Kuachana vs Talaka

Katika ndoa ya Kikristo hakuna talaka. Lakini wako watu waliofunga ndoa za kikristo kisha KUACHANA na pengine kufikia wakati mke kuolewa tena au mume kuoa mke mwingine.

Kwa kuwa hawakutengana kwa TALAKA: Je, watu hao wanaweza kuendelea kuitwa ni wanandoa?

Advertisements

33 thoughts on “Kuachana vs Talaka

 1. NDOA NI YA WATU WANGAPI? Mume mmoja, mke mmoja ( MATHAYO 19:4-5; 1 WAKORINTHO 7:2 ; WAEFESO 5:25-28 ). Popote Biblia ikisema “ mume” inafuata “mke”.Ikisema “waume” inafuata
  “wake”. Mtu wa kwanza kuoa wake zaidi ya
  mmoja alikuwa Lameki ambaye pia alikuwa
  muuaji ( MWANZO 4:19,23-24 ). Wote waliofuata tabia yake waliangamizwa kwa
  gharika na walioingia safinani walikuwa
  waume wanne, wake wanne kila mmoja na
  mkewe mmoja tu ( MWANZO 7:13 ). Huu ndio mpango wa Mungu tangu mwanzo.
  Yeyote aliye na mke zaidi ya mmoja au
  mume zaidi ya mmoja ataangamizwa.
  Inampasa kufanya malipizo ya ndoa na
  kubaki na yule wa kwanza tu.

 2. NINI MAANA YA NDOA? Kwa kukosa ufahamu, wako watu
  wanadhani ndoa harali ni pale mwanaume
  anapovaa suti na mwanamke kuvaa shera
  na Padre au Mchungaji akawafungisha ndoa
  hiyo. Wengine wamedhani kwamba ndoa
  zinazofungwa kwa Kamishna wa Wilaya au Bomani siyo ndoa harali. Wengine
  wamedhani kwamba ili iitwe ndoa, ni lazima
  kiwepo cheti cha ndoa. Wengine
  wamedhani kwamba ndoa zinazofungwa
  na Mashehe wa Kiislamu siyo ndoa.
  Wengine wamedhani kuwa ndoa zinazofungwa na Wahindu, Wabudha,
  Mashahidi wa Yehova n.k, siyo ndoa harali.
  Wengine wanadhani ndoa harali ni zile
  zinazofungwa Roman Catholic, Lutheran
  Church, Anglikana, Assemblies of God,
  Pentecoste au A.I.C n.k. Wengine wanadhani ndoa za kimila siyo ndoa. Tushike lipi basi?
  Inatubidi tuangalie Biblia! Kwa watu ambao
  hawajaokoka, yafuatayo yakitimia, hiyo ni
  ndoa tayari mbele za Mungu:- 1. Mume na mke wawe wote
  hawajawahi kuoa au kuolewa, au
  mmoja wapo au wote wamefiwa na
  mke au mume aliye harali ( 1 WAKORINTHO 7:8-9, 38-39; WARUMI 7:2-3 ). 2. Ruhusa ya mwanamke kwa kuwa
  radhi kuolewa na mume huyo ( MWANZO 24:57-58 ). 3. Mume lazima apate ruhusa ya wazazi
  wa mwanamke katika vikao vya
  majadiliano ya mahali. Ikiwa wazazi
  wa mwanamke wataruhusu waishi
  pamoja na mahali ifuate baadaye au
  vinginevyo, la msingi ni ruhusa ya mzazi ( MWANZO 34:8, 11-12; 1 WAKORINTHO 7:36 ). 4. Mume na mwanamke baada ya ruhusa
  ya wazazi wa mwanamke,
  wakiwaacha wazazi na kuambatana
  pamoja na kuishi pamoja na
  kutambulika hivyo katika jamii, basi
  hao wamekuwa si wawili tena, bali mmoja na hawawezi kutenganishwa,
  wameunganishwa na Mungu ( MATAHYO 19:5-6 ). Sala zozote au Baraka wanazofanyiwa baada ya
  hapo na watu ambao hawajaokoka,
  wawe na majina ya Mapadri,
  Wachungaji, Maaskofu, Mashehe,
  Wazee wa kimira, Msajiri wa ndoa wa
  Bomani n.k.haziongezi wala kupunguza chochote biblia inasema
  wazi kwamba sala yoyote ya mtu
  ambaye hajaokoka ni chukizo mbele
  za Mungu wala haisikiwi.sala ya jinsi
  hii haiongezi chochote mbele za
  Mungu (MITHALI 15:19; 28:9.YOHANA 9:31) Mungu haihesabu kuwa ni ndoa kwa sababu ya cheti cha ndoa au
  kufungwa kwa ndoa hiyo na”
  kubarikiwa ”na mtu ambaye sala yake
  ni chukizo Mungu anahesabu kuwa ni
  ndoa baada ya vipengele hivyo vinne

 3. TALAKA KATIKA UKRISTO . Hakuna kabisa talaka katika Ukristo. Mungu
  anachukia kuachana. Ni mume mmoja, mke
  mmoja hadi kifo kiwatenganishe ( MALAKI 2:13-16 ; 1 WAKORINTHO 7:39; WARUMI 7:2-3 ; LUKA 16:18 ). 1. VISINGIZIO VYA WATU KUACHANA. ( a ). Kwa sababu ya uasherati ( MATHAYO 19:9 ). Uasherati unafanywa kati ya msichana na mvulana siyo kwa yeyote
  aliyekwisha kuoa au kuolewa. Huyu
  anafanya uzinzi ( LUKA 16:18 ). Nyakati za Biblia, mtu akitoa posa kwa mchumba wake
  hata kabla ya kuoana waliitwa mtu na
  mkewe. Katika uchumba huu, ikithibitishwa
  kwamba msichana amefanya uasherati kwa
  mfano kuwa na mamba, mwanaume hapo
  anakuwa huru kumuacha maana amekuwa dhahiri kuwa dada huyo hakuwa
  mwaminifu, hajaokoka. Hata leo ndivyo
  inavyopasa kuwa ( MATAHYO 1;18-20; KUMBUKUMBU LA TORATI 20:23-24 ). ( b ). Kwa kuwa mwenzi ambaye hajaokoka ameondoka, mtu hafungiki ( 1 WAKORINTHO 7:12-15 ). Kinachosomwa katika mistari hii ni kwamba Mungu
  ametuita katika AMANI. Yeye ambaye
  hajaokoka akisema hataki kuishi na ambaye
  ameokoka na kukazania kwamba aondoke,
  mwache aondoke, usimfunge kamba na
  kumuweka stoo! Baada ya kumuacha hutafungika kanisani kwa maana kwamba
  hutatengwa kwa kuonekana kuwa ni mzinzi ( 1WAKORINTHO 5:9-11 ). Tutaomba na atatapikwa kama Yona. Mtu akitengana na
  mkewe anapaswa kukaa bila kuoa au
  kuolewa tena au wapatane ( 1 WAKORINTHO 7:10-11 ). Mmeo aliyekuacha hata kwa talaka potea, mtarudiana kwa
  maombi na unapaswa kukaa hivyo bila
  kuolewa.

 4. Kwa ufahamu wangu nilionao wa Neno la Mungu pale mtu akishaoa au kuolewa hakuna kuachana kamwe kwa sababu yeyote ile wala hakuna mahali popote katika maandiko panapoonyesha uhalali wa mume au mke kumwacha mwenzake kwa sababu yeyote ile! Wasomaji wengi wa Biblia wanajipa uhalali wa kuacha wenzi kwa mstari huu katika mathayo 19:9 unaosema mtu asimwache mke wake isipokuwa kwa habari ya uasherati.Hapa kuna jambo moja ambalo nadhani wengi hawafahamu kwamba neno mke limetumika kwa maana mbili….kwanza mwanamke yeyote akishaposwa na mumewe hata kabla hawajaoana yaani katika uchumba huyo aliitwa mke pia……wife in progress, huyu hapa sasa ilipoonekana kuwa kafanya uasherati biblia inaeleza wazi kabisa kuwa ulikuwa unaruhusiwa kumwacha soma katika torati utaona na yule aliyefanya naye uasherati mtu aliyeposwa tayari alilazimishwa kuoa isipokuwa kama mumewe ataridhia kuwa naye.Angalia katika mathayo sura ya 1 na 2 utaona Yusufu anaambiwa na Malaika kuwa asimuache mariamu MKEWE! JE HAPA WALIKUWA MUME NA MKE? Walikuwa ktk uchumba tu! ILA MTU AKIOA HAKUNA NAMNA YEYOTE YA KUMWACHA MKEO! Kwa hiyo mstari wa Mathayo19:9 NENO MKE linalotajwa hapo linamaanisha Mchumba na Sio mke wa ndoa!
  ANGALIZO: Shetani ametumia sana mstari huo kuvunja ndoa nyingi sana za watu hasa watu wasiopenda kufanya bidii kujifunza na kumshirikisha Roho mtakatifu katika kujua ukweli wa mambo na katika kujua tafsiri sahii ya Neno la Mungu na tukumbuke wapendwa kueleza jambo usilolijua na kupotosha wengi ni kutafuta hukumu ni Bora kukaa kimya kuliko kueleza tusiyoyajua kwa kina Mungu atusaidie sana!

