Je kuna Usawa Kijinsia?

Ukisoma kitabu cha Mwanzo 3:16, utaona kwamba adhabu ya dhambi aliyoifanya mwanamke (ya kulipeleleza, kulitilia mashaka na hatimaye KULIPUUZA agizo la Mungu) zilikuwa mbili; Moja, kuzidishiwa uchungu wa uzazi (adhabu ambayo bado mwanamke anaendelea kuitumikia hata anapookoka); Pili, kuwekwa chini ya MAMLAKA ya mwanamme.

Swali: Je, hizi harakati za usawa wa kijinsia zinazoendeshwa na wanawake wanaoliheshimu Neno la Mungu, zina uhalali wowote wa kimaandiko? Je, harakati hizi si jaribio jingine la mwanamke kujaribu KUIPUUZA adhabu halali ya Mungu?

Tujadiliane!

Bwaya

Advertisements

6 thoughts on “Je kuna Usawa Kijinsia?

 1. usawa unaosemwa ni wa kimahusiano na siyo wa kimaumbile,hvo lazma jamii ielewe hlo kwa uwaz na mapana.Mungu awabark sana.

 2. Kweli, Ndugu Milinga. Umejaliwa kutoa maelezo ya msingi kabisa. Asiyeweza kukuelewa basi hawezi kuelewa chochote. Mimi binafsi ninakerwa sana na waaalimu wa ndoa wanaofundisha kwamba Mungu alisema wanaume wawatawale wake zao hata walio ndani ya Kristo. Mwanzo 3:16 ni tamko la Mungu la kumpa adhabu Hawa na Adamu, lakini, baada ya Yesu kuchukua laana zote na adhabu hiyo ilitoka kwa yeyote aliye ndani ya Kristo. Mtume Paulo anaposema kwamba wanawake wawatii waume zao na waume wawapende wake wao ni ndani ya Kristo Yesu wala sio kuwapa adhabu wanawake. Ni muhimu sana kufahamu kwamba upendo huo na utii huo lazima utokane na Roho Mtakatifu ndani ya mhusika na sio sheria kutoka nje ya nafsi yake. Ubarikiwe sana.
  Chaku

 3. Wapendwa katika Bwana,

  Biblia inapaswa kuwa ndiyo msingi wa kujenga hoja zetu na wala tusitumie tamaduni zetu kutafsiri maandiko tupendavyo sisi.

  Swali letu la msingi hapa ni , JE, KUNA USAWA KIJINSIA KATIKA UKRISTO?

  Ukweli ni kwamba wapendwa wengi hawaelewi maana ya neno, ” JINSIA” na neno “USAWA”.

  Wengi nadhani wanachanganya neno, JINSI = SEX kwa Kiingereza na Neno JINSIA = GENDER kwa kiingereza.

  Mwanamke na Mwanamue wako TOFAUTI kwa maumbile yao ya UZAZI (Biological and sexual being) Tuseme kwamba wana JINSI tofauti lakini wako SAWA katika mahitaji ya kimwili, kiuchumi, kielimu, kifedha, kimavazi, nk au tuseme wako sawa KIJINSIA (Genderwise all are equal).

  Mwanamke na Mwanaume wanatofautiana kimaumbile tu lakini siyo kimahitaji. Au tuseme kwa kimombo, “Women and Men are different sexually but equal semantically, economically socially, etc).

  Hata hivyo, Mwanamke anatofautiana na Mwanamume sehemu zifuatazo:

  1. MWANAMKE ana matumbo mawili = Tumbo la Uzazi na Tumbo la Chakula wakati
  Mwanaume ana tumbo moja tu, tumbo la Chakula. Tumbo la uzazi hufanya kazi ya
  kuatamia yai la kike lililo na mbegu ya kiume na kulitunza kwa ajili ya kuzaliwa mtoto na
  kuendeleza kizazi cha mwanamke na mwanaume.

  2. Mwanamke ana Uke huku mwanaume ana Uume. Uke ni kiungo cha Uzazi ambacho
  kimo ndani ya mwili wa mwanamke chini ya kitovu katikati ya miguu. Wakati uume ni
  kiungo cha uzazi cha mwanaume kilichoko chini ya kitovu na kinaning’nia katikati ya
  miguu nje ya mwili tofauti na mwanamke.

  3. Mwanamke ana uwezo wa kunyonyesha mtoto aliyemzaa kwa kutumia titi au chuchu
  zake ziwe kubwa au ndogo LAKINI mwanaume HAWEZI kunyonyesha mtoto aliyemzaa.
  Ndiyo maana wanawake huwa na matiti makubwa (ingawa siyo lazima) ili kuweza
  kunyonyesha watoto wao mara wazaliwapo. LAKINI mwanaume hata angekuwa na
  matiti makubwa kivipi hawezi kamwe kunyonyesha mtoto wake.

