Mapenzi ya Mungu yatimizwe!

Je, Ni wakati gani twatakiwa au unaofaa kuomba kwamba “Mapenzi ya Mungu yatimizwe?”

Advertisements

10 thoughts on “Mapenzi ya Mungu yatimizwe!

 1. Kwako Glady,
  nimekuelewa mpendwa,
  naona maandishi yangu yalikuwa “trimmed”,ila nilichokuwa nataka kuonyesha ni kwamba;
  kwa mujibu wa mathayo,Yesu aliomba ombi hilo moja mara tatu(Mathayo 26:38-44), haituambii jibu alilopewa(kwa mara zote tatu hakukuwa na jibu)
  Lakini Luka anatuambia kilichotokea(jibu alilopewa) baada ya yeye kukubali kuuendea msalaba.(luka 22:43).”Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu”..
  Nimekupata kabisa mpendwa..
  Ubarikiwe..

 2. Kwa ndugu Amani Musomba
  Biblia inatupa jibu juu ya maombi ya Yesu aliyoomba akisema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke. Jibu alilopewa na Mungu ni -Malaika alitumwa kwenda kumtia nguvu-(encouragement, neema, nguvu, uwezo ) ya kupitia mateso yaliyokuwa mbele yake Soma Biblia yako vizuri Luka 22:43
  Ubarikiwe

 3. Wapendwa,
  mapenzi ya Mungu=Neno la Mungu..1Yoh 5: 14-15…so ukiomba kitu sawasawa na Neno la Mungu manake unaomba sawasawa na mapenzi ya Mungu..Mukiweza pata kitabu cha Haggin on Prayer Bible study case mtajifunza mambo mengi sana. Ili uombe sawa sawa na mapenzi ya Mungu, ni lazima ulijue Neno la Mungu linasemaje kuhusu hicho unachotaka kukiomba. Kwa wale ambao mmepata neema ya kusikiliza somo la Mwakasege la jinsi ya kusukuma maombi pia mtaweza kusaidia wengine hapa.
  Maombi ya Bwana Yesu pale getsemane akisema ‘ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke……ni aina mojawapo ya maombi na hayakuwa maombi yake ya kila siku (This one was a consecrational prayer kind of ).

  Mubarikiwe

 4. Nionavyo mimi,
  kauli kwamba “Mapenzi yako yatimizwe” inaweza kutumika pale ambapo kuna uamuzi ambao uko mbele ya mtu na kuna ugumu kwa namna ulivyo kuutekeleza,pale ambapo mtu anajaribu “ku-bargain” na Mungu kama kunaweza kukawa na njia mbadala ya kufikia mwisho unaotakiwa (kama vile alivyofanya samweli wakati alipoambiwa aende kumpaka mafuta daudi,Samweli aliogopa kwamba Sauli akisikia atamuua na ndipo Mungu akampa njia ya kufanya 1:samweli 16:1-2).

  Kwenye Biblia tunaona sehemu ambayo Yesu alitamka maneno hayo ni pale ambapo jambo alilokuwa analiendea lilikuwa ni gumu kwa mwili ingawa roho yake ilikuwa tayari,
  na tunaona Yesu hakupata majibu ya maombi yake kwani yalikuwa nje ya “kusudi la Mungu la kuja kwake(Yesu) duniani”, kwa sababu hakukuwa na njia mbadala ya kumkomboa mwanadamu isipokuwa njia ya msalaba..

  Biblia haijatupa jibu alilopewa Yesu aliposema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke

  ila mwandishi wa Luka anatuambia kilichotokea baada ya Yesu kukubali kuuendea

  ni namna fulani ya mahangaiko yanayokuwa ndani ya mtu hasa kama lile lililo mbele yake kama kusudi la Mungu linaonekana gumu kwa namna ya Mwili kiutekelezaji kama lilivyo..

 5. Kila wakati tunapaswa kutamani kuona mapenzi ya Mungu yakitimia. Huo ni mtazamo mzuri, ambao Mungu anapendezwa nao anapouona mioyoni mwetu.

