Mahusiano kwa vijana kuelekea ndoa!

Kumekuwa na theology nyingi sana kuhusu kuanzisha mahusiano, ambazo nyingi ni za uzoefu wa watu binafsi hasa wasiona MUNGU, au wale wanaofuata DINI tu. Nitajaribu kuzungumzia kwa kirefu zaidi kuanzisha mahusiano kwa vijana waliookoka kutakuwa na contents zifuatazo

– Mahusiano kwa vijana wasiookoka na athari zake
– Mahusiano kwa vijana waliookoka
– Maandalizi kabla ya uchumba au ndoa kwa vijana wa kike na wakiume,
– Hatua za mwanzo kabla ya uchumba
– Kupata mchumba toka kwa BWANA
– Dhana ya upendo
– Utaratibu wa kanisa katika hatua za uchumba, n.k

Lakini Kwa ufupi nielezee kuhusu mahusiano yasiyo na MUNGU.

1. *MAHUSIANO KWA VIJANA WASIOOKOKA NA ATHARI ZAKE:*

Vijana wengi ambao hawajaokoka huwa hawana hofu ya Mungu ndani yao, hivyo wanakuwa na maamuzi yoyote kuhusu kufanya dhambi, ikiwa ni pamoja na kufanya ngono pasipokupata hukumu ndani ya dhamiri zao, Sababu yake kubwa BIBILIA inasema kwamba dhamiri zao zimekufa kwani wamesha kuwa wafu japo watembea. Matakwa Yao wenyewe yasiyo na kujali kuwa hili ni kosa mbele za Mungu au si kosa ndio wanayafanya.

*KUFUATA MATAKWA YAO NA ATHARI ZAKE:***

*Uharibifu na magonjwa:*

Kuna uharibifu mkubwa ambao hujitokeza katika mahusiano ambayo hufuatwa na vijana wasio na hofu ya Mungu.

– Kupata mimba katika umri mdogo na kukatishwa masomo (wasichana)

– Kupata magonjwa ambayo hutokana na zinaa, kama vile (Ukimwi), n.k.

*Kukosa mwelekeo sahihi:*

– Pindi vijana wanapokatishwa masomo, hukosa mwelekeo sahihi wa maisha yao. Na hata baadaye wanapokuwa hawana elimu, huishia kujiingiza katika makundi mabaya.

– Kujiingiza katika (ukahaba) kwa kujiuza miili yao na hata kupata mahitaji yao (wasichana).

– Kujeruhiana baada ya kuchokana kimapenzi kwa kuachana bila taratibuKupata watoto wa mitaani

– Kuanzisha mahusiano mengine na msichana au mvulana mwingine hatakama hawajatarakiana. Na mengine mengi sana

– Kujiingiza katika makundi mabaya ya uvutaji bangi na utumiaji wa madawa ya kulevya na vitendo vya ujambazi na matokeo yake ni kifo.

1. *MAHUSIANO KWA VIJANA WALIOOKOKA*

*(Mungu ndiye Mhusika mkuu)*

Vijana wengi waliookoka, huishi maisha matakatifu ambayo humpendeza Mungu. Na pia hujiepusha kujiingiza katika vitendo vya kumchukiza Mungu Kama walivyo watu wa mataifa. Hasa pindi ambacho tamaa katika miili yao hazijaanza kuamshwa. Japo kuwa wengine wameokoka wakiwa katika umri mkubwa na waliishi isipositahili lakini wakiokoka YESU huingia ndani yao na kuzichukua zile kiu za dhambi zao.

* [Waefeso 4:22-24, inasema, Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani,unaoharibika kwa kuzifuata tama zenye kudanganya.(23) Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu. (24) Mkavae utu mpya,ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

* *Kuna mambo mengi ambayo kama vijana tuliookoka tunatakiwa kujiepusha

nayo, ili tusije tukaingia katika majaribu na kuangukia dhambini kingono.

i. *Simu za Mikononi*:

Simu za mikononi, ni jambo moja wapo ambalo linaweza kuchangia mabinti tukawa na uhusiano wa karibu sana na kijana wa kiume na matokeo yake kuvuka mipaka na kumsahau Mungu, mfano, tunaweza kujikuta tunatumiana message za kutaniana na baadaye ule utani ukaanza kuleta hisia tofauti baina yetu na baadaye tukaunda kitu, na tukaamua kufanya kweli.

