Dini vs Dhehebu

Bwana Yesu asifiwe SG, napenda kujua tofauti kati ya dini na madhehebu, nilikua mahali fulani tukaanza ubishi kwamba dini ni haya madhehebu tuliyonayo? na madhehebu sasa yatakuwa nini.

–KM, Mbeya

Advertisements

17 thoughts on “Dini vs Dhehebu

 1. Ndugu yangu Rich kidogo amenigusa na hayo majibu aliyotoa. Bado sijafahamu asili ya haya madhehebu yanayoongezeka kila kukicha. Ninachelea kusema kwamba wengi wengekuwa wanauliza chanzo cha madhehebu ya wangepigwa na butwaa. Mwandishi wa makala hii nakuomba eleza usahihi wa dini ni nini kwa kutoa ushahidi wa maandiko matakatifu na siyo maelezo ambayo yanaongeza utata juu ya dini ni nini

 2. Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu….Wokovu ni njia ya mpango wa Mungu mwenyewe kumtafuta mwanadamu….madhehebu ni hali za wanadamu kutafuta usahihi wa njia ya wokovu wa mungu.Hivyo basi wanadamu ndiyo walioleta dini na dini ndizo zilizoleta mathehebu.Wokovu au njia ya mungu ni neno lake tu,katika biblia na ndiyo njia sahihi kupita zote ya kumfikia mwenyezi mungu.Soma(zaburi 119:105).Kanisa sio dini au thehebu wala jengo fulani bali ni mkusanyiko wa wakristo yaani wa kwake yesu kristo katika kufuata na kuhubiri injili kwa wengine ili nao waijue njia ya wokovu wa mungu na kuifuata.kuongezeka kwa wasomi wengi na kukua kwa maarifa ya mwanadamu ni jambo zuri lakini kwa kiasi kikubwa sana limevuruga utaratibu wa utiifu wa mambo yahusuyo njia za wokovu wa Mungu na kuleta siasa na kushindana katika kanisa la Mungu alilolianzisha Yesu Kristo mwenyewe kwa lengo zuri.

  Hivyo basi kwa hali hiyo kanisa halishindwi na milango ya kuzimu kamwe!!..lakini wakristo inatupasa kuacha mashindano ya madhehebu na kuungana wote kwa pamoja pasipokujali tofauti zetu kwa kuwa Mungu ndiye aokoae,Soma(zaburi 68:20)..Pia tunaokolewa kwa neema wala si kwa akilizetu au matendo yetu ya haki…hakuna jambo zuri sana la haki kupita la wenzetu tunaloweza kulifanya likawa bora la kumlipa Mungu bali ni imani tu,katika Yesu Kristo na kuishi kwa uadilifu,tabia njema na upendo wa Mungu tukiongozwa na Roho wa Mungu mwenyewe…kubishana kwa wakristo kunamtukuza shetani na kuharibu kanisa la Mungu,na hilo ndilo lengo la shetani tangu mwanzo yaani kuvuruga watu wasijenge umoja wenye nguvu!!..shetani huingia akilini mwa wakristo na kuwafundisha hivi:WA THEHEBU LILE SIO KAMA SISI NA WA THEHEBU HILI SIO KAMA WALE…WALE WANAKOSEA NA KWA HIYO WATAENDA MOTONI.,NYINYI NDIO HAKI MNAOMLIPA MUNGU IBADA YA KWELI PEKEENU MSIUNGANE NAO WALE KWA KUWA NI WA MOTONI!!…kwa hiyo viongozi wengi wa makanisa hutumbukia sana katika mtego huu wa ibilisi na kusahau upendo aliotuachia yesu kristo wa kupendana na kutokuhukumu wenzetu.Wakristo wote ni:CHUMVI YA ULIMWENGU,Sasa chumvi hii ikialibika itatiwa nini tena ili ikolee?..WAKRISTO NI NURU YA ULIMWENGU,MJI(DUNIA)HAUTOSITIRIKA KAMA NURU YETU HAITAANGAZA.Tujenge tabia ya kujenga na si tabia ya kubomoa!!mwisho kabisa kanisa ni wewe au mimi mwenyewe,omba roho wa Mungu akuongoze ili uwe na serikali yako ya wokovu na ahadi na Mungu katika kumtumikia kwa uwaminifu pasipo kumuacha elimu yaani Biblia maana ndiko zitokako chemchem za uzima wako.Kumbuka yesu atakaporudi tena hatutotwaliwa kwa vikundi au makanisa bali kila mmoja atatoa habari yake mwenyewe.mbarikiwe.

