Christina Shusho kufanya maombi ya nguvu kabla ya uzinduzi wake!

Christina Shusho anataraji kufanya uzinduzi wa album yake ya NIPE MACHO leo tarehe 23 Desemba kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, na baada ya siku tatu tarehe 26 Desemba, kuendeleza Leaders Club.

Mwimbaji huyo anasema tamasha hilo ni maalumu kwa ajili ya kumshukuru Mungu katika fani ya muziki wa Injili Tanzania, pia amewashirikisha waimbaji wengi ambao kwa pamoja watakuwa na jambo la kumshukuru Mungu “Naamini kila mmoja wetu ana neno la kusema ahsante, Inawezekana katika miaka 50 hukufanikiwa kupata kile ulichokitaka lakini kuwa hai na kuwa na amani, ni jambo kubwa sana  la kumshukuru Mungu” anasema.

Akiongea zaidi anasema “Diamond Jubilee kutakuwa na maombi ya nguvu kabla ya  uzinduzi utakaoanza saa 12 jioni mpaka saa 6 za usiku kwa kiingilio cha shilingi 20,000 ambacho kitajumuisha na gharama za chakula, na Desemba 26, pale Leaders kiingilio kitakuwa ni Sh. 5,000 kwa wakubwa na Sh. 2,000 kwa watoto” alisema Shusho.

Waimbaji watakaosindikiza uzinduzi huo ni pamoja na Upendo Nkone, Bahati Bukuku, Rose Muhando, Solomon Mukubwa, Bonny Mwaitege, Jenifer Mgendi, Upendo Kilahiro, Pastor Safari na wengine wengi.

Wana Wanamuziki wa nje ni pamoja na Reuben Kagame kutoka Kenya na Mushabo kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matamasha yote hayo yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa serikali, viongozi wa dini na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi

Advertisements

7 thoughts on “Christina Shusho kufanya maombi ya nguvu kabla ya uzinduzi wake!

  1. Christina Mungu akutie nguvu, kwa kwa kipaji ulichopewa na Mungu cha uimbaji kwa mimi napenda sana kwaya. Mungu akubariki sana.

  2. Hakika unaimba vizuri na una kipaji cha kuimba, Ninaposikia nyimbo zako huwa nafarijika sana. Mungu akubariki sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  3. Napenda nyimbo za Shusho zisivyo na makeke pia amepewa na Mungu sauti ya tofauti na waimbaji wengine wengi wanaweza kuigana sauti zao ila si sauti ya Shusho kuiiga ni ngumu kidogo,endelea kujizamisha ktk nguvu za Roho Mtakatifu dadaa ili upate unyenyekevu zaidi.

  4. oh!! Mama bwana akupiganie shusho mana thamani ya wokovu wako anajua Mungu. Nakupogeza kwa album yako ni nyimbo nzuri nakuombea maisha marefu

  5. haleluya!tunatofautia hali za kimaisha jamani wapendwa,…..tunalikumbuka na hilo?

  6. praise the Lord Jesus! mimi naona kwa dizaini hii uimbaji UMEKUWA SI KWA AJILI YA KUMSIFU MUNGU bali ni BIASHARA KUBWA TU.kwa nini gharama kubwa kiasi hicho! bora wangefanya mchana kweupe hata maskini wapate sikia.hebu jiulize hivi yule anayefagia barabara Kariakoo na yule anayekaa kando akiomba kitu anaweza kuenda kuingia ukumbini? jamani acheni hujuma kwenye Neno! ila hongera Shusho kwa kuimba vizuri ila ungefanya bure ningekupa big up! ahsante.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s