 5. nashukuru kwa maandiko yenu, kwa ufupi mie ni mmoja wapo wa tatizo hilo. nimeolewa miaka saba sasa na ninawatoto watatu,baada ya mwaka nagundua mume wangu anamahusiano na mwanamke. nikamsamehe maisha yakaendelea, lakini hakuonyesha kubadilika, pamoja na kuweka password kwenye sm yake nisijuie anafanya nini.

  mwaka 2009 nikagundua mabaya zaidi , na ni badaa ya kumuambia tuachane kwa sababu haniamini na anaficha mambo yake. kwa hiyo akanipa password. ndio hapo nikagundua machafu ya mume wangu. amezaa na mwanamke aliyekuwa ex girlfriend wake mtt umri sawa na mtt wangu mdogo. na bado alikuwa na mahusiano na wanawake wengine wote niligundua na nikamuuliza. mwanzoni alikataa, lkn rafiki zake wakamsihi akiri kosa. ndio hapo akanieleza kila kitu kuhusu huyo aliyezaa naye na hao wengine. kwakweli maumivu niliyoyapata mungu anayajua na nishahidi. pamoja na matatizo mengine km kuniweka namba 3, familia yake kwanza,. kudharauriwa mbele ya familia yake na mambo mengine mengi, km matumizi ya pesa, ni juu yake na hataki uulize, anaweza kuamua kitu bila hata kukushirikisha, nikavumilia kwa kuwa mie ni mkristu na ninamuamini mungu. tatizo ni huyo mtu aliyezaa naye inaonekana hawezi kumuacha, mie niko nje ya nchi nasoma, lkn unaona kabisa mwenzagu hana upendo nami, kwa sababu pamoja na dunia yetu ya utandawazi ,mawasiliano ni shida, mawasilino yanakuwepo akiwa anakulaumu kwa kosa lolote. kwa kweli upendo sina tena kwa mume wangu hasa kwa yale anayoyafanya, na ninatamani kumueleza tutengane kwa muda, ila ndugu zangu wanasema nisubiri hadi nimalize masomo.

  nimeshafikiria sana kuachana naye tangu mwanzo nilipogundua tabia yake , kwa kweli sikumjua kabla ya hapo, kwa kuwa tuilikutana na ndani ya wiki mbili akaamua kunichumbia, na baada ya mwaka tukafunga ndoa. katika uchumba tulikuwa tunaishi mbali kwa kuwa nilikuwa nasoma , nae anasoma.

  kwa tatizo kama langu je naruhusiwa kuachana na mume wangu? kwa kuwa mie kuishi kwenye ndoa ni kwa ajili ya upendo, naona kama heshima, uaminifu, na upendo hakuna, bora kuachana na mume wangu.

  bahati nzuri mie ni mwanamke mzuri na ninajua wanaume watanisumbua sana na nisingependa kuishi mwenyewe maisha yangu yote kwa kuwa najua dhambi ya kuzini itanisumbua.niko njia panda kwakweli kuishi naye tena nikifikiria roho inaniuma, kwa kuwa hata kuja kusoma huku mbali niliamua hivyo nipate muda wa kufikiria maisha yangu na kuomba mungu anisaidie nirudishe upendo tena kwa mume wangu. matokeo yake naona mungu anazidi kunidhihilishia kuwa hajabadilika hasa kwa yeye kutojali najisikiaje kwa kuwa huku niko mpweke sina hata watoto huku ambao wangenipa faraja.kwa hiyo nilitegemea angenipa faraja ya kutosha kama mke. kila siku yuko bize hadi weekend. ukimueleza anabadilika wiki 1, hizo nyingine hajali.

  naumia sana kwa kuwa najua nahitaji mume mzuri zaidi yake yeye na ndio sala yangu kwa mungu. nimekuwa mwaminifu kwake na kwa mungu. ila sasa naona nimechoka na maisha ya kulia kila siku..

  ninashindwa kushirikisha wazazi kwa sababu, akifanya kosa, na ukijua mambo yake, na kama kukitokea ugomvi, yeye ndio anakuwa wa kwanza kwenda kushtaki kwa wazazi wake. mie nina mama tu. wakija kwenye kesi ambayo mtuhumiwa ni mimi sasa, kila mtu ananiona ninamakosa, na hata ukijaribu kuwaeleza chanzo cha ugomvi ni tabia ya uzinifu ya mume wangu, hakuna anayenisikiliza. kwa hiyo sina support upande wa ndugu zake hasa ukizingatia nao hawanipendi na wananidharau kwa yale ambayo ndugu yao ananifanyia mbele yao na zaidi yeye ndiye mkubwa katika familia na ndie anayesomesha, chakula, bili na kila kitu kwake. alishanieleza wazi atanifukuza nyumbani niondoke kwa ajili ya ndugu zake tena mbele yao, kwa maneno ya kuambiwa na yasiyo na ukweli ila kwa kuwa mie ni namba 3 anachagua kuamini ndugu zake. niliumia sita kaa nisahau.

  nilshaenda kwa mchungaji, na mchungaji wa kanisa la mkoa namaanisha dayosisi, mchungaji akamtafuta sana .lakini hakwenda na hakujali wakati mwingine hata akiona sm ya mchungaji hapokei. mie nikaamua tu kuyaacha yote na kutumaini kuwa atabadilika.

  hayo ni machache tu nikielezea hapa itakuwa nistory ndefu.

  naomba mchango wa mawazo. nitashukuru hasa nataka kujua km uamuzi wa mimi kuachana na mume wangu na kuolewa tena baadae nitakuwa nafanya makosa. nampenda sana Mungu na ninamuamini sana.

 6. Mpendwa Kinyau Haggai,

  Nimeiona tafakari yako unayotuitia, hilo ni jambo jema na la kutia moyo!
  Katika kuyatafakari hayo uliyoyaleta, kuna mambo mengine mengi kati ya hayo ambayo wachangiaji wameyatolea maelezo, labda upatapo wasaa waweza kuipitia michango hiyo ili kupata chochote kinachoweza kukusaidia katika mwendo huu tuliomo.

  Kuhusu kuitimiliza Torati. Kuitimiliza ni sawa na ‘to magnify’, yaani kuna vipengele vingine vya sheria ambavyo vilihitaji jicho la kiroho ili kuweza kuviona. Hayo macho ya kiroho ndiyo wanayopewa Kanisa, basi, kwa mfano, unapoitazama sheria inayohusu uzinzi, utaona kuwa mashiko yake yalikuwa zaidi kimwili kuliko kiroho. Yaani ili uwe na kosa la uzinzi, ili lazimu uwe umekamatwa katika tendo hilo. Lakini katika ujio wa Kristo, sasa jicho linayoitazamia hiyo sheria ni la kiroho, ambapo sasa, kuna yale mambo ya rohoni ambayo mwili ulikuwa hauyajui, sasa yamewekwa wazi. Ndio tunaona Kristo akifunua pazia kuhusu hilo na kusema, atakaye muangalia mwanamke kwa kumtamani, atakuwa amekwisha kuzini naye, na mambo mengine kama ulivyoyaorodhesha, yote sasa wigo wake ukiwa umepanukia katika anga za kiroho. Basi Torati waliyokuwa nayo, wao waliitimiza kwa sehemu tu, ya kimwili, na sehemu iliyobaki ya kiroho, ndiyo hiyo inayowekwa wazi kwao walioipokea Injili. Kwa hiyokuanzia hapo sasa Torati ni kamili.

  Haki ya mafarisayo ilikuwa katika mambo ya mwilini, haki yetu ni kuu kuliko hiyo kwani sisi sasa ni wa rohoni, hivyo upeo wetu wa kuitimiza Haki ni mkubwa kama unavyouona katika mambo hayo ya talaka na mengineyo yalivyo kamilishwa.
  Andiko ulilolinukuu kutoka Malaki, linasimama hivyo likijitegemea kulingana na hali iliyokuwepo katika wakati huo, na hivyo limetolewa na Mungu ili kuwaonya kuhusu jambo hilo. Wao walikuwa wakiwaacha wake zao kwa sababu yoyote ile iliyo wakinaisha kuhusu wake zao. Tena walikuwa wanaoa wake wengi tu, kwa kadiri ya tamaa zao za mwili. Hata Kristo anapozungumzia talaka, alikuwa akiiongelea katika rejea ya mazingira hayo. Lakini katika ujio wake, Injili anayoileta, sasa ina uwezo wa kuitiisha miili yetu, tofauti na huko nyuma. Ndio maana sasa mambo yanaletwa rohoni na si mwilini tena. Torati ilikuwa imeshindwa, kushindwa huko ndiko kulikopelekea washindwe kumuadhibu yule mwanake mzinzi, kwani wote walikuwa wamepungukiwa HAKI ya kuitimiza sheria hiyo. Kwa hiyo, hilo jambo la kupungukiwa hiyo Haki, halilifanyi jambo hilo kuwa leo, unaweza kumtaliki mzinzi, labda kwa mambo ya mwilini, lakini rohoni huyo amekufa! Uzinzi ni dhambi, nazo dhambi husamehewa zinapoungamwa. Nazo dhambi zinazoungamwa na kusameheka zinafahamika, makuhani walikuwepo kwa huduma ya dhambi hizo. Lakini dhambi ya uzinzi sheria yake ilihitaji auliwe, kifo ndiyo dhabihu iliyokubalika kwa mzinzi. Nazo sheria hizo za Torati hazikuwa Haki za Binadamu bali Haki ya Mungu! Kwa hiyo unapozungumzia kuachana, au talaka, suala la uzinzi halihusiki, bali uasherati tu.