 3. Bwana Yesu Apewe Sifa!
  Nashukuru kwa tafsiri za neno Dini zilizopita hapo juu, nami ngoja nieleze maana ya Dini kwa ufahamu niliopewa.
  Tukisoma Yakobo 1:26,27 yasema “Mtu akidhani anayo Dini, Wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya Moyoni mwake, Dini yake mtu huyo HAIFAI . Dini iliyo safi, isiyonataka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa”

  Kwa habari hiyo twajua Dini ni huduma ya matendo mazuri yanayomuonesha mtu kua anao Moyo wa kujitoa na kuchukuliana udhaifu na wengine walio na udhaifu wowote, yatima, wajane, wafungwa, dhaifu wa imani na wote ambao hawajapata neema bado ya kuokoka.

 4. Kwanza hapa inabidi tujuwe nini maana ya dini, kisha madhehebu?
  Tuseme dini ni njia!!, na Yesu anasema yeye ni njia, kwa maana iliyowazi hapa tunajifunza dini ni Yesu!!, Alaa kumbe maana ya dini ni yesu, maana dini ni njia na njia ni yesu.
  Kwa maana ya hapo juu, bado maana ya dini haijajulikana. Maana ya Yesu si dini ingawa Yesu kasema yeye ni njia.

  Nini basi dini?
  Dini ni mfumo mzima wa maisha (uliokusanya kila kitu, kitendo au kauli) ambao mtu kaamuwa kuufata mfumo huo. Mfumo huo unaweza kukufikisha kwa ufalme wa mungu (kama mfumo wako wa maisha ni ule anaoutaka mungu kupitia mafundisho ya manabii), Au ukakufikisha katika makamio ya Mungu, endapo utaacha mfumo sahihi wa mafundisho ya manabii.

  Kwa maana hiyo hapo juu, ina maana kila mtu anayo dini, kwani kila mtu hapa duniani ni lazima awe na utaratibu wa kuendesha maisha yake. (mfano; mfumo wa njia zako za kutafutia riziki..je ni halili au haramu, mfumo wa mahusiano na binadamu wenzako, mazungumzo yako ni ya kweli au uongo n.k yote haya yanamaanisha dini yako).

  Ala! kumbe basi, dini zipo za aina mbili kuu
  1. Dini ya Mungu: Iliyofundishwa na mitume wake wote (kuanzia Nabii Adam mpaka Mtume wa Mwisho). Hii ndio dini sahihi itakayomfikisha mtu katika ufalme wa Mungu
  2. Dini za Kitwaghuti: Hizi ni dini zilizobuniwa na wanadamu ili kukidhi maslaha yao na sio kumrisha Mungu: Dini hizi hazitakubaliwa mbele ya Mungu, na wafuasi wake watapata hasara kubwa.

  Nini maana ya madhehebu?
  Madhehebu inajitokeza pale waumini wa dini fulani wanapotafautiana juu ya msingi wa jambo fulani katika dini.
  Kwa hio, watu wanaweza kuwa wa dini moja, lakini madhehebu tafauti. Msingi mkuu wa imani yao unakuwa mmoja (Wote wanamuamini Mungu huyo huyo na mtume huyo huyo) lakini katika masuala ya ibada zao yakatafautiana, kutokana na ufahamu wa maandiko

 5. Ndugu Noel Msanjila, nimefurahia mchango wako. Katika maelezo yako umesema “Dini na madhehebu zinawagawa watu tu lakini kama mtu atafikiri juu ya neno kama liagizavyo kwamba iweni watakatifu, na akaendelea kutafakari kwamba nawezaje kuwa mtakatifu duniani na katika kuwa mtakatifu kwa kudhamiria,nasema lazima mungu atamfungua nakumuongoza hatimae awe mtakatifu NAKUACHANA NA HABARI YA DINI NA MADHEHEBU, AMBAYO YAMEASISIWA NA WATU WALA MUNGU HAYUMO KTK HAYO..” Kwa sababu dini na madhehebu ni mpango wa shetani Sasa naomba mnisaidie kufahamu, JE MWANADAMU AWEZA KUINGIA MBINGUNI ASIPOJIKITA KATIKA DINI WALA DHEHEBU LOLOTE?

