Malezi kwa Mkristo Mchanga

Kuna mkutano wa Injili ulifanyika katika kitongoji cha Ndala, mkoani  Tabora. Katika watu waliookoka alikuwepo pia kijana mmoja. Siku ya tatu baada ya kuokoka kwake, wakati mkutano huo bado unaendelea, alijiunga katika kucheza wakati wa mapambio ya kusifu.  Yeye alipoanza kucheza alikuwa anataka kucheza na mwanamke/msichana kama wafanyavyo kule disco: wawili wawili!

Wakati anaendelea kulazimisha msichana wa kucheza naye, kuna kiongozi mmoja wa kanisani alimuona kisha akamuita na kumwambia “Umecheza kiasi cha kutosha, hebu njoo huku nikuonyeshe kazi nyingine!”.  Kijana huyo alipewa kazi ya kupanga panga vitu sehemu ya kukaa mhubiri hadi kipindi cha sifa kikaisha.

Je, hatua hiyo iliyochukuliwa dhidi yake ilikuwa sahihi? Kama ingekuwa ni wewe uliyemuona kijana huyo ungechukua hatua gani?

Advertisements

4 thoughts on “Malezi kwa Mkristo Mchanga

  1. Cha msingi wamuelimishe juu ya kucheza mziki wa injili tofauti na mziki wa mataifa

  2. Mimi ninafikiri tukio hilo linaonyesha jambo kubwa zaidi. Sehemu kubwa ya muziki wa injili hivi leo, huo tunaoupiga katika vipindi vya “sifa na kuabudu”, unaburudisha nafsi / hisia na miili yetu zaidi kuliko kutusogeza mbele za Mungu katika ibada itokayo rohoni mwetu. Wakati ambapo ninaunga mkono hatua kiongozi huyo wa kanisa aliyoichukua kwa kijana huyo, hapana budi kwenda mbali zaidi ya hapo. Waangalie jinsi wanavyoendesha sifa na ibada, na pia watoe mafundisho sahihi ya mambo hayo, na kufanya kwa vitendo pia. Niishie hapo kwa sasa….

  3. Kwangu mimi, na hisi hiyo ni hatua sawa iliyochukuliwa kwa kijana huyo. Lakini kumkanya vijana wasifanye hivyo si rahisi kwa hivyo ni vizuri. Wachungaji wa Mungu wawe na hekima hapo.

    Wanaweza kuhubiri kwa kanisa na mikusanyiko ya vijana ili wakikanywa hivyo watahisi, uzuri wa kufikiria kabla watende jambo kama hilo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s