  Tendo la kujamiiana, kwa asili lina maana moja tu, kupata watoto. Ukitaka uhakika wa jambo hilo, hebu ichunguze nature. Watazame wanyama au ndege, wote hukutana katika tendo hilo katika kipindi maalumu ambacho huambatana na upatikanaji wa watoto au vifaranga. Mnyama mwenye watoto kamwe hapandwi. Ni binadamu pekee aliyeanguka na kuporomoka hata kuwa chini ya wanyama, maana kwake, tendo hilo limegeuka kuwa starehe kubwa na ya muda wote, mwaka mzima bila kukoma, bila kujali hata kama analea! Basi mwanamke anayetoka nje ya ndoa, tafsiri rahisi ya jambo hilo kiasili, ni kwamba anarudi na ujauzito, hata kama si wa kimwili, lakini kiroho anao ujauzito huo! Kwa hiyo unapozungumzia msamaha ni vizuri uwe katika ufahamu huo. Yaani ulichukulie hivi; kuwa umemfumania mkeo na mwanamume mwingine, kisha akalijutia jambo hilo, mkasuluhishwa mbele ya wazee wa kanisa, ukamsamehe. Baadaye ukajitokeza ujauzito na akajifungua mapacha wanne kutokana na ule uzinzi alioufanya, basi msamaha huo ulioutoa, unajumuisha na malezi ya watoto hao wanne ndani ya nyumba yako! Hata hao mapacha wanne, nao, hawaruhusiwi kuingia katika kusanyiko la Bwana hata kizazi cha kumi, hawaruhusiwi. Kizazi ni wastani wa miaka 40, basi kwa vizazi kumi ni sawa na miaka 400! Ndio maana Mungu aliamuru wazinzi wauliwe na uzao wa uzinzi huo usiingie katika Kusanyiko Lake kwa miaka 400. Hiyo ndiyo adhabu linayopewa kanisa lililoposwa kwa Kristo halafu likapokea mbegu nyingine na kuyalea mafundisho yaliyo kinyume na Neno lake!

  Dhambi ya uzinzi na dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ziko kama Maandiko yalivyoziweka, hazina msamaha, kwa hizo ni lazima uadhibiwe hata, adhabu hiyo ni kifo! Uasherati unasameheka, ndio maana Mungu hakumuua muasherati, bali amepewa adhabu ya kuachwa tu, yaani kuachwa huko kukiwa ni matokeo ya kuificha dhambi hiyo hadi ilipogundulika. Tena unapoamua kumpa talaka mke aliyeanguka katika uasherati huko nyuma, basi hilo hudhihirisha kuwa umefikia uamuzi wa jambo hilo baada ya kujiridhisha juu hilo na ukaamua hivyo ukiwa umeshindwa kumsamehe. Basi Mungu anakataza kumrudia tena huyo mwanamke uliyemtaliki.

  Kwa hiyo talaka ni sehemu ya Haki ya Mungu. Nalo kanisa likiwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, linapotokea jambo kama hilo, Roho Mt. huwaongoza katika kuitimiza Haki yote, huyo pia akiwa ndiye mwenye kuzichunguza siri za mioyoni mwetu. Kwa hiyo maamuzi yote, kama ni msamaha au talaka, vyote hufanywa chini ya uongozi huo.

  Ubarikiwe!

 7. Wapendwa, nimepitia michango yenu ambayo sikupata nafasi ya kuisoma kwa zaidi ya majuma mawili. Nimejifunza pande mbili za suala hili. Namshukuru Mungu sana kwa ajili yenu nyote.
  Kwa Ndugu yangu John Paul, nimejifunza kitu kizuri. Tusiwe wepesi kuona kisichokuwepo.

  Amani kwenu nyote!

 8. AMINA,Nakupenda Ndg yangu Haule,usiache kabisa kuniambia kama una la kuniambia…..Maana “KWA JINSI HII MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU,HATA AKAMTOA MWANAYE WA PEKEE,ILI KILA AMWAMINIYE ASIPOTEE, BALI AWE NA UZIMA WA MILELE!” U-milele huo tunao na tutadumu nao ,kwakuwa tulisha funikwa na tunaendelea na kufunikwa na UZURI wa BWANA – na sababu kubwa ya kufunikwa huko,nipale tunapo liamini Neno la MUNGU,chini ya mafundisho ya Roho Mtakatifu,ila kumbuka tu kuwa, mara zote, neno hilo ni “UPANGA UKATAO KUWILI” Yaani ule wa m-masai cha mtoto!(Maana ule wa m-masai unaweza kutenganisha NYAMA na MIFUPA tu,basi!). Nikushukuru sana ndg yangu.

 9. Wapendwa,

  Wakati tunaendelea kutafakari na kufundishana juu ya mada hii ya talaka au kuachana kwa wanandoa (waamini), naomba mnifafanulie Yesu alikuwa na maana gani aliposema;

  1. “Msidhani kwamba nimekuja kufuta Torati au Manabii, sikuja kuondoa BALI KUTIMIZA” [(Mathayo 5:17) (Biblia zingine zimeandika kuja KUITIMILIZA)].

  2. “Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya walimu wa Torati na Mafarisayo, KAMWE hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni” (Mathayo 5:20).

  Haki ya walimu wa Torati na Mafarisayo ilikuwa ipi na je sisi tunatakiwa tufanye haki gani inayozidi ya kwao?

  Nimeomba ufafanuzi huo kwa sababu naona hayo maneno ndio kama msingi wa Yeye (Yesu) kuanza kufundisha kuhusu HASIRA, UZINZI, TALAKA, KUAPA, KULIPIZA KISASI na mwisho UPENDO KWA ADUI. Na katika mafundisho hayo analinganisha na jinsi Torati ilivyosema katika Agano la Kale, na Yeye anachokitaka kifanyike katika Agano Jipya. Sasa huko kutimiliza Torati alikokuwa anakusema Yesu na haki anayotaka sisi tuwe nayo, ilikuwa na maana gani kuhusu talaka?

  Pia katika kulitafakari jambo hili, ninaomba tena mnisaidie au watu tuseme wazi kwamba Mungu anaruhusu talaka bila kujali mmoja wa wanandoa amefanya uzinzi na uasherati au la?

  Talaka maana yake ni kuachana regardless nani kampa mwenzake talaka hiyo au nani anaruhusiwa kumwacha mwenzake yaani mume au mke, (Kumb.24:1-4) lakini mwisho wake ni kwamba wanandoa wameachana, ndoa imevunjika! Sasa nataka tulijadili hilo (kwamba Mungu anaruhusu watu kuachana?) katika mtizamo wa neno la Mungu toka Malaki 2:13-16a, imeandikwa hivi;

  “Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhahabu ya BWANA kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu Yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu. Mnauliza; ‘Kwa nini?'(anajibu); Ni kwa sababu BWANA ni shahidi kati yako na MKE WA UJANA WAKO, KWA SABABU UMEVUNJA UAMINIFU NAYE, INGAWA YEYE NI MWENZAKO, MKE WA AGANO LAKO LA NDOA.

  Je, BWANA hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. KWA HIYO JIHADHARINI WENYEWE KATIKA ROHO ZENU, MTU ASIVUNJE UAMINIFU KWA MKE WA UJANA WAKE. ‘NINACHUKIA KUACHANA’, asema BWANA, Mungu wa Israeli…….”

  Hapa ndipo hasa nilipotaka tujikite katika kujadili na kutafakari; kama Mungu wa Israeli anachukia ‘kuachana’;

  Iweje Yesu mwenyewe aruhusu kuachana kwa sababu ya uasherati?

  Kama Ndugu John alivyosema, je kwa mke au mume mzinifu, iko wapi nafasi ya kusamehewa na mwenzi wake kama kwa sababu ya uasherati wanaruhusiwa kuachana?

  Je, dhambi ya uzinzi na uasherati haisameheki na kwa sababu hiyo ndio inakuwa sababu ya kuruhusiwa kuachana kwa wanandoa? (Ninavyojua dhambi isiyosameheka ni kumkufuru Roho Mtakatifu, lakini dhambi zingine zote zinasameheka-Luka 3:28-29, Mathayo 12:31-32, luka 12:10 n.k.)

  Je kusamehewa na kusahaulika kwa aliyezini au aliyefanya uasherati ndiko kutimilizwa kwa Torati? (Rejea Mathayo 6:12, 18:21-22, n.k.)

  Na huyo anayesamehe na kusahau, Je, huyo ndio anahesabika kuwa na haki inayozidi ile haki ya Walimu wa torati na Mafarisayo?

  Baraka kwenu nyote!