  Naendelea kujifunza

 6. Ndugu Noel Msanjila,

  Nimeyasoma maelezo uliyoyatoa, ni mazuri na pia nauona uchungu ulionao! Pole sana!!

  Najua katika uchungu mambo mengi yanaweza kujivuruga hata lulu zako ukazikuta matopeni.

  Ukweli ni kwamba unapokiona kitu FEKI, basi unapaswa kujua kuwa kile HALISI kitakuwepo pia! HALISI hutangulia ndipo FEKI hufuatia tena katika viwango vingi ikijitafuta kufikia ule uhalisi bila mafanikio. Ndio maana bidhaa feki huwa ni nyingi zikitofautiana tofautiana licha ya kwamba zote zinaigiza kitu kimoja. Basi na DINI pia. Iko ile DINI ya zamani ile aliyopewa Adam!

  Ubarikiwe!

 7. Asanteni kwa maelezo yenu,Dini na Madhehebu siyo mpango wa Mungu,huo ni mpango kamili wa shetani ili kuwagawa watu,maana hta yeye shetani anjua kwamba kwamba umoja ni nguvu utengano ni udhaifu,ndio maana akaleta dini na madhehebu na amefankiwa kutugawa wanadamu hilo halina ubishi,kwa maana kila mmoja anaona yuko sahihi kwa madhehebu na dini yake kwahiyo anamdharau mwenziwe ambayo tayari shetani amefanikiwa kuweka dhambi hiyo ya dharau.Swali lakujiuliza ambalo jibu lake nijepesi tu kama Mungu ni mmoja,kwa nini kuwepo na madhehebu tofauti,kwa maana hiyo kwa maana nyepesi tu,tujue kwamba kila dini na madhehebu ina Mungu na mungu wake,haiwezekani Mungu kama ni mmoja kwa madhehebu na dini zote lakini akatoa amri tofauti wakati mbingu ni moja tunayotarajia kuikaa.

  Eti Mungu mmoja halafu aamrishe hawa waoe wake wengi na hawa wanasema ‘ktk dini yetu tunaruhusiwa kuoa mke mmoja,hawa wanasema ktk madhehebu yetu sisi tunabatiza watoto wadogo lakini hawa wengine haturuhusiwi kubatiza watoto wadogo,sisi tunasali jumamosi, sisi jpili na sisi any time,sisi mtu akifa tunamuombea kwa Mungu amuweke mahali pema peponi, na wengine wanasema Mungu wetu haruhusu kumwombea mfu wala sala hiyo haikubali kama mtu hakutubu mwenyewe wakati akiwa hai basi atajiju,wengine wanasema tunaamini Maria ni mama wa Mungu na ametuagiza tusali lozali wakati wengine wanaona hata kushika lozali au tasbihi ni kuabudu sanamu,wengine wanaona swali lakusema nimeokoka ni kujikweza hupaswi kusema umeokoka,wengine wanaamini pasipo kuokoka ni hakuna mjadala ni kwamba utaenda motoni yapo mambo mengi ambayo yanatutofautisha nafikiri nikiyaorodhesha hapa ni mengi yanayoleta tofauti.

  Fikiri kama wote tungekuwa tunaamini kitu kimoja neno madhehebu na dini nakuonana kila mtu ni bora zaidi ya mwingine kusingekuwepo,ndiyo maana nasema NENO madhehebu na dini ni hila za shetani kuwafanya watu wachanganyikiwe,hata wengine ukiwaambia Mungu hatauliza dini ya mtu wala madhehebu yake siku ya mwisho, bali ataangalia UTAKATIFU ambao unapatikana baada ya mtu kutubu dhambi nakudhamiria nakuazimia kuziacha, DINI NA MADHEHEBU ZINAWAGAWA WATU TU LAKINI KAMA MTU ATAFIKIRI JUU YA NENO KAMA LIAGIZAVYO KWAMBA IWENI WATAKATIFU, NA AKAENDELEA KUTAFAKARI KWAMBA NAWEZAJE KUWA MTAKATIFU DUNIANI NA KATIKA KUWA MTAKATIFU KWA KUDHAMIRIA,NASEMA LAZIMA MUNGU ATAMFUNGUA NAKUMUONGOZA HATIMAE AWE MTAKATIFU NAKUACHANA NA HABARI YA DINI NA MADHEHEBU, AMBAYO YAMEASISIWA NA WATU WALA MUNGU HAYUMO KTK HAYO.

