilisha kaa naye pahala tukaongea na hivyo kuwa na nia moja,kwakweli kimwili sijawahi kupatana naye na tukapanga namna ya kuliongelea jambo lolote katika mijadala inayo endelea.nikili wazi mtu huyu hajawahi kujitambulisha kwangu kuwa ndiye Lwembe. Nimeona niseme wazi hilo ili ijulikane kuwa mimi siko “Bayasidi” na upande wowote,bali najadili tu kama Roho atakavyoniongoza kusema.Nikisha kusema hayo,naona nianze hivi; Kwanza Neno la MUNGU halipingani,ni lilelile kila siku. YESU alimwambia Nikodemo kwamba, kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho,…..”kama upepo huvuma na kusikika,lakini wapi unatoka na wapi unakwenda ndiyo “kasheshe” vivyo hivyo na mambo ya kiroho! Watu wanapo tumia Akili – ambao ni mwili, wanachengana na ukweli wa Jambo kiroho,nivizuri kutumia akili lakini si “BUSARA” Katika hili!Neno linasema maneno namaana za mambo kama hili tunalojadili leo,wenye akili wamefichwa…! Watu wanapaswa waingie Rohoni kujua ya Rohoni,na akili zao waziache mbali. Mtu asijaribu kulazimisha mistari ya Biblia ikubaliane na anavyotaka iwe ili “kumiti”maoni ya mawazo yake,kwanza hapa hatushindani,hatuna haja ya kujua ujuzi na akili ya mtu katika jambo husika.Wote tunapaswa kusikiliza Roho anavyo tuelekeza. Ndg zangu kama alivyofafanua ndg yetu Lwembe sijaona wapi amebakiza,….Neno linasema yafanyeni mambo yote kwa Jina la Yesu kristo. na kweli tunaona wagonjwa wanapona kwa jina la Yesu,wanaokolewa kwa jina la Yesu,minyororo mbalimbali ya maisha inafunguliwa kwa jina hilohilo la BWANA YESU KRISTO! NASHINDWA KUJUA UGUMU NI NINI. Nikweli kuwa YESU aliwaambia watu wabatizwe kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu – lakini ni wazi kuwa ktkt maneno yote matatu hapana jina hapo,ila ni sifa za kiutendaji tu.Maandiko yanathibitisha wazi kuwa Yesu ndiye Baba (bwana),ndiye Mwana (Yesu) na ndiye Roho mtatifu (Kristo) labda mnifahamishe kama Yesu mwenyewe kama Yesu alipata kubatiza mtu katika mto wowote na akatumia hilo jina la Baba na Jina la Mwana na la Roho mtakatifu-Neno linasema ……mtakacho kifunga au kukifungua Duniani na Mbinguni kitafungwa au kufunguliwa.Hii inaonyesha wazi Bwana Yesu atakuwa na watu wake wakati wote akiwafundisha na kuwaongoja cha kufanya katika kuitimiza kweli yote.Tunajua pia kwamba shetani alinukuu maandiko katika kumjaribu Yesu, nA Yesu naye alijibu mashambulizi kwa kutumia maandiko vilevile,lakini mwisho wa yote Roho mtakatifu kupitia kinywa cha Yesu akamkemea naye akaondoka. Yatupasa kuisikiliza hekima ya Roho mtakatifu katika kufikia mkataa wa jambo badala ya kutaka kutumia Akili zaidi kwa kupitia maandiko! Yesu alisema….nendeni ukawahubiri watu,wale watakao kataa kung’uteni mavumbi ya miguu yenu muondoke! Paulo naye anasema iwe malaika au mtu yeyote atakaye wahubiri injili tofauti na hii (yaani waliyoifundisha) alaniwe! Sasa kama maandiko hayapingani na yanafaa kwa mafundisho tatizo ni nini basi? labda tujiulize hivi; MITUME WALIBATIZA KWA JINA GANI ILI TUFUATE? Maana ineandikwa mtu asifundishe nje ya mafundisho ya MITUME! Bwana aendelee kutupatia chakula chetu cha kila siku.Asante.

 22. .
  Naomba mchukuline nami kidogo … Natambua thread hii yahusu Manabii,lakini nilikuwa natafakari kigezo cha 11 alichoandika Mpendwa Lwembe January 14.
  Nawasihi Tutafakari Petro alipokuwa anashindana na watu wa tohara kuhusu habari ya kornelio na Watu Mataifa kubatizwa na Roho Mtakatifu .

  Mathayo3:11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba;….Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

  Matendo10:43 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.

  Matendo11;14,15 Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo. Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.

  Tafakari:

  1.Je Tunabatizwa wakati gani(upi) na Roho Mtakatifu na kwa moto?

  (i)Tulisikapo Neno na kuliamini na kujazwa na Roho kama siku ya Pentekoste
  (ii)Tunapo Batizwa kwa maji mengi haijalishi iwe kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu au kwa Jina la Bwana Yesu.

  2.kuna andiko lolote lile linalozungumzia kuwa Mitume wa Bwana Yesu,walishawahi kubatizwa Ubatizo wa maji?, kwa mfano,

  (i)(labda tuseme Ubatizo wa Yohana/ kwa Jina la Yesu/kwa Jina la Baba….)
  (ii).Au ni ule tu wa siku ya Pentekose tu walivyo batizwa kwa Roho Mtakatifu na kwa Moto?.

  Basi wapendwa Naomba kwa Bwana ili Neno la Kristo lijae kwa wingi ndani yetu katika hekima yote.

  .

  Barikiwa.

 23. Ndugu Kinyau,

  Ninakushukuru sana kwa changamoto uliyoitoa, si kwangu tu, bali kwetu sote tulio katika kuFellowship Neno la Mungu!

  Basi katika kuirejea post yako ya mwisho, kwanza nimefurahishwa sana na kule kuzileta rejea za Biblia tofauti tofauti ili kuliweka sawa jambo ambalo kwa msomaji asiyezijua Biblia hizo na jinsi Andiko hilo linavyo onekana, angetoka na wazo finyu kama nilivyoliwasilisha. Lakini sasa wengi wetu tumepanuka katika hilo.

  Baada ya hapo, labda sasa tuyatazame yale maswali uliyoniuliza.
  Kama ulivyosema na kuonesha kwa Maandiko, suala la kuweka LA au kutokuweka, halileti tofauti yoyote katika tafsiri ya kifungu hicho; hilo ni sawa kabisa, haileti tofauti.

  Kwamba “… mtu akifundishwa au kuhubiriwa Injili na kuamini na kuzamishwa kwenye maji mengi, bila kusema chochote, ubatizo huo unakubalika kufuatana na fundisho la mitume; ILA likisemwa lile agizo la Bwana Yesu la kuwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, ubatizo huo ni batili na huo ni upagani!” Hili umelichanganya sana, ni kweli hukukielewa nilichosema. Sijalisema hilo jambo katika jinsi hii uliyoitolea maelezo, bali kwa vile nitalirejea tena hilo jambo katika majibu yanayofanana na yale ya awali, huenda tukaenda sawa.

  Kwanza katika kuweka msingi wa maelezo yangu, napenda ieleweke wazi kuwa MAANDIKO au BIBLIA ndiyo rejea ninayoitumia na ndio YAKINI au ABSOLUTE yangu. Kwa hiyo tunapokutana katika masuala haya ni katika spirit ya kujumuika pamoja katika tafakari ya Neno la Mungu, ili kufaidiana na kuizidisha furaha yetu tunapozidi katika kuijua ile KWELI.

  Ndugu Kinyau, unaposema kuwa umemhubiria mtu, ni lazima kwanza umjue aliyekuagiza ukafanye hiyo kazi ni nani. Hilo litakuweka sawa katika kuitimiza kazi hiyo kulingana na aliyekutuma. Agizo unalolizungumzia kuhusu ubatizo, hilo la Mt 28:19-20 waliopewa ni Mitume. Mimi na wewe hatukuwepo. Hao ndio wanafamilia wa Yesu alio watayarisha na kuwakabidhi hilo jukumu unalosema kuwa na wewe unalifanya. Lakini inaonekana kuwa wewe unalifanya tofauti na hao waliotumwa kuifanya kazi hiyo, kiasi kwamba ni dhahiri kuwa mtakuwa hamjatoka katika shina moja. Aidha mitume ni waongo au wewe ni muongo, maana hamuwezi kuwa mnaihubiri Injili moja halafu mtofautiane katika suala la MSINGI kama hili!

  Basi mimi, kwa uamuzi nilioufanya, nitaongozana na mitume katika maelezo yangu, kwani wao ndio walionitambulisha kwa Kristo. Jambo ambalo umenishangaza zaidi ni pale unaposema Biblia haioneshi mitume walitumia maneno gani katika ubatizo, jambo ambalo si kweli. Labda niyanukuu maelezo yako kwa uchache ili wewe mwenyewe uwe hakimu wa unachokisema: “Kwenye Matendo 2:37-38, na 8:9-17 na sehemu zingine, biblia haionyeshi wakati mitume wakiwabatiza watu kwenye maji mengi walikuwa wakisema maneno gani, au walikuwa wakiwazamisha tu kimya kimya!

  Labda nami nivinukuu vifungu hivyo vya Biblia ili tujionee wenyewe, kisha tuweze kuliamua hilo :
  Mdo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, …”
  Matendo 8:16 ‘… ila wamebatizwa tu kwa Jina lake Bwana Yesu.’
  Mdo 10:48 “Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo …”
  Mdo19:5 “Waliposikia haya wakabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu.”
  Rum 6:3 ‘Hamfahamu kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?’

  Basi vifungu hivi zaidi ya vitatu, vyatosha kwa ushahidi. Mimi naamini ndg yangu Kinyau hukumaanisha ulichokisema vinginevyo utakuwa ni mtu unayeyakana Maandiko. Ndio maana nilikuambia jaribu kuona ni nani aliye kutuma kuhubiri, huenda ni kanisa, basi ikiwa ni kanisa, yawezekana tusifike mbali sana, maana hayo yako mengi sana na kila moja lina wazo lake.

  Kwa kifupi huo ndio ule ubatizo wa Mat 28:19-20, tafsiri ya Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu ndio hiyo hapo, yaani Jina la Bwana Yesu Kristo. Usitumie akili zako katika kuyaelewa mambo ya Mungu, anahitajika Roho Mtakatifu kwani ndiye Mwalimu na kiongozi. Mitume walipojazwa Roho Mtakatifu, ndipo yalipofunuliwa mambo haya kwao, hawa wengine sijui wana roho gani, kwa hiyo unapowafuata, ni vizuri uwe mwangalifu. Kwani roho zinazohudumu kinyume na Neno la Mungu ni nyingi, ndio maana mwisho nikakuambia ni UPAGANI uliojiingiza katika Ukristo! Haiwezekani ukawa uko sawa na makosani katika jambo moja kwa wakati mmoja!

  Tena hata katika lugha ya kawaida tu, sote tunafahamu kuwa Baba si jina bali ni cheo au title tu. Hata Mwana nalo si jina, ndio maana ukiulizwa Mwana ni nani, utajibu bila kusita kuwa ni Yesu. Pia Roho Mtakatifu si jina bali ni title. Na iwapo hayo ni majina basi kile kifungu kilipaswa kuanza na “mkiwabatiza kwa MAJINA ya la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” jambo ambalo si sawa. Au kiwe kama kilivyo bali ieleweke kuwa jina hilo la “Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” katika ujumla wake wa hivyo vyeo ni jina moja. Nalo jambo hili la hilo kuwa ni jina moja, litaibadilisha Biblia nzima na kuitumbukiza katika mkanganyiko, maana hapo atazaliwa Mungu mwingine mwenye hilo jina refu kuliko majina yote niliyowahi kuyasikia!

  Lakini kwa upande mwingine, tukiyaacha Maandiko yatuongoze katika jambo hili, itaturahisishia kufika katika kuelewa ni kwanini Mitume waliutimiza ubatizo walioagizwa waufanye “kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”, lakini wao wanalitimiza Agizo hilo kwa kuufanya ubatizo huo “kwa jina la Bwana Yesu Kristo” jambo ambalo limetutatanisha wengi, hata kutupelekea kuwatilia shaka mitume. Basi hebu turudi katika Maandiko ili kulitazama hilo, tupate kuliona jambo hilo katika uwiano uliokusudiwa, huenda likatupa mwanga zaidi hata tukawaona hao waliojiingiza katika IMANI walivyoachwa nje kwa kuukosa ufunuo wa jambo hilo, hivyo wakayachukua Maandiko makavu (ambayo yanaua ) bila ya Roho (ambaye anahuisha) na kuishia katika hali hii tuliyomo.

  Ili kujihakikishia jambo hilo, na tulitazame Jina hili la Yesu ili tuone asili yake, huenda tukapata mwanga zaidi juu yake, pia iwe fursa yetu ya kujisahihisha kwa kuuangalia tena ukweli huu ambao Mungu ameuweka hapo kwa ajili yetu: Katika Yn 5:43- Kristo anasema, ‘Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, …’ Ikiwa yeye amekuja kwa jina la Baba yake, na iwapo Baba ni jina, basi Yesu alipaswa kuitwa ‘Baba’ jambo ambalo lingaliitupa Biblia yote katika mkoroganyo! Bali udhahiri wa hilo ni kwamba kama yeye Yesu amekuja kwa jina la Baba yake, basi jina alilonalo ndilo jina la Baba yake, kwa hiyo Baba yake atakuwa anaitwa YESU! Tena, katika Yn:14:26 – Kristo anasema, ‘..Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atampleka kwa jina langu…’, kwa hiyo kulingana na kifungu hiki, pia ni dhahiri Msaidizi huyo, Roho Mtakatifu, jina lake litakuwa YESU. Haya, Yesu alipozaliwa, jina hili alilopewa la Yesu halikutoka kwa Yusufu wala Mariam, bali alikuja nalo Malaika Gabriel kutoka mbinguni ili apewe huyo mwana wa Mungu atakayezaliwa, Lk 1:31 ‘Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita YESU’! Basi Petro na mitume wakiwa ni wa rohoni, wao walijua wanachokifanya tofauti na makundi yetu ya mwilini.

  Tena basi, katika kulikamilisha hilo tunaambiwa kuwa huyo Yesu, Mungu sasa amemfanya kuwa Bwana na Kristo (Mdo 2:36 “Basi nyumba yote ya Israelina wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo)! Neno ‘Bwana’ katika Biblia humaanisha Mungu au Baba, na Neno Kristo maana yake ni Upako wa Mungu au Roho Mtakatifu. Hivyo kuanzia hapo huyo Yesu sasa anaitwa Bwana Yesu Kristo, yaani:
  Baba = Bwana
  Mwana = Yesu
  Roho Mtakatifu = Kristo (Upako)

  Basi katika ujumla wa jambo hili, kulingana na mtiririko wake, Kristo ndiye aliye warithisha mitume Injili. Nao mitume wameturithisha sisi Injili hiyo hiyo. Kwa hiyo, mtu yeyote yule, ambaye anadai kuhubiri Injili, ni lazima awe katika mtiririko huu wa kurithishwa hiyo Injili, yaani legacy. Kwa hiyo ukiiona Injili tofauti, unatakiwa ujue kuwa huyo mhubiri hayumo katika huo mlolongo wa urithi wa Injili, atakuwa amejiingiza tu. IMANI au INJILI iko MOJA TU, hiyo waliyokabidhiwa mitume mara moja, tuipiganie!!!

  Ubarikiwe!

 24. Shalom…
  namshukuru Mungu kwa kunipa muda wa kupita kwenye hii blog kwa siku ya leo…. ila nimeogopa sana hayo mafundisho ya Lwembe…… hasa kwa wakristo wachanga….. Nimestuka nimeogoga sana….. ni vema wasomaji kuwa makini……
  Hii mada ni njema kama itatumika vema…na kiuadiliwa kwa nia njema yaani ya kujenga na sio kubomoa….
  ……vilivyonitisha zaidi ni hivo vigezo alivoviweka Lwembe vya kupima manabii wa uongo….
  Siku nikiwa na muda nitachangia….
  Mungu awabariki

 25. Mpendwa Haule,

  Ubarikiwe sana ndugu yangu. Mimi sikukwazika kwa ulizo lako isipokuwa nilichokuwa nakisema ni kwa ujumla wake kwamba si afya kiroho kama kila mtu atakayechangia chochote humu tujue anasali wapi au dhehebu lake ni lipi! La muhimu ambalo, naliona ni la afya zaidi kiroho kwa wote ni kuuliza kile ambacho hujakielewa kwenye post ya mtu kuliko kutaka kujua dhehebu lake. Madhehebu hayatupeleki mbinguni ingawa yana umuhimu wake.

  Kwangu mimi kama ulivyosema kwa ndugu Lwembe ni kwamba Amani ya Kristo inatawala moyoni mwangu na siku zote nabarikiwa sana na michango yako.

  Ugeni wa mafundisho ya ndugu Lwembe inawezekana usiwe kwako tu, hata mimi pia niliona hivyo na ndio sababu nikamwomba anifafanulie kile kifungu cha 11 katika yale aliyosema kuhusu fundisho la Mitume. Na hata huko nyuma kabla hajaleta yale mambo 11 kama fundisho la mitume, kuna sehemu nyingi nilikuwa bado nazivutia pumzi ili kuuliza kwa minajili ya kutaka kujua zaidi, kwa hiyo sio wewe tu uliona kama mafundisho mapya/mageni toka kwa ndg Lwembe.

  Mungu atuwezeshe kuendelea kulitafakari neno lake kila siku kwa kuwa nia uzima wetu.

 26. Haggai…
  Mafundisho ya Mpendwa Lwembe ni mageni kwangu,Nilipo utafakari mstari huu “Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao” nilitaka kujua hilo nililotaka kulijua toka kwa mpendwa,Samahani kama ulikwazika/mlikwazika kwa kutaka kufahamu hema analoabudia Mpendwa Lwembe,Hata ukirudia kulisoma lile bandiko langu utaona nilimuomba Lwembe amani ya Kristo imuongoze ktk hilo.Naendelea kutafakari mabandiko ya Ndg Lwembe..

  Neema na iwe kwenu.

 27. Ndugu Lwembe,

  Kimsingi kwa maelezo hayo sasa umeeleweka vizuri ingawa hoja yako ya mwisho ambayo ume-conclude kwa kuita ni upagani sijui ina mashiko gani!. Ni kweli biblia ya Union Version ya mwaka 1952 imeuandika mstari huo wa Mathayo 28:19 kwamba “…..mkiwabatiza kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu” kuonyesha kuwa ni Jina moja tu, yaani Jina YESU.

  Lakini Version zingine nyingi tu zimeuandika mstari huo,”…mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” Hapa chini nakupa baadhi tu ya Versions za Kiingereza zilivyouandika mstari huu.

  1. King James Version “Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name OF THE FATHER, AND OF THE SON, AND OF THE HOLY GHOST”

  2. Amplified Bible (World wide English Version). “So go and make disciples in all countries. Baptize them in the name OF THE FATHER, AND OF THE SON, AND OF THE HOLY SPIRIT”

  3. Amplified Bible (Today’s New International Version). “Therefore go and make disciples of all nations, baptizing them in the name OF THE FATHER AND OF THE SON AND OF THE HOLY SPIRIT”

  4. English Standard Version(ESV). “Go therefore and make disciples of all nations, baptizing them in the name OF THE FATHER AND OF THE SON AND OF THE HOLY SPIRIT” Footnote: ‘in’ can also be said ‘into’.

  5. New American Standard Bible. “Go therefore and make disciples of all nations, baptizing them in the name OF THE FATHER AND THE SON AND THE HOLY SPIRIT” (Hii inaendana sawa na hoja yako au ile iliyoko kwenye Union Version ambayo wewe ndio umeiona sio upagani).
  Footnote: ‘Go’ can also be said ‘Having gone’.

  5. New Life Version Bible. “Go and make followers of all the nations. Baptize them in the name OF THE FATHER AND OF THE SON AND OF THE HOLY SPIRIT”

  6. Wyclife Bible. “Therefore go ye, and teach all folks, baptizing them in the name OF THE FATHER, AND OF THE SON, AND THE HOLY GHOST”

  7. NENO BIBLIA TAKATIFU (BIBLICA). “Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”

  Nimenukuu Version hizo tofauti tofauti ili tufikiri pamoja (wewe na mimi) kwamba Version zote hizo zilizoandika ‘kwa Jina LA Baba, na LA Mwana, na LA Roho Mtakatifu’ ni kweli za kipagani, au zina maana ya majina matatu tofauti, au zina maana ya kuonyesha NAFSI TATU ZA MUNGU ZILIZO KATIKA UMOJA na zinazofanya kazi pamoja? Hatuna haja ya kulijadili sana hilo ila tujiulize wenyewe tu kwamba kweli Version hizo zina maana hiyo uliyoisema wewe?

  Ni kweli kwamba katika Agano Jipya, Mungu wetu amejifunua kwa Jina moja tu la Yesu na utimilifu wake wote umo humo(Yohana 17:6,26, 5:43, Waebrania 1:4, Wafilipi 2:9 n.k) tofauti na kwenye Agano la Kale alivyokuwa anajifunua kwa majina mengi tofauti tofauti kulingana na tukio au matukio ya eneo husika, kama vile MIMI NIKO AMBAYE NIKO, JEHOVA NISI, JEHOVA RAPHA n.k.

  Kwa hiyo, kwa uelewa wangu mimi sioni tofauti iliyopo kwa kuweka “LA” na kutokuweka, labda mpaka hapo utakaponielewesha vizuri inakuwaje upagani kwa kuweka tu kiambishi (preposition) ‘La’ kwenye sentensi hiyo. Nilivyoelewa kutokana na maelezo yako hapo juu ina maana mtu akifundishwa au kuhubiriwa Injili na kuamini na kuzamishwwa kwenye maji mengi, bila kusema chochote, ubatizo huo unakubalika kufuatana na fundisho la mitume; ILA likisemwa lie agizo la Bwana Yesu la kuwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, ubatizo huo ni batili na huo ni upagani! Sijui kama ulikuwa na maana hiyo!!

  Mwisho naomba nisahihishe kidogo jinsi wewe ulivyoelewa kuwa napotosha au nimetumia lugha rahisi sana na kwa maana hiyo nimepotosha maana halisi iliyoko kwenye biblia. Hapo sikuwa nanukuu neno lilivyoandikwa toka kwenye biblia, isipokuwa nilikuwa naonyesha kwamba mbatizaji anaweza kusema tu kwamba ‘Nakubatiza kwa Jina la Yesu’ basi akaishia hapo bila kusema ‘Nakubatiza kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu’ kama inavyosomeka kwenye version zingine za biblia nje ya ile ya Union Version? Hilo ndilo lililonifanya ni-ommit maneno mengine, ndio sababu nikaweka neno ‘bila kutumia……’ Inawezekana ni ugumu wa Kiswahili (ingawa tunakiongea kila siku), ukweli ni kwamba sikuwa na maana kwamba Mungu Baba ana jina lake, Mungu Mwana ana jina lake lililo tofauti na la Mungu Baba, wala sikuwa na maana kwamba Roho Mtakatifu naye ana jina lake ambalo ni tofauti na la Mungu Baba na Mungu Mwana. Sikuwa na maana hiyo kabisa.

  Tulichokuwa tunakijadili hapa ni maneno yapi sahihi yanatakiwa kusemwa na mbatizaji kwa anayebatizwa. Ninavyojua anayebatiza (kama agizo la Bwana Yesu linavyosema…mkiwabatiza kwa Jina….) anapaswa aseme maneno kwa mbatizwaji ili kuonyesha kwamba tendo hilo ni takatifu na kwa kuzamishwa kwenye maji utu wake wa kale wenye dhambi unazikwa katika mauti ya Kristo na unafufuliwa utu mpya kama vile Kristo alivyofufuka. Na mbatizaji hawezi kusema maneno yake anayoyataka yeye, ni lazima aseme maneno ya Mungu yaliyoko kwenye biblia kulingana na tukio hilo au kufuata agizo la Bwana Yesu. Ndipo sasa wewe ukasema ubatizo wa ondoleo la dhambi hufanyika kwa Jina la Yesu Kristo katika maji mengi. Ukaendelea kuonyesha kuwa wapo wanaonyunyizia maji kidogo waumini wao (ambalo nakubaliana nalo kuwa sio sahihi), na wapo wengine wanowazamisha katika maji mengi kweli,LAKINI,’kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu’ kinyume na fundisho la mitume.

  Na katika post yako ya mwisho umeeleza vizuri sana jinsi ambavyo ubatizo huo wa ondoleo la dhambi unatakiwa kuwa, nalo nakubaliana na wewe mia kwa mia. Kitu ninachotaka kukielewa vizuri zaidi hapo ni kwamba baada ya mtu kufundishwa au kuhubiriwa Injili ya kweli na imani yake kwa Kristo kujenga, tunakuja kwenye tendo lenyewe la kuzamishwa kwenye maji mengi au kwa kifupi kubatizwa. Tendo hilo linatakiwa litendekeje kufuatana na fundisho sahihi la mitume? Kwenye Matendo 2:37-38, na 8:9-17 na sehemu zingine, biblia haionyeshi wakati mitume wakiwabatiza watu kwenye maji mengi walikuwa wakisema maneno gani, au walikuwa wakiwazamisha tu kimya kimya! Lakini kama waliagizwa na Bwana Yesu kuwabatiza kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, na agizo hilo umesema halina utata, je kuna ubaya gani kufuata agizo hilo? Hapo ndipo nahitaji maelezo zaidi toka kwako.

  Naomba wasomaji watusamehe kwamba tumetoka nje kidogo ya mada, lakini tunahitaji kuyajua vizuri yale mambo 11 ambayo ndugu yetu Lwembe ameyaleta hapa kama ndiyo ‘gauge’ yetu ya kujua kile kilichokuwa kikifanywa na wenzetu wa kanisa la mwanzo, na kwa mantiki hiyo ni kwamba tukiyaelewa vizuri hayo ndipo tutaweza kuwaelewa vizuri manabii wa uongo na manbii wa kweli wa siku hizi.

  Ubarikiwe na Bwana.

 28. Ndugu Kinyau Haggai,

  Sasa nimekuelewa vizuri!

  Unasema sijayajibu maswali yako, lakini nadhani umejisahau tu. Swali la kuhusu kukifuta kufungu cha Mat. 28:19-20, nilikujibu kuwa sijakifuta, hicho kiko kama kilivyo katika maana kamili kama kilivyokusudiwa.

  Kuhusu ubatizo kuwepo wa aina mbili, nilikuambia kuwa kuna ubatizo mmoja tu, kama ulivyotimizwa na mitume.

  Labda sasa tuliendee hilo la tatu ambalo naona ndilo lililozaa haya maswali yote, hilo la ubatizo kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu kuwa ni kinyume na Fundisho la Mitume. Tunapoendelea katika hilo, naomba kwanza niweke sawa maelezo ya swali lako ili ninapolijibu lisizalishe utata mwingine kwa wafuatiliaji wengine wa mada hii. Ninanukuu: “Na sehemu ya pili ndipo nikakuuliza je kuna kubatizwa zaidi ya mara moja? , yaani ule ubatizo wa ondoleo la dhambi ambao unazamishwa kwenye maji mengi kwa JINA LA YESU TU bila kutumia JINA LA BABA WALA LA ROHO MTAKATIFU;..?” Ubatizo wa ONDOLEO la DHAMBI unafanywa kwa JINA LA BWANA YESU KRISTO na si kwa JINA LA YESU TU kama nilivyo kunukuu.
  Katika kusema kwangu kuwa ubatizo kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ni batili, ubatili huo niliousema haukulenga katika agizo bali katika utendaji wake. Agizo kama lilivyo halina tatizo lolote, ndio maana katika jibu langu la awali nilisisitiza kuwa Andiko hilo liko sawa kama lilivyo, pia liko katika maana yake kamili. Jambo ambalo linasikitisha ni upotoshaji wa makusudi uliofanywa kisha kuendelezwa kwa ushawishi uliofanikisha kuundoa ubatizo sahihi uliokusudiwa kuwemo ndani ya kanisa na badala yake kuupachika huu mkavu usio na maana yoyote ile kiutendaji! Unajua, ndugu Kinyau, mawasiliano yanayofanywa na wanafamilia wakati mwingine ni magumu kidogo kueleweka kwa watu wa nje. Kwa hiyo, kama unavyoliona jambo hili la ubatizo, makusanyiko yetu mengi yanatofautiana na mitume katika kuutimiza huo, ikionesha wazi kuwa wamewasikiliza wasiohusika na kuwaacha wahusika hata tumeishia kuwa katika mkanganyiko huu tuliomo.

  Agizo lililotolewa na Kristo katika Mathayo 28 ndilo linalotimizwa na mitume katika ufasaha na kuyakamilisha manufaa ya kiungu yaliyokusudiwa kwetu kulingana na Program ya Mungu ya Ukombozi. Mambo ya Mungu huenda yakijifunua taratibu. Ndio maana unaona Kristo akizungumzia kuwafanya wote wanafunzi wake, ambalo huwezekana kwa kuhubiriwa Injili inayomfunua kuwa Yeye ni nani, pia hutuweka katika uelewa wa kiasi gani tulivyo mbali na Wokovu na kutufanya tuijutie hali hayo hata tukawa na shauku ya kumkimbilia huyo Kristo. Hilo huzaa Imani ambayo hutupeleka katika kumtii na kuutafuta msamaha. Nayo njia aliyotutayarishia ili kutusafisha hata tuweze kukaa naye ndio huo UBATIZO kwa JINA LA BWANA YESU KRISTO KWA ONDOLEO LA DHAMBI kama jambo hilo linavyowekwa wazi katika mdo 2:37-38. Nalo Kanisa linapozaliwa tunawaona hapo wale 3,000 katika siku ile ya Pentekoste, Petro kwa Funguo za Ufalme alizopewa akilifungua Geti la Ufalme kuwaingiza hao watangulizi wetu. Nasi tukijumuishwa katika ahadi hiyo kama wale wote tulioitwa na Bwana Mungu wetu tumjie! Basi kwa kanisa kuuondoa Ubatizo huu, hilo laonesha kuwa aliyewaita wamjie si Bwana Mungu huyu anayemzungumzia mtume Petro, yawezekana ni mungu mwingine, licha ya kanisa kudhania ni Mungu huyu wa kweli! Unaweza kuona kama labda ni jambo lisilowezekana, bali liliwahi kumkuta Mariam na mumewe Yusuf walipotembea mwendo wa kutwa wakidhania wanaye mtoto Yesu, bali hawakuwa naye, hata siku ya tatu (Luk 2:43-46)!! Kwa hiyo usishangae kuwa kanisa limewafungia watu nje ya WOKOVU kwa zaidi ya miaka 1,000 likiwa lenyewe limedanganywa! Biblia inasema hakuna mwenye dhambi atakaye muona Mungu, sasa, mamilioni yetu ambao kanisa limetuingiza katika njia isiyo na pa kutokea, itakuwaje?!

  Yule Mtafsiri aliyemtafsiria mama yetu Hawa, ameendelea kulidanganya Kanisa tena kwa kulipa tafsiri iliyo potofu. Amechezea Maandiko na kulilisha kanisa uongo wake. Hebu ndugu yangu Kinyau irejee nukuu yako katika hii sehemu, ili uone jinsi mawazo yaliyo huru yanavyoielewa lugha katika urahisi: “…kwenye maji mengi kwa JINA LA YESU TU bila kutumia JINA LA BABA WALA LA ROHO MTAKATIFU…” Lugha uliyoitumia hapa katika kunionesha jambo ulilotaka nilione, ni lugha rahisi sana kama ilivyo katika Biblia. Unasema, kuhusu hilo JINA: “kwa Jina la Yesu tu” yaani ukimaanisha hilo jina la Yesu likisimama katika ile nafasi ya MWANA. Kisha ukaendelea, “bila kutumia Jina la Baba wala la Roho Mtakatifu”, hiyo ikionesha wazi pia kuwa Baba analo jina lake na Roho Mtakatifu pia. Yaani kwa kifupi unatudhihirishia katika uhuru wa lugha ulivyoitumia kuwa BABA si jina, wala MWANA si jina na wala Roho Mtakatifu si jina bali vyote ni vyeo! Basi ukilisoma lile Agizo pole pole, utaona kuwa limetumika neno JINA ambalo ni moja katika lugha ya kawaida. Nalo jina hilo moja ndilo linalotumika kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama Andiko lisemavyo. Tazama: “kwa JINA la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu” ; kama hizo nafsi tatu zingekuwa zinajitegemea katika majina, basi kifungu hicho kingesomeka hivi: “ Jina LA Baba na LA Mwana na LA Roho Mtakatifu” bali sivyo! Nao ubatizo wa vyeo haujaagizwa katika Biblia, ni UPAGANI!

  Kwa hiyo huo ndio urahisi wa Maandiko!

  Ubarikiwe

 29. Ndugu Ck Lwembe,

  Nafurahia mjadala huu kwa kuwa naona SUBIRA imetutawala hadi sasa. Katika vile vipengere 11 mimi nina mawazo tupitie kimoja baada ya kingine maana hapo pana mengi ya kujadili ukizingatia ni WAKRISTO wengi, wengi sana hawafanyi hivyo ulivyorodhesha. Sasa kwa kuwa tunazungumza Neno la Mungu ni vema tukapitia kimoja baada ya kingine, kwa kuwa yanatuhusu wooooote!

  Lakini naona ndugu yetu Kinyau Haggai ameshaanza na kile cha 11. Kwa maana hiyo mimi napumzika kidogo, ninywe maji, kisha nitarejea,. Kwa sasa naomba niwe msomaji tu hadi hapo nitakapoona yanipasa kuendelea!

  Nawafuatilia!

 30. Ndugu Ck Lwembe, Shallom.

  Nadhani hukunielewa kile nilichokiuliza kwenye post yangu ya mwisho ya tar.15. Mimi sikuwa naleta fundisho la ubatizo mpya, bali nilikuwa nataka kujua mantiki ya hoja yako kwamba fundisho la kweli la mitume linasema ubatizo wa ondoleo la dhambi hufanyika kwa Jina la Yesu Kristo katika maji mengi. Ukaendelea sehemu ya pili ya hoja yako kwamba wengine (siku za sasa) kweli wanabatiza na kubatizwa katika maji mengi lakini kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kitendo ambacho kwa hoja yako namba 11 ni kinyume na fundisho la mitume.

  Hapo ndipo nilipokuja na maneno ya Yesu mwenyewe kutoka Injili ya Mathayo 28:19-20, ambayo kwangu mimi nauona ujumbe/utume huu kuwa ndio utume mkuu aliowapa mitume wake kuufanya ulimwenguni kote. Na katika ujumbe/utume huo anaagiza vitu vitatu muhimu;
  1. Kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wake,
  2. Kuwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
  3. Kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.

  Ndipo sasa nikakuuliza kwamba kama umesema kwamba kuwabatiza watu kwenye maji mengi kwa kutumia Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu ni kinyume na mafundisho ya mitume, je andiko hilo la Mathayo unalifuta? Na sehemu ya pili ndipo nikakuuliza je kuna kubatizwa zaidi ya mara moja? , yaani ule ubatizo wa ondoleo la dhambi ambao unazamishwa kwenye maji mengi kwa Jina la Yesu tu bila kutumia Jina la Baba wala la Roho Mtakatifu; na ule mwingine ambao ni kinyume na fundisho la mitume yaani kubatizwa kwenye maji mengi lakini kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu?

  Sijaona mahali popote ambapo umejibu maswali yangu yaliyoibuka kutokana na majibu yako kwa ndugu John Paul kwa kuzingatia kifungu cha 11, badala yake, kwako imeonekana kana kwamba mimi ndio nimeleta fundisho geni, kitu ambacho si kweli, bali hoja hiyo imetoka kwako.

  Nimejitahidi kueleza kwa kirefu kile ambacho nilipenda kukijua kutokana na kile ulichokisema kwenye namba 11 kuhusu fundisho la mitume, na kwa maana hiyo nategemea pia utanielewesha ulikuwa na maana gani kusema kwamba wabatizao kwenye maji mengi kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu wapo kinyume na fundisho la mitume wakati Yesu ndiye aliwaagiza kufanya hivyo!!

  Pamoja na hayo yote nikupongeza sana kwa majibu mazuri uliyompa ndugu yetu John Haule aliyetaka kujua habari za lipi ‘Hema’ linalokuhudumia. Ni kweli kabisa blog hii haina hema au haifungamani na hema lolote, na ndio sababu tuna uhuru huu wa kila mmoja kuchangia chochote kufuatana na Neno la Mungu linavyosema bila kutumia misimamo ya dhehebu au makanisa yetu. Natumaini huo ndio unatakiwa kuwa msimamo wa kila mtu anayetaka kujifunza na kufunza kitu katika blog hii, alimradi haendi nje ya wigo wa Neno la Mungu.

  Ahsente na Mungu akubariki sana.

 31. Ndugu Kinyau, Haggai

  Asante kwa yote, pia hata mimi nilipoiona ile post yako ya awali, nikajua kuwa hukuliona lile jibu, lakini naona mambo yote yako shwari!

  Basi, nikilirejea swali lako la msingi kuhusu lile Andiko la Mathayo 28:19-20, kwamba, Je, ninalifuta Andiko hilo? Jibu ni hapana , silifuti. Andiko hilo linabaki kama lilivyo katika maana yake halisi kama lilivyotamkwa na Kristo na kuwekwa hapo katika Biblia na mitume kama walivyoongozwa na Roho Mtakatifu, wakiwa wamewekwa katika kweli yote.

  Kwa swali lako la pili, Jibu ni kwamba, ubatizo ni mmoja tu, kama unavyoonekana ukitimizwa na mitume katika kitabu chote cha Matendo ya Mitume unaolihusu Kanisa katika ujumla wake. Suala la kwamba ubatizo wa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ni wa kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu ni geni kwangu na sijawahi kusema hivyo wala kuliona Andiko linafunza hivyo! Labda nikuvutie subira ili nami niweze kujifunza.

  Asante ndugu Kinyau, ninasubiri kutoka kwako,
  Bwana, na akutie Nguvu zake!

 32. Mpendwa John Haule,

  Kwanza kabisa, nikushukuru kwa maombi uliyotutangulizia sote tulio katika tafakari ya mada hii! Ni kweli Bwana aziondoe njiani akili zetu na ushawishi wa yule mwovu dhidi ya Neno lake.

  Nikilirejea lile swali lako kuhusu kanisa au hema ninapoabudia, napenda niseme kwamba, nitakuwa nimeharibu mtiririko wa mada yote iwapo nitalitaja kanisa langu, maana mada yenyewe inayahusu mahema! Hata hema langu naweza kuwa ninatofautiana nalo kwa mtazamo nilionao leo hii. Kwani kama nilivyosema katika majibu yangu kwa ndugu yangu John Paul, kuwa wengi wetu hatujawahi kuyachunguza mahema tuliyomo, wengine tumezaliwa humo na tumeendelea kuwamo humo kulingana na wazazi wetu. Wengine tumefuata miujiza, wengine tumefuata wachumba nk. Kwa hiyo hii ndiyo fursa pekee inayotukutanisha mbali na wanyapara wetu, nasi tunaweza kuyakagua na kujifunza mengi yahusuyo Kweli ya Mungu katika uhuru mkubwa! Ndugu Haule, mahema na vyote vitapita, bali Neno la Mungu litadumu, basi ni bora tukiingia Humo, maana nasi tutadumishwa kwalo milele!

  Asante na
  Ubarikiwe!