  Hayo ndiyo maeneo pekee mwanamke na mwanaume wanatofautiana. Tofauti hizi tunaziita TOFAUTI ZA KIMAUMBILE na siyo TOFAUTI ZA JINSIA.

  JINSIA ni nini? (What is Gender?)

  Jinsia kwa kifupi ni Mahusiano yaliyopo katika jamii baina ya makundi rika na makundi ya wanaume na wanawake katika kujiletea maendeleo yao ya kiuchumi, kiutamaduni, nk.
  Jinsia hubadilika kulingana na wakati, teknolojia, elimu, maendeleo na mwingiliano wa kijamii.

  JINSI ni nini? (What is Sex?)

  Jinsi ni maumbile aliyonayo mtu (+ME au +KE) ambayo haiwezi kubadilishwa milele kutokana na alivyoumbika angali tumboni mwa mama yake. Hakuna mtu awezaye kubadili JINSI aliyonayo. Kujaribu kubadili JINSI aliyonayo mtu ndiyo DHAMBI KUBWA. Kwa mfano kama +ME atataka abadili JINSI aliyonayo ili awe +KE au +KE akatamani abadilike JINSI aliyopewa na Mungu ili awe +ME basi huku ndiko kutaka kuwa sawa na mwanaume au kutaka kuwa sawa na Mwanamke.

  Bibilia inasema kwamba mwanaume na mwanamke “WOTE TUKO SAWA” (Gal. 3:28)
  USAWA unaotajwa hapa siyo wa Kimaumbile (SEX) ni wa kimahusiano (Genderwise). Mtume Paul alisisitiza hilo kwani alijua utamaduni wa kiyahudi kwamba mwanamke alihesabiwa kama si chochote katika maswala ya utawala, Siasa, Uchumi, Elimu, nk. Kumbuka wayahudi waliwabagua wanawake katika kila nyanja hata wakati wa Sensa wanawake hawakuhesabiwa. Yesu alipowapa chakula maelfu ya watu, waliohesabiwa walikuwa wanaume tu. Waisrael walipotoka Misri wakiwa jangwani waliohesabiwa walikuwa wanaaume tu. Maswala mengi ya uongozi wa Kidini na kisiasa walipewa wanaume tu na wanawake waliachwa hadi pale Mungu alipokuwa akiingilia kati na kuwateua wanawake kuongoza au kuwa Manabii.

  Wakristo wengi hutoa tafsiri potofu kuhusu maandiko ya Paulo Mtume na yale ya Mwanzo Mungu alipowapa adhabu Adam na Eva. Kumbuka wote walipewa Adhabu (Mwa 3:16). Mwanamke kuzaa kwa uchungu na tamaa yake kuwa kwa Adam na Adam atamtawala. Adam naye aliadhibiwa kwa kuambiwa kwamba atakula kwa jasho lake na ardhi itamzalia miiba na magugu. Haya yote bado yapo hadi leo.

  Wengine huchanganya maandiko kutoka (1 Tim. 2:12-14) Paulo anaposema, “Simpi ruhusa mwanamke kunena au kufundisha”. Wapendwa nawaomba wasikosee kutafsiri maandiko haya kwa kutaka kuyapeleka katika USAWA wa SEX. Hapa Paulo anafundisha unyenyekevu kwa wanawake waliomwamini Mungu na alikuwa akijaribu kuwarudisha katika utamaduni wa kiyahudi. Paulo hakatazi kanisa lote ulimwenguni (Universal Church) kwamba mwanamke anakatazwa kuhubiri au kufundisha maa kama ingekuwa hivyo, Paulo asingekuwa msitari wa mbele kuwatumia wanawake kupeleka Injili.

  Aidha, kama Mungu anachukizwa kuona mwanamke akipeleka neno lake au akichunga kanisa au akipewa kuwa kiongozi sawa na mwanaume basi Mungu asingeweza kumuinua NABII DEBORA, ESTHER, MARIAM, MAGDALENA, MARTHA, nk. waliopeleka Injili tangu enzi za Manabii na enzi za Kristo na Mitume. Debora alikuwa MWAMUZI na KIONGOZI wa Israel (Amuzi 4:4). Debora alikuwa mwanamke na aliongoza taifa la Israel kwa ushujaa hadi akaitwa , “Mama mlinzi wa Israel” (Amuzi 5:6). Kama wanawake wangekuwa hawana uwezo sawa na Wanaume katika kuongoza kwa nini Mungu amteue mtu ambaye HAWEZI na ambaye angehatarisha maisha ya Taifa la Israel. Debora aliteuliwa na Mungu kuwa “Chief National Judge” au tuseme Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Israel, au Jaji Mkuu wa Taifa hilo.