 8. Shalom ndg Bwaya
  kwa mtazamo wangu, hakuna tofauti,
  imani au spirituality naona ndio dini hiyo, kwasababu ukiulizwa hata ktk form yoyote tu kwa kifupi dini yako ukitaja Mkristo tayari mtu anajua we unaamini Yesu ni Mungu wako vivyo kwa hizo dini nyingine. Tunajifunza

 9. Rosemary,

  Je, kuna tofauti yoyote kati ya Imani (spirituality) na Dini? Je, inawezekana kuwa na kimojawapo pasipo kingine? Hapa nina maana kuwa na imani bila dini au kinyume chake, yaani kuwa na dini bila imani?

 10. Shalom wapendwa
  ninajifunza mengi kwenu, kwa ufahamu wangu ni kuwa dini ni imani au kile unachoamani, kuna dini ya kishetani, islam, budha, bahai, ukristo, mizimu nk
  Dhehebu ni sehemu tu katika kile unachoamini, mfano wa Kristo ndio kuna Lutheran, Baptist, Moravian, Pentecost, Sabato nk

  Islam kuna Ishmailia, Sunni nk nk
  Ni kweli dini ni kutoka kwa Mungu, Mungu ndiye alimwamuru Adamu amtii huko ni kumwamini, aliposhindwa alimfukuza karibu nae. Kisha limwita tena Abrahamu atoke na aende atakakomwonyesha hii ni Imani na hivyo ni dini, kupingana na imani uliyofundishwa ni kuamini dini nyingine, madhehebu hutokana na taratibu nyingine nzuri nyingine mbaya lakini ktk imani moja.

  Tunajifunza

 11. Ndg Bwaya,

  Ndicho ninachomaanisha ndg Bwaya, Mungu ndiye aliyemletea Adamu Dini. usisahau kuwa Adamu aliumbwa na Mungu kwa hiyo vyote alivyo navyo kapewa na Mungu. Hata tunaona Mungu akiyakataa mawazo ya Adamu pale alipojitengenezea vazi la majani, akampa vazi la ngozi badala yake. ukienda mbele utawakuta Kaini na Habili wakifanya ibada, kule kujipatanisha na Mungu. Kaini alifanya ibada yake pasipo ufunuo, aliendelea kutumia akili zake akijiaminisha kuwa Mungu ni lazima aipokee. Ibada yake ilikataliwa kwa sababu Mungu hawajibiki kwa mawazo ya mwanadamu hata yawe mazuri vipi! Habili aliifanya ibada yake kwa ufunuo, yaani aliyafuata maelekezo aliyopewa na Mungu aliyeiasisi ibada. ‘Kwa imani, Habili alimtolea Mungu sadaka iliyo bora’ basi imani ni mawasiliano kati ya Mungu na mwaminio.

  Dini ni ustaarabu. Unapoingia katika Dini yoyote ile, hukulazimu kuuachaustaarabu na mila ulizotoka nazo kutoka huko utokako na kuuchukua huu mpya katika mambo yote. huwezi kuuchanganya! Dini ndiyo ustaarabu na mila mpya!!

  Bwana akubariki katika yote yenye kumtukuza Yeye!!

 12. Ndugu Lwembe,

  Asante sana kwa mtazamo wako wa kibiblia kuhusu dini. Hata hivyo, sina hakika kama nimekuelewa isivyo.
  Je, unamaanisha (katika maelezo yako) kwamba Mungu ndiye ALIYEMLETEA mwanadamu DINI? Mimi nilifikiri tofauti! Pili. Je, Kuna uhusiano wowote baina ya utamaduni (mila, desturi nk) na Neno la Mungu (yaani ujumbe wa Yesu kwa mwanadamu)?