 33. Ndugu John Paul,

  Asante kwa kuyapokea majibu yangu kwa maswali uliyoniuliza.

  Kuhusu kuiongeza ile list ili uwe nayo yote, nadhani hukunielewa vizuri. Katika majibu yangu nilisema kuwa Agano Jipya lote kama lilivyo, bila kulinyofoa nyofoa wala kuongeza chochote, NDILO FUNDISHO LA MITUME!

  Ndipo nikavirejea vipengele vichache kutoka hilo Fundisho, ili tuvilinganishe na mafundisho yanayoendelea katika makusanyiko yetu. Kutoka maelezo hayo niliyoyatoa, kama unavyoniambia kuwa, kwa ninavyoyaelewa mimi maandiko, mtu asipofanya hayo au akiwa kinyume na haya basi huyo ni Nabii wa Uongo! Hilo ni kweli kabisa, kwangu mimi au kwa mtu yeyote yule, kwani sote hufikia uamuzi kulingana na tunavyoyaelewa Maandiko. Nasi tutahukumiwa kwa hilo; tuliyachukuliaje Maandiko!

  Basi kama kuna jambo lolote lile ambalo ungehitaji nilitolee ufafanuzi katika umbali tuliokwenda, kwangu ni jambo la furaha, ninaamini hata kwako pia na ndugu wengine wanaofuatilia mada hii. Maana ili mradi tunamzungumzia Kristo, basi tuwe na uhakika kuwa Yu pamoja nasi maana alisema mkutanapo wawili au watatu kwa ajili yake atakuwa pamoja nasi. Naona katika hili tuko Kanisa kabisa, basi tumuombe atupe ujasiri wake tunapolikagua Neno lake!

  Ubarikiwe, ndg John na wote!

 34. Ndugu Ck Lwembe,

  Awali ya yote naomba uniwie radhi wakati napost comment yangu hapo juu sikuwa nimeona majibu yako kwa ndg John Paul ya jana tar. 14, baada tu ya kutuma, nikaona majibu yako, naomba nisamehe sana.

  Kwa leo naomba unifafanulie jambo moja tu katika yale kumi na moja uliyotumia kumjibu ndugu John Paul. Umeandika hivi kwenye namba 11;

  11. “BIBLIA INAFUNDISHA KUWA UBATIZO WA ONDOLEO LA DHAMBI HUFANYIKA
  KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO, KATIKA MAJI MENGI.
  Je, ni makusanyiko mangapi ambayo yanayo wanyunyizia maji waumini wao, na
  mengine kuwazamisha kweli, lakini ‘kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
  kinyume na Fundisho hilo?”

  Ninachoomba unifafanulie ni hili kwamba je unafuta kile kilichoandikwa kwenye Injili ya Mathayo Mtakatifu 28: 19-20? Kwa faida ya wasomaji wote imeandikwa hivi kwenye Injili hiyo;
  “BASI, ENENDENI, MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI, MKIWABATIZA KWA JINA LA BABA, NA MWANA, NA ROHO MTAKATIFU; NA KUWAFUNDISHA KUYASHIKA YOTE NILIYOWAMURU NINYI; NA TAZAMA, MIMI NIPO PAMOJA NAYI SIKU ZOTE, HATA UKAMILIFU WA DAHARI”

  Je kuna ubatizo wa aina mbili ;yaani wa ondoleo la dhambi unafanyika kwa jina la Yesu tu na ubatizo wa kuwafanya watu kuwa wanafunzi wwake unaofanyika kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu?

 35. Wapendwa John Paul na Lwembe…
  Tupo pamoja nanyi kwenye hii tafakari tunabarikiwa…wakati mkiendelea naomba mtupe baadaye nafasi nasi tuchangie haswa tafakari za mpendwa Lwembe.

  Mpendwa Lwembe kama hutakwazika wakati tunaendelea kutafakari ungetuambia unaabudu wapi?nikimaanisha kanisa(hema).Na amani ya Kristo iwe juu yako.

  kumbe wakati tukiendelea kutafakari tumuombe Roho Mtakatifu azidi kutuongoza ktk hii tafakari isiwe akili zetu tu wenyewe, au yule mwovu.

  Neema na iwe kwenu,rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu,
  Amen.

 36. Ndugu C K Lwembe,

  Nashukuru sana kwa majibu yako kwa kile nilichoomba. Nimeona orodha ya vipengere 11 ambavyo umeviita ni CHUJIO la kuwapitisha hao manahii wa sasa. Yaani, kwa unavyoyaelewa wewe maandiko, mtu asipofanya hayo au akiwa kinyume na haya basi huyo ni Nabii wa Uongo!

  Nimesoma yote na kwa kuwa bado yako mengi, basi naomba kama yapo Uyarodheshe Yote (kama inawezekana) au hata yale ya msingi ili Tuwe na List yake. Tukishapata orodha ya Mambo yaliyoko katika FUNDISHO LA MITUME ili Tutakapoanza kuyapitia Tuwe na Orodha yote iliyokamilika!

  Asante sana!

 37. Ndugu millinga,

  Ahsante kwa wewe kuwa wazi kwamba siku saba ilikuwa ni mawazo yako tu, hilo limefuta kile ambacho kingeweza kujengeka kwa watu wengine kwamba unabii wa kweli ni lazima utolewa ‘angalau’ siku saba kabla ya kudhihirika kwa unabii huo. Ubarikiwe sana kwa hilo.

  Ndugu yetu Ck Lwembe ameishia wapi katika kujibu maswali ya ndugu John Paul? Nilitarajia nisome majibu yake ili nami niweze kuuliza vitu viwili vitatu kuhusiana na post zake. Nachelea kuuliza sasa kumbe labda ningepata majibu ndani ya majibu ya maswali ya John Paul. Naomba nieleweke kwamba sio namchokoza ndugu Ck Lwembe, bali mada hii ni muhimu sana kwa nyakati hizi na kwa kanisa la Tanzania, maana ni kipindi pekee ambacho manabii wengi sana wametokea katika nchi yetu.

  Jana nilikuwa nasikiliza Radio moja hapa Arusha inayomilikiwa na Nabii mmoja na ilikuwa inaendesha kipindi cha kutoa maoni kuhusu mafundisho ya nabii huyo. Kitu kilichonishangaza kama sio kunisikitikisha ni jinsi waliokuwa wanachangia au wanaongea kwenye radio hiyo walivyokuwa wanamu-address (wanamwita) nabii huyu kwa kuanza na “MHESHIMIWA MTUKUFU BABA NABII so and so”. Hili lilinishangaza sana, kwani ni lazima Nabii, Mchungaji, Askofu, Mwinjilisti, Mwalimu, Shemasi n.k.awe addressed kwamba yeye ni mheshimiwa mtukufu baba so and so?

  Tumefika mahali tunatafuta umaarufu wa kidunia badala kutafuta utakatifu kwa Mungu wetu.

 38. Wapendwa Kinyau na Patrick?

  Asante kwa kunitakia HERI YA MWAKA MPYA?

  Aidha, nawashukuru kwa kusoma maoni yangu kuhusu mada hii. Mungu awape upeo mkuu wa maandiko na uelewa pia.

  Kuhusu maswali na maoni yenu kuhusu hoja yangu juu ya “siku angalau 7″ haya yalikuwa maoni yangu tu.

  Hoja niliijenga katika mtazamo wa Maandiko na hali ya kawaida kabisa kwamba NABII anapaswa atoe UNABII wa mambo makubwa yajayo mbele ili kuwatahadharisha watu wa Mungu wajiandae au wachukue HATUA stahili.

  Siku saba nilizotoa hazina maana kwamba ndicho kipimo cha UNABII wa kweli. Unabii waweza kuwa kuhusu jambo litakalotokea kuanzia leo na kuendelea. UNABII unaweza kutimia hata baada ya miaka zaidi ya elfu.

  Hoja yangu ya siku 7 ILILENGA kuwatahadharisha watu kuhusu MANABII WA UONGO wanaoweza kujifanya manabii kwa kanisa wakaanza kuwatabiria watu mambo ambayo wamesoma magazeti ya Nje au Vijalida na vyombo mbalimbali vya habari huku wakijifanya MANABII mbele ya waumini wasiokuwa na upeo wala uwezo wa kupata habari za nje au ndani ya nchi. Zamani kuna watu walikuwa wanadhani Marehemu Baba wa Taifa hili Julius Nyerere ati ni NABII kwa sababu alikuwa akiwaeleza mambo kadhaa yajayo kumbe yeye ameyapata kupitia vyombo vya habari. Kutokana na kwamba wananchi wengi hawakuwa na TV au Magazeti ya Nje hawakuwa wanaweza kuyasoma walikuwa wanamwona Nyerere ni Nabii kwa sababu tu alieleza mambo kadhaa ya kisiasa au kiuchumi na yakatokea baada ya muda mfupi. Kwa mfano vyombo vya Habari vinaweza kutoa taarifa kwamba Marekani itaivamia Irani kijeshi mwezi ujao. Mwananchi asiyena taarifa hiyo aweza kudanganywa na Muhubiri anayejifanya NABII kwamba, ” NATABIRI KWAMBA MWEZI UJAO TAREHE MOJA MAREKANI ITAIVAMIA IRANI KIJESHI” na waumini wasiosikiliza vyombo vya habari watadanganyika kwamba ni kweli kumbe siyo.

  Wapendwa swala la siku saba naomba lisiwe mjadala saaaana kwani yalikuwa mawazo yangu tu hasa kwa kuzingatia kwamba kama ni UNABII unaohusu kwa mfano majanga makubwa, ajali, mafuriko, ukame, kimbunga, lazima unabii huo uje siyo chini ya siku saba ili watu wa Mungu wajiandae au wachuke tahadhari.

  Unabii wa kuhus kwa mfano, kupata mtoto kama mwanamke ni tasa. Lazima unabii huo uje kwa mlengwa siyo chini ya miezi 9 ambayo mwanamke hubeba mimba na ikakomaa. Nabii hawezi kutabiri kwamba utapata Mimba na kama majirahaya utakuwa na mtoto wakati mwanamke huyo tunamwona ana mimba tena ya miezi 5 au 7.

  Unabii kuhusu ukame hauwezi ukaletwa chini ya mwaka mmoja. Lazima uje kabla ya mwaka wa ukame kutokea au kufika. Ukitabiri kwamba mwaka 2012 kutakuwa na ukame mkali kabisa wakati watu wanaona kila mahali kuna mvua nyingi hadi mafuriko, UNABII huo utakuwa “fake”

  Unabii kuhusu RAIS ajaye Tanzania unafaa utolewe sasa hivi yaani kabla ya mchakato wa kupata wagombea katika vyama vya siasa haujaanza. Kama vyama vyote vitapitisha wagombea kisha akaja NABII akaanza kujifaragua kwa wakristo eti yeye ni NABII na anatabiri fulani ndiye atashinda UNABII wake ni utakuwa siyo SAHIHI bali BAHATI NASIBU. Tunahitaji Manabii kama wapo Tanzania Mungu awatumie sasa hivi kabla joto la uchaguzi mkuu wa 2015 halijaanza. Akitokea Nabii kwa sasa yaani mwaka huu 2012 au 2013 au 2014 akatabiri kwamba Ndugu OBED J MILINGA ndiye atakuwa Rais wa TANZANIA Mwezi Oktoba 2015 na ikawa kama alivyotabiri miaka 2 au 3 iliyopita HUYO NI NABII WA KWELI.

  Kama kesho ulikuwa unapanga kufanya safari ya ndege au basi au Meli na NABII akakutabiria kwamba au akakukataza kwamba usisafiri kutokana na kwamba safari hiyo itakuwa na ajali na watu wote watakufa, kisha wewe ukashupaza shingo na ukasafiri na ukapata ajali na kufa au kujeruhiwa sana, basi usimlaumu NABII bali jilaumu wewe na roho yako.

  Mwisho nawatakia kila la kheri na Mungu awabariki. Swala la siku lisiwape taaaabu bali ni maoni yangu tu. Mtu aweza kuyakubali au kuyakataa ndiyo maana nikasema neno, ANGALAU” ingawa naona watu kama Patrick wanadhani nimesema kwamba ni lazima litokee ndani ya siku 7. Hapana sikumaanisa hivyo. Maana yangu ilikuwa kwamba NABII LAZIMA ATABIRIE WATU MAMBO YAJAYO MBELE na hutegemea na swala lenyewe linalotabiriwa kwa mfano ukimtabiria mgonjwa kwamba ukimwekea mikono atapona ugonjwa unaomsumbua, ni lazima UNABII huo utimie “on the sport” au papo hapo siyo siku saba au masaa.

  Asanteni kwa changamoto zenu motomoto. Inaonesha watu wako makini.

 39. Napenda tuwekane sawa kwenye vipengele hivi:

  1. Siyo lazima kila nabii anaandike vitabu, tuna mifano mingi kwenye Biblia ya manabii ambao hawakuandika vitabu. Gadi, Nathani, Iddo, Agabo, Yuda, Sila, Yohana Mbatizaji, Eliya, Elisha n,k hakuandika vitabu.

  2. Siyo lazima anachotabiri nabii kiwe siku 7, inaweza kuwa hata muda mfupi zaidi au mrefu zaidi. Cha msingi lazima kitokee la sivyo Nabii huyo hakumsikia Mungu. Isaya alitabiri kuja kwa Bwana Yesu miaka 500 kabla ya tukio, si ajabu walimwona nabii wa uongo maana halikutimia wakati wao. Yohana mbatizaji alisema ajaye nyuma yangu ni mkuu kuliko mimi, akasema pia yeye ni sauti ya mtu aliaye nyikani itengenezeni njia ya Bwana, akimwongelea Bwana Yesu muda mfupi tu kabla ya Bwana Yesu kuja kubatizwa naye. Issue ni je yanayosemwa na nabii yatatimia au la.

  Blessings,

  Patrick

 40. Ndugu Millinga,

  Awali ya yote nikutakie Heri ya Mwaka Mpya wa 2012!

  Kimsingi nimesoma maelezo yako na ninakubaliana nayo kwa asilimia kubwa isipokuwa kwenye kipengere kimoja tu ambacho nahitaji ufafanuzi wako. Kipengere hicho ni hiki ulichoandika kwamba;

  “Nabii lazima atabiri mambo yajayo angalau siku 7 zijazo mbele. Matukio makubwa yanayokwenda kulikumba kundi au mtu au taifa au kiongozi mkuu wa Taifa. Kama Nabii hatabiri mambo makubwa yanayolihusu taifa kisiasa, kiuchumi, kifedha, kijamii, nk huyo siyo NABII. Huyo naweza kumwita ni Mwinjilisti mwenye karama ya Unabii siyo HUDUMA YA NABII”

  Ufafanuzi ninaoutaka toka kwako ni huu;

  1. Je huu muda wa ‘angalau’ siku saba ni kibiblia au ni mawazo yako tu? Kama ni kibiblia wapi pameandikwa hivyo?

  2. Je Nabii anatabiri mambo kwa utashi wake (kufuatana na hoja yako ya muda wa angalau siku saba)au anasema kile Mungu alichoongea au kumwonyesha huyo Nabii? Je Mungu ana mpaka na muda? Je ikitokea Mungu akamweleza Nabii jambo la muhimu sana tena kubwa mno kitaifa na kimataifa na jambo hilo linakiwa litokee siku moja ijayo, huyo Nabii akae kimya asilisema kwa sababu ni chini ya siku saba?

  3. Kufuatana na hiyo hoja yako ya ‘angalau’ siku saba mbele, je utatueleza nini juu ya Ibrahimu alipoletewa taarifa na Mungu ya kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora chini ya masaa ishirini na manne? (soma Mwanzo 18:16-33 na Mwanzo 19:1-28). Hapa tunaona Ibrahimu akipewa taarifa ya kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora jioni na kesho yake asubuhi tayari miji hiyo ilikuwa imewaka moto!! Je Ibrahimu angewapa taarifa watu wa Sodoma na Gomora kwamba kesho yake wataangamia kwa moto, huo usingekuwa unabii credible kwa kuwa ungekuwa umetolewa chini ya siku saba?

  Kwa kumalizia kuhusu utata huu niliouona kwenye comment yako ni kwamba Mungu anaweza kuongea na nabii wakati wowote hata kama jambo hilo litatokea muda mfupi ujao. Ni wajibu wa nabii wa kweli kuisikiliza sauti ya Mungu na kuwafikishia watu wake ujumbe huo kama alivyoupokea toka kwa Mungu bila kujali ni muda gani. Na sisi tunaousikia ujumbe huo ni wajibu wetu kuupokea ujumbe huo na kuufanyia kazi.

  Ubarikiwe na Bwana,
  Ni mimi,
  Haggai Abel Kinyau.

 41. Brother John Paul,

  Shalom!

  Kwanza kabisa nikushukuru kwa uvumilivu wako! Pili, niseme kuwa sikuwa na nia ya kuendelea kulizungumzia jambo ambalo tumekubaliana kuliahirisha, bali kwa mtazamo wangu, niliona kana kwamba ulipoliahirisha, kuna vipengele fulani vya msingi ambavyo ulikuwa umevipeleka katika conclusion kiasi kwamba nikalazimika kuvirudisha vining’inie tena, ili iwe rahisi kwetu sote tutakapokuwa tayari kuendelea na majadiliano. Unisamehe kwa kukukwaza!

  Kuhusu Fundisho la Mitume, kama nilivyokuambia hapo awali, hili litaturahisishia sana kuifikisha mada hii tunayoiongelea katika kipeo chake, kwani ndiyo muhimili wa Ukristo wetu.

  Shauku ya kujua jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo ni kubwa kwa watu wengi, ukitilia maanani wingi wa sauti tofauti tofauti zinazotuitia wokovu kutoka kila kona ya mtaa, hata wakati mwingi tunachanganyikiwa na mwishowe tunalazimika kujiunga na kambi mojawapo ili tusionekane kama watu tusio na msimamo. Lakini ukweli ni kwamba wengi wetu hatujui hata ‘UKIRI’ wa hayo makusanyiko tuliyomo!

  Fundisho la Mitume linaanza kuonekana katika kuzaliwa kwa Kanisa. Kanisa, lilipozaliwa kwa Injili ya Bwana Yesu Kristo ndipo lilipowekwa katika Fundisho hilo nalo likadumu katika hilo (Mdo 2:41-42). Kwa hiyo kwa kifupi, INJILI, kama ilivyo katika AGANO JIPYA ndilo FUNDISHO LA MITUME. Narudia, Injili yote na sio vipande vya injili. Kwa hiyo kanisa linapaswa kudumu katika maonyo na mafundisho yaliyomo humo ili liwe na haki ya kujitambulisha na Kristo.

  Hebu tuyaangalie kwa uchache tu sehemu ya hayo katika ulinganishi na mafundisho yaliyopo:
  Biblia inafundisha:

  1. MWANAUME ASALIPO NAYE AMEKIFUNIKA KICHWA CHAKE ANAMUAIBISHA
  KRISTO (1Kor 11:1-16).
  Haya, ni maaskofu wa madhehebu mangapi wanaovaa ile mikofia ya kiPapa pamoja
  na Papa mwenyewe leo kinyume na hilo Andiko?

  2. MWANAMKE ANAPOSALI AU KUHUTUBU AFUNIKE KICHWA CHAKE, TENA
  BIBLIA INA AINISHA KUWA KIFUNIKO HICHO CHA KUFUNIKIA KICHWA CHAKE
  AMEPEWA, NYWELE NDEFU!
  Haya, wengine hawajui hata kama kuna Andiko hilo. Utawaona wanawake
  wamenyoa vipara, wengine wamekata punky nk. Wengine wamejitafsiria wanavyojua
  wenyewe kwa hiyo wamewafunga vitambaa kichwani. Yote yakiwa kinyume na
  Maandiko.

  3. SIMPI NAFASI MWANAMKE KUFUNDISHA WALA KUMTAWALA MWANAUME
  (1Tim 2:12-14).
  Je, ni wanawake wangapi leo wanasimama mimbarani kulifanya hilo walilokatazwa?

  4. ASKOFU AWE MTU WA MKE MMOJA… (1Tim 3:1-7)
  Je, ni maaskofu wangapi leo hawana wake, au wako chini ya watoto wao, au
  wapenda fedha?

  5. BIBLIA INASEMA MWOMBEZI NI MMOJA TU YESU KRISTO (Ebr 7:22-25)
  Je, ni makundi mangapi yaliyojiwekea njia nyingine kupitia watu waliokufa!

  6. MEZA YA BWANA INAHUSISHA PIA TENDO LA KUOSHANA MIGUU.
  Je, ni makusanyiko mangapi yanayotimiza hiyo physical commandment?

  7. ISHARA HIZI ZITAFUATANA NA WAAMINIO, KWA JINA LANGU WATATOA
  PEPO, ..
  Ni makundi mangapi yasiyoamini katika uponyaji wa kimiujiza? Hata wengine
  wameweka Fundisho kuwa Ishara hizo zilikoma na mitume!

  8. MNAPONENA KWA LUGHA, AWEPO MTAFSIRI, …
  Ni makusanyiko mangapi leo yanajinenea ovyo tu bila kuzingatia agizo hilo? Hata
  wametengeneza Fundisho lao la kunenea wanasema eti kanisa linajifurahisha!

  9. BIBLIA INAFUNDISHA YA KUWA IMANI NI MOJA, TENA WALIKABIDHIWA
  WATAKATIFU MARA MOJA TU!
  Leo ni makusanyiko mangapi yanayokiri imani nyingine inayoitwa ‘Imani ya Nikea’
  yaani UNIKOLAI!

  10. BIBLIA INAFUNDISHA KUWA KUNENA KWA LUGHA NI KIPAWA CHA ROHO
  MTAKATIFU.
  Je, ni makusanyiko mangapi yaliyojifunga katika Fundisho la uongo lisemalo
  ‘Kunena kwa Lugha ni Ishara ya Kujazwa Roho Mtakatifu’, hata tunawaona walimu
  wakiwafundisha jinsi ya kunena?

  11. BIBLIA INAFUNDISHA KUWA UBATIZO WA ONDOLEO LA DHAMBI HUFANYIKA
  KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO, KATIKA MAJI MENGI.
  Je, ni makusanyiko mangapi ambayo yanayo wanyunyizia maji waumini wao, na
  mengine kuwazamisha kweli, lakini ‘kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
  kinyume na Fundisho hilo?

  Nisikuchoshe, kwani msururu ni mrefu sana, bali kwa vipengele hivyo vichache, kwa kuanzia, waweza kuwapitisha hao Manabii na madhehebu yetu katika hilo chujio, ili kuujua ukweli wa madai yao ya kumwakilisha Kristo. Huo ndio urahisi wa Neno la Mungu. Kuyaona hayo hauhitaji kuwa na degree bali moyo mnyofu!

  Basi naona niishie hapa nikiamini kuwa nimebaki ndani ya wigo kama ulivyonitaka.

  Bwana atujalie Uzima na Hekima yake!

 42. Wapendwa,

  Naomba niwashukuru wote walioeleza juu ya mada hii. Nimesoma michango ya wengi inafurahisha na kuelimisha sana.

  Naomba nijikite zaidi kwenye mada kwani huu ni mchango wangu wa kwanza katika mada hii.

  Kwanza maana ya Nabii. NABII ni mtumishi wa Mungu kama ilivyo mchungaji, Mwalimu au Mwinjilisti. Hakuna tofauti katika ukubwa wa utumishi au tuseme seniority. Wote wako sawa mbele za Mungu.

  Hapa Tanzania huduma ambayo imekumbatiwa sana na wengi ni Uchungaji. Hata kama wewe ni mwinjilisti au Mwalimu wa Biblia utajikuta unabatizwa jina la Mchungaji. Ni nadra sana kuitwa Nabii.

  Tangu zamani Manabii walikuwa ni Jicho la kuona mbali kwa watawala au wafalme. Manabii walitumiwa na Mungu kuonya kuhusu yajayo mema au mabaya katika taifa la Israel. Manabii wote wakubwa na wadogo walitoka katika KIZAZI CHA SHEMU na baadaye Abrahimu na Isaka. Manabii wote wanaotambuliwa katika Maandiko walitokea mashariki ya Kati au Israel.

  Waislam wanaamini kwamba Nabii lazima awe ni mtu aliyetumwa na Mungu na ni lazima aandike Waraka au Kitabu chenye ujumbe wa Mungu. Wanatoa mifano ya Yesu, Musa, na Mhamed S.A.W kwamba wote wanvyo vitabu walivyoandika/kuandikwa ujumbe waliouleta. Waislam wanaendelea kusema kwamba tangu Nabii Issa aondoke ni Nabii Mhamad pekee aliyetumwa na Mungu akitokea katika Uzao wa Abraham upande wa Ishimail aliyezaliwa kwa Hajiri Mmisri baada ya kupewa kibali na mkewe kumwingilia mjakazi wake Abraham.

  Waislam nilioongea nao wanaamini kwamba hakuna Nabii zaidi ya Mhamad atakayekuja tena. Hii ni mitazamo ya kiislam.

  Wakristo wengi wanaotumia haya maneno: MTUME, NABII, MWALIMU, MCHUNGAJI, MWINJILISTI hunukua maandiko yasemayo; Mungu alitoa vipawa akawapa wengine kuwa Mitume, Manabii, Wachungaji, Wainjilisti na Walimu.

  Hoja hujengwa kwamba kanisa la Kristo limejengwa juu ya Huduma TANO. Huduma hizo ni; MITUME, MANABII, WACHUNGAJI, WALIMU NA WAINJILIST.

  Pamoja na kuyafahamu maandiko haya Makanisa mengi yameendeleea kudhania kwamba huduma pekee zilizopo ni UCHUNGAJI kwani ndio unaotukuzwa sana ama mtaani au makanisani mwetu kiasi kwamba kila mtu hujisikia vizuri akiitwa Mchungaji. Kwa mfano Mtu aliyezoea kuitwa Mchungaji hata kama kipawa chake ni MWALIMU kuna makanisa mengine ukikosea tu ukamwita kwa cheo au jina hilo, unaweza kupewa adhabu.

  Hata hivyo, mkanganyiko huu umekuwa unaonekana sana Tanzania au Africa zaidi ukilinganisha na mataifa mengine kama Marekani, Ulaya na Asia.

  Kisaikolojia watu huathiriwa na mazingira yao au nyakati au ulimbukeni wa maswala mbalimbali ya kijamii, akademia na uchumi au siasa. Kwa mfano Tanzania watu wengi wanadhani au kuona kwamba kama wewe ni Askofu wa kanisa usipovaa KOLA NYEUPE hupati heshima mbele ya watawala au Jamii. Huu ni ulimbukeni ulitokana na kuwaiga Maaskofu wa Katholiki na makanisa ya Kiprotestanti. Makanisa ya kipentekoste Wachungaji na Maaskofu wote walivaa TAI tu hawakuvaa KOLA NYEUPE shingoni. Kwa sasa wewe kama ni Mchungaji au Askofu na huvai KOLA nyeupe shingoni unaonekana kama vile siyo Mtumishi. HII YOTE NI MITAZAMO.

  Mtazamo au mitindo mingine iliyokuja baadaye ikawa kila mtu anayeanzisha kanisa kupenda aitwe kwa cheo cha ASKOFU na wengine ASKOFU MKUU. Wengine unakuta hata wakiwa na matawi mawili tu au kanisa halina hata tawi moja la kanisa hilo tayari wakawa wanajiita ASKOFU MKUU. Yote haya ni mitindo ya kuiga na kudhani kuwa ukiitwa hivyo ndipo utapata heshima katika Jamii.

  Miaka ya kuanzia 1990 Hivi enzi zile akina Danstan Maboya wanavuma sana Tanzania, enzi zile za “Jesuuuuus…..Power……” ndipo vyeo vya Mtume na Nabii vilipoanza kujitokeza. Akina Danstan Maboya wakaanza kuitwa MITUME. Kulikuwa na maelezo ya kwa nini wanajiita Mitume. Wanasema ilikuwa ni kutokana na jinsi walivyofungua makanisa mengi ya madhehebu yao na kutumiwa kwa miujiza sana ikilinganishwa na watumishi wa Mungu wengine waliokuwepo miaka hiyo. Nakumbuka mwaka 1993 hivi Danstan Maboya alipokuja Tabora ilikuwa ni kivumbi cha maajabu ya POWAAA, JESUS hadi akawachanganya wachungaji wa makanisa mengine kama TAG, EAGT, PENTEKOSTE, FGBF, nk.

  Vyeo vya kuitwa au kujiita NABII vimeanza kuvuma miaka ya karibuni kuanzia mwaka 2000s hivi. Makanisa mengi hasa DAR yalianza kulipuka na mikesha mikubwa, maombezi ya miujiza, kufunguliwa katika laana, matangazo makubwa Redioni, TV, Magazeti na mikutano mikubwa ya hadhara. MANABII ndipo wameanza kutokeza kwa sana. Kama nilivyoeleza tangu mwanzo watanzania wengi huvutwa sana na hisia au mkumbo kuliko utafiti na ukweli wa mambo. Kutokana na jinsi ilivyo sasa hivi, wote wanaojiita au kuitwa MANABII wametokea kuwa watu wa pekee katika jamii ya makanisa yetu kiasi kwamba wana mvuto mkubwa sana wa kuvuta umati mkubwa wa watu na jamii tofauti na ilivyo kwa wale wajiitao au waitwao WACHUNGAJI, ASKOFU, MTUME, MWALIMU au MWINJILISTI. Kutokana na hali hii, kila mtu anayeanzisha huduma mpya kisaikolojia (hata kama hana Huduma ya NABII) anadhani akitumia cheo hicho atapata Mvuto mkubwa sana kwa watu. (This is just a pyschological mind sets).Ni ugonjwa wa kujitakia vyeo hata kwa asiyestahili. Watu wanaumwa ugonjwa wa kutaka vyeo visivyokuwa vya kwao. Kila mtu anadhani akiitwa NABII ndipo anakuwa kweli mtumishi sahihi wa Mungu. Sickness. Dangerous to the Church of Christ.

  Kuna tatizo au “Syndrome” nyingine imeibuka sasa hivi ya ajabu sana. Kila mchungaji sasa hivi anakimbilia kusoma ili aanze kuitwa “Doctor” fulani. It is another pyschological academic problem among Church Ministers). Kila mtu anataka aitwe, “Dr. so and so”. Huwa nashangaa sana. Mtumishi unakuta anaitwa; Askofu Dr. Kichwa Mkia. au Mhe. Dr. Mch. Katubuka Sunuka. “This is a Doctorate sickness syndrome” among church leaders. Kwamba kama wewe siyo Doctor hupati heshima katika dunia ya leo. Hii imefanya watumishi wengine kuingia majaribuni kutaka kupata “Doctorate Degree fake” toka Vyuo vikuu hoi au fake.

  Naomba sasa nimalizie kwa kutoa maelezo ya kazi za Manabii wa Sasa (kama wapo):

  1. Nabii lazima atabiri mambo yajayo angalau siku 7 zijazo mbele. Matukio makubwa yanayokwenda kulikumba kundi au mtu au taifa au kiongozi mkuu wa Taifa. Kama Nabii hatabiri mambo makubwa yanayolihusu taifa kisiasa, kiuchumi, kifedha, kijamii, nk huyo siyo NABII. Huyo naweza kumwita ni Mwinjilisti mwenye karama ya Unabii siyo HUDUMA YA NABII.

  Kama kuna mtu anajiita NABII hapa Tanzania lakini hajawahi kutabiri maswala ya Kitaifa na yakatokea kama alivyonena NABII huyo, basi huyu siyo NABII. Endapo taifa linakumbwa na jambo kubwa zito kwa serikali na kanisa na NABII tuliyenaye au MANABII tulionao HAWAJATABIRI kuhusu maswala hayo; Huyo SIYO Nabii au hao SIYO MANABII. Ni wachungaji au Walimu tu watu wa Mungu. Taifa lolote ambamo kuna NABII au MANABII, lazima kabla halijatokea jambo katika taifa NABII au MANABII watajulishwa angalau siku 7 kabla ya tukio.

  Mfano ni Maandamano yanayotokea Nchini Nigeria kwa sasa. Mtumishi wa Mungu T.B Joshua aliyatabiri kama yanavyotokea nchini mwake tarehe 16/10/2011. Kwa wale wanaotazama Emanuel TV watakubaliana nami kwamba TB Joshua amekuwa akitabiri mambo kadhaa nchini mwake hata nchi za nje na yanatokea kama alivyotabiri likiwemo lile la Vijana wa London kuandamana, Uchaguzi Mkuu wa Nigeria 2011, Mpira wa Miguu wa kombe la dunia, hali mbaya ya uchumi na mtikisiko wa uchumi.

  Sijui kama hapa Tanzania MANABII au NABII aliwahi kutabiri lolote likatokea kama alivyotabiri. Nakumbuka tu mwaka fulani wa Uchaguzi Mkuu Tanzania Askofu Mmoja wa kanisa moja DAR alimtabiria mgombea fulani wa chama cha upinzani kwamba angeshinda uchaguzi na kuwa Rais wa Tanzania lakini haikutimia. Hadi leo hajaliambia kanisa ni kwa nini ule Unabii haukutimia kama alivyotabiri na kuingia hadi kwenye kampeni za kumpigia debe MTABIRIWA yule.

  2. Nabii lazima atabiri mambo yanayohusu Mataifa mengine. Kama NABII kweli lazima atatabiri mambo yajayo ulimwenguni au katika Taifa fulani hata kama siyo taifa lake. NABII YONA ni mfano wa hilo.

  3. Nabii lazima awe mwandishi wa vitabu Vyenye Maneno ya Mungu. SIYO KITABU bali VITABU. Kama Nabii haandiki vitabu vyenye ujumbe wa Mungu au ufafanuzi wa mambo mbalimbali katika maandiko au maisha, huyo siyo NABII. Ni mwinjilisti au Mchungaji tu. Hata hivyo siyo kila anayeandika vitabu anakuwa NABII.

  4. Nabii lazima ataishi maisha ya kawaida. Hataishi maisha yenye makeke na mikoko na ufahari. NABII ataishi maisha ya kuhurumia watu wengine. Tazama Mfano wa Nabii YONA, ELIYA, JOSHUA, MUSA, nk. Hawakuwa na maisha yenye kujikweza wala kunia makuu kama tuwaonavyo hawa watanzania waliojaliwa “Kuitwa” au “Kujiita” MANABII. Kuna NABII mmoja nasikia kila aendako analindwa na lundo kubwa na WALINZI kuzidi hata Rais Kikwete au Obama. Msururu wa magari na watu wa Usalama wamemzunguka kila kona na hakuna mtu anayeruhusiwa hata kumgusa au kumsalimia. SIJUI MFUMO HUO WANAPOUIGA AU KUUTOA. Manabii wa Tanzania wanapenda maisha ya kifahari sana. Wanapenda waishi katika majumba makubwa, wawe na magari makubwa na ya kifahari, wanataka walale katika Hotel za Hadhi ya Marais au Hote ya Nyota Tano. Wanaposafiri wanataka wapande Ndege katika daraja la Kwanza au “Business Class au Executive Class”. Hawa ndio Manabii wa Kitanzania. Sijui kama kuna Manabii wanyenyekevu na wasionia makuu hapa Tanzania. Kama wapo naomba wewe unayesoma maoni yangu unitajie watu hao. “Manabii wa Kitanzania” wanatamani kuonekana kwenye TV hata kama hawana agenda yoyote ya maana ya kurusha hewani kwenye TV. Utakuta Mtu anajiita NABII anahubiri kwenye TV mambo ya kawaida na yasiyo na uzito wowote kwa taifa na kanisa na kuombea wagonjwa tu. Wengi hutumia TV ili kuji”promote” tu wao na makanisa yao ili kuvutia watu zaidi waongozeke makanisani mwao.

  Nabii asiyekuwa na unyenyekevu hata kujishusha kuishi kama watu wa kawaida, kusaidia watu wanyonge na wahitaji wa kimwili, kifedha na kisaikolojia; HUYO SIYO NABII bali ni MCHUMIA TUMBO tu Mungu wake ni TUMBO.

  5. Nabii wa Mungu lazima atabiri mambo mbalimbali na yatokee kama Bwana Mungu alivyomwonesha. Yasipotokea vilevile kama alivyosema, huyo NI NABII WA UONGO aliyetabiriwa na Kristo kwamba nyakati za Mwisho watatokea Manabii wa uongo sana.

  Mungu akubariki sana.

  Ndimi,

  Obed Venerando Milinga.

 43. Ndugu Ck Lwembe,

  Nashukuru kwa majibu yako. Lakini kuna jambo ambalo NILIOMBA TULIACHIE HAPO lakini wewe umeliandika tena. Na katika kuliandika umeleta hoja nyingine ambayo kwa kweli siwezi kuinyamazia maana naona inanipeleka mbali kutoka ambako tulikuwa tumefika.

  Lakini kabla ya kuendelea na MAJIBU uliyonijibu sasa NINAKUOMBA TWENDE KWENYE SWALI LA MSINGI halafu tukimaliza hapo ndipo tutarejea kwenye hilo suala la Eliya ajaye pamoja na mengine yaliyojitokeza. Nimeona nivute subira nyingine tena kwa sababu majibu yako yameniacha hewani kabisaaaa! Kwa kuwa nimeshindwa kabisa kuelewa kama aliyejibu ndiye yule aliyeandika ile paragraph ambayo niliinukuu na nikauliza maswali kutoka katika hiyo!

  Lakini kwa sasa, hebu nawe nakuomba uvute subira na baada ya kufanya hivyo UJIBU SWALI LA FUNDISHO LA MITUME AMBALO KANISA LIMELIACHA na kile ulichosema kuwa jibu la swali hilo utaambatanisha nacho ambacho ni NAMNA YA KUWATAMBUA MANABII WA UONGO.

  Ninakusihi uandike majibu ya hayo tu niliyokuuliza ili tujadili hapo halafu ndipo tutaendelea na hayo mengine.

  Nashukuru kwa kuwa umenielewa na utajibu TU hayo niliyokuomba kufanya hivyo:

  Asante sana!

 44. Ndugu yangu Orbi!!!!!

  Manabii hao wanakimbia washike, wachinje, asiokoke hata mmoja.
  1fal 18: 40

  Shalom

 45. Wapendwa, Shalom.

  Nilikuwa nje ya mtandao huu wa internet kwa muda sasa baada ya kuwa kwenye likizo ya Krismasi na mwaka mpya, nadhani wote tunajua vijiji vyetu (kwa wale wanaotoka vijijini kama mimi) vingi bado havina mawasiliano haya ya kisasa achilia mbali simu za viganjani.

  Naendelea kuufuatilia mjadala huu hasa post za ndugu yangu Orbi na CK Lwembe na hatimaye ndugu yangu John Paul na Ck Lwembe. Mjadala ni mzuri ingawa kuna mahali ndg Ck Lwembe ananichanganya kama sio kunitia mashaka na kile anachoongea. Acha kwanza kwa leo niishie hapa mpaka hapo baadaye ikiwezekana nitaomba ufafanuzi kwake kwa mambo kadha wa kadha ambayo amekwisha kuyaandika.

  Hongereni nyote kwa ukomavu wenu wa kiroho na Herini ya Mwaka Mpya wa 2012.

 46. Ndg John Paul,

  Asante kwa kunivutia subira KUUUBWA!

  Yote uliyoyasema nimeyaafiki. Mwendo tunaokwenda nao nauona ni mzuri, kwani wakati mwingi kasi kubwa ina athari zake.

