WANAFUNZI WAISLAMU WATANGAZA MAANDAMANO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

NDUGU WANAHABARI

Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mola wa viumbewote. Pili tuna kushukuruni kwa kuitikia wito wetu licha ya kuwa namajukumu mengi ya kutoa taarifa kwa wananchi.Kwa mara ya kwanza tumeamua kukutana nanyi. Nasi tunatoa taarifa yetu hii kwenu ilimuifikishe kwa Watanzania na wapenda amani wote duniani. Tunakuusienijuu ya ukweli na uaminifu katika kuripoti taarifa hii. Tuna kuusieni tena kuripoti taarifa hii bila ya kupotosha maana iliyokusudiwa.Kutakuwa na nafasi ya maswali ili kuuliza ikiwa kunasehemu ambayohaikueleweka.

NDUGU WANAHABARI

Tuliowaita ni viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa KiislamuTanzania yaani Tanzania Muslim Students & Youth Association (TAMSYA).Jumuiya yetu inatambulika kisheria na inafanya kazi zake kwa kufuatasheria za nchi.

NDUGU WANAHABARI

Jumuiya yetu kama inavyojieleza inashughulika na malezi ya wanafunziwafuasi wa dini ya kiislamu waliopo katika shule, vyuo vya kati navyuo vikuu na vijana wa kiislamu kwa ujumla. Jumuiya hii inawalingania waishi kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Uislamu.

NDUGU WANAHABARI

Tumeamua kukutana nanyi ili kuzungumzia mambo ambayo yanawapatawanafunzi waislamu waliopo kwenye shule na vyuo vya serikali kwa mudamrefu. Wanafunzi waislamu wamekuwa wakinyanyaswa na kuwekewa vipingamizi vya makusudi ambavyo vinasababisha kufanya vibaya katikamasomo yao pindi wakiwapo shuleni.

NDUGU WANAHABARI

Sheria ya nchi inaruhusu uhuru wa kuabudu na kuchagua dini. Kwa mujibuwa dini yetu ya uislamu ibada haimaliziki kwa kuingia msikitini nakuswali tu bali Uislamu wenyewe ni mfumo kamili wa maisha. Ibada nikila jambo analolifanya muislamu na linaloridhiwa na Mwenyezi Mungulikiwa katika muundo wa vitendo au kauli za dhahiri na kificho.

NDUGU WANAHABARI

Tumepata malalamiko kutoka kwa wanafunzi waislamu wakikatazwa kuvaa HIJABU shuleni, Tumepata mashitaka kutoka kwa wanafunzi waislamu wakinyimwa sehemu zakusalia/kufanya ibada ya sala katika mazingira ya shule na vyuo.Tumepata mashitaka juu ya kupangwa makusudi matukio mbali mbali ya shule katika nyakati za sala za waislamu. Mfano sherehe za Mahafalizinapangwa kufanyika siku za Ijumaa muda wa sala, Ratiba za mitihanivyuo vikuu hazizingatii muda wa swala ya Ijumaa .kurefusha muda wa kusimama mstarini (Parade) mpaka muda wa swala unapita.Wanafunzi waislamu wamekuwa wakikatazwa kuvaa kofia au kanzu baada yamuda wa masomo katika shule za bweni huku wakristo wakiwa wanashinda na Rozari masaa 24. Waalimu wanaofundisha somo la maarifa ya uislamu wanawekewa vikwazo mbalimbali wakati wachungaji wanapishana katika shule bila vikwazo kwenda kufundisha baibal knowledge. Vipindi vya dini vinawekwa katika ratiba za shule muda wa saa saba mchana siku ya ijumaa wakati ambao wanafunzi wa kiislam wanapaswa kuenda msikitini kwa ajili ya swala ijumaa.

NDUGU WANAHABARI

Tutatoa mifano kadhaa katika maeneo tofauti ambayo wanafunzi waislamwamefanyiwa madhila, manyanyaso na udhalilishwaji ikiwa ni pamoja na kutukaniwa Mungu wao,mtume wao na kitabu chao (Quran tukufu) na TAMSYA imefuatilia bila ya mafanikio.

SHULE YA SEKONDARI KIZUNGUZI WILAYANI KILOSA –MOROGORO

Mwanafunzi wa kidato cha nne, Frank Thobias Cosmas, aliandika waraka ulioukashifu uislamu, Qurani tukufu na Mtume Muhammad Sallalahu alaihi wasallam.Wakati wanafunzi wakristo wakiwa wanaubandika katika mbao za matangazo shuleni hapo na kusambaziana waraka huo Tarehe 13/05/2011 mwanafunzi muislamu Saidi Suleiman aliupata na kuufikisha kwa viongozi wa wanafunzi waislamu na hatimaye malalamiko hayo yalifika kwa mkuu wa shule.Mkuu wa shule alimpa Adhabu Yule mwanafunzi aliye peleka taarifa na viongozi wa wanafunzi waislamu walisimamaishwa shule kwa muda wa siku 21, na Yule aliyendika waraka huo alibakishwa kufanya kazi za shule.Tukio hili liliripotiwa kwa Mkuu wa polisi Morogoro, Afisa Elimu Mkoa Morogoro na ofisi ya mkuu wa wilaya ambao walipuuza. Hatua hiyo ilisababisha waislamu wa Mkoa wa Morogoro kuandamana kwa amani siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti, 2011.

PIA SHULE YA SEKONDARI ULONGONI – DAR ES SALAAM

Siku ya Alhamisi,tarehe 27/01/2011Mkuu wa shule hiyo aliwalazimisha wanafunzi wa kike wa shule hiyo kuvua Hijabu wakati wa zoezi la kupiga picha kwa ajili ya Mtihani wa kidato cha nne.Alifanya hivyo kwa chuki za udini kwa sababu waraka wa baraza la mitihani unaotoa maelekezo ya namna na utaratibu wa kupiga picha kila mkuu wa shule amepatiwa na haukuagiza hivyo.

SHULE YA SEKONDARI ENGUSERO KIBAYA –KITETO

Mkuu wa shule hiyo kwa kushirikiana na Kaimu katibu Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa barua yake ya Kumb.Na.FA.58/347/01/27 aliwaamrisha wanafunzi wavunje msikiti uliopo hapo shuleni kwa madai ya kwamba katika shule za serikali hairuhusiwi kujengwa nyumba ya ibaada. Lakini sikweli kwa kuwa zipo shule nyingi za serikali zilizo na nyumba za ibada makanisa tena makubwa sana. Mfano Shule ya sekondari Ndanda, Shule ya sekondari Umbwe, Lyamungo Sekondari, Pugu Sekondari Dar es salam na karibu shule zote kubwa za Serikali nchini. Huu ndio udini na mfumo kristo unaolalamikiwa na unaoliyumbisha taifa.