* ii. **Matumizi ya mitandao ya internet.*

Hili ni janga kuu na ni kubwa sana, maana vijana wengi wamekuwa wakidanganyika kwa kuangalia picha ngono kwenye mitandao na video za ngono kwenye simu na casseti. Hivyo hili linatupasa kujiepusha Sana, ili lisitujengee akili dumavu(ukiangalia picha chafu hizo utaishia kwenye kujichua, na kujichua kunaharibu akili kwa asilimia 90%, EPUKA). pia Matumizi mabaya ya Facebook, na technology nyingine zinazokuwa kwa kasi kubwa kabisa kwa sasa.

iii. *Kwenda kuhudumu vijana wa jinsia tofauti mkiwa wawili: *

* *Tunaweza tukawa na ukaribu sana kama kaka na dada, na baadaye tukaanza kwenda kuhudumu/kushuhudia pamoja ,na itafikia hatua tutazoeana na hata kutaka kuwa na muda wa kukaa pamoja na kujifunza neno na hata kuomba pamoja, labda nyumbani kwa kijana wa kike au kijana wa kiume. Na matokeo yake tukaanza kuwa na hisia tofauti na kuona kuwa tunapendana na kuwa (tumeona maono) tutakuja kuoana, au binti akawa na hisia tofauti na kuhisi kuwa kijana wa kiume anampenda wakati sivyo. Na baadaye ikionekana kuwa yule kijana anachumbia mtu mwingine, yule binti ataumia sana na matokeo yake kuamua kuacha wokovu. Na pia tunapoenda kushuhudia inatakiwa kuwa watu watatu au zaidi ,akiwepo mmoja wa jinsia tofauti na wawili wa jinsi moja ni nzuri zaidi.Au wote tukawa jinsia moja.Hiyo inaleta ushuhuda mzuri kwa wale tutakao kuwa tunawashuhudia neno la Mungu, hawatakuwa na maswali mengi kuhusiana na sisi.Pia kukutana kwenye hotels/ hostel au mahali pa kificho kwa ajili ya kujadili huduma au appointment huku ukijua mtakuwa wawili, au kusafiri kikazi na mwanamke/mwanamme asiyeokoka au ameokoka na mkapanga HOTELI MOJA, hapo ni hatari sana.

* iv. **Binti kujiachia kwa mvulana kupita kawaida:

* *Binti aliyeokoka anatakiwa kutumia akili katika uhusiano wake na vijana wa kiume. Sawa kuwa na kaka mpendwa siyo mbaya ila inatakiwa ukaribu wetu usivuke mipaka [Mfano,utaona binti anamzoea sana kijana (kaka) na kufikia hatua kumtembelea kijana katika chumba chake anachokaa.Na hata kuanza kumsaidia kazi za ndani kama vile kudeki,kupika na hata kufua kwa kigezo cha (mpendwa).Huko ndiko binti kujiachia kwa mvulana.Kwa sababu unapoenda kwake na yeye anaishi peke yake unategemea nini? Na yeye ni mwanadamu kama wanadamu wengine anahisia kama wanaume wengine japo kuwa ameokoka, kufanya kwako hivyo hata kama ulikuwa hauna nia mbaya kutomuingiza majaribuni kijana huyo. Na matokeo yake yatakuwa mabaya na machukizo mbele za Mungu

(kuanguka dhambini kingono, tena mtaanza na kukumbatiana, then kubusiana baadae ulimini). Vyote hivyo havistahili kutajwa kwa watakatifu wa Bwana.

* v. **Uhuru wa kuchangamana na kutoka pamoja kaka na dada mkiwa wawili (outing):*

* *Tukiwa vijana tuliookoka,tunatakiwa kuangalia mambo ambayo yanaweza kutuangusha katika dhambi. Kitendo cha kutoka outing si kibaya (kama wapendwa) ila inatakawa kuwa zaidi ya watatu.Utaona kaka na dada wanatoka na kwenda, labda beach na si ajabu anaenda kwa nia nzuri tu ya kubadilishana mawazo na hata kupunga upepo ila ,shetani ni mjanja sana, pindi wakiwa ufukweni wanaweza kuwaona watu wakiwa na (wapenzi) wao. Labda wanashikana shikana na hata kula mate (romance). Na wao wakiwa kama wanadamu wenye hisia kama wanadamu wengine lazima ile hali wataiweka katika vichwa vyao. Na hata wakiwa wanaenda mara kwa mara na kuendelea kuiona ile hali,itafikia hatua watashawishika na kufanya hivyo kama wengine wafanyavyo, na matokeo yake ni kuangukia dhambini.

