Maandamano ya Waislamu Morogoro, mabomu yapigwa

Habari zilizotufikia, baadhi ya waislamu wameandamana kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa lengo kuu ni kupinga Ukristo na kutaka haki zao. Sasa, Kama hali ndiyo hii maandamano na mabomu ya machozi, nchi itakuwaje? Na viongozi wa maandamano haya wengi ni wanafunzi wa chuo kikuu cha waislamu.

Tunahitaji kuwaombea ndugu zetu hawa wampokee Bwana Yesu, Makundi yote ya Kikristo ni ombi maalumu kwa ajili ya kuombea amani nchini na kuwaombea watoto wetu. Mungu awabariki.

Advertisements

16 thoughts on “Maandamano ya Waislamu Morogoro, mabomu yapigwa

 1. kusema kweli na dhani waislamu wana kichaa hasa hawa wanao jifanya ni sala tano hufanya vitu bila kuangalia madhara kwa madai ya dini.

 2. Bwana Yesu Asifiwe.Ndugu waislamu wenzetu mnatusikitisha sana.Nyinyi hamumpedi mtume wenu,mngekuwa mnampenda mgeishi kama yeye alivyoishi,yaani mnamtangaza mtume wenu kaa kwamba alikuwa mtu katili sana na mpeeda vita wakati mtume alikuwa ni mtuu mwema!Someni vizuri na kuelewa maandiko matakatifu yaliyoandikwa kwenye vitabu vyenu vya dini.kwenye nchi za kiislam mkristu haruhusiwe hata kufanya ishara ya msalaba,waislamu wakienda kwenye nchi za kikristu wanadai wajengewe misikiti kwa nguvu na misalaba itolewe mashuleni na maofisini kwa sababu inawakwaza,huwezi ukaenda kwenye nyumba ya watu na kuanza kumwambia atoe vitu alivyoweka ndani ya nyumba yake kwa sababu vinakukwaza,huo ni uchokozi na ukosefu wa nidhamu.Hivi hamjifikirii,hizo swala tano zinafanya kazi gani ktk maisha yenu.Mungu ni wa upendo siyo wa vita.Mrudieni Mungu na tafakarini kabla ya kutenda.Mwenyezi Mungu awabariki.DAMU YA YESU IWAFUNIKE.

 3. Ninavyojua mimi, Ukristo una itikadi zake na Uislamu vilevile unaitikadi zake.Sasa shule kama shule inatarajia kupata wanafunzi wa aina mbili,moja wenyeitikadi za kidini na wasio naitikadi za Dini yoyote, jua kwamba kinachofuatwa pale ni Elimu tu basi! Na wote pale lazima wawe wanafunzi ili wafundishike, na ili wafundishike, pamoja na mambo mengine lazima wafuate sheria za shule.Lakini kumbuka kwamba BILA WAJIBU HUWEZI KUDAI HAKI! Sasa unapojiunga na Shule yoyote wanakupa kanuni za shule zikiambatanishwa na sheria pamoja na taratibu zinazotakiwa kufuatwa ukiwa pale,sasa, ukizipokea na kutia sahihi yako pale,maana yake umeingia katika makubaliano baina ya wewe na shule husika kisheria.Baada ya hapo kinachofuata si itikadi za dini yoyote ukiwemo uisilamu – BALI KILA UPANDE UWAJIBIKE NA UTUNZAJI WA MAKUBALIANO TAJWA TU BASI! Madai nje ya makubaliano yanaitwa “UTATA” SASA,jiulize wanachodai wanafunzi Waislamu kimo katika makubaliano baina yao na shule husika? kama yamo wanahaki ya kuandamana na kudai kutekelezwa KWA WAJIBU wanaoudai, la hayamo,hawana haki ya kudai HAKI ISIYO NA WAJIBU! Sheria moja wapo ya ushaidi katika kesi za madai,inasema,kama ipo hati mahakamani iliyokuwa imekubaliwa na pande zote mbili zinazo bishana,ushahidi wa mdomo hautakubaliwa! Je, unaona sasa? Kwakuwa makubaliano ya kujiunga na shule hayamlazimishi kisheria kuwepo shuleni hapo,njia pekee za Waislamu hao ni kubeba kila kilichochao nakuipa mgongo shule hiyo,ambayo kumbe haikubaliani na mambo mapya ya kuzuka nje ya kanuni, la sivyo WAVUNJE LAO JICHO waendelee kuishi na mwenyechongo huyo,Maana ni uungwana kumtumikia kafri ili upate mladi wako,tena ni busara kuinama ili uchukue kitu uvunguni, kuliko kuondoa kitanda maana unajiongezea kazi na unajipotezea muda KUMCHA MUNGU NI CHANZO CHA MAARIFA, na kinyume ca maarifa ni UPUMBAVU!