SHULE YA SEKONDARI ALDERSGATE BABATI MANYARA

Mkuu wa shule hiyo aliwanyima wanafunzi waislamu darasa kwa ajili ya kusomea somo la maarifa ya uislamu na kuwaambia kama wanataka kusoma somo la dini wachanganyike na wakristo ambao wamepewa chumba cha kusomea shuleni hapo, Jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za nchi.aidha alipiga marufuku uvaaji wa hijabu shuleni hapo kwa taarifa tuliyo letewa ya 17/03/2011.

SHULE YA SEKONDARI LUGOBA

Mwalimu aliwataka wanafunzi waislamu washerehekee Krismas walipokataa akawaambia tutaweka Taarabu maana waislamu mnapenda sana taarabu.Siku ya 21/01/2011 kwa makusudi Makamu Mkuu wa shule hiyo aliingia na viatu katika eneo la chumba wanachotumia waislamu kuswalia na kuwaamuru watoke katika chumba hicho wakati wa swala.Makamu Mkuu huyo alikwenda tena siku ya tarehe 31/01/2011 kwa hasira na kundi kubwa lililo sheheni wanafunzi wakristo kwa ajili ya kuwafanyia fujo waislamu waliokuwa wakiswali.  Jambo ambalo lileta tafrani kubwa shuleni hapo cha kusikitisha ni kuwa ukweli ulipotoshwa na hatimaye wanafunzi waislamu walionekana ndio chanzo cha tatizo.

SHULE YA SEKONDARI ILBORU ARUSHA

Mwanafunzi Juma Hassan alifukuzwa shule 13/01/ 2006 ikiwa ni wiki tatu kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita. Sababu ya kufukuzwa shule ilidaiwa alimsukuma Mama Mkwizu mwalimu sheleni hapo alipotaka kuingia msikitini.

SHULE YA UFUNDI TANGA JIJINI TANGA

Mwaka 2006 Mkuu wa shule hiyo bwana T. Z. Kinala amekuwa na tabia ya Kutoa salamu ya HALELUYAH mstarini wakati wa PAREDI huku akijua kwamba wanafunzi walio mbele yake ni mchanganyiko wa waislamu,wakristo na watu wa dini nyingine.Lakini si hivyo tu, Tarehe 24/7/2006 mkuu wa shule alileta kikundi cha kwaya cha kanisa wakati PAREDI na kuimba nyimbo za ibada ya kikristo. Wakati alipo kuwa akiongea na wanafunzi wa, katika hafla fupi ya kuwakaribisha kidato cha tano mnamo tarehe 28/4/2006 Pia alitamka wazi wazi kuwaambia wanafunzi waislamu kuwa hapa shuleni hakuna kuswali swala tano kwani hii siyo seminari.Mnamo tarehe 18/06/2006 aliwaambia wanafunzi wa kiislamu wanaovaa mavazi yanayotambulisha uislamu wao, kama Kofia, Kanzu na Kilemba lau kama angeliwajua asingewachagua kujiunga na shule yake. Mnamo tarehe 02/08/2006 aliwaita waislamu wanaovaa mavazi ya kiislamu kama kanzu kuwa ni Mashoga

NDUGU WANAHABARI CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

Madhila haya na manyanyaso hayawasibu wanafunzi wa kiislam waliopo mashule tu lakini hata wale waliopo vyuo na vyuo vikuu pia hawajasalimika hapa tutatoa mfano wa chuo kimoja tu cha Dodoma (UDOM)

ambako wanafunzi wa kiislam chuoni hapo wamekuwa wakidhalilishwa, kwa kutukaniwa dini yao na mtume wao mfano wa haya ni mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo yalibandikwa matangazo yenye ujumbe unaowatukana na kukejeri uislam na waislam kuwa ni watu wasioweza na wasiostahiki kuongoza,jambo ambalo liliwafanya wanafunzi wakiislam chuoni hapo kuripoti katika uongozi wa chuo na vyombo vya usalama bila ya kupewa msada, hatimae waislam waliamua kujitowa katika mchakato huo wa kampeni na uchaguzi wakiwa na nia njema ya kujiepusha na uadui na uhasma baina yao na wanafunzi wa dini zingine, lakini hata hivyo baada ya uchaguzi walitukanwa na kukashifiwa wazi wazi na wakirsto wakishangilia kwa kusema Yesu ameshinda na Mohammad ameshindwa katika kona zote za chuo, bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka husika za chuo na serikali.

NDUGU WANAHABARI

Tukio kubwa na la kusikitisha kwa wakati huu ni hili la shule ya sekondari NDANDA iliyopo mkoa wa MTWARA wilaya ya Masasi tarafa ya Chikundi kata Mwena kijiji cha Ndanda. Mpaka hivi sasa tunapozungumza nanyi wanafunzi ishirini (20) wa kiislamu wamefukuzwa shule watano (5) wakiwa ni kidato cha tano na kumi na tano ni kidato cha sita ambao wanatarajiwa kufanya mtihani wa mwisho mwanzoni mwa mwezi wa pili.Aidha wengine waliosalimika kufukuzwa shule wamewekewa masharti magumu ya kusaini ikiwa wanataka kuendelea na shule hiyo ya serikali.Miongon mwa masharti hayo ni kutojihusisha na dini yao wakiwa shuleni sharti ambalo linapora haki ya kikatiba ya kuabudu.Sababu na kosa la kufukuzwa wanafunzi hao wa kiislam likiwa ni kuuomba uongozi wa shule uwape eneo maalumu la kufanyia ibada (Msikiti) kama vile walivyotengenezewa wanafunzi wakirsto kanisa kubwa shuleni hapo,kulalamika lugha za kashfa na dharau ambazo zinatolewa na mkuu wa shule dhidi ya wanafunzi wa kiislamu uislamu shuleni hapo.

Kilichowaponza wanafunzi waislamu ni kupinga udini wa mkuu wa shule na upendeleo kwa wanafunzi wakristo, mfano kitendo cha mkuu wa shule kuteua viongozi wa serikali ya wanafunzi kiholela na kiupendeleo kwa wakirsto huku wakitoka nje ya shule wakishangilia na kusema Muhammad ameshindwa katika uchaguzi mwache bwana Yesu atawale shule!!! Haya yamefanyika mkuu wa shule akiyaona bila ya hata kukemea na kuwaadabisha wanafunzi wahusika jambo ambalo linaonesha wazi wazi kuwa ni mpango maalum ulio sanifiwa kwa mfumo maalum.

NDUGU WANAHABARI

TAMSYA mikoa, wilaya na matawi, shule na vyuo kwa muda mrefu imefanya jitihada mbalimbali za kuonana na wakuu wa shule na watendaji husikaNkatika kadhia hizi na kuishia kupuuzwa bali na kupewa majibu ya kejeli na jeuri. Na baadhi ya wakuu wa shule kuomba msamaha na kuahidikutorudia tena, lakini baada ya muda mfupi hurejea na kuendeleza dhulma na madhila kwa wanafunzi wakiislam kwa kasi ya ajabu.