  Kuudhihirishia ulimwengu kwamba Mwanamke na Mwanaume WAKO SAWA katika mahitaji ya Kiroho na Kimwili, Mungu aliamua YESU KRISTO AZALIWE bila kutumia mbegu ya Kiume. Kama mwanaume angekuwa NDIYE YUKO JUU ya mwanamke BASI MUNGU angemleta YESU KRISTO kutoka katika mbegu za kiuno cha YUSUFU mume wake na Mariam.

  Mwanamke alipandishwa hadhi kijamii kwa kumzaa YESU bila hata kulazimisha mbegu za kiume kutoka kwa YUSUFU zichangamane na YAI la MARIAM kwani hili lingewezekana tu. KWA NINI MUNGU alitumia sayansi hiii? USAWA ndio uliokuwa unarudishwa.

  Najua kwamba watu wanasoma maandiko yasemayo kuwa “mwanaume atamtawala mwanamke…..”

  Ukweli ni kwamba NENO hilo liko katika kueleza kwamba ADAM atatawala hisia za kimapenzi za EVA. Mungu anaposema, ….naye atakutawala…… alimaanisha kuwa mwanamke atakuwa anamhitaji ADAM ili aweze kutosheleza au kutawala hisia za ngono za EVA na ndipo waweze kupata watoto. Mwanamke aliambiwa kuwa ….tamaa yako itakuwa kwa mumeo…….. Hapa Mungu anamaanisha EVA atakuwa anamtaka kimapenzzi ADAM na ADAM ndiye atakayeweza kuzitawala HISIA hizo basi.

  Mungu alifanya hivyo ili wanadam wasiwake tamaa ya ngono baina yao na wanyama au malaika. Mungu pia alifanya hivyo ili ADAM na EVA waweze kutamaniana kimapenzi na kuweza kuzaa watoto wa kuijaza dunia.

  Hivyo basi, MWANAUME anatawala HISIA za MWANAMKE na wala haina maana ya kutawala kisiasa au kiuchumi, kielimu na kihuduma kanisani.

  Ukitaka kulielewa NENO hilo kwamba lina maana hiyo soma vizuri Mkutadha uliopo wakati Mungu anatoa maagizo hayo ambayo wengi huyatafsiri kama adhabu kwa EVA.

  Swala hili waliomo katika ndoa ndio wanaoweza kulielewa vizuri. Kwamba mwanamke Humtamani mwanaume kimapenzi. HISIA ZA NGONO ZINAKUWA KALI SANA KIASI KWAMBA ASIPOPATA MWANAUME WA KUZITAWALA HISIA HIZO ATACHANGANYIKIWA KISAIKOLOJIA. Swala hilo lipo sana kwa wanawake wengi na ndiyo maana wengi huhitaji wanaume wanaoweza KUTAWALA HISIA ZAO ZA KIMAPENZI na wala siyo WANAOTAWALA PESA, MASHAMBAA, MAGARI, MAJUMBA, nk.

  Mwanamke anaahitaji Mwanaume atawale HISIA zake za kimapenzi wakati huo huo na wewe mwanaume uridhike kimahaba kwa kutokwa jasho uwapo katika tendo la ndoa. Hii ni kuifanya miili ya wote wawili +ME na +KE waridhishane kwa kila mmoja kutuliza HISIA za mwenzake.

  Biblia inapsema mwanamue ni KICHWA haina maana kwamba ndiye yuko juuuu ya kila kitu. Aidha, Bibilia inaposema, …enyi wanawake watiini waume zenu kama kumtii Bwana wenu….. haina mana kwamba Biblia inawaweka JUU wanaume na kuwaweka CHINI wanawake katika maswala ya siasa, uchumi, utamaduni, nk.

  Biblia inamaanisha kwamba … WANAWAKE wanapaswa kuwatii wanaume na kuelewa kwamba pasipo wanaume, HISIA zao za kibayolojia hazitaweza kupata tiba pasipo kukubali kuishi na mwanaume. Kumbuka ilifika mahala wanawake enzi zile walitaka wawe wanawanyima waume zao. Mtume Paulo akaamuru kwamba ……MSINYIMANE…. (1kor. 6:1-13) kwani mwanamke hana AMRI juu ya mwili wake na mwili alio nao siyo mali yake hali kadhalika mwanaume hana amri juu ya mwili wake.

  Paulo anataka wanawake na wanaume wajue kuwa pasipo NDOA takatifu ambamo mwanamke na mwanume hujitoa kwa hiari kuungana basi hakuna utakatifu. Mwanamke anapaswa kumtii mume wake kwa maana ya KUTII KIU yake ya tamaa ya kibayolojia inayoelekezwa kwa mwanume. Utii unaosemwa na BIBLIA siyo utii kama ule wa BOSS na wafanyakazi wake, AFANDE na makruta wake au Mfalme/Rais na majeshi yake. Wala utii unaosemwa hapa siyo ule wa kisiasa au kifedha. Utii unaosemwa na Paulo ni ule wa matamanio ya kibayolojia (biological and sexual desires of women towards men).
  Utii unaosemwa katika Biblia kwamba wanawake wote wawe nao siyo ule ambao wanaume wanautaka kwamba WAKITOA AMRI KAMA AFANDE JESHINI haraka sana itekelezwe na mwanamke bila ubishi. Kwamba ni kule kutoa maagizo kwa mwanamke kisha anatekeleza, siyo maana yake hapa.