 10. Mpendwa Lwembe,uendelee kubarikiwa,maana kama kubarikiwa ulishabarikiwa tangu ZAMANI! Ndg yangu nimeelewa na pia nimejua,ila niongezee tu pia kuwa,hata katika sheria za ndoa nilishapata kuelezwa na waliobobea ktk taaluma ya ndoa na taraka,kuwa mwanamke aking’ang’ana kutoa taraka anapaswa kumlipa huyo mmewe anayetaka kumtariki! – sasa nazidi kuelewa kuwa mwenye kutoa taraka ni mwanamme. Kwako mpendwa Haule na wengine wote ambao wamenielewa kama ambavyo ndg yangu Haule alivyonielewa,kwanza nikubaliane nawe kuwa UOGA NI DHAMBI. Maana maandiko yanasema mtu mwoga hampendi MUNGU! mimi NAJUA KUWA KAULI NJEMA AU MBAYA INATEGEMEA MWENYE KUIPOKEA KAELEWAJE, na kosa hujulikana kuwa ni KOSA kwa mtendewa! – Wanafarisafa husema kuwa “ukiomba msamaha kabla hujaambiwa kuwa kile ulichofanya ni kosa,basi wewe ULIFANYA MAKUSUDI” Na kutanguliza SAMAHANI kwa kila sentesi unayoianza kuisema kuna thibitisha kuwa,kunachukuliwa kuwa mnenaji HAJIAMINI,kwa hiyo wafundishaji wa elimu ya mahusiano wasema ukienda kwenye usaili wowote hata ule wa kuomba kazi ustumie neno SAMAHANI bila kutakiwa kufanya hivyo,utaona na kusikia pia hata wabunge hambiwa au hutakiwa kuziondoa ,kuzifuta na ama kuziombea SAMAHANI kauli zao,wanapotakiwa tu kufanya hivyo – yaani mtu anapogundulishwa kosa lake ndipo anapoomba msamaha, Sasa mimi binafsi sijui kama ROHO MTAKATIFU anaweza kukugundulisha kuwa umekosea,halafu uliowakosea wakakataa kuwa hujatukosea!Nitafurahi ukinifundisha juu ya maana ya sentesi hii aliyoitumia YESU alipokuwa akiwafundisha wafuasi wake kusali, maana naye alisema msalipo salini hivi,……….”UTUSAMEHE MAKOSA YETU KAMA VILE NA SISI TUNAVYOWASMEHE WALIOTUKOSEA………”! Kaka sasa sijui kama nitakuwa namsingizia YESU nikisema kuwa yeye ndiye yule ROHO MTAKATIFU ambaye ndiyo anawaambia wanafunzi kuwa MUNGU anawasahe iwapo nanyi unawasamehe Ndg zenu,mnaowajulisha makosa yao kisha mkawasamehe. AU uungwana ni upi,kumjulisha ndg yako kosa lake,ili asijelifanya tena ama kumsamehe kimyakimya kwa vile amekuomba msamaha kwa jambo ambalo unajua wewe kuwa si kosa? sijajua pia kama Roho mtakatifu anaweza akakuambia wewe kuwa UMENIKOSEA na wakati huohuo asiniambie mimi nilyetendewa kama nimekosewa? kutumia neno samahani mara kwa mara ndiyo ishara ya unyenyekevu anaoutaka MUNGU? Je, tunapaswa kuwasamehe watu bila kujua kuwa kweli wametukosea ali mladi wameomba msamaha? au basi maana ya neno hili ni nini,…..”Ndg yako akikukosea naye akakuomba kuwa amekosa,msamehe” au mtu analejezwa wakati gani….anapoomba tu msamaha bila kujua kosa lake au ndg wanpogundua kuwa ndg yao huyo amewakosea? Binafsi sijaona kosa la ndg PAUL hata aombe msamaha,hata hivyo nia yangu ilikuwa kumtia moyo asijione mnyonge hata kushindwa kutoa maoni yake kwa kuogopa kukosea,mimi najua kuwa kukosea njia ndipo kujua njia. Naomba azidi kuelewa kuwa sisi ni ndg na kwamba hayupo mjuzi wa neno ila ROHO MTAKATIFU! WOTE TUNAFUNDISHWA NA HUYO. Kuhusu KAZI maalumu kwa ndg Lwembe CK, ni kweli anayo……hapo niseme kwa kifupi tu kwamba NDIYO anakazi maalum! kwani wewe hujui hilo? …………umekuwa mwanafunzi wa BWANA YESU KRISTO nawe hujui hilo, kuwa ndg yako huyo ameajiliwa siku nyingi? NARUDIA KUSEMA KUWA NI WEWE TU BWANA YESU UNAYEWEZA KUMKINZA SHETANI ILI BWANA LWEMBE AKESHE HATA KWA SAA MOJA TU PAMOJA NAWE ILI ILE KAZI ULIYOMPA AIKAMIRISHE, MBONA WEWE BWANA YESU ULISEMA ‘imekwisha’pale msalabani ulipokamilisha kazi uliyoiijia? Watu wanauliza kwani Lwembe anakazi gani? hivi nawewe Bwna Yesu ni kweli kuwa hujui kama Lwembe ni mtumishi katika shamba la BABA yako avune humo hata mazao yote japo ni megi na watenda kazi kama L WEMBE NI WACHACHE? Kwakuwa wewe ndiye huyohuyo mwalimu tufundishe tujue kuwa wewe unaajili watu katika shamba la BABA yako!

 11. Bwana Yesu apewe sifa

  Nami nafahamu kama Lwembe alivyofafanua,

  Lakini tukitafakari zaidi kwa mujibu wa maaandiko Wayaudi walikuwa hawana uchumba,Tunaona hata kwa Yosef anambiwa na malaika mtwae mkeo siyo mchumba pale alipotambua kuwa mjamzito pasi yeye Yoseph kumjua bado.Hata Yesu anataja Mke kwa habari ya Uasherati na wala sio mchumba.kama nilivyosema awali nafahamu uasherati ni kwa mtu asiyeoa na uzinzi ni kwa walio ktk ndoa sawasawa na bandiko la Lwembe

  Wapendwa nawaomba tulitafakari ili andiko
  “Mathayo5:32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini”.

  swali langu huu mstari unakataza mtu asimwoe huyu mwananke aliyeachwa akimwoa anazini.,na pia yule mwanamume dhambi yake ni kumfanya huyo mke kuwa mzinzi.sioni mwamume wapi anafungwa na huu mstari asioe? naomba mnifundishe hapo

  Tunaona tena maneno yote mawili yakitumika Uasherati na Uzinzi

  Tunajifunza

 12. Mabinza
  Kuomba msamaha kama umekosea sio uoga,UOGA NI DHAMBI.Kuomba msamaha kunaletwa na huzuni ya kimungu ambayo inakupelekea kutubu(Toba).
  Kitu kingine naomba kukijua mpendwa Lwembe kuna kazi maalum amekuja kuifanya!!??kiasi Bwana amkemee shetani!!!?? Mimi nadhani tuko hapa kufaidiana ktk kutafakari kama wa-Kristo,Tunafahamu kwa sehemu, CK Lwembe/John Paul wanafahamu kwa sehemu,Sisi sote tunafahamu kwa sehemu,Wakati tukiendelea kutafakari tuepuke mashindani,ubishi na vitu vinavyofanana na hivyo.
  John Paul Bwana akutie nguvu,
  Wapendwa tusijaribu kujitwalia Utukufu,Utukufu ni wa MUNGU..
  Nawatakia Amani ya Bwana.

 13. Mpendwa Mabinza,

  Shalom!

  Ninakushukuru kwa yote, pia sote tu salama katika Yeye atutiaye nguvu!

  Kwanza kabisa ningependa kusema kuwa Waisraeli hawatofautiani sana na sisi au kabila nyingine za dunia haswa katika mahusiano, yaani katika kuoa na kuolewa. Mwanamume HUOA, na mwanamke HUOLEWA. Nayo mambo ya uchumba huanzia katika familia ya mwanaume ndio wanaokwenda kuposa kikeni. Nalo jambo hili linaendana na maumbile kama Maandiko yanavyo tufunza, kuwa mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume. Basi maumbile hayo ndiyo yanayoifanya Talaka itolewe na mwanaume na si mwanamke. Labda katika mambo ya kiserikali na haya ya Haki za Binadamu, ndio tunaona wanawake wakiwataliki waume zao!

  Pia ukiziangalia rejea zote za Biblia zinazohusu Talaka, humhusisha mwanaume kumtaliki mke, mwanamke ndiye huolewa na kuachwa. Kum. 24:1 “Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake na kumtoa katika nyumba yake”, hii ndiyo tafsiri ya talaka, hii ndiyo anayoirejea Kristo katika Mt 5:31. Kwa hiyo kwa kifupi Talaka hutolewa na mwanaume kama Maandiko yanavyo tudhihirishia.

  Lakini katika mazingira mengine mwanamke huweza kuamua kuondoka na kumuacha mumewe labda akiwa ameshindwa kuzivumilia hali fulani. Hivyo huweza kuondoka na kurudi nyumbani kwao au kokote kule. Labda mume akimfuata ili arudi naye mwanamke akakataa katu katu, mume huweza kulazimika kumpa talaka mwanamke huyo ili aendelee na hamsini zake. Kuondoka huku ndiko anako kurejea Mtume Paulo anaposema mke asimwache mumewe, akiwatoa kutoka katika utaratibu huu wa zamani na kuwaingiza katika utaratibu mpya katika Kristo ambao mwanamke wa jinsi hiyo hapewi talaka tena, bali akae asiolewe au angojee kupatanishwa na mumewe. Kwa hiyo katika utaratibu huu mpya, hakuna tena ‘kuachana kwenye mataa!’

  Basi mambo hayo yanawezekana kwa hawa walioingia katika huu utaratibu mpya. Maana katika huo, Upendo wa Kristo unawafunga pamoja hata akikosekana mmoja kati yao, basi kusanyiko zima huingia katika huzuni, nayo maombi ya watakatifu huishinda ile nguvu ya utengano na kuwarejesha pamoja katika ile Furaha ya Bwana. Hawa ni WAAMINIO.

  Kwa WASIOAMINI, Talaka haiwahusu wala utaratibu huu mpya katika Kristo hauwahusu pia. Basi akiwepo wa jinsi hii aliyeolewa na au kuoa mwaminio, naye kwa sababu hiyo akaona hawezi kuendelea, Biblia inasema: 1Kor 7:15 “Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki.” ASIYEAMINI ANAONDOKA tu!