  Kabla ya kusonga mbele katika hatua nyingine, napenda kuongeza ufafanuzi kidogo tu katika muhtasari ulionipa kwenye kile kifungu na. 3 kuhusu “Hakuna awezaye kuokoka bila Huduma ya Nabii Eliya Ajaye.” Swali uliloniuliza na jibu nililolitoa, kimsingi vinabaki hivyo katika maana ya kuokoka. Ninachopenda kukiweka wazi zaidi ni kwamba huyo nabii Eliya ajaye, haji nje ya Maandiko bali ndani ya Maandiko, hivyo ujumbe anaokuja nao ni sehemu ya Injili. Kwa hiyo, hiyo Injili inayookoa leo chini ya Neema, kadiri Mungu mwenyewe alivyoiweka, Injili hiyo itabadilika katika ujio wa Eliya maana atarejesha yote yaliyopotoshwa. Labda leo unaweza kuokoka kwa injili ya “Maria mama wa Mungu utuombee sasa na saa ya kufa kwetu” lakini akija Eliya ataiondoa injili hiyo na kuirejesha ile halisi ambayo muombezi ni mmoja tu, Yesu Kristo! Basi baada ya hapo yeyote atakaye endelea na hiyo injili ya “Maria mama wa Mungu…” hata okoka!

  Sasa nitaendelea kuijibu ile sehemu iliyobakia, pia kama nilivyokueleza, kuhusu Fundisho la Mitume, jibu lake nitalijumuisha katika majibu nitakayokupa kadiri tunavyoendelea.

  2. Je, ni sawa kusema kuwa “Kila aliyebatizwa kwa jina lake Bwana Yesu Kristo” tayari ana ROHO YA UNABII NDANI YAKE? Hapana, bali kila anayebatizwa hivyo huingia katika Ukristo. Navyo vipawa Mungu huvigawa kulingana na mapenzi yake.

  3:1 ‘Mchungaji’ kwa upande mmoja, katika ulinganishi na ‘Nabii’ au ‘Mtume na Nabii’ kwa upande mwingine, basi hawa wakiwa ni wale watumishi wa mshahara (Yhn 10:12 “Mtu wa mshahara, wala si mchungaji,…”), ili kuwavuta kondoo wengi kwao, wamejivika HUDUMA YA UNABII ili kuwaleta watu chini yao katika tegemeo kuu la kupata mawasiliano na Mungu moja kwa moja juu ya shida na matamanio yao mbali mbali, badala ya kumngojea mchungaji na mahubiri yake ya Injili. Kwa hiyo uchungaji hauwezi kuwa kivutio tena katika kuimarisha kundi la hao wa mshahara ndio maana unawaona manabii utitiri na sio wachungaji utitiri!

  3:2 Mafanikio ya KIHUDUMA ambayo kwa kanisa hili yanaishia katika maslahi binafsi, ni kwamba ukiwa NABII/MTUME, kutokana na kuwavuta watu wengi, hilo huleta sadaka nyingi zaidi, nayo mafanikio yake huonekana mwilini katika ufahari na utajiri kuliko mchungaji ambaye amejichelewesha katika cheo hicho hivyo atasota saaana!

  3:3&4 Unabii/Utume unaoendelea sasa hivi ni shughuli ya kujiajiri, ambao ndio UJASIRIAMALI wenyewe, ila hawa bidhaa wanayoshughulika nayo ni Injili au kwa usahihi zaidi, bidhaa hiyo ni roho za watu!

  3:5 Kambi ziko mbili tu. Kuna ya Kristo na ya Mpinga Kristo. Kwa hiyo kwamba roho ndizo zitendazo kazi ndani ya watu, basi wanaochomoka si watu bali ni roho, ila kwa vile roho hizo hujiwakilisha ndani ya watu ndio maana nikasema, “Mtu akichomoka…”. Kwa hiyo, kulingana uhalisi wa kinachoendelea kama tulivyokileta katika kipimo cha Maandiko, na kutuonesha kuwa ni UJASIRIAMALI, basi roho hizo huchomoka kutoka kambi ya Mpinga Kristo, 1fal 22:20-22 “BWANA akasema, ni nani atakaye mdanganya Ahabu, ili akwee Ramoth-Gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. Akatoka pepo, akasimama mbele za BWANA akasema, mimi nitamdanganya. BWANA akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. “

  3:6 “ Watu watamuelewa” ni phrase au msemo unafanana na ‘Aminia babaake” ambayo huonesha kuaminika kwako kwa wafuasi wako na wanaoshawishika kukufuata.

  3:7 Katika ujasiriamali, au biashara yoyote ile, ni lazima uangalie mahitaji ya watu ndipo uweze kuifanya biashara. Danieli nabii, Mungu alimpandisha juu kisha akamuacha aitazame siku yetu ya leo, ambapo aliiona kasi ya maendeleo ya siku za mwisho. Maendeleo huja na pressure katika mifumo ya maisha. ili ku catch-up, watu huhangaika hapa na pale lakini vikwazo na nguvu ya umasikini ni kubwa. Nao MANABII wakiwa na majibu yake katika urahisi, ndipo biashara inaponoga hata muda wa Injili katika maana ya KUOKOKA na UTAKATIFU huwa haupo na mwishowe huondoka kabisa katika programu zao!!!

  3:8 Miujiza inachangamsha! Kama uliwahi kuhudhuria ile mikutano ya November Crusade enzi za akina Roy Durman, itakuwa rahisi kwako kuuona uchangamfu unao wapata watu miujiza inapotendeka, hata leo makusanyikoni mwetu kuliko na miujiza watu wanachangamka, pita kwa mchungaji Gwajima uone watu wanavyo dai mali zao!

  3:9 Kila mtu anapata anachotaka! Watendaji/ watumishi wote wako uwanjani, Ukimtaka Mungu yachunguze Maandiko uone iwapo huduma iko sawa nayo. Naye Mungu aichunguzaye mioyo yetu huwajibika kwa hilo. ATAKUONGOZA!!!
  Ukitaka mali au utajiri au ufahari au mambo ya mwilini na matamanio yake, basi injili yake pia ipo, nayo utapewa na kuongozwa huko!!

  Ndugu yangu, nimejaribu kuyajibu maswali hayo yaliyobaki, nimeliacha lile la Fundisho la Mitume ili jibu lake liweze pia kuunganisha Jinsi ya Kuwatambua Manabii wa Uongo, kwani Fundisho hilo ndilo linalo watenganisha.

  Asante sana,

  Bwana na atujaze Furaha Yake!

 47. Ndugu Ck Lwembe,

  Nashukuru kwa ufafanuzi wako wa Kina. Kuna mambo ambayo nilikuwa nayatafuta ii nijue msimamo wako juu ya hayo. Sasa naomba kufupisha kama ifuatavyo:

  Katika maswali niliyokuuliza, nashukuru majibu yake yote umeyapanga kwa mtiririko ambao niliuliza. Hii inapendeza sana na inatupatia nafasi ya kwenda sambamba.

  Ufuatao ni muhtasari wa nilivyoelewa na kama kuna ufafanuzi zaidi unaohitajika.

  1, Karama ya unabii inatenda kazi ndani ya Kanisa la Kristo kupitia Manabii wa makusanyiko madogo madogo. Ila Huduma ya Unabii, kwa kiwango kinachovuka mipaka ya makusanyiko madogo kwa sasa haipo!

  2. Suala na Nabii Elia Ajaye nimesoma ulivyoandika. Lakini bado kuna ufafanuzi zaidi. Lakini pamoja na hivyo nimeona niliachie hapo. Natumaini tutapata muda mwingine ili tulijadili peke yake, maana naona sasa litachukua nafasi ndefu na muda mwingi huku lengo mdingi mkuu wa mada ni Kufahamu kama kuna manabii, Kazi zao ni nini na Tunawezaje kuwatambua! Kwa hiyo nimevuta subira KUUUBWA ili tuendelee na mada. Maana najua wengi wanafuatilia mada,sasa nikiwa mbinafsi sana haitakuwa vema. Naomba na ninashauri hili tuliache kwanza. Natumaini tutapata muda mwingine mzuri huko mbele!

  3. Kuna mahali uliandika kuwa Hakuna awezaye kuokoka bila Huduma ya Nabii Eliya Ajaye. Nami nikakuuliza kuwa Je, ina maana sasa watu hawaokoki? (yaani hadi hapo Huduma ya Nabii Eliya ajaye itakapokuja?] Na katika jibu lako umesema kuwa INJILI NDIYO INAYOOKOA. Hilo ni tumaini jema kuwa KUMBE WATU SASA WANAOKOKA TU. Kwa hiyo naona tunaachana na DHANA kwamba “Hakuna kuokoka hadi huduma ya Eliya Nabii ajaye! Bali Injili iendelee kuhubiriwa maana ndiyo IOKOAYO WATU na SIYO HUDUMA YA NABII ELIYA AJAYE!

  4.Nashukuru kwa maelezo yote mengine, ikiwa ni pamoja na kufafanua upofu wa kanisa pamoja na ule mfano wa Sodoma. Ila suala la FUNDISHO LA MITUME nalo limebakia. Sasa hili utalijibu ambapo utaona inafaa kufanya hivyo, kama ulivyosema litaandamana na namna ya kuwatambua manabii hao wa Uongo!

  Natumaini umeyapitia hayo na kama kuna mahali labda nimepeleka vingine unaweza kuweka sawa, safari hii kwa namna ya kumalizia, ili tuendelee kwenye yale maswali yaliyobakia katika maoni yangu ya tarehe 29, Dec, 2011. Lakini kama utaona hakuna la kuongezea hapo basi unaweza kuacha tu kisha ukaendelea kujibu yale maswali yaliyobakia, na ambayo nimeona nitayasogeze hapa karibu, kama yafuatavyo:

  ******************************

  2. Wakati unamjibu ndugu Orbi ulisema namna moja wapo ya kumtambua “Mtume na Nabii” wa kweli ni kama “Kabatizwa kwa maji mengi” jambo ambalo mahali pengine umeliita “Kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo”. Halafu katika maoni yako ya mwisho umemuandikia ndugu Orbi yafuatayo:

  “Nenda ukabatizwe kwa jina la Bwana Yesu Kristo upewe ‘EYE SALVE’ utayaona yote na mengine mengi kwani sasa utakuwa ni MKRISTO, vinginevyo , manna utapewa ili uishi muda wako lakini muda wako wote utakuwa ni wa kuzunguka jangwani!!!”.

  Kama nimekuelewa vizuri maneno hayo YANA MAANA kila mtu “Aliyebatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo huwa ana uwezo wa kuyaona yote na mengine [kwa kuwa akibatizwa anapewa EYE SALVE]. Kama nilivyokuelewa ni sahihi:

  Je, ni sawa kusema kuwa “Kila aliyebatizwa kwa jina lake Bwana Yesu Kristo” tayari ana ROHO YA UNABII NDANI YAKE?

  3. Ninanukuu:

  “Halafu tatizo lako jingine ndugu yangu Orbi, huendi na wakati. Hivi wewe kwa mawazo yako unadhani uchungaji ni jambo la kujivunia katika mafanikio ya kihuduma? Uchungaji ni kazi ya kuajiriwa! Wachungaji wameajiriwa huko Katoliki au Lutheran nk. Kwa wajasiriamali wa Injili, unachomoka na Unabii au Utume au vyote ‘Mtume na Nabii’ hapo ndio watu wanakuelewa. Watu wenyewe kwanza wanataka miujiza. Kama hauna hata kamuujiza kakuwachangamsha kama haya makanisa ya zamani basi wapige hata na muujiza wa majengo makubwa ya kifahari watakuelewa!”

  Ndugu Lwembe mimi Nimesoma maneno hayo niliyonukuu nikapatwa na maswali mengi sana. Nitauliza kwa uchache na nitaomba unijibu kwa mtiririko niliyouliza ili niweze kufuatilia vizuri:

  1.Kutokana na “wakati” uliomuambia ndugu Orbi haendi nao Je, unamaanisha “UCHUNGAJI” ni huduma ILIYOPITWA NA WAKATI?

  2. Ni “mafanikio” gani ya “KIHUDUMA” ambayo atayapata mtu akiwa “NABII/MTUME” tofauti na anayoyapata MCHUNGAJI?

  3.Kwa kuwa uchungaji ni kazi ya kuajiriwa, Je, unamaanisha UNABII/UTUME ni kazi ya KUJIAJIRI?

  4. Je, “WAJASIRIAMALI WA INJILI” ni watu gani?

  5. Mtu “akichomoka” na Unabii au Utume au vyote kwa pamoja “Mtume na Nabii”Je, ANACHOMOKA navyo kutoka WAPI?

  6. Umeandika kuwa mtu akichomoka na Utume na/au Unabii ndipo WATU WAYAMUELEWA. Swali ni kuwa WATAMUELEWA KUWA YEYE NI NANI au watamuelewa vipi? Naomba ufafanue hapo ndugu yangu!

  7. Umeandika kuwa kwa sasa watu “WANATAKA MIUJIZA”. Je, unamaanisha kuwa HIYO ndiyo sababu MANABII/MITUME waliopo hawahubiri sana habari za KUOKOKA na UTAKATIFU bali “wanatangaza” tu habari ya mafanikio ya kimwili?

  8. Umeandika hivi “kamuujiza kakuwachangamsha”. Je, unamaanisha KAZI YA MIUJIZA ni KUCHANGAMSHA watu?

  9. Una ushauri gani kwa watumishi: WAWAPE WATU KILE MUNGU ANACHOTAKA au WAWAPE WANACHOKITAKA WATU WENYEWE?

  Naomba niishie hapa kwa sasa ili nisubiri majibu ya maswali hayo ambayo naamini yatasaidia katika kujifunza ‘KAZI YA MITUME/MANABII kwa siku zetu!

 48. Ndugu John,
  Kwanza nikushukuru kwa uvumilivu wako.
  Nimekuelewa ulichokisema, wakati mwingine hunilazimu kutoa maelezo marefu kidogo kwa faida ya kulileta katika urahisi wa kueleweka jambo tunaloliongelea nikitilia maanani kuwa uelewa haufanani. Naamini kwa kauli yako kuwa nawe umeliona hilo hivyo. Bwana na atupe subira yake sote!
  Nitaendelea katika kukujibu kama ifuatavyo:
  1. i) Karama ya unabii inatenda kazi ndani ya watu, Yoh 17:23 “Mimi ndani yao, …” .
  ii) Katika maelezo ya awali niliyoyatoa, katika kuwatofautisha Manabii nilisema hawa manabii wa jinsi ya Musa, Eliya , Isaya na wengineo, ambao Mungu amewatumia katika kulileta Neno lake hata kuweko katika Maandiko, hao niliwafananisha na wale ndege TAI. Hao ndio wale tunao waita wa HUDUMA YA UNABII. Hawa nilisema huduma yao inavuka makusanyiko yetu madogo madogo. Nikasema huduma ya hawa huikamata dunia nzima. Nikasema ujio wa hawa huwakilisha mambo mawili, Hukumu kwa waliomkataa na Neema kwa wampokeao. Kundi la pili nilisema ni hawa manabii wa KARAMA YA UNABII ambao unabii wao ni huduma ya ndani ya kusanyiko tu. Hata unabii wao hulazimika kupimwa na uongozi wa kanisa kabla ya kuchukuliwa. Tena wakati mwingine manabii hawa huweza kutumika katika karama hiyo mara moja na isimrudie tena, pia iwapo Bwana atapenda kumtumia wakati wote, basi hilo litajidhirisha lenyewe, naye huyo huwa ni nabii katika kiwango hicho cha kusanyiko. Kwa hiyo hawa pia ni MANABII. Hawa wakijikusanya kutoka makusanyiko yao, wakaja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ‘Mkutano Mkubwa wa Injili’, basi kundi hilo ndio sawa na lile aliloshuka nalo Agabo.

  2. i) Kwenye Karama ya Unabii tunao manabii hao kama Neno lilivyo sema. Mungu aliposema na liwepo jua, kama jua lisingetokea na kuwepo, basi Mungu asingekuwa Mungu tena! Kwa hiyo kama amesema amewafanya wengine kuwa manabii, lazima wapo. Najua hawonekani katika makanisa mengi kwa sababu ni tishio kwa ustawi wa makanisa hayo kimaslahi, kwani huduma yao ni ya mambo ya sirini ambayo inatusumbua sote tokea kuanguka kwa Adamu. Watu wanapenda kujua mambo ya mbele au ya siri. Kwa hiyo kutokana na mifumo ya kanisa iliyopo, akiwepo mtu wa jinsi hiyo waumini watamheshimu kuliko hata askofu wao!
  ii) Zile Huduma Tano ni za Kuwakamilisha Watakatifu kama ulivyosema. Hizo ziko kanisani kwa kazi hiyo. Wale makristo na manabii wa uongo hujipenyeza katika kanisa hilo lililo na hizo huduma, nao huinua huduma replica ya hizo za kweli hata mwishowe hulitoa kusanyiko katika njia ya kweli bila kujijua. Kwamba jambo hilo litatokea, Mungu alilijua na badala ya kulizuia lisije, yeye alituonya kimbele ili wakija hao tuwajue, nasi kwa Neno tena, tumshinde Ibilisi na hila zake kama ilivyokuwa kwa Kristo alipojaribiwa. Basi pia ni vizuri ukafahamu kuwa hizi huduma tano kwa pamoja ndizo zinazo mkamilisha mtakatifu katika maana nzima ya kumhudumia katika upana huo wa hizo huduma. Basi kanisa lolote linalosimamisha dai la kuwa liko chini ya Roho Mtakatifu, linapaswa kuwa na hizo HUDUMA TANO, kusanyiko lolote dogo lapaswa kuwa hivyo. Sio oh, sisi mwalimu anatoka Uingereza au Mbeya au Makao makuu, hapana, kanisa la Mungu halina Makao Makuu, makao yake makuu ni ROHO MT.! Kwa hiyo pale Kanisa linapokuwa limetolewa nje ya ile NJIA, linapofika umbali fulani katika hiyo njia ya giza, nao watoto wa Mungu wakiwemo humo, vilio vyao humfikia Mungu, naye katika majira yake humsimamisha nabii wake (mmoja tu) kuyarejesha makusanyiko katika Njia ya Wokovu. Huduma hiyo huvuka mipaka ya makusanyiko na hata nchi, yaani hiyo huwa ni huduma kwa mwili wa Kristo.

  5. i) Kifungu ulichonukuu kiko kama kilivyo andikwa. Ila kumbuka kwamba unaposoma kifungu hicho, ili kukielewa vizuri inakupasa kwanza urudi huko kinakotokea ili uweze kuelewa vizuri utimiaji wake. Huko nyuma kidogo niliwahi kukupa mfano mwingine unaohusiana na unabii nikakuambia kuwa kuna vifungu vya unabii ambavyo hutimia kwa sehemu katika nyakati tofauti hata mpishano wa zaidi ya miaka 2000 kwa koma au nukta tu. Nikakupa mfano wa Isaya 61: 1-3 “Roho ya Bwana Mungu i juu yangu ; … Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu….” Kristo alipokisoma kifungu hiki katika Luka 4:18-19 aliishia “Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,” akafunga chuo kisha akawaambia LEO MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MASIKIONI MWENU. Hakumalizia kile kipande kilichobaki kinacho husu kisasi cha Mungu kwani siku yake ilikuwa bado nayo ndiyo tunayoiendea ambapo Kristo atarudi tena kwa ajili hiyo. Pia nilikuambia kuwa Nabii yule Tai, hutambulika kwa huduma. Ni lazima awe amenenwa humo katika Maandiko. Nikasema hata Kristo aliwaambia kuwa hayo Maandiko wanayo yasoma na kuyang’ang’ania yanamshudia yeye. Basi nilipo yanukuu Maandiko ya Malaki 4:5-6 “Angalieni, nitawapelekeeni Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, …”,matumizi ya nukuu hii niliyarudisha katika Huduma kwanza ili kuwa na uhakika wa hilo. Mimi ninayaamini Maandiko katika kujitosheleza kwake, ndio maana nilikuambia kuwa Maandiko haya bahatishi.

  Nilitegemea kuwa, kwa kunisisitizia kuwa ile Malaki 4:5-6 imetimia kikamilifu utanionesha pia na ile Siku ya BWANA iliyo kuu na kuogofya ilipotimilia au utanipa maelezo ya siku hiyo ya kutokutimia kwake kwa miaka 2000 toka ujio wa Yohana. Pia iwapo hiyo Huduma imeyarejesha upya yote, basi hata hao manabii wa uongo watakuwa ni wa kweli, maana nao watakuwemo katika urejesho huo!

  Lakini kama tukiyaamini Maandiko bila kuyatilia shaka, tutayaona kama yanavyosema. Nilikuonesha uwiano wa ule mstari wa 6 na kile kifungu cha Luka 1:17 (“ Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, …”) ambacho kinaonesha bila KIFICHO huduma iliyofanyika kulingana na unabii wa Malaki ni ipi. Pia kwa kukijua kifungu hicho kama kilivyojifunua, hilo ndilo linalo tujulisha kuwa Siku ile ya BWANA iliyo kuu na kuogofya yaja kwani inaambatana na utimilifu wa kifungu hicho cha 6. Nasi hatuiogopi, kwani twafahamu kwa kuyasoma Maandiko kama Danieli (Dan 9:2 “Mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nilifahamu hesabu ya miaka, ambayo Neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, …”, kuwa Mungu atatuletea tena nabii Eliya katika huduma ya kumalizia kile kifungu cha 6 ile nusu iliyobaki ili kukikamilisha, hapo ndipo lile Andiko la Marko 9:12-13 litakapokuwa limekamilika, kule KUYAREJEZA YOTE UPYA. Vinginevyo inakubidi ndg John unioneshe ni wapi ile nusu ilipotimilia maana kwa ushahidi wa Maandiko nimekuonesha ile nusu ya kwanza kutimia kwake katika hiyo Luka 1:17 pia siku ya BWANA haijaja hata leo hii tunapoyachunguza Maandiko pamoja. Basi yatakuwaje yote yamerejeshwa upya bila ushahidi wa nusu ya andiko hilo kutimia kiHuduma kiMaandiko??

  Pia kuhusu yule rafiki yako, tukio hilo lingekudhihirishia nguvu na uwezo wa upako ulio juu ya makristo na manabii wa uongo! Hata hivyo huyo rafiki yako hakuingia katika “imani fulani” bali aliingia katika msimamo fulani, kwani IMANI ni moja tu (Yuda 1:3-4 “… ili niwaonye kwamba muishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. …”)

  ii) Kwamba nawe umeona kwamba bado kuna manabii , wale Tai wanaopaswa kuja katika Agano Jipya, hiyo ni hatua inayoweza kukupa tumaini katika kazi ya Mungu inayoendelea ukawa uko up-to-date na Injili.
  Kuhusu huyo Eliya ajaye na KUREJEZA YOTE UPYA, kama nilivyokuambia kuwa NUSU haiwezi kuwa YOTE au kitu kizima. Kwa hiyo ukimkuta mtu anafundisha kuwa nusu ni kitu kizima utajua kuwa kuna walakini. Basi huduma inakamilishwa na Eliya huyo huyo aliyeifanya ile nusu, ndiye anayeimalizia hata Kristo alipoiangalia katika ukamilifu wake akatoa hilo jibu kama lilivyo, nao wale wanafunzi kulingana na wakati wao katika Programu ya Mungu walichukua kilicho wahusu kwani ndicho kilichofunuliwa katika akili zao, Luka 24:45 “ … ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na Maandiko.”

  iii) [a&b] Kuhusu watu kuokoka. Njia ya kuokoka ni moja tu. Marko 16:15-16 “… Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Basi wokovu u katika kuiamini Injili. Kwa hiyo kulitilia shaka jambo lolote lile katika Injili, hilo litakufanya uukose wokovu kwani Mungu haliruki Neno lake, Mt 4:4 ‘ … Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Iwapo mtu ameitilia shaka sehemu ya Neno la Mungu, je, Mungu atamvishaje wokovu mtu wa aina hiyo? Labda wokovu wa kujivika mwenyewe kama Adamu alivyojivisha majani!

  6. i) Makanisa yote mawili yanahubiri Injili ya Kristo. Kanisa la Mungu linaambatana na Neno lote litokalo kinywani mwa Mungu. Nayo Neema ya Mungu huambatana nao katika majaribu yote yanayowakabili. Kanisa jingine ni lile la Kaini ambalo lenyewe linajiendesha kwa kuliigiza hilo la Mungu, kwa hiyo nalo huihubiri injili kwa vipande likiyakana Maandiko mengine. 2Tim 3:5 “Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake …”

  ii) Namaanisha Nabii Eliya ajaye. Yule ajaye kuikamilisha ile nusu ya ile huduma ya Malaki 4:6 kule ‘kuigeuza mioyo ya watoto iwaelekee baba zao’ yaani sisi tuliozaliwa katika Injili ya mitume halafu leo tuna migongano ya mawazo, yaani madhehebu, zaidi ya elfu kumi duniani kote, tukiwa na mafundisho tofauti tofauti; basi akija ataturejeza pale mwanzo yaani katika imani ya kanisa la Mitume.

  iii) Kupigwa Upofu. Injili inapohubiriwa hufanya mambo mawili; humfungua yule wa kuokoka na pili humfunga yule aliye wa kupotea. Basi injili inapohubiriwa katika mchakachuo, hilo huhakikisha kuwa hatutafunguka macho yetu. Yaani kipofu akimuungoza kipofu. Kwa hiyo haijalishi ulipofuka vipi, ilimradi umepofuka kiinjili, basi kama ilivyokuwa Sodoma hata sisi tulio nje ya mfumo ni wasulubishaji wa Neno. Nasi tutafungiwa hilo LANGO (Yoh. 10:9 “ Mimi ndimi mlango …“), tusiingie. Nayo ahadi ya moto ingalipo, sijui unatafuta unafuu upi. Maana shughuli inayo kuja labda ni zaidi ya ile ya Sodoma!!

  iv) Ujio wa Eliya utakuwa lini? Mungu ni mwaminifu. Yeye hulitimiza Neno lake. Basi kama alivyo ahidi lazima na hilo atalitimiza. Jambo la msingi ni kwa sisi kuliamini Neno lake bila kulichanganya na mafundisho yetu. Mchanganyiko wa mafundisho, yaani Neno na akili zetu utatupeleka mbali na Mungu kama ulivyo wafanyia Wafarisayo. Kristo alipokuja makuhani hawakumtambua licha ya ishara ya masihi iliyofanywa mbele yao mara nyingi km vipofu kuona, kusoma siri za mioyoni nk. Lakini yule mwanamke Msamaria kwa ishara ile ile aliweza kumtambua Masihi!!!! Basi hata ujio wa Eliya utakuwa hivyo hivyo, watamtambua wanao mtarajia kwani wanayo ishara mioyoni mwao.

  v) Fundisho la Mitume. Hili naona tukiliweka katika mtiririko wa ile namba 2 italeta maana zaidi kwani pia itahusisha kuwatambua Manabii wa Uongo!

  Nina kushukuru kwa uvumilivu wako.
  Bwana na akutie nguvu na ujasiri wake!

 49. Ndugu Ck Lwembe,

  Nimesoma ufafanuzi wako. Sasa naona kama tukiendelea kwanza hapo hapo kwenye vipengere hivyo 6, tutakuwa tunatengeneza mtiririko mzuri. Lakini la muhimu sana katika mjadala huu ni kuwa tufike mahali TUELEWE kama KUNA MANABII, na kama WAPO, KAZI ZAO NI ZIPI na pia TWAWEZAJE KUMTAMBUA NABII WA KWELI {kama sasa wapo}.

  Ninajua kuwa unayo mengi sana ya kueleza hapa ndiyo maana ukiandika unaandika kwa kirefu. Sasa kinachotokea ni kuwa katika kuandika kwa kirefu kunajitokeza maswali/mambo mengine ambayo inabidi nikuulize ufafanuzi au majibu yake. Ni kisema uandike kwa ufupi nitakuwa nakuzuwia kufafanua kwa kina jinsi unavyoona kuwa kwa kufanya hivyo ndiyo utaeleweka. Kwa sababu hiyo ninakuomba SUBIRA kwa kuwa wewe ni VEMA UKAANDIKA KIREFU, na katika kuandika huko MIMI NAPATA MASWALI na ni MUHIMU NIYAULIZE maana tukisema NISIYAULIZE, nifukie tu SITAKUWA NAJIFUNZA CHOCHOTE na nitakuwa sijitendei haki. Kwa hiyo mimi nakubaliana na majibu yako marefu, ambayo ndani yake yanaleta mawazo mapya, NAWE NAKUOMBA UKUBALIANE na maswali yangu mengi maana ndipo ninajifunza, USIJE kuona kama kwa kuuliza maswali mengi ninakusumbua. Subira itawale katika mjadala huu maana naamini kwa kufanya hivyo tunaweza kufikia lengo letu.

  Sasa, nikirudi kwenye mada yenyewe:

  1.Umeandika hivi:

  “Nchini Tanzania Hakuna Nabii yeyote wa kweli katika siku ya leo, bali Karama ya Unabii ipo na inatenda kazi ndani ya Kanisa la Kristo!”

  Swali hapa ni hili:

  i). Hiyo Karama ya Unabii inatenda kazi ndani ya Kanisa la Kristo kupitia WAPI, Ni angani au Ndani ya watu?

  ii). Kama ni “ndani ya watu” kwa nini wasiitwe Manabaii maana ndiyo wanayoibeba Karama hiyo? {Maana hata Nabii Elliya na Wenzake walivuviwa Roho ya Unabii na Mungu mwenyewe, na kwa kuwa walikuwa wanaibeba ikabidi waitwe MANABII. Kamwe hawakutenda kazi hiyo ya Unabii kwa nguvu zao wenyewe!!! Sasa kama na leo wapo wanaobeba Karama hiyo, Kwa nini wasiitwe Manabii??}

  2. Nanukuu: “Kwa hiyo huduma iliyopo ndani ya Kanisa ndiyo hiyo ya Roho Mtakatifu mwenyewe akihudumu katika kiwango cha hiyo Karama ya Unabii na vipawa vinginevyo kama alivyoviweka kanisani kwa kusudi kamili. Basi katika kiwango hicho ile Huduma ya Unabii haipaswi kuwepo maana yenyewe hutenda kazi ya kulirudisha Kanisa lililopotoka katika NJIA ya KWELI” Mwisho wa kunukuu.

  i).Kwa kuandika: “Kwa hiyo huduma iliyopo ndani ya Kanisa ndiyo hiyo ya Roho Mtakatifu mwenyewe akihudumu katika kiwango cha hiyo Karama ya Unabii na vipawa vinginevyo kama alivyoviweka kanisani kwa kusudi kamili”…. Natumaini unamaanisha Roho mtakatifu ANAHUDUMU KATIKA KIWANGO CHA HIYO KARAMA YA UNABII na UALIMU, UINJILISTI, UTUME na UCHUNGAJI…kwa kusudi kamili katika kanisa.

  Kama hivyo ni kweli: Kama Roho ni Yule Yule anayehudumu NA kwenye UALIMU tuna WAALIMU, Kwenye UINJILISTI tuna WAINJILISTI, Kwenye UTUME tuna MITUME na Kwenye UCHUNGAJI tuna WACHUNGAJI:

  Sasa ni kwa nini KWENYE UNABII, na kwenye Unabii tu, TUSIWE NA MANABII?

  ii).”Basi katika kiwango hicho ile Huduma ya Unabii haipaswi kuwepo maana yenyewe hutenda kazi ya kulirudisha Kanisa lililopotoka katika NJIA ya KWELI”

  Kutokana na maneno hayo nimeelewa kuwa KAZI YA HUDUMA YA UNABII NI KULIRUDISHA KANISA LILILOPOTOKA KATIKA NJIA YA KWELI. Na ninavyojua mimi hiyo ndiyo JUMLA YA MAKUSUDI YA HUDUMA ZOTE ZILE 5…Kuwakamilisha Watakatifu…kusudi mwili wa Kristo Ujengwe! Na vyote hivi vinafanya Kazi Chini ya Uongozi wa Roho Mtakatifu maana ndiye Mwenye HUDUMA na KARAMA ambavyo humpatia mtu kwa kadri apendavyo yeye!

  Yaani kazi ya Kulirudisha Kanisa katika Njia ya kweli si kazi ya UNABII peke yake bali huduma zote zile 5. Sasa kusema kuwa UNABII PEKE YAKE ndiyo unaweza kurudisha kanisa katika njia ya kweli ni KUZIKATAA ZILE HUDUMA 4 ZILIZOBAKI.

  Na huduma zote hizo 5 zinatenda kazi bega kwa bega, katika Kanisa. Sidhani kama zinatenda kazi ZAMU KWA ZAMU bali vyote vipo kazini. Mitume wanaendelea na Utume, Wainjilisti wanaendelea na Uinjilist, Waalimu wanaendelea Kufundisha, Wachungaji Wanaendelea kuchunga wakristo na MANABII NAO WANAENDELEA NA UNABII wao. Kama hivi ni kweli basi Katika Kanisa KUNA MANABII!!

  Kama nimekosea nisahihishe!

  3 & 4. Kwenye Vipengere cha tatu na cha nne sina zaidi.

  5. Hapo kwenye NABII ELIYA AJAYE ndipo bado ninashauku sana ya kujua kilichojificha hapo.

  i).Katika maandiko niliyonukuu, Marko 9:12-13 kuna maneno ya Bwana Yesu yafuatayo:

  “Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza yote upya; lakini pamoja na haya ameandikwaje mwana wa Adamu kwamba atateswa mengi na kudharauliwa? Lakini nawaambia Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa”.

  Andiko hilo linaonyesha kuwa Eliya Ajaye au Atakayekuja NA KUREJEZA YOTE UPYA {kama ilivyotabiriwa na Malaki} ni YOHANA MBATIZAJI na Bwana Yesu alithibitisha mwenyewe, kwa kinywa chake. Na hiyo inaonyesha kutimia kwa Unabii huo wa Malaki 4:5-6.. Sasa huyo unayesema HAJAJA NI YUPI TENA? Kwa andiko lipi?

  [[Kuna imani fulani, ambayo kuna mtu alikuwa rafiki yangu mara akaingia huko. Wao walikuwa wanatumia Andiko hilo ya Eliya Ajaye kuthibitisha kuwa KIONGOZI wa imani hiyo ndiye ELIYA AJAYE, Kwamba sasa ameshakuja kurejeza yote upya! La kusikitisha rafiki yangu huyo sasa ni Mpagani tu kwa kuwa hapakuwa na fundisho lolote la Injili ya Yesu Kristo, iletayo wokovu. Sasa, hapa niko makini sana katika kipengere hiki kwa kuwa tayari nina ushahidi wa jinsi andiko hilo lilishachakachukuliwa na kuwa MSINGI wa IMANI POTOFU]]

  ii).Andiko lako pekee ulilotumia kuhusu Eliya Ajaye, linaoloonekana baada ya Bwana Yesu ni hilo katika Ufunuo 11:3-13. Lakini kama HOJA YA ELIYA AMBAYE BADO HAJAJA ni Kurejeza yote Upya, natumaini andiko hilo HATUWEZI KULITUMIA kwa hao manabii WAWILI maana wao kazi yao itakuwa ni KUWATESA WAKAAO JUU YA NCHI, Ufu 11:10 na wala SI KUREJEZA YOTE UPYA!

  Bwana Yesu alishasema Eliya Ajaye na KUREJEZA YOTE UPYA ALISHAKUJA naye ni Yohana Mbatizaji. Sasa huyo mwingine ni YUPI?

  iii).”Hakuna anayeweza KUOKOKA bila huduma ya Eliya nabii ajaye! Ni sawa. Maana Mungu anapolileta Neno la Upatanisho la Wakati, basi asiyelipokea hukatiliwa mbali. Basi Nabii Eliya akija na lile Neno la KUREJESHA UPYA, halafu ukalikataa, hakuna NEEMA tena juu yako bali HUKUMU!”

  a).Kama ni hadi huduma Eliya nabii ajaye NDIPO mtu anaweza kuokoka, Je, SASA HIVI WATU HAWAOKOKI?, yaani INJILI SASA HAIKOI tena?

  b). Kama WANAOKOKA, wanaokoka kwa HUDUMA IPI YA NABII ELIYA AJAYE?

  6.Umeandika hivi:

  “Nao kazi wanayoifanya kwa upako ule ule (ambao ndio huu wa Math 24:24), wanatupiga upofu tusiuone MLANGO. Nao MLANGO wa leo ni KRISTO ambaye ni NENO”

  i). Je, una maanisha kwa SASA HAKUNA POPOTE PANAPOHUBIRIWA HABARI ZA INJINLI YA YESU KRISTO?

  ii).Umeandika pia hivi: ”

  “Je, hilo kusanyiko, atakapokuja huyo Nabii kulingana na Mpango wa Mungu wa siku hiyo, kundi lolote lililochini ya Fundisho la jinsi hiyo, ninaamini ni lazima limkatae na kumuona ni Nabii wa Uongo. Huo ndio upofu wenyewe”

  Je, kwa kuandika “atakapokuja huyo Nabii kulingana na Mpango wa Mungu wa siku hiyo”….hapa unamaanisha NABII ELIYA AJAYE au NABII GANI?

  iii). Umeandika: “Na huo ndio upofu wenyewe. Mwz 19:11 “Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango”!!

  -Ninatofautiana nawe katika tafsiri na hatimaye matumizi ya andiko hilo, kama ifuatavyo:

  Wale waovu walipigwa upofu kwa kuwa walitaka kuingia ndani kuwafanyia mabaya wale malaika. Wala hawakupigwa upofu kwa kuwa walitaka kuingia ndani ili wawe salama, Ilikuwa ni ADHABU wala SI FITINA.

  Watu sasa tunatafuta mlango ambao ni Yesu ili tuingie uzimani. Kwa hiyo kupigwa upofu kwa watu SASA inatakiwa kuwa ni FITINA wala si ADHABU. Na kama ni fitina basi sharti ifanywe na watumishi wa shetani na wala si WATUMISHI WA MUNGU kama ilivyokuwa kwa wale MALAIKA. Kama manabii wa uongo ni watumishi wa shetani, basi hatupaswi kuwalinganisha na malaika ambao ni watumishi wa Mungu.

  Lengo la mimi kuandika haya ni kushauri kuwa TUSITUMIE (nikiwemo na mimi) maneno mahali pasipo pake pengine kwa ajili ya KUHALALISHA HOJA zetu.

  Kama nimekosea hapo waweza kunisaidia pia.

  iv). Nanukuuu: “kulingana na Programu ya Mungu, kama huu ujio wa Eliya!”
  Je, twaweza kupata katika Biblia UJIO WA ELIYA UTAKUWA LINI?

  v). Ni FUNDISHO gani la MITUME ambalo kanisa la sasa LIMEACHA?

  Hayo ndiyo yaliyojitokeza baada ya kuwa nimesoma majibu yako na ninaamini BADO uko na subira kwa ajili ya kuyajibu.

 50. Ndg John Paul,

  Pole kwa kukusubirisha zaidi, bali yote yametokana na kubanwa kidogo katika majukumu mengine ya kawaida. Uniwie radhi.

  Muhtasali wa majibu yangu uliouandika uko sawa kabisa kimsingi, bali inahitajika kuupanua kidogo ili kuuleta katika ukamili wa wazo. Nitauweka hivi:

  1. Nchini Tanzania Hakuna Nabii yeyote wa kweli katika siku ya leo, bali Karama ya Unabii ipo na inatenda kazi ndani ya Kanisa la Kristo! Lakini, Manabii wa Uongo wa Karama na Huduma, hao wapo tena kwa wingi wakitenda kazi katika lile kanisa jingine!