 4. Mimi kinachonishangaza kwa wanaomiliki shule za Kikristu,kuwazuia waislam wasivae hijabu zao,jamani lazima tulielewe Neno wala tusiparamie(WAKOLOSAI 2;20-23)kwa nini msumbuke au mzuie mambo ambayo hayafai kitu kwa kuzuia tamaa za mwili,hivi kuizuia hijabu kwani hiyo ni mini skirt ,sasa kama mnawazuia waislam wasije katika shule zenu mtawahubiria vipi injili ?Lakini pia kwa upande wa Waislamu kwa nini muwalazimishe Wakristu na Wakristo kuvaa hijabu,jamni mambo ya Mungu huwa halazimishwi mtu ila anashauriwa tu akitaka anafuata asipotaka moto ataupata mwenyewe,muwe na HEKIMA NA USTAARABU

 5. Ndugu zangu waislam wenzangu, Salaam Alleykum? Naamini Mola Muumba wa Mbingu na Ardhi yuko upande wa wenye hakhi. Allah karimu atawapatieni majibu ya dua zenu kama kweli. Salaam Alleykum wallahmdurah wabaraktu.

  Baada ya salam za kheri kwa waislamu wote, mimi nina hoja chache tu za kuwashauri.

  Kwanza, kabisa Waislam wanapaswa kujua kwamba Allah amekataza waja wake kutoa kashifa kwa watu wasiokuwa waislam au watu wa dini nyingine ikiwemo Wakristo. Qurani tukufu imekataza kabisa kutoa kashfa kuzielekeza kwa dini zingine kama ilivyoandikwa katika:

  SURATUN AN NAHL 16: 125, nanukuu aya kama isemavyo:

  “Waite (waite watu) katika njia ya Mola wako kwa hikima na mauidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora (siyo kwa kuwatukana wao au kutukana dini yao. Kwa njia hii huwezi kumvuta mtu) Hakika Mola wako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake, naye ndiye anayewajua walioongoka.”

  Hapa Quran tukufu imewakataza waislam wote wasitoe matusi au maneno ya kejeli kwa dini nyingine. Wanashauriwa watumie upole na hikima ili kuweza kuwavuta watu wengine katika dini yao kwani Mola ndiye ajuaye walioongoka.

  Hivi waislam, hapa aya hii huwa wanaisoma au hawaisomi? Hawa wanazuoni waliobobea katika maandiko ya Quraani tukufu kwa nini hawatumii aya hii kueneza dini yao bila bughudha kwa watu wa dini nyingine?

  Hebu angalia pia aya hii ya SURAT AL AN-AM 6: 108, inasema hivi; nanukuu, ” Wala msiwatukane wale ambao wanawaabudu, kinyume cha mwenyezi Mungu, wasije wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri zao bila kujua. Namna hivyo tumewapambia kila watu vitendo vyao. Kisha marejeo yatakuwa kwa Mola wao. Naye atawaambia (yote) waliyokuwa wakiyatenda.

  Kama kweli wanaoendesha harakati za kutaka Uislam uenee dunia nzima ni waislam kweli, basi watuambie wao wanafuata kitabu gani? Je, ni Quran tukufu au vitabu vya dunia tu visivyoshuka kutoka kwa Allah wao?

  Pili, waislam wanapaswa kukumbuka aya za Kitabu Kitukufu chao kwamba hawapaswi kujaribu kulazimisha watu waingie kwenye uislam kwa namna yoyote ile. Kitabu kimekataa katu katu. Hebu soma aya hii; SURAT AL BAQARAH 2: 256, Quran inasema hivi; “Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini. Uongofu umekwisha kupambanuka na upotofu. Basi anayemkataa shetani na akamwamini mwenyezi Mungu bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichokuwa na kuvunjika. Na mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kujua”.

