Ninateseka, niombeeni!

Shalom wapendwa wa blog hii! Ninaomba ye yote atakayesoma ujumbe huu aungane nani katika maombi. Nimeolewa na sasa ni mwaka wa sita sijafanikiwa kupata mtoto. Pia shetani amefunga mafanikio yangu katika nyanja zote, ninateseka sana lakini namtumainia Mungu kupitia Yesu Kristo atanitendea muujiza. Sasa ninaomba mniombee kunihamisha kutoka kwenye nguvu za giza. Shetani anataka nimtumikie nami sitaki kabisa kufanya kazi ya mizimu. Nahitaji kuwa mtumishi wa Yesu. Naomba sana mniommbee nami naamini yote yana mwisho.

Magda

Advertisements

21 thoughts on “Ninateseka, niombeeni!

 1. Wakati naandika email hii sijisikii kabisa kukuita Magdalena najisikia kukuita mama …………..yaani huyo babygirl ambaye naamini ndo unaitwa hivyo. Mimi ni Mtazania ninaishi Kenya niliangalia kipindi kimoja jana kinaitwa FARAJA ni kwenye station ya K24. Kipindi kimeelezea maisha ya mama aliyeishi kwenye ndoa kwa miaka 31 bila mtoto ikafika anakaribia Menopause akahisi amefikia hicho kipindi lakini hajisikii vizuri akaendelea kuomba na kushukuru Mungu. Akaendelea kutojisikia vizuri akaenda kwa daktari kupima si alikua mjamzito na hivi ninavoongea ana mapacha watatu. Kwahyo usikate tamaa tupo pamoja kwa maombi na Mungu atakufungulia kupata si mtoto tu ni watoto.

 2. Acha wasiwasi dada. aliyekuumba anampango mkubwa sana kwako. amekuandalia uzao na wewe uzao wako utamiliki.Yeremia 29:11 Mungu anakuwazia yaliyo mema.Anza kuimba wimbo wa kumsifu kwasababu anakuwazia yaliyo mema.

 3. Pole Magda.yakupasa uvumilie! kuchelewa kuzaa,haimaanishi kuwa hutozaa kabisa.Sarah alizaa akiwa mzee.
  1.Kumbuka huko nyuma.Kama kuna dhambi ulifanya ambayo yaweza kukusababishia usizae kwa miaka sita,ingia moja kwa moja kuomba rehema(omba Yesu akusamehe).
  2.Hiyo ndoa ni halali? kama sio,tafuta jinsi ya kutoka ili ujitenge na dhambi.
  3.Kama kwenye familia yenu kuna kesi kama hizo za kutozaa,vunja hizo laana na minyororo ya mizimu inayokufatilia.
  4.Kazana kufunga na kuomba ukikataa kazi zote za wachawi.
  5.Ni vizuri,umeshaamua kumfuata Yesu.sasa,endelea kujilinda nafsi,roho na mwili.ishi katika utakatifu.
  6.Jinenee mema na ushindi.Waebrania 11:1,amini kuwa mtoto anakuja na utazaa muda si murefu.ikiwezekana tafuta hata jina la kumpa ukiendelea kuamini,nunua hata nguo za mtoto na uziweke ndani,andaa hata kitanda cha mtoto,mwandalie ukiendelea kuamini.Jibatize hata jina.kama wamezoea kukuita Magda jina lako,waambie unaitwa mfano,mama Ebenezer!.
  Hiyo ndo imani wala,sio kupungukiwa akili.yaangalie yote hayo huku tukiendelea kukuombea.nitafute ktk email;krecious@yahoo.com ili tuangalie jinsi ya kukutana niweze kukusaidia hata namna ya kuomba.Precious.

 4. Shalomu,

  Dada Magda

  Naomba ujipe moyo kwani utashinda.