Pia walimu walezi wa wanafunzi wa kiislamu au hata walimu waislamu wanao thubutu kuhoji juu ya ubaguzi wa kidini pia huonekana vioja huku wakichekwa na hatimae kupewa adhabu ya kuhamishwa kituo cha kazi kiholela mfano dhahiri ni walimu wawili pekee wakiislam wa Ndanda Sekondari ambao wamefungashiwa virago vyao na kupelekwa vijiji vya mbali kosa lao likiwa ni kutaka haki itendeke baina ya wanafunzi wote,na wakati mwingine walimu waislam hujikuta wakiambulia vichapo na vipigo kama alivyofanyiwa mwalim Halima wa Ifunda sekondari pale alipopinga dhulma, uonevu na udhalilishwaji dhidi ya wanafunzi waislam shuleni hapo mwaka 2009 akajikuta anaambulia kipigo kutoka kwa mwalim wa kikristo.

NDUGU WANAHABARI

Hapa tumeonesha sehemu ndogo ya madhila yanayowasibu wanafunzi wa kiislam nchini kama mifano tu. kwani ni vigumu kueleza madhila ya kila shule au chuo kwa njia hii. Jambo la faraja ni kuwa kila mtanzania anajua haya hata watu wa kawaida pia Kwa kuwa tatizo hili ni la muda mrefu na baadhi ya viongozi wa serikali mfano Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mh. Benjamin Mkapa alipoulizwa juu ya hali ya uwiano wa waislamu na wasiokuwa waislam katika sekta ya elimu alikiri kuwepo matatizo na uduni kwa upande wa waislam na matatizo mengi huku akisema kuwa si kosa la serikali bali ni tatizo la kihistoria.

Sisi wanafunzi wa kiislam Tanzania tunasema wazi na tunao ushahidi kuwa hili si tatizo la kihistoria bali ni mpango maalum uliosanifiwa na serikali ya awamu ya kwanza kwa lengo la kuwadhulumu na kuwakandamiza waislam kielimu kwa mbinu mbalimali kama hizi zilizotumiwa na uongozi wa shule ya sekondari Ndanda na wanaharakati wengine wa mfumo kiristo katika sekta zote za elimu nchini.Wanafunzi wa kiislamu Tanzania tunajua kuwa kitendo kilichokifanywa na mkuu wa shule ya Ndanda na Bodi ya shule pamoja na maafisa elimu cha kuwafukuza shule wanafunzi ishirini (20) wa kiislam na wengine kuwekewa masharti magumu ya kuacha wito wa dini yao ili waruhusiwe kurudi shuleni si kitendo kipya bali ni muendelezo wa dhulma ambayo walifanyiwa babu na baba zetu ambapo walilazimishwa wachague aidha kuacha dini au kusoma, Alhamdul llah tunashukuru kwa kiasi Fulani walifanya maamuzi magumu ya kulazimika kuacha kusoma na kubaki na dini yao kwani kama wangechagua la pili basi huenda nasi leo tusingekuwa katika dini ya haki ya uislam. Ama leo hii sisi wanafunzi wa kiislamu Tunasema kusoma ni sehemu ya dini yetu kama tulivyoamrishwa na Allah (sw) Quran (96:1-5) kwa hiyo hatutokubali tena kuacha wito wa dini yetu kwa kutenganisha dini na elimu kwani ikiwa tutafanya hivyo basi itakuwa tumefanya dhulma kubwa kabisa. Hapa tunawapongeza wanafunzi wa kiislam wa Ndanda sekondari kwa kujitambua na kujua haki zao za kiiman na kikatiba kwa kutoutii uongozi wa kidhulma wa shule ya ndanda pale ulipowalazimisha kuacha wito wa dini yao ili wasome, wanafunzi wa Ndanda wamefanya jambo tukufu linalopaswa kuungwa mkono na kuigwa na kila mtu mwema. Na napenda kutoa wito kwa wanafunzi wakiislam nchini kote ya kuwa wanapaswa kuwaiga na kuungana na ndugu zao zao wa Ndanda sekondari kwa kutokubali dhulma ya namna yoyote ile.

NDUGU WANAHABARI

Kadhia ya Ndanda ni mzito sana ambayo imegusa hisia ya kila muislam na kila mtanzania mpenda amani na haki, ukweli wa hili unathibitika wazi wazi kwa kila mwenye uhuru wa kufikiri kwani vijana wale wa kidato cha sita waliofukuzwa ni nguvu kazi muhimu sana kwa ujenzi wa taifa ambao tayari kusoma kwao wangeweza kuiokomboa jamii na taifa kiujumla.Lakini jambo la kusikitisha ni kuona viongozi wenye dhamana katika wizara ya elimu wakilichukulia swala hili kisiasa kinyume na uhalisia wake. Kwa kufanya ziada na uchunguzi wa kubahatisha bila umakini hatimae kutoa taarifa zilizojaa usiasa ndani yake, kuwa eti maamuzi ya bodi ya kuwafukuza wanafunzi (20) wa kiislam ni sahihi huku akieleza kuwa amefika Mtwara na kuongea na Bodi ya shule, mkuu wa shule, walimu na serikali ya wanafunzi hatimae wanafunzi wote Paredi bila ya kuwaruhusu kuuliza maswali au kutoa maoni yao hatimae kutoa hukumu.Hukumu hii haiwezi kuwa sahihi kwani hajawashirikisha wahusika wa upande wa pili wa mgogoro ambao ni wanafunzi wa kiislam kwa kuwasikiliza hoja zao madai yao ya msingi, huku ni kuisaliti katiba ambayo wameapa kuilinda ambayo inarususu uhuru wa kutoa mawazo na kila mmoja kuheshimiwa kwa nafasi yake. Jambo zito zaidi ni kuona naibu waziri anaungana na watu madhalimu waliovunja katiba ya nchi kwa kuwalazimisha wanafunzi kuacha wito wa dini yao ili warudi shule sharti hili linavunja katiba Ibara ya (19:1-2) kinachozungumzia uhuru wa imani na kuabudu.Kutokana na uzito na unyeti wa kadhia hii na madhila haya yanayoendelea kufanywa dhidi ya wanafunzi wa kiislam nchini leo hii tunapenda tuutangazie uma kuwa sasa basi hatutaki kuendelea tena kudhulumiwa na kunyanyaswa, sisi ni watanzania na tuna haki zote kama wanajamii wengine.Kwahiyo tumeitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanya mambo yafuatayo;

Tunaitaka wizara ya elimu kuwarejesha wanafunzi wote walofukuzwa na wengine bila masharti yeyote ndani ya siku tano (5) kuanzia tarehe 13/01/2012.

Tunaitaka serikali kuunda Tume huru itakayo chunguza kero wanazopata wanafunzi waislamu katika shule za serikali nchi nzima.

Tunaitaka serikali kuwawajibisha watendaji wa sekta ya elimu wanaoendekeza udini ubaguzi na unyanyasaji kwa wanafunzi wa kiislamu.