  Unajua wakati mwingine sisi hulazimisha mambo hata kufikia kujiaminisha kuwa mwenzi wangu ameamini Injili. Lakini mbele ya safari uigizaji huweza kumshinda na hivyo kurudia kutokuamini kwake, nalo jambo hilo hutuletea shida kubwa. Basi kulijibu swali lako kadiri Maandiko yanavyo tufunza; iwapo hali itakuwa hivyo basi huyo asiyeaamini ATAONDOKA!!!

  Umeelewa Ndg Mabinza? NENO linasema huyo asiyeamini ATAONDOKA, akiwa mwanaume ATAONDOKA, na akiwa mwanamke pia ATAONDOKA, ilimradi ni asiyeamini basi kwa nguvu na mamlaka ya Neno, ATAONDOKA! Huo ndio muujiza wenyewe!!!

  Ubarikiwe

 14. Ndugu Mabinza,

  Nashukuru sana kwa kunitia moyo kuwa nisiwe mwoga! Imeniongezea ujasiri. Lakini kwa “kosa” la kusoma vibaya nililolifanya hilo lilisababisha niandike yale ambayo niliposoma vizuri maandiko hayo kumbe SIKUPASWA KUANDIKA. Ilikuwa ni kwa sababu nilikosea kusoma. Sikuwa nimeandika yale ninayoyajua bali niliandika yale nililoyajua kutokana na kusoma vibaya maandiko. Ni kosa la kusoma vibaya. Ndiyo maana nikayabatilisha kwa kuwa nilicho nacho moyoni siyo hicho. Natumaini umenielewa, mpendwa!

  Asante sana na tuendelee kujifunza!

 15. Asante kaka Lwembe,nathubutu kusema ‘BW. YESU AENDELEE KUMKEMEA SHETANI ILI ASIFANYE LOLOTE HADI UMALIZE KAZI!’ Ndg yangu John paul,Usiwe “MWOGA” Unapojadili jambo. sasa utajifunzaje iwapo unaogopa “kukosea?” wewe ungejua wala usingeomba msamaha, maana yale unayoyasema ndiyo uyajuayo hivyo ndiyo mjadala unakolea sasa. kwa sababu hapo ndipo unafanya ROHO afafanue hoja ili tuelewe wengi,mimi pia sijui nakutegemea wewe useme ili nasi tujifunze.Kaka, nakutegemea sana! Naomba niongezee kidogo katika maelezo na ufafanuzi aliotoa Ndg yangu CK, Kuhusu Ndoa na Taraka,ukisoma vizuri maelezo ya Yesu ktk Mathayo 5:27-28, utaona wazi mzinifu “hatarikiwi” yeye nikifo cha kupigwa mawe- hilo sina tatizo nalo,pengine tatizo lipo kwa paulo ktk kitabu chake cha wakor. wa kwanza 7 kuanzia mstali wa 3 hadi ule wa 20 au zaidi,kuna neno “ASIYEAMINI” Mbona hapo mnapaacha wakubwa wangu? mbona mimi naona sababu zipo mbili za kutoa taraka harali? yaani kwa mtu aliyefanya uasherati na kwa mtu asiye Amini? (akipenda) nijuavyo mimi maana ya Dhambi ni KUTOAMINI, yaani kutoamini Neno la MUNGU,sasa, kama uasherati ni kosa la taraka je, kutoamini ni kosa linalostahili Adhabu gani? iwapo uzinzi ni Dhambi na adhabu yake ni kifo je, inapotokea mke au mme haamini tena lile neno la MUNGU itakuwaje? Naomba kufahamu tafadhali.

 16. Ndugu C K Lwembe,

  Nashukuru sana kwa kunisahihisha, jambo ambalo nimeliona kabisa kuwa nilifanya makosa makubwa!

  Naomba radhi kwa kila mtu ambaye tayari alikuwa amesoma maoni yangu hayo. Lilikuwa ni kosa la kusoma halafu likapelekea niyaelewe tofati yale maandiko.

  Kwa maneno haya ninafuta, au ninabatilisha maoni yangu ya tarehe 15, Jan 2012, saa 1:29 pm. Na ninawaachia waliokuwa wanaendelea na mjadala huu waendelee tu hapo walipofikia ambapo ndugu Orbi alisema akipata muda atajadili 1Kor 7:10.

  Samahani sana kwa usumbufu uliojitokeza!

  Nawapenda wooooote!

 17. Ndugu yangu John Paul,

  Naona tumekutana tena! Ndugu wanapokutana, ni jambo la kumshukuru Mungu!

  Kwanza napenda tuwekane sawa katika jambo moja ambalo binafsi naona ni la msingi sana; kwamba yatupasa kufika katika kiwango cha kufamu kuwa Biblia ni Neno La Mungu. Yaani hakuna Neno la Mwanadamu humo licha ya kadiri tuisomavyo tunawaona wanadamu wakiongea. Kama inavyojishuhudia kuwa Maandiko yote yamevuviwa na Roho Mtakatifu, basi udhaifu wowote unaouona au kuukisia lazima uwe umejifunua katika Maandiko hayo hayo, na si kuuunganisha kutoka hisia zetu.

  Basi ndugu yangu nilitaka kukukumbusha tu kuwa hicho kifungu ulichokinukuu cha 1Kor 7:10, ulipokifafanua, umekigeuza katika maana hata kinaonekana kana kwamba Mtume Paulo alijisemea tu mambo yake, jambo ambalo si kweli! Nadhani ukikichukulia kama mtume Paulo alivyokileta, hizo fafanuzi tano ulizozitoa zitaondoka, maana mt. Paulo anasema Bwana ndiye anayeagiza, “…WALA HAPA SI MIMI, ILA BWANA;…” basi udhaifu uliousema utakuwa si wa mt. Paulo ila wa Bwana au Roho Mtakatifu aliyeyavuvia hayo tunayo yaweka katika kipimo leo hii!

  Nilikuwa najaribu tu kuonesha kuwa tunapolitilia shaka Neno la Mungu, ni kiasi gani inaweza kutuathiri huko mbele ya safari, au katika huo mwendo tunaoukaza kuikimbilia hiyo Taji!!!

  Bwana na atukumbatie katika mapenzi yake!

 18. Nimekuwa nikifuatilia mada hii nami nimeona nichagie, japo kwa ufupi.Kuchangia kwangu ku katika maandiko yafuatayo, kama yalivyonukuliwa na ndg Orbi:

  “1Wakorinto 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana NAWAAGIZA; wala hapa si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini , ikiwa ameachana naye , na akae ASIOLEWE, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”.

  Nafafanua hivi:

  1.Mtume Paulo “anaagiza” na
  2.Anafahamu kua “agizo” lake si sheria na ni dhaifu
  3.Kwa kuwa si sheria linaweza kubatilika kwa watu “kuachana”
  4.Haelezi sababu ya “kuachana” huko
  5. Anaagiza hao waliaochana kuto -“kuoa” au “kuolewa”

  Kwa hiyo:

  Mtume Paulo anaelewa kuwa wanandoa wanaweza kuachana “kwa sababu ya uasherati” na ndiyo sababu inayomfanya mwanandoa awe huru (Kwa kadri ya Maneno ya Yesu). Kwa hiyo hapa Mtume Paulo anaelewa kuwa walioachana kwa zababu ya “uasherati” yule aliyeachwa yuko huru, kuoa. Kwa hiyo anaposema “wasiachane” anamaanisha “wasiachane kama sababu siyo uasherati”. Hivyo wakiachana kwa sababu ambayo SIYO uasherati inabidi wasijiingize katika katika mahusiano mengine. Na badala yake ni bora kusahemeana na kurudiana.

  Bwana Yesu alisema kuwa kwa sababu ya uasherati ndoa inaweza kuvunjika na yule aliyeheshimu ndoa yuko huru (huru kuoa/kuolewa). Lakini Hili Nalo haliondoi nguvu ya msahama, kwamba: kama mtu kamfumania mwenzi wake bado naye anaweza kumsamehe na maisha yakaendelea. Lakini aliyeshindwa kusamehe “hafungukiki” na kosa la kutokusamehe kwa kuwa kosa la aliyetoka nje ya ndoa linamfungua huyo.

  Hivyo ndivyo nilivyoelewa mimi.

  Yawezekana ninakosea pia kuandika hivyo lakini ni bora nikosee ili nisahihishwe!

 19. Mwenda,

  Ndugu yangu Mwenda, mimi siikatai tafsri hii hiyo ya Maandiko………Lakini kwangu mimi naona kama unalazimisha Maandiko yaseme yasichotakiwa kusema……angalia nukuu zako hizi……

  .Paulo anayanukuu katika Mathayo hiyo hiyo 5:32 kwamba kwa waliooana ni mwiko kuachana kwa sababu yoyote ile. Ndivyo Mtume Paulo alivyomwelewa Yesu, na pia ndivyo alivyomaanisha Yesu Kristo.”

  Je ni kweli Paulo anasema “Waliioana ni Mwiko” kuachana kwa sababu yoyote ile?

  Paulo uliyemnukuu mwenyewe hasemi hivyo! Angalia …..kwa kutumia nukuu yako……

  “1Wakorinto 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana NAWAAGIZA; wala hapa si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mkewe; lakini , ikiwa ameachana naye , na akae ASIOLEWE, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”.

  Hebu soma taratibu…..” LAKINI IKIWA AMEACHANA NAYE”………..(Paulo anakubali kuachana)

  Na Yesu alisema “ISIPOKUWA KWA SABABU YA UASHERATI”……..(Yesu anakubali kuachana……kwa sababu ya Uasharati)

  Nadhani mahali ambapo inabidi tupate jibu…..Je baada ya Kuachana unaweza kuoelewa? au Kuoa? Na kuachana huko kunatakiwa kuwe kwa sababu ya Uashareati

  Labda nikipata muda tutajadili zaidi 1KOR 7:10 ambayo naona unaikubali nusu yake tu!