  Yesu akubariki!

 13. Ninaamini ndg Bwaya ametoa tafsiri inayo kidhi haja na shauku ya kujua Dini ni nini na Dhehebu nini. Pia ameonesha uhusiano wa mambo hayo katika mtazamo ulio rahisi.

  Nikiondoka katika hayo maelezo ya msingi yahusuyo mambo hayo, basi napenda kulikazia hilo katika mtazamo wa ki-Biblia.

  Dini, katika namna yoyote ile utakayoiangalia, ni jambo linalohusu uhusiano kati ya Mungu na binadamu. Kwa hiyo ilimradi liko hivyo, basi ili kulijua ni nini, itatulazimu kurudi kule Mwanzo. Huko ndiko kuna majibu ya asili ya yote tunayoyaona hapa duniani. Yote tunayoyaona, hata kama tutayaona ni mapya, ukweli ni kwamba si mapya labda ni mabadiliko ya hali tu yanayotufanya tuyadhanie kuwa ni mapya. Basi hata hili la Dini na Dhehebu si jipya, litakuwepo huko Mwanzo, maana hicho ndicho kitabu cha Mbegu!

  Dini ni vazi au kifuniko, yaani ‘covering’. Tukirudi kule nyuma tunawaona Adamu na Hawa wakiwa uchi nao hawakuwa na tatizo lolote lile kimtazamo juu ya hali hiyo. Tunawaona ni wenye furaha na amani nao wakiendelea na shughuli zao bustanini kama lilivyokuwa kusudi la Mungu. Hawa walikuwa wamefunikwa na Neno la Mungu ambalo ndilo walilokuwa wakiliishi humo Bustanini. Basi unapokuwa umefunikwa na Neno la Mungu, maisha yako huwa ni shwari kama mtoto mdogo. Hebu mtazame mtoto mdogo jinsi alivyo huru na maumbile. Yeye huweza hata kucheza na nyoka au ‘nge nk. Akiisikia sauti ya mama yake, basi hata kama ametoka kuoga na hajavalishwa nguo, atakimbia aje amtafute mamaye hata ikiwa ni mbele ya kundi la watu. Subiri afike miaka 18 halafu uingie chumbani kwake bila hodi wakati akijitayarisha kuvaa, uone atafanya nini!! Basi, kufunikwa na Neno la Mungu ndiyo Dini ya asili aliyotupa Mungu tuifuate siku alipo tuumba. Maana yeye ametupa uhuru wa utashi naye akatuwekea Neno lake litufunike ili tuwe katika harmony na maumbile yote. Nasi kwa hicho kifuniko au upako, maumbile yote yalitutii.

  Baada ya kuliacha Hilo Neno, tukawa tumelivua hilo vazi. Yaani tukaiacha ile Dini yetu ya asili, lile Neno. Basi lilipoondoka ndipo wakajiona kuwa wako uchi! Wakaanza kutumia akili zao wenyewe katika kutafuta namna ya kujihifadhi. Wakatengeneza Dini yao mpya ya Majani (Mwa 3:7 “ … wakashona majani ya miti wakajifanyia nguo). Hata Mungu alipowatembelea wakajificha maana ile Dini ya Majani haikuweza kuwasitiri pale Mungu alipowakaribia. Basi Mungu ilimbidi awatengenezee vazi jingine, Mwa 3:21 “Bwana Mungu akawafanyia Adam na mkewe mavazi ya ngozi akawavika”. Kwa vazi lao hilo jipya ambalo sasa laweza kuwasitiri hata waweze kuonana na Mungu, ili lazimu Mwanakondoo achinjwe kisha ngozi yake ndiyo wavishwe, yaani INJILI!!! Hiyo ndiyo Dini tuliyopewa. Hebu litazame jambo hilo pale katika Warumi 3: 21-26, utaliona hilo vazi tulilovikwa. Hilo vazi la ngozi walilovishwa Adam na mkewe likiwa mfano wa hili tunalovishwa sisi leo Vazi la Haki kupitia Sadaka iliyotolewa Msalabani nasi kuvishwa!
  Hizi dini nyingine unazoziona, ni uigizaji tu wa hiyo Dini. Nayo madhehebu yanatokana na uigizaji huo. Kwa tafsiri rahisi, Dhehebu ni jamii iliyokubaliana yenyewe juu ya utaratibu wa kumwabudu Mungu ulio bora kuliko wa wengine. Kwa tafsiri yake tu yaonesha chimbuko lake ni kutumia akili, yale majani. Basi pale unapoyaona matumizi ya akili yanaingia katika jambo lolote lile, mgongano wa mawazo ni lazima utokee. Nayo migongano hiyo ya mawazo ndio inayozalisha madhehebu pale tunapokuwa tumetoka katika ile DINI ya Asili na kuingia katika Dini Hybrid ambazo idadi yake pia ni ndefu; tukianza na dini ya Ufarisayo, Ukristo (ambayo ndani yake mna migongano ya mawazo yaani madhehebu zaidi ya 5000), Uisilamu (nao ndani yake mna madhehebu mengi tu), Ubudha, Utao, Upagani ambao nao ndani yake mna madhehebu mengi tu yaani zile kabila na mila zake) nk. Kwa hiyo hizi Dini Hybrid ndizo ndani yake kuna machipuo ya madhehebu, yaani Dini yoyote iliyojitengeneza nje ya lile Neno, hiyo ni Mbegu ya Hitilafu – seed of discrepancy. Basi mapando ya mbegu hiyo huendelea kujizalisha katika namna ya Madhehebu, au Huduma nk.