Tunaitaka serikali ithibitishe au ikanushe juu ya madai ya mkuu wa shule Ndanda na badhi ya viongozi wa serikali kuwa mashule yaliyotaifishwa na serikali, serikali inamiliki majengo tu ama ardhi na mamlaka ya matumizi yake yako chini ya Taasisi zake za asili.

Shule zote za serikali zitenge maeneo malum ya kufanyia ibada kwa ajili ya watu wa dini zote.

Asilimia kubwa ya wakuu washule za sekondari za serikali ni wakristo, hivyo basi tunaomba serikali iweke mgawanyo sawa wa nafasi hizo.

Kila jambo linapaswa kuwa na mwisho, hatuwezi kuendelelea kuvumilia uonevu wa wazi wazi siku zote.Hatuwezi tena kuendelea kuishi kama wanafunzi daraja la pili katika nchi yetu.Lazima haki sawa na uhuru upatikane kwa wanafunzi wa dini zote na sio kukandamiza waislamu. Hivyo basi tunalazimika kupaza sauti zetu kwaNkuingia barabarani kuonesha hisia zetu katika hali ya unyonge wetu

NDUGU WANAHABARI

Tunakusudia kufanya maandamano ya amani nchi nzima 20 Januari 2012 ambayo yatapeleka ujumbe kwa kila kiongozi wa Elimu katika mkoa yaani Afisa Elimu Mkoa na waislam wa Mkoa wa Dar es salaam watapeleka ujumbe moja kwa moja kwa waziri wa elimu.Kwa lengo la kutaka azingatie madai yetu ya kutonyanyaswa na kubaguliwa katika shule ya serikali.Lakini hatutoishia katika maandamano iwapo hali ya ubaguzi haitokoma. Tutatumia njia nyingine za kujikomboa katika madhila haya. Tunasema“tumenyanyaswa,tumedhaliliswa, tumebaguliwa kwa miaka 50 ya uhuru na tukavumilia na kusubiri vyakutosha leo tunasema inatosha na tumechoka tunaitaka serikali itambue haki,heshima na utu wetu kama wanavyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine mashuleni na mavyuoni.”Tunataka tuheshimiwe kama wanaadamu, kama wanatanzania huru, wanafunzi halali mashuleni na vyuoni kama wananyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine. Tumeanza muda mrefu kudai haki zetu kwa njia za kidiplomasia lakini hatujasikilizwa na leo tunatumia njia nyingine ya kidiplomasia na kikatiba ambayo ni MAANDAMANO ya amani huenda kwa njia hii serikali na jamii itasikia kilio chetu.

ACHENI KUTUDHALILISHA NA KUTUNYANYASA WANAFUNZI WA KIISLAM MASHULENI NA MAVYUONI SASA BASI INATOSHA TUNAOMBA WAISLAM WOTE NA WAPENDA AMANI WOTE MTUUNGE MKONO KATIKA MAANDAMANO HAYA YA AMANI.

Ahsanteni. JAFARI SAIDI MNEKE RAISI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI NA VIJANA

WA KIISLAMU TANZANIA (TAMSYA)

Advertisements

17 thoughts on “WANAFUNZI WAISLAMU WATANGAZA MAANDAMANO

 1. Kuleta chokochoko kwao ni kitu cha kawaida, mtambue ya kuwa asili ya dini yao ni mpinga kristo ukisoma ile ufunuo 13, mnyama apandaye kutoka baharini, na huyu ni mpinga kristo, ndio maana siku zote wao huanzisha chokochoko dhidi ya wakristo. biblia inasema roho yoyote isiyokiri ya kuwa Mungu (Yesu) amekuja katika mwili haitokani na Mungu, na kama haitokani na Mungu imetoka kwa shetani. ndio maana wenzetu na majini ni damu damu. unategemeaje mema toka kwa shetani? kila asiye na Roho wa Mungu lazima atakuwa na roho chafu haiwezekani mtu kuwa neutral. kuhusu kulalamika wakristo wanatembea na rozali wakati wote wakati wao wanakatazwa kofia zao nadhani si kilinganishi kizuri, wangesema wamekatazwa tasbih hapo sawa.

  Mimi Denno

 2. Sababu ya kusema kuwa wale waliokuwa waislam wanao mchango mkubwa wa kuwasaidia Waislam ni kuwa wengi wanafuata tu jazba, mkumbo, bila kutafakari kwanza. Quran 51:56 Quran 17:88 Allah S.W. Anasema kuwa nimewaumba majini na mwanadamu ili muniabudu, na kwamba Muhamed alitumwa kwa wanadam na majini, kulingbna na andiko hili waislam wote duniani huamini kuwa Mtume Muhamad alitumwa kwa wanadam na kwa viumbe hawa majini walioumbwa kwa moto Quran 15:27, hivyo Mwislam anaamini kuwa majini wana haki ya kusikiliza mahubiri na kuamini kama wanadam Quran 72:1…2 tunaöa hapo kuwa kundi moja walisikiliza na wakaamini, Quran 46:29 Na -( wakumbushe) tulipokuletea kundi la majini kuja kwako kusikiliza Quran. Basi walipoihudhuri walisema -(kuambiambiana) NYAMAZENI MSIKILIZE Maneno ya Mwenyezi Mungu. Na wakisema enyi watu wetu hakika tumesikiliza kitabu kilichotelemshwa baada ya Musa kinachosadikisha…,kinachoongoa,.hivyo wale ambao walisikiliza ila hawakuamini hao ndio MASHETWANI, majini katika imani ya kiislam kwa kuwa wana haki ya kuabudu na kusikiliza nao watahukumiwa siku ya kiama pamoja na wanadam.

  Wengine watenda peponi na wengine motöni,. Quran 42:25 huthibitisha kuwa majini wazuri, wale walioslim, ni ndugu wa mwislam na kuwa huwasindikiza kila wanapotembea, na kuwaongoza kutenda mema. Nimekupa mifano michache kuwa Quran hnaeleza mambo mengi, lakini niwaombe ndugu zangu Waislam, Mungu wa kweli hamlazimishi mtu kumtii, hamlazishi mtu kwenda Mbinguni, katika Kumb 30:19…20. NAZISHUHUDIZA MBINGU NA NCHI JUU YENU HIVI LEO, KUWA NIMEKUWEKEA MBELE YAKO UZIMA NA MAUTI, BARAKA NA LAANA, BASI CHAGUA UZIMA, ILI UWE HAI, WEWE NA UZAO WAKO.KUMPENDA BWANA, MUNGU WAKO, KUITÍI SAUTI YAKE, NA KUSHIKAMANA NAYE, KWANI HiYO NDIYO UZIMA WAKO, NA WINGI WA SIKU ZAKO, UPATE KUKAA KATIKA NCHI BWANA ALIYOWAAPIA BABA ZAKO, IBRAHIM, NA ISAKA NA YAKOBO. KUWA ATAWAPA. Nilichotaka tuöne ni kwamba Mungu wa kweli halazimishi mtu kumtii, kwa kuwa hamlazishi mtu, ukiona mtu analazimisha mtu afanye mambo ya Mungu au ya dini, hata ingeitwa ni ya mwenyezi Mungu..tujiulize ni Mungu yupi huyo!!,?. Tafakari. Asanteni.