 6. Kwa kweli biblia kila wakati huonekana nijibu sahihi katika maisha ya mwanadamu, kwa kila anayeiamini nakujifunza kwa bidii.

 7. Swali hili limeleta changamoto sana, hasa kwangu! Maana mara nyingi, kama siyo mara zote, ninaposikia watu wakituma maombi ya kuombea mgonjwa, kila anayehitaji husema kuwa anaamini Mungu atamponya, au anaamini katika Mungu atashinda. Sijawahi kusikia au kusoma mahali popote mtu akiombea mgonjwa kisha akasema kuwa pamoja na maombi hayo lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe!

  Nyakati zote, tunapolia kwa Mungu katika jambo fulani, huwa tunahitaji Mungu atuepushie au atue mzigo fulani uliokok moyoni au mwilini.

  Ngoja nisikilize niendelee kujifunza kwa wachangiaji!

 8. Shalom!

  Tunapaswa kuomba mapenzi ya Mungu yatimizwe kila wakati na kwa kila jambo, coz hayo ndiyo mapenzi yenyewe ya Mungu. It is written in isaiah 46:9-10 …for I am God, and there is no one else; I am God, and there is none like Me,Declaring the end and the result from the beginning, and from ancient times the things that are not yet done, saying, My counsel shall stand, and I will do all My pleasure and purpose,” Psalms 33:11 “The counsel of the Lord stands forever, the thoughts of His heart through all generations.” tena mhubiri anasema katika Ecclesiastes 3:14 “I know that whatever God does, it endures forever; nothing can be added to it nor anything taken from it. And God does it so that men will [reverently] fear Him [revere and worship Him, knowing that He is]

  Kimsingi anything less than the perfect will of God leads into Gods Judgment. kama ukiomba chochote ambacho kiko tofauti na mapenzi matimilifu ya Mungu uwe na uhakika unaweza ukakipata, lakini matokeo yake ni hukumu ya Mungu inayoambatana nacho. so to stay safe; Omba mapeni ya Mungu yatimizwe kwa kila jambo, kila wakati.

  mbarikiwe.

 9. Ni wakati wote ule au “katika maombi yetu yote”.

  Kwanini nasema hivi?
  Yesu alisema; “…nanyi msalipo…MAPENZI YAKO YATIMIZWE…”. Japokuwa
  mapenzi ya Mungu yaweza kuwa ni kutupitisha mahali fulani tusipotaka
  ni lazima tung’amue kuwa YEYE ANATUWAZIA YALIYO MEMA NA MAWAZO YAKE
  YAKO JUU SANA YA YALE TUWAZAYO.

  Barikiwa!

 10. Shalom,

  …………Kila wakati, katika kila maamuzi na katika kila jambo tunaloliendea.
  Hatujakatazwa kuomba mahitaji au ‘desires’ (matamanio ya mioyo yetu), lakini Yeye anaona ‘beyond’ ya kuona kwetu, anajua ni kwa namna gani, wakati gani na mahali gani . Anajua hatari na faida zilizopo mbele ya yale tunayoyaomba. Anaweza kujibu sawa sawa na tunavyoomba au tofauti lakini wakati wote ‘NI KWA FAIDA YETU WENYEWE’

  Mithali 3; 5-6
  Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,wala usizitegemee akili zako mwenyewe,
  katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako

  Kuna wakati tunaomba lkn tunakuwa hatujui future ya yale tuyaombayo. Ukiamini Mungu anakupenda basi utahofu kumwamini kuwa atatenda kwa namna ambayo itakuletea furaha ya kudumu.

  Watu wengi wanadhani kuwa Mungu anaweza kukukomoa ukimwachia Yeye atende, tunaanza kutumia akili, hisia na mazingira na mwisho wake tunaishia kulia, kujilaumu na kujuta.

  Waebrania 10; 35-36
  Kwa hiyo msilitupe tumaini lenu, kwa maana lina thawabu kubwa mno. Inawapasa kuvumilia ili mkiisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi.

  IMANI inayoambatana na SUBIRA;ni jambo la msingi sana katika kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie katika maeneo mbali mbali ya maisha yetu.

  Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s