* vi. **Mahusiano ya kadi za Valentine kwa kaka na dada ni kinyume na mapenzi ya Mungu: *

* *Ni vijana wengi tuliookoka pindi ifikapo siku ya Valentine,tunajishughulisha kwa kununua kadi na maua na kupeana, kama kaka
na dada. Na bila kujua nini maana ya siku ya Valentine na ilitokana na nini.Inatakiwa kabla ya kufanya kitu tuangalie kwanza mwanzo wake ni nini? (Mf. Tunasherehekea Chrismas kwa sababu tunajua mwanzo wake ni nini, tunapeana kadi na hata zawadi pia ikibidi) lakini sherehe ya valentine inahusiana na Uzinzi, kama tukifuatilia mwanzo wake tutajua hilo.Vijana tuliookoka tunatakiwa kufanya mambo ambayo ni mapenzi ya Mungu si kuiga tu mambo ya dunia hii.Na matokeo yake kutumiana kadi na maua (kaka na dada), inakuja kuunda kitu tofauti kabisa katika akili zetu na mwisho wake ni kuangukia dhambini.

* vii. **Kujiepusha kuingia maeneo yasiyo husika:*

* * Sisi kama vijana tuliookoka inatakiwa tuangalie sehemu ambazo tunaingia, mf ,Utakuta kijana aliyeokoka anaingia Night clubs, Casino .n.k. Na sehemu kama hizo mara nyingi uasi mkubwa hutendeka na matokeo yake shetani anaweza kukushawishi na ukaangukia dhambini na kufwatisha uasi huo.Kwa hiyo sisi kama vijana tuliookoka tunatakiwa tuangalie sehemu za kuingia siyo kila sehemu ,sisi tunaingia.Na mwisho wake tunaweza kumtenda Mungu dhambi.

* viii. **Kuzoea kuingia kwenye vyumba vya Wasichana au Wavulana:*

* *Mazoea ya binti kuingia kwenye vyumba vya wavulana na kukaa kwenye kitanda cha mdada, si jambo jema na hata mvulana kuingia kwenye chumba cha binti si jambo jema na si heshima.Inatakiwa tuheshimiane sisi kwa sisi .Na si kwamba siyo heshima tu, bali tunaweza kujikuta tunaangukia dhambini kutokana na mazoea kama hayo.

* ix. **Kuwa na Boyfriend na Girlfriend, mara nyingi inapelekea vijana wengi dhambini:*

* *Kwa habari ya kuwa na Girlfriend au Boyfriend, ni kweli wakati bado hatujampokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yetu,wengi wetu tulikuwa nao.Lakini inashangaza na kusikitisha na hata leo katika Kanisa la Kristo vijana tuna kuwa na tabia kama ya mwanzo ambayo tuliishazizika. Na matokeo makubwa ya kuwa na uhusiano huo, mwisho wake ni kuangukia dhambini. Kwa hiyo sisi kama vijana tumtumikie Mungu,wakati ukifika Bwana atafanya njia na atatupa waume na wake kutoka kwake. Na watakuwa baraka
katika maisha yetu.

Katika mahusiano yetu sisi kama vijana tuliookoka inatupasa kutunza ushuhuda wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Anthony Mwenda–

Advertisements

23 thoughts on “Mahusiano kwa vijana kuelekea ndoa!

 1. oooh somo zuri.
  barikiwa sana mtumishi hakika somo pamoja na comments zlizotangulia znafunfsha kabsa..

 2. mm ni kijana ambaye nimeokoka,kwa kweli mm nina rafiki ambaye ni binti, urafiki wetu hauna maana mbaya kwani mm ni kama kaka kwake na yeye dada kwangu so inafikia stage mm namsaidia kimasomo na hata ki mambo ya Mungu eg maombezi kwani alikuwa anasumbuliwa na pepo lakin naamin Mungu kamfungua,kiukweli nampenda sana rafiki yangu na yeye pia na nimekuwa nikimuomba sana Mungu aupe kibali urafiki wetu na asiwepo mtu wa kuja kuwaza mambo machafu baina yetu.so naombeni ushaur watumishi kama nipo kinyume,na yapi nifanye nisimkosee mungu kwa hilo na nifanye nn ili niendelee kumfurahisha Mungu ktk urafiki wetu?