 3. Na ya kuwa katika uumbaji wa Mungu, mara nyingi alitumiwa na Mungu kuleta vifaa vya uumbaji hususani alipokuwa anamuumba Adam, Mungu alimtumia Lucifer kuleta udongo uliomtengeneza Adam, hivyo basi baada ya uumbaji wa Mungu,akatoa mtihani kwa Lucifer na Adam wa kuita majina vitu. Lucifer hakuweza, ndipo Adam akafaulu kuviita majina, ndipo Mungu akamwambia kuwa inabidi Lucifer amheshim Adam kwa kumsudjudia, akakataa akasema udongo uliomuumba ni mimi niliagizwa, pia akasema yeye hakuumbwa kwa udongo, hivyo Mungu akamlaani. Surat Al Harf 7:11….18, Al..Kahf 18:50, Albagaral 2:33. Na baada ya Lucifer kutupwa duniani, akawamega hao majini au mapepo akaja nao, na akaendelea kuwa mkuu wao. Ukisoma Quran 6:128 majini wanawapotosha wanadam ili wapate wa kwenda nao jehanam. Nirudie kusema, watu waliokuwa Waislam wana mchango mkubwa wa kuwasaidia ndugu zetu waislam, watawasaidia kwa kutumia Quran, inajieleza kabisa, tatizo wengi hawaijui, nawaomba wasifanye chochote kwa jazba, Mungu wa kweli hapiganiwi, hatetewi, anasema kisasi yeye ndiye anamlipia mtu. Yatafakarini .hayo.asanteni.

 4. 72:9 Quran, hiyo Mbingu ya juu ina utisho wa moto, ila Akhera hakuna shida kwao. Kulingana na jinsi Allah asemavyo ndani ya Quran kuwa nimeumba binadam na majini ili muniabudu Quran 57:58 na kuwa miongoni mwao majini wamo waabuduo, majini waabuduo, yani waliosilimu, Quran 72:14 ambao ni wema wanaosafiri na kurithi uzima wa milele upatikao (AKHERA )KUZIMU Ndugu zangu mliokuwa waislam, na mkatokewa na neema híi ya Yesu Kristo, msinyamaze, ninyi mnajua vizuri Quran, wasaidieni. Kihalisi Quran haikubali kuwa majini walikuwa malaika walioasi Mungu, na ya kwamba wamekwisha kuhukumiwa, ila huwatetea mapepo hao, na kuwashirikisha Imani yao ya kiislam, na kuwashilikisha kufanya yale yaliyoamliwa na Allah (S.W) Na kuyapa tumaini kuwa siku moja yataurithi uzima wa milele, Quran 72:3 nayo hujifariji katika hilo. Japo yanasema kuwa nasi tulijua ya kuwa hatuwezi kumshinda mwenyezi Mungu katika Nchi wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia (katika Mbingu) maana yameshajikatia tamaa. Ndani ya Quran haigusii chochote juu ya malaika walioasi, pamoja na Lusifa, bali Muislam huamini kuwa Lucifer alikuwa malaika mkuu……..

 5. Nichukue nafasi hii kuchangia swala hili. Niwaombe Wale wote waliokuwa waislam, kisha wakaokoka, ndio watakaowasaidia Waislam waweze kuifahamu kweli. Watumie Quran, maana inasema wazi wazi kuhusu Mungu. Mfano…. Quran 72:1..14 hiyo inaitwa Suratuljinn, ni sura ya majini, ukisema jini ni kiarabu, ukiwa na maana pepo mchafu. Ni kama mtu akisema spoon/kijiko ni kitu kimoja, pia ndani ya Quran neno Pepo limetumika kama paradiso, mbinguni, lakini pia tunapata neno jingine liitwalo Akhera, ambalo halimaanishi paradiso, bali kwa lugha ya kiarabu neno hili Akhera lina maana ya kuzimu. Na tukiangalia ndani ya surajinni Quran 72:1..2, 8..9, 12 mapepo haya yanajieleza wazi kabisa kuwa mwanzo walíishi Mbinguni, kisha walipogeuka walitengwa na Mungu, walipohubiriwa na Mtume Muhamad katika safari yake ya kurudi Taifa mwaka 620AD Wapo walioamini na kuona kuwa Quran ni ya ajabu, ya kuwatangangazia neema ya kuabudu, katika Vol 8….9, husema wanapojaribu kwenda Mbinguni hukuta ile Mbingu imezungushiwa vimondo vya moto, hivyo hudai kuwa mbingu yao iko Akhera yaani kuzimu, maana Mbingu ya juu ina moto na hawana uwezo wa kwenda huko inaendelea..

 6. Ndugu yangu katika Kristo (Milinga),

  Nimekuelewa vizuri na nisamehe kwa kukosea kidogo jina lako (Veneranda badala ya Venerando).Nilivyosoma kwa haraka haraka post zako nikaona kama vile ni watu wawili tofauti wanaochangia mada hii, hivyo umeutoa utata huo ulioanza kujengeka kwangu. Kwa sasa sina cha kusema labda mpaka hapo baadaye.

  Ubarikiwe kwa mawazo yako na kuweka wazi kwamba mwanzo ulikuwa mwislamu na baadae ukamkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Tuendelee kung’ang’ania kwa Yesu maana Kwake ndiko kuna usalama wa maisha yetu ya sasa na yajayo.

 7. Mpendwa Kinyau Haggai, Shalom?

  Mimi ndiye Milinga Venerando. Naishi Kigoma Ujiji. Majina yangu kamili niliyobatizwa nayo kanisani mwaka 1990 ni OBED VENERANDO MILINGA. Kabla sijabatizwa nilikuwa naitwa JUMA MILINGA. Ila jina la JUMA silitumii kanisani nalitumia kazini tu na kwenye vyeti vyangu vya shuleni. Ndiyo maana napenda zaidi watu waniite MILINGA na hayo majina mengine siyo lazima uyataje.

  Kwa hiyo mpendwa Haggai ukiona jina la Milinga au Obed Venerando (siyo Veneranda) Milinga ndiyo mimi.

  Hiyo post kuhusu vijana wa kiislam na ile ya kuhusu maandamo ya vijana wa Kiislam Morogoro ni mimi nimeziandika. Wala usiwe na wasiwasi. Wala usidhani nimekwazika.

  Hivi Kinyau wewe hujanielewa Post zangu zilivyo? Mie nadhani hata nisipotaja jina langu ukiziona tu utazielewa kwani zinakuwa za kina na uchambuzi wa kina. AU SIYO MZEE?

  Au kuna lolote nimekosea naomba unikosoe wala usiwe na hofu ya kunikwaza. Mimi huwa napenda “both positive and negative critics”.

