DHAHABU

NAPENDA DHAHABU!

Nikifikiria kuhusu Mbinguni, naona Dhahabu. Kwa kweli napenda sana dhahabu na hata nilichagua rangi ya dhahabu kuwa rangi ya mavazi na mapambo yaliyotumika katika harusi yangu. Ni rangi nzuri sana nami ndiyo ambayo huwa naipendelea. Rangi hii hunikumbusha kuhusu Mungu!

 JE!, UNAJUA?

Ili dhahabu isafishwe, ni lazima ipitishwe kwenye moto mkali. Moto huu ndio husafisha dhahabu, kwa sababu hutenganisha uchafu wote kutoka katika dhahabu hiyo. Uchafu wote ukiungua, hubaki dhahabu iliyosafishwa. Msafisha dhahabu huweza kujua kuwa dhahabu imeshakuwa safi ikiwa ataangalia katika dhahabu iliyosafishwa naye akajiona uso wake, kama vile katika kioo. Njia hii ya kusafisha dhahabu kwa kutumia moto ndiyo njia pakee ya kusafisha dhahabu na hakuna mbadala wala njia ya  mkato.

Kama vile msafisha dhahabu anavyoweza kujua kuwa dhahabu yake sasa iko safi kwa kujiangalia ili ajione uso wake, nasi twaweza kujua kuwa tunaelekea kufanana na Mungu wakati mtu anayetuangalia tunapopitia katika majaribu na mateso atajiona kupitia maisha yetu.

Ee Bwana, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako.  Zaburi 26:2-3

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza na ukamilifu. Warumi 12:2

Unajua kuwa unafanana na Mungu wakati unapokutana na majaribu na kukimbilia upande wa pili. Unapoweza kujizuia kufanana na dunia, halafu ukachagua kumruhusu Roho mtakatifu afanye upya fikra zako. Unapoweka mbali kila kipingamizi cha fikra kinachokuzuia katika kutekeleza wito wako, na wakati unapokuwa umetumia nguvu zako zote katika kuitikia wito wa Mungu kwako. Unapokuwa una hofu ya yajayo, lakini bado unaweza kuruhusu Mungu aongoze mipango yako. Wakati hofu inapokuwa imekuzunguka lakini ukakataa kuiruhusu iteke fahamu zako. Wakati kila mmoja yuko kinyume nawe lakini una amani kwa kuwa unajua Mungu yuko upande wako, hapo ndipo UNAPOWEZA KUJUA , kuwa unasafishwa ili utoke ukiwa DHAHABU!

Ni wangapi wetu ambao wamewahi kupitia katika hali ngumu, na hatimaye kugundua kuwa hali ya kumtegemea Mungu inaongezeka zaidi na pia uhusiano baina yetu na yeye unakuwa bora? Mungu huwa hatuachi, Yeye yuko nasi kwa ajili yetu! Nafikiria wakati Shadraki, Meshaki na Abednego walivyotupwa kwenye tanuru la moto. Hawakuwa peke yao. Mungu alikuwa humo humo kwenye moto, pamoja nao.

Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara, na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu. Daniel 3:25

Ni jinsi gani ni jambo la kufariji kujua kuwa Bwana yule yule aliyekuwa na hawa watu watatu yuko hapo hapo kwa kila mmoja wetu alipo! Kilicho cha kushangaza sana kwangu ni kuwa hata katika nyakati za majaribu makubwa zaidi katika maisha yetu, ingawa ni lazima tupite hapo, hatupo peke yetu!

Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, Yeye aliyekuumba, Ee Israel, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa, nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe, na katika mito, haitakugharikisha, uendapo katkia moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Isaya 43:1-2

Fikiri kuhusu jambo hilo. Mungu hufanya nini tunapoingia katika kipindi cha kujaribiwa nasi tukapaza sauti kumlilia kwa ajili ya msaada? Kwa njia moja au nyingine, Yeye huwaokoa watoto wake.

