Rais Kikwete kuhudhuria MKESHA MKUBWA KITAIFA

Tanzania Fellowship of Churches ( TFC) Wakishirina na makanisa yote Tanzania wameandaa Mkesha mkubwa wa kuliombea Taifa, utakaofanyika uwanja wa Taifa tarehe 31 Desemba 2011, mkesha unategemewa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Taifa, Vyama vya siasa na mabalozi. Ambapo mgeni rasmi ni Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Askofu Godfrey Emmanuel Malasi amesema “Kila mtu anapaswa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uchumi wa Taifa letu ambalo sasa limetimiza miaka 50 ya Uhuru, kila mtu anapaswa kutambua nafasi yake tusikae na kubweteka, tusilalamike, kila mtu ajue ni wakati wa kumiliki na kurithishwa rasilimali zilizopo katika Taifa hili, mjitokeze na kutamka maneno ya kupokea miaka 50 ijayo kama ishara ya kupokea kizazi huru cha watanzania

Mikoa mingine itakayofanya mkesha ni:-

Mwanza- CCM KIRUMBA,
Arusha – SHEIK AMRI ABEID,
Bukoba – KAITABA,
Dodoma – JAMHURI STADIUM,
Songea – SAMORA,
Zanzibar – MAO TSEITSUNG,
Kilimanjaro – MAJENGO,
Tabora – MAJI MAJI, Singida – NAMFUA

Kiingilio ni bure, Chai na kahawa vitakuwepo, Timu kubwa ya kusifu na kuabudu itakuwepo.

……MNAKARIBISHWA…..

Advertisements

2 thoughts on “Rais Kikwete kuhudhuria MKESHA MKUBWA KITAIFA

  1. Ni vyema viongozi wetu wakuu wa Kitaifa wakahudhuria kwenye matukio makubwa kama haya ili achukue sehemu yake kama Baba. Pia wakati Mungu anapotupatia nafasi kama hizi ni wakati wa kumweleza dukuduku zetu hasa kuhusu hali ya uchumi wetu ilivyo na elimu kwa watoto wetu ambao hawana madarasa, madawati, vitabu wala vifaa vya maabara katika mashule yetu kwa mtazamo wa viongozi wa Kanisa. Pia kwa kanafasi kama haka tusikose kutoa hoja zetu kuhusu hatma ya taifa letu hususani kuhusu mabadiliko ya katiba. Ni nini kanisa linataka?? Mwambieni rais yale tunayoona yawepo kwenye katiba mpya hata kama ni mapema si atakuwa amesikia?? Mwambieni asiitumie siku ya Bwana kwa shughuli yoyote ya kitaifa mbali na kuabudu tu ndivyo biblia inavyosema isiwe siku ya kupiga kura nk (chomekeni mambo kama hayo ndugu zangu). Asanteni sana!!

  2. Sasa Kikwete kuhudhuria itaongeza thamani ipi katika hayo maombi maana naona ndio kichwa cha habari hapo juu.
    Ila msisahau kuwahubiria injili waokoke

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s