  Hebu Kaka Kinyau leta maoni yako tuwafundishe hawa vijana wa kiislam. Mimi nina mengi ya kusema kuhus waisla na dini yao lakini siyo lazima kuyasema yote hapa maana hapa Kigoma ninaishi nao. Nimepanga nyumba ya Mwislam tena Shekhe kabisa. Huwa ninateta naye sana. Tunaishi kama familia moja.

  Asante.

  Mimi Ndimi, Obed Venerando Milinga
  Ujiji- Kigoma.

 8. Shallom wapendwa.

  Wewe Milinga (Ujiji-Kigoma) ndiye Milinga Veneranda au ninyi ni watu wawili tofauti?! Samahani kama kwa kuuliza hivyo nimekwaza mtu. Nahitaji kuwatofautisha ili niweze kufuatilia vizuri post zenu. Nasisitiza kuwaomba radhi kama nitakuwa nimewa-offend!

  Barikiweni!

 9. Bwana Yesu asifiwe!!!!

  Hawa ndg. zetu siyo wenyewe ni mapepo tu yanawasumbua wanahitaji maombi kweli kweli wakamjue Mungu wa kweli anayestahili kuabudiwa ambaye ni Yesu Kristo aliyewambwa pale msalabanPekee basi. wanatia huruma, kwa kuwa wanatia huruwa tuombe huruma ya kristo iwafikie wajue, watambue, wafahau nini kinachohitajika kufuatwa au kuabudu. Nasema hawajitambui wamefungwa hao hapa nilipo katika ofisi yetu waisilamu ni wengi kuliko wakristo.

  Betty kipala

 10. Asalaam Alleykuum,

  Nadhani Hawa vijana wa kiislam wana tatizo la kufikiri mambo kwa kina. Huenda Hawana uelewa wa Historia za dini ya Kikristo na Kiislam hapa Tanzania.

  Aidha, wanasahau kwamba Nchi hii haina Dini ingawa inaongozwa na watu wenye dini. Kama malalamiko yao ni ya kweli viongozi waliopo serikalini ambao waislam nadhani ni wengi kuliko wakristo wangeweza kuyatatua haraka sana.

  Kwa mfano, Rais wa nchi ni Muislam, Makamu wa Rais ni Muislam, IGP ni Muislam, Wakuu wa Mikoa na makamanda wa Polissi Mikoani wengi ni waislam. Tena waislam hawa walioko madarakani ni wenye ELIMU kubwa tena wana uelewa wa mambo kuliko hawa vijana wa shule za kiislam? Pamoja na kwamba viongozi wakuu wa nchi ni waislam, wao wanaendelea kutupia lawama Uongozi wa Awamu ya Kwanza enzi za Mwalim Nyerere. Huku ni kukosa uelewa wa mambo kwa kina.

  Kama awamu ya Kwanza ilitawaliwa na Mkristo, na kama angekuwa mwenye msimamo mkali kuelekea dini yake, nadhani Tanzania nzima ingekuwa ni NCHI ya KIKRISTO. Naamini Nyerere angeweza kulifanya hilo. Mbona alitaifisha Shule zote za dini zikawa chini ya Serikali. Mbona alitaifisha mashirika Binafsi akayafanya kuwa ya serikali. Mbona Nyerere alilazimisha wananchi wote wahame makazi yao ya Asili na kuanzisha maisha mapya Vijiji vya ujamaa? Mbona Nyerere huyo anayesingiziwa eti ameanzisha mfumo Kristo serikalini alifuta utawala wa Machifu na watemi hadi leo haupo tena kama ilivyo kwa Uganda?

  Hivi Nyerere aliyeweza kufuta mifumo hiyo ya maisha kwa Watanganyika angeshindwa kutangaza kuwa Tanzania ni nchi ya Kikristo? Ikiwa Nyerere aliweza kufuta Machifu, Akafuta makazi yasiyokuwa vijiji, akawanyang’anya viongozi wa dini taasisi zao, angeshindwaje kutangaza rasmi kuwa TANZANIA NI NCHI YA KIKRISTO?

  Waislam watambue kwamba kama kuna chochote wanachodai kutendewa kinyume na katiba ya nchi au kinyume na Imani yao waelewe kwamba wanatendewa hivyo siyo kwa sababu za ubaguzi wa dini au kuichukia dini yao. Hata kama kuna kiongozi anayetenda hivyo kwa chuki dhidi ya Uislam waislam wajue kwamba mtu huyo anatenda hivyo kwa sababu zake mwenyewe na wala siyo kwa sababu kuna mfumo Kristo hapa Tanzania.

  Hivi wakristo mbona wao wanatendewa makosa mengi sana na hawaonekani wakirandaranda barabarani eti kudai kunyanyaswa kwa dini yao?

  Mbona Waislam peke yao ndio wanaruhusiwa kitaifa Kuchinja Wanyama kama vile Ng’ombe, kuku, mbuzi, na wakristo wanakula nyama hizo bila hata kulalamika?

  Mbona Waislam wamepewa Majengo ya TANESCO Morogoro iwe chuo Kikuu cha Kiislam na Wakrsito hawajalalamika kwa nini majengo ya taaisisi ya umma wapewe dini ya Kiislam wakati wote tulichangia kuyajenga kwa kodi zetu?

  Mbona Watoto wa Kike wanavaa hijabu katika shule ambazo siyo za Kiislam na Wakristo hajalalamika kwamba wao wananyanyaswa? Mbona wakristo hawasemi kwamba Tanzania inaendeshwa na Mfumo Islam?

  Mbona kila Msikiti una vipaza sauti vingi tena kwenye makazi ya wakristo wengi na waislam wachache na vipaza sauti hivyo vinafunguliwa Alfajiri saa 10.30 na kuanza kupigwa Adhana tena kwa fujo kama vile watu wote wa eneo hilo ni waislam. Mbona hilo wakristo wamelinyamazia na wanaendelea na maisha yao bila malalamiko?

  Hebu wakristo wajaribu na wao kuweka vipaza sauti kwenye nyumba zao za Ibada na kisha ikifika Alfajiri saa 11.00 waviwashe na kuanza kuvitumia kuita waumini wao? Weeeeeee, heee, waislam watakavyokuja juuuuu utaniambia. Wataandamana hadi Ikulu, kisa…. wakristo wanawapigia kelele. AJABU SANA.

  Mbona Waislam wanachoma nyumba za Ibada (Makanisa) na wakristo wanakaa kimya tu hawaandamani? Kule Zanziba Makanisa mengi yametiwa moto. Kule Kigamboni Dar makanisa yamechomwa moto, kule Singida, Mwanza, Kigoma, Tabora, nk.tena yanachomwa na wajiitao vijana wa kiislam wenye msimamo mkali. Mbona wakristo hawajawahi kuchoma misikiti? Hebu wakristo wajaribu kuchoma Msikiti waone cha moto?