  Nimesoma ufafanuzi wako kuhusu shida ulizonazo. Ukweli ni kuwa Mungu wetu ndiye Jibu na Kimbilio. Yeye atakufungua kutoka kwenye shida na mateso. Lakini jambo la msingi ni kusimama imara kujifunza neno la Mungu.

  Pamoja na kukuombea, ningependa kukupa ushauri kuwa uonane na watumishi wa Mungu ili uweze kushauriana nao kwani si rahisi kueleza kila kitu na kupata msaada kwa njia hii.

  Mungu akuwezeshe

 5. Kwanza anapenda sana kukupongeza kwa uamuzi wako mzuri wa kutafuta msaada wa maumbi hali ukijua hakika yakuwa katika jina la YESU kuna nguvu ya uzima tena ya ajabu kukutosha kukupa ukombozi na kupata mtoto wa halali toka kwa Mungu.Nipende kukuambia kuwa ukikubali kwenda kwa waganga tambua kuwa utakachokipata kule kitakuwa cha masharti tu ni cha muda mfupi mno,lakini kwa YESU utapata cha milele na kudumu wala hana masharti yoyote
  Amini haya nayo yatakuwa yako daima kwa maana umeamini na kutambua wakati………:shetani wewe uliye baba wa uongo na mlaghai nakuamuru kwa jina lipitalo majina yote jina la YESU TOKA KWA MAMA HUYU,MWACHIE NA AWE HURU SASA NA MILELE,ACHIA UZAO WAKE WA TUMBO LAKE>Hataitwa tena tasa bali ataitwa MAMA WA WATOTO NA FAMILIA NA JAMAA:KATIKA JINA LA YESU,Akae aishi na kufurahia ukombozi wa YESU AMEN

 6. nashukuru kwa yote wapendwa katika Bwana dada Glady niandikie namba yako nitakupigia nashukuru sana ndugu zangu kwa kunipatia ushauri mzuri yote nayafanyia kazi mbarikiwe.

 7. Bwana Yesu apewe sifa Dada Magda, nimesoma ombi lako nimekuelewa. Kwanza pole sana na kisha hongera kwa kugundua kuwa ni Mungu pekee awezaye kuondoa shida zako.

 8. Dada Magda,
  Nakushauri uondoe Uchungu ndani ya moyo wako. Ingawa mume wako hajaokoka, naomba uendelee kumpenda tena ongeza upendo zaidi, yale mabaya anayokunenea usiyajali kabisa kwa sababu yanatoka kwa yule mshitaki wetu, hayatoki kwa mume wako. Nakushauri usiache kumwombea Mume wako.Ninaamini mume wako ataokoka. Pamoja na kwamba tutaomba , jitahidi kumshirikisha Mchungaji wa Kanisa lako, ninaamini atakusaidia sana.
  HAKUNA JAMBO LINALOMSHINDA.

 9. BWANA Asifiwe!Je umeokoka kama bado UOKOKE! na njia halisi ya kukataa kazi za shetani ni kufanya kazi za MUNGU kama hujaokoka fuata sala hii fupi sema ee Bwana Yesu nakuja kwako mimi mwenye dhambi unisamehe dhambi zangu zote na mikataba yote niliyoingia kwakujua na kutojua futa jina langu katika kitabu cha hukumu nakuomba uandike jina langu katika kitabu cha uzima AMEN!Tafuta kanisa linalo hubiri habari njema za wokovu penye huduma za maombi na maombezi iliuweze kukulia wokovu na mizimu itakimbia BWANA atakuweka huru na mizimu inayozuia kupata mtoto na kufunga mafanikio ukifunguliwa itakukimbia utakuwa huru kweli kweli AMEN!Barikiwa

 10. Mpendwa Magda naomba uandike email yako hapa au namba ya simu nikupatie watumishi wa Mungu watakaokusaidia shida uliyo. Usiogope, Please toa namab ya simu au email hapa.

