MAOMBI KWA AJILI YA AFYA YA KANISA

Uponyaji na afya njema wakati wote kwa watu wa Mungu ndiyo mapenzi ya Mungu. Ndio maana Yesu alipokuwa anawatuma, aliwaagiza kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Hii ni kwa sababu magonjwa mengi yanahusiana sana na matendo ya mapepo ndani ya miili ya wanadamu. Na katika huduma yake alipokuwa duniani kila mahali alipokwenda aliponya watu na kutoa pepo. Biblia inasema: Habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye (Matendo ya mitume 10:38).

Tena: Hulituma Neno Lake, huwaponya, huwatoa katika maangamizo yao (Zaburi 107:20). Tena: Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwewe Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka akawatumikia. Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na Nabii Isaya, akisema:- Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, na kuyachukua magonjwa yetu (Mathayo 8:14-17).

Tena: Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, ufalme wa Mungu umekaribia (Luka 10:8-9)
Tena: Akawaita wale thenashara; akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote kuponya maradhi (Luka 9:1).
Tena: Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili; akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina (Mathayo 10:1).

• Baba Mtakatifu Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Israeli hakika tumejua kuwa ni mapenzi yako kuwa Kanisa lako ambalo ndilo mwili wako, liwe na afya njema.
• Kwa jina la Yesu Kristo, na kwa mamlaka ya Yesu Kristo, tunaamuru magonjwa kuondoka katika miili yetu.
• Pepo mchafu aletaye magonjwa ya kila aina miilini mwetu; tunakufunga kwa jina la Yesu, na kukuzuilia katika shimo lisilo na mwisho hadi siku ya hukumu.
• Baba, utuponye na ugonjwa wa kansa ya ubongo, kansa ya maini, figo, uti wa mgongo, mapafu, koo, kibofu cha mkojo, mfumo mzima wa haja ndogo na haja kubwa, ngozi, macho, damu, na kansa ya mifupa na viungo vyangu vingine.
• Baba, utuepushe na ugonjwa wa Kisukari na wale wote walio na ugonjwa wa kisukari, nyosha mkono wako na kumgusa, ili awe mzima, gusa mfumo wao wa kutoa “insulin” na kemikali ya kupunguza sahasi ili kurekebisha sukari mwilini.
• Baba utuepushe na kutuponya ugonjwa wa shinikizo la damu na kiharusi.
• Baba, utuepushe na kutuponya na ugonjwa wa kifafa na ugonjwa wa kuchanganyikiwa akili na ukichaa.
• Baba, uniepushe na tatizo la kusahau na ugonjwa wa kupungukiwa akili.
• Baba, utuponye magonjwa ya kuumwa vichwa.
• Baba utuponye na magonjwa ya tumbo
• Baba, utuponye na magonjwa ya masikio.
• Baba, utuponye na magonjwa ya macho, ngozi.
• Baba, utuponye na ugonjwa wa manjano, mafua, fluu na koo.
• Baba, utuponye na kutulinda na ugonjwa wa ukimwi na kifua kikuu.
• Baba, utuponye na magonjwa ya mifupa na misuli pia uvimbe na maumivu kwenye magoti.
• Baba, utuponye na uele, ndui, na tauni ya ghafla.
• Baba, utuepushe na homa ya manjano.
• Baba, utuepushe na kutuponya uvimbe wa kila aina katika tumbo, ini, figo, mapafu, uti wa mgongo na sehemu za siri.
• Baba utulinde kutokana na utumbo mdogo au mkubwa kujikunja.
• Baba, utuepushe na utumbo mdogo kuingia ndani ya utumbo mkubwa.
• Baba, utuepushe na utumbo kuingia kwenye tundu la kitovu.
• Baba, utulinde ili kwamba tundu la kitovu lisipanuke na kusababisha henia.
• Baba, utulinde ili kwamba henia za kila namna zisitajwe kwetu wala zisitokee kwa watoto wa Mungu.
• Baba, utuepushe na tatizo la moyo kupanuka na kuwa mkubwa, moyo kwenda mbio au mapigo ya moyo kuwa madogo kuliko kawaida.
• Baba, utulinde na tatizo la mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo kuziba.
• Baba, utulinde na tatizo la mishipa inayotoka kwenye moyo na kupeleka damu kwenye mwili wote kuziba.
• Baba utulinde kutokana na tatizo la mishipa inayotoka kwenye moyo na kupeleka damu kwenye mwili wote kuzima.
• Baba, utulinde kutokana na tatizo la mishipa mikubwa, na midogo kwenye sehemu mbalimbali mwilini kupasuka.
• Baba, utulinde na tatizo la kuharibika kwa ini, ngozi nyembamba inayozunguka ini, mishipa ya damu ya ini na utendaji kazi ya maini.
• Baba, utulinde ili kwamba ini lifanye kazi yake ya kuchuja damu ifanyike vyema siku zote.
• Tunaamuru, kwa jina la Yesu, pumu zote zilizojaa kwenye ini kuyeyuka na kutoweka ini lolote lisafishike na kuwa safi toka sasa.
• Baba, tunaingiza figo zetu katika damu ya Yesu Kristo.
• Baba, utuponye na magonjwa mbalimbali ya figo.
• Baba utuponye na kutuepusha na mawe yanayokaa katika figo.
• Dalili zote za kuwepo mawe katika figo zetu, zitoweke katika Jina la Yesu.
• Dalili zote za figo kutofanya kazi ya kuchuja sumu toka mwilini, zitoweke katika jina la Yesu Kristo.
• Katika jina la Yesu, figo zote ziwe na afya njema na kufanya kazi vizuri katika siku zote za kuishi duniani.
• Baba, tunaweka Bandama zetu katika mikono yako na kuzifunika kwa damu ya Yesu Kristo.
• Baba, Bandama yangu iwe na afya njema.
• Baba, bandama yangu iwe na uwezo wake mzuri wa kuhifadhi damu ya kutosha.
• Baba, bandama yangu isipate ugonjwa au uvimbe wa aina yoyote bali ifanye kazi yake vizuri katika kipindi chote cha maisha yangu hapa duniani.
• Bwana Yesu, kama vile wanafunzi wako walivyokufuata kila mahali na kukuhudumia wakiwa wameponywa magonjwa mbalimbali, utujalie kukufuata tukiwa tumeponywa magonjwa ya kiroho na ya kimwili.