  Hivi kwa nini waislam wao wanalalamika kila kukicha? Kuna wakati aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Bwa. Yusufu Makamba alitafsiriwa kwamba yeye ni kibalaka wa Wakristo kwa kisa tu kwamba yeye hakuunga mkono maandamano yao ya KUDAI KWAMBA YESU SIYO MUNGU. Kila mara mwislam mwenzao asipounga mkono madai yao wanamwona kama adui wa Uislam. Hii ajabu sana.

  Enyi Vijana wa kiislam, nawasihini kwa huruma zake Mungu jitahidini kuwa waislam safi watiifu, wachambuzi wa mambo kwa kutazama pande zote mbili, waungwana, watu wa amani na muwe watu wenye kuheshimu IMANI ZA wenzenu.

  Asalaam Allyekum, Walahamdullulah Wabarakat.

  Milinga (Ujiji- Kigoma)

 11. Mimi ni mzaliwa na ni mwenyeji wa Ndanda, hawa ndugu zetu walishinikizwa na waalimu fulani wachache wa itikadi hiyo kudai wawe na mahala pa kuabudia eneo la shule , wakisema kuwa kanisa lipo hapo, wakasahau kuwa hiyo shule kwanza ilikuwa ya hao wamission, pili hilo kanisa ni la miaka mia na zaidi pale , tena haliko eneo la shule , hayo madai tujue kuwa vijana wanatumiwa walikwenda kwa DC Masasi (kwa miguu zaidi ya km 30) kudai akawaelimisha vizuri , akawarudisha kwa gari, kama kawaida hawaelewi siku ya siku wakanzisha vurugu hadi ikalazimu FFU kutinga shuleni hapo, nashangaa wanapotoa taarifa za uongo. Jamani tuwaombee kweli kama wengi walivyosema hawa ndg zetu hawana utulivu moyoni., maana hawana mfalme wa amani “YESU KRISTO” Wanamhitaji Yesu ili watulie. .

 12. Wanafunzi wa kiislamu Popote pale mlipo hapa Tanzania.

  Waraka huu unasikitisha kama sio kuhuzunisha na kufanya niwaone ninyi mlioshiriki kuandika waraka huu kwamba ni vipofu na wenye uelewe finyu sana pamoja na kwamba angalau sasa mko level nzuri kidogo ya kielimu, yaani sekondari.

  Serikali ya Tanzania haina dini wala si serikali ya kidini. Dai la kutaka katika kila shule ya serikali pajengwe nyumba za ibada linatoka wapi? Serikali gani makini ambayo itatumia mamilioni kama sio mabilioni kujenga nyumba za ibada kwenye maeneo ya shule zake? Kwa nini mabilioni hayo yasitumike kujenga hosteli, vyumba vya madarasa na maabara kwa ajili ya ninyi wanafunzi kujifunza vizuri zaidi kuhusu masomo? Kwa nini hela hizo zisitumike kununulia vitabu vya kiada na ziada(?) kwa kusudi hilo hilo la ninyi kupata elimu bora zaidi?

  Kwangu mimi kama mngetaka kuandamana ili serikali ifanye hayo niliyoyaeleza hapo juu, ningekuwa wa kwanza kuwaunga mkono kwa kila namna. Sisi tuliosoma zamani kidogo kwenye shule za serikali tunajua vizuri sana jinsi ilivyokuwa wakati huo tukilala kwenye mabweni mazuri, hatuendi na magodoro, Jumamosi tunapewa sabuni za kufulia na kuogea, madaftari tulikuwa tukipewa na tukifunga tunasafiri kwa warrant na mikate na juice za Trufru tunapewa kwa ajili ya kula njiani.

  Shule zote ambazo sasa ni za serikali na zina majengo ya ibada kwenye maeneo yake ni lazima shule hizo zilikuwa zinamilikiwa na taasisi za kidini hasa za kikristo kama ilivyo Ndanda Sekondari. Mimi nimesoma sekondari kuanzia 1975 na kumaliza kidato cha sita 1981. Nilianzia shule ya Sekondari Old Moshi (Moshi Sc School) na kumaliza kidato cha sita Musoma Alliance (Musoma sec. School); wakati huo hakuna mwanafunzi wa kike aliyekuwa anavaa hijabu hapa Tanzania, na katika shule hizi za serikali wanafunzi wa kiislamu na wa dini zingine hapakuwa na tofauti zozote. Ikifika vipindi vya dini kila watu wanaenda sehemu zao na wanaendelea na mambo yao.

  Nina imani hata sasa kwenye shule hizi utaratibu huo bado upo; shida imekuja baada ya serikali ya awamu ya pili kuliruhusu vazi la hijabu kama sehemu ya sare ya shule katika shule za serikali. Kwa uongozi wa serikali ya wakati huo kufanya hivyo, ndipo mlango ulipofunguliwa wa waislamu kutaka kila kitu chao kiruhusiwe mashuleni.

  Shule za serikali sio shule za kidini kwamba zinawaandaa wanafunzi waje kuwa masheikh au mapadri, shule hizi zinawaandaa Watanzania ili wawe raia wema wanaoipenda nchi na kuitumikia kwa mioyo yao yote; na pia nchi kuwa na watalaamu wa kutosha katika nyanja mbali mbali. Mwanafunzi wa kiislamu aliyeko kwenye shule ya serikali anayetaka siku ya Ijumaa aache vipindi vya darasani ili aende msikitini kusali, hiyo ni hiyari yake, lakini hawezi kulazimisha kwamba vipindi visimame vya masomo ya kawaida mpaka yeye arudi toka msikitini ndipo walimu waendelee kufundisha.

  Siku zote mimi husema uislamu umejengwa juu ya misingi ya chuki, kutokupendana, kulalamika, uvivu wa kufanya kazi na uvivu wa kufikiri, kuunda vitu vya uongo na kuvifanya vionekane vya kweli na mengine mengi yafananayo na hayo!

  Kwa mfano swala la kijana aliyefukuzwa Ilboru Sekondari ambalo limenukuliwa kwenye waraka huu, kijana huyu alimpiga mwalimu wa kike ambaye ni mama mtu mzima kuliko hata mama yake, tena alimpiga mpaka akamwangusha chini, halafu leo mwanafunzi huyo aachwe tu kwa sababu yeye ni mwislamu. Tukifanya hivyo tujenga taifa gani la kizazi kijacho?

  Bahati nzuri sana mke wangu ni mmoja kati ya wakuu wa shule hapa nchini, ugomvi mkubwa kwenye shule anayoiongoza ni wasichana wa kiislamu kufunga hijabu huku nywele zao zimewekwa dawa na ni ndefu hawataki zikatwe ati kwenye hizo nywele ndiko maruhani yao yapo. Ajabu na wazazi wengine huja juu wakati walimu wakiwakata nywele hizo kwa nguvu. Sheria za shule zinasema mwanafunzi hata kama amefunga hijabu lazima nywele ziwe fupi ambazo hazijawekwa dawa, sasa wakiaambiwa hivyo wanasema wanafunzi wa kiislamu wananyanyaswa. Huu ni uvivu wa kufikiri na ufinyu wa mawazo.