  2. Roho ya Unabii ni Roho ya Kristo. Wote watoao unabii hufanya hivyo kupitia Roho Mtakatifu (2Petro 1:21). Kwa hiyo si kwamba hakuna sababu ya nabii kuwepo, bali Mwenye Unabii wake yupo ndani ya Kanisa lake akiendelea kulikamilisha katika mambo madogo madogo hadi makubwa. Hilo ndilo linaloiondoa Huduma ya Unabii kama kile kifungu cha Webrania kinavyotudhihirishia: “Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, lakini katika siku hizi za mwisho amesema nasi kwa njia ya Mwanawe..” Kwa hiyo huduma iliyopo ndani ya Kanisa ndiyo hiyo ya Roho Mtakatifu mwenyewe akihudumu katika kiwango cha hiyo Karama ya Unabii na vipawa vinginevyo kama alivyoviweka kanisani kwa kusudi kamili. Basi katika kiwango hicho ile Huduma ya Unabii haipaswi kuwepo maana yenyewe hutenda kazi ya kulirudisha Kanisa lililopotoka katika NJIA ya KWELI.

  3. Uwepo wa lundo la manabii walioko leo ni batili! Kweli ni batili

  4. Manabii wa Uongo wataendelea kutenda kazi hadi ya siku ya mwisho! Sawa .

  5. i).Eliya Nabii BADO HAJAJA! Hajaja Bado na Amekwisha kuja. Kama Maandiko yasemavyo, ndivyo ilivyo! Roho ya Eliya, Mungu katika mapenzi yake anaitumia kuhudumu katika kiwango cha SHOWDOWN au KUWAUMBUA manabii wa uongo na kulirejesha kanisa katika Fundisho la kweli au njia ya wokovu pale linapokuwa limepoteza mwelekeo. Tunaiona Roho hiyo ya Eliya Mungu akiitumia mara tano:

  i). Eliya mwenyewe – 1Fal 18:17-40 ‘… naye akajibu, si mimi niliyewataabisha Israeli; bali wewe na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za Bwana; nawe umewafuata mabaali. … Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.”

  ii). Elisha – 2Fal 2:15 “ Nao hao wana wa manabii, waliokuweko Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha”.2Fal 3:11-20 “ Lakini Yehoshafati akasema, Je, hapana hapa nabiiwa BWANA, ili tumwulize BWANA kwayeye? … Uende kwa manabii wa babayo, na manabii wa mamayo. … kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme waYuda, singekutazama, wala kuonana nawe.”

  iii). Yohana Mbatizaji- Luka 1:17 “ naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, …” ; Malaki 4: 5-6 “ Angalieni nitawapelekea Eliya nabii, … Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, …”

  iv). Eliya (atakayerejesha yote upya) Malaki 4: 5-6 “ Angalieni nitawapelekea Eliya nabii, …,na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, …”

  v). Eliya (kule Israeli)– Kati ya wale manabii wawili waUfunuo 11: 3-13

  Kwa hiyo Eliya nabii Bado hajaja na Amekwisha kuja. Itategemea unamzungumzia Eliya yupi au huduma ipi ya Eliya. Kwa hiyo Eliya niliyemzungumzia mimi, ambaye Kanisa lililo katika Fundisho la Mitume linamsubiri aje, ni yule Eliya ajaye kurejesha yote upya, yaani kulirudisha kanisa la leo lililoondoka katika Fundisho la Mitume na kuingia katika mafundisho ya mapepo. Kwa hiyo ajapo huyu Eliya ndiye atakayewakabili hawa manabii wa uongo kwa Upanga wa Neno, nao wana wa Mungu waliomo ndani ya makambi hayo wataisikia sauti yake na kutoka humo (Yoh 10:4). Hao watarejeshwa upya katika Fundisho la Mitume, nayo Injili kwao itakuwa MPYA. Mtoto akikutana na babaye, nifuraha iliyoje!!! Maana kanisa likirejeshwa katika FUNDISHO la MITUME ndipo litakuwa na ile IMANI aliyoiuliza Kristo kuwa akija ataikuta(“…walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Luka 18:8) ? Hebu nieleze iwapo Kristo atashuka leo, hiyo IMANI aliyoiulizia ataikuta kwenye kusanyiko la Nabii yupi? Katoliki au Lutherani au Anglikana ile ya mashoga wa Marekani au Assemblies au kwa Nabii na Mtume yupi kati ya hawa kundi kubwa? Yoh 10:16 “Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwapo kundi moja na mchungaji mmoja”.

  Tena katika hili la Huduma ya Unabii, ukiliangalia chini ya darubini, utawaona wengine wengi sana ambao hujawahi kuwadhania, wamesimama katika nafasi hiyo ila tu hawajawahi kujitangaza kama Manabii, lakini kulingana na Maandiko, hiyo ndiyo huduma wanayoifanya. Nabii huja na ‘BWANA ASEMA’. Kwa hiyo Nabii anapotokea uwanjani, hulibadilisha mwelekeo kundi lote la watakaompokea. Kama tunavyo yaona makundi ya Wafarisayo, Wasadukayo na Waandishi katika ujio wa Nabii Yohana Mbatizaji na Bwana Yesu Kristo (Mwana wa Adam – Nabii), waliowapokea walibadili mwelekeo na kuingia katika Ukristo. Hivyo basi, ukiyaangalia makusanyiko yetu, katika migawanyiko yake, kila kundi moja lilipopasuka kuzaa kundi jingine, lile kundi lililoondoka kujitenga, hufanya hivyo kwa kulipokea neno la utenganisho kutoka kwa kiongozi mwenye hilo ONO la kujitenga ambalo huwa ni ‘BWANA ASEMA’ kwa kikundi hicho! Kwa kifupi viongozi wa MADHEHEBU yote DUNIANI ni Manabii! Katika kujaribu kuliweka vizuri hilo, hebu tuchukulie kwa mfano Kanisa Katoliki. Kiongozi wake wa juu ni Papa. Yeye ndiye anayeliongoza kanisa kiimani kulingana na Fundisho la kiKatoliki ambalo ndilo Injili ya Kweli kama Mungu alivyowaongoza katika hilo. Na iwapo kuna mawasiliano yoyote yalihusuyo kanisa basi Papa ndiye hupewa hayo. Ndiyo maana katika Fundisho lao, kuna kipengele kinachotamka kuwa Papa HAKOSEI! Basi huyo ndiye NABII katika ulimwengu wa kiKatoliki, wao humsikiliza yeye kwani ndiye aliye na ‘BWANA ASEMA’. Vivyo madhehebu mengine yote. Hakuna anayemsikiliza nabii wa kundi jingine, kila kundi na ulimwengu wake chini ya Nabii wao. Bali wote hawa dai lao ni moja: WANAUPOKEA UJUMBE KUTOKA KWA KRISTO. Je, kama huu si unafiki wa kiwango cha juu, ni nini jamani!!!!

  ii). Hakuna anayeweza KUOKOKA bila huduma ya Eliya nabii ajaye! Ni sawa. Maana Mungu anapolileta Neno la Upatanisho la Wakati, basi asiyelipokea hukatiliwa mbali. Basi Nabii Eliya akija na lile Neno la KUREJESHA UPYA, halafu ukalikataa, hakuna NEEMA tena juu yako bali HUKUMU!

  6. i). Kanisa la Mungu kwa sasa NI KIPOFU!
  Ndio ni kipofu nalo linahitaji Eye Salve ambayo yaja katika Huduma ya Eliya. Sodoma, ulifanyika muujiza mmoja tu, nao ulikuwa ni kuwapiga upofu wasiuone MLANGO! Basi leo tena huo ndio muujiza wa kiroho unaoendelea kabla ya dunia kupigwa kiberiti. Hili lundo la manabii unalo liona halina tofauti na wale waliomdanganya Ahabu. Naye Ahabu wa leo ndio sisi tujiitao wakristo tuliojirundikia hawa manabii katika ujumla wao. Nao kazi wanayoifanya kwa upako ule ule (ambao ndio huu wa Math 24:24), wanatupiga upofu tusiuone MLANGO. Nao MLANGO wa leo ni KRISTO ambaye ni NENO. Hebu fikiria jambo hili; anaposimama Nabii kisha akalifundisha kusanyiko kuwa Huduma ya Unabii katika Agano la Jipya hakuna tena kwa sababu Waebrania 1 inatuambia siku hizi tunahudumiwa na Mwana mwenyewe. Je, hilo kusanyiko, atakapokuja huyo Nabii kulingana na Mpango wa Mungu wa siku hiyo, kundi lolote lililochini ya Fundisho la jinsi hiyo, ninaamini ni lazima limkatae na kumuona ni Nabii wa Uongo. Huo ndio upofu wenyewe . Mwz 19:11 “Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango”!!

  ii). Kanisa la Mungu, pamoja na kuwa limepofuliwa lakini, liko Imara. Sawa, uimara wake watokana na ile NEEMA, ambayo hulitunza hata litakaposafiwa kulingana na Programu ya Mungu, kama huu ujio wa Eliya!

  iii). Yeyote anaye operate nje ya FUNDISHO LA MITUME ndilo dude linalojiwakilisha kama Kanisa. Sawa!

  Asante sana, natumai nimeeleweka katika hilo wazo.

  Ubarikiwe!

 51. Ndugu C k Lwembe,

  Rejea summary yangu ya tarehe 2/1/2012 niliyoandika ili unihakikishie kama nilivyokuelewa ndivyo hivyo au sikukuelewa vizuri. Ninakusubiri wewe maana kuna maswali mengi ambayo yanahitaji kujibiwa na yote ni muhimu katika kujadili suala hili.

  @ Abigail David,

  Nakubaliana nawe kabisa kuwa mjadala huu ni muhimu sana, kweli kabisa. Lakini mimi naona mambo ya msingi katika mjadala huu ni:

  1. KUWEZA KUFAHAMU KAMA KWELI MANABII WAPO,

  2. Kama wapo, KAZI ZAO NI ZIPI?

  3. WANAWEZAJE KUTAMBULIWA (hao manabii wa kweli)

  Saa tukishafahamu hao MANABII WA KWELI basi yeyote akija toauti na manabii hao wa kweli tayari tutajua kuwa ni WA UONGO.

  Kuwatambua manabii wa Uongo inaweza kuwa vigumu sana IKIWA HATA HAO WA UKWELI HATUWAJUI KABISA. Bila kuwatambua hao wa KWELI hatuwezi kuwatambua wa UONGO. Ni rahisi sana kudanganywa.

  Kuna mtu mmoja aliniambia kuwa wafanya kazi wa benki wao hujifunza namna ya kutambua Pesa halali. Kwa hiyo chochote kinyume na hiyo basi watajua ni FEKI. Ni kweli. Hata mimi nilikubali kwa sababu pesa feki zaweza kuwa za aina tofauti tofauti na kila mara panafanyika utaalamu mpya wa kutengeneza pesa feki. Kwa hiyo siyo rahisi kufahamu ni aina gani nyingine ya pesa feki itakwenda kutengenezwa!

  Hata katika MANABII ni hivyo hivyo. Manabii wa Uongo wanaweza kuja na mbinu tofauti tofauti ambazo zingine ni vigumu mno kuzitambua, yaani hadi mtu awe mkristo kweli kweli mwenye uhusiano HAI na Mungu. Kwa maana hiyo ni kazi ambayo haiwezekani kuzijua na kuzipata tabia zooote za Manabii wa Uongo na kuziweka hadharani. Kama mbinu za matapeli zooote zingekuwa zinajulikana basi matapeli wasingetapeli tena. Kama tunaweza kufahamu mbinu zoote za Manabii wa uongo basi hawawezi tena kuendelea kuwepo maana watakuwa wameumbuka!

  Kwa hiyo mi naona kuwa TUKISHAELEWA SIFA NA TABIA YA NABII ALIYEWEKWA NA MUNGU hapo tutakuwa tumekamilika. Maana YE YOTE ambaye hana SIFA hizo,tayari tunajua ni wa Uongo! Hata kama atakuja na mbinu alizobuni siku hiyo hiyo!

  Hata hivyo katika maswali niliyomuuliza ndigu C k Lwembe kuna swali nililomuuliza ambalo akilijibu tutapata jibu kuhusu mambo yanayoashiria kuhusu Nabii wa Uongo na nini kifanyike kukabiliana na tatizo hilo.

  @ Ndg Orbi,

  Mi nafuatilia maelezo yako yote ila kwa sasa niko na ndugu Lwembe, nimeona nitulie naye twende pole pole katika kujifunza suala hili. Mungu akuzidishe zaidi katika huduma yako!

  Tuendelee kujifunza!

 52. Wapendwa,
  Kama walivyokwisha sema na kuthibitisha kwa maandiko wengi waliotangulia, manabii wa agano la kale hawapo leo, ila karama na huduma ya unabii ipo katika kanisa leo. Zile huduma tano zinazotajwa katika Waefeso 4:11 ni HUDUMA na siyo KAZI au VYEO na anayezitoa ni Bwana Yesu, hivyo kusema maneno kama “kwa nini wasikubali waitwe wachungaji tu” siyo sahihi kwani uchungaji ni HUDUMA kama hizo nyingine nne hujipachiki mwenyewe unayoipenda, na wala huisomei ila ni vizuri kujifunza neno la Mungu kwa utaratibu na mpangilio mzuri ama kwa kwenda Bible School au vinginevyo ikiwa una wito wa kumtumikia Mungu maana hata Paulo alimsisitizia Timotheo ajifunze neno ili aweze kuwa mtenda kazi mzuri asiye na sababu ya kutahayari.

  Kila mwamini anaweza kutumiwa na Roho Mtakatifu kutoa unabii, lakini huko hakumfanyi mtoa unabii kuwa nabii, hiyo na karama ya unabii. Yule Filipo mwinjilisti wa kitabu cha matendo alikuwa na binti wanne waliokuwa wanatoa unabii, hawakuitwa ni manabii, ila Agabo na wenzake
  wao waliitwa wazi kuwa ni manabii.

  Kulingana na 1Kor 14:3 mtu yeyote anayehudumu kwa kupitia karama ya unabii basi ataleta maneno ya kujenga, kutia moyo na kufariji tu na wala si zaidi ya hapo. Anayehudumu kama nabii anaweza kuleta neno lenye kujenga, kufariji, kutia moyo na vilevile kuonya, kuimarisha(confirm), kufunua yajayo au yaliyofichika, n.k lengo likiwa ni kushirikiana na huduma zile nne zingine ili kulijenga kanisa la Kristo ili wote tuufikie umoja wa imani na utimilifu wake Kristo mwenyewe. Nabii wa leo anatakiwa awepo katika kanisa na kuwa sehemu ya uongozi wa kanisa pamoja zile huduma zingine.

  Kwa ujumla leo makanisa yanaongozwa kimsingi na Wachungaji tu(japo wengine wanaojiita wachungaji wana huduma zingine ila sijui ni kwa hofu au sababu zingine hawataki kuzitaja waziwazi) mithili ya wakurugenzi na makampuni yao huku huduma zingine zikisukumiwa kando wakati zote zinahitajika la sivyo Bwana Yesu asingezitoa. Sijui kwa nini watu wengine wanapata shida sana ukitaja mtume au nabii ila ukisema Mwalimu au Mwinjilisti au Mchungaji au Askofu(hii siyo huduma ila ni kazi tena unaweza kuitamani bila matatizo ili mradi uwe na wasifu unaotakiwa kulingana na 1 Tim 3: 1 – 7) ahh hakuna tatizo…Je ni kutokuelewa hizi huduma au ni nini hasa? Hizi huduma zote zilikuwepo tokea kwenye kanisa la mwanzo, huduma za manabii na mitume zilikoma lini? Kama tatizo ni watu kujipachika unabii kama vile ni cheo fulani ili wajifaidishe wenyewe basi hilo ni suala jingine, ila huduma ya nabii ipo leo.

  (Matendo 11: 27 – 28)
  27 Wakati huohuo, manabii kadhaa walikuja Antiokia kutoka Yerusalemu. 28 Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote (Njaa hiyo ilitokea wakati Klaudio alipokuwa akitawala).

  Hapo tunaona “manabii kadhaa” walikuja Antiokia toka Yerusalemu siyo mmoja tu, ila anayetajwa kwa jina ni Agabo aliyesimama na kutoa unabii…

  Na hapohapo Antiokia walikuwepo manabii katika kanisa.

  (Matendo 13:1) Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na walimu; miongoni mwao akiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.

  Vilevile kulikuwa na manabii wengine waliotajwa kwa majina Yuda na Sila.

  (Matendo 15:32)
  Yuda na Sila, ambao nao walikuwa manabii, walizungumza na hao ndugu kwa muda mrefu wakiwatia moyo na kuwaimarisha

  Naomba nimalizie kwa kusema kuwa manabii wapo katika kanisa la Kristo leo hii.

 53. Mpendwa wangu Orbi, kwanza lazima nikiri wazi kuwa MUNGU amekujaria uwezo mkubwa wa kujadiliana na watu,wewe hutishwi na lugha na matamshi yanayotumika,upo pamoja na watu wote unaotaka wakuelewe! Kaka yangu, mimi sijui kiukweli unachotaka, nisaidie tafadhali.Najiuliza hivi,……..au, kwanza nisaidie nijue hivi:- Wewe hutaki wawepo hao manabii, au maandiko ndiyo hayataki wawepo hao manabii? kwanza naomba ujue hivi mimi siungi mkono kila Nabii,pili,Naamini juu ya miujiza na kwamba ipo, tatu naamini kuwa MUNGU MWENYEZI ana manabii wake (anowatumia ktk Kanisa lake), lakini naamini pia, shetani ana manabii wake (anaowatumia katika kanisa lake pia) Kama ndivyo. utaona nia yangu ni KUPOKONYA MATEKA wa BW. YESU KRST mikononi mwa shetani,kwa njia ya uelewa nikimwachia ROHO MTAKATIFU apenyeze ufafanuzi ulio bora na rahisi katika vichwa vya watoto wake anaotaka wajue siri za neno lake,MAAMA YEYE NDIYE HIYO MISTARI NA NUKUU SAHIHI ZA BIBLIA……yeye ndiye mwalimu na ndiye atakaye tafsiri, ndyo maana siko zaidi katika kukaririsha nukuu ya mistari iliyomo ktk Biblia,sisemi kuitaja mara kwa mara na kuinukuu kwa nia ya kuwaelewesha wasomaji ni vibaya……..hivi ulipata kujiuliza ni kwanini shetani alinukuru maandiko wakati alipo mjaribu BW.YESU KRST naye YESU akalazimika kutaja maandiko katika kumpinga shetani? (Mpendwa sheri za kawaida za madai husema kuwa……Ushahidi utahitajika tu iwapo kunajambo linabishaniwa na iwapo kuna hati mahakamani inayokubalianwa basi ushahidi wa mdomo hautakubaliwa) naomba nisiende ninje ya maada nimalize tu kwa kusema kwamba, MANABII (Bila kujari ni wauongo au waukweli,bila pia kujali wapi ni wengi) NI LAZIMA WAWEPO,MAADAMU IMEANDIKWA KUWA WATAKUWEPO, basi hakuna zaidi! chamsingi nikumpa sasa ROHO MTAKATIFU tena bila ubishi mawazo yetu ili.atufundishe. atutafasrie,atujulishe na au atuwekee wazi kuwa manabii wa uongo ni wapi na wale wa ukweli ni wapi. NINACHOJUA NA NILICHONACHO UHAKIKA NI KWAMBA HAIJAPATA KUTAJWA NA ROHO MTAKATIFU POPOTE,SIKU YEYOTE NA MAHALI POPOTE KUWA HAKUTAKUWEPO NA MANABII! kaka yangu mpendwa Orbi, kama wewe ulishawahi kuona mahali popote ktk BIBLIA basi ningependa unipe sasa ushahidi,nami nipate kutoka kAtita kujidanganya kwa kuamini jambo lisilokuwepo. NENO LINASEMA WENYEKUDANGANYA WAZIDI KUDANGANYA…….hao ndio manabii wa uongo,wanafanya mambo kwa maslahi yao na baba yao. vivyo hivyo wasemao kweli na wazidi kuinena ile kweli………kweli ni nini? kweli ni neno la MUNGU MWENYEZI. HAO NAO WANAFANYA HAYO KWA MASLAHI YASIYOYAO,BALI NI YA BABA YAO! Ubarikiwe,tafadhali usinikatie tamaa.

 54. Nawasalimu ktk Jina la Bwana wetu Yesu Kristo,Wapendwa
  Tafakari ni njema tunabarikwa kwa kweli,Tupo kwa ajili ya kufaidiana.

  “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana”.1kor12:6

  Niaanze kwa swali,Unabii ulikuwako mpaka wakati wa Yohana,ndio Unabii huu wa sasa huduma/karama(ofisi)za Roho Mtakatifu?

  Unabii kama karama/huduma(soma1kor12)haupewi nafasi ktk kanisa la leo,Manabii waleo ni wanamna yake,ni wa agano la kale wakitumika ktk agano jipya,

  “ Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue’.1kor14:28”

  Siku hizi Nabii ni mmoja tu , Na ndio kiongozi wa hilo hema(Kanisa),Tumetweza unabii .Manabii wa leo ni watukufu.

  Wapendwa..
  “Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, lakini katika siku hizi za mwisho amesema nasi kwa njia ya Mwanawe..”Waebrania1:

  Tatizo hizi huduma (5)siku hizi zimebatilika nakuwa AJIRA,ndio…Kama kuna Mchungaji/Muinjilisti kwanini kusiwe na Nabii/Mtume anaongoza kanisa(hema)lake,Wakati maandiko yaonyesha Mtume apaswa aende huko kwa mataifa(makabila)apeleke injili ,Mtume wa leo ameketi watu wamfuate/waifuate injili.

  Mpendwa Orbi.. Unanibariki sana
  “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu……1kor13:8”

  Nahitimisha

  “ Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele… ndiye Roho wa kweli… atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia… yeye atanishuhudia…..atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo *YAJAYO atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. SITAWAACHA NINYI YATIMA; NAJA KWENU” Yoh14:15,16,17,25 – 15:25 -16:14,13(mwenye ufahamu na afahamu Nabii).
  KWA MAANDIKO HAYA YA YOHANA MTUME, UNABII WA AGANO LA KALE ULIKOMA.
  *
  Tunajifunza,Barikiwa

 55. Mjadala huu ni muhimu, mbarikiwe wote mnaochangia, kwa vile maandiko yalishasema kuwa watakuwepo manabii wa uongo ( Mathew 24:24) naona ni vema wachangiaji mngejadili jinsi ya kuwatambua hao wa uongo maana Yesu alisema wataweza kuwadanganya yamkini hao wateule! Tukishajua wa uongo wanafanya nini basi itakuwa wazi pia na wa kweli wanafanya nini leo ktk kanisa kama wapo.

 56. Wapendwa, wanablog Mungu awabariki!

  Nashindwa nianzie wapi, kujibu hoja za wengi na kutoifanya mada ichukue mkondo mwingine, Kwa ndugu yangu Mabinza naona umetoa maelezo marefu, Na kusema Manabii LAZIMA watakuwepo TU LEO LAKINI BILA HATA KUTHIBITISHA KWA ANDIKO LOLOTE kutetea hoja yako! unasema kwamba hoja zangu hazisimami kwa Paulo, ni Kweli , lakini kwa upande wangu nadhani nikimtumia Paulo nitamaliza hoja hii mapema mno ! Mimi naamini usipomwelewa Yesu ni nani, alifanya nini, anafanyi nini sasa hivi Mbinguni, NI vigumu mno kumwelewa Paulo! Ilifanyika hivyo huko nyuma kwa makanisa ya kwanza na inafanyika hivyo hivi leo kwa Kanisa la sasa! Paulo alimwelewa Yesu…..! Na ukimwelewa Paulo na mafundisho yake ni vigumu mno kusimama na kuwashabikia Mitume na Manabii hawa wa leo! (Nikipata muda nitaanza kupitia Nyaraka za Paulo hatua kwa hatua, waraka kwa waraka tuone hawa Manabii wa kizazi hiki wanaochunga na kulea Makanisa wanasimama wapi hata katika Injili ya Paulo!

  Kwa wengi wanaotetea mfumuko wa Manabii wanaanza kwanza kwa kutumia kwanza Agano la Kale hata kabla ya kuja Agano jipya na kumtumia PAULO……Hebu leo nilipitie hili.

  Kwanza kabisa kuwalinganisha Manabii wa Leo na wa Agano la Kale ni upofu mkubwa wa kutoyatafakari Maandiko. Huwezi kabisa kuwaweka Manabii wetu wa leo Wanaolea na kuchunga Makanisa KITU AMBACHO HAKIKO KABISA KATIKA BIBLIA katika kundi moja na Manabii wa Agano la Kale! Na kabla sijaanza kutumia Maandiko kuwatofautisha….labda niulize swali, Hivi nikiwaomba wale mnaotetea manabii mfanye summary fupi ya kazi ya Manabii Agano la Kale (na unabii wao) unaweza kutoa hitimisho gani? Kwa upande wangu mimi nitasema hivi;

  “MANABII KATIKA AGANO LA KALE WALIZUNGUMZA MANENO YA MUNGU KWA ISRAEL NA UNABII WAO MKUU WALIOUTOA NA KUTUACHIA NI UNABII WA UJIO WA YESU (MESSIYA) AMBAYO NDIO KUSUDI KUU LA MUNGU LA KUREJESHA UHUSIANO WAKE NA MWANADAMU.

  Hebu tuanze na Musa kama Nabii, na tutembee Naye mpaka Agano Jipya……unaweza kufanya safari hii na Manabii Wakuu (Major prophets) na Manabii wadogo ( Minor Prophets) ukifuatilizia Nabii zao kukufikisha kwa Yesu na Wokovu wake! Hii ndio iliyokuwa sehemu kubwa ya kazi yao! Kama tunajifunza kitu kwa Manabii hawa kazi yao haikuwa miujiza tu…..Haikua kushusha moto!…..Kusimamisha mvua…..nk

  MUSA;

  Kabla ya Israel kuingia nchi ya ahadi Musa nasema;

  “ BWANA MUNGU WAKO ATAKUONDOSHEA NABII MIONGONI MWA NDUGU ZAKE KAMA NILIVYO MIMI MSIKILIZENI YEYE……MIMI NITAWAONDOKESHEA NABII MIONGONI MWA NDUGU ZAKO NAMI NITATIA MANENO YANGU KINYWANI MWAKE MSIKIENI YEYE (Kumbu 18:15,18)

  Na baada ya miaka mingi mno kupita angalia unabii huu unavyoendelea…..

  PETRO;

  “KWA MAANA MUSA KWELI ALISEMA YA KWAMBA MUNGU ATAWAINULIENI NABII KATIKA NDUGU ZENU KAMA MIMI MSIKIENI KATIKA MAMBO YOTE ATAKAYONENA KWENU…….NAAM NA MANABII WOTE TANGU SAMWELI NA WALE WALIOKUJA BAADA YAKE WOTE WALIONENA WALIHUBIRI HABARI ZA SIKU HIZI (Matendo 3:22-24)

  “LAKINI MAMBO YALE ALIYOHUBIRI MUNGU TANGU ZAMANI KWA KINYWA CHA MANABII WAKE WOTE YA KWAMBA KRISTO ATATESWA AMEYATIMIZA HIVYO (Matendo 3:17)

  LUKA:

  (Anaandika kile alichosema Yesu)

  “AKAANZA KUTOKA MUSA NA MANABII WOTE AKAWAELEZA KATIKA MAANDIKO YOTE YANAYOMHUSU YEYE (Luka 24:27)

  “KWA MAANA MANABII WOTE NA TORATI WALITABIRI MPAKA WAKATI WA YOHANA (Mathayo 10:13) (Maneno ya Yesu)

  Angalia Yesu alipokutana na Manabii wakuu Musa na Eliya…..Sauti ya Mungu ilisema nini? “HUYU NI MWANANGU MPENDWA MSIKIENI YEYE”

  Sasa ndugu zangu wapendwa nimeanza na Unabii unaotokea Kumbukumbu la Torati na unotiririka hadi kumfikia Yesu…..na Yesu anauthibitisha, maana tumeona Nabii kuu za Manabii Agano la Kale ni kutupeleka kwa Yesu…sasa hawa Manabii wa leo wanatabiri lipi jipya? Au wanafunua nini kilichofichika toka kwa Mungu? Au ndio wanafichua kuwa wao watakaa pembezoni mwa kiti cha enzi na kumsaidia Yesu kutuvika Taji? Maana ndio ujumbe tulioupata kipindi Fulani toka kwa Nabii anayejiita wa taifa….!

  Wapendwa, Maandiko tunayo……Roho Mtakatifu, msaidizi wa kutufikisha kwenye Kweli yote yupo……Tunaweza kupangia Patakatifu kwa NJIA ALIYOTUANZISHIA……Sasa hawa Manabii wa leo ambayo tunaona wakilea makanisa badala hata ya kutumia karama za kinabii ndani ya Kanisa wana lipi jipya?…..Je ni kutoa pepo……Ni kufanya miujiza……Je hii kweli ni kazi ya Nabii……ndio Mwenyezi Mungu ametuletea kufanya hayo?

  MBARIKIWE

 57. Mpendwa wangu ORBI. Nimefurahi kuona kwamba mjadala huu nimeuanzia kati, nikweli kwamba sijapitia nukuu na maelezo yote yako juu ya jambo hili. Kwanza niseme kwa kifupi tu kwamba “nimekubaliana na wewe” kwamba manabii wa leo wamekuwa wengi,kama vile wanajitokeza tu bila mpango! kwakweli ni wengi.lakini watu hawa wapo vile kwa sababu ya matamushi ya MUNGU MWENYEZI, na si vinginevyo! MUNGU akisema amesema,pia yeye bidii yake kubwa kuliko yote ni kuchunguza kile alichokwishasema APATE KUKITIMIZA-tena Neno lake analiheshimu sana kupita hata JINA LAKE! Kwa mjibu wa BIBLIA kuhusu MANABII wa leo ni fupi tu ni kwamba WATAKUWEPO! Wewe ni msomaji wa Biblia, upo wakati YESU alisema watakuwepo……WAUONGO! Mitume nao walipata kusema kuwa watakuwepo…..KAMA MOJAWAPO YA HUDUMA KANISANI. Sasa utaona kwamba, kumbe manabii hawa wapo wa aina MBILI, yaani WAUONGO NA WAUKWELI! tunawajua si kwa “kuzuka” kwao kama uyoga, bali kwa kile WANACHOFANYA,Jiulize polepole bila jaziba wana”FANYAJE?” WANATENDA KAMA BWANA YESU KRISTO na wanakwenda na mafundisho ya MITUME? Ukiona ndiyo, hao ndiyo manabii ndani ya huduma ya kanisa la BW.YESU KRST. Manabii wakweli hatuwatambui kwa miujiza wanayo ifanya,maana BW.YESU KRST. Aalisema, wakati alipomtendea mtu muujiza”IMANI” yako imekuponya, kumbe utaona kuwa mtu akiamini lile neno bila hata kujali ni nabii wa aina gani kasema mtu huyo atapona kwakuwa lile neno lililoaminiwa lipo! BW. YESU KRST, aliwaambia wanafunzi wake wasifurahishwe na matokeo ya miujiza wanayoifanya bali tu”KWAKUWA MAJINA YAO YAMEANDIKWA” Labda nisimalize bila kusema hiviKWAKUWA NENO LINASEMA KUTAKUWEP MANABII WAUONG,BASI NA WAUKWELI LAZIMA WAWEPO! maana bila giza mwaga nao haupo, huwezi kusema nguo hii ni chafu bila kuilinganisha na ile safi.SASA LABDA NISEME KAMA KICHAA KWAMBA,UKIONA MANABII WAUONGO WANAZUKA KAMA UYOGA NAMNA INAYOKUJURISHA KAMA NI WA UONGO, PIGA KELELE NA USHANGILIE SANA KWAKUUWA NENO LA MUNGU KUMBE NI LA KWELI NA LIMEHAKIKISHWA KAKA YANGU MPENDWA NAOMBA NISEME TENA KAMA KICHAA KWAMBA,HEBU ZUNGUMZA POLEPOLE NA PAULO KATIKA MAKALA ZAKE,HUMO UTAGUNDUA UTAJIRI MKUBWA WA SILI ALIZOFUNULIWA ILI ATUAMBIE SISI TULIOKUWA WA MATAIFA,PAULO NDIYE JAMAA YETU SISI WA NJE YA UYAHUDI KWA VYOVYOTE VILE ANAJUMBE KWETU TUKIITIMIZA HAKI YOTE HAKUTAKUWAPO NA SILI TENA. amesema hivyo ktk 1korintho 13:9-10. Nisamehe kaka kama kama nimezungumza mengi yapo nje ya kile hasa unachotaka. “

 58. Shalom watumishi wa Mungu!

  Nashukuru kwa mleta mada hii, maana hakika nimejifunza kitu. Lakini ningependa kujifunza zaidi ili niweze kuelewa kuhusu hii huduma. Nitashukuru sana mtumishi Urbi katika somo lako kama utaweka pia yafuatayo:
  -Nabii ni nani, hapa namaanisha inabidi uwe na sifa/karama zipi ili uwe nabii wa Mungu?
  -Katika Biblia, manabii waliokuwepo ktk agano la kale au hata jipya kama walikuwepo, walianza wenyewe kujiita manabii au kutokana na karama zao wapendwa wanaowazunguka wanawaita manabii???
  -Wanaowatawaza au kuwapaka mafuta kuconfirm kuwa ni manabii ni wakina nani? Au hili la kutawazwa halipo katika huduma hii?
  -Nimeona mtumishi mmoja ana karama za kinabii lakini yupo chini ya mchungaji ambaye haamini haya mambo ya hizo karama, sasa hapa inakuwaje wapendwa?

  Natanguliza shukrani.

 59. Nadhani nami nilitumia muda fulani kuchangia mada hii na ninashukuru kuwa watumishi wa Mungu mmejitahidi sana kufundisha na kuelekeza kuhusiana na mjadala huu kwa moyo mmoja.

  Lakini mimi binafsi napata shida na maelezo ya ndugu Orbi kuhusiana na tafsiri ya meelezo yake.

  Kwake analeta picha ya huduma ya agano la kale na agano jipya akitenganisha huduma katika meneo matatu yaani: Unabii,Ukuhani na Ufalme.
  Sipati tatizo kama tafsiri hii anaitazamisha kwenye agano la Kale ingawa ninatofautiana naye kwa kiasi kikubwa.Endapo nitapata nafasi tena nitajaribu kuogolea huko.
  Lakini leo ninataka kufunua kile nikijuacho kuhusiana na ufafanuzi wa ndugu yangu mpendwa na kile ambacho Bwana Yesu amekifunua kwenye mafundisho yake.
  Wapendwa hebu tujaribu kutulia na kusoma vizuri waraka kwa waebrania na tutaona jinsi Bwana Yesu alivyofunua ufalme wa Mungu kwa namna ya ajabu kabisa.
  Labda nitofautiane kwanza na mpendwa wangu kuhusiana ufafanuzi wake katika maeneo yafuatayo:

  Kwa kuzingatia 2Kor5:18-19 tunafahamu kuwa Mtu akiwa ndani ya Kristo anakuwa kiumbe kipya ambacho ndani yake kunakuwa na NENO LA UPATANISHO ambalo kwa anayefahamu huduma ya makuhani wa agano la kale anafahamu kuwa hii ndiyo ilikuwa huduma yao kuu.Walipokea dhambi za watu (Hes18:21-24;Mambo ya walawi 16:18 n.k) wakazipeleka mbele ya kiti cha rehema ili kufanya upatanisho.Pia walikuwa na jukumu la kuwakilisha mahitaji mbali mbali ya wana wa Israeli na kuyafikisha kwa Mungu.Hatimaye walikuwa wakipokea maneno kutoka kwa Mungu (Aidha kwa kusoma Torati ama kupokea maagizo toka kwa Musa,Haruni ama makuhani waliosimama kwenye nafasi ya ukuhani mkuu)na kuyapeleka kwa wana wa Israeli. Lakini katika agano jipya,KIUMBE KIPYA anakuwa na neno la upatanisho ndani hivyo ANAKUWA NA UJASIRI WA KUKIENDEA KITI CHA REHEMA CHA MUNGU (Ebrania inatufundisha hivi).Kwa hiyo UKUHANI KATIKA AGANO JIPYA SI HUDUMA ILIYOTENGWA KAMA HUDUMA NYINGINE BALI NI HUDUMA YA LAZIMA KWA KILA AAMINIYE.NI SEHEMU YA MAISHA YAKE YA KILA SAA YA WOKOVU ndiyo maana mtume paulo katika 1Korintho14:1-2 anasema kuwa “Takeni sana Karama zilizo kuu lakini zaidi sana Mpate KUHUTUBU”

  Kuhusu huma ya Kifalme ambayo nadhani mpendwa alitaka iwe huduma kama UTAWALA FULANI HIVI.Bwana Yesu anatufundisha kuwa UFALME WAKE SI WA DUNIA HII tena anatufundisha kwa kinywa cha mtume Paulo kuwa tutazame juu Kristo alipo ameketi kwenye kiti cha enzi cha Mungu baba.Kitabu cha Waebrania katika mojawapo ya mafafanuzi yake kuhusiana na UKUHANI WA YESU inasema kuwa ukuhani wake Yesu ni kwa mfano wa Melkizedeki,akimaanisha kuwa sisi tuliookolewa na Yesu ni Makuhani na pia Wafalme kwa mfano ule ule wa melkizedeki katika ulimwengu wa Roho si katika mwili huu. Hivyo kwa hakuna tofauti kati ya kuwa KUHANI NA MFALME KATIKA AGANO JIPYA.
  Kuhusu huduma ya UNABII,niwe wazi kuwa sioni tatizo la tafsiri kwa huduma hii kwani ni moja ya HUDUMA kati ya zile tano ambayo jukumu lake ni kuwakamilisha watakatifu ili mwili wa kristo ujengwe hata kufikia cheo na utimilifu wa kristo. Tatizo tulilo nalo leo hii ni kuzifanya baadhi ya HUDUMA KUWA NI VYEO kama uchungaji,uinjilisti,ualimu n.k kwa hiyo tunataka na CHEO CHA UNABII NACHO KITAMBULIKE.Lakini kwangu mimi naona kuwa tunao manabii na wanafanya kazi zao vizuri tu ila tatizo ni kuwa tumeshindwa kuwapambanua kwa kujaribu kulinganisha huduma hiyo kwa kipimo cha vyeo vya makanisa yetu ya siku hizi,jambo ambalo naona kama limelifanya kanisa kudumaa.

  Nadhani inapendeza tunapoingia kwenye ulimwengu wa Roho na kutafuta kwa kina mafundisho ya kweli ya Kristo Yesu ambaye alituahidi kumleta kwetu msaidizi ambaye mojawapo ya majukumu yake makubwa ni KUTUKUMBUSHA KUYASHIKA YOTE ALIYOTUAMURU.
  Mungu awabariki sana wapendwa wake Yesu Kristo.