Neno lako linasema:
Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale thenashara walikuwa pamoja naye, na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalena aliyetokwa na pepo saba, na Yoana mkwewe Kuza, wakili wake Herode na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao (Luka 8:1-3).

Katika Jina la Yesu wa Nazareti, ninaiamuru roho ya udhaifu kuondoka katika mwili wangu wote. Ninaifunga na kuizuia katika shimo lisilo na mwisho chini ya minyororo ya mbinguni hadi siku ya hukumu.
• Baba, unitie nguvu katika miguu yangu, mikono yangu, mishipa yangu yote.
• Unitie nguvu nitembeapo, nifanyapo kazi za mikono au kazi nyingine yoyote.
• Unitie nguvu katika viungo vyangu vyote kila niamkapo ili kuona siku nyingine ya kutekeleza kazi yako na kusudi lako katika maisha yangu.
• Baba, uniepushe na misuli na mishipa inayouma miguuni, mikononi na katika mwili wote.
• Baba, ninauingiza uti wangu wa mgongo katika Damu ya Yesu.
• Unilinde na ajali zinazoweza kutegua uti wangu wa mgongo.
• Baba, uniepushe na madhara ya pingili za uti wa mgongo kuteleza na kutoka katika sehemu yake, au kusagika, au kupasuka.
• Baba, uniponye na maumivu ya shingo na uharibifu wa pingili za mifupa ya shingo na kusababisha maumivu.
• Baba, uniponye na maumivu ya kiuno.
• Baba, uniepushe na kujikwaa kwenye mawe, au kwenye visiki au kwenye samani nyumbani, na kung`oa kucha au kutoa damu vidoleni.
• Baba unilinde na kukanyaga na kuchomwa na misumari, vyuma vyenye ncha kali, miba ya miti, kukanyaga na kuumwa na nyoka au inge au mdudu yoyote mbaya.
• Baba, uniepuhe na ugonjwa wa tetanasi.
• Baba, uniepushe na magonjwa yote mabaya yanayowapata watu wasiokuamini wewe.

Neno lako linasema:
Akawaambia kwamba, utaisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wako na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nikuponyaye (Kutoka 15:26). Tena Neno linasema: Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakubarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako (Kutoka 23:25).  Tena: Na Bwana atakukondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yoyote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao (Kumbukumbu la Torati 7:15).

• Baba, Asante kwa kuyaondoa magonjwa mabaya juu yangu.
• Bwana Yesu ninakushukuru kwa sababu uliyatwaa magonjwa yetu yote na kuzichukua huzuni zetu juu ya mwili wako mwenyewe na kutuponya kabisa. Maana kwa kupigwa kwako sisi tuliponywa.
• Baba, tunakupa sifa na utukufu sasa na hata milele. Tunashukuru mno kuwa Baba umesikia maombi yetu na kuyatekeleza. Ainuliwe na kutukuzwa katikati ya Kanisa siku zote.

Asante Baba, kwa kutubariki kwa afya njema – Amen.

Pastor Ryoba, CAG

Advertisements

4 thoughts on “MAOMBI KWA AJILI YA AFYA YA KANISA

  1. Hii sala ni nzuri sana kama tukiisema ktk roho ila inabidi tuwe makini tusije kurudi kule tulikotoka tulipokuwa tunakariri sala ya Baba yetu uliye mbinguni,Jina lako litukukuzwe,ufalme wako uje nk

  2. Mtumishi wa Mungu Ryoba

    Asante sana kwa sala na Maombi mazito, kwangu mimi naona fahari katika maombi haya yanagusa moyo na mwili kwa kila kitu kwangu mimi Asantae Yesu; nasema Amen Amen Amen.

    Makunzo (Songea)

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s