  UBARIKIWE!

 20. Ndg Bernard Mwenda,

  Jina la Bwana lipewe sifa!

  Nami pia kama wewe, nimevutiwa na mada hii, kwani inayagusa maisha yetu ya kila siku katika namna mbali mbali.

  Katika uliyoyaandika, kwa upande wangu, kulingana na Maandiko, naona umefika katika kina cha jambo hili kama mafundisho na maonyo yake yalivyo kusudiwa.

  Kwamba umeweza kufika katika kiwango cha kuuona utenganisho wa maneno haya mawili; UZINZI na UASHERATI yenye kubeba uzito mkubwa sana katika kuufikia uamuzi wa kuzivunja ndoa au kujiingiza katika hukumu, ni jambo la kumshukuru sana Mungu! Maana yeye huiangalia kiu na shauku ya mioyo yetu ya kulijua Neno lake, naye katika upendo wake hutufunulia mambo hayo tupate kuenenda sawasawa na mapenzi yake.

  Basi kutoka katika maelezo uliyoyaandika, napenda kuweka sawa kidogo tu ili kulileta somo lote ulilolifafanua katika ukamilifu wa Fundisho hilo la NDOA na TALAKA kama Maandiko yanenavyo.

  Kwanza ni vizuri kwetu sote tukatambua kuwa mambo haya yanamhusu mwaminio tu. Asiye amini hahusiki na Fundisho hili, isipokuwa awe ameliridhia mwenyewe kwa hiari yake kama mtume Paulo anavyofundisha kwamba mwenza wa jinsi hii husafika kwa mwenzi wake. Kwa hiyo ni vizuri wakristo tukawa makini tunapoyaendea mambo haya.

  Sasa, tunapoliendea jambo hili, kwanza ningependa ifahamike kuwa kuna ulazima wakulirejea hilo kulingana na mwongozo wa maisha kama ulivyo katika Maandiko na si katika mambo ya siasa zinazo geuka geuka kila kukicha. Maana siasa ni mitazamo ya kibinadamu, kwa hiyo haifai kuileta kushiriki kuliongoza kanisa. Basi, ki-Biblia mwanamke hamtaliki mume, bali anaweza kujitenga na mumewe akingoja kupatanishwa. Ninafika katika uelewa huu kulingana na vifungu vinavyozungumzia talaka, vyote humhusisha mume kumtaliki mke tu. Naye anayetalikiwa ndiye anayefungwa asiolewe. Kuhusu Mume aliyemtaliki mke, Biblia iko kimya, haijamfunga, ingawa makanisa humfunga sijui kwa Andiko lipi. Bali mume aliye muacha mke kwa sababu yoyote ile mbali na uasherati huyo Maandiko yanamfunga asioe, pia mke asiolewe.

  Nitakinukuu kifungu kimoja kwanza, ili tuliendee hilo ninalotaka kulizungumzia kwanza, kuhusu UASHERATI.
  “Kwa ujumla wake ni kwamba, uasherati huhusika na watu ambao hawajaoa/olewa au wachumba. Kama ni wachumba mmoja anapoona mwenzi wake amekengeuka, kimaandiko mwingine anaruhusiwa kumwacha na kuoa/kuolewa na mwingine.”

  Maelezo hayo ya uasherati ni sawa kabisa. Katika kuhusisha talaka, pia kuna mazingira ya uasherati ambayo yanaweza kujitokeza baada ya wachumba kuoana na kudumu katika ndoa yao hata kwa zaidi ya miaka kumi. Katika uchumba, kuna mambo ambayo yanapaswa kuwekwa wazi kabla ya kufunga ndoa. Jambo la mahusiano, kwa mwanamke, lina ulazima wa kuwekwa wazi katika wakati huo ili yule mwanamume aijue hali hiyo kisha afanye uamuzi juu yake, wa kuendelea na ndoa au la. Iwapo mwanamke atayaficha mahusiano yake na wanaume wengine, au akadanganya, akihofia ndoa kutokufanyika, basi hiyo dhambi isiyo ungamwa itamfuata popote alipo. Basi huko mbele ya safari iwapo yule mumewe atagundua kuwa kumbe mkewe kabla hajamchumbia na kumuoa, alikuwa na mahusiano ya kimapenzi labda na ndugu yake wa karibu huyo mume, hilo linampa ruhusa ya kumtaliki mkewe. Kwa hiyo, iwapo yule mke angeiungama ile dhambi yake ya uasherati mapema, hata hizo habari zinapomfikia mume huwa hazina nguvu tena, maana ni dhambi iliyoungamwa, Mungu haihesabu tena! Basi kama Maandiko yanavyojionesha, suala la Talaka linahusishwa na uasherati tu!!!

  Nukuu ya pili inahusu UZINZI:
  “Uzinzi huhusika na watu waliooana tayari; mmoja anapotoka nje ya ndoa na kufanya ngono, huyo anakuwa anafanya uzinzi, na iwapo mmoja akagundua kuwa mwenzi wake anafanya uzinzi, bado haruhusiwi kumwacha”

  Tafsiri ya uzinzi uliyoitoa iko sahihi kabisa. Tatizo ninaloliona mimi ni katika hitimisho ulilolitoa: “…na iwapo mmoja akagundua kuwa mwenzi wake anafanya uzinzi, bado haruhusiwi kumwacha”. Kwa hitimisho hili Injili itakuwa imekosa mwelekeo, maana iwapo muasherati anatalikiwa, iweje mzinzi apone na alazimishwe kuishi na mumewe? Pia hakuna Andiko la jinsi hiyo. Labda katika kuliweka sawa hilo, yatubidi turudi katika Torati ili kuona liliamuliwa vipi jambo hili la uzinzi. Huko katika Torati mzinzi alipigwa mawe hadi kufa! Hata tunaona Kristo aliletewa mwanamke mzinzi ili amuhukumu, naye aliipitisha hukumu ile kulingana na Torati, bali kulikuwa hakuna wa kuitekeleza hukumu ile kulingana mahitaji ya Torati inayowataka walio safi tu ndio waitimize. Licha ya kwamba alimsamehe mwanamke yule, hakuitangua sheria ile, ipo hata leo. Mt 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.” Ndio maana hata katika swali la talaka aliloulizwa aliishia kuiruhusu talaka kwa kosa la uasherati tu na si UZINZI. Uzinzi, adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka ufe, je, utamtaliki marehemu???? Hebu litazame jambo hilo la “kuitimiliza Torati” anavyolifanya ili uuone wigo wa kuwakamata wazinzi alivyoupanua Kristo; Mt 5:27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini, lakini mimi nawaambia, kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Hapo nadhani unaweza kuelewa huo umati utakaopigwa mawe utakuwa mkubwa kiasi gani. Yaani, wazia hili: kwamba mko katika uwanja mpya wa taifa nao umefurika, halafu akapita mwanamke kule chini mbele yenu wote mliokaa vitini, labda wanaume 60,000, mwanamke huyo ni mnene kiasi kwa maumbile naye amevaa kisuruali kinachombana na kitop chake, akapita akijitingisha mwili wake, haswa makalio yake, hebu niambie, ni wangapi atakao enda nao kuzimu? Usikute uwanja mzima? Au mchukulie mwanamke anayeiheshimu ndoa yake vizuri sana, anaimba kwaya kanisani, pia ni mwenye msaada mkubwa hapo kanisani. Naye bila kujua amevutiwa na kafasheni ka kuacha matiti wazi kidogo, anonekana ni wa kileo, yuko up-to-date. Lakini kwa yale mavazi yake, wanaume wengi wemevutiwa naye kwa kuyaangalia yale matiti yaliyoachwa wazi kidogo, naye mchungaji wake amewaambia Mungu hatazami mavazi bali mioyo; siku ya hukumu atakapokusanywa na wale wanaume wote waliokuwa wakimtamani, wakisimama hapo mbele ya hakimu kwa kosa la UZINZI, naye maskini hajawahi hata siku moja kutoka nje ya ndoa yake, itakuwaje hapo??

  Bwana atuhurumie!

 21. Mpendwa Orbi,

  Bwana apewe sifa.

  Nimefuatilia mada hiiyenye ujumbe, “Kuachana vs Talaka”. Katika kufuatilia kwangu nimeguswa sana na nimeona pia name nichukue nafasi hii niweze kuchangia kile ninachokiamini, kuhusiana na wanandoa wanaokuwa katika Bwana.

  Nimejaribu kufuatilia kwa makini maelezo na maoni yako kuhusu wanandoa katika Bwana, nimekuelewa kuwa iwapo mmoja anakuwa amegundulika kufanya tendo la ngono nje ya ndoa basi mmoja aliyegundua hali hiyo ya mwenzake anaruhusiwa kutoa talaka kwa aliyekiuka msingi wa ndoa yao.

  Katika kusoma kwangu mada hii nimejiuliza, kwamba, huyo aliyempa talaka mwenzake na akaamua kuoa/kuolewa na mwingine, je, hatakuwa anafanya kosa lile lile ambalo amemhukumu mwenzake nalo?

  Mimi maoni yangu ni haya yafuatayo: Kwa vile mmoja anakuwa amemwacha mwenzake kwa kosa la kumkuta anafanya tendo la ngono na mtu kmwingine, yeye naye akitoka na kufanya tendo hilo hilo la ngono na mwingine atakuwa anafanya kosa lile lile. Maandiko katika eneo hili yanasema; 1Wakorinto 7:10-11 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapa si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”.