  Unaweza pia kusoma SURAT AL FURQAN 25:63, inasema hivi, “Na waja wa Mwenyezi (anaowapenda ni wenye sifa hizi): Ni wale wanaokwenda (na kurejea kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama”.

  Natamani kuona waislam wenye kusoma na kutiii kitabu chao. Hebu niambie wewe ukisoma aya hizo unaelewaje. UISLAM NI DINI YA FUJO AU AMANI? Au hawa vijana wanaosoma vyuo vya kiislam wao SIYO WAISLAM?

  Kama ni waislam wa UKWELI aya hizo haziwahusu? Hebu tazama pia aya hii ya SURAT YUNUS 10: 99-100, inasema hivi;”Na kama angalitaka Mola wako (kuwalazimisha kwa nguvu kuamini) bila shaka wangaliamini wote waliomo katika ardhi (asibaki hata mmoja) (Lakini Mwenyezi Mungu hataki kuwalazimisha watu kwa nguvu) Basi je, wewe utawashurutisha (utawashurutiza) watu kwa nguvu hata wawe Waislamu? Na hakuna mtu anayeweza kuamini isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia uchafu uwafike wale ambao hawatumii akili zao”.

  Ukweli unataka kuonekana kwamba Waislam wanaposoma aya hizi labda wanafumba macho yao wasipasome au wanapotoshwa na watu wenye nia mbaya dhidi ya dini ya Kiislam wanaotaka Uislam uonekane kuwa ni dini ya FUJO na GHASIA wakati Maandiko matukufu ya Kiislam yanakataza yote hayo.

  Mwisho, mimi naunga mkono jeshi la polisi na uongozi wote wa jeshi hilo chini ya IGP (Muislam) Mheshimiwa Said Mwema na makamanda wote wa Mikoa kwa kuwahi eneo la tukio kudhibiti makundi ya Vijana wa Kiislam wasiojua vyema Uislam na kudhani kuwa hata watu wengine hawaujui Uislam.

  Kila Mwislam ajue kwamba Uislam maana yake ni AMANI, UPENDO, UPOLE, UTII NA UNYENYEKEVU. Huwezi kumsalimia Muislam mwenzako kwa kusema, Asalaam Alleykuum (Maana yake: Amani ya Mola iwe kwako) na wakati huo huo wewe siyo mtu wa AMANI. Pia tukumbuke kwamba maana ya Neno “Islam” kwa kiingereza ni: Peace, submit yourself to Allah, Obedient, nk.

  Waislam wenzangu mlioko Tanzania nawaomba musiwaige waislam walioko nchi za jirani zetu Afrika Magharibi kama Nigeria au Somalia na kwingineko palipo na Fujo.

  Napenda kukazia sana hapa kwamba Muislam anayedai kuwa yeye ni muislam kabisa anayefuata Maandiko Matukufu ya Quran, anayeshiriki vitendo vya Ghasia na Machafuko iwe Tanzania au kwingineko; huyo SIYO MWISLAM SAFI bali Kafiir (Mpagani) sawa na Makafiir wengine wasiomfuata Mola Muumba wa Mbingu na Ardhi.

  Mimi nang’atuka, lakini nabaki nikiamini kwamba Tanzania isiyoegemea upande wowote wa dini kubwa au ndogo nchini ndiyo Tanzania itakayodumu kuwa yenye Amani na Utulivu Kisiasa, kiuchumi, kielimu, kiutamaduni, kijamii na Kimawasiliano.

  Asanteni wote, Asallaam Alleykuum wallahmdullah Wabillalamin Wabaraktu.

 6. cha msingi kikubwa ninachokiona hapa ni kumwomba Mungu Mtakatifu wa mbinguni aingilie kati hizi dizi. yaani atuamue kwa haki maana nchi yetu si ya udini. kila mtu ashike imani yake na mwenye dini ashike dini yake pasipo kutumia nguvu. vurugu zote zinatoka wapi jamani? hebu tuwe werevu na tutumie hekima. kama hekima haipo tumwombe Mungu atupe hekima na maarifa ili yatuongoze, na si tuenende kama watu waliopungukiwa na akili.

  BARIKIWA!

 7. Ndugu zangu waislamu nawapendwa kwasababu wote ni wana wa Mungu.
  Ebu nyinyi wasomi kaeni chini na kusoma historia kwasababu madai yenu si ya kweli kwa mujibu wa historia kwasababu.Wakristo wameendelea zaidi katika elimu,afya na ustawi kwasababu wamisionari walijikita katika kutoa huduma badala ya biashara ya utumwa tofauti na Waarabu waliokuwa wanashughulika na biashara za utumwa.