 3. Asante kwa elimu yako ndugu maana vijana wengi twaangamia kwa kukosa maharifa. Sasa umenipa maharifa kazi nikwangu sasa.

 4. Ukialikwa ulaya sidhani kama utakemea dhambi ya uzinzi au girlfriend and boyfriend relationship ukatoka salama bila kupigwa mawe. ULAYA NI ULAYA NA TANZANIA ni Tanzania yetu yenye baraka. mbarikiwe kwa michango yenu. kama ukitaka kuenenda kwa akili na vigezo vya kibinadamu, mafundisho haya hayatakufaa hata kidogo. haya ni kwa ajili ya wale wenye nia ya dhati kuto haribu maisha yao ktk ujana wao. barikiwa sana.
  Anthony

 5. Haya mafundisho nimeyashika toka ujana wangu , sasa hivi nakaribia miaka 40, nahisi yamkini siko sawa , na mara nyingi haya mafundisho hayanifundishi tena bali yananitisha , nikijilinganisha na wenzangu niliokua nawaona wanakosea dah eeee mungu nisaidie

 6. Vijana Vijana Vijanaaaa! Huu ujana unamambo mengi na unataka vitu vingi tena kwa haraka kwavile tu Ujana ni kipindi cha Mpito (Transition Period).

  Ashukuriwe Mungu na Mtumishi wake aliye tupa mafundisho yaliyo vuviwa na Nguvu ya Mungu ili Kutuponya Vijana.

  Naomba nitoe wazo langu kwenu wote wasomaji kwamba;

  1. Tambua kuwa Hakuna urafiki kati ya KIJANA wa kiume aliye Okoka na Kijana wa KIKE aliye okoka unaowafanya wawe wawili tu katika urafiki wao. Meaning that In Christianity conducts there is no BOY FRIEND and GIRL FRIEND Relationships which exists as COUPLES!!!!

  2. Sisi tulio okoka na kujazwa Roho mtakatifu Tunashauri urafiki wa Jinsia Tofauti uwe hivi.

  (a). Wavulana wawili na Msichana mmoja
  (b). Wasichana watatu Mvulana mmoja.
  (c). Wasiwe na mawazo ya kujakuoana baadae.
  (d). Iwepo sababu maalumu ya kukutana na kutembeleana eg Masomo,Discussion etc.

  Pia kama tunavyo soma Biblia kuwa Mke mwema hutoka kwa BWANA, wewe kwanini umwandae kupitia mazoea ya Urafiki (Boy/Girl Friend)?

  Yesu alipo kaa na yule mwanamke kisimani hakuwa Girlfriend wake na nia ya Yesu haikuwa kama sisi tunavyo fanya. Pia kumbuka Yesu hakumfuata wala hakuitwa na yule mwanamke Msamalia na alikuwa hamfahamu kabla japo Roho Mtakatifu alimjulisha kuwa yule mwanamke ni kahaba.

  Vijana Tuache kuiga mambo ya kigeni, always Future is Unfair jaribu kutofautisha kati ya wazungu na tamaduni zetu, Musa alikulia kwa farao lakini aliishi kufuata desturi za Ki-Ebrania. Daniel aliishi katika nyumba ya mfalme lakini Hakutaka kujitia unajisi maana alitambua yeye ni Mwebrania.

  Natamani kuongea mengi lakini muda sina.
  Mungu atusaidie Vijana.

 7. ujue bwana ukiwa umejazwa Roho Mtakatifu na umemruhusu atawale katika mahusiano hamuwezi mkashawishika kufanya ngono kwa sababu mtu anaweza akawa ameokoka ila Roho Mtakatifu hayupo ndan yake kwa sababu anakuwa hajaokoka katika roho na kweli au ameokoka katika Roho na kweli ila hajajazwa Roho Mtakatifu au hajamruhusu Roho Mtakatifu atawale katika eneo hilo

 8. Nashukuru kwa ushauri wako mzuri kaka kuhusu maisha ya yetu ya ujana. Lakini naomba ufafanuzi kwenye hili suala la girfriend na boyfriend. Umeseme haishauriwi kwa sisi tuliookoka, sasa kama ni hivyo ina maana Huyo mtu ambaye Mungu ananiandalia kuwa mume wangu atashuka tu na kuwa mume ghafla bila kupitia hizo process za urafiki? Nadhani ungetusaidia tu kama ungeweka mipaka iliyopo kati ya watu wawili walio katika stage ya urafiki kuelekea uchumba na ndoa. Asante.