  Kwa hiyo kwa kifupi, Mungu ametupatia Dini moja tu ili tuweze kuwa na mawasilano naye tena, nayo ni kupitia Damu ya Mwanakondoo.

  Nayo Dini ndiyo ukomo wa ustaarabu. Yaani Dini ndiyo inayotutambulisha. Utamaduni wetu ni Dini yetu. Hata ukiangalia tu ustaarabu uliopo, utaona kwa sehemu kubwa umejikita katika dini zetu. Waisilamu wanazo hijabu zao, wahindu, wapagani kwa mila zao nk. Katika haya makundi yote ya dini ni kundi la Wakristo tu katika uvuguvugu tuliomo ndio tusiojua hata ustaarabu wa Dini yetu! Hatujui hata tujisitiri vipi miili yetu licha ya mafundisho yote yaliyomo ndani ya Biblia. Utawaona wachungaji wakituongoza kwa hisia tu. Leo utamkuta mzee wa kanisa kasimama mlangoni anawagawia khanga wanawake waliokuja kanisani wametinga vimini, kanisa jingine wanawaambia wavae tu vimini vyao kwani Mungu haangalii mavazi na mambo mengi ya aibu. Hiyo ndiyo Dini ya kuigiza na madhehebu yake yanavyo ishamirisha!

  Mbarikiwe nyote!

 14. Cecilia, labda nichangie tena.

  Kimsingi, Yesu mwenyewe hakuja kuanzisha dini kwa maana ya taasisi! Wala hajawahi kuonyesha nia hiyo! Kwanza Yeye mwenyewe alihudhuria mikusanyiko ya kidini iliyokuwepo, alishiriki sikukuu za kidini na kadhalika na kadhalika!

  Lakini kwa sababu dini ni sehemu ya HULKA za mwanadamu, baada ya Yeye kuondoka, wafuasi wake walijitengenezea dini (kwa maana ya mfumo) unaotafuta kushika mafundisho yake na kuwafanya watu wengine kuwa wanafunzi wake!

  Nilitangulia kusema, huwezi kuzungumzia kiu/shauku ya mwanadamu kuhusiana na Mungu, halafu ukaiweka dini pembeni! Huwezi kukusanyika na wenzako wenye imani kama ya kwako, mkifuata taratibu fulani za kiimani, mkiwa na makatazo fulani (don’t’s) halafu ukakanusha kwamba wewe si mfuasi wa dini!

  Wanaokana kwamba Ukristo si dini pengine wana hoja. Kwamba Ukristo ni mahusiano ya Mungu na mwanadamu, hilo ni sawa. Hata hivyo, kule kuwa na tunu za pamoja (values), kule kujipambanua kutoka kwenye mifumo mingine ya kiimani, na kuamini kuwa unachoamini ndicho kinachotakiwa, hiyo ndiyo dini!