 60. Ndugu Oguda,

  Kwanza niombe msamaha kwako na labda kwa wengi, inawezekana lugha yangu kwe wengine imekuwa ni makwazo, sikuwa na maana ya kumkwaza yoyote, Kusema kuwa “manabii wanachipuka kama uyoga” ni matumiza ya lugha ya picha tu, yaani kitu kinachoota au kinachotokea haraka! Au kinakua kwa haraka.Je si kweli labda mtazamo wangu, hebu angalia wingi wa manabii na mitume wanaotokeza leo nchini! Naogopa kutumia neno “wanaochipuka” leo Tanzania, Kila kukicha kuna Nabii….Mtume……Je hii haileti maswali?( Kitabu cha Matendo ya mitume ambacho kina coverage kubwa ya Muda yaani kupaa kwa Yesu na hadi Paulo akiwa Rumi kina manabii wachache sana kuliko mlipuko wa manabii wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano! ) Hata kwa wale wenye msimamo wa Kuwa Mungu anatusimamishia Manabii leo, nao pia wanashangaa kuwa basi lazima Mungu anataka kutuambia kitu fulani labda cha tofauti….unique…..ambacho tumeshindwa kukielewa hivyo akaamua kila kukicha kutuletea Nabii!

  Sasa Labda nirudi kwenye Nukuu yako ya Luka 11:47- 52. Kwanza sijaona nukuu hiyo ikifungua mlango wa kuwepo kwa Manabii, context ya Maandiko ambayo imetokea kuanzia Injili ya Mathayo 23:1-23 Haizungumzii ujio wa manabi bali ni kuonya UNAFIKI WA MAFARISAYO! Na tukitaka kuyaweka maandiko mahali pake hasa mstari wa 47 uliounukuu unaona Yesu anawaambia Wayahudi kuwa wanajenga Maziara ( Monuments) ( tombs) (Makumbusho labda ingekuwa tafsiri sahihi) ya Manabii waliopita lakini baba zao ndio waliowaua hao Manabii ambao Mungu alikuwa amewatuma kwa taifa la Israel.Kwa kifupi Yesu anazungumzia Unafiki wa Mafarisayo…..kuwa mnatukuza Makaburi/Makumbusho ya Manabii lakini kumbe ni baba zenu ndio waliowauwa Manabii hao hao! Ni contradiction!

  Na ndugu yangu Oguda ukitaka kuyatendea haki Maneno haya ya Yesu Uliyoyanukuu unaona ambavyo Yesu anakumbusha kuwa Israel wameletewa manabii (Kipindi chote cha Agano la Kale – Manabii; Agano jipya; Mitume ) Lakini ni nini yalikuwa matokeo yake? “TAZAMA, NITATUMA KWAO MANABII NA MITUME NAO WATAWAUA BAADHI YAO NA KUWAFUKUZA”

  Na kwa vile Maandiko ndio hutafsiri Maandiko hebu soma Mahubiri yote ya Stephano Matendo 7:1- 53 Na Stephano anamalizia mahubiri yako kwa Kusema ” Enyi wenye singo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio sikuzote mnapinga Roho Mtakatifu….kama baba zenu walivyofanya na ninyi hivyo.NI YUPI KATIKA MANABII BABA ZENU HAWAKUMUUDHI? NAO WALIWAUA WALE WALIOTABIRI HABARI ZA KUJA KWAKE YULE MWENYE HAKI”

  Hivyo ndugu yangu sioni nukuu yako ikitoa mchango wowote kuwatetea hata kuonya kuwapinga Manabii walioko leo. Na hata hivyo sijakuelewa ulivyotumia neno “MAZIARA”

  Wakati natafuta muda kuendelea kujibu hoja zako, Labda niseme neno “USIHUKUMU” ambalo umeniasa nalo, ningependa kusema halitumiki vyema Leo! Ni sawa na Neno “Usimnenee vibaya Mtumishi wa Bwana” Naomba Neno hilo au Maandiko hayo yatumike ipasavyo katika wigo wa MAANDIKO! Je ni kila mtu anayejiita Mkristo ni mtumishi wa Bwana? Ni kweli kila anayejiita Nabii ni nabii wa Bwana? Au Mtume?Au anahitaji maombi yangu? Au ya watakatifu wa Bwana? Utasemaje juu ya mbwa mwitu waliovaa ngozi ya Kondoo? Basi Biblia isingetuonya kwa hilo! Kwangu mimi ndugu aliyekatika Kristo ni yule ambaye HUDUMA YAKE, MAFUNDISHO YAKE, MWENENDO WAKE UMEJENGWA KATIKA MANENO YA MUNGU! Sio title! Sio Upako! Sio miujiza tu!

  Kama nilivyosema nitaendelea baadaye kwa yale uliyoniuliza.

  ubarikiwe.

 61. SHALOM MTUMISHI ORBI?

  Samahani ndg wapendwa ktk Bwana Yesu, kwani, nimekuwa kimya, ni ajili kutokutulia chini, sehemu moja. Sasa, tuendelee, kwakuwa, ni mdau eneo hili sana.

  Pia, naomba nitahadharishe wandugu kuwa, mimi, sichungwi na Mtume wala Nabii awaye yote, yaani, siko chini ya watumishi wanaoongoza huduma ama makanisa kwa huduma hizo, hivyo, ujadili wangu haufungamani na kundi lolote, zaidi ya mitazamo yangu binafsi kama mtumishi wa injili.

  NINAPENDA KUJIFUNZA ZAIDI TOKA KWAKO, HASWA KTK MADA ZENGINE, NAAM, KTK MADA HII NIMEJIFUNZA PIA KITU LAKINI ZAIDI KWA MWL.ANTHONY MWENDA, NIMEFURAHISHWA ZAIDI NA JINSI ALIVYOTOA FAFANUZI MURUA JUU YA AINA ZA UTENDAJI WA HUDUMA HIZI KTK MAAGANO YOTE MAWILI NDANI YA BIBLIA HII TAKATIFU.

  Ktk majibu yako kwa maswali yangu, bado sijakupata sana, kwakuwa,, sehemu kubwa hukunijibu, bali umeniswali tena, namna hii, sivyo mtumishi.

  Mimi, ninadhani ndg. yangu, tuwe, SINCERE tu, kwani, ninachokiona hapa katika mjadala huu uliouanzisha wewe binafsi, ili kupata mawazo ya wengi, umekuwa CRITICIZER Zaidi, hukuwa UMELENGA tuelimishane juu ya baadhi ya hizi Huduma kama za KITUME na KINABII, bali ULILENGA kwa kuweka msingi tuanze kuchambua hao Watumishi wanaotumika katika vipawa hivyo, na sasa, nime note, umeendelea sana, siyo mbaya, lakini, ntajitahidi nijibu baadhi ya hoja ulizonielekezea.

  Naomba nianze na hili la ulilohoji, kuwa, wengine twawatetea, ………….”KUWATETEA”………….., niseme jambo hapa, though kwakweli, si kwamba TWAWATETEA, bali ni kujaribu KUMJUA Mungu, kwani, katika kitabu cha LUKA 6:37, anasema, “MSIHUKUMU, hamtahukumiwa, M S I L A U M U, ………………………..”,. My point is, tusiwe wepesi kulaumulaumu tu kila tukio la kijanga linapotokea, WALA TUSIWAFANANISHE Watumishi, tutakosea, namaanisha, usiwafananishe hawa, na labda Nabii T.B. Joshua, wa Nigeria, ntakwambia sababu, ‘Unaweza ukawa mtu wa Rohoni sana, Bwana asikufunulie baadhi ya mambo, kwani, mafunuo ni neema ya Bwana pia, na mapenzi yake, vilevile; kwani, haikuandikwa kuwa, ” Ombeni, mtapewa”, je, ni kila ukiombacho unakipata?

  Kuna sehemu umeshauri vizuri sana ya kuwa, kama, kuna mtu anakuja kwa ajili ya KUWATETEA hawa Manabii, aje na maandiko, lakini pia, ukaongeza kuwa, hata Bwana Yesu mwenyewe hakuwahi kuwatetea ( have i misquoted you, Sir?). Hebu naomba tulitazame hili andiko la LUKA 11:47-52, anawaasa nini Wanasheria; “OLE WENU, kwakuwa, MWAJENGA MAZIARA YA MANABII, na baba zenu ndio waliowaua. Basi, nawashuhudia na kuziridhia kazi za baba zenu kwakuwa, wao waliwaua, NANYI MWAWAJENGEA MAZIARA. Na kwa sababu hiyo, Hekma ya Mungu ilisema, Tazama, NITATUMA KWAO MANABII NA MITUME, NAO WATAWAUA baadhi yao na KUWAFUKUZA, ili kwa kizazi hiki itakwe damu ya Manabii wote iliyomwagika tangu misingi ya ulimwengu”.

  Hii habari ya ‘MAZIARA’ ni ya kujiadhari nayo sana, kuwaita majina kadha wa kadha humu mtandaoni ni kuwajengea maziara, sijaelewa kama ndo CRUSADING against God’s servants, utanisaidia.

  Orbi ndg yangu, kitu kikubwa hapo jaribu kuwaombea ili waondokane na mapungufu unayoyashuhudia kwao.

  Jambo lengine ambalo yamkini, wewe unalisahau, au pengine unaamini katika misingi ya Kichungaji tu, ni hili, Bwana Yesu HAKUSAZA kitu kuhusiana na habari za huduma zile tano, YOHANA 10:11-13, anatujuza zaidi, akijifafanua kwetu ya kuwa, yeye ndiye Mchungaji mwema hakuna mwengine, maana, wengine hukosa HURUMA na Kondoo zake, tena anasema ya kuwa, hao ni Wachungaji wa MISHAHARA, lakini, akaenda mbali kidogo, akazungumzia na WAHUBIRI (Evangelists), katika WAFILIPI 1:15, anasema, ” Wengine WANAHUBIRI habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitna; wengine kwa nia njema”.

  Mimi ushauri wangu tu kwako, uwaonapo hao Mitume ama Manabii, kwa upande wako, hawana viwango kama akina Mtume Paulo, please, mosi, waombee.

  Pili, licha ya kuwaombea ili wapate mabadiliko, lakini pia hili la ya kuwa, hawana viwango vya kuwalingana wale wa kwenye Biblia kama akina Paulo, na wengineo, jambo moja ningependa nikwambie, pengine na wengine wetu mahala hapa, KAMWE, hili la kuwalingani ahalitakaa liwe, kwa maana, imeandikwa ya kuwa, “LAKINI, kila MMOJA HUPEWA Ufunuo wa Roho kwa KUFAIDIANA”, na katika aya nyengine, anaongeza, “LAKINI KAZI hizi zote HUZITENDA Roho huyo mmoja, yeye yule, AKIMGAWIA KILA MTU PEKE YAKE kama APNDAVYO YEYE”, 1KOR.12:7,14.

  Zipo lugha nazisoma humu, kwa mfano, ‘ Hao Manabii WANAOIBUKA kama UYOGA’, hizi ndg, si zenyewe, sisi tumekombolewa, we have our own language commands, let it be pleasant, please, na pia, hata hayo ma UYOGA si kweli ndg,hii ni EXAGGERATION ambayo imepandwa vinywani mwa watakatifu nyakati hiz za mwisho, nikuulize tu swali lepesi, hata kwa haya macho ya nyama, kanisa Tanzani lina idadi ya Wakristo wangapi walioamini, pmj na madhehebu yao na dini zao, wanalingana kweli na hicho unacokiona kanakwamba ni sura ya uyoga??? Simply, does the number of believers, and their denominations match with the so called uyoga ama utitiri huo? Mbona hao Mnabii wenyewe wanahesabika tu, tena kwa mimi, binafsi, mtizamo wangu, na baado sana wanapaswa wawepo, kwani, ni ahadi ya Bwana Yesu mwenyewe, maana, amesema, ‘na wengine’, hatujapewa namba yao itakuwa ngapi, tusiizuie kazi ya Bwana ndg yangu. Kwanza ni hapa tu kwetu ndo tumechelewa ku implement maandiko, ili Bwana ajitukuze miongoni mwetu.

  Lakini pia, usisahau jambo hili ya kuwa, hao Manabii na Mitume, wanayo makundi ya kondoo za Bwana wanayoyaongoza, watatoa hesabu,kama ilivyo, nami, nawe, tutatoa hesabu mbele za Bwana, ndio maana, Mtume Paulo alipoona aina hii ya mashambulizi, kwakuwa, wakristo wa wakati huo, wengine alikuwa wamehubiriwa na akina Petro, Yohana na Mitume wengine, hawakumjua Paulo na aina ya mafunuo yake mengimengi, walimwita kwa lugha hizi hizi kama tunavyowaita hawa kuwa ni mauyoga, ama mautitiri, na kuwakana, ndiposa, akaamua kuwapiga muhuri wale aliowahubiri na kuwaleta kwa Yesu, akisema; “Je, mimi si huru? Mimi si Mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? NINYI SI KAZI YANGU ktk Bwana? Kwamaana, IKIWA MIMI SI MTUME KWA WENGINE( WATANZANIA, WAPENTEKOSTE), LAKINI NI MTUME KWENU NINYI; Kwamaana, NINYI NDINYI MHURI wa Utume wangu katika Bwana!!Hilo ndilo jawabu langu kwa wale (Wa Tanzania, Wapentekoste wa leo) WANAONIULIZA”. 1KOR.91-3.

  Ninapomalizia elimu hii kubwa kwa kufaidiana, natanguliza shukrani zangu za dhati katika Roho mtakatifu, nikitumai, mtapokea kwa furaha ya ushindi ujumbe huu, pasipo makwazo, nami, kama mtu tu, ninaomba nisamehewe in advance. LAKINI PIA, tukumbushane kwa mwenendo huu, 2TIM.3:16, “KILA ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU LAFAA KWA MAFUNDISHO, ILI…………”.

  Wako katika utumishi,

  OGUDA J.E.

 62. Ndugu yangu Mabinza,

  Labda urudie tena maandiko yangu ambayo nadhani yako wazi mno, kiasi cha kwamba ndugu John na Lwembe wameweza kuuendeleza Mjadala! Kwa kifupi aliyesoma post zangu atatambua kuwa napata mashaka na kwa sehemu kubwa natatizika na huu mfumuko wa Manabii na Mitume wa leo! Nadhani ukirudia maandiko yangu utaona wazi ni kwa sababu gani………na baadhi ya posts za wanablog zimedhirisha wazi kuwa si wote wanakubali huu mfumuko wa Mitume na Manabii leo!

  Labda kwa kukujulisha tu ndugu yangu Mabinza mimi si mtu “Nayekubali yaishe kirahis tu ….Hukubali kwa kuwa convinced kwa Maandiko tu…….katika wigo mpana wa Imani hii…..” Rudia tena post zangu nyingine katika blog hii…….

  Na tena kwa kukujulisha tu kuzitambua “roho zidanganyazo” hufanyika kwa kuifahamu KWELI ya Mungu tu kama inavyofunuliwa na Maandiko! Kwani roho zidanganyazo zitakuja kwa njia nyingi, kwa sura nyingi! zililisumbua kanisa la mwanzo…….zimelisumbua kanisa kipindi chote cha uhai wake…….na roho hizi zitalisumbua kanisa mpaka Yesu atapokuja mara ya pili! Hivyo Njia rahisi kabisa ya kuzitambua roho hizi ni kukaa katika Kweli!ambayo ni yeye KRISTO!

  UBARIKIWE!

 63. Ndugu Lwembe,

  Nilikuwa nafuatilizia mjadala kwa mbali……..nikitaka kusikia mawazo ya wengine……..nimefurahishwa labda niseme nimecheka mwenyewe kwa nukuu yako hii uliyomjibu ndugu John……..sikutegemea msimamo huu toka kwako……..!

  “……… kutokana na ufahamu huo……… simuoni yeyote kati ya manabii walioko hapa Tz wa kumnyooshea kidole kuwa amesimikwa na Mungu kwa ajili ya Huduma ya Unabii! Katika kambi zao zote, ninachokiona ni miujiza ya uponyaji na utajirisho na mambo mengine ya mwilini……..”

  Ndugu yangu Lwembe unaweza kuulizwa na Wapendwa………Kama hawa Manabii walioko Tanzania hawajasimikwa na Mungu, wamesimikwa na nani basi?

  Hebu tusikie wengine wanasemaje!

  MBARIKIWE

 64. SALAAM KATIKA BW. YESU KRST. NIONAVYO MIMI NDUGU LWEMBE NA NDUGU ORBI, WAKO PAMOJA. TATIZO LIKO KATIKA KUELEWA, ORBI HAJAJUA KUWA KTK KUMTETEA YESU NA KUONA KUWA YEYE (YESU) NDIYE ANAPASWA KUSIKILIZWA KULIKO MTU MWINGINE YEYOTE KUNA MAANA ILEILE KUWA NDIYO KUWASIKILIZA MITUME (KAMA VILE PAULO NA WENZAKE). HAINA MAANA KUSEMA UNAMSIKILIZA YESU ZAIDI NA SI MITUME WAKE. YESU KATIKA MANENO YAKE MWENYEWE YANAONYESHA WAZI KUWA “ALIWAKUBALI” SANA MITUME WAKE! LIPO NENO LA YESU LINASEMA …..”…NA JUU YAKO…… (akamtaja jina mmoja wa mitume) LITAJENGWA KANISA”. NA KWINGINE…….NAKUPA FUNGUO “FUNGUENI NA KUFUNGA” NAKWINGINE………..INGIENI KWAO MKAHUBIRI……….”ATAKAYE KATAA KUNG’UTENI MAVUMBI YA MIGUU YENU MUONDOKE….(Wapate laana)!” KUONYESHA KUWA NA MITUME WAJUA KUWA WAMEKUBALIKA,WALISEMA ……HATA IWE MALAIKA AU MTU YEYOTE ATAKAPO FUNDISHA INJILI ISIYO “YA MITUME WALE (Yaani akina Paulo) apate laana!” SASA SIJUI NDG YANGU ORBI HAKUBALI NINI! NA KWA UPANDE WA NDG YANGU LWEMBE ORBI ANACHOJARIBU KUSEMA NI KAMA HAWAKUBALI HAWA WATU WAJIITAO MITUME (Wa leo) KITU AMBACHO NDG LWEMBE KTK MAJIBU YAKE NAYE NI KUWA HAWAKUBALI HAO MITUME (Wanaozuka kivyao) AU WEWE NDG. ORBI UNAWAKUBALI ILA UNAZUGA TU? KAMA NDIYO SEMA NDIYO ILI UFUNDISHWE KUZITAMBUA ROHO ZIDANGANYAZO KAMA SIYO SEMA SIYO WAZIWAZI ILI YAISHE!

 65. Ndg C k Lwembe,

  Nashukuru kwa majibu yako. Nilichoelewa au muhtasari wa majibu yako kwa maswali niliyouliza kama yalivyokuwa ni:

  1. Nchini Tanzania Hakuna Nabii ye yote wa kweli!

  2. Kwa sasa Hakuna sababu ya Nabii kwa kuwa Roho mtakatifu Ndiye Nabii wa Leo!

  3. Uwepo wa lundo la manabii walioko leo ni batili!

  4. Manabii wa Uongo wataendelea kutenda kazi hadi ya siku ya mwisho!

  5. i).Eliya Nabii BADO HAJAJA!
  ii).Hakuna anayeweza KUOKOKA bila huduma ya Eliya nabii ajaye!

  6. i). Kanisa la Mungu kwa sasa NI KIPOFU!
  ii). Kanisa la Mungu, pamoja na kuwa limepofuliwa lakini, liko Imara
  iii). Ye yote anaye operate nje ya FUNDISHO LA MITUME ndilo dude linalojiwakilisha kama Kanisa.

  Nahitaji uthibitisho wako kama Nilivyokuelewa ndivyo ulikuwa unamaanisha. Nimeona nifupishe majibu hayo ili kama kuna mahali sijakuelewa vizuri upafafanue. Nimefikiria nisiulize maswali mengine kwanza hadi nione kama Nilivyoelewa ndivyo Ulivyokuwa umemaanisha!

  Nasubiri toka kwako!

 66. Naam, ndugu John Paul!
  Jina la Bwana libarikiwe!
  Kama ulivyo suggest, ni kweli, hii inaleta maana zaidi. Basi katika kuendelea katika hilo, kile kipengele cha (b), yale maneno ‘Pia nabii’ hayakupaswa kuwepo ni kosa la kutaipu tu, hivyo uniwie radhi kwa hilo pamoja na yeyote yule anayefuatilia mada hii.
  Katika kipengele ulicholiuliza swali lako la kwanza nimeandika: ‘(b) Nabii husimikwa na Mungu’. Hivyo ndivyo ilivyo kama nawe ulivyonithibitishia kwa Maandiko pale ulipowataja nabii Isaya na Yeremia. Kwa hiyo suala la nabii kumsimika nabii hilo halipo. Hilo si la kiBiblia! Hata Eliya hakumsimika Elisha, bali Mungu mwenyewe.
  Pili, kama utakumbuka katika maelezo yangu ya awali, niliongelea kuhusu Neno la Mungu kuwepo hapo kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa. Yaani Mungu alilinena huko nyuma ya wakati, nalo hilo Neno limekuwepo hapo likitanukia wakati (stretched out in time), na nikasema nabii anaponena si kwamba Mungu kaongea naye saa hiyo, bali huyo nabii amepelekwa juuuu, naye hulitazama hilo Neno katika utulivu wake, kulingana na wakati, naye hushuka nalo chini na kuwajulisha kusanyiko/taifa. Maana Mungu ayajua yote. Yeye ni Mwanzo na Mwisho! Basi tukiwa tumejengwa juu ya ufahamu huu, nasi katika wakati, tukiwa katika ile saa ya ukamilifu, mambo yote ya Torati yakiwa yamefafanuliliwa kwetu, twapaswa kuwa tumekua katika kimo kuhusu mambo ya Mungu. Hata akiinuka mtu yeyote kati yetu akasema mimi ni nabii, nasi Neno la Mungu likiwa limejaa ndani yetu, basi na atuambie na kutuonesha kwa Maandiko alipotabiriwa kuwepo, nayo Maandiko yatatudhihirishia hilo pamoja na huduma anayopaswa kuja nayo! Kristo aliwarudisha katika Maandiko ili wajishuhudie wenyewe kuhusu Yeye na Huduma yake.
  Pia nilisema Mungu humtumia mtu mmoja tu aliyejiachilia kwake katika kipindi. Pale kanisa linapokuwa limeiacha njia ya wokovu na kujichanganya na dunia, basi inapofikia katika wakati, kulingana na majira ya Mungu, Yeye huinua Nabii ili kulirejesha Kanisa lake katika njia Yake. Kamwe hatumii watu wawili au kundi. Watu wawili wangeleta mgongano wa mawazo kama unavyoiona migongano iliyopo leo hii. Tena, Mungu humkamata mtu wake kabla ya kanisa! Yeye humfanya mmoja tu kuwa Nabii wake, naye Mungu hujidhihirisha kupitia huyo.
  Basi, kukujibu swali lako, kutokana na ufahamu huo niliokueleza hapo juu, simuoni yeyote kati ya manabii walioko hapa Tz wa kumnyooshea kidole kuwa amesimikwa na Mungu kwa ajili ya Huduma ya Unabii! Katika kambi zao zote, ninachokiona ni miujiza ya uponyaji na utajirisho na mambo mengine ya mwilini. Sijaona huduma yoyote ile imhusuyo nabii, bali naona karama zisizo na majuto zikitenda kazi. Jambo jingine unalopaswa kutokulisahau ni nguvu ya Imani kwa Neno la Mungu. Imani huja kwa kusikia Neno la Kristo. Ukiyachunguza Maandiko vizuri, utaona kwamba asilimia kubwa ya walioponywa na Kristo, Imani yao kwa Neno la Mungu ilihusishwa; “Nenda, imani yako imekuponya”. Yule mwanamke aliyekuwa akivuja damu alipoligusa pindo la nguo ya Kristo, Kristo aligeuka na kuuliza aliyemgusa. Wanafunzi wake walimshangaa maana kutokana na umati alioongazana nao, watu kibao walikuwa wakimgusa hapa na pale, bali mguso wa yule mwanamke ulikuwa tofauti, ulibeba IMANI. Ndipo akamwambia ‘Imani yako imekuponya”. Umeona! Kazi nyingi wanazojivunia hawa wanaojiita manabii wa leo, kubwa ni uponyaji ambao kanuni yake ndiyo hiyo hapo; IMANI YAKO! Basi hata ibilisi akihubiri Injili watu watapona!!! Lakini Kristo alipofika kaburini kwa Lazaro na kumwita atoke humo, hiyo ilikuwa shughuli nyingine, hakuna IMANI ya Lazaro hapo! Kwa hiyo kimsingi, yeyote anayejiona ameitwa kuwa nabii, kabla hajatutangazia hilo, yampasa kumuuliza Mungu amuoneshe kazi anayomuitia katika PROGRAMU yake kama ilivyo katika Biblia. Kama hana sehemu humo basi na tujue kuwa huo ni UKOMA!!!
  Swali la pili na la tatu naona yanaendana. Kwa hiyo nitajaribu kuyajibu kwa pamoja.
  Ujio wa Roho Mtakatifu umeboresha mawasiliano kati ya Mungu na Kanisa. Pia ni jambo la muhimu kujua nafasi zetu katika uhusiano na Mungu. Iwapo tutajihesabia katika nafasi ya Israeli katika kulipokea kwetu Neno la Mungu, jambo hilo litatuondoa katika mtiririko tunaopaswa kuwepo. Wokovu wa Israeli unahesabika kitaifa. Lakini sisi wa mataifa ni tofauti, tunahesabika mmoja mmoja! Basi tunapoingizwa sisi katika Ufalme wake, mdundo ulibadilka kutoka ule mfumo wa Israeli kuja kwenye huu mfumo mpya wa Agano Jipya ambao unatuingiza humo. Ndio maana Kanisa limejengwa juu ya msingi wa Mitume na Manabii. Kwani kama ulivyosema; msafirishaji wa ujumbe kati ya Mungu na watu sasa hivi ni Roho Mtakatifu, ni sawa kabisa. Hilo linaendana na mfumo huu mpya kwa kadiri tunavyohusika sisi wa mataifa. Ndio maana Mungu ameziweka zile Karama tisa na huduma tano, vyote vya Roho Mt. ndani ya makusanyiko yetu madogo kwa ukamilifu huo wa uongozi na mawasiliano. Kwa kusisistiza hilo, Roho Mt. ndiye Nabii wa leo! Tukisoma katika Injili ya Yohana 16 kuazia mstari wa 13 inasema: Yeye atakapo kuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote. Kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayasema na mambo yajayo atawapasha habari yake .Yeye ananitukuza mimi kwa kuwa anatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.” ‘Yeye’ ni personal pronoun, yaani utu – kama kiswahili changu kiko sawa. Basi huyo lazima awe Kristo mwenyewe katika utu wa Roho Mtakatifu akiliongoza kanisa lake, akiwa tena ni Nabii kama alivyokuwepo katika mwili, yule Nabii wa Galilaya. Kwa hiyo hawa manabii rundo tulionao leo hii, watakuwa wanatenda kazi zao nje ya mfumo huu mpya, nadhani hawajauelewa bado, wakiuelewa watatafuta vyeo vingine!
  Kuhusu kuwaumbua hawa manabii waigiza vipawa, ni kweli katika Agano la Kale mambo hayo yalikuwa yakitokea. Lakini tukumbuke kwamba hao manabii wa uongo walikuwa na muda wa kutenda kazi kwanza ndipo ukaja muda wa kuumbuliwa kwao. Kwa hiyo, hata manabii hawa waliopo leo hii, pia wanaendelea kulingana na Programu ya Mungu kama alivyoionesha katika Mathayo 24:24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, yumkini, hata walio wateule.” Basi kulingana na Programu hiyo ya Mungu, hawa manabii wanaotokea katika siku za mwisho, hao wataendelea hadi Siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya itawafika wakiwa kazini, kama siku ile Sodoma ilipopigwa kiberiti! Lakini kanisa la Mungu lipo, nalo limeonywa kuhusu hao mapema. Jambo la kusikitisha ni kwamba hata hawa manabii wenyewe hawajui kuwa wanatumiwa katika uharibifu. Zile roho za kidini zinazowatumia, zinawatumia katika kiwango cha ‘VITI’ kama ambavyo wale roho wachafu wanavyo wafanya watu, bali kwa hawa ni katika ustaarabu na mambo hayo ya kuhubiri injili na miujiza. Kwa hiyo kuumbuka kwa hawa katika kiwango kidogo ndiko huku kunakoendelea sasa hivi kama ambavyo ndg Orbi na wengine waliopata Nuru wanavyofanya.
  Kuhusu Eliya nabii, nimekirejea kifungu hicho cha Malaki 4:5-6, ili kuonesha hicho nilichokiandika kuwa Huduma hiyo ya Nabii yapaswa kuja katika siku yetu ya leo kulingana na Nuru ya Maandiko inavyotuangazia. Vifungu vyote ulivyovinukuu kuhusu Yohana Mbatizaji kuwa ndiye Eliya, hilo ni sawa kabisa, kama Maandiko yanavyonena. Labda tukiangalie tena hicho kifungu tuone kinachosema. Nakinukuu tena: “ANGALIENI, NITAWAPELEKEENI ELIYA NABII, KABLA HAIJAJA SIKU ILE YA BWANA ILIYO KUU NA KUOGOFYA. NAYE ATAIGEUZA MIOYO YA BABA IWAELEKEE WATOTO WAO, NA MIOYO YA WATOTO IWAELEKEE BABA ZAO, …” Kama nilivyosema hapo awali, nabii hutambulika kwa huduma yake kimaandiko. Maandiko ndiyo yanayo mtambulisha. Sasa, kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye Eliya ajaye, hilo ni kweli kama Kristo alivyowafunulia wanafunzi wake, nasi pia. Hapa pia waweza kuona jinsi uigizaji ulivyo na hasara kwa wafuasi wake, maana makundi yote ambayo hawakumpokea Kristo, wengi kwa ushawishi wa viongozi wao ambao walikuwa wakitenda kazi nje ya mfumo, wapo hapo mpaka leo wakimsubiri Eliya yule aliyekwisha kuja! Kristo ni Neno, kwa hiyo hakosei wala hadanganyi. Hata unabii huo umetolewa kwa roho yake. Katika kuwajibu wanafunzi wake aliwaambia, NI KWELI ELIYA YUAJA KWANZA, NA KUREJEZA YOTE UPYA. Basi tunapoitazama huduma ya Yohana Mbatizaji, tunaiona ikitimia kulingana na Maandiko pia majira. Je, huduma ya Yohana Mbatizaji ilirejeza yote upya? Huduma ya Yohana Mbatizaji imewekwa wazi katika Luka 1:17 “ Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, …” Hii ndiyo inayoitimiza ile Malaki 4:5-6 Ile huduma aliyotengewa huyo Eliya ikitimia hapo katika kiwango kilichokusudiwa katika kipindi hicho cha kumtangulia Kristo katika kuja kwake kwa kwanza. Ukirudi katika lile andiko la Malaki utaona kwamba huduma ya Yohana Mbatizaji ili cover nusu ya sentensi tu, yaani hadi ile koma ya mstari ule wa sita. Yaani ‘ALIIGEUZA MIOYO YA BABA IWAELEKEE WATOTO’ tu. Maandiko hayakosei wala haya bahatishi. Basi tuyaonavyo ndivyo yalivyo, ndio maana hata lile Neno la Eliya KUYAREJEZA YOTE UPYA ni dhahiri kuwa linaambatana na huduma yake tena huyo Eliya atakapokuwa akiimalizia ile nusu ya sentensi (NA MIOYO YA WATOTO IWAELEKEE BABA ZAO,) ambayo Yohana Mbatizaji hakuitimiza, ambayo ndiyo inayoambatana na ile Siku ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya ambayo haikuja katika ile huduma ya Yohana Mbatizaji, kama nasi tulivyo mashahidi maana leo ni mwaka wa 2012 tokea nusu ya Andiko hilo litimie. Ujio wa Kristo ulikuwa wa kulivusha kanisa katika hatua mpya. Naye Yohana aliwatayarisha wale mababa wa Torati kumpokea Kristo (mitume – watoto) kama Maandiko yanavyo tufunza katika Mdo 19:4 “ Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu.” Nasi tumeingia katika Injili katika mtiririko huo.
  Pia, Ndugu John, mambo mengi katika Agano la Kale yanafungukia katika Agano Jipya. Unaweza kukisoma kifungu katika A/kale ukakiona kimejitosheleza, yaani ukakiona kana kwamba katika kutimia kwake itakuwa wakati fulani yaani wakati mmoja. Kama vile kuzaliwa kwa Kristo nk. Lakini kuna vifungu pia ambavyo hutimia kwa sehemu katika nyakati tofauti hata mpishano wa zaidi ya miaka 2000 kwa koma au nukta tu. Tazama kifungu hiki cha Isaya 61: 1-3 “Roho ya Bwana Mungu i juu yangu ; … Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu….” Kristo alipokisoma kifungu hiki katika Luka 4:18-19 aliishia “Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,” akafunga chuo kisha akawaambia leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Hakumalizia kile kipande cha kilichobaki kinacho husu kisasi cha Mungu kwani siku yake ilikuwa bado nayo ndiyo tunayoiendea ambapo Kristo atarudi tena kwa ajili hiyo. Je, akirudi ghafla leo hii akawakuta hawa manabii walivyowakusanya watu wasio na hatia ndani ya makusanyiko yao yaliyo nje ya mfumo wa Mungu, itakuwaje, si tutaangamia wengi kwa kukosa maarifa! Ndio maana atatangulia tena Eliya nabii ili AYAREJEZE YOTE UPYA yaliyopotshwa ili Kristo akija aikute IMANI. Hiyo ndiyo huduma ya ile nusu ya sentensi ‘NA MIOYO YA WATOTO IWAELEKEE BABA ZAO’ inayotuhusu sisi ya kutugeuza sisi tuliozaliwa katika Injili ya mitume na mbele huko tukakengeuka na kuiacha Injili hiyo na kugeukia mafundisho ya mapepo yaliyotugawa makundi makundi yaliyojaa fitina, wivu, unafiki na uchafu wote kiasi kwamba hakuna anayeweza kuokoka bila ya huduma hiyo kutujia. Pia kulingana na kanuni yake Mungu aliyojiwekea, Kristo hawezi kuja bila kuwajulisha watumishi wake manabii kwanza, basi twapaswa kumshukuru Mungu kwa hilo na tumtegemee nabii huyo Eliya ili tuweze kupewa hiyo Siri ya Mungu itakayo kuja na huo urejezo.
  Kuhusu kanisa kupofuliwa, wewe mwenyewe ni shahidi. Idadi ya manabii wanaopingana na tofauti za kidhebu zilizopo zinathibitisha hilo. Matumaini yanapopotea, ndipo Mungu huingilia kati. Kama vile Elia alivyomlilia Mungu akidhani kwamba watu wote wamepotea , wanampigia magoti Baali, Mungu alimwambia anao 7000! Basi tumaini letu liko katika Ahadi yake ya kutuletea Eliya nabii.
  Kanisa la Mungu lipo imara. Kama unavyoliona katika siku ya Eliya, alipodhania limepotea, bado Mungu alimjulisha kuwa lipo! Hata leo ndivyo ilivyo kwani uhai wa Kanisa umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu (Kol 3:3)! Na hata kama ulikuwa umestray ukatekwa na adui na kupofuliwa macho, Sauti ya Mungu itakapoita kupitia nabii wake, Eliya, basi kama ilivyokuwa kwa Samson, yule mnadhiri wa Bwana aliyetekwa na Wafilisti, nawe utaitafuta NGUZO yao kuu ya hao manabii na kuivunja ili BWANA atukuzwe tena kupitia wewe!
  Dude linalojiwakilisha kama kanisa kwa kifupi ni yeyote yule anaye operate nje ya mfumo uliowekwa, yaani FUNDISHO LA MITUME
  Ninakushukuru kwa kutoa wasaa wako kwa ajili ya Injili
  Ubarikiwe!

 67. Mpendwa C k Lwembe, Nashukuru kwa kuniruhusu kuuliza maswali hayo sasa. Nayo ni haya yafuatayo:

  1.Sina mashaka na kazi (a) na (c) za Nabii kwa kuwa hiyo ni Biblia kabisa! Lakini swali langu linakuja katika sehemu (b) ambapo umeandika: “Nabii husimikwa na Mungu mwenyewe. Pia nabii”

  Katika Biblia kuna maandiko yanayoonyesha jinsi Mungu mwenyewe alivyokuwa anawaambia manabii kama Isaya na Yeremia kuwa amewaweka yeye mwenyewe, na jinsi alivyowachagua kwa ajili ya kazi zao. Nao kweli wakasimama na kuendelea na utumishi huo wa Unabii na watu wakatambua kuwa kweli hawa ni manabii. Lakini katika kizazi chetu cha sasa Je,

  i) Kuna nabii ye yote, kwa jina, ambaye tunaweza kumnyooshea mkono kuwa HUYU NI NABII? Iwe ni kwa kuwekwa na Mungu au nabiii mwingine? Maana mtu akisema yeye ni MCHUNGAJI wala hakuna mtu anauliza uliza, lakini mtu akisema yeye ni NABII…Lo! Utakuta tayari watu wanaanza kutafuta maandiko! Sasa kwa ujuzi wako, kama inawezekana na kama utajisikia amani, unaweza kuelekeza mfano wa Nabii mmoja unayemfahamu wewe, hasa walioko Tz na ikiwezekana utoe na sababu za kumuona hivyo!

  Natumaini tukiwa hata na mfano mmoja wa Nabii wa KWELI tunaweza kuupeleka mjadala wetu vizuri!

  2. Katika agano la Kale, kabla ya ujio wa Roho Mtakatifu mioyoni mwa waaminio, palikuwa na mtu mmoja tu aliyekuwa anasafirisha ujumbe kati ya Mungu na watu. Lakini kwa kuwa sasa kuna ROHO MTAKATIFU, Je! Bado ni lazima kuwa kuna mtu MMOJA TU MAALUM WA KUSAFIRISHA UJUMBE KATI YA WATU NA MUNGU? [Zingatia pia kupasuka kwa pazia la Hekaluni siku ya kifo cha Yesu]

  3. Umeandika hivi;

  “Tena NABII wa Huduma ya Unabii huwa ni mmoja tu uwanjani katika kipindi kwa shughuli maalumu kama ilivyo katika program ya Neno”

  Angalia kwa SASA tuna manabii WENGI sana kwa WAKATI MMOJA, tena wengine wakitamba hadharani kuwa yeye peke yake ndiye wa kweli wengine feki na Wengine wanarushiana maneno kwenye Tv na Redio. Je! Ni sahihi kuwepo MANABII wengi hivi, kila kona nabii, nabii….?

  4.Umeandika hivi:

  “Pia kumekuwepo na matatizo mengi sana katika kanisa la Mungu yaliyotokana na huduma ya lile kanisa jingine lenye kuigiza vipawa. Kazi ya manabii wa kanisa hili ni kuwadanganya watu ili kuwaondoa katika katika ibada ya kweli na kuwapeleka upotevuni”

  Ndugu Lwembe, Katika Agano la Kale walikuwepo pia hao “wenye kuigiza vipawa” na walifanya hivyo mchana kweupe. Lakini walipofanya hivyo wale ambao “vipawa ni vyao” WALIUHAKIKISHIA ulimwengu kuwa hao wanaoigiza “si lolote, si chochote”. Tunaona mfano wa hayo kwa Musa katika Kutoka 7:8-13 na wale waganga wa Misri ambao NYOKA wa Musa, aliyetokana na “fimbo” aliwameza nyoka wao feki. Tunawakuta pia Manabii wa BAALI 450 katika 1Wafalme 18:17-40 ambao Eliya aliwaua baada ya BAALI wao kushindwa kushusha moto uchome ile sadaka.