 9. katika mahusiano ni vema kizingatia kuwa ulimwengu wa fikra na ulimwengu wa uhalisia viko tofauti japokuwa vyote hutegemeana. hivyo ni vema kuhakikisha umakini katika mambo haya mawili kabla ya kuhusiana

 10. Ndugu mwandishi, ni kweli mambo mengi uliyoyataja hapo juu yanaweza kumpelekea mkristo kijana kuingia kwenye mahusiano mabaya ya ki mapenzi.
  Lakini naona kuna kitu cha zaidi ambacho kija huyu wa kikristo anatakiwa kuwa nacho ambacho kitamfanya asimkosee mungu pindi awapo kwenye internet,anapowasiliana kwa simu na mchumba wake au rafiki wa jinsia tofauti,awapo beach na mchumba wake,ikitokea amekwenda kwenye chumba cha mwenzake,n.k.

  Kwani ni nini kilichomfanya kijana Yesu ashinde dhambi pale kwenye kisima na yule kahaba msamaria na walikuwa wawili tu? Hicho ndicho kinatakiwa kuwa ndani ya vijana wa kikristo hata leo. Yesu hakuogopa kukaa pale kisimani ati kwa sababu walikuwa wawili tu.

  Nasema hivyo kwa sababu mambo mengi ambayo umeyasema katika mafundisho bwana mwandishi yako ” applicable” zaidi katika mazingira la Tanzania.
  Ziko nchi(eg USA) kijana huyu atakwenda atajikuta yuko na mchumba wake sehemu fulani pekee yao tena kwa muda mrefu tu, na hakuna mtu hata wa kutaka kujua wanafanya nini, maana kila mtu yuko ” busy” na mambo yake. Je kijana huyu anashindaje katika mazingira na utamaduni wa namna hii?

  Lakini pia najiuliza,ivi maana ya girl friend/boy friend ni rafiki wa kike/wa kiume kwa Kiswahili? Na je mtu akiwa girl friend/ boy friend wako kwani ni lazima mkutane kimwili kama ambavyo wasiookoka wanafanya?

  Kama Mary Damian ni rafiki yangu, yeye ni msichana na mimi ni mvulana kwa hiyo si ni rafiki yangu wa kike( girl friend) na mimi ni rafiki yake wa kiume (boy friend). Mimi sioni sababu ya neno hili kuhusishwa na dhambi. Wanaolitumia vibaya ni wasiookoka.

  Mimi naamini siwezi kumchumbia mtu ambaye hajawa rafiki yangu kwanza.
  Mimi nafikiri vijana tusisitizwe kuwa ukiwa na rafiki wa kike / wa kiume au mchumba hamtakiwi kufanya tendo la ndoa, lakini si kuambiwa kwamba hutakiwi kuwa na girlfriend au boy friend, maana yake ni sawa na kutuambia kuwa hatutakiwi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti katika kristo, kitu ambacho si sawa.

 11. ahsante sana kwa ujumbe huu mzuri kuhusu vijana nami napenda kushauri vijana kwamba tusijidanganye kwamba tunaenda na wakati huko ni kupotea

 12. Nimefurahishwa sana na mada hii umeongea vitu haswa vilivyomo na ni vitu halisi.umeweka vitu wazi kwa namna ya kueleweka,ubarikiwe.

 13. Asante kwa somo zuri Mungu atusaidie vijana tuweze kuenenda kwa katika njia itupasayo kwani shatani hututega sana katika eneo la uzinzi, Asante Yesu kwaajili ya teknolojia ya simu na inaneti lakini bado hatujaenenda kwa hekima na kujua namna ya kutumia teknolojia hii hasa unapokuja kipengele cha facebook kimezua matatizo makubwa sana

 14. Asante kaka!nahitaji kujifunza zaidi kama kijana, hivi kwa siye tulio okoka kipengele cha uchumba tunakiruka au tunashauriwa tukae hapo kwa mda gani kabla ya kuitana mume na mke?

 15. ASANTENI KWA UJUMBE NAOMBA MNISAIDIE ELIMU ZAIDI KTK JAMBO HILI MIMI NI KIJANA AMBAYE SIELEWI JINSI YA KUMWOMBA MUNGU ANIPATIE MKE MCHUMBA KISHA AWE MKE MWEMA NAOMBA ELIMU ZAIDI

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s