  Kwa mtazamo wangu, hapa ni kwamba kuna uwezekano wa kuachana iwapo maisha yameshindikana kabisa ya kuishi pamoja, lakini pamoja na kuachana bado maandiko yanasema haturuhusiwi kuoa/olewa bali tufanye jitihada za kupatana ili ndoa zetu ziendelee.

  Tunapokuwa tunachambua biblia, lazima tuangalie mambo mengi yanayokuwa yameandikwa katika kile tunachojaribu kukichambua au kufundisha. Mimi katika biblia yangu, katika eneo hili tunalolijadili naona kuna maneno mawili yanayohusiana na kile tunachokijadili. Kwanza kuna neno “Uasherati” na pili kuna neno “Uzinzi”. Maneno haya mawili, wakati tunapojaribu kuchambua biblia, lazima tujiulize kwa nini yalitumika yote mawili kuelezea tendo la aina moja.Tukiangalia mfano, katika Mathayo 5:32 tunasoma “……kila amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya “UASHERATI”, amfanya kuwa “MZINZI” na mtu akimwoa yule aliyeachwa, “AZINI”. Kwa nini maandiko hayasemi isipokuwa kwa habari ya “UASHERATI” amfanya KUWA “MWASHERATI” bali yanasema amfanya kuwa “MZINZI”?. Ukiwa katika hali hiyo ya kujiuliza bila shaka Roho wa Mungu atakufunulia na kukuonesha kuwa, kumbe “uasherati” na “uzinzi” ni matendo mawili tofauti yanayofanywa katika mazingira ya watu tofauti!.

  Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba, kumbe uasherati na uzinzi ni matendo yanayofanana katika utekelezaji lakini yanatendwa na watu wa mazingira tofauti. Katika kuzidi kuendelea kuliangalia maneno haya mawili, hebu tuangalie pia maandiko katika biblia ya Kingereza ya KJV inavyotofautisha “uasherati” na “uzinzi” kisha tutajadili tuone tofauti hizi zinamaanisha nini kwa kuangalia katika Kamusi ya Kingereza!.

  Tukianza na Matthew 5:32 we read “But I say unto you, That whosoever shall put away his wife, saving for the cause of “FORNICATION”, causeth her to commit “ADULTERY”: and whosoever shall marry her that is divorced committeth “ADULTERY”. Katika maandiko haya pia tunayaona maneno mawili tofauti kwa tendo la aina moja “Fornication and Adultery”. Pia katika Matthew 19:9, also we read, “And I say unto you, Whosoever shall put away his wife, except [it be] for “FORNICATION”, and shall marry another, committeth “ADULTERY”: and whoso marrieth her which is put away doth commit “ADULTERY”. Katika Mathayo 5:32 na 19:9 tunaona pia kuna maneno mawili yametawala kuhusiana na mambo ya talaka, nayo ni Adultary na Fornication.

  Adultary ni nini na Fornication ni nini! Tuanze na Adultary; katika dictionary ya Oxford Dictionaries, wameandika, Adultary [mass noun] voluntary sexual intercourse between a married person and a person who is not their spouse: she was committing adultery with a much younger man. Tunaona kumbe Adultary ni tendo la ngono linalofanywa na yule aliyeona tayari, anapofanya tendo hilo huku amemwacha mwenzi wake, anakuwa anafanya tendo la “Adultary” ambalo ni dhambi. Hivyo iwapo mtu atamwacha mwenzi wake kwa sababu yoyote na akaona/olewa na mwingine katika maisha yake yote atakuwa anafanya adultery.

  Tuangalie pia neno “Fornication”. Katika Katika kitabu hicho hicho cha Oxford dictionaries wameandika hivi, Fornication [mass noun] sexual intercourse between people not married to each other: laws forbidding adultery and fornication. Kumbe “Fornication” ni tendo la ngono kati ya wawili ambao hawajaoa/olewa. Hapa ndipo Yesu aliporuhusu kuwa wanaweza kuachana.
  Ili tujifunze zaidi juu ya hili, kuna post moja ya Julai 16 2011 ambayo nilijaribu kuandika kuhusiana na mada hii nime-copy na kui pest hapa chini kama ilivyo waweza kuipitia kusoma.

  Mbarikiwe wapendwa,
  Suala la ndoa kwa sisi waKristo, mimi nakumbuka kuna wakati fulani kati ya mwaka jana niliwahi kufafanua ninavyofahamu juu ya ndoa za ki-Kristo.
  Wengi tunapotoshwa na hatujaelewa vizuri maana halisi ya maneno haya mawili yalivyotumika katika biblia “UASHERATI” na “UZINZI”.
  Ninapenda nieleze kuwa; uasherati na uzinzi ni maneno mawili tofauti japo yanahusiana. Tukisoma katika Mathayo 5:32 tunaona maneno haya “…lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya UASHERATI, amfanya kuwa MZINZI; na mtu akimwoa yule aliyeachwa AZINI” Maana yake ni nini..! Katika maandiko haya, tunajifunza wazi kabisa kuwa uzinzi ni dhambi, na wafanyao huo uzinzi maandiko yanatuambia kuwa hawataurithi ufalme wa Mungu. Tunasoma hilo katika Ufunuo 21:8 Bali waoga……..na WAZINZI…..sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti…..
  Kama wa-Kristo tunaoutazamia ufalme wa Mungu, katika sehemu hii lazima tujiulize. Kwa nini Mungu aruhusu kuachana na kuoa/kuolewa na mwingine tena Mungu huyo huyo aseme kuwa wazinzi hawataurithi ufalme wa Mungu? Anayefanya uzinzi ni yupi; aliyeachwa au aliyeacha? Tukisoma andiko; Mathayo hiyo hiyo 5:32, linasema; “…..na mtu akimwoa yule ALIYEACHWA azini!. Unaona! Je aliyeacha akioa/olewa?!.. Tusome tena Mathayo 19:9…..Kila mtu ATAKAYEMWACHA mkewe……akaoa mwingine, AZINI, naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Katika ufafanuzi huo, tunaoneshwa kuwa kuacha mke/mme na kuoa/kuolewa tena ni dhambi kabisa mbele za Mungu.
  Uzinzi ni nini?!.

  Uzinzi ni tendo la mtu mume aliyeoa au mtu mke aliyeolewa anapotoka nje ya ndoa na kufanya ngono na mtu asiye mumewe/mkewe, huo ndiyo uzinzi. Mungu anakataza kabisa kwa mtu anayetazamia kumwona Mungu kufanya huo uzinzi.
  Uasherati ni nini?! Tukisoma katika Mathayo hiyo hiyo 19:9, inatuambia, “Kila mtu atakayemwacha mkewe, ISIPOKUWA NI KWA SABABU YA UASHERATI akaoa mwingine, azini”.

  Tunapoangalia kwa makini, katika eneo hili, tunaona kuwa Yesu anaruhusu kuoa/kuolewa tena, iwapo mmoja ataonekana amefanya uasherati. Uasherati ni nini tena?! Kwa kifupi, uasherati haufanywi na watu waliooana tayari, bali hufanywa na wachumba au watu ambao hawajaoa au kuolewa bado.

  Uchumba katika biblia haukutajwa sana, isipokuwa kila waliokuwa wachumba, walitambulishwa kama mke na mme. Ndiyo maana sasa tunaona katika Mathayo 1:18 inasomeka; “……Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, KABLA HAWAJAKARIBIANA, alionekana ana mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”. Kabla hawajakaribiana maana yake walikuwa wachumba si ndiyo?!…. Mst. wa 19 tunasoma… “Naye Yusufu MUMEWE kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, ………aliazimu KUMWACHA…….”.

  Hapa tunaona anatajwa Yusufu kuwa ni mumewe Mariamu japo walikuwa wachumba. Lakini pamoja na kutajwa hivyo, bado tunaona Yusufu alitaka kumwacha. Kumbe hatua alizotaka kufanya Yusufu za kumwacha Mariamu mkewe, mbele za Mungu ilikuwa ni halali kwa sababu yule mke alikuwa ni chumba tu; walikuwa bado hawajaanza kushiriki unyumba, hivyo ilikuwa ni halali kumwacha kwa sababu Mariamu alidhaniwa kuwa si mwaminifu.

  Yesu Kristo alipokuwa anawaeleza wale mafarisayo juu ya ndoa, alikuwa anawaeleza waliooana na waliokuwa wachumba bado. Nyakati zake, alipokuwa akitaja, isipokuwa kwa habari ya “UASHERATI” walikuwa wanamwelewa kuwa anazungumzia nini na pia alipokuwa anataja juu ya habari ya “UZINZI” pia walimwelewa alimaanisha nini.
  Kwa ujumla wake ni kwamba, uasherati huhusika na watu ambao hawajaoa/olewa au wachumba. Kama ni wachumba mmoja anapoona mwenzi wake amekengeuka, kimaandiko mwingine anaruhusiwa kumwacha na kuoa/kuolewa na mwingine.
  Uzinzi huhusika na watu waliooana tayati; mmoja anapotoka nje ya ndoa na kufanya ngono, huyo anakuwa anafanya uzinzi, na iwapo mmoja akagundua kuwa mwenzi wake anafanya uzinzi, bado haruhusiwi kumwacha.

  “1Wakorinto 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana NAWAAGIZA; wala hapa si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mkewe; lakini , ikiwa ameachana naye , na akae ASIOLEWE, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”.
  Maneno haya, Paulo anayanukuu katika Mathayo hiyo hiyo 5:32 kwamba kwa waliooana ni mwiko kuachana kwa sababu yoyote ile. Ndivyo Mtume Paulo alivyomwelewa Yesu, na pia ndivyo alivyomaanisha Yesu Kristo.