Wenye haki hulia na BWANA husikia, naye huwaponya na tabu zao zote. Zaburi 34:17

Nilitaka kuwashirikisha kidogo mahali moyo wangu ulipokuwa nilipokuwa naandika wimbo huu (tutakaousoma huko mwishoni). Nilipata maono asubuhi moja ya wingu kubwa la kijivu lililokuwa likiingia na kutoka katika madirisha ya nyumba na majengo…….Nililiona liingia katika chumba cha mama mmoja aliyekuwa amekaa katika dawati akifanya kazi, huku akionekana amechoka na kulemewa na mawazo; halafu katika nyumba ambayo nilimuona mama aliyelemewa na kukata tamaa na hali ngumu ya maisha;  Nililiona likiingia katika darasa ambalo mwalimu alikuwa amechoka  na wanafunzi waliokuwemo darasani humo wakiwa wenye tabia mbaya kabisa; katika hospitali zilizojaa kukosa matumaini; na makanisa ambayo wachungaji wake walikuwa dhaifu, wameishiwa nguvu na wako tayari kukata tamaa! Yalikuwa ni maono ya kuogofya!

Nilianza kuomba katika roho, na kisha nikamuuliza Mungu, Kwa nini? Kwa nini alikuwa ananionyesha yote haya? Yalikuwa maombi yasiyo na matumaini lakini nilijua tumaini lipo. Ghafla nilijisikia Uhitaji wa kushirikisha watu kwa neno rahisi “USIKATE TAMAA!”

Kwa ye yote anayesoma ujumbe huu, na amekuwa akibeba uzito wa  majaribu na mateso ya maisha; hata kama ni ugonjwa, kupotelewa na wapendwa, kupoteza kazi, matatizo ya kifamilia na ndoa, ndoto zilizoyeyuka, au pengine unajisikia kukosa matumaini na kukata tama, una huzuni, unajisikia kukandamizwa na kushindwa: USIKATE TAMAA! USIKATE TAMAA! Kuna TUMAINI!

Ziangalie mbingu! Itafute Kweli! Ufahamu Ushindi wenyewe ulivyo! Majaribu haya, moto huu ni kwa ajili ya kujenga tabia ya ki-Mungu ndani yetu ili kuleta maishani mwetu Subira, Uvumilivu, Kudumu na Kuendelea katika Mungu. Yote hayo yakiwa na lengo la Kusafisha Imani yetu na kuondoa au kusahihisha udhafu ndani yetu!

Majaribu haya yanadhihirisha kuwa Imani yako ni halisi. Hapo Imani inasafisha kama vile moto usafishavyo dhahabu – ingawa Imani yako ni ya thamani sana ikilinganishwa na dhahabu. Kwa hiyo Imani yako ikiendelea kuwa imara hata baada ya majaribu mengi, itakuletea sifa nyingi na utukufu na heshima katika siku ile Bwana wetu Yesu Kristo atakayodhihirishwa kwa ulimwengu wote. 1Pet 1:7

Utapita katika katika majaribu, maumivu, kukataliwa, uchungu, kudhihakiwa, kuzomewa, kunyanyaswa, kuchekwa, kuchukiwa, kuumizwa na hata kuwa na utayari wa kuuawa kwa ajili ya Kristo. Huku ndiko kunakoitwa “ Dhahabu inasafishwa kwa Moto”.

Lakini yeye aijua njia niendeayo, Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.  Ayubu 23:10

Katika miaka michache iliyopita nimepitia hali hiyo ya “kupita kwenye moto” katika baadhi ya majaribu yangu magumu kabisa, yaliyohusu mashambulizi katika familia yangu, tabia yangu na Huduma. Nilijisikia kutendewa isivyostahili, Kuwakilishwa isivyostahili na Kueleweka vibaya. Nilijisikia kuvunjika moyo na kukatishwa tama, kuchukiwa na kukataliwa. Katika yote hayo nikajifunza kuwa kusimama kwa ajili ya Kweli kuna gharama. Kuna watu watasikia na kushangilia, wengine watachukia na kuogopa. Wakati Mungu anaanza kukuinua juu, wapo wale ambao husubiri kukurudisha chini, kwa kiburi chao, wivu na ubinafsi. Kama unafanya jambo ambalo linaleta changamoto kwa wengine, hali kadhalika tegemea kupatwa na changamoto. Mungu anapokuwa amekutenga (amekuweka maalumu kwa ajili yake), dunia haiwezi kufurahia nafasi hiyo uliyowekwa kwa kuwa inasababisha hatia kwao. Ilinibidi pia kupitia hali hiyo ya kujisikia hatiani na ukweli unaouma, jambo ambalo lilinielekeza katika hali ya kuumiza lakini nzuri sana na halisi kabisa ya Kutubu. Ilinibidi kukubali kuwa mimi pia ni binadamu na najisikia kuchoka, na kupungukiwa nguvu. Nilijisikia kukandamizwa kunanijia lakini nilishinda. Nimejifunza kupiga vita ndani yangu kwa kutumia Upanga wa Roho, nikikataa kukatishwa tama ili nisonge mbele kuelekea thawabu yangu. Mungu ameendelea kuwa Mwamba na Ngome yangu, Amekuwa Mkombozi wangu na Bwana wa Majeshi, Mshindaji. Amebaki kuwa mwaminifu na kunipitisha katika nyakati za udhaifu wangu, Hakuniacha nikimbie wala kukata tama. Kwa kweli amekuwa akinivuta juu zaidi. Amenitembeza katika Bahari ya Shamu na kunilinda na adui zangu. Nimeona miujiza, ishara na maajabu! Nimeshuhudia maongezeko Yake, Wema na Baraka. Ninaamini nina nguvu zaidi! Nimekuwa mpiganaji bora! Naweza nikachukuliana na mengi zaidi. Naweza kupigwa ngumi! Naweza nikasukumwa chini, lakini nikainuka wima tena! Sikati tamaa kwa kuwa Siko peke yangu! Nina lengo! Nina ushindi uliohakikishwa, bila kujali utagharimu kiasi gani!