  Swali:Waarabu na Wazungu ni nani aliyeanza kutawala?ACHENI KUPOTOSHA JAMII ONENI KINACHOWAPATA NIGERIA

 8. Nakumbuka hata mnajimu wa dini ya kiisilamu alisema, “Kama nchi hii itakukuja kuharibika basi itakuwa imeharibiwa na waisilamu siyo wakristo”

  Kweli haya yanaaza kujionyesha wazi kuwa waisilamu hawaitakii nchi hii mema.

  Sisi tuendelee kuomba kwa bidii.

 9. Wakubwa zangu watoto wa MUNGU,Shetani kila siku yupo “Bize”,usishangae kusikia kuwa wale watoto wa kambo wanaoismbua Naijeria ‘Harufu’ yao inaletwa huku,unakumbuka azimio la Abuja? Huoni kama ni wenda wazimu,ati unampigani Mungu,unamtafutia Mungu wafuasi kwa mtutu wa Bunduki,hivi huyo mungu ni dhaifu kiasi gani,hata umtetee na kumpigani wewe?! Kama M ungu ni “mchovu” vile hata ategemee nguvu zako,si bora umwambie Mungu huyo akuabudu wewe?! Mtu mbaya mara zote huona anaonewa,…waliotutagulia husema, ukienda kwa mwenye chongo vunja lako jicho. Haiwezekani kwenda kwa jirani yako ukafosi kuwa mzazi wao! wewe umekwenda kusoma fuata sheria za shule,wenyeakili watakuona chizi ukitumwa mawe mlimani,ukarudi mikono mitupu kwa maelezo kuwa hukuona mawe,ati umekosa! Mashule yale ni ya wakristo wewe unataka wakupe msikiti,wewe si mwehu unayetafuta shari kutokana na ubinafsi wako? Mimi binafsi nimechoka kusikia mara kwa mara waislam waleta madai ya kidini,kwa vitu vitu ambavyo ni vya kitaifa au vya watu binafsi,utasikia wamechoma mabaa Zanzibar yawatu,wamechoma makanisa ya watu, wamevamia mabucha ya nguruwe za watu nk. Kinachonifanya kunyamaza ni kwakuwa najua mambo hayo ni lazima yaje,ili mwisho nao uje! Natulia kwa amani kwa sababu atendaye ubaya ndiye anaye sababisha kuonekana kwa wema! Siwezi kuujua uzuri wa kristo iwapo shetani hatanitendea ubaya,nafikia pahala nashangaa hekima ya Yesu aliposema WAPENDENI ADUI ZENU! lakini nikiwa mtoto wa Mungu,nitamtakia mema Adui yangu,lakini akinipa kinywaji kilichochanganywa na sumu,sitakunywa hata kama nitakipokea kutoka mikononi mwake! maana niknywa – ati MUNGU atanilinda hakika yake nitakufa kwa ujinga,maana Mungu hajaribiwi!….SASA. tusilipize kisasi maana kisasi ni juu ya BWANA……..YAKIMBIENI MATENDO YAO, Maana hakuna haki bila wajibu!

 10. Labda tuulizane hivi:

  Kuna shule ngapi za serikali zilizokuwa za kiislamu ambazo zilitaifishwa kama zilivyofanyiwa Ndanda, Ilboru, Bihawana nk?

  Kama Zipo, je katika shule hizo (zilizokuwa za kiislamu), hapo kuna makanisa?

  Kama hakuna makanisa, wakristo nao wanadai kuwa serikali iwajengee makanisa huko?

  Hivi kwenye bajeti ya Wizara ya Elimu kuna fungu la kujengea nyumba za kuabudia katika mashule? Tumefikia huko kweli?

 11. waisilam kutaka haki ni sawa lkn sio kulazimisha selikali iwajengee shule, shule za kiisilam wajenge wenyewe na waweke misikiti shule nzima hakuna wa kuwauliza lkn shule za selikali kutaka wajengewe misikiti hilo haliwezekani, maana shule hizo zilijengwa na dini,hivyo wajenge zao,sioni kama wakirsto wanawanyanyasa waislam, wamezoea kulaumu,lawama ni sehemu ya ibada zao

 12. Jamani hawa waisilamu wanaiponza nchi yetu kimataifa. Msimamo wa Tanzania kupinga Israeli na kuunga mkono wapalestina, Gadafi, Irani na mataifa yenye utata inatuletea matatizo.