  Katika siku zetu KILA anayesema ni Nabii hupata kipingamizi toka kwa jamii ya Wasio wakristo, Wakristo wenyewe na hata kutoka kwa “Manabii” wengine. Lakini upinzani huo huwa ni wa maneno tu na wala si wa matendo kama walivyofanya mabanii wa kwenye Bible.

  Nijuavyo mimi KAMA KWELI kuna manabii, na wengi waliopo ni “waigiza vipawa” KWA NINI HAITOKEI KUWA NABII JAPO MMOJA WA KWELI “amuumbue” japo mmoja huyo wa Uongo ili kweli ijulikane kuwa kuna Mungu wa Kweli wa nabii fulani wa Kweli???????

  [Sikia hadi sasa tunaimba kuhusu Mungu wa Eliya tu katika nyimbo kama vile:

  “Na ijulikane kwamba yupo, Mungu wa Eliya-a-a,”
  “Na ijulikane kwamba yupo, Mungu wa Eliya”]

  5.Nanukuu:
  “….katika Malaki 4:5-6 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. …”, kwa hiyo huduma hiyo ya huyo nabii ajaye, kanisa lilipaswa kuwa katika kuingojea ili ikija iwaondoe kutoka lindi la matope……..”

  Ndg Lwembe, Watafsiri wa Biblia na ninaamini na wanazuoni WAMELINGANISHA au WANAHUSISHA andiko hilo la Malaki 4:5-6 na Yohana 1:21, Luka 1:17, Marko 9:11-13 na Mathayo 11:14, maandiko yanayozungumzia kuwa Eliya ajaye ni Yohana Mbatizaji. Hebu ona hata maneno ya Yesu mwenyewe:

  Mathayo 11:14 – “Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja”

  Marko 9:12-13 – ‘Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza yote upya; lakini pamoja na haya ameandikwaje mwana wa Adamu kwamba atateswa mengi na kudharauliwa? Lakini nawaambia Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa”.

  Sasa ndugu Lwembe umeandika kuwa kanisa lilipaswa kuwa katika kuingojea huduma hiyo ya nabii Eliya ajaye wakati YESU MWENYEWE ANASEMA ELIA AJAYE NI Yohana Mbatizaji.

  UKWELI ni upi katika Hili? Yesu Kristo alikosea au alidanganya kusema kuwa Nabi Eliya ajaye ni Yohana mbatizaji ambaye TAYARI ALISHAKUJA kabla yake?????

  6. Nanukuu:

  “….yaonesha jinsi ambavyo kanisa la Mungu lilivyotekwa na kupofuliwa macho na sasa hilo dude linalojiwakilisha kama kanisa la Mungu ,ni chombo cha kuwapoteza zaidi wote wenye shauku ya kumjia Mungu na hivyo kuishia katika mikono ya wevi!”

  i). Kama kanisa la Mungu “limetekwa na kupofuliwa macho” ina MAANA KANISA LA MUNGU LA TANZANIA SASA NI KIPOFU na hakuna matumaini TENA?

  ii). Yesu alisema “na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda” Math 16:18. Sasa kama kanisa la Tz limepofuliwa macho HUONI KUWA MILANGO YA KUZIMU TAYARI IMELISHINDA?

  iii).Unaposema “hilo dude linalojiwakilisha kama kanisa la Mungu” una maanisha NINI? Yaani “dude” ni akina nani ili watu wafunguke na kanisa lisipofuliwe macho tena?

  Hayo ndiyo yaliyojitokeza ambayo nimeona niyaulize kwanza ndipo utaendelea na yale maswali mengine. Nakuomba tu uandae muda wako vizuri maana naona mjadala huu unaweza kuendelea kwa muda mrefu!

  Asante.

 68. Ndugu John Paul,

  Asante kwa kunivumilia.

  kuhusu mwongozo, mimi naona suggetion yako ya pili ni bora zaidi maana hiyo ingeleta maana halisi ya kufellowship Neno la Mungu. Mimi au wewe twaweza kukosea, na mara nyingi tunakosea. Lakini Yeye (KRISTO) hakosei, basi tumtegemee Yeye katika kutuongoza zaidi kwani tunamzungumzia YEYE, naye alituahidi kuwa tukutanapo wawili au watatu kwa ajili ya Neno lake, atakuwa pamoja nasi.

  Bwana na atupe ujasiri wake!

 69. Wapendwa wote mnaochangia mada ,

  Inapendeza sana tukiendelea kujibizana ktk utulivu namna hii, maana wengi tunataka kujifunza na kujua ukweli bila kupendelea upande mmoja wowote. Na kama kuna vifungu vya biblia tu’quote’ ili tuweze kujenga misingi ktk maandiko matakatifu. niwashukuru tena kwa utulivu wenu ktk maelezo yenu hapo juu ndugu John na C.K Lwembe.

  Shalom! Shalom.

 70. Ndugu C k Lwembe,

  Nashukuru kwa mchanganuo wako juu ya mada inayoendelea. Ninashukuru pia kwa kuwa umeshaanza kujibu maswali niliyokuuliza. Asante sana mpendwa.

  Lakini NAOMBA MUONGOZO WAKO kwamba katika hayo uliyoandika kuna mambo ya MSINGI SANA ambayo yamejitokeza na ninaona ni vema TUKAKUBALIANA pia ili tuweze kwenda pamoja. Ninachoomba mwongozo ni kuwa NI KIPI kinafaa kati ya haya mawili:

  1. Nikuanche ujibu kwanza maswali yote 9 ndipo niulize maswali mengine, AU

  2. Niulize sasa hivi ili tukitoka hapo kwenye SWALI LA KWANZA tuwe tumetoka kabisa?

  Naomba ushauri wako na ninakuomba pia uwe na subira kwa kuwa naona mada hii ni NYETI kwa kuwa NI HALI HALISI inayokumba KANISA LA SASA kwa hiyo ina mengi sana ya KUJADILIANA kwa faida yetu wote!

  Nasubiri toka kwako!

 71. Ndg John Paul,

  Nimeona ulichokiandika, katika maana ya maelezo na maswali uliyoyauliza, ninakushukuru kwa vyote.

  Kabla sijayaendea hayo uliyotaka kuyajua, kwanza ningependa kuweka sawa jambo moja la msingi ambalo naona limeleta mkanganyiko kidogo katika muendelezo wa michango inayoendelea katika mada hili.

  Katika ujumla wa uchangiaji nilioutoa, ambao naamini ndio uliousoma na kukusababisha uniulize maswali, hata umeniambia kuwa maneno niliyoyaandika ni mengi, bali hujaona kama nimeonesha popote KAZI YA MANABII kwa sasa ni ipi. Ni kweli, sijaonesha wala kuzungumzia jambo hilo, kwani michango yangu hiyo unayoisoma wewe haikuwa ikijibu swali hilo la ‘KAZI YA MANABII KWA SASA NI IPI?’ bali swali la msingi aliloliuliza ndg Orbi mwanzoni katika post ya ‘Nabii Flora’ ambalo aliuliza: JE, NABII NI NANI. Ninanukuu kumbushio ya swali hilo nililolijibu:
  Dec.09, 2011. Wapendwa, Bado naomba kusaidiwa……Je Nabii ni nani hasa Kimaandiko…..naamini maandiko matakatifu yana majibu……Je ni uponyaji? Wingi wa watu? Watu wanaokoka? Ni nini hasa kinamfanya mtu akaitwa Nabii? Hebu nisaidieni kwa Kutumia Maandiko?
  Basi majibu yangu yote yalilenga kujibu jambo hilo. Bali baadaye muulizaji alimodify swali lake kutoka lile la msingi; JE, NABII NI NANI kuja hili jipya la ‘KAZI YA MANABII KWA SASA NI IPI?’ bali katika post tofauti. Kwa hiyo waendesha mtandao yaani SG, wamehamisha ile michango ya awali kutoka post ya Nabii Flora kuja kwenye post hii ya swali jipya kukidhi haja na pia convenience na relevance ya michango kulingana na mada.
  Baada ya kuweka sawa jambo hilo, basi nitajaribu kuyajibu mambo matatu uliyoyaorodhesha pamoja na maswali yake tisa uliyoyaambatanisha kama ulivyonitaka.
  1. KAZI YA MANABII:
  a) Nabii ni mjumbe anayeleta kwa kusanyiko au kanisa Ujumbe kutoka kwa Mungu.
  b) Nabii husimikwa na Mungu mwenyewe. Pia nabii.
  c) Nabii ni kinywa cha Mungu, pia husimama kumuwakilisha Mungu na katika uwakilishi huo iwapo kanisa litaingia katika tatizo lolote lile na likaona ni vema lipate uongozi wa Mungu wa moja kwa moja, basi nabii aliyeko hupewa ujumbe wa haja hiyo naye huiwakilisha kwa Mungu na kuwaletea jibu lake.

  Basi, kwa kifupi, kazi ya nabii ni kuchukua ujumbe kutoka kwa Mungu kuja kwa kanisa na pia ujumbe kutoka kwa kanisa kwenda kwa Mungu. Naye Mungu katika kusisitiza umuhimu wa ofisi hiyo ya Unabii akasema katika Amos 3:7, “Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote, bila kwanza kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.” Kwa hiyo SIRI ya Mungu, kama alivyoifunga hapo juu, hufunuliwa kwa manabii wake kwanza kabla hajaitimiza. Tazama pale Mungu alipotaka kuichoma Sodoma na Gomora, ilimbidi amjulishe nabii wake Ibrahim kwanza.

  Pia Karama ya Unabii, Mungu ameiweka katika makusanyiko madogo madogo tangu Agano la Kale hata Agano Jipya, ila ufafanuzi wake umewekwa wazi zaidi katika Agano Jipya. Kwa hiyo karama hii huwepo katika nchi kulingana na wingi wa makusanyiko hayo madogo madogo yaliyopo. Ukiangalia katika AK katika ulinganishi, utawaona watoto wa manabii wakitoa unabii nk lakini pia, nabii, yule wa Huduma ya Unabii, licha ya uwepo wa manabii hao wa karama, yeye huwepo uwanjani ili kuwa ile tofauti katika viwango vya utendaji. Basi Karama ya Unabii na Huduma ya Unabii vyote hutenda kazi ile ile ya kuleta ujumbe kwa kanisa, Karama ya Unabii kwa kusanyiko dogo na Huduma ya Unabii kwa Taifa/ulimwengu mzima. Tena NABII wa Huduma ya Unabii huwa ni mmoja tu uwanjani katika kipindi kwa shughuli maalumu kama ilivyo katika program ya Neno. Maana Mungu, Neno lake, si kwamba kwamba analinena wakati huo kwa hao manabii, hapana, bali alikwisha linena na limekuwepo hapo kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa likitanukia wakati (stretched out in time). Kwa hiyo nabii anachofanyiwa ni kuinuliwa juu katika anga za kiroho na kulitazama hilo Neno katika utulivu wake lihusulo hicho kipindi na kurudi nalo hapa chini kwa ajili ya kusanyiko.

  Sasa, katika jambo hili la Unabii, tunapolitazama ni vizuri tukalitazama katika chimbuko lake. Unabii huwakilisha mawasiliano kati ya Mungu na wanadamu. Basi tunaporudi kule Mwanzo, kule Edeni, tunaona kuwa Nabii wa kwanza alikuwa ni Mungu mwenyewe. Biblia inasema Mungu aliwatembelea wakati wa jua kupunga kuja kuongea na Adamu (Mwz 3:8). Hata tunamuona tena Mungu akimuonya Kaini. Baada ya hapo tunaona katika kizazi cha Adamu, wakati wa Seth ndipo wanadamu walipoanza kuliitia jina la Bwana (Mwz 4:26), naye Mungu akajipatia manabii kutoka hao akiwaweka kulingana na program yake ya ukombozi hata leo.

  Hata hivyo, katika jinsi hii ambavyo Mungu amekuwa akiliendesha kanisa lake, Ibilisi naye kupitia kizazi cha Kaini, alitengeneza pia kanisa lake ambalo limekuwa likiliigiza kanisa la Mungu katika maana ya Huduma kama ya Unabii na Karama ya Unabii. Katika utendaji, kanisa la Kaini, hujihusisha zaidi na mikakati ya kuingiza ubaridi ndani ya Kanisa la Mungu na hivyo kulifanya vuguvugu. Kwa hiyo kuanzia hapo tunaona makanisa mawili yakizaliwa, moja la Mungu na jingine la Kaini. Yote mawili yakifanya ibada kwa Mungu kama tunavyo waona Kaini na Habili wakiwa katika ibada ya kujipatanisha na Mungu! Basi Mbegu hizi mbili zimekuwa zikikua zote kwa pamoja kutoka Mwanzo. Hakuna jambo jipya duniani, jambo lolote unaloliona leo hii, asili yake ni kitabu cha Mwanzo. Mwanzo ndio kitabu cha Mbegu!

  Tunapofika katika Agano Jipya, tunayaona makanisa haya mawili yakiwa yamekua katika kimo. Kanisa la Mungu wakati wote limekua likiendelea katika program yake tokea huko nyuma, yaani katika A/Kale, Mungu amekuwa akilisogeza mbele kutoka familia moja ya Adam, ikiwa ndilo kanisa hadi kufikia taifa teule la Israeli ambamo tunaona mifumo iliyo imarika ya utawala chini ya uongozi wa Mungu mwenyewe kupitia Huduma ya Unabii na pia Karama ya Unabii. Pia kumekuwepo na matatizo mengi sana katika kanisa la Mungu yaliyotokana na huduma ya lile kanisa jingine lenye kuigiza vipawa. Kazi ya manabii wa kanisa hili ni kuwadanganya watu ili kuwaondoa katika katika ibada ya kweli na kuwapeleka upotevuni.

  Sasa jambo unalopaswa kulielewa vizuri, ni kwamba wao pia ni manabii licha ya huduma yao kuwa ni ya uovu. Bado wanao uwezo na upako wa kulifikia Neno la Mungu kwa kiasi na kulileta katika kusanyiko. Si kwamba eti ni watupu, hapana, Biblia inatufunza kuwa wanao upako, ndio unao wainua hata wakaitwa manabii. Ndio maana kuna maonyo mengi kuhusu hao MANABII WA UONGO katika Biblia. Ukipenda kujihakikishia hilo nenda katika kitabu cha Hesabu umtazame nabii Balaamu na kazi zake. Licha ya kuwa alikuwa ni nabii wa uongo, bali kwa upako, alijua jinsi ya kulifikia lile Neno kwa namna ya kutoa sadaka nk. Yeye ndiye aliyeutoa unabii maarufu kuhusu Israeli: “Ambarikiye atabarikiwa na amlaaniye atalaaniwa”, na pia alitabiri kuzaliwa kwa Kristo. Lakini alikuwa nabii wa uongo! Ndio, asingeweza kuwa wa kweli maana nabii wa kweli Musa, alikuwapo uwanjani akiongozana na kusanyiko la Mungu.
  Umeyaona hayo makanisa mawili? Kanisa la Moab, uzao wa loti (hawana safari yoyote), linaye nabii wake Balaamu, ambaye leo huja na Neno, kesho hushughulika na uchawi na kesho kutwa hufanyia biashara Neno la Mungu! Lakini chini ya vilima kuna kanisa la Mungu, uzao wa Ibrahim, wao wako safarini kuelekea Kaanani nao wanaye nabii wao Musa. Wivu na biashara ya Injili kutoka kanisa la Moab, likawafanyia hila hata maafa yaliyotokana na hasira ya Mungu yakaliangukia kusanyiko la Israeli!!

  Makanisa haya yanaendelea katika A/Jipya, bali huku viwango vimeongezeka. Mungu amepandisha kiwango cha wanaye na Ibilisi naye kapandisha. Katika ujio wa Kristo, Mungu ameuleta katika ukamilifu mfumo wake wa utawala kwa kanisa. Katika mfumo huu sasa, Mungu anakuja kuishi ndani ya watu wake, akiyatawala mawazo yao na vyote. Yaani kwa wanae, sasa preeminence yao ni Kristo! Mfumo huu mpya wa utawala, msingi wake ni manabii, nao mitume ndio wanaomalizia ujenzi wake hata kanisa sasa kujengwa juu ya msingi huo wa MITUME na MANABII, (Efe 2:20). Kanisa la wa mataifa limejengwa juu ya msingi huo. Basi kazi ya ujenzi inayoendelea hufuata Master Plan. Kuhusu hilo mt. Paulo anasema: 1Kor 3:9-10, “… ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu. Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. …” Basi katika plan hiyo ndimo tunaona nafasi ya Karama ya Unabii ikipewa umuhimu wake na kuwekwa ndani ya kanisa pamoja na vipawa vingine. Kuhusu ile Huduma ya Unabii, pia bado ipo kwa kanisa, si kama kusanyiko dogo bali kama mwili wa Kristo. Nayo huduma hii sasa katika mfumo huu mpya, inaonekana kulingana na Master Plan, kutengewa kazi tunapokaribia mwisho wa wakati kama jinsi inavyoonekana katika Malaki 4:5-6 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. …”, kwa hiyo huduma hiyo ya huyo nabii ajaye, kanisa lilipaswa kuwa katika kuingojea ili ikija iwaondoe kutoka lindi la matope lilimotumbukizwa na lile kanisa la Kaini na katika uchafu huo ni vigumu hata kuwatenganisha, yupi wa Kanisa la Mitume na yupi wa kanisa la Kaini. Maana lile kundi la Balaamu na manabii wake wa karama pia wamerukia juu ya Ule Msingi uliojengwa juu ya Mitume na Manabii nao wanajenga kanisa lao hapo juu, tena wanajenga majumba mabovu nakasi yao ni kubwa na kelele nyingi sana!

  Matokeo ya jambo hilo, ndio kama lawama hizi za mafuriko zinazotolewa na kanisa likiwashangaa manabii lukuki waliopo kushindwa kuwataarifu kanisa kuhusu mafuriko yajayo. Kwani athari zake zilikuwa ni kubwa hata nyumba za Bwana nyingine zimeharibika na vifaa vingi vya thamani kuharibiwa mithili ya kuchukuliwa mateka na Wafilisti! Lakini ukweli ni kwamba iwapo kanisa lingekuwa limesimama katika nafasi yake, yaani chini ya Fundisho la Mitume (Mdo 2:42), kwao, baada ya kuusikia utabiri wa mafuriko, kama kanisa, walipaswa waiwasilishe shida hiyo kwa Mungu kupitia manabii wao waliomo ndani ya makusanyiko yao. Kwamba hawakulifanya hilo, yaonesha jinsi ambavyo kanisa la Mungu lilivyotekwa na kupofuliwa macho na sasa hilo dude linalojiwakilisha kama kanisa la Mungu ,ni chombo cha kuwapoteza zaidi wote wenye shauku ya kumjia Mungu na hivyo kuishia katika mikono ya wevi!

  Kwa leo naona niishie hapa, kipengele cha pili nayanayofuatia nitaendelea kukujibu.

  Bwana na atupe subira yake!

 72. Mrs Otaru,

  Asante Mungu na Mungu Akubariki, ila Narudia tu dadangu, haya tunayojadili si maswala ya upuuzi…..wala si kusema hayana faida….au ni mashindano ya hekima…….yenye kuleta ugomvi………..hii ni kutokana na mistari uliyotumia.

  Sipingi kabisa Karama za kinabii….lakini huu mfumuko wa Manabii leo unazua maswala mengi.Kwa kifupi tu kutotaka kujifunza kwa kuuliza maswali magumu kunaweza kuleta maangamizi kwa kanisa! Imani hii tunayoiamini imetufikia kwa watu kuuliza na kujibu maswala Magumu! Hebu fikiria kama Paulo angaliogopa kuwaandikia Wakoritho kuwa amesikia kuna wazinzi ndani ya Kanisa la Mungu kwa sababu tu ya kuwaogopa walio nje watasemaje! Angelisaidia Kanisa?

  Hivyo napenda ufahamu kuwa hatuogopi walio nje watasema nini, wao wanahitaji ukweli wa Injili tu! Je unadhani hata wao hawashangai na utitiri wa Manabii katika imani yetu? Unafikiri hawashangai wanapoona vitu kama kikombe cha mizizi ya BABU? Unafikiri hawashangai wanaposikia kwenye TV na Radioni matangazo ya Manabii na Mitume ambayo hayana tofauti na waganga wakienyeji! Hivyo sisi Waumini Tutakapo jibu maswali kama haya na mengineyo kwa kutumia Biblia hata wao wanaweza kuelewa maana ya UKRISTO WA KWELI NI NINI! Wanaweza kujua Pumba na Makapi ni yapi! Kwa kukaa kimya na kudhani hatuna tatizo ni mbaya zaidi……..Hatujenge wala kuitetea Imani tunabomoa!

  Hivyo nakukaribisha hata wewe kuchangia na kusaidia hasa huweka hii kazi ya Manabii katika wigo wa Maandiko Matakatifu! UBARIKIWE!

 73. Jamani hawa manabii wa Taifa wanashindwa hata kutuambia kuwa kuna janga la mafuriko tujiandae…….? Agabo katika Matendo ya Mitume alilionya Kanisa kuhusu Njaa itakayoshukia Jerusalem? Unabii wao uko kwa lipi hasa? Kwa nini wasikubali kuitwa Wachungaji tukajua moja?

  Mathayo 18:15-17 Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja ama wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.

  Tito 3:9; ‘’Lakini maswali ya upuuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria (Neno la Mungu). Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana’’

  Wakolosai 4:5 enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu’’.

  mimi naona hii mada ingeandikwa hivi,”NAOMBA KUFAHAMISHWA/KUFUNDISHWA KUHUSU HUDUMA YA UNABII/KARAMA YA NABII,AU WANA SG MNAIELEWAJE HUDUMA/KARAMA YA UNABII?”

  Naona kama ingeleta maana nzuri zaidi na isingeleta picha mbaya kwa walio nje ya YESU.

  NIONAVYO MIMI,MBARIKIWE WAPENDWA NA ZAIDI MTOA MTAZAMO NDG.ORBI

 74. Antony,

  Nashukuru,

  Labda nitakujibu kwa kifupi kutokana na muda nilionao…….mtazamo wangu nikiyatazama maandiko kwa upana wake unanipeleka kwamba hatuna huduma ya Manabii Kabisa na badala yake tuna huduma ya unabii ndani ya kanisa ikifanya kazi.Na hii ni Karama ya Roho Mtakatifu……

  Nadhani kama tutapata muda tutaangalia Matendo 11:27-28 Matendo 13:1 Matendo 21: 9 nakuona karama ya unabii kwa njia ya Roho Mtakatifu ikitenda kazi, Na manabii hawa huwawezi kabisa kuwaweka katika kiwango cha utendaji wa Manabii kama Eliya, Elisha nk Watu kama akina Agapo hawakutengeza mwelekeo wa Kanisa………bali ni Paulo na mitume….kinyume kabisa na Manabii wa leo ambao unaona wazi wana nia ya kulipeka kanisa mahali wanapopajua wao!

  Nadhani kama nilivyosema mahali pa kuanzia ni kuangalia Huduma ya Yesu (akizibeba huduma zote zilikokuwepo Agano la Kale)……Kazi ya Roho Mtakatifu……..na halafu la Msingi kabisa ni Neno (Scripture, New Testament Canon) ambalo halikuwepo wakati wa Matendo ya Mitume……..kwani hata mkusanyiko wa Maandiko tuliyonayo leo nikiwa na Maana Agano jipya ulikusanywa baada ya watu aina ya Manabii waliojitokeza wakati huo na kudai wana mafunuo au wao ni sauti ya Mungu kama manabii wanaojitokeza leo na ikabidi Kanisa lipitie wakati mgumu wa kukusanya Maandiko na kuamua hicho ndio kitakua kipimo cha mwisho cha kuisikiliza sauti ya Mungu.

  Kwa hitimisho tu msimamo wangu ni kuwa tuna Karama ya unabii…..na Roho Mtakatifu anaweza kumvuvia yoyote yule katika kusanyiko la mahali kusema chochote kile cha kulijenga Kanisa….nikiwa na na Maana sio mafunuo mapya……Maana hata Manabii katika Matendo ya Mitume hawakuja na mafunuo yoyote yale!

 75. Orbi,

  Nashukuru kwa kutoa ufafanuzi kwa kifupi kuhusu mada hii motomoto, ni mchango mfupi lakini unaeleweka zaidi kuliko niliopost mimi. naomba somo hili lipostiwe kwa kirefu zaidi ili nijifunze. naamini wapo wengi wa mlengo huo watafaidi kama mimi nilivyoona unakitu.

  Ila nomba ufafanuzi zaidi kama kwa sasa hatuna huduma ya manabii kabisa na badala yake tuna karama ya unabii ambayo anayetoa unabii anaweza asiwe na huduma ya unabii bali ni karama ya Roho mtakatifu? ni kama nina elewa hivyo ila kama ndugu Orbi waweza fafanua zaidi hapo ndio kwenye shida kwa watu wengi nikiwemo na mimi.

  Barikiwa sana

 76. Ndg C k Lwembe,

  Nami ni mmoja wa wanaofuatilia mjadala huu. Bado najifunza na ninaendelea kujifunza kwa kadri maoni yanavyoendelea kutolewa hapa. Nafahamu lengo kuu la mada hii ni KUBAINISHA KAZI ZA MANABII kwa sasa kama ziko tofauti ikilinganishwa na wafanyavyo wachungaji, walimu wainjilisti na mitume. Nami naamini katika kujadiliana hili kuna mengi yanaweza kujitokeza lakini natumaini kuwa mtu anayefuatilia mjadala huu hatimaye ataweza kuorodhesha kuwa kumbe kazi za manabii wa siku zetu ni moja, mbili, tatu na kuendelea. Naamini tukifikia hapo majadiliano haya yatakuwa na maana sana.

  Nimesoma maneno yako ambayo kweli umeandika mengi. Lakini katika mengi hayo binafsi sijaona kama umeonyesha popote KAZI YA MANABII kwa sasa ni ipi. Kutokana na maneno uliyoandika yanaonyesha kuwa unaifahamu vizuri huduma ya UNABII kwa siku zetu na hivyo unaweza kusaidia katika kufahamisha msomaji hapa juu ya kazi ya Manabii.

  Ninayokuomba ni haya:

  1.Kama inawezekana, ufafanue KAZI YA MANABII au pengine inaweza kuhitajika kuorodhesha ili mimi na mwingine tuweze kufahamu.

  2. Wakati unamjibu ndugu Orbi ulisema namna moja wapo ya kumtambua “Mtume na Nabii” wa kweli ni kama “Kabatizwa kwa maji mengi” jambo ambalo mahali pengine umeliita “Kubatizwa kwa jina la Yeu Kristo”. Halafu katika maoni yako ya mwisho umemuandikia ndugu Orbi yafuatayo:

  “Nenda ukabatizwe kwa jina la Bwana Yesu Kristo upewe ‘EYE SALVE’ utayaona yote na mengine mengi kwani sasa utakuwa ni MKRISTO, vinginevyo , manna utapewa ili uishi muda wako lakini muda wako wote utakuwa ni wa kuzunguka jangwani!!!”.

  Kama nimekuelewa vizuri maneno hayo YANA MAANA kila mtu “Aliyebatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo huwa ana uwezo wa kuyaona yote na mengine [kwa kuwa akibatizwa anapewa EYE SALVE]. Kama nilivyokuelewa ni sahihi:

  Je, ni sawa kusema kuwa “Kila aliyebatizwa kwa jina lake Bwana Yesu Kristo” tayari ana ROHO YA UNABII NDANI YAKE?

  3. Ninanukuu:

  “Halafu tatizo lako jingine ndugu yangu Orbi, huendi na wakati. Hivi wewe kwa mawazo yako unadhani uchungaji ni jambo la kujivunia katika mafanikio ya kihuduma? Uchungaji ni kazi ya kuajiriwa! Wachungaji wameajiriwa huko Katoliki au Lutheran nk. Kwa wajasiriamali wa Injili, unachomoka na Unabii au Utume au vyote ‘Mtume na Nabii’ hapo ndio watu wanakuelewa. Watu wenyewe kwanza wanataka miujiza. Kama hauna hata kamuujiza kakuwachangamsha kama haya makanisa ya zamani basi wapige hata na muujiza wa majengo makubwa ya kifahari watakuelewa!”

  Ndugu Lwembe mimi Nimesoma maneno hayo niliyonukuu nikapatwa na maswali mengi sana. Nitauliza kwa uchache na nitaomba unijibu kwa mtiririko niliyouliza ili niweze kufuatilia vizuri:

  1.Kutokana na “wakati” uliomuambia ndugu Orbi haendi nao Je, unamaanisha “UCHUNGAJI” ni huduma ILIYOPITWA NA WAKATI?

  2. Ni “mafanikio” gani ya “KIHUDUMA” ambayo atayapata mtu akiwa “NABII/MTUME” tofauti na anayoyapata MCHUNGAJI?

  3.Kwa kuwa uchungaji ni kazi ya kuajiriwa, Je, unamaanisha UNABII/UTUME ni kazi ya KUJIAJIRI?

  4. Je, “WAJASIRIAMALI WA INJILI” ni watu gani?

  5. Mtu “akichomoka” na Unabii au Utume au vyote kwa pamoja “Mtume na Nabii”Je, ANACHOMOKA navyo kutoka WAPI?

  6. Umeandika kuwa mtu akichomoka na Utume na/au Unabii ndipo WATU WAYAMUELEWA. Swali ni kuwa WATAMUELEWA KUWA YEYE NI NANI au watamuelewa vipi? Naomba ufafanue hapo ndugu yangu!

  7. Umeandika kuwa kwa sasa watu “WANATAKA MIUJIZA”. Je, unamaanisha kuwa HIYO ndiyo sababu MANABII/MITUME waliopo hawahubiri sana habari za KUOKOKA na UTAKATIFU bali “wanatangaza” tu habari ya mafanikio ya kimwili?

  8. Umeandika hivi “kamuujiza kakuwachangamsha”. Je, unamaanisha KAZI YA MIUJIZA ni KUCHANGAMSHA watu?

  9. Una ushauri gani kwa watumishi: WAWAPE WATU KILE MUNGU ANACHOTAKA au WAWAPE WANACHOKITAKA WATU WENYEWE?

  Naomba niishie hapa kwa sasa ili nizubiri majibu ya maswali hayo ambayo naamini yatasaidia katika kujifunza ‘KAZI YA MITUME/MANABII kwa siku zetu!

 77. Antony,

  Wakati natafuta muda wa kuingalia Huduma ya Yesu kama Nabii na pia zaidi ya Nabii, ningetaka sana wale wanaotetea Manabii wa leo hasa hapa Tanzania watuambie tu hata kwa kifupi tu ujumbe halisi wa Manabii hawa! Kwanza wenyewe wanapishana kwa ujumbe wao! Hilo linatosha kusema Si Mungu anayewapa ujumbe huo! Na hata kama hawa Manabii na mitume wanatoka kwa Mungu, kwa nini wajazane Dar tu! Au DAR ndio inahitaji Manabii?

  Hebu ziangalie kazi za Manabii na mitume wa leo Tanzania , wengine wanafungua Benki, utafikiri tatizo la waumini wa Tanzania ni mahali pa kuweka pesa zao! Wengine hata kwa mafundisho tu…….Wokovu si Kitu kitu Power! Wokovu ni mchakato…..ukiokoka hufanyiki Mwana wa Mungu……..bali mpaka uingie madarasa katika makanisa yao ili wakufanye mwana wa Mungu! Na hata wengine wamewaambia waumini wao waache kutumia Biblia yenye rangi nyeusi……maana inamaanisha giza giza…..na laana! Utafikiri wanajua rangi ya Biblia ya kwanza ilikuwaje!

  Hebu ndugu zetu wanaotetea hawa Manabii na Mitume wa Leo ujumbe wao ni upi hasa! Umelifanyia nini kanisa la leo! Tanzania ya Leo huoni huwezi kusema Wakristo ni chumvi au Nuru………rushwa…..ubakaji……ufisadi…..kuchinja maalbino……..maasi! Mbona hatuoni taifa likigeuka kwa ujumbe kutoka katika vinywa vya manabii?

  Jamii ya Tanzania ilichoweza kujifunza kutoka kwa Manabii na mitume wa Leo ni kusema “USHINDWE ULEGEE”

  Hebu tofautisha leo na Miaka ya themanini……..ambako hawakuwepo Manabii na Mitume Tanzania! Tanzania ilikuwa inapita kipindi kigumu mno! Wokuvu ulikuwa unajulikana ni nini kwa kila mtu! Leo je kwenye lindi la Utitiri wa mitume! Tumekuwa vituko! Na miujiza ya kukufua misukule tunaonekana kama tunacheza maziombwe!

  Nitaendelea baadaye!

 78. Antony,

  Nakushukuru kwa Mchango wako, kinachowasumbua wengi na hata kuibuka kwa hawa Manabii wa leo ni kutojua kabisa Maandiko, nikiwa na maana kujua Mungu alifanya nini katika AGANO LA KALE na Mungu anafanya ni nini katika AGANO JIPYA! Usipoweka maandiko katika hali inayotakiwa (right perspective) Biblia inaweza kuwa kitabu cha ajabu mno wala kisicho na utaratibu wowote wa kumuelewa Mungu.Kila mtu anaweza kutumbukia na kuja na lake!

  Nashangaa kwa nini hawajitokezi MAKUHANI! Mbona wako katika Biblia? Kwa kifupi kutoielewa KAZI YA KRISTO AU UJIO WAKE KIKAMILIFU NDIO KUNAZAA MAFUNDISHO YASIYO SAHIHI YA MANABII.

  Antony, Ukiangalia Biblia unaona wazi utendaji wa Mungu juu ya watu wake Israel uligawanyika katika Huduma tatu kuu.

  1. Huduma ya kwa kutumia Manabii; Mfano Nathani; 2 Samweli 7:2

  2. Huduma kwa kutumia Makuhani: Mfano Abiathari 1 Samweli 30: 7

  3. Huduma kwa kutumia Mfalme: Mfano Mfalme Daudi 2 Samweli 5: 3

  Na kama utasoma kwa makini Biblia huduma hizi zilikuwa zina utofauti……….

  – Manabii: Walizungumza Neno litokalo kwa Mungu kwa watu wake Israel

  – Makuhani: Walitoa zaka zilizotakiwa, walifanya maombi, na kutoa sifa kwa Mungu kwa niaba ya watu wake

  – Na mfalme alitawala Israel akiwa mwakilishi wa Mungu duniani

  Kwa kifupi kazi hizi zote (Huduma hizi zote) zilikuwa zikifanyika kama Kivuli tu cha Huduma ya Mungu itayodhihirishwa na Kristo! ( Namshauri yoyote anayetaka kujifunza asome kitabu cha WAEBRANIA ambacho kinaliweka Agano la Kale na Huduma hizi za utendaji wa Mungu kutoka AGANO LA KALE kuja AGANO JIPYA MAHALI PAKE!

  Hivyo kama nikipata muda……nitaanza kutoa maelezo ya Huduma ya Yesu kama NABII……..kama KUHANI……….kama Mfalme.

  Ukiangalia kazi ya Bwana wetu Yesu Kristo katika Biblia akiwa ni NABII…..KUHANI….MFALME utabakia kushangaa kabisa na huu uyoga wa manabii…..! Kwani hawana jipya la kufunua nje ya Nabii Mkuu Kristo….! Hawana kazi yoyote ya kutuendea kwa Mungu kama Makuhani………!

  Ndio maana Yesu alifundisha mno kuhusu Manabii wa Uongo! Maana hiki ndio kipindi chao hasa! Hiki si pindi cha Manabii ni upofu tu wa watu wa Mungu wa kutokaa chini na kujifunza maandiko!

  UBARIKIWE

 79. Mrs Otaru,

  Pole sana kwa uchungu uliokupata….Sikuandika kabisa kwa madhumuni hayo.

  Lakini Mrs Otaru si kila mtu anayejiita Nabii ni ndugu yangu katika Kristo kama unavyosema wewe! Yesu ametuonya kwa hilo!Je ni kila anayejiita MKRISTO ni ndugu yako? Naamini si hivyo, maana wako Makristo wa uongo wapo! Hivyo ndivo Biblia isemavyo! Na kwa upande wangu sijaigeuza Blog hii “Kuwa genge la usengenyaji na kuzodoana” Naandika wazi wazi na kinachonisukuma kufanya hivyo ni wasiwasi wangu na huu mfumuko wa Manabii ambao kila kukicha wanazidi kuibuka katika anga la Tanzania! Je kufanya hivyo ni dhambi? Maandiko yananiruhusu kutozikubali kila “roho” Sio kuzodoa Nabii yoyote!

  Halafu napenda sana kukutahadharishia na huu usemi huu ambao umeenea katika kundi la watu wa Mungu “USIMNENEE VIBAYA MPAKA MAFUTA WA BWANA” Hivi mpaka mafuta wa Bwana ni nani hasa? Huu ni mstari wa Agano la kale, Je katika Agano jipya ni nani Mpaka Mafuta wa Bwana? Hebu jibu swali hilo kwa kutumia Maandiko tafadhali.

  Na kwa mantiki hiyo ya kwako Je kila anayejiita Nabii au Mtume ni mpaka mafuta wa Bwana? Au kila anakuja na miujiza na Lugha za kiroho ni mpaka Mafuta wa Bwana! Mrs Otaru Biblia haisemi hivyo! Na imetupa uhuru wa kuzichunguza kila roho na fundisho kwa kipimo cha Maandiko! Wala si kwa mafunuo!

  Jambo la mwisho ambalo Nakusihi Mrs Otaru usiogope mtu! Mwogope Mungu na Neno lake! Hapo ndipo mahali Imara! Waumini wa leo wengi wamekumbwa na kuwa na hofu na majina ya watumishi , mitume, manabii kuliko Mungu anavyozungumza katika Neno lake!

  Naomba Msamaha tena kama hili nalo litakukwaza.

  UBARIKIWE

 80. Shalom SG,
  Kutokana na ukali wa mada yetu hii imenifanya nipite hapa na pale na kupata yafuatayo ambayo nime ‘’edit’’ kwa kadili nilivyoelewa naomba tuendelee kujifunza na tuweza kuchallengi ukweli huu, yapo mengi ninaendelea kuedit nitapostpia
  MANABII
  KTK AGANO LA KALE, Kazi yao kubwa haikuwa kutabiri yatakayotokea, bali kuwa madaraja kati ya Mungu na watu wake, wakiwafahamisha yeye anawaza na kutaka nini. “Nabii” ni hasa mtu “anayesema kwa niaba” ya Mungu. Si lazima aandike kitu
  Manabii katika Agano la Kale na Agano Jipya

  Katika Agano la Kale huduma ya Nabii ilikuwa imelengwa zaidi kwa taifa la Israeli. Wakati mwingine walitoa tu Neno la Bwana kwa mataifa, na baadaye kwa wale tu waliokuwa na mahusiano na Wayahudi. Kazi na kusudi / malengo ya Nabii wa Agano Jipya hutofautiana kwa mitazamo mingi na ile ya Agano la Kale.