  Ninachokisema ni hiki: Pamoja na kuwa anayetafutwa (Yesu) hakuwahi kuwa na nia ya kutengeneza dini, hata hivyo wanaomtafuta (wanaomfuata na kutafuta kuwa kama Yeye) wamejikuta wakijitengenezea mfumo wa kumtafuta! Ndiyo maana maneno “Ukristo”, “Wakristo” na kadhalika yanaonekana baada ya kuondoka kwa Yesu.

  Hiyo yaweza kuwa sehemu ya sababu kwa nini hata hao wanaomtafuta Yesu wamejikuta wakitofautiana mitizamo. Mitizamo hiyo tofauti, ambayo ndiyo madhehebu, ni sehemu ya jibu la karibu kuwa Ukristo ni dini.

 15. Asante mtoa mada, naomba nitaje kwa mifano dini ni zipi, KKKT, EAGT, PAG, TAG, Anglican, RC nk, hizi ni dini. Madhehebu ni doctrine za hizo dini. Ukristo kamwe sio dini, Yesu hakuleta dini duniani. Naomba tusaidiane katika hili. Mubarikiwe

 16. Dini ni utamaduni. Ni sehemu ya ustaarabu wa jamii unaojaribu kuhusianisha maisha ya watu na ulimwengu usioonekana ama nguvu zilizo juu ya uwezo wa mwanadamu. Ulimwengu huu usioonekana waweza kuwa kwa jinsi ya miungu, mizimu ama namna fulani ya hofu (uchaji) za kiroho.

  Ndio kusema, hatua zozote anazochukua mwanadamu kujaribu “kujiunganisha” na kile anachokihisi kuwa “nguvu” zilizo juu ya uanadamu wake, ili kujitafutia ridhiko/majibu ya maswali yanayokuhusu kusudi la uwepo wake hapa duniani, ndicho kinachoitwa dini.
  Kijamii, dini ni mfumo wa imani (beliefs) na ibada (rituals) unaongoza mtindo wa maisha ya watu na hivyo kuwafanya watu hawa kuwa na mtazamo unaofanana wa masuala ya kiroho na hivyo kuwaweka pamoja (kama waumini). Hapa nina maana ya dini kama TAASISI yenye turufu katika masuala kama vile maadili, tafsiri ya wema na uovu na kadhalika.

  Hata hivyo lengo hili la kuwaweka watu pamoja, mara nyingi huishia kusababisha tofauti kubwa zinazojenga mifumo inayotofautiana ya kidini. Tofauti hizi kimsingi ndizo zinazoeleza uwapo wa dini zilizopo kuanzia zile za asili (upagani) hadi hizi zilizomaarufu sana.

  Ndani ya dini hizi, bado hujitokeza tofauti ndogondogo ambazo huzaa namna tofauti za ibada kiisha kutengeneza vijimfumo vidogo vya kidini viitwavyo madhehebu. Hivyo, wanachama wa madhehebu mawili huwa ni wanadini wasioelewana katika baadhi ya mambo!

  Je, dini zina msaada kwa mwanadamu? Je, Ukristo ni dini? Jibu la swali hili, litamtegemea anayejibu.

 17. Bwana Yesu asifiwe,
  Kwa uelewa wangu, dini ni njia ya kumfuata mwanyezi Mungu kupitia watumishi wake aliowatuma kutuletea mafundisho yake.
  Kwetu sisi Wakristo tunaamini njia ya kufika kwa Mungu ni Kristo, ndie njia ya uzima na ukweli bila yeye hatuwez kufika kwa Baba. Ndio maana Tuna dini yetu ya Ukristo.
  Waislam kadhalika wana iman zao zilizoletwa na Muhamad kwamba Uislam ndio njia ya kwenda kwa Mungu wao …dini ya uislam.
  NB: Upagani siyo dini. wapagan hawafuati Ukristo wala uislam.
  sasa ndani ya hiz dini mbili kuna migawanyako ambayo tunaita madhehebu
  Mfano katika ukristo kuna dhaebu la Anglican, Pentecost, Catholic ,Sabato etc
  Ktk uisalam kuna Shekha, hamadia etc

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s