Tazama kwa jicho la Imani!

Tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele ( 2 wakorintho 4:18 )

Imani ni ya roho, siyo ya hisia. Kama wakristo tunatawala na kushinda katika maisha katika kanuni za imani. Tunafikia mafanikio yetu, ushindi, maendeleo katika maisha kwa kuchochea kanuni fulani za kiroho ambazo tunapata katika Neno la Mungu. Moja ya kanuni hizo ni kuona kwa ”jicho la Imani” kuuona muujiza wako kwanza ndani; hiyo inaitwa ”KUONA VISIVYOONEKANA!”

kabla ya kufunuliwa kimwili kwa Utukufu na Nguvu ya Mungu katika maisha yako, unapashwa kuona kwanza ndani yako. Mara tu unapoweza kuona katika roho yako kwa macho ya imani, basi kitu hicho tayari ni chako.

Huwezi kuwanacho nje kama hujawa nacho kwanza ndani. Hapa ndipo baadhi wamekosa, wanataka kuona kwanza kwa macho yao ya kimwili kabla ya kuita halisi kile ambacho. Mungu ameahidi. Hiyo siyo imani

Imani ni kuita halisi kile ambacho hisia za mwili haziwezi kutambua.

Ni kama mwanamke mjamzito; itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kusema, ” Mimi simuoni mtoto; hiyo inamaana kwamba hakuna kitu katika tumbo lake.” Mtoto yupo ndani hata kama hakuna mtu anayeweza kumuona. hata kabla ya tumbo kuwa kubwa, mtoto alikuwepo ndani wakati wote.Tumbo limekuwa kubwa tu kwa sababu mtoto ambaye yupo ndani tayari  anakuwa mkubwa. Wakati wa mwisho wa kipindi cha ujauzito mtoto atazaliwa.

Katika njia hiyo hiyo, huo ujauzito wa muujiza ulionao hiyo baraka ambayo umekwishaona na kuchukua milki yake katika roho itakuwa wazi na  kutukia kama ukikataa kusita na kuyumba katika imani yako. Kwa macho yako ya imani, ona hiyo kazi mpya unayoitaka, ona mafanikio yako, afya, amani na maendeleo,wokovu wa marafiki na wapedwa.

Anza kutangaza kwa kinywa chako hayo ambayo umeshayaona ndani; siyo ili yatokee, bali kwa sababu unajua  kwamba katika  ulimwengu wa Imani tayari yapo!

Malkia Pamela

5 thoughts on “Tazama kwa jicho la Imani!

  1. Unachokisema mtumishi wa Mungu ni kweli kabisa. Mwaka huu liwe ombi la kila mmoja wetu macho yetu ya rohoni (ya imani) yawe wazi kila wakati hata tulalapo yabaki yanatazama. Mi Mungu mwaka huu nipe macho nione, macho ya rohoni.

  2. Ni kweli kwamba, kila kitu unayoiwazia kuitaka sana maishani ni kama, mama mjamzito nayataka mtu ashikilie imani kuwa atamzaa huyo mtoto. Iliafanikiwe.

  3. Yaani nimejifunza kitu cha pekee kuona kwa jicho la imani yaan kuona jibu la hitaji hata Kama halijawa dhahiri. Yaani nimeona nguvu ya ukiri duh nimeipenda hii Mungu awabariki kwa hili.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s