  Tunapolinganisha huduma mbili tutatambua kwamba muonaji / Nabii wa wakati wa Agano la kale aliposimama mbele ya Wafalme na Taifa akiwaita
  wamrudie Mungu, Agano Jipya linaleta /onyesha picha ya tofauti. Hapa nabii analiambia kanisa lakini hana tena huduma kwa taifa na watawala wake. Kwa hiyo, huduma ya kinabii ya Agano Jipya inajidhihirisha yenyewe hasa ndani ya mipaka ya kanisa. Nabii hata hivyo anaweza kutumika kuhudumu kwenye mwili wa Kristo katika kanisa la mahali pamoja, kimkoa, kitaifa na hata ngazi ya kimataifa. Huduma ya kinabii ya kweli ya kitaifa na hasa ya kimataifa daima itakwenda sambamba na ufunuo wa Mungu kwa wengine ambao wana huduma ile ile.

  Tunapaswa kuelewa wazi kwamba katika kipindi cha kanisa, MUNGU
  HADHIHIRISHI TENA MIPANGO YAKE KWA MTU MMOJA TU, kama ilivyokuwa katika Agano la kale, bali katika mwili wake kwa ujumla. Huduma ya manabii wa Agano la kale inajumuisha utabiri, ambayo iliikuwa sahihi zaidi, kwa matukio yajHuduma ya manabii wa Agano la kale inajumuisha utabiri, ambayo iliikuwa sahihi zaidi, kwa matukio yajayo kuhusu Israeli. Kwa nyongeza, nabii zilitolewa kwa undani zaidi/kinaganaga kuhusu kuzaliwa, maisha, mateso na kazi ya Masihi. Katika Agano Jipya tabiri za mambo yajayo siyo sehemu muhimu ya huduma ya nabii. Wakati tabiri za kweli zitakapotabiriwa daima zitakuwa ndani ya mipaka ya maandiko, zikielezea na kumulika kweli ambazo tayari zilikuwepo.

  Kwa hiyo haziwezi kufunua kweli mpya zinazohusu mafundisho na mpango wa Mungu uliokwisha kuwepo kwa ajili ya vizazi. Hata tabiri zilikusudiwa kwa mmoja mmoja kulingana na Agano jipya, zilitumika tu kama kuthibitisha au jibu la moja kwa moja la maombi ya mtu binafsi, kama tutakavyoona baadaye.ayo kuhusu Israeli.

  Sifa za huduma ya kinabii

  Nabii wa Agano Jipya ni mtu ambaye ana uwezo wa Ki-Mungu kutafsiri maandiko yanayohusiana na hali ya kanisa iliyopo. Anaweza akatambua kupungua kiroho, uzushi, na uhitaji wa kutia moyo kama ule uliofichika na dhambi iliyowazi katika mwili wa Kristo / Kanisa. Mungu anafunua hali za kiroho za kanisa kama zile za kila mtu, nabii anaweza kuona zaidi ya uwezo wa kawaida wa kuona. Watu wengine huchanganya kipawa cha unabii na huduma ya nabii. Kipawa cha nabii, kimeorodheshwa katika 1 Wakorintho 12, ni sehemu ya huduma ya kinabii, kama neno la maarifa na vingine. Hivyo, si kila mtu ambaye anaweza kutoa unabii au kupokea neno la maarifa ni lazima
  afikiriwe kuwa nabii moja kwa moja. Tunahitaji kukumbuka utofauti kati ya huduma za kiroho na vipawa vya madhihirisho, kama ilivyoelezwa mapema. Kipawa cha unabii au neno la maarifa halimwezeshi mtu kuwa nabii. Kwa kawaida nabii atavitendea kazi vipawa hivi, lakini vitakuwa sehemu kubwa ya huduma. Tunapaswa kuelewa kuwa huduma ya nabii hutegemea wito ambao umekwisha tolewa kwa “wengine” (Waefeso 4:11). Paulo anasisitiza ukweli huu wakati anapotoa swali katika 1 Wakorintho 12:29: “Je wote ni Mitume? Wengine wamepokea tu wito wa hizi huduma. Watu wengi hawaelewi wakati Paulo huyo huyo anawatia moyo waamini wote kutoa unabii (1 Wakorintho 14:1). Kwa kufanya hivyo hamtii moyo kila mtu kuwa nabii, ila badala yake kutafuta kipawa cha kuhutubu. Ni lazima isisitizwe kwamba si kila mtu anayetoa unabii ni nabii. Manabii wa Agano Jipya, pamoja na mitume waliweka msingi wa imani yetu ya Kikristo na mafundisho (Waefeso 2:20), haki ambayo manabii wa leo hawana, zaidi ya kazi hii maalumu, huduma ya kinabii ya leo haijabadilika sana katika tabia / sifa na kazi zake.

 81. Waebrania 1:1 Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, lakini katika siku hizi za mwisho amesema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, ambaye kwa Yeye aliuumba ulimwengu.

  nilikuwa naelewa hivi zamani Roho wa Bwana aliingia kwa mtu mmoja na mtu huyo alipewa siri za Bwana na Mungu alizungumza naye mtu huyo siri zake ambazo alitaka nabii huyo awasilishe kwa watu wake”.kama waebrania1:1 INAVYOELEZA

  lakini kwa sasa naelewa hivi, mtu yeyote anaweza kutoa unabii kwani nguvu na uweza wa roho wa Mungu ni kwa yeyote aliyeokoka. hivyo naweza toa unabii leo lakini nisiwe nabii wa kujitangaza au kutangazwa maana huduma hii ipo kwa kila mmoja wetu

  haya kama ni mawazo yangu tu lakini naendelea kujifunza ktk mjadiliano motomoto yanayoendelea. ila kama kuna mtu anajua atuelezee unabii na mitume ilivyokuwa kataa agano jipya ukilinganisha na agano la kale.

  Mubarikiwe
  Anthony

 82. Ndugu yangu Orbi,
  Yaonekana tunafanya mhadhara wa dini ambapo mara nyingi wale wazungumzaji wanakuwa wako katika automation hivyo hata mdundo unapobadilika kwao si rahisi kugundua, basi wao huendelea na kupoteza maana nzima ya jambo! Waberoya hawakuwa wapagani, walikuwa nayo Torati. Humo ndimo walimo yakagua maelezo ya mt. Paulo yamhusuyo Kristo ili kujiridhisha na wakaridhika!

  Unisamehe sana kwa kukuita wewe MMATAIFA, maana hata wewe mwenyewe unajua kuwa tumekutana kwenye mtandao tu nikiamini kuwa nawe ni mswahili kama mimi, kwa hiyo isingelikuwa rahisi kwangu kukutambua kuwa wewe ni MYAHUDI au MSAMARIA!
  Hata hili jambo ambalo nilitaka unifafanulie naona halina haja tena kwa vile wewe si mmataifa, lakini kwa faida ya wasomaji wengine nitaliweka hapa ili akiwepo msomaji ambaye ni mmataifa basi nukuu hii uliyonipa wewe iweze kumhakikishia zaidi katika kile nilichokuambia wewe ukakikataa halafu ukakinukuu tena kunifunza mimi kile kile nilichokueleza; ndio maana ninaona unakuwa mhadhara, nanukuu kisehemu : “Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo kwa ajili yenu ninyi mataifa. …” (Efe 3:1-12). Kama nilivyosema katika maelezo ya nyuma kuwa Mungu hakurupuki na watumishi wake. Mara zote anakuwa specific katika jambo analowaitia, naye huenda nao katika hilo hata kulitimiza. Basi katika nukuu hiyo kwa Waefeso Paulo anadhihirisha UTUME wake kwa MATAIFA, Mdo 9:15 “Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, …” Hiyo ndiyo kazi aliyoitiwa mtume Paulo. Dhamira ya maelezo yangu katika kukuelekeza kuwa ukae chini ya Paulo ilikuwa kwa kiasi kikubwa kukupeleka kwa mwalimu aliyekabidhiwa rasmi kukufunza maadili na mwenendo katika Kristo. Pia hakuna mtume aliye mkuu kuliko wengine maana hakuna aliye na chake katika Injili bali vyote ni Kristo. Japokuwa kuna mgawanyo wa kazi kama tunavyoona hapo Bwana alipoongea na Anania na hata kwa kauli za Paulo zinasisitiza hilo. Hebu itazame hii kauli nzito anayoitoa mtume Paulo: “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawasawa na Injili yangu katika Kristo Yesu” Rum 2:16. Utake, usitake mambo ndivyo yatakavyokuwa siku hiyo! Ukiwa mtiifu kwa Mungu itakusaidia sana kuyajua mambo ya Ufalme wake, naye hukupa Roho wake akuongoze katika kweli yote –Mwanzo hadi Ufunuo.

  Naona unaliogopa sana neno hili la ‘DNA’, hii ni maendeleo ya kisayansi tu leo katika kuichunguza asili, lengo haikuwa kukutisha bali kukupa jambo la msingi na jepesi katika kujua hali ya yeyeto yule anayedai kuwa yeye ni mkristo. Kipimo hicho ndicho alichokitumia mtume Paulo katika Mdo 19:3-5 “… Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani?…” Kutokana na maelezo yako mengi ambayo nayaona kama sahani ya santuri iliyokwama, hivyo kujirudia rudia, nahisi sehemu uliyokwamia itakuwa hii ya ukaguzi kupitia UBATIZO kama mitume walivyofundisha. Inaonekana kama ubatizo wenyewe huujui sawasawa au si lazima sana kwa ‘MTU ALIYEMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE’! Nimekutana na watu wengi sana waliojiaminisha katika uongo wa kinafiki wa jinsi hii, wakijiaminisha katika jambo wasilolijua. Wengine wamekaririshwa kifungu cha Rum 10:9 “Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.” Basi ukikikariri kifungu hiki na kukirudia (mimic) baada ya nabii wako au askofu mkuu au mwinjilisti au mchungaji, yeye hukutangazia kuwa umeokoka! Jamani, huyo askofu wako ndiye anayesimika hao wanawake kuwa wachungaji halafu eti leo kakukaririsha kifungu cha Biblia halafu kakudanganya kuwa umeokoka, eti nawe umempokea Yesu kuwa ni Bwana kwa kukikariri kifungu hicho! Yesu ni NENO, (Yoh 1:1). Hilo wanalokufundisha mitume ndiye Yesu Mwenyewe! Kama amesema simpi ruhusa mwanamke, wewe ukimpa ndio umemkataa huyo Yesu unaye jidanganya kuwa umempokea. Pia kama umeukataa ubatizo kama ulivyotimizwa na kuelekezwa na mitume (Mdo 2:38 nk) hutaweza kuelewa mambo makuu ya Mungu. Kwa kifupi wewe si mkristo katika maana halisi ya ukristo.

  Unasema hakuna SIRI ya MUNGU leo hii kwenu nyie ‘MLIYEMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WENU’, sijui hili Andiko la Ufu. 10:7 utaliweka wapi? “Isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.” Iwapo nimeiamini kauli yako wewe ndugu Orbi, kuwa hakuna SIRI tena; basi hebu nieleze ni lini huyo malaika wa saba alipiga hiyo baragumu na ilkuwa ni nini???
  Hivyo vifungu vya Injili mnavyokaririshwa na kujivika wokovu, vingine Mungu, kwa rehema zake aliwawekea wenzetu waliopita katika mateso na vifo kwa ajili ya kumkiri Kristo,‘Dark Ages’, hawakuwa na uhuru na nafasi tuliyonayo mimi na wewe. Kwa wenzetu shida ilikuwa kubwa sana. Unagongewa mlango alfajiri, ukifungua unakutana na askari wa Kirumi, anakuuliza, Unaitwa Lwembe? Unajibu , Ndio. Tumepata habari kuwa jana ulikuwa na yule mwinjilisti Orbi anayepoteza watu kiimani, je, ni kweli kuwa nawe umekubali kuwa mkristo? Unakaa kimya kidogo halafu kile kifungu cha Warumi 10:9 kinapita katika mawazo yako, ni kitamu kuliko asali! Kwenye zile sekunde ulizokuwa kimya, yule askari anakubembeleza, Ukiikana hiyo imani sisi tunaondoka, vingenevyo wewe mwenyewe unafahamu Kaisari amri yake, tutakupeleka kwa wale simba wenye njaa!!! Ndio, … nilimpokea Yesu jana, Yesu kwangu sasa ni Bwana na Mwokozi wangu, nipelekeni kwa hao simba!!! Sasa, leo ni hilo Neno. Nalo linakwambia uende ukabatizwe kwa jina lake Bwana Yesu Kristo upate ONDOLEO LA DHAMBI!! Utamsogeleaje Mungu na dhambi zote hizo ulizozibeba tangia una umri wa miaka 13? Orbi, hebu tafakari hili; ni nguvu gani inayowazuia watu wasibatizwe kama mitume walivyofundisha? Hiyo ndiyo nguvu ya mtawala wa dunia, amesimama mlangoni kuzuia watu wasiingie.
  Nimeuona wito wako kwa wana Strictly Gospel. Unawatisha bure tu! Hiyo nukuu yangu kuhusu watu kupenda miujiza uliyoninukuu na kujaribu kwatishia nayo wana SG unapowauliza, “…Kwa hiyo ukubwa wa jengo unaweza kufanya watu wakaielewa Injili! Hivi anayefanya miujiza ni mwanadamu au Mungu?”, unashangaza sana hapo unapoyachukua tena Maandiko ku confirm usahihi wa jambo hilo hilo unalolipinga na kulibeza! Angalia conclusion yako kuhusu hilo: “Kupenda miujiza na Ishara kama ilivyosema Biblia ndio kutakua kiini cha kupotea kwa wengi hasa waumini katika siku hizi za mwisho……na baadhi ya watu hasa waumini wa leo kutendeka kwa “miujiza” wingi wa watu na majengo makubwa kama anavyosema “Nabii Lwembe” ndio kimekuwa kipimo au kigezo cha kuwa Bwana anatembea katika yetu!” Baada ya hapo nimeona tena ukiendelea kunukuu Maandiko kuhusu UPOTOFU utakaoinuka kutoka ndani ya kanisa. Je nilipokueleza kuwa kuna makanisa mawili pacha, moja la Kristo ambalo linadumu katika Fundisho la mitume Mdo.2:41- 42 “…Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume…”; fungu la 47 “… Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa”. Na kanisa jingine nikakuambia linaigiza hilo la Kristo isipokuwa wao wanadumu katika mafundisho mengine yaliyochakachuliwa kama huko kusimika wanawake kuwa wachungaji, ubatizo batili nk Hukunielewa? Basi nukuu ya Maandiko uliyoitumia, Mdo 20:30, ndiyo inayozungumzia hilo nililokuambia la makanisa pacha!!!
  Haya mambo ya manabii ndugu yangu Orbi, unayotaka kuyajua hutaweza kuyapambanua kwa kutumia akili zako. Shetani ana akili nyingi sana na uzoefu mkubwa sana wa udanganyifu. Amekuwepo hapa kwa zaidi ya miaka elfu sita, wewe humuwezi! Ni Kristo tu anayemuweza. Naye Kristo hawajibiki kwa wanaowabeza mitume wake. Nenda ukabatizwe kwa jina la Bwana Yesu Kristo upewe ‘EYE SALVE’ utayaona yote na mengine mengi kwani sasa utakuwa ni MKRISTO, vinginevyo , manna utapewa ili uishi muda wako lakini muda wako wote utakuwa ni wa kuzunguka jangwani!!!
  Bwana na atuondelee moyo wa jiwe!

 83. Wana Strictly Gospel

  Baada ya kurudia rudia Maandiko ya huyu ndugu Lwembe, nimeona ni wazi kuwaonya waumini na “roho” hizi zidanganyavyo zilizozagaa hivi leo………nashauri kila mtu asome kwa uangalifu post za huyu ya ndugu Lwembe……..kwa mtazamo wangu anawakilisha kabisa “roho” zilizozagaa hivi leo zilizobeba upotovu. “ROHO” hizi za ukengeufu hutumia Biblia! Hutumia Lugha za Kiroho! Hutumia Miujiza! Najua wengi watakuja juu na kusema nahukumu….Lakini hebu angalieni nukuu hii….na kuiweka katika wigo wa Maandiko! Je Miujiza katika Biblia ilifanyika kwa maana hii? Someni nukuu hii ya Bwana Lwembe;

  “WATU WENYEWE KWANZA WANATAKA MIUJIZA…….KAMA HAUNA HATA KAMUUJIZA KAKUWACHANGAMSHA …..WAPIGE BASI HATA NA MUUJIZA WA MAJENGO MAKUBWA YA KIFAHARI WATAKUELEWA”

  Kwa hiyo miujiza iko kuwachangamsha watu! Sio kuwaleta kwa Kristo! Hii kweli ni Injili mpya! Huioni kabisa katika Biblia! Na kama watu hawaelewi “injili hii ngeni” Inabidi wapigwe na majengo ya kifahari….ndio watakuelewa! Kwa hiyo ukubwa wa jengo unaweza kufanya watu wakaielewa Injili!Hivi anayefanya miujiza ni mwanadamu au Mungu?

  Hebu angalia Biblia inasema nini…..

  “Yesu akasema msipoona Ishara na maajabu hamtaamini kabisa?” (Jn 4:48)

  Kupenda miujiza na Ishara kama ilivyosema Biblia ndio kutakua kiini cha kupotea kwa wengi hasa waumini katika siku hizi za mwisho……na baadhi ya watu hasa waumini wa leo kutendeka kwa “miujiza” wingi wa watu na majengo makubwa kama anavyosema “Nabii Lwembe” ndio kimekuwa kipimo au kigezo cha kuwa Bwana anatembea katika yetu!

  Hebu tutafakari Maandiko haya;

  “Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi. TEN KATIKA NINYI WENYEWE watainuka watu WAKISEMA MAPOTOVU wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao” (Matendo 20:30)

  Biblia iko wazi, hawa ni watu wanaoinuka ndani ya waumini! Paulo hazungumzii wanafunzi nje ya kanisa! Hawa watu wana “uwezo” wa KUWAVUTA watu! Kwa kuchanganya Maandiko! “Kutengeneza” miujiza, iwe inaletwa na ile “roho” ya uasi au kwa kuja na vitu vinavyoonekana kama majengo makubwa, magari ya kifahari nk! NK

  Na jambo la kusikitisha ukitaka kusimama na kupinga na roho hizi chafu utasikia watu wakiwatetea kwa kusema “Mbona Injili inahubiriwa” “Mbona watu wanafunguliwa” “Mbona mtumishi/mtume/nabii amebarikiwa” Wapendwa Hivyo ni vigezo duni sana vya kuiangalia Kazi ya Mungu! Kumbukeni ni Paulo aliyesema “Lakini Injili Inahubiriwa” Lakini ndiye aliyeonya kwa nguvu mafundisho potofu katika Nyaraka zake karibu zote!

  Wapendwa hebu kumbukeni kwamba, Paulo alipambana na Mafundisho potofu……Nyaraka ambazo ziliandikwa na watu na kusema za Paulo! Na Nyaraka za Paulo kama Maandiko yanavyoonyesha nyingi likuwa dhidi ya “roho” zenye mfano wa Malaika wa Nuru zenye Lengo la Kuwapoteza Waumini!

  Sikatai na sipingi Roho ya Kinabii inavyoweza kutenda kazi leo! Lakini tuwe na tahadhari na tuwe jasiri kuzipinga….kuzikemea na kuzifichua……. Miujiza, lugha za kiroho na mafunuo visiwe ni vigezo vya kupima kazi ya Bwana……huo ni Uchanga Kiroho.

  Mnaoweza kumsaidia “Nabii” Lwembe na mafunuo yake mnaweza kuendelea!

 84. Ndugu yangu Lwembe,

  Nimeyasoma maandishi yako, naamini na wengi katika Blog hii wameyasoma, nadhani unasahau kabisa kuwa kwa maandishi tu unamtambua mtu aliyeandika ni wa namna gani, au ana “roho” wa aina gani inayomsukuma kuandika, na alikuwa katika hali gani, kwa hilo nitaawachia wanablog waamue wenyewe, kwani maandiko yako yanazungumza kwa sauti kubwa mno kuonyesha dhahiri wewe ni mtu wa namna gani, aina ya ukristo wako na ufahamu wako wa Neno la Mungu.

  Umeandika kurasa karibia nne, na badala ya kuja na hoja za Maandiko kutetea hoja, au maswali niliyokuuliza wewe umekuja na mashambulizi binafsi dhidi yangu (Personal attack) Naamini kama hii ndio ya “Roho ya Manabii” Inatenda kazi ndani yako, basi nadhani itakimbiza wengi na kuzidi kuitilia mashaka huduma hii………HEBU ITETEE HUDUMA HII KWA MAANDIKO BAYANA!

  Anyway siwezi kuzibu mashambulizi yako yote ya kurasa nne leo, lakini nitakuwa nikijibu hoja zako taratibu kila nipatapo muda, naamini hii itasaidia Wakristo wengi kutambua Upotofu uliyojengwa katika huduma hizi nyingi za Kinabii, ambazo kwa kifupi ni potofu na zimejengwa nje kabisa katika ufunuo wa Neno la Mungu (Extra Biblical Revelation)
  Hebu tuanze kwa kuiangalia nukuu yako hii;

  “Wewe Orbi ni mmataifa, kaa chini ya Injili ya mtume Paulo ndio utayajua mambo ya Mungu kwa kina. Usijifanye unamjua sana Yesu kuliko waliokuletea habari zake.”

  Ningependa kukuuliza Ndugu yangu Lwembe (japo wewe umeisha nihukumu mimi ni mmataifa! Sijui na hili umelipata kwa ufunuo wa kinabii!) Hivi kuyajua mafundisho ya Mungu kwa kina inatubidi tukae katika Injili ya Mtume Paulo tu? Maana Paulo hakufundisha hivyo! Au ndio mafunuo ya Kinabii yanasema hivyo? Au Ni wapi Maandiko yanasema hivyo? Sasa naogopa kabisa hata kuja na aya kutoka katika Biblia….maana kila nachokuletea wewe hukitaki!

  Ni Andiko gani hasa liko juu ya jingine? Maandiko ya Paulo yana uvuvio zaidi na Maandishi ya Injili NNE zenye matamko ya Yesu Mwenyewe? Nadhani umesahau kabisa kanuni ya Msingi kuwa Imani hii imejengwa juu ya Yesu Kristo! Na si kingine kabisa!
  Utasemaje Nukuu hii kutoka kwa Paulo Mwenyewe;

  “ KILA ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU LAFAA KWA MAANDIKO “ 1 Tim 3:14

  Sasa ni Andiko lipi katika Biblia linaloweza kutufanya tumfahamu Mungu kwa kina? Je ni Maandiko ya Paulo? Kama unavyosema wewe au Je ni Maandiko ya Mathew, Luke, Mark, na John? Au Petro? Yakobo?

  Kama wewe kweli ni mwanafunzi au Mfuasi wa Yesu ungalitambua wazi KUWA MAANDIKO YOTE NDANI YA BIBLIA YAMEJENGWA TUMFAHAMU YESU! TUITAMBUE KAZI YAKE YA MSALABANI NA WOKUVU WAKE MKUU! HAKUNA KINGINE ZAIDI YA HICHO! HAKUNA CHA “DNA” WALA “MYSTRY” WALA KITU CHOCHOTE KILICHOFICHIKA KWA MTU ALYEMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KAMA WEWE NA MANABII WA LEO WANAOJITOKEZA MITAANI WANAVYOTAKA TUAMINI!

  Hebu soma nukuu hii Yesu anasema nini Juu ya Maandiko; ( Ingawa naona umeanza kuyakataa Maneno ya Yesu)

  “ AKAANZA KUTOKA MUSA NA MANABII WOTE AKAWAELEZA KATIKA MAANDIKO YOTE YALIYOMHUSU YEYE MWENYEWE” (Luka 24:27)

  Kwa kifupi Maandiko yote yanataka tumjue Yesu yeye ni nani!

  Sasa labda nije kwa Paulo ambaye wewe umedai mimi sijui Nyaraka zake….hivyo simjui Mugu kwa Kina! Je Paulo alifundisha “Mysteries” mpya ambao manabii wa leo kama wewe mnadai kuzifichua? Hebu msome Paulo;

  “ KWA SABABU HIYO MIMI PAULO NI MFUNGWA WAKE KRISTO KWA AJILI YENU NINYI MATAIFA.IKIWA MMESIKIA HABARI YA UWAKILI WA NEEMA YA MUNGU NILIYOPEWA KWA AJILI YENU.YA KWAMBA KWA KUFUNULIWA NALIJULISHWA SIRI (MYSTERY)HIYO KAMA NILIVYOTANGULIA KUANDIKA KWA MANENO MACHACHE. KWA HAYO MYASOMAPO MTAWEZA KUTAMBUA UFAHAMU WANGU KATIKA SIRI (MYSTERY) YAKE KRISTO!SIRI (MYSTERY) HAWAKUJULISHWA WANADAMU KATIKA VIZAZI VINGINE KAMA WALIVYOFUNULIWA NA MITUME WAKE NA MANABII WA ZAMANI HIZI KATIKA ROHO…….MIMI NILIYE MDOGO WA WATAKATIFU WOTE NALIPEWA NEEMA HII YA KUWAHUBIRIA MATAIFA UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA NA KUWAANGAZIA WATU WOTE WAJUE HABARI ZA MADARAKA YA SIRI (MYSTERY) HIYO AMBAYO TANGU ZAMANI ILISITIRIKA KATIKA MUNGU ALIYEVIUMBA VITU VYOTE HIVI SASA KWA NJIA YA KANISA…….! (WAEFESO 3:1-12)

  Hebu nieleze hawa Mitume wa leo na hawa Manabii wapya wanakuja na siri gani mpya! Au ndio hiyo ya “DNA”

  Tatizo kubwa la Manabii na Mtume kama wewe mnakuja na mafundisho kama mna “Hidden Revelation” ambayo Hakuna mwingine aliyenayo……..Na kama nyie ndio mna “access” tofauti na muumini yoyote ambaye amempa Yesu Maisha yake ! Ni mafundi mno i wa kuchanganya Maandiko na kuleta “utiisho” na roho ya kejeli kwa yoyote anayekuja kinyume cha “mafunuo” yenu Potofu! Hii sio enzi ya “Upapa” ! Maandiko sio mali yenu! Yako kwa kila Muumini anayejitoa na kujifunza kwake kama wale WABEROYA! Ambao hawakumeza kila kitu cha Paulo! Bali Walikaa wakatafakari na kuangalia kile alichosema Paulo kama kinaendana sawa na Maandiko Mengine!

  Nadhani nikipata muda nitakuja Na Maandiko ya Paulo unayedai simuelewi kuhusu Manabii wa Uongo!Na Labda kukufundisha kuwa Kwa nini Paulo aliniandika Nyaraka zake…zilikuwa na Maana gani kwa Makanisa aliyoyaandikia, na zina maana gani kwetu leo! Mambo ambayo kutokana na maandishi yako umeonyesha wazi wewe ni kipofu! Kwa leo ndugu yangu Lwembe Kwa leo Tafakari hili!

  UBARIKIWE!

 85. Ndugu Orbi,
  Kwanza, ni vizuri ikiwa utafika katika umbali wa kutambua kuwa kuyasoma Maandiko na kuyaelewa yanachosema ni jambo moja; na kuyaamini Maandiko katika yanachosema ni jambo jingine! Kuyasoma hukupa uelewa tu, kama ambavyo kila mtu anavyosoma na kuyaelewa kivyake, yaani madhehebu yetu.

  Kuyaamini Maandiko huzaa ufunuo. Tazama, Kulingana na Maandiko, mitume na jamii yote ya Israeli walikuwa wakimtazamia Masihi aje. Bali pia walifahamu ya kuwa kabla ya kuja kwake Masihi atatanguliwa na Eliya nabii. Basi hawa wanafunzi kwa kuyaamini Maandiko, Kristo alipowafanyia ile ishara ya Masihi waliyoisoma katika Maandiko, walimpokea hata tunaona akiwafunulia ya kwamba Eliya kisha kuja. Wale wengine, Maandiko wanayo hadi leo yakiwasubirisha katika jambo lilokwisha tendeka!
  Kwako pia nauona ugumu wa kuyaamini Maandiko. Wewe mwenyewe umenipa msururu wa Maandiko yanayozungumzia uwepo wa manabii. Umenukuu vifungu vingi sana vinavyotahadharisha juu ya ujio wa manabii wa uongo katika Agano Jipya, halafu tunakwambia ndio hao hapo uwanjani leo hii wakijitangaza kama waganga wa kienyeji, pia wakiwavutia watu huko gizani kwa mamilioni kwa staili lukuki za vitimbi, unaona kama tunanena kwa lugha! Tunakwambia Biblia ilisema hao wana UPAKO (makristo) wa uongo, yaani injili wanayoihubiri ni ya uongo, wameichakachua, naona hata huelewi, umeng’ang’ania mambo ya mwilini tu. Oh sijui kwanini hawajatutabiria mafuriko? Subiri wakubuhu, watakutabiria vyote hivyo na makuu zaidi ya hayo, hapo ndipo utakwenda kuwaungamia ulivyowakosea adabu kwa kuwadhalilisha kwenye mtandao, ili uende mbinguni!! Kwa sasa hivi utitiri wa manabii wako bado ni watoto, Nigeria ndiko wengi wamekubuhu tayari kama akina T.B. Joshua nk. Kama utakumbuka yuko nabii mmoja kutoka huko alitembelea hapa kwetu, tunabii twako unatotupigia kelele tukapigishwa magoti na kuwekewa mikono! Au Orbi unadhani tumekwisha kulivuka Agano Jipya? Bado tumo humo na sehemu ya Maandiko ndiyo hii inatutimilia!

  Halafu tatizo lako jingine ndugu yangu Orbi, huendi na wakati. Hivi wewe kwa mawazo yako unadhani uchungaji ni jambo la kujivunia katika mafanikio ya kihuduma? Uchungaji ni kazi ya kuajiriwa! Wachungaji wameajiriwa huko Katoliki au Lutheran nk. Kwa wajasiriamali wa Injili, unachomoka na Unabii au Utume au vyote ‘Mtume na Nabii’ hapo ndio watu wanakuelewa. Watu wenyewe kwanza wanataka miujiza. Kama hauna hata kamuujiza kakuwachangamsha kama haya makanisa ya zamani basi wapige hata na muujiza wa majengo makubwa ya kifahari watakuelewa!

  Basi Orbi, Biblia ikikuambia kuwa watokea manabii wa uongo, jua ni kweli watatokea. Utawatambuaje, watavaa mabango au watajitambulisha wenyewe? Nanukuu nukuu uliyonipa: ……”MTAWAJUA MANABII WA UONGO KWA KWA MATUNDA YAO”. Kwa faida ya kumuelimisha mtu ulipaswa uendelee kunielewesha Matunda hayo ni nini kuliko ulivyoibandika tu nukuu kavu bila ufunuo hata sielewi watakuwa na matunda gani, machungwa au yepi? Kama utazungumzia tunda la roho au la mwili utachukua muda mrefu sana kuwatambua maana nao wanakusomea vifungu hivyo hivyo wakikuhimiza katika hayo. Ndio maana tunazunguka kama pia kutoka kwa nabii huyu kwenda kwa mtume yule kila kukicha tuna bahatisha tu mpaka leo hii tunamtaka atakaye tutabiria mafuriko!

  Wewe Orbi ni mmataifa, kaa chini ya Injili ya mtume Paulo ndio utayajua mambo ya Mungu kwa kina. Usijifanye unamjua sana Yesu kuliko waliokuletea habari zake. Hivyo vitabu kama Wakorintho, Wagalatia nk ni maroho hayo mtume Paulo anayopambana nayo ambayo hayafi. Si unayaona hata leo hayo hapo yanasimamisha tena wanawake makanisani mpaka majumbani. Manabii uchwara wako hawajui hata kinachoendelea! Orbi, kaa katika fundisho la mitume ndio njia pekee unayoweza kuwatambua manabii na makristo wa uongo. Wingi wa watu au uponyaji au kutajirika au kuheshimiana hakumfanyi mhudumu yeyote yule kuwa mtumishi wa Mungu hata akijitambulisha hivyo. Mtumishi wa Mungu atajitambulisha na fundisho la mitume katika ujumla wake sio nusu nusu. Fundisho la Mitume ndio DNA yenyewe. Ndio maana nilikuambia kipimo kimojawapo kagua kama amebatizwa maji mengi kwa jina la Bwana Yesu Kristo kwa ondoleo la dhambi kama ilivyohubiriwa na mitume ili ujue kipawa hicho ni cha kweli au la. Badala yake eti unaniuliza iwapo Yohana Mbatizaji alibatizwa hivyo. Kumbe hujui hata ubatizo wa Yohana ni nini na ulikuwa na faida gani kiungu? Hebu sikia, Mdo 19:3-5 “… Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.” Yohana alitoka kwa Mungu na huduma hiyo na kazi hiyo akaimaliza na kuondoka akimuacha Kristo uwanjani, sasa iweje tena aje abatizwe ubatizo huu, yaani afufuliwe? Maana ubatizo huu umeanza kutumika rasmi siku ya Pentekoste.
  Basi hao wachungaji wako unaodhani NDIO, wengi wao ni makristo. Wanaoperate nje ya realm ya fundisho la mitume hawana ONDOLEO LA DHAMBI, hawakupita kwenye ule mlango alioufungua Petro siku ile katika Mdo 2:38, kwa hiyo hawana vazi jeupe. Wameloweshana nguo tu na maneno ya dini wasiyoyaelewa wakaondoka na UPAKO wa uongo nao HAWAJUI!
  Tazama Maandiko yanasema mwanamume asifunike kichwa asalipo; 1Kor 11:4 ‘Kila mwanamume, asalipo au anapohutubu, naye amefunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake (Kristo)’ Angalia maaskofu wako na makofia yao makubwa wanayoyavaa! Tena majuzi nimewaona nao wapentekoste wameyavaa. Wengine wamechukua kutoka vifungu hivyo hivyo halafu wanawafunga wanawake vitambaa kichwani makanisani mwao kinyume na Maandiko au mitume wanachofundisha. Umeelewa Orbi? Mafundisho ndio matunda yenyewe ya leo, kama hayako sawa na mitume hata kwa nukta, kimbia uiponye roho yako na ghadhabu ya Mungu inayokuja!

  Basi mpaka ukae kwanza chini ya mitume ndio utayaelewa mambo haya sio chini ya mchungaji au nabii nk. Kung’ang’ania mafundisho ya Yesu kama vile na wewe ulikuwa naye ni kujipumbaza. Mitume ndio waliokutambulisha habari za Yesu wao ndio wanatueleza yote yaliyotokea, maneno yote aliyofundisha wao mitume ndio wanatuelezea sisi, akina Yohana, Mathayo na wengineo. Sasa wewe unapojifanya unamjua sana Yesu kuliko hao waliokuletea habari zake inashangaza! Hao wanakwambia hivi: Gal 1:8 “Lakini japokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri na alaaniwe.” Sasa ni jambo gani lililo gumu hapa kulielewa, kwamba Injili waliyokuhubiri ndiyo hiyo ya ubatizo kwa jina la Bwana Yesu Kristo, maji mengi, sasa ukimkuta nabii au yeyote yule anawanyunyizia maji katika ubatizo, au anawaloweka kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, si unatakiwa ujue moja kwa moja kuwa huyu ni nabii wa uongo na kwa injili anayofundisha basi lazima awe amelaaniwa! Iwapo unababaika na maamuzi basi hata Injili yenyewe utakuwa huijui labda misale ya waumini. Fundisho lolote lile likiwa tofauti na la Mitume hicho ni kifo moja kwa moja!

  Siku ya Pentekoste, Kwa taarifa yako ndugu Orbi, Yesu alirudi kama alivyowaahidi; Mt 28:20 “… na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari”. Basi unapowaona mitume jua umemwona Yeye. Yeye ndiye hayo Maandiko uliyoyanukuu ukisema ya mwandishi usiyemjua. Kweli kwa jinsi unavyojieleza, umesema kweli, humjui! Ondoka katika kiwango cha mwilini ingia kile cha Rohoni basi utamwona Mwandishi wa Vitabu vyote katika Biblia kuwa “…ni Yeye yule, jana na leo na hata milele”. Hebu nieleze kitabu cha Mwanzo, Mungu alipoanza uumbaji, Musa aliyekiandika alikuwepo? Mambo yote yanayomhusu Mungu huanzia Rohoni sio mwilini. Hata hawa manabii wako unaowapiga vita ambayo hutashinda ni sehemu ya Neno la Mungu linalopaswa kutimia. Si kwamba eti mimi nawatetea, hapana mimi nilikuwa nakuonesha tu kuwa hao wanapaswa kuwepo kulingana na Neno. Je, Mungu akikutahadharisha kama alivyofanya halafu wasitokee, si atakuwa muongo! Tuliza munkari Orbi, hao manabii wako hawana namna ya kujirudi, shetani alikwisha zing’oa breki zote. Hao ni kama Kaini, hawana uwezo wa kutubu licha ya Mungu kumhubiri au Yuda, alipoambiwa aende akatimize azma yake, si angelianguka hapo kifudi fudi akaitubia dhambi yake, lakini badala yake akasonga mbele. Hawa nao ndio hivyo, si umesoma gazeti la kikristo la hapa kwetu lililotujuza kuwa Askofu Mkuu mmoja wakipentekoste hapa kwetu kamsimika shoga kuwa mchungaji!!!! Basi ikiwa uko chini ya mafundisho ya watumishi wa jinsi hii utapata faida gani?

