Mwaka 2012 ni Mwaka wa Kazi

“Mungu hatakupatia zawadi kwa kuwa umeokoka, bali kwa kuwa ulifanya kazi yake, kwa kuwa kuokoka ni kwa faida yako mwenyewe. Tufanye kazi ya kuujenga ufalme wa Mungu. Hata tunapofanya kazi zetu za kimwili, tukipata kipato zaidi, kipato hicho kitatusaidia katika kuifanya kazi ya Mungu kwa kiwango cha juu zaidi”

Tukisoma Luka 19:11-26 tunaona jinsi ambavyo watu walipewa fedha. Katika waliopewa fedha hizo wapo waliozalisha lakini kuna mwingine hakuzalisha chochote bali alificha na kuirudisha vile vile kama alivyopewa. Waliozalisha walipewa zawadi lakini yule ambaye hakuzalisha alinyang’anywa hata kile alichokuwa amepewa.

Fundisho kuu la maneno hayo ni kutuelekeza KUFANYA KAZI ili tuzalishe. Tuwe watu wenye kuzalisha.

Rev. Wilson Kimaro –  Calvary Temple – Arusha alipokuwa akihubiri katika Ibada ya Jumapili ya tarehe 1/1/2012 na kuukaribisha mwaka 2012.

Advertisements

4 thoughts on “Mwaka 2012 ni Mwaka wa Kazi

 1. Hongereni sana wana SG kwa maoni mnayotoa, na pia nawapongeza viongozi wa mtandao huu kwa kutufanyizia fursa ya kujua nani kafundisha nini, na hapo hapo mkatupa uwanja wa kutoa maoni yetu.
  ila ninashauri, kabla ya sisi kutoa maoni yetu, ingalifaa tuwe na fursa ya kupata ujumbe mzima wa fundisho lililotolewa, na hasa mambo ya msingi yaliyozungumzwa katika fundisho hilo.
  baada ya ushauri huu, acha nirejee kwako Frank. Nairejea kauli yako inayosema “Hubirini habari za ufalme wa Mungu ninyi wachungaji mnaosimama katika madhabahu”. Mimi nasumbuka na neno “Madhabahu”. natamani kujua ni kitu gani kinachomaanishwa, naomba unielimishe tafadhali. Pili nakuunga mkono kwamba, sisi tunahitaji kusikia habari za Ufalme wa Mungu. Kimsingi haya ndio mapenzi ya Mungu kwa nyakati hizi, tangu wakati Yohana mbatizaji. Yesu mwenyewe anasema;
  Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu. Luka 16:16
  Jambo la kusikitisha, hawa wanaotuhubiria leo juu ya kuujenga Ufalme wa Mungu, hawaachi kututengenezea MSETO, kwa kutuhubiri habari za Ufalme wa Mungu wakizichanganya na maagizo ya sheria (Torati). Ndio sababu mimi napendekeza tuandikiwe kitu kizima alichohubiri mtu kabla ya kuchangia lolote.
  Kwa ajili ya kuchokoza mada, acha nitoe mfano mmoja wa mseto wa habari za Ufalme wa Mungu na maagizo ya sheria. Siku hizi za hivi karibuni, wameanza kutudai tuwapelekee Malimbuko ya mshahara na faida ya Biashara ya mwezi wa kwanza, kwa kutusomea maandiko ya Agano la Kale. Baya zaidi, hata maandiko hayo wanayachakachua, na hawako radhi na mtu yoyote anayetaka kuwahoji. Wanachokidai ni kwamba; tunawajibika kutoa hayo malimbuko kwa ajili ya kuujenga ufalme wa Mungu.
  Kwa mtazamo wangu, wanafanya kitu ambacho hakina tofauti na kile alichokifanya Mfalme Sauli, kwa kisingizio kwamba ni kwa ajili ya Bwana. (1Samweli 15)
  18 Kisha Bwana akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia.
  19 Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana?
  20 Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa.
  21 Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali.
  22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

  Wapendwa, naomba turejee Luka 16:16 hapo juu, tuone iwapo ni kweli watu wenye kuwafundisha Wakristo kushika maagizo ya sheria ya Musa, ni mawakili wa Ufalme wa Mungu au la. Kumbuka, hawa akina Rev Wilson Kimaro ndio wenye kudai Malimbuko na Zaka kwa kisingizio cha kuujenga Ufalme wa Mungu. Tena wakiwa tayari wameyachakachua (Kuyapindisha) maandiko yenye kuzungumzia maagizo hayo, ili yakidhi malengo yao. Nawasilisha kwa ajili ya mjadala zaidi, lakini pia nasisitiza hoja zetu ziambatanishwe na ushahidi wa Neno la Mungu, tena kwa matumizi halali.

 2. kweli, vile mchugaji alivyosema kwani Mungu hufungua njia lakini ni mtu binafsi aamue kutembea. Afike atakapofaa.
  Mwanafunzi wa Yesu wa Imani ‘Paulo’ mwenyewe alikuwa mtu wa bidii.

  Inatufaa tutumie vipawa vyetu, kwani kila mtu aliumbwa na kipawa fulani.

  Kwani nanena kwatafsiri yangu mwenyewe ya biblia imeandikwa kwamba Kipawa cha mtu hufungulia mtu njia.

 3. Ndo ukweli,mahubiri mengine ya kudanganyana kuwa BWANA atafanya muujiza wakati hufanyi kazi kwa bidii ni uongo.Mara huyu kitambaa cha upako huyu mwingine fruto wengine maji ya upako.Tumechoka na hizo sound zao.Hubirini habari za ufalme wa Mungu ninyi wachungaji mnaosimama katika madhabahu.Khaa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s