  Mungu bado yupo HAI

 11. Soma Yeremia 1 yote uone kazi ya MUNGU uliyoitiwa

  kwakupitia wewe mumeo atamjua MUNGU wako unayemuamini,kwa kupitia wewe amilia yako itamjua MUNGU anayeishi na kutawala dunia yote na vyote viijazavyo.

  kila pando lililopanda ambalo baba(MUNGU) akulipanda lizima ling’olewe ili tupande na kujenga.

  Utazame msalaba pale kalivali kama wanaisrael walipo itazama nyoka ya shaba wakapona

 12. Dada Magda

  Ahimidiwe Mungu wetu kwa BWANA wetu YESU kristo aliyekuleta katika dunia hii na kukupa mume.

  mimi nitakuomba maombi unayoyataka yaanzie nyumbani kwako wewe na mumeo maana neno linasema popote walipowawili na zaidi wamekusanyika kwa jina langu(YESU KRISTO) chochote watakachokiomba nitawajibu pili kama unataka kweli kumuishia MUNGU hapa duniani nyenyekea kwenye kiti chake yaani amini kuwa yeye yupo na kila siku anatenda. ukisoma waebrania 11.6 inasema pasipo imani hatuwezi kumpendeza yeye. kama unaomba amini MUNGU anaungoja wakati wake. najua shida za kisaikorojia unazozipata katika dunia hii ya watu wanaojivunia kuwa na watoto,lakini yupo mfalme wa amani YESU KRISTO(mzee wa siku,mwamba imara,simba wa Yuda)

  Ombi langu kwako,anza kusoma BIBLIA kuanzia kitabu cha MWANZO hadi UFUNUO mwaka huu uone kama MUNGU hatajitukuza juu yako.Neno linasema neno la MUNGU likae kwa wingi moyoni mwako ili uwe na amani na kumshinda mtesi wetu LUSIFA(ibirisi,mlaaniwa,muongo,mwenye hila) ndiyo maana umekosa amani kwa kuwa neno la kukupa faraja halipo moyoni mwako

  anza na BWANA 2012 DADA yangu

 13. Jambo gani lililogumu la kumshinda Mungu?

  Jipe moyo, Mungu ni mwaminifu maadamu unamwamini na kuziamini kazi zake usikate tamaa wala usichoke kumwomba Mungu siku zote kwani yeye hakawii wala hachelewi.

  Kwanza umshukuru kwa mapito hayo yote, mwombe msamaha na kuwasamehe waliokukosea, mtolee Mungu dhabihu ya kushukuru ndipo umwite katika mateso yako. ameahidi kuokoa. Soma Zaburi ya 50: 14 na 23.

  Unaweza pia kupata ushauri wa kiroho na maombezi. kwani uko wapi?

  Bwana akupelekee msaada kutoka patakatifu pake na kukutegemeza kutoka mbinguni.

 14. nashukuru wapendwa kwa maombi yenu ni kwamba nimeokoka ila nahitaji msaada zaidi jinsi ya kusimama. kuna wakati nakuwa nakata tamaa sijui kwanini wakati ninasoma biblia na ahadi za Mungu juu ya matatizo nazijua ila kibinadamu kuna wakati nakuwa na uchungu sana hasa ninaponenewa lolote na mume wangu, ila yeye hajaokoka na wala si mwendaji wa kanisani na katika kujitoa nimeamua kabisa kutoka moyoni mwangu namtumikia Bwana Yesu kristo aliye hai na kuhusu kujua kumtumikia shetani wakati ninapoombewa mizimu huwa inasema inanitesa kwasababu sitaki kuwa mganga so bado naendelea kuikana na kumtegemea Mungu. ni mengi nayapitia wapendwa ni Mungu tu ananishindia naomba muendelee kunitia moyo na kuniombea nami naendelea kuzidi kuomba manake inafika wakati nakosea naomba huku nikiwa na huzuni.Mbarikiwe