Nakaza mwendo, niifikilie mede ya dhahabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. Filp 3:14

Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu. Mdo 20:24.

Tena tusichoke katika kutenda mema, maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Gal 6:9

Matunda ya kujaribiwa kwetu yataongeza zaidi na zaidi thamani yetu katika ufalme wa Mungu. Hivyo, basi, na tuwe na ujasiri kuwa matatizo yetu ya sasa yatakwisha, na mwisho wake utakuwa mzuri. Amebarikiwa mtu yule astahimiliye majaribu. Kwa sababu akishakukubaliwa, ataipokea taji ya uzima ambayo Bwana amewaahidi wale wampendao. Yakobo 1:12

Mashairi ya Wimbo wa DHAHABU:

 ****Kisichoweza kukuua hicho kinaweza kufanya uwe na nguvu zaidi!

Nimepigwa mara kadhaa, lakini ni mzima, na unajua ninasomga mbele!

Nimeshaangushwa chini, lakini nikasimama tena, na wala sikimbii!

Kwa hiyo ninachukua muda kushukuru, kwa namna ambavyo nimeongezewa nguvu!

Kwa kupita katika moto, lakini nikatoka nikiwa DHAHABU!

Na ninaendelea juu zaidi, miguu yangu ikiwa bado imesimama sakafuni.

Nilisukumwa nyuma, Nikasukumwa chini, Nikasukumiliwa mbali,

Lakini ni sawa tu maana ninazidi kuendelea mbele!

Kupigwa kwa maneno, kila neno baya walilonisemea,

Hiyo hainifanyi nifikirie. Hapana!

Kwa hiyo ninachukua muda kushukuru, kwa namna ambavyo nimeongezewa nguvu!

Kwa sababu naweza kuchukua maumivu, ambayo hata hivyo ni kwa faida yangu,

Kwa sababu sitavunjika, Upendo umenikamatisha.

Moto huu unanifanyba bora zaidi, nimesafishwa bila kujali kama,

Naonekama kama aliyeshindwa, kwa sababu nitawaonyesha kuwa mimi ni mshindi!

Mnaweza kuchukua vyote kwa sababu mimi ni mtoaji,

Lakini sikati tama wala sikimbii!

Kwa hiyo ni heri mkajua, Nitatoka nikiwa DHAHABU!****

Dunia inahitaji kutuona, mimi na wewe, tukisimama imara wakati wa kusafishwa na moto, kisha tutoke tukiwa DHAHABU.

USIKATE TAMAA!

Nawapenda,

—Beckah Shae–

Advertisements

4 thoughts on “DHAHABU

  1. More love, more power, more strenght more on you in mylife…. Glory to God #GOD IS REAL

  2. Asante sana kwa ujumbe huu, unainua wale waliovunjika mioyo, unakumbusha wale wanaojisahau. Unaelekeza wale wanaotaka ushindi. Asante na ubarikiwe.

  3. Nashkuru sana kwa ujumbe wako wa “DHAHABU” kwa maana umenipa moyo! Ubarikiwe sana.

  4. thank you for your testimony of the holy wonders

    its all above the rest of the world

    Keep shining and your glory should reap others stolen soul

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s