  Bwana azidi kuwa pamoja nasi, hasa nyakati hizi za mwisho, Shalom.

 22. Bwaya,

  Nashukuru kama umenielewa kwenye ile post ya awali,

  Sasa tuje na hilo andiko au Matamshi ya Yesu;

  31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

  Tafsiri mojawapo ya mstari huo

  1. Yesu anakubali Talaka kama Maandiko yalivyosema (Agano la kale)

  2. Yesu anakubali talaka iliyojengwa kwa sababu ya Mwanandoa mmojawapo kuwa Muasherati ( Angalia andiko ISIPOKUWA KWA KWA HABARI YA UASHERATI)

  HIVYO BASI:

  Kama Yesu anakubali talaka ambayo sababu yake ni Uasherati…….Hii inamfanya yule aliyeachwa kuwa huru! Maana talaka hiyo si batili! Ni halali!

  Na kwa mantiki hiyo TALAKA ambayo haijajengwa au haitokani na SABABU YA UASHERATI NI BATILI!

  Na kwa sababu hiyo yoyote anayemuoa mtu aliyeachika/ aliyepewa talaka ambayo haikusababishwa na UASHERATI anazini! Hivyo ndivyo Yesu anasema katika Maandiko hayo!

  Labda unaweza kuniuliza Je ndoa ya Kikristo haiwezi kuvunjika? Ukiangalia Mstari huo ndoa ya Kikristo INAWEZA KUVUNJIKA! NA Sababu TU inayoweza kuvunja ndoa hiyo ni UASHERATI!

  Labda utauliza tena Mbona Yesu alisema “ALICHOKIUNGANISHA MUNGU MWANADAMU ASIKITENGANISHE”

  Jibu ni NDIO! Lakini UASHERATI ni dhambi MBAYA MNO kwani INA UWEZO WA KUTENGANISHA KILE ALICHOKIUNGANISHA MUNGU! (Rudia dhambi ya Uasherati ndani ya Biblia na madhara yake! Na vile vile mfano wa ndoa unavyotumika kuunganika kwetu na Kristo! Ambako kunaweza kuvunjika tukiruhusu dhambi!)

  Hiyo Bwaya hii inaweza kuwa Tafsiri mojawapo ya Andiko hilo.

  Lakini ndugu yangu BWAYA kwa mtazamo wangu…….Mwanandoa anayemfahamu Mungu na Msamaha wake anao uwezo wa aliopewa na Mungu kumsamehe Mwanandoa mwenzake aliyeanguka katika dhambi ya UASHERATI……Tuna nguvu ya MSAMAHA KUKILINDA KILE ALICHOKIUNGANISHA MUNGU KISITENGANISHWE! soma tena Biblia kuhusu somo la Msamaha!

  ubarikiwe na mawazo yangu……

 23. Ndugu yangu Orbi, nimekupata. Na nikiri kwamba jambo hili limesumbua uelewa wangu na kwa kweli sikuwa nalielewa jambo hili kwa mtazamo huu. Bado najifunza.

  Tafadhali naomba tusome kutoka Mathayo 5: 31-32:

  31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

  Na katika Injili ya Luka 16: 18 Bwana Yesu anasema: “18 Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na muwewe azini.
  Ninachotafuta kuelewa, ni hiki. Huyu mwanaume ameachwa. Je, huyu mwanamke anayeolewa na mwanaume aliyeachwa, hazini?

  Pili. Je, kuna mazingira yoyote yanayoweza kumfunga mwanandoa (of course aliyeokoka) anayeachana na mwenzake? Hii ni kusema, ni wakati gani mwanamme/mwanamke aliyeachana na mwenzake hawezi kuwa huru isipokuwa tu, pale mwenzake (mtalaka) anapofariki?

  Samahani kama ninarefusha mambo yanayoeleweka. Naomba tuchukuliane.

 24. Bwaya,

  Kwa mtazamo wangu mimi “Asiyeamini” Ni yule alyemwamini Yesu Kabla ya ndoa na sasa hamwamini Yesu tena! Yaani ameacha kule kuamini kwake! Au yule ambaye hajaamini kabisa! Asiyeamini ni asiyeamini haijalishi ni lini!

  Hebu angalia muumini aliyeamini anapochukuliwa kama asiyeamini

  “Na ndugu yako akikukosa (yaani anayeamini) enenda ukamuonye……..na asipokusiliza liambie Kanisa na asipolisikiliza kanisa na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru (Mathew 18: 15-18)

  Hebu angalia na Paulo anasemaje

  ” Lakini mambo yalivyo naliwaandikia msichangamane na MTU AITWAYE NDUGU akiwa MZINZI…..MWENYE KUTAMANI…..MLEVI……MNYA’NGANYI …MTU WA NAMNA HII MSIKUBALI HATA KULA NAYE………NANYI MWONDOENI YULE MBAYA MIONGONI MWENU..”1KOR 5: 6-13

  Hapa tunamwondoa kati yetu……Lakini kuna wakati mtu aitwaye ndugu anajiondoa mwenyewe kwenye kundi!

  Sasa ndugu yangu Bwaya, kwa case uliyotuletea Mwanadoa ameacha kuamini….inawezekana kaonywa na Kanisa kwa njia mbali mbali na mara nyingi kwa maamuzi anayotaka kuchukua lakini kaondoka hata kufikia hali ya kuolewa na Mataifa! Sasa utasemaje? Huyu si ndugu tena! Wala sio Muumini! Kwa kuolewa tu tayari amekuwa mzinifu! Sasa kwa nini yule aliyekimbiwa na huyu asiyeamini asioe!

  Kwa kuolewa tu nje ya Ndoa inayotambulika ameisha zini! Hivyo kajiondoa na kumpa uhuru yule mwingine kuoa/Kuolewa!

 25. Orbi. Nashukuru. Heri ya mwaka mpya!

  Andiko hilo ndilo alilolitumia Askofu. Hata hivyo, context ya maandiko hayo, nionavyo mimi, ni pale Mkristo aliyeokoka anapokuwa na mke asiyeamini. Ni nini hasa tafsiri ya “asiyeamini”?

  Ningependa kujua mazingira yanayohusiana na maandiko ya mstari wa 10 na 11? “10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asichane na mumewe; 11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”

 26. Jesus words are very clear to me:

  Matthew 19:9 And I say unto you, Whosoever shall put away his wife, except it be for fornication, and shall marry another, committeth adultery: and whoso marrieth her which is put away doth commit adultery.

  You can only divorce ONLY if there was fornication.

  Jeremiah 3:8 (KJV) and 1 Corinthians 7 (KJV) does not give any exceptions.

  How can it be not a sin?

 27. Bwana Yesu asifiwe,

  Jamani tunaomba michango yenu watumishi wa Mungu hasa Wachungaji, Wainjilisti pamoja na Maaskofu kwa maana mada hii inahusu sana nyakati tunazoishi kwa sasa maana kama si kwako atakuwa ndugu au jirani. Tunaendelea kujifunza kutoka kwenu.

 28. Bwaya……umepotea ndugu yangu! Mungu Akubariki nafurahi kuona Maandiko yako!

  Kwa mtazamo wangu, Mwanandoa aliyekuwa anadai ameokoka na akajiondoa katika ndoa……hata akafikia hatua ya kufunga ndoa na mmataifa, ananipa wasiwasi hata kuutambua Wokovu wake tokea awali! Na hii inanipa mwanya wa kutumia andiko la Paulo….”LAKINI YULE ASIYEAMINI AKIONDOKA NA AONDOKE…….HAPO NDUGU MUME AU NDUGU MKE HAFUNGUKI: 1COR7: 15,Kwa kigezo hicho cha Maandiko haya inampa nafasi MUME/MKE aliyeachwa kuoa/kuolewa (Hapo ndugu ( huyu ni aliye katika Bwana) Mume/Mke Hafunguki (Yuko huru!)

  Ubarikiwe!

 29. Labda na mimi niongeze swali: Mwanandoa ni nani? Mambo gani huufanya uhusiano wa watu wawili wa jinsia tofauti kuwa ndoa?

  Aidha, nadhani hapa panaweza kuwa mahali sahihi kupata maoni zaidi kuhusu eneo ninalotaka kujifunza zaidi. Nisamehewe kama nitakuwa nimekwenda nje ya mada.

  Wanandoa wawili waliookoka walihitilafiana kiasi cha kufikia “kutengana” (kwa maana ya kila mtu kuishi maisha yake pasipo kuingiliwa na mwingine). Suala hili lilishughulikiwa katika hatua mbalimbali (na kanisa) pasipo muafaka kufikiwa. Hatima ya yote mke akaamua kuolewa na mtu mwingine wa mataifa. Kilichofuata, mume (aliyeokoka) alishauriwa kutafuta talaka. Inasemekana juhudi za mahakama kuwaunganisha zilifanyika na kushindikana na hatimaye mume akapewa talaka yake.

  Pengine mpaka hapo sikushangaa sana (maana siku hizi imeanza kuwa kawaida kwa “wakristo” kuachana!). Kilichonishangaza (zaidi) ni pale tulipotangaziwa kwamba mume huyu aliyepewa talaka na mahakama kwa sasa yu huru kuoa!

  Mpaka hapo sijahukumu. Bado najifunza. Ningependa kuelimishwa zaidi kuhusu tukio hili la Mkristo kupewa talaka, na kisha kuwekwa huru kuoa!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s