  Karibuni Waziri wa Ulinzi wa Israeli Ehud Baraka aliiponda Tanzania na akasema Si lolote si chochote. Akaiweka nambari wani katika nchi uchwara, Alitaja Tanzania, Mauritania na nchi ya kubuni tu aliyoitaja kama “Tripolitania”

  Alifanya hivi kwa makusudi kabisa kwa kuwa zote hizi ni nchi zenye waisilamu wasio na elimu.

  Sasa nimesikia na mama yetu aliyekuwa anafanya kazi umoja wa mataifa ameachwa kwenye orodha wa wafanyakazi na hivi tunavyoongea anarudi Tanzania.

  Badala ya kutetea utaifa mtu anakuwa anatetea dini yake na kuendeleza watu wa dini yake.

  Nani anataka Taarabu Marekani?

 13. bila bugudha wanapaswa kusikilizwa vitu wanavyodai, na kuwa addressed kiscietifiki, na undani wa wanachodai. ikiwa wanadai katika hali ambayo ni safe isiyoumiza wengine, wanapaswa kusikilizwa. ila msipowasikiliza, basi kinachofuata ni kuwa frustrated na kuumiza wengine. Jambo la muhimu ni kusikilizwa maada zao. kama ni maada zinazowezekana kutekelezwa basi, shida yao itakuwa solved.

  Hata majumbani watoto wengi huwa frustrated maana wazazi wengi wanapuuzia madai na maoni ya watoto wao. Wanapaswa kuelewa kuwa society wanayoishi inapolicy kuwa mtu anaoutashi wa kuamini chochote bila bughudha na kulindwa kikamilifu na nchi na vyombo vya ulinzi vilivyopo nchini humo. nchi yetu ni ya kidemokrasia tangia tulipopata uhuru. kuamini bila bughudha ni jambo mwalimu Nyerere alitilia mkazo. alitulea vizuri kushirikiana na kila mtu wa dini yoyote bila kujali tofauti za watu. na ndio maana hatuna ukabila kama waKenya wanvyoonyesha conflict kati ya wajaluo na kikuyu. hizi ni tofauti mbaya sana katika jamii zinaleta chuki na mafarakano makubwa. BILA KUWACHELEWESHA RAISI kIKWETE anapaswa kuongea nao akiwa kama muislam mwenzao kuwaelewesha mambo. kwani yeye amesoma missionary school anajua mengi.

  Nakumbuka kuna wakati wanafunzi wa kiislam walilalamika kwa Mkapa wakasema eti , wanafunzi wa kikrristo wanapendelewa. Raisi alisema kwenye mtihani hakuna John wala Rashidi, ila ni namba za mitihani zinatumika. na anayesahihisha hajui hii namba ni ya nani pia alisema tutayachunguza madai yenu kiundani na kiscietifiki chini ya kamati zetu.

  mambo ni kama hayo.

 14. Waislamu tunawaasa kujenga shule zenu za kiisilamu. Wakristo wamekuwa wakijenga shule zao miaka nenda rudi. Kama siyo shule za wakristo hata hao viongozi wenu wasingesoma. Ukiona vinaelea vimeundwa

 15. Naipenda nchi yangu Tanzania, siyo nchi ya dini na hatuwezi kulazimisha udini wetu kushikamana na serikali, hii haiko sahihi.

  Ni wakati wa kusema na Mungu wangu, Musa alipoinua fimbo yake juu wana wa Israel wakashinda aliposhusha mkono wakapigwa, nitaliinua jina la Mungu kwa zamu yangu. Ngome za mwovu zitaangushwa hii hajalishi ziko ngome ngapi nchi nzima, Ngome zitaanguka kwa Jina la Yesu.

 16. Maandamano yalikuwa ya amani, hakuna mtu aliyedhurika. Na amehudhuria waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi dk. Shukuru Kawambwa. Kama waislamu tukiona hatutendewi haki, tusiseme? wanafunzi 20 wa kiislamu wamefukuzwa shule kutoka Ndanda sekondari, Tumeamua kuchukua hatua

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s