 15. SHALOM,UKISOMA KWENYE BIBLIA SEHEMU TOFAUTI TOFAUTI UTAONA SWLA LA IMANI LIKIZUNGUMZIWA KARIBU KILA CHAPTER,NDUGU YANGU KATIKA KRISTO UTAKAVYO KIRI NDIVYO UTAKAVYO POKEA JAMBO LA MSINGI NATAKA NIKUELEZE/NIKUTIE MOYO NI KUHUSU HABARI ZA WATUMISHI WA MUNGU KAMA WAKINA ELIA,ELISHA MESHAKI,SHEDRA NA ABERNEGO,SAMWELI DAUDI NA WENGINE WOTE WALIPITA KATIKA MAPITO MAGUMU LAKINI KILA WLIVYOKUWA WAKIMKIRI MUNGU ALIYE HAI NDIVYO MUNGU ALIJIDHIHIRISHA KWAO MFANO MWANGALIE DAUDI ALIMWAMBIA GOLIATI,NINAKUJIA KWA JINA LA BWANA WA MAJESHI…ANGALIA ALIVYOMKIRI MUNGU KWA IMANI NI NINI KILICHOFUATA?JIBU NI USHINDI WAANGALIE SHEDRAKI MESHAKI NA ABERNEGO WALIJUA WANAENDA KWENYE MOTO NA WATAKUFA LAKINI KWA IMANI WALIMKIRI MUNGU KATIKA MAPITO MAGUMU WALIYOKUWA WAKIPITIA NA MUNGU AKAJIDHIHIRISHA KATIKATI YA TANURU LA MOTO HIVYO NDUGU YANGU MWAMINI MUNGU,UJAPOPITA KATIKATI YA BONDE LA UVULI WA MAUTI YUPO PAMOJA NA WEWE,MWANGALIE SARA ALIMWAMINI MUNGU NA MUNGU AKAJIBU,KWA JINA LA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI NINA AMURU KWA MAMLAKA NILIYOPEA UPOKE SAWA SAWA NA HITAJI LA MOYO WANGU KWA KUWA SI MM NINAISHI BALI KRISTO NDANI YANGU,SHETANI NA JESHI LAKO NAKUAMURU HUNA MAMLA JUU YA MTUMISHI WA MUNGU KUANZIA SASA NA HATA MILELE.AMEN,ENDELEA KUOMBA PIA KUAMINI.

 16. Shalomu,

  Dada Magda,

  Nimesoma maelezo yako na ninakupa pole kwa magumu unayoyapitia katika maisha yako, hata hivyo, naamini Mungu atakusaidia na kukufungua kutoka kwenye hayo magumu. Hata hivyo, nimeona nikuulize maswali machache ili kuona kama tunaweza kukusaidia kimaandiko pia.

  Umesema unahitaji maombi ili uweze kuhamishwa kutoka nguvu za giza, ningependa kujua kama umeokoka au la.

  Umesema kuwa shetani anataka umtumikie nawe hutaki kufanya kazi ya Mizimu, unaweza kufafanua kidogo kuhusu hili la kutakiwa kufanya kazi za mizimu?

  Mungu akubariki.

 17. Bwana yesu asifiwe mpendwa, huna haja ya kukiri kuteseka kama umeokoka na unajua kuwa Yesu kristo alikuwa kwa ajili yako,ukisoma katika warumi 8;31 biblia inasema bwana akiwa upande wetu hakuna lililo juu yetu na biblia pia imesema jambo hili hsaliwezekani bali kwa kufunga na kuomba, omba mpendwa funga Mungu atakujibu maana amesema sikio lake sio zito wala mkono wake sio mfupi hata usiweze kuokoa bali dhambi zetu ndio zimetutenga na yeye.jitoe kwa Mungu kikamilifu hayo yote yatakukimbia maana hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu baba ni hilo tu na tunaendelea kuomba na wewe na Mungu akubariki

 18. shika neno lake na ulitende kwa uaminifu na MUNGU atakuinua kwa yote. Baba wa mbinguni na akutimizimie haja ya moyo wako.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s