  Lakini yote katika yote Yesu wetu anatuambia “Mpende jirani yako kama nafsi yako”. Amri hii haijasema ‘mpende jirani yako mkristo kama nafsi yako’, bali ‘jirani’ ikiwa ni pamoja na waislamu. Tunawapenda na kuwajali sana, ila lazima tuwape onyo kwamba wasijaribu kuvuruga amani ya nchi yetu; ili sisi tuendelee kumwabudu Mungu wetu katika Roho na Kweli.

  Mbarikiwe!

 13. “Tutatumia njia nyingine za kujikomboa katika madhila haya”.

  Msije tu mkaigeuza Tanzania kuwa Naijeria maana kwa muislam KUUA na/au KUUAWA ndizo njia mbadala za kujikomboa!!

  “TUNAOMBA WAISLAM WOTE NA WAPENDA AMANI WOTE MTUUNGE MKONO KATIKA MAANDAMANO HAYA YA AMANI”

  Kwa kuwa Uislamu si dini ya AMANI siyo rahisi kukawa na “mpenda Amani” ambaye atashirikiana na Uislam ili kuleta amani. Kila palipo na Uislamu, basi hapo hakuna Amani. Yaani hata wakibakia wenyewe tu! Tunaona jinsi ambavyo Shia na Suni wanamalizana!

  Kwa hiyo ndg Waislam, amani inakuja kwa kutimiza matakwa ya dini yenu ninyi wenyewe na wala si kwa kutaka Nchi Yoooote na watu woooote wapige magoti mbele ya Uislam!

  Inawezekana kabisa kuwa na sehemu za kuswalia pasipo kulazimisha SERIKALI KUWAWEKEA MAENEO YA NINYI KUSWALIA. Mi nakumbuka wakati niko Sekondari, tulikuwa tunakutana nyumbani kwa mwalimu, tunafanya ibada kwa Mungu pale, kisha tunarudi mabwenini kuendelea na ratiba zingine za shule. Sasa inakuwaje ninyi hamuwezi KUTUMIA AKILI na kubuni ufumbuzi wa matatizo, hata hayo madogo hadi, SERIKALI IHUSIKE?

  Hii kusema eti “Shule zote za serikali zitenge maeneo malum ya kufanyia ibada kwa ajili ya watu wa dini zote” ni uzushi tu!!!!! Kwani mmesikia DINI ZINGINE zinalalamika au WAMEWATUMA KUWAFIKISHIA MADAI YAO KWA SERIKALI? Dini zingine wako kimya na wanaendelea na ibada kwa mujibu wa dini zao pasipo kulazimisha serikali “kuwatafutia”! Hivyo kinachidaiwa ni “maeneo maalum ya kufanyia ibada kwa waislamu”. Jambo ambalo kwangu naona hakuna ulazima wowote wa serikali kuhusika.

  Nawatakia waislamu uvumilivu, wawe ni watu wenye kuvumilia, kama kweli wanapenda amani. Pia wafanye mambo yao katika mipaka ya dini yao na si kulazimisha serikali itimizwe matakwa ya waislamu!

 14. Tuzidi kuwaombea, wameanza kulalamika katika majukwaa yao, wanakuja katika taasisi zao za vijana, wataingia katika taasisi zao wanawake kila kona, Hii ni Ideology of “Hatred” na kwa kweli ukifuatilia kwa makini kabisa juu ya wanachokidai na kukipandikiza utakuta kuna Fingerprints za shetani na signature yake ipo hapo, Roho chafu ya Ibilisi toka kuzimu ipo nyuma yao. Na nia au lengo lao sio zuri hata kidogo. Shetani atanochotafuta katika taifa la Tanzania, ni kuondoa amani, na amani ikishaondoka injili haiwezi kuhubiriwa tena, shetani anataka kuweka blocked kwasababu anaona future ya taifa linapoelekea na hataki kuona Ufalme wa Mungu na Mapenzi ya Mungu yanafanikiwa juu ya taifa la Tanzania na watu wake wapate kuokolewa na kumrudia Mungu kwa toba na hatimaye Mungu kuli rehemu taifa. Hii ni vita ambayo uwanja wake wa mapambano haupo katika kujibizana wala kupangua hoja kwa njia ya mdomo wala maandishi, adui amejipanga toka katika ulimwengu wa Roho hapo ndipo uwanja wa vita upo, na sisi vita yetu siku zote ipo hapo, tukiharibu na kupangua kila fikra, mawazo yote yajiinuayo dhidi ya Kristo. Hakuna haja sana ya mabishano ya kidini, kwasababu ndio kwanza yanachochea moto, tuwe kama Eliya, ” na ijulikane leo, kama baali ndio mungu au Mungu wa Israel ndio Mungu, ijulikane leo kama “allah” ndiyo Mungu au Mungu wa Bwana na mwokozi wetu yesu kristo ambaye niBaba Yetu ndiye Mungu, na ijulikane sasa, na njia ya kufanya hivyo ni kuingia magotini na kuomba, Mungu wa israel apate kujidhihirisha, allah atajificha na kukimbia na kuwaacha watoto wake.Allah ni Mungu gani asiyewapa uvumilivu wala pumziko ndani ya mioyo yao, hata kama wanaona wananyanyasika, kukosa amani na pumziko ndani ya roho zao ni kwasababu kuna roho nyingine ya kipepo ambayo imewashikilia

 15. Amen…Dini ya amani ndiyo dini ya kweli na Yesu Kristo ndiye Mfalme wa amani. Ambao hawana hawatulii mioyo yao. Tuwaombee waislamu waokoke, wapate amani.

 16. Mwanzo 16:12 Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, Mkono wake utakuwa juuya watu wote na Mkono wa watu wote utakuwa juu yake.

  Sasa Mmeshaambiwa atakuwa PUNDA-MWITU. Kumbuka siyo Punda wa Kufugwa!! na Huyu Punda mwitu atakuwa katikati ya watu.

  Halafu Mkono wake utakuwa juu wa watu wote. —YAANI kila anakokwenda NGUMI MKONONI.

  Na watu hawatakubali: Watajibu mapigo. Hiyo Ndio Roho iliyomo ndani yao.
  Roho wa Amani ni Roho wa Kristo.

 17. Bwana Yesu asifiwe sana! Nilisikia hii habari ilinisikiisha jinsi wanavyopangilia hayo maandamano kwa lazima. Sisi ni Wakristo, sijawahi kusikia mahali wakristo wananyanyasa hawa ndugu ila wao ndio huwa kila mahali wanalalamika kunyanyaswa.

  Sisi kazi yetu ni kuhubiri Injili ya upendo wa Kristo na kuwaombea na tuombe amani itawale Tanzania kuna uchochezi wa udini unaotaka kusambazwa Tanzania na kwa jinsi hii wengi kuchafuliwa moyo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s