  Maana yake zaidi ni kwamba ….WANAWAKE WANAPASWA KUTII WAUME ZAO na wala wasikatae kutii ombi la mwanaume iwapo anamhitaji kwa tendo la ndoa kwani hakuna mwenye AMRI JUU YA MWILI WAKE.

  Paulo anawaamuru wanaume ….. WAWAPENDE WAKE ZAO … kama KRISTO alivyolipenda kanisa hata akakubali kufa msalabani. HUU ni upendo ambao Wanaume wengi hawana KABISAAA. Kama wanaume wengi wangekuwa na UPENDO kwa wake zao kama KRISTO alivyolipenda kanisa, BASI ndoa nyingi zingekuwa na AMANI sana.

  Kama unampenda sana mke wako kama Kristo kwa Kanisa hautafanya yafuatayo:

  1. Hautamzalisha watoto wengi sana (zaidi ya watoto 5) kwani kuzaa sana huzorotesha afya ya mke wako na huhataraisha uzima wake.

  2. Kama unampenda mke wako kweli kweli, Hautaacha kumsamehe makosa yake yote saba mara sabini kwa siku moja. Hata kama amefanya kosa la zinaa, ameweka chumvi nyingi, amevunja chupa ya chai, nk.

  3. Kama unampenda kweli, Utamsaidia kufanya kazi za nyumbani ikiwemo kuonyoosha nguo zako, za kwake, za wato, kuosha masahani au vyombo vya jikoni, kupika chakula, kufua nguo, kupika, kuteka maji, kufagia uwanja wa nyumba, nk.

  4. Kama unampenda mke wako utamtawala HISIA zake za ngono kwani bila wewe tamaa zake za ngono hana mwingine wa kuzitawala. Hivyo hupaswi kumnyima haki yake.

  5. Kama kweli unampenda, utamlaza mahala pazuri, utamhurumia endapo amechoka, utambebea mizigo yake, utamvika nguo nzuri, utampa fedha ya matumizi binafsi, utamjalia awapo mgonjwa.

  6. Kama kweli unampenda mke wako, utamwambia siri zako zote kwani yeye ni mke wa kifuani mwako asiyetakiwa kutojua siri zako ikiwemo mshahara wako, hati za nyumba, kadi ya gari zako, Viwanja vya nyumba zako, Akaunti za Benki, Madeni uliyonayo, Ugonjwa ulio nao, nk.

  7. Kama kweli unampenda mke wako, utamsindikiza kwenda Kliniki awapo mjamzito. Utafuatilia maendeleo yake kiafya hadi anapojifungua.

  Mpendwa, naomba niishie hapa kwani mada hii ya USAWA ni ndefu sana. Naomba niwaachie wengine wachangie zaidi.

  LAKINI kwa ufupi USAWA katika UKRISTO siyo UASI. Nawaunga mkono watu wote wanaopigania USAWA WA KIJINSIA kanisani na Serikali ILA SIUNGI MKONO wanaopigania “USAWA WA JINSI” Kwamba MWANAMKE ABADILISHWE JINSI ALIVYO aweze kuwa kama JINSI mwanaume alivyo kimaumbile.

  Nawatakia UASAWA wa JINSIA na wala SIYO USAWA WA JINSI.

 4. Ni kweli mt. Kanisa kufuata hilo ni kinyume,kwasabu hata efeso 5:22-25. Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu…… 25 enyi waume wapendeni wake zenu…. Haya mambo ya ‘haki sawa’ ni hatari mno katika ndoa kwani ni sawa yule malaika aliyetaka kuwa sawa na Mungu hatima yake kutupwa duniani hata leo angalipo. 2 be continued.!

 5. Haleluya, kimsingi hizi harakati za wanawake kutaka usawa wa kijinsia ni kutokujikubali kwao na kutaka kujifananisha na wanaume, kanuni ya Mungu haitabadilika na itabaki kuwa kanuni juu ya kanuni Isaya 28:13. Nadhani wanajiona kama wamepungukiwa na kitu fulani ndio maana wanadai usawa wa kijinsia kitu ambacho hakiwezekani. Cha muhimu upendo na amani utawale pasipo kuwanyanyasa wanawake na wao wajikubali na pia watii mamlaka kama neno linavyoesema katika Efeso 5:22-33

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s