  Hata hicho kifungu cha unachopenda kukinukuu: “MUNGU AMBAYE ALISEMA NA BABA ZETU KATIKA MANABII KWA SEHEMU NYINGI NA KWA NJIA NYINGI, MWISHO WA SIKU HIZI AMESEMA NA SISI KATIKA MWANA ALIYEMWEKA KUWA MRITHI WA YOTE TENA KWA YEYE ALIUFANYA ULIMWENGU….(Heb 1:2)” badala ya kukupeleka katika uelewa zaidi wa Neno la Mungu, naona kwa msingi uliojengewa, unazidi kwenda mbali na Neno hata unajiaminisha kwa msingi wa mafundisho unayopewa kuwa hakuna tena manabii wa kweli leo hii wanaopaswa kuwepo. Kama wa uongo wapo na tunawaona, sembuse wa kweli? 1Kor 12:28 inakufundisha hivi: “Na Mungu ameweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii…”; halafu nikakuambia makanisa yako mawili ambayo ni mapacha. Moja “limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.” (Efe 2:20) hawa ndio kanisa la Kristo aliowafia, wapo na vipawa hivyo wanavyo! Huduma yao haina makelele kama ya hili kanisa jingine, hili la uongo ambalo umeonywa kuwahusu. Ukiwasikiliza sana kelele zao na mafundisho yao ya uongo ndio unaishia kuwa mbishi hata kwa vitu usivyovielewa. Wao wanakwambia na kukusisitizia kama unavyo fanya wewe (sijui wewe nawe ni mwalimu wa dini au mwanafunzi unaye elekea kufuzu), kuwa kwa andiko hilo hakuna tena Nabii anayepaswa kuja, yule tai mkubwa. Hebu nieleze, lile Andiko katika Malaki 4:5 “Angalieni, nitawapelekeeni Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA iliyo kuu na kuogofya”, utalitupia wapi hili hata useme eti hakuna nabii ajaye? Wapakwa mafuta wa uongo wengi hulazimisha lile Andiko ambalo Kristo aliwafunulia wanafunzi wake kuhusu Yohana Mbatizaji kuwa ndiye huyo Eliya Mt 11:14 na hivyo kulitamatisha Andiko hilo kana kwamba limemalizikia hapo katika kutimia kwake wakivuna juu ya upako walio nao ambao huwapofusha wafuasi wao macho yao ya kiroho. Basi kama Andiko hilo limetimia kwa ukamilifu wake, iko wapi hiyo Siku ya BWANA, ndugu Orbi? Maana ilipaswa ije baada ya YohanaMbatizaji lakini haikuja, kulikoni? Ukiambiwa hujayachunguza Maandiko vizuri, unawaka moto vibaya sana kulinda mafundisho yenu dhaifu!
  Haya, sogea karibu na Biblia yako, jiachilie toka vifungo vya mafundisho ya kimwili, njoo rohoni sasa. Fungua hiyo Malaki 4:5 ; hiyo ni ahadi kamili kutoka kwa Mungu. Nae Mungu hawakurupushi tu manabii wake kuwaleta duniani bila kuiweka wazi huduma watakayoifanya kama ibilisi anavyowakurupusha manabii wake, eti kazi utaikuta stendi! Kazi ya manabii wa Mungu amekwisha wawekea hapo kabla hata hawajazaliwa, wakifika wanaflow nayo tu hawabahatishi. Kwa hiyo kazi ya nabii Eliya ile huduma atakayokuja nayo Mungu amewafunulia wanae mapema, ndio huo mstari wa 6. Malaki 4:6 “ Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, …”. Sasa, iwapo Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye huyu Eliya anayetabiriwa hapa, yatupasa tuangalie pia iwapo huduma hiyo aliyotengewa Eliya ilifanyika au la. Biblia inathibitisha jambo hilo kufanyika sawa sawa katika kiwango kilicholihusu. Luka 1:17 “ Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, …”. Unaona, Orbi, Yohana Mbatizaji alitimiza nusu tu ya lile Andiko. ‘Aliigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto’ tu! Ndio maana ile Siku ya BWANA bado dunia haijaifikia! Aliigeuza mioyo ya baba, yaani Torati, iwaelekee watoto, yaani Yesu na mitume wake! Ile nusu ya pili ya lile Andiko ndiyo inayokuhusu wewe na mimi na utitiri wa manabii wako hao wanaofundisha mambo yao kutoka vichwani mwao kwa uvuvio wa teologia zao. Hawa ni watoto waliozaliwa kutoka Injili ya mitume wamekengeukia mbele huko wakayaacha mafundisho ya mitume wakageukia mafundisho ya mapepo, hawa sasa ndio hiyo huduma ya kuwarejesha kuwageukia baba zao wa Imani mitume, inawahusu na kutoka huduma hiyo ndio ninakwambia urudi Orbi ukae chini ya mitume uiponye roho yako maana hiyo ‘Siku ya BWANA iliyo kuu na kuogofya’ haiko mbali tena nawe yaweza kukuta unashangaa; si ilikuwa tunyakuliwe kwanza, mbona sasa umekuja huu moto! Unyakuliwe na mashoga???
  Unaweza kuniona kama kinywa cha manabii, bali huo ni uchanga tu, nilikuambia hao manabii wako wamejaa chuki, tamaa, wivu na ni waoga wa kubaki peke yao kiasi kwamba huyang’ang’ania makusanyiko yao kama luba tena humlaani yeyote anayewakimbia; basi kwa tabia hiyo wanaweza kuwa na kinywa kimoja kweli?
  Orbi, acha uoga, Biblia imebeba Mystery ya Mungu, mapepo yakiijua itakuwa tabu sana ndio maana Mungu, Siri yake ameificha humo humo ndani ya Biblia mpaka akuoneshe mwenyewe. Nenda naye polepole ukikurupuka utajikuta nawe umevishwa KOFIA KUUUBWA na FIMBO, halafu unahutubu au una nena kwa lugha; hebu niambie hivyo vicheko vya mapepo vitakuwaje??????
  Bwana na atupe sote macho ya Rohoni!

 86. bwana Yesu asifiwe ndg.orbi na wengine
  naomba niseme kwa uchungu kwamba post hii haikuwa kwa lengo la kujenga ila kubomoa.nasikitika kuwa post hii imelitukana jina la Yesu na wengi wameanguka kwa kusoma post hii.nashauri sisi watu tuliookoka tutume post ambazo zitatujenga na wala sio kuwaharibu wenye kusikia.halafu tungesoma pia habari za nabii elisha jinsi ambavyo mtoto wa mwanamke mshunami alivyokufa,nabii alisema kuwa Bwana amemficha jambo hilo namaanisha kwamba kuna mambo mengine Mungu anaweza kuyaficha kwa kusudi maalum.na kuhusu suala la mabondeni,tukumbuke kwamba janga hili halikuwa kwa watu wa mabondeni tu ila kwa watu pia wasiokuwa mabondeni.

  mimi nasema kwa ujasiri kwamba aliyetuma hiyo post hajajenga wala hajatoa changamoto ila amebomo,kwasababu anatakiwa akumbuke kwamba huyu anayejiita nabii ni ndugu yake katika kristo hivyo hakutakiwa kumnyooshea mpakwa mafuta wa Bwana kidole ila amuombee na kama anaweza kuzungumza naye akazungumze naye.naomba wapendwa tusigeuze blog hii kuwa genge la usengenyaji na kuzodoana.

  nionavyo mimi, mbarikiwe wapendwa

 87. bila maombi na kusimama katika wokovu hatutaweza kupambana na matatizo yanayowakumba watanzania Mungu atusaidie.watumishi tuombeane na tusisengenyane au kusemana kwa mabaya.tumweleze Roho Mtakatifu ili aendelee kuwagusa watu waokoke ili tumzalie Bwana matunda yampendezayo yeye.amen.

 88. Ndugu yangu Lwembe,

  Nimeyasoma maandishi yako, naamini na wengi katika Blog hii wameyasoma, nadhani unasahau kabisa kuwa kwa maandishi tu unamtambua mtu aliyeandika ni wa namna gani, au ana “roho” wa aina gani inayomsukuma kuandika, na alikuwa katika hali gani, kwa hilo nitaawachia wanablog waamue wenyewe, kwani maandiko yako yanazungumza kwa sauti kubwa mno kuonyesha dhahiri wewe ni mtu wa namna gani, aina ya ukristo wako na ufahamu wako wa Neno la Mungu.

  Umeandika kurasa karibia nne, na badala ya kuja na hoja za Maandiko kutetea hoja, au maswali niliyokuuliza wewe umekuja na mashambulizi binafsi dhidi yangu (Personal attack) Naamini kama hii ndio ya “Roho ya Manabii” Inatenda kazi ndani yako, basi nadhani itakimbiza wengi na kuzidi kuitilia mashaka huduma hii………HEBU ITETEE HUDUMA HII KWA MAANDIKO BAYANA!

  Anyway siwezi kuzibu mashambulizi yako yote ya kurasa nne leo, lakini nitakuwa nikijibu hoja zako taratibu kila nipatapo muda, naamini hii itasaidia Wakristo wengi kutambua Upotofu uliyojengwa katika huduma hizi nyingi za Kinabii, ambazo kwa kifupi ni potofu na zimejengwa nje kabisa katika ufunuo wa Neno la Mungu (Extra Biblical Revelation)
  Hebu tuanze kwa kuiangalia nukuu yako hii;

  “Wewe Orbi ni mmataifa, kaa chini ya Injili ya mtume Paulo ndio utayajua mambo ya Mungu kwa kina. Usijifanye unamjua sana Yesu kuliko waliokuletea habari zake.”

  Ningependa kukuuliza Ndugu yangu Lwembe (japo wewe umeisha nihukumu mimi ni mmataifa! Sijui na hili umelipata kwa ufunuo wa kinabii!) Hivi kuyajua mafundisho ya Mungu kwa kina inatubidi tukae katika Injili ya Mtume Paulo tu? Maana Paulo hakufundisha hivyo! Au ndio mafunuo ya Kinabii yanasema hivyo? Au Ni wapi Maandiko yanasema hivyo? Sasa naogopa kabisa hata kuja na aya kutoka katika Biblia….maana kila nachokuletea wewe hukitaki!

  Ni Andiko gani hasa liko juu ya jingine? Maandiko ya Paulo yana uvuvio zaidi na Maandishi ya Injili NNE zenye matamko ya Yesu Mwenyewe? Nadhani umesahau kabisa kanuni ya Msingi kuwa Imani hii imejengwa juu ya Yesu Kristo! Na si kingine kabisa!
  Utasemaje Nukuu hii kutoka kwa Paulo Mwenyewe;

  “ KILA ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU LAFAA KWA MAANDIKO “ 1 Tim 3:14

  Sasa ni Andiko lipi katika Biblia linaloweza kutufanya tumfahamu Mungu kwa kina? Je ni Maandiko ya Paulo? Kama unavyosema wewe au Je ni Maandiko ya Mathew, Luke, Mark, na John? Au Petro? Yakobo?

  Kama wewe kweli ni mwanafunzi au Mfuasi wa Yesu ungalitambua wazi KUWA MAANDIKO YOTE NDANI YA BIBLIA YAMEJENGWA TUMFAHAMU YESU! TUITAMBUE KAZI YAKE YA MSALABANI NA WOKUVU WAKE MKUU! HAKUNA KINGINE ZAIDI YA HICHO! HAKUNA CHA “DNA” WALA “MYSTRY” WALA KITU CHOCHOTE KILICHOFICHIKA KWA MTU ALYEMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KAMA WEWE NA MANABII WA LEO WANAOJITOKEZA MITAANI WANAVYOTAKA TUAMINI!

  Hebu soma nukuu hii Yesu anasema nini Juu ya Maandiko; ( Ingawa naona umeanza kuyakataa Maneno ya Yesu)

  “ AKAANZA KUTOKA MUSA NA MANABII WOTE AKAWAELEZA KATIKA MAANDIKO YOTE YALIYOMHUSU YEYE MWENYEWE” (Luka 24:27)

  Kwa kifupi Maandiko yote yanataka tumjue Yesu yeye ni nani!

  Sasa labda nije kwa Paulo ambaye wewe umedai mimi sijui Nyaraka zake….hivyo simjui Mugu kwa Kina! Je Paulo alifundisha “Mysteries” mpya ambao manabii wa leo kama wewe mnadai kuzifichua? Hebu msome Paulo;

  “ KWA SABABU HIYO MIMI PAULO NI MFUNGWA WAKE KRISTO KWA AJILI YENU NINYI MATAIFA.IKIWA MMESIKIA HABARI YA UWAKILI WA NEEMA YA MUNGU NILIYOPEWA KWA AJILI YENU.YA KWAMBA KWA KUFUNULIWA NALIJULISHWA SIRI (MYSTERY)HIYO KAMA NILIVYOTANGULIA KUANDIKA KWA MANENO MACHACHE. KWA HAYO MYASOMAPO MTAWEZA KUTAMBUA UFAHAMU WANGU KATIKA SIRI (MYSTERY) YAKE KRISTO!SIRI (MYSTERY) HAWAKUJULISHWA WANADAMU KATIKA VIZAZI VINGINE KAMA WALIVYOFUNULIWA NA MITUME WAKE NA MANABII WA ZAMANI HIZI KATIKA ROHO…….MIMI NILIYE MDOGO WA WATAKATIFU WOTE NALIPEWA NEEMA HII YA KUWAHUBIRIA MATAIFA UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA NA KUWAANGAZIA WATU WOTE WAJUE HABARI ZA MADARAKA YA SIRI (MYSTERY) HIYO AMBAYO TANGU ZAMANI ILISITIRIKA KATIKA MUNGU ALIYEVIUMBA VITU VYOTE HIVI SASA KWA NJIA YA KANISA…….! (WAEFESO 3:1-12)

  Hebu nieleze hawa Mitume wa leo na hawa Manabii wapya wanakuja na siri gani mpya! Au ndio hiyo ya “DNA”

  Tatizo kubwa la Manabii na Mtume kama wewe mnakuja na mafundisho kama mna “Hidden Revelation” ambayo Hakuna mwingine aliyenayo……..Na kama nyie ndio mna “access” tofauti na muumini yoyote ambaye amempa Yesu Maisha yake ! Ni mafundi mno i wa kuchanganya Maandiko na kuleta “utiisho” na roho ya kejeli kwa yoyote anayekuja kinyume cha “mafunuo” yenu Potofu! Hii sio enzi ya “Upapa” ! Maandiko sio mali yenu! Yako kwa kila Muumini anayejitoa na kujifunza kwake kama wale WABEROYA! Ambao hawakumeza kila kitu cha Paulo! Bali Walikaa wakatafakari na kuangalia kile alichosema Paulo kama kinaendana sawa na Maandiko Mengine!

  Nadhani nikipata muda nitakuja Na Maandiko ya Paulo unayedai simuelewi kuhusu Manabii wa Uongo!Na Labda kukufundisha kuwa Kwa nini Paulo aliniandika Nyaraka zake…zilikuwa na Maana gani kwa Makanisa aliyoyaandikia, na zina maana gani kwetu leo! Mambo ambayo kutokana na maandishi yako umeonyesha wazi wewe ni kipofu! Kwa leo ndugu yangu Lwembe Kwa leo Tafakari hili!

  UBARIKIWE!

 89. Ndugu Orbi,
  Kwanza, ni vizuri ikiwa utafika katika umbali wa kutambua kuwa kuyasoma Maandiko na kuyaelewa yanachosema ni jambo moja; na kuyaamini Maandiko katika yanachosema ni jambo jingine! Kuyasoma hukupa uelewa tu, kama ambavyo kila mtu anavyosoma na kuyaelewa kivyake, yaani madhehebu yetu.

  Kuyaamini Maandiko huzaa ufunuo. Tazama, Kulingana na Maandiko, mitume na jamii yote ya Israeli walikuwa wakimtazamia Masihi aje. Bali pia walifahamu ya kuwa kabla ya kuja kwake Masihi atatanguliwa na Eliya nabii. Basi hawa wanafunzi kwa kuyaamini Maandiko, Kristo alipowafanyia ile ishara ya Masihi waliyoisoma katika Maandiko, walimpokea hata tunaona akiwafunulia ya kwamba Eliya kisha kuja. Wale wengine, Maandiko wanayo hadi leo yakiwasubirisha katika jambo lilokwisha tendeka!

  Kwako pia nauona ugumu wa kuyaamini Maandiko. Wewe mwenyewe umenipa msururu wa Maandiko yanayozungumzia uwepo wa manabii. Umenukuu vifungu vingi sana vinavyotahadharisha juu ya ujio wa manabii wa uongo katika Agano Jipya, halafu tunakwambia ndio hao hapo uwanjani leo hii wakijitangaza kama waganga wa kienyeji, pia wakiwavutia watu huko gizani kwa mamilioni kwa staili lukuki za vitimbi, unaona kama tunanena kwa lugha! Tunakwambia Biblia ilisema hao wana UPAKO (makristo) wa uongo, yaani injili wanayoihubiri ni ya uongo, wameichakachua, naona hata huelewi, umeng’ang’ania mambo ya mwilini tu. Oh sijui kwanini hawajatutabiria mafuriko? Subiri wakubuhu, watakutabiria vyote hivyo na makuu zaidi ya hayo, hapo ndipo utakwenda kuwaungamia ulivyowakosea adabu kwa kuwadhalilisha kwenye mtandao, ili uende mbinguni!! Kwa sasa hivi utitiri wa manabii wako bado ni watoto, Nigeria ndiko wengi wamekubuhu tayari kama akina T.B. Joshua nk. Kama utakumbuka yuko nabii mmoja kutoka huko alitembelea hapa kwetu, tunabii twako unatotupigia kelele tukapigishwa magoti na kuwekewa mikono! Au Orbi unadhani tumekwisha kulivuka Agano Jipya? Bado tumo humo na sehemu ya Maandiko ndiyo hii inatutimilia!

  Halafu tatizo lako jingine ndugu yangu Orbi, huendi na wakati. Hivi wewe kwa mawazo yako unadhani uchungaji ni jambo la kujivunia katika mafanikio ya kihuduma? Uchungaji ni kazi ya kuajiriwa! Wachungaji wameajiriwa huko Katoliki au Lutheran nk. Kwa wajasiriamali wa Injili, unachomoka na Unabii au Utume au vyote ‘Mtume na Nabii’ hapo ndio watu wanakuelewa. Watu wenyewe kwanza wanataka miujiza. Kama hauna hata kamuujiza kakuwachangamsha kama haya makanisa ya zamani basi wapige hata na muujiza wa majengo makubwa ya kifahari watakuelewa!
  Basi Orbi, Biblia ikikuambia kuwa watokea manabii wa uongo, jua ni kweli watatokea. Utawatambuaje, watavaa mabango au watajitambulisha wenyewe? Nanukuu nukuu uliyonipa: ……”MTAWAJUA MANABII WA UONGO KWA KWA MATUNDA YAO”. Kwa faida ya kumuelimisha mtu ulipaswa uendelee kunielewesha Matunda hayo ni nini kuliko ulivyoibandika tu nukuu kavu bila ufunuo hata sielewi watakuwa na matunda gani, machungwa au yepi? Kama utazungumzia tunda la roho au la mwili utachukua muda mrefu sana kuwatambua maana nao wanakusomea vifungu hivyo hivyo wakikuhimiza katika hayo. Ndio maana tunazunguka kama pia kutoka kwa nabii huyu kwenda kwa mtume yule kila kukicha tuna bahatisha tu mpaka leo hii tunamtaka atakaye tutabiria mafuriko!

  Wewe Orbi ni mmataifa, kaa chini ya Injili ya mtume Paulo ndio utayajua mambo ya Mungu kwa kina. Usijifanye unamjua sana Yesu kuliko waliokuletea habari zake. Hivyo vitabu kama Wakorintho, Wagalatia nk ni maroho hayo mtume Paulo anayopambana nayo ambayo hayafi. Si unayaona hata leo hayo hapo yanasimamisha tena wanawake makanisani mpaka majumbani. Manabii uchwara wako hawajui hata kinachoendelea! Orbi, kaa katika fundisho la mitume ndio njia pekee unayoweza kuwatambua manabii na makristo wa uongo. Wingi wa watu au uponyaji au kutajirika au kuheshimiana hakumfanyi mhudumu yeyote yule kuwa mtumishi wa Mungu hata akijitambulisha hivyo. Mtumishi wa Mungu atajitambulisha na fundisho la mitume katika ujumla wake sio nusu nusu. Fundisho la Mitume ndio DNA yenyewe. Ndio maana nilikuambia kipimo kimojawapo kagua kama amebatizwa maji mengi kwa jina la Bwana Yesu Kristo kwa ondoleo la dhambi kama ilivyohubiriwa na mitume ili ujue kipawa hicho ni cha kweli au la. Badala yake eti unaniuliza iwapo Yohana Mbatizaji alibatizwa hivyo. Kumbe hujui hata ubatizo wa Yohana ni nini na ulikuwa na faida gani kiungu? Hebu sikia, Mdo 19:3-5 “… Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.” Yohana alitoka kwa Mungu na huduma hiyo na kazi hiyo akaimaliza na kuondoka akimuacha Kristo uwanjani, sasa iweje tena aje abatizwe ubatizo huu, yaani afufuliwe? Maana ubatizo huu umeanza kutumika rasmi siku ya Pentekoste.
  Basi hao wachungaji wako unaodhani NDIO, wengi wao ni makristo. Wanaoperate nje ya realm ya fundisho la mitume hawana ONDOLEO LA DHAMBI, hawakupita kwenye ule mlango alioufungua Petro siku ile katika Mdo 2:38, kwa hiyo hawana vazi jeupe. Wameloweshana nguo tu na maneno ya dini wasiyoyaelewa wakaondoka na UPAKO wa uongo nao HAWAJUI!

  Tazama Maandiko yanasema mwanamume asifunike kichwa asalipo; 1Kor 11:4 ‘Kila mwanamume, asalipo au anapohutubu, naye amefunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake (Kristo)’ Angalia maaskofu wako na makofia yao makubwa wanayoyavaa! Tena majuzi nimewaona nao wapentekoste wameyavaa. Wengine wamechukua kutoka vifungu hivyo hivyo halafu wanawafunga wanawake vitambaa kichwani makanisani mwao kinyume na Maandiko au mitume wanachofundisha. Umeelewa Orbi? Mafundisho ndio matunda yenyewe ya leo, kama hayako sawa na mitume hata kwa nukta, kimbia uiponye roho yako na ghadhabu ya Mungu inayokuja!

  Basi mpaka ukae kwanza chini ya mitume ndio utayaelewa mambo haya sio chini ya mchungaji au nabii nk. Kung’ang’ania mafundisho ya Yesu kama vile na wewe ulikuwa naye ni kujipumbaza. Mitume ndio waliokutambulisha habari za Yesu wao ndio wanatueleza yote yaliyotokea, maneno yote aliyofundisha wao mitume ndio wanatuelezea sisi, akina Yohana, Mathayo na wengineo. Sasa wewe unapojifanya unamjua sana Yesu kuliko hao waliokuletea habari zake inashangaza! Hao wanakwambia hivi: Gal 1:8 “Lakini japokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri na alaaniwe.” Sasa ni jambo gani lililo gumu hapa kulielewa, kwamba Injili waliyokuhubiri ndiyo hiyo ya ubatizo kwa jina la Bwana Yesu Kristo, maji mengi, sasa ukimkuta nabii au yeyote yule anawanyunyizia maji katika ubatizo, au anawaloweka kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, si unatakiwa ujue moja kwa moja kuwa huyu ni nabii wa uongo na kwa injili anayofundisha basi lazima awe amelaaniwa! Iwapo unababaika na maamuzi basi hata Injili yenyewe utakuwa huijui labda misale ya waumini. Fundisho lolote lile likiwa tofauti na la Mitume hicho ni kifo moja kwa moja!

  Siku ya Pentekoste, Kwa taarifa yako ndugu Orbi, Yesu alirudi kama alivyowaahidi; Mt 28:20 “… na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari”. Basi unapowaona mitume jua umemwona Yeye. Yeye ndiye hayo Maandiko uliyoyanukuu ukisema ya mwandishi usiyemjua. Kweli kwa jinsi unavyojieleza, umesema kweli, humjui! Ondoka katika kiwango cha mwilini ingia kile cha Rohoni basi utamwona Mwandishi wa Vitabu vyote katika Biblia kuwa “…ni Yeye yule, jana na leo na hata milele”. Hebu nieleze kitabu cha Mwanzo, Mungu alipoanza uumbaji, Musa aliyekiandika alikuwepo? Mambo yote yanayomhusu Mungu huanzia Rohoni sio mwilini. Hata hawa manabii wako unaowapiga vita ambayo hutashinda ni sehemu ya Neno la Mungu linalopaswa kutimia. Si kwamba eti mimi nawatetea, hapana mimi nilikuwa nakuonesha tu kuwa hao wanapaswa kuwepo kulingana na Neno. Je, Mungu akikutahadharisha kama alivyofanya halafu wasitokee, si atakuwa muongo! Tuliza munkari Orbi, hao manabii wako hawana namna ya kujirudi, shetani alikwisha zing’oa breki zote. Hao ni kama Kaini, hawana uwezo wa kutubu licha ya Mungu kumhubiri au Yuda, alipoambiwa aende akatimize azma yake, si angelianguka hapo kifudi fudi akaitubia dhambi yake, lakini badala yake akasonga mbele. Hawa nao ndio hivyo, si umesoma gazeti la kikristo la hapa kwetu lililotujuza kuwa Askofu Mkuu mmoja wakipentekoste hapa kwetu kamsimika shoga kuwa mchungaji!!!! Basi ikiwa uko chini ya mafundisho ya watumishi wa jinsi hii utapata faida gani?

  Hata hicho kifungu cha unachopenda kukinukuu: “MUNGU AMBAYE ALISEMA NA BABA ZETU KATIKA MANABII KWA SEHEMU NYINGI NA KWA NJIA NYINGI, MWISHO WA SIKU HIZI AMESEMA NA SISI KATIKA MWANA ALIYEMWEKA KUWA MRITHI WA YOTE TENA KWA YEYE ALIUFANYA ULIMWENGU….(Heb 1:2)” badala ya kukupeleka katika uelewa zaidi wa Neno la Mungu, naona kwa msingi uliojengewa, unazidi kwenda mbali na Neno hata unajiaminisha kwa msingi wa mafundisho unayopewa kuwa hakuna tena manabii wa kweli leo hii wanaopaswa kuwepo. Kama wa uongo wapo na tunawaona, sembuse wa kweli? 1Kor 12:28 inakufundisha hivi: “Na Mungu ameweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii…”; halafu nikakuambia makanisa yako mawili ambayo ni mapacha. Moja “limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.” (Efe 2:20) hawa ndio kanisa la Kristo aliowafia, wapo na vipawa hivyo wanavyo! Huduma yao haina makelele kama ya hili kanisa jingine, hili la uongo ambalo umeonywa kuwahusu. Ukiwasikiliza sana kelele zao na mafundisho yao ya uongo ndio unaishia kuwa mbishi hata kwa vitu usivyovielewa. Wao wanakwambia na kukusisitizia kama unavyo fanya wewe (sijui wewe nawe ni mwalimu wa dini au mwanafunzi unaye elekea kufuzu), kuwa kwa andiko hilo hakuna tena Nabii anayepaswa kuja, yule tai mkubwa. Hebu nieleze, lile Andiko katika Malaki 4:5 “Angalieni, nitawapelekeeni Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA iliyo kuu na kuogofya”, utalitupia wapi hili hata useme eti hakuna nabii ajaye? Wapakwa mafuta wa uongo wengi hulazimisha lile Andiko ambalo Kristo aliwafunulia wanafunzi wake kuhusu Yohana Mbatizaji kuwa ndiye huyo Eliya Mt 11:14 na hivyo kulitamatisha Andiko hilo kana kwamba limemalizikia hapo katika kutimia kwake wakivuna juu ya upako walio nao ambao huwapofusha wafuasi wao macho yao ya kiroho. Basi kama Andiko hilo limetimia kwa ukamilifu wake, iko wapi hiyo Siku ya BWANA, ndugu Orbi? Maana ilipaswa ije baada ya YohanaMbatizaji lakini haikuja, kulikoni? Ukiambiwa hujayachunguza Maandiko vizuri, unawaka moto vibaya sana kulinda mafundisho yenu dhaifu!

  Haya, sogea karibu na Biblia yako, jiachilie toka vifungo vya mafundisho ya kimwili, njoo rohoni sasa. Fungua hiyo Malaki 4:5 ; hiyo ni ahadi kamili kutoka kwa Mungu. Nae Mungu hawakurupushi tu manabii wake kuwaleta duniani bila kuiweka wazi huduma watakayoifanya kama ibilisi anavyowakurupusha manabii wake, eti kazi utaikuta stendi! Kazi ya manabii wa Mungu amekwisha wawekea hapo kabla hata hawajazaliwa, wakifika wanaflow nayo tu hawabahatishi. Kwa hiyo kazi ya nabii Eliya ile huduma atakayokuja nayo Mungu amewafunulia wanae mapema, ndio huo mstari wa 6. Malaki 4:6 “ Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, …”. Sasa, iwapo Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye huyu Eliya anayetabiriwa hapa, yatupasa tuangalie pia iwapo huduma hiyo aliyotengewa Eliya ilifanyika au la. Biblia inathibitisha jambo hilo kufanyika sawa sawa katika kiwango kilicholihusu. Luka 1:17 “ Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, …”. Unaona, Orbi, Yohana Mbatizaji alitimiza nusu tu ya lile Andiko. ‘Aliigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto’ tu! Ndio maana ile Siku ya BWANA bado dunia haijaifikia! Aliigeuza mioyo ya baba, yaani Torati, iwaelekee watoto, yaani Yesu na mitume wake! Ile nusu ya pili ya lile Andiko ndiyo inayokuhusu wewe na mimi na utitiri wa manabii wako hao wanaofundisha mambo yao kutoka vichwani mwao kwa uvuvio wa teologia zao. Hawa ni watoto waliozaliwa kutoka Injili ya mitume wamekengeukia mbele huko wakayaacha mafundisho ya mitume wakageukia mafundisho ya mapepo, hawa sasa ndio hiyo huduma ya kuwarejesha kuwageukia baba zao wa Imani mitume, inawahusu na kutoka huduma hiyo ndio ninakwambia urudi Orbi ukae chini ya mitume uiponye roho yako maana hiyo ‘Siku ya BWANA iliyo kuu na kuogofya’ haiko mbali tena nawe yaweza kukuta unashangaa; si ilikuwa tunyakuliwe kwanza, mbona sasa umekuja huu moto! Unyakuliwe na mashoga???

  Unaweza kuniona kama kinywa cha manabii, bali huo ni uchanga tu, nilikuambia hao manabii wako wamejaa chuki, tamaa, wivu na ni waoga wa kubaki peke yao kiasi kwamba huyang’ang’ania makusanyiko yao kama luba tena humlaani yeyote anayewakimbia; basi kwa tabia hiyo wanaweza kuwa na kinywa kimoja kweli?

  Orbi, acha uoga, Biblia imebeba Mystery ya Mungu, mapepo yakiijua itakuwa tabu sana ndio maana Mungu, Siri yake ameificha humo humo ndani ya Biblia mpaka akuoneshe mwenyewe. Nenda naye polepole ukikurupuka utajikuta nawe umevishwa KOFIA KUUUBWA na FIMBO, halafu unahutubu au una nena kwa lugha; hebu niambie hivyo vicheko vya mapepo vitakuwaje??????
  Bwana na atupe sote macho ya Rohoni!

 90. Hahaha! Ndugu Amin umenichekesha sana, Kumbe TMA “WALISHATABIRI”. Kama ndivyo kwa mlioko Dar es Salaam mlipata “ujumbe”. Sasa inakuwaje tunadai tena utabiri toka watumishi wa Mungu? Au ili “ku confirm”? Mtumishi mmoja wa Mungu alishawahi kusema “walio kwenye makazi holela wahame na wengine wasijenge kwenye makazi holela”. Pia alisisitiza kuwa “MAKAZI HOLELA NI MPANGO WA SHETANI…” Sidhani kama wengi WAMELIELEWA na wamezingatia hilo.

 91. Nilikuwa kwenye luninga yangu nikimwangalia mtumishi wa Mungu kutoka Zimbabwe Mrs.Angel akifundisha somo fulani zuri kuhusiana na ufalme wa Mungu.Wakati akifundisha na baadaye akitabiri kwa watu akasema kuwa,kuna tofauti ndogo sana kati ya IMANI NA UPUMBAVU (there is a very narrow line which separate faith and stupidness).Na akatoa mfano wa mzungu mmoja aliyeokoka ambaye alikuwa anaendesha gari lake kutoka nyumbani kwenda kazini.Katika safari yake mafuta kwenye gari yakaisha na kwa bahati alikuwa karibu sana na kituo cha mafuta (Fuel filling station).Badala ya kwenda kununua mafuta ili atie kwenye gari lake na aendelee na safari ya kuwahi kazini,mzungu yule aliamua kufanya maombi na kuvunja nguvu za giza kukemea roho ya kumaliza mafuta kwenye gari na kisha akaita upako wa kuyageuza maji yawe mafuta ya kuendeshea gari.Akamimina debe kadhaa kwenye gari na akatia mafuta.UNAWEZA KUPATA JAWABU HAPA NINI KILITOKEA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Hivi waliojenga mabondeni walikuwa wanasubiri watumishi wa Bwana watoe unabii ili wahame mabondeni???? Wanakumbuka sauti ya YUSUFU MAKAMBA MIAKA ILE ALIYOKUWA MKUU WA MKOA,WANAKUMBUKA MIITO MBALI MBALI YA VIONGOZI WA SERIKALI KUHUSIANA NA UKAAJI WAO WA MABONDENI.Tena hali ya hewa walishatabiri jambo hili hivi karibuni na wakatoa tahadhari kuhusiana na wakaazi wa mabondeni. Kwa hiyo nashauri kuwa watu waache kulaumu manabii kwani Mungu tayari alishasema na watu mfalme wa NINAWI ALIVYOMSIKIA BWANA NA KUTOA AMRI KWA WATU WAKE KUTUBU.

  Kama kuna mtu aliyeokoka anakaa jangwani,bonde la kigogo na alitegemea kuoteshwa na Mungu kuhusiana na mvua hiyo basi aanze kufanya toba kwani Mungu alishasema naye kwa sauti ya Makamba na hali ya hewa.

  Mungu awabariki sana

 92. Ninachokiona mimi hawa Manabii wa Tanzania wakikifanya ni Kuombea watu, ambapo maombezi hayo yanaitwa ‘Deliverance”. Vile vile huhubiri Neno kwa namna ya kuwapa watu matumaini na kuwaahidi wakati ujao wenye mafanikio. Kwa ufupi yangu ni hayo.

 93. Ndugu Oguda,

  Umeniuliza swali…Je, dini ama dhehebu lako lina ukiri wa hivyo vipawa vya Mungu ambavyo tumeahidiwa na Bwn? Ninatumai ya kuwa mnavikiri, lakini, Je, ni kweli mnayatekeleza yale yaliyoandikwa ama ni kwa baadhi ya Huduma na Karama tu?

  Ndugu yangu Oguda……mimi sio muumini wa dini au dhehebu……na linachofundisha Dhehebu langu au kanisa langu hakina maana kabisa kama mafundisho hayo hayajasimama Imara katika maneno ya Mungu……….Sisimami katika Imani hii kwa ukiri wa dhehebu…..!mimi ni Mkristo…….Namwamini Yesu…….Naamini maneno ya Mungu……..Na ndio maana nimeuliza swali hilo.Hawa Manabii waliotapakaa leo kama Uyoga kazi yao ni ipi hasa? Wana sifa za Unabii kwa kufanya kazi kama wale Mitume na Manabii walioko Tuliofunuliwa na maneno ya Mungu, maana katika kazi ya mojawapo ya Manabii katika Biblia ni kunena yatakayoikumbuka jamii kwa yale yatakayokuja, au yatakayoikumbuka……Tanzania imekuwa na huu utitiri wa Mitume na Manabii…….Hebu mnifungue macho nini hasa hasa kazi yao….msaada kwa Kanisa….na jamii ya Watanzania na Serikali?

 94. Orbi, jina la Bwana lihimidiwe mtumishi wa Mungu?

  Nionavyo mimi, ni kwamba, miongoni mwa mafundisho manyonge na yasiyokidhi ktk Kanisa haswa la Tanzania ya leo, ni pamoja na kutokufundisha kweli ya Mungu kuhusiana na Huduma na Karama za Roho Mtakatifu ndani ya Kanisa.

  Ntakuuliza swali; Je, dini ama dhehebu lako lina ukiri wa hivyo vipawa vya Mungu ambavyo tumeahidiwa na Bwn? Ninatumai ya kuwa mnavikiri, lakini, Je, ni kweli mnayatelkeleza yale yaliyoandikwa ama ni kwa baadhi ya Huduma na Karama tu?? Ntarejea tena.

  Mungu akubariki.

  OGUDA J.E.

 95. Wapendwa katika Kristo Yesu.

  Nachukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kutulinda Mwaka mzima wa 2011 na tunaumaliza kwa ushindi hivyo jina la Bwana Yesu litukuzwe.

  Pili nimefurahi kuona hii mada nzuri na hasa ilipoambatanishwa na Picha za matukio ya mafuriko hapa DSM hasa maeneo ya mabondeni. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao katika janga hili na pia wale waliopoteza mali zao, madhali Mungu amewaacha hai basi watapata nyingine hata kama muda utakuwa mrefu.

  Tatu ni kuhusu swali kwamba kazi ya manabii ni nini?? Naomba nisijibu swali hilo ila niseme hivi, mwanadamu amepewa akili ya kujua mema na mabaya, na uchaguzi ni wake hivyo katika hili huhitaji mtumishi wa Mungu unahitaji kutumia Common sense!! Nasikitika kusema kuwa ndugu zetu hasa wale waliokuwa pale jangwani waliwahi kufukuzwa, nyumba zao zikabomolewa kwa FFU na wakarudi pale wenyewe NA KUJENGA NYUMBA ZA KISASA kwa nguvu zao na ukaidi wao. Sasa ndugu zangu tunahitaji NABII HAPA???????

  Haya, Idara ya Hali ya Hewa (TMA) (hawa sio manabii ni watabiri wa hali ya hewa)waliwaambia kwamba waondoke kwani itanyesha mvua kubwa wao wakasema (nasikitika kunukuu ” Maji yanakimbia watu” mwisho wa kunukuu!! Sasa ndugu zangu ni wapi tunamwitaji Nabii???

  Wapendwa wakati watu hawa walipoenda kununua maeneo yale hawakuona hata kama hawakuona si kila mwaka kunakuwa na mafuriko?? Kwanini wao wasishtuke na kuondoka?? Sasa nawaambia hata Mheshimiwa Rais kasema serikali inaandaa mpango wa kuwaondoa wote pale kwa nguvu, nina wasiwasi hata wengine hawataondoka watamngojea NABII!!!

  Mungu awabariki, Nawatakia Krismasi Njema, msherekee kwa Amani na Furaha Kuu.

 96. Praise Jesus,
  Mi nadhani katika hili,hamna haja ya kuzungukazunguka sana,manabii watuambie,hili limeathiri wengi hata ambao hawajajenga kwenye mabonde,nabii kama nabii wito huo unajulikana kabisa.

 97. Asante kwa maelezo,Sasa kama tunaishi katika kipindi cha “Karama za Kinabii” zinatendaje kazi karama hizi? Zinahitaji manabii kama hawa waliochipuka kama uyoga leo? Hebu tusaidie kuhusu Karama hizi katika kipindi cha Agano jipya? Au Kipindi cha Kanisa?

 98. kazi za manabii katika agano la kale ni tofauti na kazi za manabii katika agano jipya nabii wa mwisho katika orodha ya manabii wa agano la kale ni Yohana mbatizaji ndio maana utendaje wake ni tofauti na manabii katika kipindi hiki chetu
  katika agano la kale manabii walileta ujumbe kwa Taifa la Israeli tu ila ilipolazimu Mungu aliwatuma nje ya taifa mfano Yona, pia manabii wa agano la kale walihusika kuwasimika wafalme

  zipo kazi nyingi ila kwa agano la kale tunaishi katika kipindi cha karama za kinabii kwani unabii wote unatakiwa ubalance katika maneno ya biblia, kipindi hiki nabii analeta ujumbe katika kusanyiko la mahali pamoja na sio taifa wala serikali za kibinadamu, hivyo Mungu anasema na kusanyiko lake ila baadhi ya matukio katika dunia ni matokeo ya wanadamu kutofuata kanuni za asili ambazo Mungu alishaziweka tangu mwanzo

  Kwani haihitajiki Roho Mtakatifu ili mtu kujua kuwa kujenga katika njia ya maji kuna madhara, kwani Mungu alikwisha mpa mwanadamu akili na utashi wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

  nitaannda somo hili vizuri na kulileta kwenu

  pastor thobiasi tag mponda

 99. Swali rahisi saaana na gumu saaana.

  Sina uhakika kama ni kwanini hawajatoa taarifa na tahadhari, ila nina swali je ni kila jambo wakiambiwa wanasemaga au huwa wanaambiwa waseme? Labda wenye ufahamu juu ya utendaji wa “ofisi hii ya kinabii” watujulishe.
  May be yawezekana ni “fimbo” but who can say so unless a prophet unveil this-Amos3:7.

  Sijajua kama mtu akiitwa mchungaji, mtume, mwinjilisi au nabii inabadilisha kile alichonacho. Je vyeo hivi hutolewa na sisi tunaowaita?

  Mlioko Tanzania penye janga hili twawapenda, tunawaombea. Mungu awape kupona na kushinda yote yanayowakumba.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s